read


Mwelekeo Katika Kutafsiri Ugaidi (Terrorism)

Makala haya yameandikwa na:
Shaykh Muhammad 'Ali Taskhiri
Yametarjumiwa na:
Amiraly M.H. Datoo (PO Box 838 Bukoba, Tanzania)

Pande Mbili Zinapo Pingana, Kila Mmoja Humwita Mwenzake Kuwa Ni Mgaidi
Sasa Je Mgaidi Ni Nani Baina Yao ? Tusome...

Azimio 20/5 - (I.S) la Mkutano Mkuu wa tano uliunga mkono wazo la kuitisha Baraza la Kimataifa chini ya Umoja wa Mataifa ili kuzungumzia swala la ugaidi wa kimataifa na kuweza kufafanua na kutofautisha baina ya harakati za wananchi kwa kutambua haki zao za kitaifa na ule ukombozi wa ardhi zao.

Hivyo inamaanisha kuwa sisi, katika kikao hiki tuzingatie hatua zifuatazo:

• Turejee kwanza kabisa katika vianzo vya Islam ili kutengeneza hoja madhubuti, kutambulisha misingi kwa mujibu wa malengo na matendo ya kibinadamu yakadiriwavyo, na kubuni misingi juu ya uamuzi wetu katika masuala mbalimbali.

• Kuchunguza hali halisi ya maumbile ya binadamu yasiyokuwa na tuhuma yoyote ili kuweza kutambulisha hukumu za kibinadamu zinazoweza kuletwa mbele ya jumuiya ya Kimatafa zikiwa ni kama misingi ya kibinadamu ya kupambanua. Kwa ajili ya haya, matokeo ya masomo yetu lazima yazingatie nyanja mbalimbali za mtazamo wa Kimataifa na kutoa mpangilio wa utekelezaji kwa ujumla.

• Kutokana na kanuni hizi za Kiislamu na kibinadamu, sisi tunadadisi ufafanuzi sahihi na aina yake pekee, i.e. ikizungukia sifa zote za ugaidi na kutoa nadharia za kupambanua ugaidi ambapo haiwezekani kukubalika kama ndiyo kanuni nzuri.

• Hivyo basi, inatubidi kuweka mpambanuo halisi maana na ufafanuzi wa ugaidi mbele ya jumuiya za nchi na kimataifa. Inatubidi kuchunguza kila mojawapo kwa ukaribu katika mwangaza wa matokeo, na hivyo kutoa uamuzi sahihi ambao utakuwa huru bila ya chuki au kupotosha na kulitazama kila jambo kwa malengo sahihi.

Katika mwangaza wa utambulisho huu, mazungumzo yetu yatakuwa yamebakia katika nyanja zifuatazo:

Hoja ya kwanza

Ni dhahiri kuwa kila Taifa, kila Nchi au kwa uhalisi kila Jumuiya inakuwa na wapinzani wake ambayo yanataka kuwatokemeza wapinzani wao, na vile mzozo wao utakavyoendelea kukua basi hugeukia sura ya fujo, kila upande unajaribu kuharibu jina la mpinzani wake kwa tuhuma za kuwaita waasi, majangili, wavunja sheria, matendo yasiyokuwa ya binadamu, magaidi, na majina tele yanayowezekana kutumiwa.

Sisi tunaona kuwa kila upande unajiingiza katika tuhuma kama hizo ili kutekeleza mipango ambayo inauondolea upande wa pili haki kwa masingizio ya kushirikiana pamoja na maadui wao au kufanya njama dhidi ya matakwa yao halali.

Ili kufanikisha mpango huu, kila upande unatumia kishawishi chake cha Kimataifa ili uweze kuwavutia pande nyingineo ili uwaunge mkono. Aidha kuwaweka katika matendo au katika sura ya kuwaunga mkono katika jumuiya ya Kimataifa. Hivyo swala linachukua sura ya bandia kidhahiri na ushindi katika hali ya kubana, kushawishi na nguvu za kushurutisha kuliko kulichukulia kuwa swala la mantiki ya kawaida.

Kwa hivyo, hisia zinakuwa zimetawaliwa na jazba zinachafuliwa ki-ghilba kwa ajili ya kutekeleza mipango kama hiyo iliyoanzishwa kwa misingi ya matakwa ya kibinafsi. Chini ya utambulisho wa vita dhidi ya ugaidi. Ili kuwa na hakika, ugaidi unalaumiwa na binadamu ( iwapo tutatupilia mbali malengo na madhumuni yao). Hivyo hakuna mtu aliye na akili timamu atakaye kubali tishio kwa hadhi ya binadamu, uhuru, mali, heshima, usalama, kazi, n.k. Hisia hii halisi na isiyo na shaka inayo inakubalika kwa wote.

Hoja ya Pili

Iwapo sisi tutaangali maana ya neno ugaidi kwa upande mmoja, na kuangukia kwake tu na kupuuza alama zilizoachwa kwa mwanadamu kwa upande wa pili, basi tutaona kuwa ugaida unatekelezwa katika hatua mbalimbali. Kuna ugaidi unaotishia usalama, heshima, mali na vinginevyo kama hivyo; vile vile kuna ugaidi wa kitamaduni ambao unachana sehemu mbili utambulisho wa kibidamu, na kuelekeza katika shimo kubwa la kupotea milele bila ya uokovu na kutokuwa na madhumuni; vile vile kuna ugaidi wa habari ambao unamnyima mtu uhuru wake wa kupumua kifikra katika ulimwengu usiochafuliwa. Sisi tunaweza kuzungumzia aina nyingi za ugaidi kama vile ugaidi wa kiuchumi, ugaidi wa kisayansi, ugaidi wa kibalozi, ugaidi wa kijeshi, n.k.

Hata hivyo upo mgawanyiko unaotokana na aina ya mtendaji wa ugaidi, ambavyo ni lazima izingatiwe vyema. Ni mgawanyiko katika ugaidi halali na usio halali - Ugaidi rasmi - ambayo ndiyo hatari kabisa -- zikiwemo hatua zinazoungwa na jumuiya ya Kimataifa au Taifa, ama ikiwa kwa jeshi la Taifa hilo au sura mbalimbali au katika sura za operesheni kwa ajili ya manufaa ya sehemu iliyotajwa. Kinyume na ugaidi huu, ni ule ugaidi usio rasmi.

Hoja ya tatu

Sisi tunaweza kuchunguza, katika tendo lolote au hali, juu ya harakati mbili:

1. Madhumuni ya mtenda

2. Kukubalika kwa tendo kibinadamu.

Hizi sura haziwezi kutenganishwa. Madhumuni ya kibinafsi ya mtendaji inaweza kuonekana ikiwa ni ubinadamu kwake lakini sivyo machoni mwa umma mzima. Kinyume na hayo, mtendaji inawezekana asiwe na sababu za kibinadamu mawazoni mwake au labda analo kusudi, anayoichukulia yeye kuwa si ubinadamu lakini inachukuliwa na umma kuwa ni tendo la kibinadamu.

Hivyo, maoni yanaweza kutofautiana katika maamuzi iwapo tendo kama hilo ni zuri au baya ( wanazuoni wa elimu ya usuli wamefanya utafiti mzuri kabisa juu ya misingi ya busara ya kutofautisha baina ya matendo mema na mabaya, lakini hapa si mahala pa kuyazungumzia hayo kwani ni somo moja pana sana na linahitaji muda mwingi kulichambua). Kile kilicholazima kuelezwa hapa ni kuwa hakuna hata sehemu mojawapo, ikichukuliwa mbalimbali, inatosheleza kuamua ukubaliaji au kushutumiwa kwa tendo au kuamua tendo kama linastahili ama halistahili. Ili kutoa uamuzi na tendo ni lazima kukadiria kwa usahihi inavyostahili katika sehemu zote mbili.

Kwa sababu hiyo, inatubidi kuhakikisha madhumuni katika utafiti wetu ili kutafuta mizania ya kupambanua ukubalikaji kibinadamu wa tendo kutokana na misimamo vyote : Uislamu na ubinadamu kwa ujumla.

Ama kuhusiana na msimamo wa Kiislamu, sisi inatubidi turejee Shariah, imani na hukumu ambazo zinahusiana na swala zima la ugaidi -katika hali yake ilivyo - ili kwa ujumla kutoa maana ya ugaidi unaolaaniwa, i.e. ugaidi unaokanushwa na Uislam ikiwa kama pingamizi katika hatua za ukamili wa mwanadamu kama ilivyoamuliwa na Allah swt kwa ajili ya mwanadamu kwa kupitia maumbile ya kibinadamu na kuelezwa kwa kupitia ufunuo wa ayah takatifu.

Wakati tunapozungumzia mafundisho ya Kiislamu, sisi tunaona kuwa Uislamu ni wenye hazina kubwa mno katika uwanja huu, na sisi tunaona kuwa Mahakimu wa Kiislamu wamechungua sana katika mitazamo mbalimbali ambayo zinahusiana na somo.

Sisi tunao hukumu juu ya al-baghy i.e. uasi wa kijeshi unaofanywa na kikundi kimoja dhidi ya serikali halali, tishio kwa umma mzima, na kwa kujitafutia malengo maovu ya kisiasa ambayo yanahatarisha umoja wa kitaifa na usitawi.

Vile vile sisi tunazo hukumu juu ya al-harabah, ambayo inaelezwa kama ni utumiaji wa silaha, juu ya ardhi au maji, usiku au mchana, kwa ajili ya kutishia watu, katika mji au mahala pengine, awe mwanamme au mwanamke, mwenye nguvu au dhaifu. Allah swt anabainisha katika Quran: 5 : 33

Kama itakavyokuwa imeonekana, Ayah inaelezea somo na maana, kwa vita shidi ya jamii na kueneza uovu (ufisadi) juu ya ardhi. Vile vile imeelezea adhabu kali kutolewa kwa wale watendao, jambo ambalo linatuthibitishia umuhimu wake katika Uislamu kuhusiana na swala hilo.

Vilevile zipo Shariah kuhusu wizi na mauaji ambazo zinaweza kutajwa katika sura hii. Kama vile, sisi tunayapitia maandiko matakatifu ya Kiislamu yanayozungumzia masuala tuliyonayo mbele yetu, kama mauaji ( al-fatk), udanganyifu (al-ghilah), na njama za kuchochea watu kuasi serikali (al-'i'timar ).

Vile vile kuna maandiko ambayo yanagusia kila masuala yahusianayo na mikataba na maahidiano hata kama itakuja kujulikana hapo baadaye kuwa yalikuwa yakipendelea upande mwingine. Hadi hapo watakapokuwa wamebakia katika makubaliano yao, basi ni lazima maafakiano yote yaheshimiwe na kutekelezwa ipasavyo.

Zaidi ya hayo, sisi tunahitaji mpango wa maadili ya Kiislamu ambao unao imani zisizojulikana kwa kanuni stahiki wakati hapo hapo yamekuwapo hata kufikia mizizini mwake mwa mpango wao. Udanganyifu, kwa mfano, inaweza kufikia kiwango cha dhambi kuu na hivyo inaweza kuanza masingizio. Hivyo sisi tunaona kuwa Uislamu unataka uadilifu ili kulinda uhuru wa kila aina wa mwanadamu, na kuhami hadhi ya kila mmoja na jamii, vile vile ushikamano wa jamii na hadhi ya familia, ikichukulia hujuma yoyote ile dhidi yao kuwa kosa la jinai listahilialo kupewa adhabu kali kabisa ambayo inaweza hata kutolewa hukumu ya kifungo, kifo na kama hizo.

Uislam daima unaheshimu na kusisitiza kanuni za uwajibikaji wa mtu binafsi na kuchukulia hujuma juu ya watu wasio na hatia kama ni dhambi kubwa kabisa. Unamtetea na daima kumhami yule aliye dhaifu na mnyonge, mnyenyekevu na aliyedhulumiwa na unatangaza jihad kwa ajili ya kuwahami hao: 4 : 75

Na kwa nini msipigane kwa ajili ya Allah, na kwa ajili ya wasiojiweza wazee wanaume na wanawake …

Mwislamu anatakiwa daima asimame kidete kwa ajili ya yule aliyedhulumiwa hadi hapo watakapopatiwa haki yake. Imam 'Ali (a.s.) akiwapa nasaha watoto wake wawili, aliwaambia:

"Muwe wapinzani wa wakandamizaji na watetezi wa wadhulumiwa"

"Kwangu mimi wanyonge huwa waheshimiwa hadi mimi niwapatiapo haki zao, na wenye nguvu ni wadhaifu hadi hapo mimi nijitoleapo kazi hizo kutoka kwao."

Labda kuelezwa katika Qur'an Tukufu kuhusu baraka za usalama "Na amewafanya wasalimike dhidi ya khofu" 106 : 4 ni uthibitisho bora kabisa juu ya umuhimu wa usalama.

Hata hivyo, itachukuwa muda mrefu sana iwapo tutakaa kujadili na kufafanua zaidi juu ya masuala yahusikanayo. Hivyo tutachukua pambanuo la kwanza katika kutambulisha ubinadamu kuwa ni nia ya mtendaji na kukubalika kwa tendo hilo katika Din kufuata Shariah na imani.

Tukigeukia mpangilio wa pili, yaani mpangilio wa kibinadamu kwa ujumla, sisi tunaweza kukubalia kanuni hizo ambazo zote kwa pamoja zinaheshimiwa na binadamu kama zinavyowakilishwa na vyombo vyao halisi, Taasisi zao mashuhuri,dhamira na jazba zao, zikiwa ndizo nyanja za kupambanua ili kuthibitisha kuwapo kwa ubinadamu au kupinga kwake kwa nia ya mtendaji, na juu ya yote yaliyokwisha elezwa kwa ujumla (ingawaje sisi tunaamini mipambanuo hiyo miwili kuwa zinajifunika).

Kwa mfano kabla ya kuendelea mbele, sisi tunaweza kuuona uhasama uliopo wa binadamu kwa kuzingatia kuwa yafuatayo yatakuwa si ubinadamu:

• umalaya na kutengeka kwa uhusiano wa kifamilia;

• madawa ya kulevya na kutengeka hadhi ya mtu mweyewe;

• ukoloni na kuwadharau na kuwadhalilisha watu na kupora mali na heshima zao;

• ukiukaji wa haki zote zinazotambuliwa na uvunjaji wa maandikiano ( ahadi ) ;

• kupiga kwa mabomu maeneo yanayokaliwa na raia wasio na hatia, utumiaji wa mabomu ya sumu za kemikali, kushambulia ndege za abiria, treni za kitaifa, vyombo vya biashara na utalii, na njama kama hizo ambazo zinalaaniwa na dunia nzima katika vita.

Hakuna kupinda kokote pale kuhusiana na hali ya unyama katika sura hizo hapo juu. Kwa hivyo, ukiukaji na uvunjaji wa haya na kama hayo yanatupa maoni kuwa tubuni mapambanuo ambayo yatachukua sura ya kuelezea kwetu, na tendo lolote lile litakalokuwa kutokomeza na kupinga hayo yatakuwa ni ubinadamu ambayo kwa hali lazima iungwe mkono iwapo nayo pia haitaambatanishwa na uvunjwaji wa haki na heshima za wanaadamu wengine.

Hoja ya Nne: Tafsiri ya ugaidi

Katika nuru ya hapo juu, sisi tunafikia tafsiri halisi ya matendo ya ugaidi, tafsiri ambayo inakubalika na ambayo ndiyo itakuwa upande wetu. Na kabla ya kuleta hoja zetu za kupendekeza tafsiri, inatubidi kwanza tujikumbushe mambo yafuatayo:

1. Tishio na ukiukaji wa usalama wa aina yoyote;

2. nia na malengo ya kinyama;

3. ubinadamu kutokubalia hatima na sababu na tendo lenyewe.

Kwa hayo, tafsiri yetu inaweza kuwa kama ifuatavyo:

Ugaidi ni tendo litendwalo kwa ajili ya kufikia shabaha zilizo za kinyama na ufisadi (mufsid), na ikiwa ni tishio kwa usalama wa aina yoyote ile, na ukiukaji wa haki zinazotambuliwa na dini na ubinadamu (utu).

Kwa ajili ya kutaka kufafanua zaidi, tunaweza kuongezea nukta zifuatazo:

1. Sisi tumetumia neno binadamu badala ya kimataifa kwa ajili ya kuchukua maana kwa ujumla, kihalisi au vinginevyo, ili kusisitiza tabia ya ujumla ya taarifa ya binadamu.

2. Sisi tumetumia neno ufisadi katika kuielezea malengo ya kinyama i.e.kueneza maovu juu ya ardhi, na ikiwemo ushurutishwaji wa kuepukana na malengo kama hayo.

3. Sisi tumezungumzia ugaidi wa aina mbalimbali kwa tungo usalama wa aina yoyote.

4. Sisi tumetaja mipambanuo miwili yaani kidini na kibinadamu, ya wali ikiwemo katika imani yetu na ndipo kuizungumzia kiujumla.

5. Kama itakavyokuwa imeonekana, ni ukweli kuwa operesheni ni mbaya na haimaanishi hali ya kusema kuwa ni swala la ugaidi. Katika mwangaza wa tafsiri ya hapo juu, sisi tutaweza kuhakiki sura ya moja au nyingine na kuamua iwapo ni swala la ugaidi. Sisi tutakubaliana kuwa tafsiri haitatumika katika yafuatayo:

a. matendo ya upinzani wa kitaifa unaofanywa dhidi ya majeshi ya wavamizi (yaliyokalia ardhi kwa mabavu ), wakoloni na waliokalia kwa mabavu.

b. Upinzani wa watu dhidi ya vibaraka waliowekewa juu yao kwa nguvu na ushurutisho wa majeshi

c. Kupinga udikteta na aina zote za utawala wa kidhalimu na hatua zozote za kudhalilisha Taasisi zao;

d. Upinzani dhidi ya ubaguzi wa rangi na kuwashambulia wanavuguvu hao;

e. ulipaji wa kisasi dhidi ya ukandamizaji wa aina yoyote ile iwapo hakutakuwa na sura nyingine.

Vivyo hivyo, tafsiri ya ugaidi haiwezi kutumiwa kwa hatua yoyote ile ya kidemokrasia isiyoambatanishwa na ugaidi hata kama haitakuwa na malengo mema. Na wala haitatumika kwa matendo ya kiharibifu yatendwavyo na watu binafsi iwapo hakutakuwa na athari za kijamii.

Tafsiri hiyo vile vile haitatumika kwa ajili ya yafuatayo:

a. matendo ya uharamia juu ya ardhi, angani na baharini;

b. operesheni zote za kikoloni zikiwemo vita na harakati za kijeshi;

c. matendo yote ya kidikteta dhidi ya watu na sura zote za kulinda udikteta, bila ya kutaja kuhadaa kwao mataifa;

d. mbinu zote za kijeshi zilizo kinyume na desturi ya mwanadamu, kama vile utumiaji wa silaha za kemikali, kushambulia makazi ya raia wasio na hatia, kulipua majumba, kuwatawanya raia, n.k.;

e. uchafuzi wa aina zote za mazingira, utamaduni na habari. Kwa hakika, ugaidi wa kiakili unaweza kuwa ni ugaidi ulio wa hatari kabisa;

f. hatua zote zile ambazo zinadhuru uchumi wa kitaifa au kimataifa, kuwaathiri hali ya masikini na wanyonge, kuharibu utamaduni na uchumi wa jamii, na kuyafunga mataifa kwa madeni makubwa;

g. matendo yote ya njama ambayo yanalenga kuvunja nguvu za mataifa kwa ajili ya kupigania ukombozi na kuwa huru, na kuwawekea vipingamizi viovu ili kuwadhoofisha;

Kwa hakika orodha ya mifano ambayo inaweza kuambatanishwa pamoja na tafsiri hii, kwa kweli haina mwisho.

Hoja ya tano

Ingawaje mikutano mingi mno imekwisha itishwa na majaribio mengi yameshafanywa kupiga vita ugaidi, lakini inaonekana kuwa imeshindwa kufanikiwa kwa sababu zifuatazo:

• Hazikuwa zikitokana na mtazamo wa kibinadamu wa kimataifa bali zilikuwa zimelengwa kuleta mafanikio finyo kimsingi.

• Wao hawakuzingatia hali iliyopelekea kutokezea ugaidi huo, wala kamwe wao hawakufuatilia malengo ya ugaidi. Kwa hakika ni jambo la kuchekesha mno kuona kuwa Marekani, ambayo ndiyo mama wa ugaidi ulimwenguni, na mtungaji wa hali zote za udhulumaji na ukandamizaji na kuwakandamiza watu, kwa kuwaunga mkono serikali za kidikteta na kuunga mkono ukaliaji wa mabavu ardhi za nchi zingine na kuimarisha mashambulizi katika maeneo ya raia wasio na hatia, n.k. wajaribu kukutana na kuwa na kauli moja juu ya kupigana na ugaidi, i.e. jambo lolote lile linalopingana na matakwa ya kibepari.

Mauaji ya mtu katika pori ni dhambi isilosameheka,

Lakini mauaji ya nchi yenye amani ni swala la kujadiliwa.

Kwa kiasi chochote kile, tiba halisi ya ugaidi -- hasa matendo ya ugaidi wa kibinafsi - yanakuwa, katika mtazamo wetu, ni kule kuondoa ile hali iliyoifanya hivyo kutokea.

Uislamu, katika kutibu makosa yote yapotokayo, inasisitiza mno hoja hii. Inamtaka kwanza mtu arekebishe hali ya kijamii na atokomeze vishawishi vyote vya madhambi. Vile vile inasisitiza mno mtu ajizuie kwa kutokana na elimu ya undani mwake na kwa kuipatia nafsi yake umbo la binadamu bora ambayo inamfanya apinge na kulaani aina yoyote ya dhuluma kwa adabu zote za mwanadamu na anahukumu kwa mujibu wa Shariah. Kwa kuongezea,Uislam haikatazi kutengeneza muswada kamili, wenye uhakika na kunjufu za vikwazo ambayo yatahusiana na ukweli kwa mujibu wa athari za jamii zao.

Tukirudia ukweli wetu huu, ni lazima tutafute kuwapo kwa utaratibu wa haki na kuepusha ukandamizwaji na kujiingiza katika haki za watu wengine. Katika hali kama hizo wakati mtu anapojiachia mwenyewe kuendeshwa kama kikaragosi ili kutenda ugaidi au uukandamizaji, basi atambue wazi kuwa ulimwengu mzima wa binadamu utasimama dhidi yake. Iwapo, hata hivyo, kama sisi tutashindwa kutimiza kiwango hiki, basi tiba zetu zote zitakuwa hafifu na kitulizo; ingawaje inaweza kutuliza maumivu, lakini hazitatokomeza sababu ya ugonjwa huo.

= Tamati =

Maswala ya kuzingatia

1. Tumeona kuwa ktafaruku katika serikali mbalimbali basi kikundi kimoja kinajitenga na kutoa maoni yao ya upnzani. Muda si muda, uhasama unavyozidi kuongezeka, mmoja mwenye uwezi zaidi anamwita mwenzake kuwa ni mgaidi na kuthubutu kupitisha sheria ya kutaka auawe. Hivyo kusababisha huyo kukimbilia nchi nyingine au kuanzisha vita vya msituni huku akiitwa mgaidi. Na baada ya harakati za muda, iwapo atapata ushindi akaweza kunyakua madaraka basi utaona wote wakimwita mheshimiwa, baba wa nchi, mkombozi sasa ukweli na haki ipo wapi ?

2. Kuna nchi moja inayo sheria au kanuni Tano kuu.

• Kanuni ya kwanza inasema kuamini katika Mungu wakati harakati zake zote zinatumbukia katika uadui na Mungu na kuhujumu sheria za Mungu (Din)

• Kanuni ya pili inasema Uzalendo inamaanisha kuwageuza watu kwa mujibu wa taratibu za kipagani za kijahiliyyah - mchanganyiko wa masiha kabla ya Uislamu na Umagharibi.

• Kanuni ya tatu inasema Ubinadamu inakuja kumaanisha kuwa Majenerali, jamaa na marafiki zao, mabwana zao na watawala tu ndio watu wanaostahili kuitwa binadamu na wapewe heshima na haki zote za kibinadamu.

• Kanuni ya nne inasema kuwa Demokrasia kushirikisha umma inamaanisha kuwa umoja wa kamati za kutawala na wadhalimu ndio chombo halali.

• Kanuni ya tano inasema Haki kwa jamii nzima inamaanisha kuwa majenerali wote ni watu wema na wenye huruma na kamwe hawatakubali wanyonge wafe kwa njaa.

Kwa hakika hizi ndizo serikali nyingi humu duniani ambazo ndizo zinazowajibika kuubuka makundi ya upinzani nchini mwao na hatimaye kuhatarisha amani na usalama wa taifa zima kwa ujumla. Hivyo inawabidi wao wakae na kutafakari sababu zinazowazaa magaidi kabla ya kutafuta mbinu za kuwatokomeza.

3. Serikali nyingi duniani kwa makosa yao wenyewe wanawakamata watu ovyo na kuwaweka vizuizini na hata kuwapoteza wengine kwa kuwaua. Jambo ambalo linawakasirisha wapinzani wao ambao wanajitolea mhanga kutenda matendo ya kuhujumu Serikali hizo kama vile kulipua mabomu, kuteka nyara n.k. Hapa pia inabidi pande zote mbili zikae na kutafakari hali ya kuweza kukomesha uhasama wao kwani kuna hatari ya raia wasio na hatia kupoteza mali na maisha yao.