read

Toba Hukubaliwa Kwa Kumtawassuli Imam Hussein a.s.

Makala haya yamekusanywa na kutarjumiwa na:

Amiraly M.H. Datoo (PO Box 838 Bukoba, Tanzania)

*****

Makala hii ni fupi sana lakini inaelezea namna Toba yetu inaweza kukubalika na dhambi zote kusamehewa.

*****

Sisi huwa daima tunaomba, "Ewe Mola wetu! Tujaalie Tawfiqi ya Toba ili tuweze kusamehewa madhambi yetu na kiza cha moyo wetu kuondoka."

Wakati tuombapo, huwa hatujui iwapo dua yetu ni Tawbatan Nasuuha au imekubalika kutufanya tusamehewe madhambi yetu yote. Hapo hapana haja ya kuhangaika kwani inatubidi kulia sana na vile vile kumtawasuli Imam Hussein (a.s.) kwa kuomba msamaha wa madhambi yetu. Ipo riwaya isemayo kuwa,moyo wowote ule ulio katika hali ya kuhuzunika kwa mateso yaliyompata Imam Hussein (a.s.) na ahali yake na wafuasi wake, basi Allah (swt) huirehemu kwa baraka za Imam Hussein (a.s.).

Imam Ja'far as-Sadiq (a.s.) amesema: "Atakayemkumbuka Imam Hussein (a.s.) na kutokwa na machozi walau kidogo sana, basi atapewa malipo yake kutoka kwa Allah (swt) na ataridhiwa Jannati (peponi)! (Thawabul a'amaal Na. 631 aya ya 2).

Lakini kumlilia Imam Hussein (a.s.) peke yake haimaanishi kuwa ni uokovu, bali itatubidi kujibu maswali juu ya haki za watu, madhambi makuu (dhunub al-kabira) hadi hapo tutakaponuia kwa moyo thabiti wa kuacha madhambi na kutenda mema ndipo tufanye tawba kamilifu.

Baadhi ya riwaya zinasema kuwa madhambi yote yatasamehewa ila madhambi makuu. Madhambi hayo makuu kamwe hayataweza kusamehewa ila kwa Toba kamilifu.

Na hii ndiyo maana Allah (swt) amechukua ahadi ya tawba tu:

Kwa hakika, Allah (swt) husamehe dhambi zote kwa pamoja (Sura az-Zumar, 39:53)

Na rejeeni kwa Mola wenu... (39:54)

Kwa hivyo kutokana na tawassul au Shafa'a kunaweza kusamehewa madhambi ili mtu asiseme kuwa yeye anayo madhambi mengi na hivyo ataingia Motoni tu, hivyo inambidi atambue wazi wazi kuwa kuomba msaada wa Imam Hussein (a.s.) kutamfanya kusamehewa madhambi yake na hivyo inambidi awe mwenye kutegemea msamaha wake Allah (swt).

Inambidi kila mtu ajiepushe na mapotoshi ya shetani kwa kila hali na hivyo tujitahidi kufanya Toba. Iwapo baada ya juhudi zetu hizi kutabakia kasoro zozote zile, basi Allah swt atatusamehe kwa msaada wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) na Ahali yake watukufu (a.s.)

Hapa nitapendekeza kusomwa vitabu vilviyoandiikwa katika lugha ya Kiswahili:

(1) Uchunguzi juu ya Uwahhabi Kilichoandiikwa na Sheikh Ja'afar Subhanii na kilichotolewa na Ahlul Bayt (a.s.) Assembly of Tanzania P.O.Box 75215 Dar Es Salaam na

(2) Upotofu wa madhehebu ya Wahhabi na hatari zake Kilichoandikwa na Khalifa M. Hamisi Mohammad na kilichotolewa na Sherman Islamic Book Stall P.O.Box 5444 Dar es Salaam Tanzania E.A.

Katika vitabu hivyo utaweza kusoma mengi pamoja na: Maana ya Wasila, Itsighatha (kuomba msaada kwa viumbe): Tawassul; kumzuru Mtume s.a.w.w. Madina; Mtume (s.a.w.w.) yu hai kaburini mwake; kuomba shafa'a (yaani kuombewa) siyo Shirki.

Ningalijaribu kuyadondoa machache hapa lakini itahitaji nafasi kubwa na si rahisi kuchukua machache kuyaacha mengi yaliyomo.