read

Ukweli kuhusu Uislamu na Ushia
Wanachosema wasiokuwa Waislamu kuhusu… Uislamu

Makala hii inaeleza ‘Maoni Chanya’ ya watu mashuhuri kuhusu Dini ya Uislamu kama ni Dini yenye Mwongozo kamilifu ya mwanadamu.

Translated by:
Dr M S Kanju
Al`Itrah Foundation
P O Box 1017
Dar es Salaam
Tanzania
Tel 255 22 2110640
Email alitrah@daiichicorp.com
Website www.alitrah.org

Dini inayokuwa haraka sana ulimwenguni

Huu ni mkusanyo mfupi wa nukuu kutoka kwa watu mashuhuri mbali mbali wasio Waislamu, wakiwemo wasomi, waandishi mafilosofa, washairi, wanasiasa, na wanaharakati wa Mashariki na Maghribi. Kwa tunavyojua hakuna hata mmoja aliyewahi kuwa Mwislamu. Kwa hiyo maneno haya huonesha maoni yao binafsi juu ya vipengele mbali mbali vya Uilsmau.

Sarojini Naidu (1879-1949)
Mwandishi mshairi na mmoja wa viongozi wenye kuonekana zaidi wa kabla ya Uhuru wa India. Rais wa National Congress ya India na gavana wa kwanza mwanamke wa India huru.

• “Hali ya uadilifu ni moja ya fikra nzuri mno za Uislamu kwa sababu kila nikisoma katika Quran huona zile kanuni zenye nguvu za maisha, sio fumbo bali maadili ya kiutendaji kwa ajili ya uendeshaji wa maisha uliofaa kwa ulimwengu wote.”

• Ilikuwa ni dini ya kwanza kuhubiri na kutekeleza demokrasi, ndani ya Misikiti wakati mwito wa Salat (Adhana ) unaposikika na wenye kuabudu wanapokusanyika pamoja, demokrasi ya Uislamu imeunganishwa mara tano kwa siku wakati mkulima masikini na mfalme wnapopiga magoti sambamba na kutamka: “Mungu peke yake ndiye Mkubwa.” Nimeshangazwa sana tena sana kwa muungamo huu wa Uislamu usiokatika ambao humfanya mtu kwa silika kuwa ni ndugu”.

[Lecture on “The Ideals of Islam.” angalia khutuba na maandishi ya Sarojini Naidu, Madras, 1918 uk. 167-9]

* * * *

Arnold J. Toynbee (1889-1975)
Mwanahistoria wa Kiingereza, mhadhiri wa chuo kikuu cha Oxford.

• “Kukomeshwa kwa dhamiri ya utaifa kati ya Waislamu ni moja ya mafanikio makubwa ya Uislamu, na katika ulimwengu huu huu kama inavyojitokeza kuna kilio cha haja ya kuhubiri maadili haya ya Ki-Islam.”

[Civilization on trial, new York, 1948, P 205]

* * * *

William Montgomery Watt (1909- 2006 )
Profesa (wa heshima) wa masomo ya Ki-Arabu na ki-Islamu kwenye chuo kikuu cha Edimburgh.

    • Mimi sio Mwislamu katika hali halisi, ingawa natumaini ni Mwislamu kama mtu aliyejisalimisha kwa Mungu, lakini naamini kile kilichotiwa ndani ya Qur’ani na maelezo mengine ya maono ya Ki-Islamu kwamba ni bohari kubwa za ukweli wa Mungu ambao kwamba mimi na watu wengine wa magharibi bado tunayo mengi ya kujifunza, na kwa hakika Uislamu ni mshindani mwenye nguvu wa utoaji wa mfumo wa msingi wa dini moja ya baadae.”

[Islamic and Christianity Today, London, 1983, p. ix]

* * * *

Bertrand Russel - (1872-1970)
Filosofa wa Kiingereza, Mwanahisabati, na tunzo ya Nobel ya Laureate, ambaye kwamba msisitizo wake juu ya uchambuzi wa kimantiki kwa kiasi kikubwa sana umeshawishi mwenendo wa filosofia ya karne ya 20.

• “Utumiaji wetu wa msemo “zama za giza” kuelezea kipindi cha kuanzia 699 mpaka 1.000 huonyesha kujishughulisha kwetu mno na ulaya ya magharibi… Kuanzia India mpaka Spain ustaarabu mzuri sana wa Ki-Islamu umestawi. Kilichopotea kwenye ukristo wakati huu, hakikupotea kwenye Ustaarabu, bali kinyume chake kabisa… Kwetu sisi huonekana kwamba ustaarabu wa ulaya ya magharibi ndio ustaarabu, lakini huu ni ufinyu wa mawazo.

[History of Western Philosophy, London, 1948, p. 419]

** * *

Hamilton Alexander Roskeen Gribb - (1895-1971)
Mwanachuoni mutashiriki anayeongoza wa wakati wake.

• “Lakini Uislamu bado una huduma zaidi ya kutoa kwenye mwenendo wa ubinadamu. Hata hivyo umesimama karibu zaidi upande wa mashariki kuliko ulaya inavyofanya, na una utamaduni mkubwa wa kuelewana na ushirikiano kati ya jamii na jamii. Hakuna jamii nyingine ambayo ina sifa ya mafanikio ya kuungana katika usawa wa hadhi, fursa na katika juhudi nyingi mno na jamii nyingi mbali mbali za binaadamu . Uislamu bado una uwezo wa kuunganisha kwa wazi elementi zilizotengana za taifa na utamaduni. Kama upinzani wa kale na kale wa jamii mkubwa za mashariki na magharibi ungebadilishwa na ushirikiano, upatanisho wa Uislamu ni shariti lenye kukubalika. Katika mikono yake liko suluhisho kubwa sana la tatizo ambalo kwamba Ulaya inakabiliana katika uhusiano wake na Mashariki .”

[Whither Islam, London 1932,P.379]

• “Kwamba mageuzi yake (Muhammad) yamezidisha hadhi ya wanawake kwa ujumla, (hilo) hukubalika kwa wote.”

[Mohammedanism, London, 1953, P.33]

*****

James A. Michener.(1907-1997)
Mwandishi anayeongoza wa Kimasikani, mpokeaji wa shahada za heshima ya udaktari katika fani tano kutoka vyuo vikuu thelathini na pamoja na tunzo ya medali ya Rais ya Uhuru (Presidential Medal of freedom) tunzo la kiraia la juu kabisa la Amerika.

• “Hakuna dini nyingine katika historia iliyoenea haraka sana kama Uislamu. Watu wa Magharbi wameamini zaidi kwamba ueneaji huu wa dini ulifanywa uwezekane kwa upanga. Lakini hakuna mwanachuoni wa kisasa anayekubali wazo hilo, na Qur’an kwa uwazi kabisa inaunga mono Uhuru wa dhamiri.”

[Islam- The Misunderstood Religion, Readers’ Digest ( American Edition)May 1955]

****

Edward Gibbon (1737-1794)
Anachukuliwa kama mwanahistoria mkubwa wa Kiingereza wa wakati wake.

• “’Naamini katika Mungu Mmoja na Muhammad Mtume wa Mungu’, ni ungamo jepesi na lisilo badilika la Uislamu. Mfano wa kielimu wa Mungu kamwe haujatwezwa kwa sanamu linaloonekana; utukufu wa Mtume kamwe haukupituka kipimo cha maadili ya mwanadamu, na maisha yake ya maadili yamezuia shukurani za wafuasi wake ndani ya mipaka ya akili na dini.”

[History of the Saraan empire, London1870-54]

 “Halisi zaidi kuliko mfumo wa Zoroasta, wenye mawazo mapana na huru zaidi kuliko sheria ya Musa, dini ya Muhammad yaweza kuonekana kwamba haikinzani sana na akili kama itikadi ya fumbo na ya kidhana, ambayo katika karne ya saba imetweza wepesi wa Injil.i”
[The history of the Deline and fall of Roman Empire, vol.5.p 487]

*****

Javed Diamond
Profesa wa fiziolojia katika chuo kikuu cha UCLA school of Medicine, mpokezi wa tunzo ya Pulitzer prize for General Non- fiction katika 1998

• “Uislam wa zama za kati uliendelea kitekinolojia, na (milango) wazi kwa ijitihadi, umefanikiwa kwa mbali zaidi katika viwango vya elimu kuliko wenzi wao wa ulaya, umenyonya urithi wa ustaarabu mkubwa wa kigiriki mpaka kufikia hatua ambayo kwamba vitabu vingi vikubwa sasa vimejulikana kwetu kwa kupitia tu nakala za ki-Arabu. Uligundua kinu cha upepo, trigonometria, tanga la pembe tatu, na wakafanya maendeleo makubwa katika ufuaji, ufundimitambo na uhandisi kemikali na njia za umwangiliaji. Katika zama za kati mtiririko wa tekinolojia ulikuwa ukiingia kwa nguvu kutoka kwenye Uislamu kwenda Ulaya kuliko kutoka Ulaya kwenda kwenye Uislamu. Ni baada tu ya miaka ya 1500 ndipo mwelekeo wa mtiririko ukaanza kwenda kinyume.”

[Guns, Germs and Steel-The fates of Haman Societies 1997, P 253]

* * * *

Annie Besant (1847-1933)
Mwanateosofia wa Kiingereza na kiongozi mzalendo katika India, Rais wa India National Congess l 917

• “Mara nyingi huwa nafikiri kwamba mwanamke yuko huru zaidi katika Uislamu kuliko katika Ukristo. Mwanamke amehifadhika zaidi na Uislamu kuliko alivyohifadhiwa na imani inayohubiri mke mmoja. Katika Qur’an sheria kuhusu mwanamke ni ya haki na ya uhuru zaidi. Ni katika miaka ishirini tu iliyopita ndipo wakristo wa Uingereza, wanatambua haki ya mwanamke kumiliki mali, ambapo Uislamu umeruhusu haki hii kuanzia mwanzo”

[The life and Teachings of Muhammad Madras 1932 p. 25-26]