read


Wanaopendwa Na Wasiopendwa Na Allah
Makala haya yametarjumiwa na kushereheshwa na:
Amiraly M.H.Datoo
P.O.Box 838
Bukoba – Tanzania

Makala hii fupi imeweka bayana kina nani wanaopendwa na Allah swt na kina nani wasiopendwa kwa dalili za aya za Qur’ani.

Wale Wanaopendwa Na Allah Swt

Hadithi hii ilisomwa na :
Sheikh Akmal Hussein Taheri – Bukoba

1. Allah swt huwapenda wafanyao ihsani, Al-Qur’an Sura Al-Baqarah (2) Aya 195
‘Wa-ahsinu Innallaha yuhibbul muhsiniin
Hakika Allah huwapenda wafanyao wema

2. Allah swt huwapenda wafanyao Tawba, Al-Qur’an Sura Al-Baqarah (2) Aya 222
‘Innallaha yuhibbut-tawwabiina wa yuhibbul muta-tahhiriina
Hakika Allah huwapenda wanaotubu na huwapenda wanaojitakasa.

3. Allah swt huwapenda watimizao ahadi wazitoazo, Al-Qur’an Sura Aali Imran (3) Aya76
‘Balaa Man awfa biahdihi wat-Taqaa fa-innallaha yuhibbul Muttaqiin
….. Allah huwapenda wajilindao

4. Allah swt huwapenda wafanyao subira, Al-Qur’an Sura Aali-Imran Aya (3), 146
‘Innallaha yuhibbus-Saabiriin
Na Allah anawapenda wafanyao subira

5. Allah swt huwapenda wenye nia halisi, Al-Qur’an Sura Aali-Imran (3), Aya 148
‘Wallahu yuhibbul Muhsiniin
Allah anawapenda wafanyao mema

6. Allah swt huwapenda wenye kufanya al-faaf, Al-Qur’an Sura Al-Maidah (5), Aya 42
‘Innallaha yuhibbul Muqsitiin
Bila shaka Allah anawapenda waadilifu.

7. Allah swt huwapenda wenye taqwa , Al-Qur’an Sura Al-Tawbah ( 9 ) Aya 4
‘Wa’alamu annallaha ma’al Muttaqiin
Allah anawapenda wanaomuogopa.

Wale Wasiopendwa Na Allah Swt

Hadithi hii ilisomwa na :
Sheikh Akmal Hussein Taheri – Bukoba

1. Allah swt hawapendi wafasiqi, Al-Qur’an Sura Saffa’ (61), Aya 5
‘Wallahu la yahdil qawmal faasiqiin
Allah hawaongozi watu waovu

2. Allah swt hawapendi wafasidi, Al-Qur’an Sura Al-Maidah (5), Aya 64
‘Wallahu la yuhibbul Mufsidiin
Allah swt hawapendi waharibifu

3. Allah swt hawapendi wadhalimu, Al-Qur’an Sura Al-Tawba ( 9 ) , Aya 19
‘Wallahu la yahdil qawma-dhalimiin
Allah hawaongozi qaumu dhalimu

4. Allah swt hawapendi wasaliti, Al-Qur’an Sura Al-Haj (22), Aya 38
‘Innallaha la yuhibbu kulla khawanina kafur.
Allah hampendi kila haini, asiyeshukuru

5. Allah swt hawapendi wenye kiburi, Al-Qur’an Sura An-Nahl (16 ), Aya 22
‘Innallaha la yuhibbul Mustakbiriin
Kwa hakika Yeye hawapendi wanaotakabari