Mungu wa Biblia

Je, wewe unaona huyu Mungu wa Biblia ni wa namna gani? Kama Mungu anao mwili, nywele na vazi , anaishi katika mahala, hajui kitu kilichojificha nyuma ya mti , anadanganya watu, huvunja ahadi yake, je binadamu yukoje?

Swali: Ati Mwenyezi Mungu ana sura ya binadamu?

Jibu: Sivyo Kamwe. Lakini katika Biblia kitabu cha kwanza kiitwacho Mwanzo, Sura ya 1, aya ya 26 na 27, Imeandikwa hivi: “Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu na Mungu alimwumba, Mwanamume na Mwanamke aliwaumba.”

Swali: Ati Mwenyezi Mungu anazo nywele? Anacho kivazi?

Jibu: Sivyo kamwe. Lakini katika Biblia kitabu cha Danieli, Sura ya 7, Aya ya 9, imeandikwa hivi: “Ni katazama hata viti vya enzi vikawekwa, na Mmoja aliye mzee wa siku (Mwenyezi Mungu) ameketi, mavazi yake yalikuwa meupe kama theeluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi

Swali: Ati Mwenyezi Mungu anayo miguu miwili?

Jibu: Sivyo Kamwe. Lakini katika Biblia kitabu cha kutoka sura ya 24, aya ya 10, Imeandikwa hivi: “Wakamwona Mungu wa Israeli: chini ya miguu yake palikuwa na kama sakafu iliyofanyizwa kwa yakuti samawi… Nao wakamwona Mungu, wakala na kunywa.”

Swali: Ati Mwenyezi Mungu ana pahala ambapo anaonekana?

Jibu: Sivyo kamwe. Lakini Biblia katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana, Sura ya 4, aya ya 2, Imeandikwa hivi: “Na mara nalikuwa katika Roho: na tazama, Kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kiti: na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe laq yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi.”

Swali: Ati Mwenyezi Mungu hutembea?

Jibu: Sivyo kabisa. Lakini katika Biblia Kitabu cha Kwanza kiitwacho Mwanzo, sura ya 2, aya ya 8, imeandikwa hivi: “Kisha wakasikia (Adamu na mkewe) sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga. Adam na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone."

Swali: Ati Mwenyezi Mungu hutembea?

Jibu: Sivyo Kamwe. Lakini katika Biblia Kitabu cha Pili kiitwacho kutoka, sura ya 19, aya ya 20, imeandikwa hivi: “Bwana akaushukia mlima, Bwana akamwita Musa aende hata kilele cha mlima. Musa akapanda juu.”

Swali : Ati Mwenyezi Mungu huteremka juu ya wingu na anakwenda mbele ya mtu?

Jibu: Sivyo kabisa Biblia Kitabu cha Pili kiitwacho “Kutoka” katika sura ya 34 aya ya 5 na 6, imeaandikwa hivi: “Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana. Bwana akapita mbele yake.”

Swali: Ati Mwenyezi Mungu huchagua mahala pa kukaa yeye?

Jibu: Sivyo kabisa. Lakini katika Biblia Kitabu cha Zaburi ya 132, aya 13, imeandikwa hivi: “kwa kuwa Bwana ameitamani akae ndani yake.”

Swali: Ati Mwenyezi Mungu mjinga? Hapambanui kati ya milango ya wenye kuamini na makafiri ila kwa alama?

Jibu: Sivyo Kabisa. Lakini Biblia Kitabu cha Pili, Kiitwacho Kutoka, sura ya 12, aya ya 12 na 13, imeandikwa hivi: “Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wanadamu na wanyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lolote likawaharibu nitakapoipiga nchi ya Misri.”

Swali: Ati Mwenyezi Mungu hawezi kujua kwamba mtu amejificha katika mti? Vile vile hajui nani amemfundisha binadamu?

Jibu: Sivyo kabisa. Lakini Biblia katika kitabu cha Mwanzo sura ya 3, aya 9-11, imeandikwa hivi, “Bwana na Mungu akamwita Adamu, akamwambia uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi, nikajifificha. Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi?”

Swali: Ati Mwenyezi Mungu anavunja ahadi zake?

Jibu: Sivyo kabisa. Kuvunja ahadi ni aibu kubwa. Lakini Biblia katika Kitabu cha Kwanza cha cha Samweli, Sura ya 2, aya ya 30 na 31, imeandikwa hivi: “Kwa sababu hiyo, Bwana, Mungu wa Israel, asema, “Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele:lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe mbalinami…Angalia, Siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa mbali ya baba yako, hata nyumbani mwako hatakuwa mzee.” Mungu yu mbali na uzushi huu juu yake. Kama vile, ati aliwaahidi Eli kwamba ukuhani wake ulikuwa wa maisha juu yake na wanawe, lakini baadaye hayo hayakutekelezwa.

Na vilevile katika sura ya 13, aya 13 imeandikwa hivi:
“… Bwana angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele. Lakini sasa ufalme wako hautadumu.”

Mungu yu mbali na uzushi huu juu yake kama vile, ati alimwahidi Sauli ufalme wake kuwa imara milele, na baadaye akavunja ahadi na akampa ufalme mtu mwingine.

Swali: Ati upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu?

Jibu: Sivyo Kabisa. Mwenyezi Mungu si mpumbavu kamwe, basi vipi itakuwa upumbavu wake una hekima zaidi ya wanadamu: Lakini Biblia katika Waraka wa Kwanza wa Mtume Paulo kwa Wakorintho, sura ya kwanza, aya ya 25, imeandikwa hivi: “Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu.”

Swali: Mwenyezi Mungu hujuta akisha tenda jambo?

Jibu: Sivyo Kabisa. Lakini Biblia katika Kitabu cha Kwanza cha Samweli, Sura ya 15, aya ya 10 na 11, imeandikwa hivi, “Ndipo neno la Bwana likamjia Samweli, kusema, “najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe Mfalme.”

Swali: Ati Mwenyezi Mungu husikitika na kuwa na majonzi kwa kitendo alichofanya?

Jibu: Sivyo kabisa. Lakini katika Biblia Kitabu cha Mwanzo, Sura ya 6, aya ya 6 na 7, imeandikwa hivi: ‘Bwana akaghairi kwa kuwa amefanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. Bwana akasema, “Nitamfuatilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi.”

Swali: Ati Mwenyezi Mungu hushinda mweleka na mtu?

Jibu: Sivyo kabisa. Lakini Biblia katika Kitabu cha Mwanzo, sura ya 32, aya ya 24 na 28, imeandikwa hivi: Yakobo akakaa peke na mtu mmoja akaashindana naye mweleka hata alfajiri.. Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana unashindana na Mungu.”

Swali: Ati Mwenyezi Mungu husema uwongo hali nyoka husema kweli?

Jibu: Sivyo Kabisa. Lakini Biblia Katika kitabu cha Mwanzo, sura ya 3, aya ya 3 hadi ya 6 , imeandikwa hivi: Lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani. Mungu amesema , msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na baya.”

Baadaye imeelezwa kwamba Adamu na Hawa baada ya kula matunda ya mti huo, wakawa hai … yameelezwa mambo ambayo si shani ya Mwenyezi Mungu kuambiwa hivyo.

Swali: Ati Mwenyezi Mungu hushuka kutoka mbinguni ili kuchafua umoja wa watu ili wasisikilizane kwani anaogopa umoja wao?

Jibu: Sivyo, sivyo kabisa mara elfu. Lakini Biblia katika Kitabu cha Mwanzo, Sura ya 11, aya ya kwanza hadi 9, imeandikwa hivi: “Nchi yote ilikuwa na na lugha moja na usemi mmoja. Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambalale katika nchi ya Shinari, wakakaa huko. Waliambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni tujifanye jinaa: ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha moja : na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno
Wanalokusudia kulifanya, Haya, na tushuke huko huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno yao. Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni paa nchi yote . wakaacha kujenga ule mji. Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Baabeli.”

Swali: Ati Mwenyezi Mungu husema kitu baadaye akafanya mengine?

Jibu: Sivyo Kabisa. Lakini Biblia katika Kitabu cha Mwanzo, Sura ya 6, aya ya 3, inasemaa hivi: Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na wanadamu milele kwa kuwa yeye naye ni nyama: basi siku zake zitakuwa miakaa mia na ishirini.”
Hayo yalikuwa mwanzo wa kuumba Binadamu, hebu tutazame, Mungu alifuata ahadi yake? Biblia inasema Mungu aligeuza maneno yake, Kwa hivyo watu wengi waliishi juu ya umri alioahidi Mungu. Kwa mfano, imeandikwa katika Mwanzo, Sura ya tisa, aya ya ishirini nia nne (mwa 9:28), kwamba, “Na Nuhu akaishi baada ya ile ghaarika miaka mia tatu na hamsini. Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafaa.”