Khadija-tul-Kubra

Author(s): 
Publisher(s): 

Maisha ya Khadija yamejaa utajiri wa mwongozo wa kimungu. Sifa yake kubwa katika maisha yake ya kiutakatifu, ilikuwa ni imani yake isiyo na kifani katika Uislamu. Imani yake ilikuwa kama jabali katika bahari iliyochafuka.

Imani za watu wachache kamwe hazikuwekwa katika mtihani mkali kama ile imani ya Khadija. Imani yake ilijaribiwa kwa njaa, kiu, uhamisho na hatari kubwa katika maisha yake na kwa wapendwa wake. Kusema kweli, wakati wa kwanza wa mika kumi ya Uislamu, maisha yake yalikuwa ya mfululizo wa mitihani isiyo na mwisho.

Khadija alifuzu katika mitihani yote. Ufunguo kwenye mafanikio yake ilikuwa ni upendo wake kwa Mungu, mapenzi kwa mume wake na kuji¬tuma kwake ili kuufanya Uislamu ufanikiwe.

Khadija aliweka mfano ambao wanawake katika Uislamu wanaweza kuuiga mpka mwisho wa dunia. Wanawake wanweza kuona katika maisha yake vipi mu'mun wa kweli anavyoweza kufanya tabia ya maisha yake kuwa bora sana na ya utukufu.

Translator(s): 
Category: 
Topic Tags: 
Person Tags: 

Utangulizi

Khadija, mke wa kwanza wa Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na Muumini wa kwanza, ambaye alikuwa na hisia za mtu asiye wa kawaida kabisa. Aliwajibika sana katika histo­ria ya uchanga wa Uislamu. Alikuwa yeye pamoja na Abu Talib, mmoja miongoni mwa watu wawili wafadhili wakubwa kabisa wa Uislamu na Waislamu. Wakati ambapo Uislamu ulikuwa kwenye shinikizo la utekwaji wa kudumu; na ulikuwa umezingirwa kwa kipin­di cha mfululizo wa miaka mitatu, aliudhamini kwa kujitolea kwake mhanga wa kushangaza sana.

Uthabiti wake usiobadilika, ushupavu wake, kuwa na uwezo wa kupeleka fikra mbali ya siku za usoni, na uthabiti wa imani yake kwa Mwenyezi Mungu, na kwa ujumbe wa Muhammad Mustafa - Mjumbe wake wa mwisho na mkubwa kuliko wote - haya mambo yalikuwa lazima yawepo kwani humo ndimo Uislamu uliegemea kwa kipindi cha miaka kumi ya mwanzo wake.

Kwa sababu zisizoeleweka, nafasi ya Khadija - ambayo ndiyo ilikuwa kiini cha kujenga hatima ya Uislamu- haijatambuliwa ipasavyo, kutoka kwa waandishi wengi wa wasifu na wanahistoria wa Kiislamu. Utambulisho kama huo ambao wameutoa, ni wa majaribio tu na bila uangalifu. Kwa kadiri ya ninavyo elewa na imani yangu mimi, wasifu halisi na sahihi wa Khadija, bado haujachapishwa. Huu ni upungufu mkubwa wa kusikitisha kwenye mvuto wa maandiko ya Uislamu, husu­san wakati ambapo katika nchi za Magharibi kuna mwamko mkubwa wa imani ya Uislamu, na katika simulizi zinazohusiana na viongozi wake katika siku zake za mwanzo.

Maandishi yaliyopo hadi leo juu ya maisha ya Khadija katika vyanzo mbalimbali ni machache na vipandepande. Hata haya maandishi machache na vipande pande sio salama kutokana na maelezo yasiy­obadilika au tafsiri potofu ya historia. Mwandishi wa wasifu au mwana historia, lazima alete hali ya msisimko ya kuelewa Uislamu sahihi, na lazima afanye makadirio ya haki ya majukumu ya watu wale ambao wameitengeneza historia yake.

Khadija ni mmoja wa watu waliokuwa na uwezo mkubwa na muhimu katika historia yote ya Uislamu. Haiwezekani kuzungumzia historia ya Uislamu bila kuyataja mambo aliyoyafanya kama mchango wake uliofanikisha Uislamu kuendelea kuwepo, kuimarika, na hatimaye kupata ushindi.

Uislamu una deni lisilolipika kwa Khadija. Kwa hiyo, ninaamini kwam­ba kuchapishwa kwa wasifu wa Khadija - unaoakisi moyo wa kisayansi na kanuni za kisayansi -ambazo wakati fulani niliziona kuwa za muhimu, sasa zinawakabili waandishi wa wasifu na wana historia wa Kiislamu kama sharti la ziada.

Sababu nyingine kwa nini inawalazimu Waislamu wote kupata fursa ya kuijua historia ya maisha ya Khadija, ni kwamba, kama alivyo mumewe, Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) yeye pia ni alama ya umoja wa umma wake. Yeye (Khadija) ni alama ambayo hulea umoja wa umma wa Waislamu.

Juhudi imefanywa kwenye kitabu hiki kuweka pamoja maandishi yote yale juu ya maisha ya Khadija, ambayo yalipatikana katika vyanzo vingi vilivyotawanyika huku na huko.

Lakini, hili ni juhudi ambayo lazima likubaliwe kwamba haina matumaini ya kutoshelezea. Huelekeza kwenye mukhtasari tu-ambao utakuwa ni wa kusomwa tu. kwa ajili ya rejea, mpaka hapo wakati utakapokuwa ambako maandiko sahihi zaidi juu ya somo hili yatakapo patikana.

Hata hivyo, ni muhimu kwa Waislamu wote, hususan wanawake wa Kiislamu, wajue historia ya maisha ya Khadija na jinsi alivyotumikia Uislamu. Aliunganisha nafsi yake na Uislamu kwa ustadi wa hali ya juu sana hivyo kwamba Khadija alikuwa moyo na kiini cha Uislamu.

Kwa maana halisi, Khadija aliishi na kufa kwa ajili ya Uislamu.

Kama wanawake wa Kiislamu wanatafuta furaha hapa duniani na wokovu baada ya kufa, lazima waishi kwa kuiga maisha ya utakatifu wa Khadija. Yeye ni kiongozi wa siri ya kufuzu kupata radhi ya Mwenyezi Mungu; na yeye ndiye mwenye ufunguo utakao wafungulia wao milan­go ya kufuzu katika sehemu mbili, duniani na Akhera. Angefurahi kugawana nao 'siri' hii, kama watataka kujua siri hiyo ni nini, na atafu­rahi kuwapa 'ufunguo' huo, kama watautafuta kutoka kwake.

Mwenyezi Mungu na amrehemu Khadija na familia yake.

Neno La Mchapishaji

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la"Khadija-tul-Kubra) kilichandikwa na Mwanachuoni mwanahistoria na mtafiti, Sayyed A. A. Razwy

Bibi Khadija alikuwa ndiye mke wa kwanza wa Mtukufu Mtume. Bibi huyu alikuwa tajiri miongomi mwa matajiri wakubwa wa Makka. Mtume alikuwa na miaka 25 alipomuoa bibi huyu, aliopofikisha miaka 40, alitoa tangazo la kwanza la utume wake, mtu wa kwamza kuamini utume wake alikuwa ni bibi Khadija, na hivyo kuamini Upweke (tawhid) wa Allah swt. Na kuwa Mwislamu wa kwanza ulimwenguni.

Waabudu masanamu wa Makka hawakufaurahishwa na tangazo hili, ukazuka uadui mkubwa sana kati ya Mtukufu Mtume na waabudu masanamu hawa. Kutokana na hali hii ilibidi Khadija atumie utajiri wake wote kuuhami Uislamu chini ya hifadhi kubwa ya ami yake Mtume, Abu Talib.

Mchango wa bibi huyu ni mkubwa sana katika Uislamu, lakini bahati mbaya yeye na Bwana Abu Talib wamekuwa ni madhulumu wa historia ya Uislamu. Si wanahistoria Mustashirik tu, bali hata wanahistoria wa Kiislamu wamekwepa kuandika wasifu wake kwa ukamilifu kama ambavyo wamekwepa kuandika kwa ukamilifu wasifu wa Bwana Abu Talib na kumsingizia ukafiri.

Katika kitabu hiki mwandishi ameandika angalau kwa kiasi cha kurid­hisha wasifu wa Bibi Khadija. Wasifu huu umeanzia kabla ya kuolewa na Mtukufu Mtume na baada ya kuolewa naye. Na mwandishi ameji­tahidi kuandika matukio muhumi yanayohusiana na bibi huyu, kwa kutumia vyanzo sahihi vya Kiislamu.

Kutokana na umuhimu wa maudhui ya kitabu hiki, tumeona tukutoe kwa lugha ya Kiswahili ili kizidishe mwanga wa elimu kwa Waislamu wazungumzaji wa Kiswahili.

Na hili ndilo lengo kubwa la Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' katika kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

Tunamshukuru Ndugu yetu al-Akhy Salman Y. Shou kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Mchapishaji:
Al-Itrah Foundation
S. L. P. 19701
Dar-es-salaam.

Sura Ya Kwanza: Makkah Mnamo Karne Ya Sita

Mnamo Karne ya Sita A.D. Makka ilikuwa soko muhimu Arabuni. Mji huu ulikuwa kituo cha kimataifa cha biashara na uchuuzi. Mizigo kuto­ka India yenye bidhaa kama viungo, matunda, nafaka, vyombo vya ufinyanzi na nguo vilikuwa vikiteremshwa kwenye bandari za Yemen na kutoka hapo bidhaa hizo zilibebwa pamoja na zile za Arabu ya Kusini, kama vile kahawa, dawa, manukato na mafuta mazuri kwa kutumia ngamia kwenda Makka, na kutoka hapo kuendelea Syria hadi nchi zili­zozunguka bahari ya kati.

Makkah yenyewe ilikuwa kituo cha misafara mingi ya "udi na ubani" ya Arabuni na "viungo" vya India. Misafara mingine ilipitia Makka na Yathrib wakati inaelekea kaskazini ambako iliungana na misafara ya njia kubwa ya biashara ya hariri toka China.

Misafara kutoka kaskazini, pia ilisimama Makka. Ngamia na farasi wal­ibadilishwa hapo na mahitaji kujazwa tena hapo na halafu misafara huendelea hadi kwenye bandari za kusini ya rasi ya Bahari ya Arabuni.

Aidha, Makka ilikuwa kituo cha kubadilishana mali na bidhaa kwa ajili ya makabila ya Kiarabu yasiyo hamahama na yale yanayo hamahama; na ilikuwa sehemu ya kugawa bidhaa za kilimo na zilizotengenezwa na kupelekwa katikati ya Hijaz.

Makabila hayo yalikuja kutoka mbali katikati ya Arabuni na hata Arabia ya mashariki kwa madhumuni ya kununua bidhaa hizo ambazo zilikuwa hazipatikani nchini kwao. Sehemu kubwa ya biashara hii ya maingiliano ya makabila ilifanyika Makka kwa mfumo wa kubadilishana mali kwa mali.

Makuraishi wa Makka walikuwa kabila muhimu sana kutoka Magharibi ya Arabuni. Wote walikuwa wafanyabiashara wakubwa. Kwa kufanik­isha usafirishaji wa hariri kutoka China, bidhaa kutoka Afrika Mashariki na vitu vya thamani kutoka India - Makuraish walitawala biashara kati ya ustaarabu wa Mashariki na ule wa nchi za Bahari ya Mediterania. Ni dhahiri kwamba sehemu kubwa ya biashara hii ilikuwa ya bidhaa za anasa, lakini bidhaa za kawaida pia zilikuwepo kwenye biashara, kama vile nguo za rangi za zambarau, majora ya nguo, nguo zisizowekwa urembo wa kufuma na zile ambazo ziliwekewa nakshi ya dhahabu, zafarani, melimeli, majoho, mablanketi, mishipi, manukato ya mgando, mvinyo na ngano.

Kwa jinsi hii, uzalishaji, uuzaji, ubadilishaji na usambazaji wa bidhaa, kuliwafanya Makuraishi kuwa matajiri. Lakini palikuwepo na kitu kingine kilichowafanya kuwa matajiri. Al-Kaaba na Jiwe lake Jeusi lilikuwa mashuhuri, vilijengwa mjini Makka. Waarabu walikwenda Makka kuhiji na kuitembelea Al- Kaaba. Kwao Makka ilikuwa takatifu kama vile Jerusalem ilivyokuwa kwa Wayahudi na Wakristo.

Al-Kaaba ilikuwa hekalu kubwa la miungu wa masanamu waliomiliki­wa na koo za makabila mbalimbali ya Kiarabu. Mahujaji walileta sada­ka nyingi na zisizo za kawaida kwa ajili ya kuwafurahisha wale miun­gu-sanamu waliowaabudu. Mahujaji waliporudi makwao, makuhani wa hekalu walichukuwa sadaka zote kuwa mali yao. Misafara ya hija ilikuwa njia moja yenye kuwaingizia mali nyingi sana raia wa Makka.

Hata kama Makuraishi wa Makka wasingejishughulisha na biashara, bado wangenufaika na kutajirika kwa kazi za kutoa huduma mbalimbali ambazo walizifanya kwa kipindi cha mwaka mzima kuhudumia misa­fara ya biashara na mahujaji kutoka Kusini kwenda Kaskazini na kuto­ka Kaskazini kwenda Kusini. Lakini kama ambavyo imekwisha fahamika mwanzoni Makuraishi wengi walikuwa wafanya biashara hodari, kwa hiyo walileta utajiri mwingi Makka kutoka nchi jirani.

Ingawaje wafanya biashara wa Makka walipeleka msafara mmoja tu Syria na mmoja Yemen kwa kipindi cha mwaka mzima, palikuwepo na misafara mingine mingi sana midogo midogo ambayo ilifanya biashara katika sehemu nyingi za ghuba ya Uajemi mwaka mzima. Mingi ya misafara hiyo ama ilianzia humo humo Makka au ilipitia Makka kwen­da sehemu nyingine. Kwa hiyo, kulikuwepo na msongomano mkubwa wa misafara ya biashara Makka.

Misafara ilitofautiana kwa ukubwa. Kuanzia Misafara ya "wenyeji" iliyo na kiasi cha chini kabisa ngamia kumi, mpaka ya misafara ya "kimataifa" yenye wingi wa ngamia kiasi cha kufikia maelfu. Kupanga misafara ya biashara ilikuwa shughuli kubwa katika Bara Arabu.

Sura Ya Pili: Maisha ya Mwanzo ya Khadija -tul-Kubra (R)

Khadija alizaliwa Makka. Alikuwa mtoto wa kike wa Khuwaylid bin Asad bin Abdul Uzza bin Qusayy. Qusayy alikuwa babu aliyejulikana sana kwenye ukoo wa Khadija vile vile kwenye ukoo wa Muhammad Mustafa, wa uzao wa Bani Hashim, aliyekuja kuwa Mtume wa Uislamu (S.a.w.). Kwa hiyo Khadija alitokana na nasaba yenye asili moja na Bani Hashim. Baada ya Bani Hashim, familia yake ilikuwa tukufu na yenye kuheshimika sana Arabuni pote. Familia ya Khadija haikuwa mashuhuri kwa utajiri tu bali pia kwa ubora wa tabia yake.

Khuwaylid, baba wa Khadija pia alikuwa mfanyabiashara kama wenza­ke wengine wengi wa kabila la Quraysh wa Makka. Kama walivyokuwa wafanyabiashara wa kabila la Qurayshi wengi, baba yake Khadija naye alipata mafanikio ya utajiri kutokana na biashara ya nje. Wafanyabiashara wa Makka walituma misafara miwili kila mwaka mmoja wakati wa kiangazi ambao ulikwenda Syria na mwengine wakati wa kipupwe ambao ulipelekwa Yemen.

Misafara hii ya kibiashara ilibeba mazao ya jangwani na bidhaa zilizo tengenezwa Makka na sehemu za jirani yake na ziliuzwa kwenye masoko ya Syria na Yemen. Aidha waliuza farasi-chotara Syria. Aina hii ya farasi ilithaminiwa sana Syria na nchi jirani. Baada ya kuuza bidhaa zao na farasi-chotara wao, wafanyabiashara hao walileta nafaka, mafuta ya zeituni, matunda, kahawa, nguo, bidhaa za anasa na vitu vingine vilivyotengenezwa kwa ajili ya kuviuza Makka. Hivyo walipata faida Syria, Yemen na Makka.

(Biashara hii ya Makka imetajwa kwenye Quran Majid, Sura ya 106)

Biashara ya nje ilikuwa ndio msingi mkubwa wa uchumi wa Makka. Makka ilikuwa haina ardhi ya kilimo wala maji ya kilimo cha umwag­iliaji. Watu wa Makka, katika hali hiyo, hawakuweza kulima mazao ya chakula. Walitegemea biashara baina yao na Syria na Yemen ili wajil­ishe. Kutokana na faida waliyopata walinunua nafaka na vitu vingine muhimu katika maisha.

Kila msafara ulikuwa na kiongozi. Kiongozi huyu alitakiwa kuwa mtu mwenye sifa zisizo za kawaida. Usalama na kufaulu kwa msafara kati­ka biashara ya mauzo na manunuzi, ilitegemea sana maamuzi ya kiongozi. Kiongozi alikuwa na kazi ya kulinda msafara usishambuliwe na wanyang'anyi na mabedui wa jangwani. Kiongozi aliweza kufanya kazi hii kwa kuandikisha wapiganaji kutoka makabila mbalimbali na kuunda vikosi kufuatana na ukubwa wa msafara. Vikosi vilisindikiza misafara mpaka mwisho wa safari. Misafara yote iliyokwenda masafa marefu, ilikuwa chini ya ulinzi wa kijeshi.

Kiongozi wa msafara pia alitakiwa kuwa na kipaji cha pekee kwa kumuongoza kwenye jangwa lisilo na njia wakati wa mchana, na ali­takiwa kuwa na uwezo wa kutambua njia ya msafara wakati wa usiku. Kiongozi alitakiwa kuwa na ujuzi wa kuzitumia nyota katika safari wakati wa usiku. Alikuwa anatakiwa kuhakikisha kuwepo kwa maji wakati wa safari ndefu ya kwenda Syria au kwenda Yemen. Alitakiwa kuchukuwa tahadhari dhidi ya majanga yasiyotegemewa kama vile kim­bunga cha mchanga na msongamano wa miale ya taa za misafara. Alikuwa anatakiwa kuwa na uwezo wa kutoa huduma ya kwanza ya tiba endapo msafiri aliugua au aliumia.

Kwa ujumla, kiongozi alitakiwa kuwa na uwezo wa kushughulikia dharura yoyote ile. Wafanyabishara wa Makka, walimteua kiongozi wa misafara yao baada ya kuchunguza historia yake kwa uangalifu sana. Jopo la wasafiri wazoefu lilipitia majina ya watu waliopendekezwa kwa kazi hiyo.

Jopo la wachunguzi halikuridhishwa na sifa yoyote iliyo chini ya kiwan­go cha uwezo wa kiongozi wa msafara kuongoza kwa ustadi kwenye njia zisizo na michoro kwenye "bahari" ya mchanga, na kufaulu kwake kurudisha misafara ya "meli za jangwa" yaani ngamia pamoja na mizigo yao nyumbani salama. Ili akubalike kwa jopo, mtahiniwa alitakiwa kuonyesha kwamba alikuwa na uzoefu wa kutosha sana kuhusu utarati­bu wa usafirishaji wa misafara ya biashara na "vitambulisho" vyake vil­itakiwa awe hana kosa.

Mama yake Khadija alikufa mnamo mwaka wa 575 A.D.,na Khuwayled baba yake, alikufa mnamo mwaka wa 585 A.D. Baada ya kifo cha Khuwayled, watoto wake walirithi utajiri wake na waligawana mali hiyo. Utajiri una hatari zake. Utajiri unaweza kumfanya mtu akaishi maisha ya kubweteka na anasa. Khadija alitambua tabia ya utajiri kwa undani, na aliamua kutoruhusu utajiri kumfanya yeye asifanye kazi.

Khadija alikuwa na akili ya kiwango kisicho cha kawaida na uwezo wa tabia ya kuishinda changamoto ya utajiri, na aliamua kujenga himaya ya urithi kutoka kwa baba yake. Alikuwa na ndugu wengi lakini miongo­ni mwa wote hao, ni yeye peke yake ndiye aliyerithi uwezo wa baba yao kuwa tajiri. Lakini alionyesha katika kipindi kifupi sana kwamba hata kama hangekuwa amerithi utajiri wa baba yake, bado angeweza kupata utajiri kwa bidii yake mwenyewe.

Baada ya kifo cha Khuwayled, Khadija alichukuwa kazi ya kusimamia biashara ya familia na aliipanua haraka sana. Faida aliyoipata aliwa­saidia fukara, wajane, watoto yatima, wagonjwa na wasiojiweza.

Endapo palikuwepo na wasichana fukara, Khadija aliwasaidia waolewe na aliwapa mahari.

Mmoja wa wajomba zake alijitolea kumsaidia kama mshauri wake katika kuendesha biashara, na ndugu zake wengine kati­ka familia pia walimsaidia katika biashara wakati wowote alipohitaji msaada wao. Lakini hakumtegemea mtu yeyote katika kufanya uamuzi. Khadija alitegemea zaidi uamuzi wake mwenyewe ingawaje alikubali kushauriwa na kufikiria namna ya kuutumia ushauri huo. Ndugu wakubwa katika familia walitambua kwamba alikuwa hapendi ubia.

Wafanya biashara wengi waliokuwa na mizigo ya kuuza Syria au Yemeni, walisafiri na misafara yao wenyewe na kushugulikia mauzo yao binafsi. Lakini wakati mwingine mfanyabiashara alishindwa kuon­doka Makka. Katika hali kama hiyo mfanyabiashara huyo alimkodi mtu kwenda na msafara badala yake. Mtu aliyeteuliwa kwa madhumuni haya, alitakiwa awe na tabia njema kwa uaminifu wake na uwezo wa kufanya biashara. Mtu wa namna hii aliitwa Wakala au Meneja.

Khadija alikuwa mtu wa nyumbani pia ndugu zake na binamu zake hawakupenda kusafiri na misafara. Kwa hiyo, alimuajiri wakala wakati wowote msafara ulipotoka kwenda nje (ya Hijazi), na kumfanya wakala huyo kuwa na madaraka ya kupeleka bidhaa zake kwenye masoko ya nje kuziuza huko.

Kwa uwezo mzuri wa kuteua mawakala, na kununua na kuuza wakati na mahali muafaka aliweza kupata faida kubwa sana, na baadaye, akawa mfanyabiashara tajiri sana wa Makka. Ibn Sa'ad anase­ma kwenye Tabqaat yake kwamba misafara ya wafanya biashara wa Makka ilipoanza safari, mzigo wa Khadija peke yake ulikuwa sawa na mizigo ya wafanyabishara wengine wote wa Qurayish katika msafara huo.

Alikuwa dhahiri kwa kila mtu ni kama msemo "golden touch" ("mguso wa dhahabu") yaani kila atakacho kigusa hata kama ni vumbi litageuka kuwa dhahabu. Watu wa Makka, katika hali hiyo, walimpa jina la Malkia wa Qurayish. Aidha walimwita Malikia wa Makka.

Wakati huo Bara Arabu ilikuwa jamii ya kipagani, na Waarabu wali­abudu masanamu mengi na miungu masanamu, ambao waliamini walikuwa na uwezo wa kuleta bahati njema kwao. Lakini ibada yao ya kuabudu masanamu haikuwa adilifu na ilikuwa ibada ya kishenzi, tabia, mila zao na adabu zilikuwa za kukatisha tamaa.

Ulevi ulikuwa mojawapo wa uovu wao, na walikuwa wacheza kamari wasiokanyika. Walikuwa wanagaagaa kwenye shimo la dhambi na ujin­ga. Qur'an Majid inasadikisha hali yao kwenye Aya ifuatayo:

هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِنْ كَانُوا مِنْ قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُبِينٍ {2}

"Yeye ndiye aliyempeleka Mtume kwenye watu wasiojua kusoma, awa­somee Aya zake na awatakase na awafunze Kitabu na Hekima, ijapokua kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhahiri" (Qur'an 62:2).

Lakini si kwamba nchi ilikuwa haina watu ambao waliona ibada ya masanamu kuwa ya kuchukiza. Watu hawa ambao walikuwa wachache sana kwa idadi waliitwa "Mahanifi" ("Hanifs") yaani wanaume na wanawake "ambao waliasi ibada ya kuabudu masanamu." Makka nayo ilikuwa na watu hao wachache kwa idadi "Mahanifi" na baadhi yao walikuwa kwenye ukoo wa Khadija. Mmoja wao alikuwa binamu yake wa kwanza, Waraqa bin Naufal.

Waraqa alikuwa mkubwa katika ndugu zake wote, na nywele zake zote zilikwisha kuwa rangi ya jivu.
Aliwashutumu Waarabu kwa kuabudu masanamu na kwa kuacha njia ya kweli ya mababu zao - Mitume Ibrahim na Ismaili. Ibrahim na Ismaili walifundisha somo la Tauhiid -Imani ya Kumpwekesha Muumba. Lakini Waarabu walisahau somo hilo, na wakaingia kwenye shiriki. Waraqa aliwadharau Waarabu kwa ibada yao ya kishirikina na maadili ya ufisadi. Yeye mwenyewe alifu­ata dini ya Mtume Ibrahim, mtumishi wa kweli na Mwaminifu wa Mwenyezi Mungu. Hakumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu cho­chote. Hakuwa mlevi na hakucheza kamari. Na alikuwa mwema kwa fukara na walioishiwa.

Mojawapo ya tabia za kutisha za Waarabu wakati ule ilikuwa ni kuwazi­ka watoto wa kike wakiwa hai, punde wazaliwapo.

Pale ambapo Waraqa alisikia kwamba mtu alitaka kumzika mtoto akiwa hai, alik­wenda kumshauri mtu huyo asifanye hivyo, na kama sababu ya kumuua mtoto huyo ilikuwa umaskini, alijitolea kumkomboa mtoto huyo na kumlea kama mtoto wake. Katika mifano mingi, baba wa mtoto alijutia kosa lake baadaye, na alikuja kumdai mtoto wake. Waraqa alikuwa aki­taka ahadi thabiti kutoka kwa baba mhusika kumpenda mwanae wa kike na kumtendea wema, na hapo tu ndipo alipomruhusu amchukue.

Waraqa aliishi kwenye zama za ulimwengu wa upagani. Ulimwengu karibu ulikuwa unakaribia kufurika Mwanga wa Uislamu - Dini ya Mwenyezi Mungu - iliyo bora sana - Imani ya zama za kale, iliyoanzishwa karne nyingi za nyuma na Ibrahim Rafiki na Mtumishi wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Alikwisha mteuwa Mtumishi wake Muhammad Mustafa bin Abdullah, wa ukoo wa Bani Hashim, kuwa Mjumbe Wake mpya na wa mwisho hapa duniani. Mtume Muhammad (S.a.w.) alikuwa anaishi Makka wakati huo lakini alikuwa bado hajatangaza ujumbe wake.

Waraqa alikuwa mmojawapo wa watu wachache sana wa Makka walioelimika. Inasemekana alitafasiri Biblia kutoka kwenye lugha ya Kiebrania kuwa Kiarabu. Aidha alikwisha soma vitabu vingine vilivyoandikwa na wanatheolojia Wayahudi na Wakristo. Alikuwa mtafutaji makini wa ukweli ndani ya giza la dunia inayoendelea kuwa ndani ya giza nene zaidi, na alikuwa na nia ya kuupata ukweli huo kabla ya kifo chake, lakini hakujua angeupataje.

Khadija aliathiriwa sana na fikira za Waraqa na alikubaliana na Waraqa kuichukia ibada ya masanamu na watu waabuduo masanamu.

Hakumshirikisha Muumba na kitu chochote. Kama alivyokuwa Waraqa na ndugu wengine katika familia, naye pia alikuwa mfuasi wa Mitume Ibrahim na Ismaili.

Khadija alikuwa Muwahhid ( mwenye kumwamini Mungu Mmoja wa Pekee)! Khadija hakujua kwamba baada ya miaka michache hatima yake ingeingiliana na hatima ya Muhammad Mustafa, Mtume wa Imani ya Mungu Mmoja (Tauhiid); na hatima ya Uislamu, imani ya Mungu Mmoja.

Kabla ya Uislamu Bara Arabu ilikuwa haina mpango wowote wa kisi­asa, na haikuwa na miundo mbinu ya aina yoyote. Hapakuwepo na mahakama au polisi au mfumo wowote wa sheria. Kwa hiyo, hapakuwepo na chombo cha kuzuia utendaji wa makosa, au kuwazuia wahalifu. kama Mwarabu alifanya kosa, hakuonyesha kujuta kokote. Badala yake alijivuna na kutamba kwamba angeweza kufanya lolote bila kujali, na kuweza kuwa katili na mkorofi.

Rasi yote ya Arabuni iliendeshwa kwa mfumo-dume. Mwanamke hakuwa na daraja kwa vyovyote vile. Waarabu wengi waliamini kwam­ba wanawake walileta mikosi. Kwa ujumla waliwaona wanawake kama mali inayohamishika na si watu.

Mwanaume aliweza kuoa wanawake wengi kwa idadi aliyopenda. Na wakati akifa, mtoto wake wa kiume wa kwanza aliwarithi wanawake (wakeze marehemu baba yake) wote isipokuwa mama yake. Kwa maneno mengine aliwaoa mama zake wa kambo wote isipokuwa mama yake aliyemzaa. Jambo kama hili, sheria na kanuni za maadili hazikuwepo kumzuia kwa njia yoyote ile. Uislamu ulisitisha desturi hii kisheria.

Waarabu walioishi kabla ya Uislamu hawakuwa na maadili mema. Mwarabu alitumia maisha yake yote kwenye ghasia za kivita. Mauaji na uporaji ilikuwa ndio kazi yake kubwa. Aliwatesa wafungwa wake wa kivita hadi kufa, na kuwatesa wanyama ilikuwa moja ya mambo yake ya kupitisha wakati.
Mwarabu alikuwa na ukaidi wa hisia ya utukufu, ambao ulifanya auwe mtoto wake mwenyewe wa kike. Kama mkewe alizaa mtoto wa kike, alikuwa hawezi kuzuia uchungu na hasira zake.

"Na mmoja katika wao anapopewa khabari ya (kuzaliwa kwake) mtoto wa kike, husawijika uso wake ( huwa mweusi) akajaa sikitiko!.

(Akawa) anajificha na watu kwa sababu ya hatari mbaya aliyoambiwa! (anafanyashauri) Je, akae naye juu ya fedheha hiyo au amfukie udongo­ni (karibuni na hali ya kuwa mzima ili afe)? Sikilizeni! Ni mbaya mno hukumu yao hiyo. (Quran 16:58-59)

Mara nyingi Mwarabu alimuua mwanae wa kike kwa kuogopa kwamba angekuwa mateka wa kivita wakati wa vita vya kikabila, na kwa hiyo, kuwa mtumwa wa adui, na daraja lake kama mtumwa kungeleta aibu kwa familia yake na kabila lake. Angeweza pia kumuua kwa kuhofia kwake umasikini. Aliamini kwamba binti yake angekuwa tatizo la kiuchumi kwake. Uislamu ulifanya mauaji ya watoto kuwa ni dhambi kubwa kabisa.

وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُمْ خَشْيَةَ إِمْلَاقٍ ۖ نَحْنُ نَرْزُقُهُمْ وَإِيَّاكُمْ ۚ إِنَّ قَتْلَهُمْ كَانَ خِطْئًا كَبِيرًا {31}

"Wala msiwaue wana wenu kuogopa umasikini. Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao ni hatia kubwa." (Qur'an 17:31).

Vilevile walikuwepo Waarabu ambao hawakuwaua watoto wao, lakini waliwanyang'anya haki zao zote. Walifikiri kwamba kwa vile binti zao watakapoolewa watakwenda kuingia nyumba nyingine za waume wao, hapakuwepo na haja ya kutumia gharama yoyote juu yao.

Ilikuwa katika mazingira ya namna hii ambayo Khadija alizaliwa, akakua na kuishi mazingira ya "kumkataa mwanamke."

Kutokea nyumbani kwake Makka, Khadija aliendesha biashara iliyokuwa inaendelea kukua na kuenea kwenye nchi za jirani. Kile ambacho alikwisha faulu kukipata kingekuwa cha kusifika katika nchi yoyote, katika kipindi chochote na kwa mtu yoyote mwanamume au mwanamke. Lakini mafanikio yake yamesifika mara mbili pale ambapo mtu atafikiria ule "mfumo-dume" wa kumpinga mwanamke, ulioen­dekezwa na Waarabu. Huu ni uthibitisho wa uwezo wake wa kumudu hatima yake kwa kutumia akili yake, nguvu ya dhamira na tabia. Wafanyabiashara wenzake walikubali mafanikio yake walipomwita Malikia wa Makuraishi na Malkia wa Makka kama ambavyo imetamk­wa huko nyuma.

Lakini zaidi ya sifa, Khadija pia alipata cheo cha tatu. Aliitwa "Tahira" maana yake ni "aliyetakasika." Nani aliyempa cheo cha "Tahira"? Ajabu ni kwamba, alipata cheo hiki, kutoka kwa Waarabu haohao waliokuwa na sifa mbaya kwa ujeuri, majivuno, kiburi na ujinsia. Lakini, tabia ya Khadija ilikuwa mfano mzuri wa kuigwa hivyo kwamba ilitambuliwa hata na wao, na wakamwita "aliyetakasika."

Ilikuwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Arabuni kwa mwanamke kuitwa Malikia wa Makka na aidha kuitwa "Tahira." Waarabu walimwita Khadija Malkia wa Makka kwa sababu ya utajiri wake na walimwita Tahira kwa sababu ya utakatifu wa sifa zake. Pia walikuwa wanaelewa kwamba alikuwa na tabia njema. Kwa hiyo alikuwa mtu wa kuheshimika hata kabla ya Uislamu - kipindi cha Ujahiliya.

Ilikuwa ni jambo lisilopingika kwamba Khadija angetamaniwa na Waarabu mashuhuri na wana wa Wafalme. Wengi wao walipeleka posa ili wamuoe.

Lakini hakutaka kuolewa na yeyote kati yao. Wengi wa hao watu mashuhuri na wana wa Wafalme waling'ang'ania kutaka wamuoe.

Bila kukatishwa tamaa na kukataa kwake, waliendelea kutumia washen­ga wanaume na wanawake wenye kuheshimika kuendelea kumbem­beleza. Lakini bado aliwakataa wote. Hii labda ni kwa sababu Khadija hakutilia maanani sana umuhimu wa uongozi wa mfumo-dume uliotawaliwa na wanaume katika jamii "inayowapiga vita wanawake."

Kukataa kwa Khadija kuolewa na Waarabu mashuhuri na wenye hadhi za juu, kulizua dhana nyingi kwamba ni mwanamume wa aina gani atakaye muoa. Lilikuwa ni Swali ambalo hata Khadija mwenyewe hakuweza kulijibu. Lakini majaliwa yalifahamu jibu lake; alikuwa aolewe na mwanaume ambaye si tu alikuwa bora kabisa kuliko wote katika nchi yote ya Arabu lakini alikuwa pia bora sana kuzidi viumbe wote. Ilikuwa ni majaliwa yake iliyomchochea kukataa maombi ya kuolewa na binadamu wa kawaida.

Sura Ya Tatu: Muhammed Mustafa (s) Aliyetegemewa Kuwa Mtume wa Uislamu

Ingawaje nchi ya Arabu haikuwa na serikali yoyote- ya kitaifa, kijimbo au kienyeji - jiji la Makka lilikuwa linatawaliwa na kabila la Qurayishi, kama ilivyotajwa kabla. Kabila la Qurayish lilikuwa na koo kumi na mbili. Koo hizi zilishirikiana majukumu ya kudumisha kiasi kidogo cha sheria na utulivu katika mji wa Makka.

Moja ya koo za kabila la Qurayshi ilikuwa Bani Hashim. Kila ukoo ulikuwa na kiongozi wake. Kiongozi wa Bani Hashim alikuwa Abu Talib bin Abdul Muttalib bin Hashim bin Abd Manaf bin Qusayy. Kama walivyokuwa babu zake, Abu Talib pia alikuwa mfanyabiashara. Zaidi ya kuwa mkuu wa ukoo, alikuwa pia mlezi wa Al-Kaaba - Nyumba ya Mwenyezi Mungu - iliyojengwa Makka, karne nyingi zilizopita, na Mtume Ibrahim na Ismaili na wakaitoa wakfu imtumikie Mwenyezi Mungu.

Abu Talib alikuwa na mdogo wake aliyeitwa Abdullah. Mwaka wa 570 A.D., Abdullah alikwenda Syria na msafara wa biashara. Miezi michache kabla hajasafiri kwenda Syria alimuoa Amina binti Wahab, mwanamke kutoka Yathrib (Madina).

Wakati Abdullah alipokuwa anarudi kutoka Syria, aliugua na kufa. Alikuwa na umri wa miaka 17 tu alipokufa. Alipoondoka Makka, mke wake alikuwa mja mzito na alikuwa anaishi nyumbani kwa shemeji yake, Abu Talib. Miezi miwili baada ya kifo cha Abdullah, alijifungua mtoto wa kiume. Babu wa mtoto huyu, Abdul Muttalib, alimpa jina la Muhammad. Muhammad alizaliwa tarehe 8, Juni, 570, nyumbani kwa baba yake mdogo, Abu Talib mjini Makka.

Siku za usoni, mtoto mchanga Muhammed alikuwa ateuliwe na Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwa Mjumbe Wake wa dunia yote, na alikuwa abadilishe majaliwa na historia ya binadamu daima milele.

Muhammad alikuwa na umri wa miaka sita wakati mama yake, Amina binti ya Wahab, alipokufa baada ya kuugua kwa muda mfupi. Kutokana na kifo chake hicho, babu yake Muhammad, Abdul Muttalib, alim­chukua ili amlee nyumbani kwake. Lakini ilikuwa baada ya miaka miwili tu Abdul Muttalib naye alifariki.

Abdul Muttalib alikuwa na watoto wa kiume kumi. Alipokaribia kufa, aliwaita watoto wake wote, na alimteuwa mwanae Abu Talib kama mkuu mpya wa ukoo wa Bani Hashim.

Pia alimfanya mlezi wa Muhammad. Wote wawili Abu Talib na Abdullah, baba wa Muhammad, walikuwa watoto wa mama mmoja, ambapo watoto wengine wa Abdul Muttalib walizaliwa na wakeze wengine.

Abu Talib alimpeleka Muhammad nyumbani kwake. Muhammad ali­washinda wote (kwa tabia). Abu Talib na mkewe walimpa Muhammad mapenzi makubwa sana. Walimpenda zaidi kuliko walivyowapenda watoto wao. Muhammad alizaliwa ndani ya nyumba yao. Kuzaliwa kwa Muhammad ndani ya nyumba hiyo ilisababisha nyumba hiyo iwe na neema nyingi; na sasa baada ya kifo cha Abdul Muttalib, alirudi tena ndani ya nyumba hiyo.

Muhammad alipokuwa mtoto, hakuonyesha kuvutiwa na mwanasesere na michezo ya watoto. Katika ujana wake, hakuonyesha kupenda michezo na burudani, au kuwa katika makundi ya vijana wa rika lake. Pamoja na kwamba alikuwa kijana, alipendelea zaidi upweke kuliko kuchanganyika kwenye makundi ya vijana wenzake.

Kama walivyokuwa watu wengine wa kabila la Qurayish, Abu Talib pia alikuwa akipeleka bidhaa zake Syria na Yemen kila mwaka. Wakati mwingine alikwenda yeye mwenyewe na misafara, na kipindi kingine aliajiri Wakala ambaye aliuza bidhaa zake kwenye masoko ya nchi hizo.
Mnamo mwaka wa 582 A.D. Abu Talib aliamua kutembelea Syria akiwa na msafara. Mpwa wake, Muhammad, alikuwa na umri wa miaka 12 wakati huo. Abu Talib alimpenda sana hivyo kwamba alikuwa hawezi kuachana naye hata kwa muda wa miezi michache. Kwa hiyo, alimchukua na kwenda naye Syria.

Akili ya Muhammad ilikomaa upesi, na pamoja na kwamba umri wake ulikuwa bado mdogo sana, alikuwa mchunguzi na mdadisi aliyebariki­wa. Wakati wa safari yake nje na ndani ya Syria, kwa uangalifu sana ali­wachunguza watu na mila zao, desturi zao, namna wanavyo abudu, mavazi yao, hotuba na upembuzi wao wa mambo. Na kila alichokiona, alikumbuka.

Aliporudi Makka, aliyakumbuka yote yale aliyoyaona toka mwanzo hadi mwisho na aliweza kukumbuka uchunguzi wake wote bila kubakisha kitu. Hakusahau kitu; kwa hakika, alikumbuka kila kitu. Ingawaje alikuwa mdogo kwa umri, alikomaa kihekima na matumizi ya akili ya kawaida. Abu Talib alitambua kwamba Muhammad alikuwa na hekima na akili iliyopevuka kuliko umri na uzoefu wake. kwa hiyo, hakumchukulia kama mtoto mdogo kwani ilibidi aonyeshe heshima kwake kama ile anayostahili kupewa mtu mzima wa jamii ya Kiarabu.

Haikupita muda mrefu Muhammad alipata umri unaozidi miaka kumi. Ingawa katika rika la kijana aliye balehe, alikuwa bado hakuvutiwa na starehe ambazo vijana wengine huzitafuta. Alijiepusha na purukushani za aina zote na kama ilivyoelezwa huko nyuma, alipendelea kuwa peke yake na tafakuri yake. Alikuwa na fursa ya kutosheleza upendeleo huu alipokwenda kuchunga kondoo wa ami yake. Alikuwa peke yake chini ya anga. Jangwa lililo kimya na kujitandaza hadi upeo wa macho, na ambalo lilimpa matumaini ya kutafakari kuhusu maajabu ya Uumbaji, siri za mbingu na ardhi, na maana na madhumuni ya maisha.

Alitazama mandhari ya ardhi kutoka upeo wa macho huu hadi mwingine, na ilionekana kama vile ukubwa wa ulimwengu ulikuwa ndio swahiba pekee "aliyekuwepo" pamoja naye. Upweke kwake ulionekana kuwa "kipimo" kipya cha ulimwengu wake. Wakati Muhammad alipokuwa amevuka ujana wake, watu wa Makka walikwishaanza kumtambua. Walijua kwamba kamwe hakupotoka kuto­ka kwenye maadili mema na utu mwema na hakufanya kosa kamwe. Aidha walitambua kwamba hakupenda kusema sana na alipofanya hivyo, aliongea kweli tupu, na alitamka maneno ya hekima tu. Kwa kuwa watu wa Makka walikuwa hawajamsikia akisema uongo, wal­imwita "As-Sadiq" (Mkweli).

Katika kipindi cha miaka michache iliyofuata, raia wa Makka walimpa Muhammad cheo kingine. Kwa kutambua kwamba alikuwa makini sana, wengi wao walianza kumpa mali zao ili awatunzie kama vile: fedha taslimu, vito, mapambo, na vitu vingine vya thamani. Wakati mtu yoyote alipotaka mali yake, Muhammad alimrudishia yote. Kamwe hapakutokea kasoro yoyote katika kurudisha mali za watu.

Baada ya kuthibitisha kuwa alikuwa na tabia ya namna hiyo, kwa kipindi cha miaka kadhaa watu walianza kumwita Muhammad "Al-Amin". (Mwaminifu) Ni yeye, na yeye peke yake aliyeitwa As-Sadiq na Al-Amin na watu wa Makka.

A. Yusuf Ali mtarjumi na mfasiri wa Qur'anTukufu, amelielezea neno "A-Amin" kama ifuatavyo:
"Al-Amin Mtu ambaye amana imewekwa kwake, pamoja na maana mbali mbali kidogo zimedokezwa:

1. Aanyestahiki kuaminiwa;

2. Anayewajibika kuitoa amana yake, kama Mtume yeye huwajibika kutoa Ujumbe wake;

3. Anawajibika kabisa kutenda kama ambavyo amana inaelekeza, kama mtume anawajibika
kufikisha Ujumbe wa Mwenyezi Mungu tu, na asiongeze chochote cha kwake, na

4. hatafuti masilahi yake mwenyewe."

Waarabu walioishi kabla ya Uislamu kila mwaka walifanya "Msimu wa maonyesho" sehemu mbalimbali za nchi. Baadhi ya maonyesho haya yalionyeshwa Makka na sehemu nyengine za karibu yake. Maonyesho yaliyojulikana sana ni: Ukkaz, Majanna na Dhul-Majaz. Muhammad aliyatembelea maonyesho hayo pale muda ulipomruhusu kufanya hivyo. Maonyesho yote haya yalionyeshwa wakati wa miezi minne mitakatifu ya Rajab, Dhil-Qaada, Dhil-Hajj na Muharram, kufuatana na mila za Waarabu wa kale. Ndani ya miezi hii minne, mambo yafuatayo yalip­igwa marufuku: vurugu, vita, kuteka nyara na unyang'anyi. Mnamo mwanzo wa "Msimu wa amani" tangazo la kusimamisha vita lilitolewa. Tangazo la kusitisha vita lilitambuliwa na kuheshimiwa na makabila yote ya Waarabu.

Wafanya biashara, wakulima na wastadi (wachonga sanamu) waliku­sanyika kwenye maonyesho haya kutoka sehemu za mbali na za karibu (kwa ajili ya) kuuza, kununua na kubadilishana. Walileta pamoja nao mazao yao yaliyo bora kabisa, na kwa fahari waliyafanyia maonyesho. Sanaa nyingine za amani, mashairi yakiwa miongoni mwao, yalikuzwa (na kutukuzwa katika wakati zilipositishwa vurugu (na vita)

Mashairi yalikuwa penzi la kwanza la Waarabu. Kama kipaji cha mashairi kiligunduliwa kwenye kabila lolote, lilikuwa jambo la kush­erehekewa na kila mmoja. Makabila mengine yenye uhusiano mzuri na kabila husika, yalilipongeza kabila hilo kwa kuzalisha kipaji cha namna hiyo. Waarabu walikuwa washabiki wakubwa wa maneno ya Kiarabu na maana yake nyingi. Wao walijiita "watoto wa Kiarabu."

Kwenye maonyesho haya washairi walisoma tunzi zao mpya, sifa ambayo Waarabu waliithamini kuwa ya muhimu na maana sana. Mojawapo ya misemo yao ni kwamba uzuri wa mwanamke upo kwenye uso wake; lakini uzuri wa mwanamume upo katika uhodari wake wa kujieleza. Walipenda ustadi wa utunzi na ufasaha wa yale yanayosemwa kwenye mashairi.

Mafumbo yasiyo ya kawaida ya jangwani na watabiri wanao­fanana na wanyama pori na waaguzi wa makabila, huwafurahisha wasikilizaji kwa hotuba zao za mafumbo hadithi zao za mafumbo na siri za ubashiri, hata hivyo, wachache waliweza kuelewa ishara hizo. Waarabu wengi waliamini kwamba utabiri wa nyota uliamua mwisho mzuri au mbaya wa maisha ya mtu.

Kwa hiyo, watu wa nchi nzima waliwaogopa watabiri, iliaminika kwamba walikuwa na uwezo wa kuzungumza na nyota. Waimbaji, wacheza dansi, wachekeshaji, wana sarakasi na wana mazingaombwe wote walishindana ili wapate kusifiwa na watazamaji.

Maonyesho haya yalihudhuriwa na watawa, makuhani na watu watakat­ifu ambao walihubiri imani ya ibada zao. Wote walikuwa huru kueneza itikadi zao na fikira zao bila woga wa kuonewa na mtu yeyote katika kipindi chote cha miezi minne. Amani na sanaa za amani vilishamiri dhidi ya mfululizo wa mambo ya uchangamfu wa binadamu usio na mipaka.

Kwenye maonyesho haya, Muhammad alipata fursa ya kuchunguza wakazi wa rasi ya Bara Arabu. Pia alijifunza, kwa mara ya kwanza, mila na imani za watu wa jamii tofauti, na utamaduni na usuli za kijogorafia.

Mnamo majira ya kuchipua ya mwaka wa 595 A.D., wafanyabiashara wa Makka walikusanya msafara wao wa majira ya kiangazi ili wapeleke bidhaa zao Syria. Pia Khadija alitayarisha bidhaa zake lakini alikuwa hajapata mtu mwanamume atakayesimamia msafara wake na kuwa wakala wake. Majina machache yalipelekwa kwake lakini hakupata lililompendeza.

Kupitia kwa baadhi ya weza wake wa chama katika wachuuzi wa Makka, Abu Twalib alipata habari kwamba Khadija alikuwa anatafuta wakala ambaye atachukua mizigo yake pamoja na msafara kwenda Syria na kuiuza kule.

Ilipita akilini mwa Abu Twalibu kwamba mpwa wake Muhammad ambaye sasa alikuwa na miaka ishirini na tano angelifaa kwa kazi hiyo Alikuwa na hamu kubwa ya kumtafutia kazi mpwa wake. Alijua kwam­ba yeye (Muhammad) hana uzoefu wa kazi ya uwakala lakini pia alijua kwamba yeye (Muhammad) angeweza kazi hiyo kwa sababu ya kipaji chake.

Alikuwa na imani na uwezo na akili za mpwa wake na alikuwa na uelewa wa kutosha kufanya kazi yake ya uwakala kwa tajiri yake. Kwa hiyo, pamoja na makubaliano yake ya kimya (na Muhammad), alikwenda kwa Khadija, na alianzisha mazungumzo kuhusu suala la uteuzi wake (Muhammad), kama wakala wake mpya.

Kama ilivyo kwa raia wengine wengi wa Makka, Khadija pia alikwisha sikia kuhusu Muhammad. Khadija alijua kwamba hangehoji kuhusu heshima ya Muhammad. Aliona kwamba angeweza kumwamini Muhammad kwa wazi na kwa siri. Kwa hiyo alikubali kumteua Muhammad kuwa wakala wake. Hakufikiria kutokuwa na uzoefu ingekuwa tatizo kwa Muhammad, na akasema kwamba, kwa jinsi yoy­ote ile, angempeleka mtumwa wake Maysara, ambaye alikuwa na uzoe­fu wa kusafiri, awe pamoja naye (Muhammad) amsaidie katika kazi zake.

Khadija alikuwa mwendeshaji mzuri sana na mpangaji aliyekamilika. Lakini pia alikuwa na bahati njema. Kila mara alikuwa na bahati ya kupata mawakala wazuri kwa biashara yake. Hata kama alikuwa na hali ya kufuzu, alistaajabu baada ya kipindi kifupi kugundua kwamba akiwa na Muhammad kama wakala wake, bahati yake iliongezeka kwa kiwan­go ambacho ilikuwa haijapata kutokea. Kwa Khadija, kamwe palikuwa hapajatokea siku za nyuma, na kamwe haingetokea kwa siku za baadaye kuwa na wakala kama Muhammad.

Kama Khadija alikuwa na kile kitu kinachoitwa "mguso wa dhahabu" (golden touch) mkononi mwake, Muhammad alikuwa na "mguso wa baraka" mkononi mwake.

Khadija na Abu Talib walitayarisha vipengele vyote vya mpango mpya. Na Muhammad alipokwenda kumuona tajiri wake mpya kwa madhu­muni ya kukamilisha mkataba, alimwambia mambo yote kuhusu biashara hiyo. Muhammad alielewa haraka sana katika yote Khadija aliyomwambia na hakuuliza swali lolote lile lililohitaji ufafanuzi. Khadija alimwambia Abu Talib kwamba ujira ambao atampa Muhammad kwa kazi yake utakuwa mara mbili zaidi ya ule aliokuwa anawapa mawakala wengine huko nyuma.

Jambo ambalo Khadija hakulijua wakati huu ni kwamba ulikuwa ni ule mkono wa majaliwa ndiyo uliokuwa unafanya kazi katika kuusukuma mpango huu. majaliwa yalikuwa na mipango mingine kwake yeye na Muhammad. Mipango hiyo ilivuka mipaka ya ulimwengu huu na masu­ala ya thamani ndogo ya pesa, kama kupata faida kwenye biashara, kama ambavyo hivi punde matukio yatakavyoonyesha.

Kwa wakati huo, "msafara wa kiangazi" wa wafanya biashara wa Makka ulikwisha kamilika, na ulikuwa tayari kuondoka kuelekea kwenye safari yake ndefu. Wafanyabiashara walileta mizigo yao kuto­ka kwenye maghala ili ipakiwe kwenye ngamia. Mikataba ilitayarishwa na kusainiwa. Mahitaji ya njiani yalichukuliwa, na viongozi na wasindikizaji waliajiriwa. Kwa muda uliopangwa, Muhammad na Abu Talib na ami zake wengine walifika. Walisalimiwa na ami yake Khadija ambaye alikuwa anawangojea akiwa na Cheti cha orodha ya Shehena na hati nyingine.

Muhammad aliamua kuhesabu mali ya kuuza huko Syria. Akisaidiana na Maysara, alikagua mali yote na aliona kila kitu kiko sawa sawa. Maysra alifanya kazi ya makaratasi yahusuyo mauzo na manunuzi. Alikuwa mtunza taarifa ya mali.

Abu Talib alitoa maelekezo maalumu kwa Maysara na kwa kiongozi wa msafara kuhusu usafiri wa raha na salama kwa Muhammed. Waliahidi kuhakikisha kwamba Muhammed angesafiri kwa raha na salama. Abu Talib na ndugu zake waliwashukukuru kwa kuonyesha ushirikiano kuhusu safari ya Muhammad.

Walimwombea dua apate mafanikio kati­ka kazi yake mpya na kurudi salama. Halafu wakamkabidhi Mwenyezi Mungu amlinde arudi salama, na wakaagana.

Wakati wa kiangazi misafara mingi ilisafiri usiku kukwepa joto kali la mchana, na kupumzika mchana. Safari ya mchana ingechosha sana wafanya biashara, ngamia na farasi. Kwa hiyo, misafara mingi iliondo­ka Makka saa za alasiri, kama walivyosema Waarabu, au jua linapokuwa limepita katikati, na joto huwa limepungua.

Msindikizaji mmoja aligonga kengele. Wasafiri wote walijitayarisha na msafara ulikuwa tayari kuondoka. Ngamia waliokuwa wamepumzika walisimama, bila kupenda, walionyesha kutokutaka kuondoka kwa kukataa na kukoroma lakini waliingia kwenye msafara. Takribani saa tatu kabla ya jua kuchwa kiongozi wa msafara alitoa ishara, na msafara ukawekwa tayari kwa kuondoka.

Msafara ulielekea Kaskazini. Ndugu na marafiki wa wasafiri walikaw­ia kwa muda fulani huku wakiwa wanapunga mikono na kutazama msa­fara unavyosonga mbele. Ngamia wa mwisho alipokingizwa na vilima, wasindikizaji nao walisambaa.

Wasafiri wapya walikaa pamoja na wasafiri wazoefu ambao walikuwa wanawaonyesha sehemu za kuvutia walizokuwa wanazijua na walielezea upekee wa sehemu hizo. Maysara alimwonyesha Muhammad sehemu nyingi za kupendeza. Muhammad pia alizitambua sehemu nyingi alizoziona barabarani alipopita humo miaka kumi na tatu iliyopita akiwa na ami yake. Hakuna kilicho badilika wakati wa miaka hiyo 13.

Maysara alithibitisha kuwa msafiri mwenza mchangamfu ambaye aliweza kusimulia hadithi nyingi na aliweza kukumbuka matukio mengi sana aliyoyaona wakati wa safari zake za siku za nyuma. Muhammad aligundua kwamba wasafiri wengine pia walikuwa wachangamfu na wenye kufanya urafiki.

Baada ya takribani mwezi mmoja, msafara ulifikia mwisho wa safari yake ulipofika Syria. Mipango ya nyumba ya kupanga ilikwisha tayarishwa kwa ajili ya wasafiri waliochoka kwa msafara, na wote wal­itaka kupumzika baada ya safari ndefu iliyowapitisha kwenye mandhari zilizosababisha safari kuwa ngumu na joto kali. Waliweza kupumzika kiasi cha wiki moja ili kuponyesha sehemu muhimu za mwili zilizo athirika.

Wafanyabiashara walipokwisha pumzisha viungo vyao vilivyokuwa vinauma na kupata nguvu upya tena, walikwenda sokoni kuuza mali zao walizoleta kutoka Makka. Kiasi fulani cha mali waliuza kwa fedha taslimu, na iliyobaki walibadilisha mali kwa mali kwa bidhaa za Syria. Iliwabidi pia wanunue bidhaa kwa ajili ya soko la nyumbani, na wal­itafuta na kupata mali nyingi yenye faida. Shughuli za msafara ziliweza kudumu kuanzia miezi miwili hadi minne.

Muhammad pia aliuza na kununua mzigo mpya. Ingawa kwake yeye ilikuwa msafara wa kwanza wa kibiashara, hakusita kwa sababu ya kutokuwa na uzoefu, katika shughuli za biashara. Hakika alimshangaza Maysara kwa werevu wake katika biashara. Aidha Maysara aligundua kwamba Muhammad alikuwa mwepesi kuelewa na kuamua katika mazungumzo ya biashara na upevu wake wa akili na uaminifu wake kama muuzaji. Muhammad alilinda maslahi ya tajiri yake na wateja wake, na bado alipata faida kubwa zaidi katika shughuli hiyo ya Khadija kuzidi mara zote alizokuwa amefanya biashara tangu bibi huyo kurithi biashara ya baba yake. Na bidhaa alizonunua Syria kwa ajili ya biashara ya Khadija zilikuwa safi sana kwa ubora wake na hakika zingepata bei nzuri Makka, na ilitokea hivyo.

Huko Syria yeyote aliyemuona Muhammad, alivutiwa naye. Alikuwa na umbo la kuvutia ambalo liliwafanya watu wasimsahau hata kwa kumuona mara moja tu. Ingawa Muhammad alijishugulisha na kuuza mali, mapatano ya biashara, kuchunguza soko, na kununua, Maysara aling'amua kwamba hata hivyo alipata muda wa kukaa peke yake.

Kwa maoni ya Maysara, hivi vipindi vya ukimya wa Muhammed, vilikuwa chanzo cha jambo lililojificha, lakini hakuviingilia kati. Maysara hakuwa anajua kwamba bosi wake mwenye umri mdogo alikuwa na desturi ya kutafakari kuhusu hali na majaliwa ya mwanadamu.

Wakati akiwa Syria Muhammad alikutana na Wakristo na Wayahudi wengi. Alidhani kwamba kila kundi kati ya hayo mawili yangekuwa na "imani ya Mungu Mmoja." Lakini alistaajabu alipofahamu kwamba haikuwa hivyo. Makundi yote mawili yaligawanyika katika makundi mengine madogo mengi, na aina ya ibada ya kila kundi ilikuwa tofauti na ile ya makundi mengine. Miongoni mwao kundi lipi lilikuwa sahihi na lipi halikuwa sahihi? Hili lilikuwa swali ambalo lilimsumbua Muhammad.

Utafiti wa udadisi wa jibu la swali hili, na maswali mengine madogo madogo yenye kufanana na hili yalimfanya Muhammad asilale usingizi wakati kila mmoja amekwenda kulala.

Hatimaye, shughuli za biashara zilipokwisha, na zawadi za ndugu na marafiki kununuliwa, msafara ulirudi Makka. Kwa wasafiri wakum­bukao sana nyumbani, kurudi nyumbani mara zote ni tukio la kufu­rahisha. Ni tukio lililojaa matumaini kwani mtu atakutana na awapendao ambao mtu hakuwa nao kwa miezi mingi. Wasafiri wachovu hawawezi kungoja kwa muda mrefu kusikia vicheko vya furaha vya watoto wao na wanatambua kwamba wakati mzuri kama huo ukiwadia hawawezi kuzuia na kuficha machozi.

Wanajua kutokana na uzoefu wa muda mrefu kwamba pangekuwapo na kulia machozi - machozi ya furaha. Kicheko na Machozi vyenye mchanganyiko ulio huru kabisa katika vipindi vya heri na furaha isiyo na upeo.

Kuwasili kwa msafara mara kwa mara kulisisimua mji. Kwa hakika ulikuwa wakati wa kusherehekea kwa kila mkazi wa Makka na vitongoji vilivyomo pembezoni mwake. Sehemu zilizotengwa maalum kwa ngamia kushushia abiria na mizigo, zilikuwa changamfu mno. Raia walio wengi na hata yale makabila yanayohamahama waliona pilika pilika za kuwasili kwa msafara kwamba yalikuwa mabadiliko ya kutia moyo katika mwenendo wa maisha.

R.V.C. Bodley, ameandika katika kitabu chake:

"Kuwasili na kuondoka kwa misafara yalikuwa matukio muhimu kwa maisha ya watu wa Makka. Karibu kila mkazi wa Makka alikuwa na aina fulani ya uwekezaji kwenye mali iliyobebwa na maelfu ya ngamia, mamia ya watu, farasi na punda:- bidhaa hizo zilikuwa ngozi, zabibu kavu, vinoo vya fedha, na walirudi na mafuta, manukato na bidhaa zili­zozalishwa viwandani kutoka Syria, Misri na Uajemi, na viungo na dhahabu kutoka Kusini.

(The Messenger- the life of Muhammed,1946)

Watu walikuja kuwasalimia wapenzi wao ambao walikuwa wanarudi nyumbani baada ya kutokuwepo kwa kipindi cha miezi sita. Wengi wao walikuja wakiwa na fikira mchanganyiko wa matumaini na woga.

Ilipotokea mtu anaondoka mjini kwenda na msafara, hapakuwepo na njia yoyote kwa ndugu zake kujua kama wangemuona akiwa mzima tena. Wasafiri wengine walikufa wakiwa safarini na walizikwa kwenye sehemu ambazo ni njia za ndani ndani sana, na hazipitiki. Ndugu zao kamwe hawakuweza kuyatembelea makaburi yao.

Na ilikuwa hapo tu ambapo msafara ulifika ndipo wakazi wa Makka waliweza kusikia habari za dunia nje ya bara Arabu. Waarabu wa siku hizo waliishi katika hali ya upweke sana katika dunia yote. Katika dunia hiyo Waarabu walikuwa na njia moja tu ya kupata habari nayo ni msa­fara.

Takriban kila raia wa Makka aliwekeza fedha kwenye msafara wa biashara. Watu matajiri miongoni mwao waliweza kutembelea nchi za nje kwa muda mrefu zaidi wa miezi mingi. Lakini watu ambao hawakuwa na uwezo wa kifedha walibaki nyumbani.

Hivyo, waliwapa bidhaa zao watu walio waaminifu kuwa mawakala wao wauze kwa niaba yao, na waliwapa wao fedha ya kwenda kununua bidhaa ambazo zilikuwa zinatakiwa Arabuni na ziliweza tu kupatikana kwenye masoko ya Syria, Yemen, Habeshi na Misri.

Baada ya mawakala wao kuleta mali za nje Makka, waliuza bidhaa hizo na kupata faida. Ulikuwa ni utaratibu ambao baada ya uzoefu wa muda wa miaka mingi, mpango huu ulionekena unafaa na unatekelezeka.

Wafanyabiashara na mawakala waliokuwa kwenye msafara pia walileta zawadi kutoka nchi za nje na tuzo kwa ndugu na marafiki zao, kufuatana na mila za zamani. Kila mtu alitaka kuona zawadi hizo ambazo zili­wakumbusha utajiri uliopo Syria na anasa za Falme za Ajemi na Roma.

Muhammad alipofika Makka, kitu cha kwanza kufanya ni kuzunguka Al-Kaaba mara saba kama ilivyokuwa desturi, na halafu alikwenda kumuona muajiri wake.

Alimwelezea tajiri wake kwa kina kuhusu safari na shughuli za biashara alizozifanya kwa niaba yake. Baadae, alimwelezea ami yake Abu Talib, kuhusu matukio ya kuvutia kwenye uzoefu wake kama mfanyabiashara.

Maysara, mtumwa wa Khadija, naye alikuwa na taarifa yake mwenyewe ya kumpa mmilki wake. Alimwambia Khadija kuhusu safari ya kwen­da na kurudi kutoka Syria, na faida ambayo Muhammad aliingiza kwenye biashara yake. Lakini kwake yeye (Maysara), kilichompendeza zaidi kuliko kufuzu katika biashara, ni tabia na utu wa Muhammad. Maysara alimwambia Khadija kwamba alipendezwa na kipaji cha Muhammad katika biashara. Aliendelea kumtaarifu Khadija kwamba uwezo wa Muhammad kuona mbali kibiashara ilikuwa kinga; uamuzi wake ulikuwa wa uhakika na uelewa wake haukuyumba. Maysara pia alimwambia Khadija kuhusu bashasha, uungwana na kukubali madara­ka yaliyo chini ya uwezo wake, Muhammad.

Khadija alivutiwa na taarifa hiyo, na alimuuliza Maysara maswali kuhusu msimamizi wake mpya, Muhammad. Pengine Khadija hange­shangaa hata kidogo kama Maysara angemwambia kwamba Muhammad alikuwa mtu asiye wa kawaida kulinganisha na watu ambao amewaona katika maisha yake, na alikuwa mtu anayeweza kufanya mambo yasiyo ya kawaida.
Siku iliyofuata, Waraqa bin Naufal alikwenda kumuona Khadija. Yeye pia alitaka kusikia habari zilizoletwa na wasafiri kutoka ng'ambo. Habari zilizomvutia yeye sana ni zile za ugomvi wa siku nyingi baina ya Falme za Ajemi na Roma.

Kila moja ya hizo Falme ilitaka kuwa na mamlaka kwenye kanda yote iliyojulikana kama "Bara lenye Neema." Pengine pia kama walivyokuwa raia wengine Waraqa aliwekeza fedha kwenye biashara ya Makka ya kusafirisha nje na kuingiza ndani ya nchi bidhaa na alitaka kujua jinsi ambavyo msafara ulifanikiwa kibiashara.

Khadija alimwambia binamu yake habari zote kama alivyozipata kuto­ka kwa Muhammad mwenyewe na Maysara. Aidha alisema kwamba msimamizi wake mpya alipata faida kubwa ambayo hakuitegemea.

Waraqa pia alizungumza na Maysara kuhusu safari na kuhusu Muhammad. Maysara, hata hivyo, alitaka kuzungumzia tu kuhusu Muhammad. Hakuna kitu kingine chochote kilichomvutia, hata hizo shughuli za biashara za kuuza na kuuziwa hakuzitia maanani kabisa..

Waraqa aliposikia taarifa hiyo ndefu inasemekana alipatwa na mawazo mengi sana. Baada ya kipindi kirefu cha kimya, alimwambia Khadija:

“Baada ya kusikia yale ambayo wewe na Maysara mmesema kuhusu Muhammad, na pia kufuatana na vile ninavyomjua, mimi ninaona kama kwamba anazo sifa zote, tabia, ishara na uwezekano wa kuwa Mjumbe wa Mungu. Hakika, inawezekana Muhammad atakuja kuwa mmoja wao katika siku zijazo."

Kwa mtazamo wa makini ndani ya giza la upagani wa Arabuni, Waraqa aliwezeshwa labda na ubashiri wake, kuona dalili ndogo za Mwanga wa Uislamu ambazo si muda mrefu zingejitokeza kwenye upeo wa macho na Muhammad ndiye ambaye angeleta Mwanga huo.

Vitabu vingi vinavyoeleza maisha ya Muhammad Mustafa, Mtume wa Uislamu (S.a.w.) vimetaja miujiza kadhaa inayodaiwa kufanywa naye wakati wa safari yake ya kwenda na kurudi kutoka Syria. A. Yusuf Ali, mtrjumi na mfasiri wa Qur'an Tukufu, ameandika ifuatavyo: "Hakuna Mtume yeyote aliyeweza kufanya mujiza wowote au kuonye­sha "Alama", bila ridhaa ya Mungu.

Ridhaa ya Mungu (Mashiyat) ni Mpango wenye hekima unaohusu dunia yote, mpango huu upo si kwa faida ya kabila, mila, kipindi au nchi moja. Mujiza mkubwa kuliko yote katika historia ni Qur'an.

Tunaweza kutambua uzuri wake na utukufu wake leo kama ambavyo walitambua watu wa zama za uhai wa Mustafa, hata zaidi, kwani jumuisho la uelewa wetu kuhusu asili na Uumbaji wa Mungu umeongezeka."

Mahali pengine A. Yusuf Ali anasema: "Dalili zilizopelekwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad, zilikuwa:

(1) Aya za Qur'an na (2) Maisha na kazi yake, ambamo humo mpango na makusudio ya Mungu yalifunuliwa."

Inaonyesha kwamba uchangamfu na kipaji cha Muhammad pia vil­imuathiri Khadija. Kama ilivyotokea kwa Maysara, Khadija naye aliin­gia kwenye kundi la watu wanaompenda Muhammad, na ni nani awaye yeyote miongoni mwa watu ambaye angekataa kumpenda. Khadija alimfahamu Muhammad kuwa mtu mpole mwenye staha, mkimya na asiye mpinzani.

Aidha Khadija alitambua kwamba watu wa Makka walimpa jina la Sadiq na Amin. Na sasa alionyesha uwezo wake wa kuwa mfanyabiashara.

Ustadi na werevu wake vilikuwa sababu ya mtu huyo kuwa na kipaji. Tathmini mpya ya Khadija kuhusu Muhammad, ni kwamba mtu huyu hakuwa mwenye masihara bali alikuwa na uwezo wa kufanya mambo.

Tathmini hii ilimshawishi Khadija kufanya uamuzi wa kumwajiri Muhammad kuwa Meneja wa biashara yake kwenye misafara yote ya baadaye.

Sura Ya Nne: Ndoa Ya Muhammad Mustafa (s) Na Khadija

Msafara wa kibiashara wa Muhammad kwenda Syria ulikuwa ndio chanzo cha ndoa yake na Khadija.

Mtarjumi na mfasir wa Qur'an Majid, A. Yusuf Ali, anauliza swali: "Tunaweza kushangaa jinsi Yakuub alivyokutana tena na mwanawe Yusuf, au jinsi Musa alivyokutana na Harun, au jinsi Muhammad Mustafa alivyokutana na Bibi Khadija?"

La. Hatuwezi kushangaa. Ilikuwa ni amri ya Mwenyezi Mungu kwam­ba watumishi wake wawili- Muhammad na Khadija wangekutana kati­ka ndoa, na walioana.

Kuna taarifa isemayo kwamba mmoja wa marafiki wa Khadija alikuwa anatoka kwenye ukoo bora wa Makka jina lake Nafisa (au Nufaysa) binti Mumyah. Mwanamke huyu alikuwa na habari kwamba Khadija alikwisha kataa posa nyingi za ndoa. Alikuwa anashangaa kama pange­tokeza mtu katika Bara Arabu ambaye angekuwa wa kiwango alichoafi­ki Khadija. Marafiki hawa wawili walilizungumzia jambo hili mara nyingi.

Hatimaye, Nafisa alifanya mazungumzo ya mara ya mwisho kuhusu jambo la ndoa yake Khadija na akapata kutambua kwamba rafi­ki yake (Khadija) hakujali utajiri, cheo au uwezo wa mume mtarajiwa. Nafisa alijua kwa hakika kwamba rafiki yake Khadija alitaka kuolewa na mtu mwenye tabia nzuri, tabia inayokubalika. Khadija alitaka kuole­wa na mwanamume mwenye maadili mema na msimamo wa uadilifu.

Pia Nafisa (au Nufaysa) alijua kwamba alikuwepo mtu wa aina hiyo Makka na jina lake alikuwa Muhammad.

Kuna taarifa isemayo kwamba siku moja Muhammad alikuwa anarudi nyumbani kutoka Al-Kaaba, Nafisa alimsimamisha na mazungumzo yalifanyika kama ifuatavyo:

Nafisa: Ewe Muhammad, wewe ni kijana wa kiume na bado hujaoa. Wanaume ambao unawazidi umri, wamekwisha oa na wengine wamezaa watoto. Kwa nini hujaoa?

Muhammad: Bado sina uwezo wa mali; mimi ni fukara. Nafisa: Bila kujali ufakiri wako, ungejihisi vipi endapo ungemwoa mwanamke mwenye sura nzuri, tajiri, mashuhuri na mwenye kuheshimika?

Muhammad: Mwanamke huyu anaweza kuwa nani?

Nafisa: Mwanamke huyu ni Khadija, binti Khuwaylid.

Muhammad: Khadija? Inawezekanaje Khadija kukubali kuolewa na mimi? Unajua kwamba wanaume wengi matajiri na uwezo na wakuu wa makabila wamemposa na amewakataa wote.

Nafisa: Kama wewe upo tayari kumuoa Khadija, sema hivyo, na niachie mambo mengine mimi. Nitapanga kila kitu.

Muhammad alitaka kumwambia ami wake na mlezi wake, Abu Talib, kuhusu azima ya Nafisa, na kupata ushauri wake kabla hajatoa jibu.

Abu Talib alimfahamu Khadija kama alivyokuwa anamfahamu mpwa wake. Alikubali ushawishi wa Nafisa. Hakuwa na shaka kwamba Muhammad na Khadija wangekuwa wanandoa makini. Kwa hivyo, alilibariki pendekezo la ndoa yao.

Hapo hapo Muhammad alimtaarifu Nafisa kwamba pendekezo lake limekubaliwa na hivyo amepata mam­laka ya kuendeleza mazungumzo kuhusu ndoa yake na Khadija.

Mara tu baada ya Abu Talib kuthibitisha ndoa hiyo, alimtuma dada yake, Safiya, kumuona Khadija, na kuzungumza naye kuhusu jambo hilo. Wakati huohuo, Nafisa alikwisha fanya mazungumzo ya awali, na Khadija alikuwa anategemea kupata mgeni kutoka nyumbani kwa wakwe wategemewa.
Khadija alimpokea Safiya kwa uchangamfu, alimkirimu, na kumwambia kwamba yeye Khadija alimteua mpwa wake Safiya kuwa mwenzi wake wa maisha bila masharti yoyote. Safiya ali­furahishwa sana na mafanikio ya ujumbe wake. Kabla hajaondoka kurudi kwao, Khadija alimpa Safiya kanzu nzuri sana na ambayo ali­ikubali kwa furaha na shukrani nyingi.

Abu Talib aliamua kutekeleza kanuni za desturi za ndoa. Alimpa Khadija zawadi, na aliwachukuwa kaka zake, Abbas na Hamza, wote watatu wakaenda nyumbani kwa Khadija na kulifikisha pendekezo la ndoa ya mpwa wake na Khadija rasmi. Khadija alikubali zawadi ali­zopewa na Abu Talib na kama ilivyotarajiwa alikubali pendekezo la ndoa. Pande zote mbili zilikubaliana na kuweka tarehe ya harusi.

Abu Talib mwenyewe alichukuwa madaraka ya matayarisho ya ndoa ya mpwa wake mpendwa. Kwa ajili ya tukio hilo lenye baraka, Abu Talib alileta kumbukumbu zote zenye kuheshimika sana za urithi wa familia. Vitu hivi vilikuwa pamoja na joho na fimbo ya Abdul Muttalib, mare­hemu, mkuu wa kabila la Bani Hashim. Bwana harusi alivaa joho na kuishika mkononi mwake ile fimbo. Abu Talib alimvisha kichwani Bwana harusi kilemba cheusi cha ukoo wake, na alivaa pete yenye kito cha kijani kwenye kidole chake. Pete hii, ilikuwa raslimali ya Hashimu bin Abd Manaf bin Qusayy - mnamo siku za nyuma.

Harusi ilihudhuriwa na wakuu wote wa Quraysh na mamwinyi wa Makka. Bwana harusi alipanda farasi mwenye kutembea kwa majivuno, na vijana mashujaa wa Bani Hashim walitikisa Majambia yao yaliyokuwa yanameremeta juu ya vichwa vyao wakati walipokuwa wana msindikiza kutoka nyumbani kwa Abu Talib kwenda nyumbani kwa Khadija. Wanawake wa ukoo wa Quraysh walikwisha mtangulia bwana harusi, na tayari walikuwa wanakirimiwa nyumbani kwa bibi harusi.

Nyumba ya Khadija ilipambwa kwa taa nyingi sana. Ndani ya nyumba, mashada ya taa zenye mapambo yalining'inizwa kwa minyiroro ya dha­habu kwenye dari, kila shada lilikuwa na taa saba. Wageni walifika wakati giza lilianza kuingia. Msimamizi mkuu wa eneo la makazi ya Khadija aliunda kamati ya kumkaribisha Bwana harusi na wageni mashuhuri. Kamati ya makaribisho iliwaongoza wageni ndani ya nyumba kupitia kwenye lango la juu na kuingia kwenye ukumbi wenye umbo la mstatili ambao kuta zake zilibandikwa vigae na dari yake ili­pakwa dhahabu. Wageni waliketi kwenye mazulia na mito.

Kwa madhumuni ya shughuli hii maalum, Khadija aliagiza washonewe sare watu wote wa nyumbani mwake - wanaume na wanawake. Wanaume walivaa vilemba vyenye kumetameta, mashati mekundu, na walivaa mikanda (mishipi) kwenye viuno vyao yenye rangi nyeusi. Mashada ya hariri yenye rangi ya pembe za ndovu yalishikizwa kwenye vilemba. Wasichana walivalia mavazi yaliyonakishiwa kwa kutonewa dhahabu na kumetameta. Walivalia taji dogo kichwani na lulu nyingi na vito vyenye kumetameta. Nywele zao ziliporomoka hadi kwenye mabega na kutoka kwenye mabega hadi kiunoni zilisokotwa kwa lulu.

Mapambo ya chumba cha Bibi harusi yalikuwa mazuri sana, na hakika hayakuzidiwa kwa ustadi. Hariri iliyoning'inizwa na nguo iliyotariziwa kwa rangi nyingi nyororo, ilipamba ukuta; na busati, jeupe laini lili­tandikwa sakafuni. Moshi wa ubani ulichomoza kutoka kwenye chate­zo cha rangi ya fedha na almasi inayometameta, johari ya rangi ya bluu na rubi.

Khadija, bibi harusi, aliketi kwenye jukwaa lililofunikwa kwa nguo iliy­onakishiwa kwa urembo mwingi wa kufuma. Alionekana mchangamfu na kung'aa kama jua linalochomoza. Kichwani kwake alivaa taji la dha­habu na lulu yenye thamani na uzuri wa kushangaza. Gauni lake, lenye mchanganyiko wa rangi nyekundu iliyoiva na kijani, ilirashiwa dhahabu na kuwekwa mapambo ya lulu na Zamaradi. Walikuwepo wanawake wawili wa kumsaidia yeye binafsi, kila mmoja wao alikuwa amevalia taji la dhahabu, gauni la hariri lenye rangi ya zambarau, na makubazi yaliyotapakaa vito. Baada ya wageni wote kuketi kwenye nafasi zao, Abu Talib, mlezi wa Bwana harusi, alisimama na kusoma hotuba ya harusi.

"Utukufu na sifa zote ni zake mwenyezi Mungu, Muumba wa Mbingu na dunia, na shukrani zote ni Zake kwa neema Zake zote, riziki na huru­ma. Ametuleta sisi hapa duniani kutokana na vizazi vya Ibrahim na Ismael. Alitufanya sisi waangalizi wa Msikiti na kuwa viongozi wa Nyumba yake, Al- Kaaba, ambayo ni kimbilio la viumbe wake wote. Baada ya utangulizi huu Abu Talib aliendelea:

"Mpwa wangu, Muhammad bin Abdullah bin Muttalib, ni mtu mzuri kuliko wote katika jamii ya binadamu kiakili, hekima, uzao ulio safi, utakatifu wa maisha yake mwenyewe, na kwa heshima ya familia. Anazo dalili zote za mtu ambaye hatimaye atakuwa mtu mkubwa.
Anamuoa Khadija binti Khuwayled kwa mahari ya vipande 400 vya dhahabu. Natangaza kwamba Muhammad na Khadija sasa ni mume na mke. Mwenyezi Mungu na awabariki wote, na Awe Mlinzi wao.”

Kwenye hotuba yake, Abu Talib alitangaza kwamba ukoo wa Bani Hashim walikuwa warithi wa Ibrahim na Ismail, na walikuwa wabebaji au wachukuaji wa urithi huo. Kwa hiyo, hawakuchafuliwa na ibada ya masanamu.

Abu Talib alipomaliza hotuba yake, Waraqa bin Naufal alisimama kuso­ma hotuba ya harusi kwa niaba ya bibi harusi. Alisema: "Sifa zote na utukufu wote anastahili kupewa Mwenyezi Mungu.

Tunashuhudia na kukiri kwamba yale ambayo umeyatamka kuhusu Bani Hashim ni kweli. Hapana mtu anayeweza kukanusha ubora wao.

Kwa sababau ya uzuri wao, tunakubali ndoa ya Khadija na Muhammad. Ndoa yao inaziunganisha familia zetu mbili na kuoana kwao imekuwa chanzo cha furaha kubwa kwetu. Enyi Walezi wa Quraysh, nawatakeni kuwa mashahidi kwamba ninaridhia Khadija kuolewa na Muhammad bin Abdullah kwa mahari ya vipande 400 vya dhahabu. Mwenyezi Mungu na ajaalie ndoa yao iwe ya furaha.”

(M. Shibli, mtaalam wa historia kutoka India, anasema kwamba mahari ya Hadhrat Khadija ilikuwa vipande 500 vya dhahabu - Siira).

Amr bin Asad, ami yake Khadija mwenye umri mkubwa, naye pia alise­ma kwenye sherehe hiyo na aliyaunga mkono, kwa maneno yake mwenyewe, yale aliyoyasema Waraqa bin Naufal. Na alikuwa yeye ambaye kama mlezi, wa bibi arusi, aliridhika na kumtoa Khadija aolewe na Muhammad bin Abdullah. (Abu Talib alilipa mahari ya mpwa wake.)

Edward Gibbon

“Nyumbani na ng'ambo, wakati wa amani na vita, Abu Talib, ami wa Muhammad aliyekuwa anaheshimiwa sana, alikuwa kiongozi na mlezi wa kijana wake; wakati alipotimu miaka 25 alimuoa mwanamke tajiri mwenye daraja kubwa na mkazi wa Makka, ambaye aliuzawadia uaminifu wake kwa kukubali kuolewa naye pamoja na mali yake. Mkataba wa ndoa, katika jinsi rahisi ya kizamani, unasema kuhusu maelewano ya kimapenzi kati ya Muhammad na Khadija, unamwelezea yeye kama ni mtu hodari sana miongoni mwa kabila la Quraysh na unataja mahari ya wakia kumi na mbili za dhahabu na ngamia ishirini, ambayo ilitolewa kwa ukarimu wa ami wake.”

(Rejea: The Decline and Fall of Roman Empire)

Washington Irving

“Khadija alijaa imani ya kusisimua aliyokuwa nayo kwa msimamizi wake bora sana, Muhammed. Kwenye sherehe ya harusi yake, Halima ambaye alikuwa yaya wa Muhammed wakati alipokuwa mtoto mchanga, aliitwa na kupewa zawadi ya kondoo arobaini.”

(Rejea: The Life of Muhammed).

Wageni wote walimpa hongera Muhammad Mustafa siku ya harusi yake na walimtakia maisha ya furaha. Pia walimpongeza ami wake Abu Talib, kuhusu hafla yenye heri. Pande zote mbili Bwana na Bibi harusi, wali­washukuru wageni wao kwa uchangamfu.

Baada ya kwisha sherehe hizo, Mkuu wa Itifaki aliwaagiza watumwa kugawa chakula. Chakula kilikuwa kingi kupita kiasi kwani ilikuwa haijapata kutokea hapo Makka. Wageni walikula chakula kizuri sana na kila mlo ulikuwa wa mapishi ya aina yake. Wageni walituliza kiu kwa kinywaji kilichochanganywa na maji matamu yatokanayo na maua.

Baada ya chakula kila mgeni alipewa zawadi ya kanzu ya heshima, ili kuafikiana na mila za kale na uungwana wa Arabuni.
Wakati huo huo mkuu wa Itifaki alitangaza kwamba Bibi harusi alikuwa tayari kuondoka.

Ngamia jike aliyetandikwa mapambo ya kitajiri, alibe­ba kibanda mgongoni kwake, alikuwa anangoja kwenye lango la nyum­ba. Wageni wote walikusanyika sebuleni kumwona Bibi harusi akisindikizwa kwenye lango. Watumishi wake walimsaidia Bibi harusi kupanda kwenye kibanda cha harusi.

وَقَالَ ارْكَبُوا فِيهَا بِسْمِ اللَّهِ مَجْرَاهَا وَمُرْسَاهَا ۚ إِنَّ رَبِّي لَغَفُورٌ رَحِيمٌ{41}

"Na akasema: Pandeni humo kwa Bismillah, kwa Jina la Mwenyezi Mungu, kwenda kwake na kusimama kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." (Qur'an 11:41)

Mmojawapo wa watumishi wa kike aliketi kwenye kibanda na Bibi harusi. Kwenye kichwa chake, alivalia tiara la maua na nywele zake zil­isokotwa kwa utepe wa buluu na ncha zenye lulu za kifahari. Alivalia bangili zenye nakshi ya vito vigumu na zenye kung'aa, na alishika kipepeo kilichopambwa na vito.

Kikundi cha watumwa wa Kinubi walibeba mienge, walitembea mbele ya ngamia jike kulia na kushoto.

Bwana harusi naye pia alipanda farasi wake, na yeye, na ami zake, vijana wa Bani Hashim na wageni wao, walirudi nyumbani kwa Abu Talib katika hali na mavazi yale yale waliyoenda nayo mapema siku ile nyumbani kwa bibi arusi.

Wakati msafara huu ulioongozwa kwa mienge ya moto ulipofika nyum­bani kwa Abu Talib, mke wake na dada zake Abu Talib walimsaidia Bibi harusi kuteremka kutoka kwenye kipando chake, ngamia jike. Msimamizi mkuu alimkinga kwa mwavuli wa hariri nyeupe juu ya kich­wa chake na akamwongoza kwenye vyumba vya ndani zaidi kwenye nyumba hiyo.

وَقُلْ رَبِّ أَنْزِلْنِي مُنْزَلًا مُبَارَكًا وَأَنْتَ خَيْرُ الْمُنْزِلِينَ {29}

"Na sema; Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye bara­ka, na Wewe ni Mbora wa wateremshaji."(Quran 23:29).

Kila kitu kilifanyika kwa usahihi wa kiwango cha juu sana. Mawasiliano yalikuwa mazuri sana toka mwanzo hadi mwisho.

Kuoana kwa Muhammad na Khadija ni tukio lililomfurahisha kila mtu lakini furaha ya Abu Talib ilivuka mipaka ya kawaida. Alikuwa na dukuduku la kumuoza mpwa mke mzuri. Dukuduku hili liligeuka kuwa furaha kubwa isiyo na kifani baada ya mpwa wake na Khadija kuoana. Haingekuwa rahisi kupata malingano kama hayo. Abu Talib alimshuku­ru Mwenyezi Mungu kwa furaha mpya aliyoipata, na furaha yake iliwa­pata pia ndugu zake, Abbas na Hamza na watu wengine wote wa ukoo wa Hashim.

Siku tatu baada ya harusi, Abu Talib alifanya karamu ya chakula kush­erehekea tukio ambalo tangu hapo mpaka sasa linaitwa "karamu ya wal­ima." Jiji lote lilinga'a kwa ukarimu wake. Kila mkazi wa Makka alikuwa mgeni mwalikwa wa karamu hiyo. Muhammad, ambaye alikuwa Bwana harusi, alikuwa anawakaribisha wageni. Yeye mwenyewe (Muhammad), ami zake, Binamu zake na vijana wote wa ukoo wa Bani Hashim, walijivunia kuwa wenyeji wa sherehe hiyo. Karamu hiyo ilidumu kwa muda wa siku tatu. Miaka mingi baadaye,
Uislamu uliifanya karamu ya walima kuwa kumbukumbu ya karamu ya Abu Talib aliyoifanya kwenye harusi ya Muhammad na Khadija, na kui­weka kama desturi ya ndoa zote za Waislamu. Abu Talib alikuwa mtu wa kwanza kuitekeleza. Karamu ya walima haikujulikana katika bara lote la Arabu kabla ya harusi ya Muhammed na Khadija.

Abu Talib alilazimika kufikiri kama ingewezekana ndugu yake mpend­wa Abdullah na mkewe Amina, Mwenyezi Mungu awateremshie rehe­ma zake, wao pia kama wangekuwepo kushuhudia na kuibariki ndoa ya mtoto wao, na kushiriki pamoja katika ile furaha yake (Abu Talib). Lakini hata kama Abbullah na Amina wangekuwepo, harusi ya mtoto wao hainge sherehekewa kwa fahari na tamasha kuzidi alivyofanya Abu Talib kama mlezi wa Muhammad.

Ilifuata zamu ya Khadija kuonyesha ukarimu na wema wake. Ukarimu na wema yalikuwa mazoea yake makubwa. Na hafla gani ambayo ingemfaa zaidi au kupendelea kama si kwenye sherehe ya harusi yake kutosheleza hulka yake? Kwa hiyo, Khadija, alimwagiza mkuu wake wa Itifaki kutayarisha mipango kwa kuandaa karamu/tafrija kubwa kabisa ya chakula na kuweka historia katika Makka.

Hiyo ilikuwa karamu ya kukumbukwa kweli. Hata ombaomba wa Makka na makabila ya watu wanaohama hapa na pale na wanawake, walikuwa kwenye kundi la waalikwa. Watu walikula vyakula ambavyo kamwe hawajapata kuviona. Wale Waarabu wa jangwani ambao kamwe walikuwa hawajawahi kuonja kitu chochote isipokuwa maji ya chumvichumvi au yanayonuka katika maisha yao siku hiyo walikunywa maji ya waridi wakiwa wageni wa Khadija. Kwa muda wa siku nyingi wageni waalikwa matajiri na fukara, mashuhuri na wenye daraja la chini, mamwinyi na wanyonge, vijana na wazee walikula nyumbani kwa Khadija. Khadija aliwapa wageni waalikwa walio maskini, vipande vya dhahabu na fedha na nguo, na alijaza nyumba za wajane wengi na wato­to yatima mahitaji mengi ya muhimu ambayo hawakuwa nayo.

Khadija alikaa miaka mingi ya maisha yake akingojea mwanamume anayefaa kumuoa. Alipata mafanikio baada ya kungoja kwa muda mrefu alipojitokeza Muhammad, na wakaunganishwa katika ndoa takat­ifu.

Ndoa ya Muhammad na Khadija ilikuwa ya kwanza na ya mwisho kwa aina yake hapa duniani. Ilikuwa ni ndoa hiyo tu duniani pote ambayo ilipata neema za akhera na mali za hapa duniani. Ilikuwa ndoa ambayo ilipata rehema nyingi zisizo na kipimo na hesabu za peponi na hapa duniani.

Inawezekana kabisa kwamba katika Bara Arabu lote, hakuna mwanamke yeyote ambaye alipata kwenda nyumbani kwa mumewe na mahari nyingi kiasi hicho kama alivyofanya Khadija.

Ilijumuisha watumwa, wasichana, mbuzi na kondoo, na nguo zake binafsi za bei ghali, vitu vya ziada, vitu vya urithi visivyoweza kukadiriwa bei, mapambo, vitu vya thamani vya chuma, vito vya thamani na dhahabu nyingi na vipande vya fedha.

Mahari hii, ambayo haikutazamiwa kuwa hivyo kwa ubora na wingi wake, haikuwa zawadi aliyopewa Khadija, Bibi harusi na ami zake au kutoka kwa kaka zake.

Haya yalikuwa ni matokeo ya jitihada zake mwenyewe. Alizalisha mali hiyo kwa uangalifu wake, bidii yake, busara zake na uwezo wa kuona mbali kifikira.

Lakini huu haukuwa ndio tu utajiri aliokuja nao Khadija. Khadija pia alikuja na utajiri wa moyo na akili, na hivi vilikuwa havina kipimo na visivyokwisha. Katika miaka iliyofuata, Khadija aliyatajirisha pasipo kipimo maisha ya mumewe kwa kutumia vipaji hivyo.

Mara tu Khadija alipoolewa, alionekana kupoteza upendeleo wake kwenye biashara na milki yake ya biashara. Maisha ya ndoa yalibadil­isha tabia yake, kujitolea kwake, na wajibu wake. Alimpata Muhammad Mustafa, hazina kubwa kuliko zote hapa duniani. Mara Khadija alipompata Muhammad, dhahabu, fedha na almasi zilipoteza thamani; kwake Muhammad Mustafa Mjumbe mtarajiwa wa Mwenyezi Mungu na Mtume mtarajiwa wa Uislamu, akawa ndio tu, kitu cha kuelekeza mapenzi yake, uangalifu wake na bidii yake.

Mambo kama yalivyokuwa, hakupoteza uwezo wake mkubwa wa kupanga mambo, lakini badala ya kutumia uwezo huo katika biashara zake, aliutumia kwa kumtumikia mumewe. Aliyapanga maisha yake yote upya na kumfanya Muhammad Mustafa kuwa ndio mhimili wake wa maisha.

Khadija hakusitisha biashara zake nyingi mara moja. Alizisimamisha kwa awamu. Kwa hiyo, kwa viwango alisimamisha biashara ya kuin­giza mali ndani ya nchi na kutoa nje ya nchi ambayo baba yake ali­ianzisha.

Miaka iliyofuata baada ya ndoa yake, Muhammad alianza kusafiri tena na misafara ya Khadija kwenda Syria. M. Shibli, mtaalam wa historia kutoka India, anasema kwamba pia alikwenda Yemen. Popote alipokwenda, alipata faida kubwa. Khadija pia aliajiri Mameneja wengine ambao waliuza bidhaa zake, au walinunua bidhaa kwa ajili ya mauzo yake, na wao pia walipata faida. Lakini, msisitizo ulibadilishwa, badala ya kupanua biashara yake kama alivyokuwa anafanya kabla ya kuolewa, Khadija alianza kupunguza bidhaa polepole hadi hapo ambapo bidhaa zote ziliuzwa, na alikusanya fedha zote kutoka kwenye miradi.

Wakati Malikia wa Makka alipoingia nyumbani kwa mumewe, Muhammad Mustafa, awamu ya maisha yake ya furaha kubwa ilianza. Awamu hii ilidumu miaka ishirini na tano - hadi kifo chake. Mara moja Khadija alibadili maisha yake na kuafikiana na mazingira mapya. Tangu siku ya kwanza alianza usimamizi wa kazi yake ambayo ilikuwa kuyafanya maisha ya mume wake kuwa ya furaha na mazuri. Katika kufanya kazi hii alifuzu vizuri sana kama historia ya siku zilizofuata ilivyosadikisha kwa ufasaha kabisa.

Maisha ya ndoa yalifungua ukurasa mpya ya maisha ya Muhammad na Khadija. Jambo la msingi la "ukurasa" huu mpya ilikuwa furaha - fura­ha isiyo na dosari. Pamoja na kwamba ndoa yao ilipewa baraka za fura­ha, pia ilipata neema ya watoto. Mtoto wao wa kwanza, alikuwa wa kiume aliyeitwa Qasim.

Ilikuwa baada ya kuzaliwa Qasim, baba yake Muhammad Mustafa alipewa jina la Abul-Qasim - (baba wa Qasim) ­kufuatana na mila za kiarabu.

Pia mtoto wa pili alikuwa wa kiume. Jina lake lilikuwa Abdullah. Alipewa majina ya lakabu ya Tahir na Tayyib. Watoto wote wawili walikufa wakiwa bado wachanga.

Mtoto wa tatu na wa mwisho na ndio huyo tu aliyeishi muda mrefu miongoni mwa watoto wa Muhammad na Khadija alikuwa binti yao, Fatuma Zahra, mtoto wa kike. Ingawa Mwenyezi Mungu aliwatunuku zawadi nyingi, hakukuwepo na chochote kile kingine walicho kithami­ni zaidi ya binti yao. Fatuma alikuwa "mwanga wa macho" ya baba yake, na alikuwa "starehe ya moyo wa baba yake." Alikuwa pia "Kiongozi wa Wanawake wa Peponi." Baba na mama walimpenda sana, na alileta pamoja naye matumaini na furaha na baraka na huruma Zake Mwenyezi Mungu ndani ya nyumba yao.

Sura Ya Tano: Mwanzo Wa Kutangazwa Kwa Uislamu

Pamoja na ukweli kwamba nchi ya Arabuni ilikuwa dimbwi la dhuluma na ngome ya ibada za masanamu na kumshirikisha Mwenyezi Mungu, Muhammad mwenyewe hakushiriki katika uovu huo na hakutenda dhambi, na hakulisujudia hata sanamu moja. Hata kabla ya kutangaza kwamba alikuja kuanzisha Ufalme wa Mbinguni hapa Duniani, mwe­nendo na tabia yake ulionyesha maelekezo ya Qur'an Majid - Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Rasimu ya Uislamu.

Hata maadui zake hawakuweza kuonyesha tofauti baina ya tabia yake na maandiko ya Qur'an- wakati wowote - kabla na baada ya kutangaza ujumbe wake ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Baada ya Kutangaza ujumbe wake kama Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alipiga marufuku uendeshaji wa mila za upagani. Lakini hakuna ushahidi kwamba kabla ya tukio hilo, yeye mwenyewe alikwisha jihusisha na tendo la upagani, au tendo lolote linalopingana na Qur'an.

Inaonyesha kama vile Qur'an Majid iliandikwa kwenye moyo wa Muhammad toka mwanzo hadi mwisho na inaonyesha pia kwamba ali­hubiri Uislamu hata kabla ya kutangazwa kwa ujumbe wake, lakini, kwa matendo yake na si maneno yake.

Matendo yake yalieleweka wazi kama maneno yake, na yaliitangazia dunia kwamba yeye alikuwa mtu wa aina gani. Hata hivyo, wapagani ndio waliompa jina la As-Sadiq (Mkweli) na Al-Amin (Mwaminifu), na watu hao hao ndio, baada ya miaka kupita, walimtesa, walimuwinda, walimtenga na walikuwa tayari kumpa zawadi mtu atakayemuua.

Mwenendo wa maisha ya Muhammad ulihubiri mahubiri ya kimya kimya!

Pamoja na kwamba wapagani wa kiarabu walikuwa wapotofu na wako­rofi, hata hivyo walivutiwa na ukweli na uliwavutia hata kama ulikuwa kwa adui. Walivutiwa na Muhammad kwa sababu ya ukweli wake, laki­ni mapenzi yao hayakuwazuia wao kufanya njama ya kutaka kumuua aliposhutumu ibada za masanamu na ushirikina. Hawakupenda kitu kingine kama kumuua tangu hapo alipowaambia waingie kwenye Uislamu, lakini hawakuhoji hadhi yake na uaminifu wake.

Kwa jambo hili hapawezi kuwa na ushahidi wa kutokutuhumiwa zaidi kuliko tabia yao.

Raia wa Makka hawakupenda uaminifu wa Muhammad tu lakini pia walipenda uamuzi wake. Ilitokea wakati fulani, Maqurayshi walikuwa wanaijenga upya Kaaba, na kwenye mojawapo ya kuta zake ilitakiwa Jiwe Jeusi libandikwe. Palihitajika mtu alilete Jiwe Jeusi kwenye eneo la jengo, alinyanyue kutoka chini na kuliweka mahali pake ukutani. Nani angeifanya kazi hiyo?

Kila ukoo wa Quraysh ulidai heshima ya kustahili kufanya kazi hiyo lakini koo nyingine hazikuwa tayari kushindwa katika jambo hili.

Kutokukubaliana huko kulisababisha kutolewa hotuba zenye kuashiria vita, na haikupita muda mrefu watu walikuwa tayari kupigana. Mapigano hayo yangeamua nani angeweka Jiwe Jeusi kwenye ukuta.

Wakati huo huo mzee mmoja wa Kiarabu aliingilia kati, na kushauri kwamba badala ya kupigana na kuuana, Wakuu wa koo wangoje mpaka kesho yake asubuhi waone nani angekuwa mtu wa kwanza kuingia kwenye eneo la Al-Kaaba, na halafu wapeleke kesi hiyo kwake kwa uamuzi.

Ushauri huo ulikuwa wa busara na wakuu walitumia hekima kuukubali. Asubuhi ya siku iliyofuata, lango la Al-Kaaba lilipofunguliwa wal­imuona mtu wa kwanza aliyeingia ni yule aliyepewa majina ya Sadiq na Al-Amin. Wote walifurahi kwamba alikuwa yeye, na wote walikubaliana kupeleka shauri lao kwake, na kuahidi kukubali uamuzi wake.

Muhammed aliagiza nguo iletwe na itandikwe chini. Halafu akaliweka Jiwe juu ya nguo hiyo, na alimtaka kila mkuu wa ukoo anyanyue mojawapo ya pembe ya nguo hiyo, na kubeba mpaka chini ya ukuta wa Al-Kaaba. Baada ya kufanyika hivyo, yeye mwenyewe alilinyanyua Jiwe na kuliweka mahali pake.

Uamuzi wa Muhammad ulimridhisha kila mmoja. Kwa kutumia hekima yake, alizuia yasitokee mambo ya kufedhehesha na aliondoa umwagaji damu.

Tukio hilo pia lilithibitisha kwamba wakati wa machafuko, Waarabu waliheshimu maoni yake. Walijua kwamba Muhammad alikuwa na sifa za kiwango cha juu kulingana na mizani ya maadili yao.

Muhammad alikuwa kiongozi wa binadamu aliyefanya kazi hiyo kwa msukumo wa wahyi.

Bwana Willam Muir

“Hali iliyosababisha fursa ya Muhammad kutoa uamuzi wakati Al-Kaaba ilipokuwa inajengwa upya na kuweka Jiwe Jeusi mahali pake, inavutia kuonyesha kwamba hapakuwepo na chombo chenye mamlaka kuu hapo Makka.”

(The Life of Muhammed, London, 1877).

Wakati huu Muhammad alikuwa na umri wa miaka 35. Mashavu yake yalionyesha rangi ya fedha iliyofifia. Alikuwa mtu ambaye aliyeipenda sana familia yake, alikuwa anawapenda sana watoto. Watoto wake wanaume, Qasim na Abdallah, walikufa wakiwa wachanga. Baada ya vifo vya watoto wao, yeye na Khadija walimchukua Ali kuwa mtoto wao wa kiume. Ali alikuwa mtoto mdogo zaidi ya watoto wote wa ami na mlezi wa Muhammad, Abu Talib.

Alikuwa na umri wa miaka mitano alipokuja nyumbani kwao, na aliziba pengo katika maisha yao, walim­lea na kumsomesha. Hadi alipokua, alikuwa katikati ya mapenzi yao.

Katika miaka iliyofuata, Ali alijionyesha kwamba alikuwa natija bora sana ya malezi na elimu ambayo Muhammed na Khadija walimpa. Ali alikuwa na bahati ya kuwa kijana hodari katika msafara wote wa Muhammad, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu.

“Mara baada ya Al-Kaaba kujengwa upya, Muhammad alijiliwaza kutokana na hasara ya kumpoteza mtoto wake mchanga Qasim kwa kumfanya Ali, mtoto wa rafiki yake na mlezi wake huko nyuma, Abu Talib, kuwa mwanawe.

“Ali wakati huo akiwa na miaka mitano au sita, wakati wote alikuwa na Muhammad na walionyeshana huba ya mzazi na mtoto.”

(The Life of Muhammed, London, 1877.)

Kama ambavyo imeelezwa kwenye kurasa za nyuma, Muhammad ali­jaaliwa akili ya tafakuri sana. Jinsi muda ulivyopita, alizidi kuwa kati­ka hali ya kutafakari, alikwisha gundua pango liitwalo Hira, lililopo maili tatu kwenye vilima vilivyopo Kaskazini Mashariki ya Makka.

Ili kuondokana na fadhaa za kutoka nje na usumbufu wa aina yoyote, wakati wa kutafakari, alihama jiji,
alikwenda kwenye vilima na alipi­tisha siku zake nyingi za msimu wa kipupwe huko katika pango la Hira.

Wakati mwingine Muhammad Mustafa alikwenda Hira peke yake, laki­ni mara nyingi alikuwa anamchukua Khadija na kijana mdogo Ali. Wote watatu walipitisha siku yote juu ya kilima cha Hira walirudi nyumbani jioni.

Kutoka kwenye majabali ya Hira, Muhammad aliweza kutazama mand­hari ya ukubwa wa mbingu na dunia, na kwa mshangao wa kimya ali­fikiria mahali zilipokutana.

Vipi mtu ataweza kutambua ukubwa wa Muumba Ambaye ameumba ukubwa huo na Ambaye huudhibiti wote? Kipi kilichokuwa cha kushangaza sana kama nyota zimemetukazo kati­ka anga iliyotulizana, au kama kuvutia sana kama yalivyo majaliwa ya mwanadamu? Na je, mtu yeyote anaweza kupima siri ya dhana mbili kubwa ambazo zimeshikilia ulimwengu - anga (Makan) na zama (Zaman)? Muhammad alitafuta majibu ya maswali ambayo hushika­mana na siri za kudumu za kuwepo kwa mwanadamu.

Kwa maoni yake, Uumbaji wote ulifunikwa kwenye ghaibu. Alitumia muda wa saa nyin­gi akitafakari juu ya akili ya kutisha na uthabiti wa Uumbaji.

Lakini kama ulimwengu ulivyokuwa wa siri, ilikuwa dhahiri kwa Muhammad kwamba ulitawaliwa na sheria zisizobadilika. Alikuwa takriban anaona utaratibu na mfumo huo ukifanya kazi, bila ya utarati­bu na mfumo huo matokeo yake yangekuwa vurugu tupu kwenye Uumbaji wa mbingu na dunia.

Miaka michache baadaye Muhammad alipowaambia Waarabu kwamba Mungu amemtuma miongoni mwao ili awe mjumbe Wake, walimpa changamoto wakimtaka awaonyeshe "mujiza." "Mujiza?" aliuliza Muhammad.

Kuona mujiza, walichotakiwa kufanya ni kufungua macho yao na kutazama kile kilicho wazunguka. Je! Si kweli kwamba ulimwengu umejaa miujiza? Kuna miujiza yenye kustaajabisha zaidi ya kuchomoza na kuchwa kwa jua, mwezi mpevu ulioko kwenye mwendo kukatiza anga, nyota zilizopo kwenye mizunguuko, mbingu yenye nuru na joto, mabadiliko ya majira, kina cha bahari kinachobadilika, na mapenzi ya mama kwa mtoto?

Kama ukubwa na utukufu wa Uumbaji ulijaza akili ya Muhammad mshangao, pia moyo wake ulijaa unyenyekevu. Inaweza kuwa ilitokea kwake kwamba kama akili haikuweza kumtambua Muumbaji na kazi zake nzito, labda mapenzi yangeweza. Kwa hiyo, aliruhusu akili kuzidi­wa na mapenzi - mapenzi kwa Muumbaji wake.

Pia Muhammad alitafakari kuhusu hali ya Waarabu, ibada zao za masanamu, tamaa yao ya kuua, na kuua watoto wa kike, na maisha yao yasiyo na maana, mwelekeo, matumaini na ya kuhuzunisha.

Lakini, miaka mingi ya "mazoezi ya kiroho" na uvumbuzi wake wa pekee kuhusu miliki ya roho, ilikuwa inakaribia kufikia mwisho.

Inawezekana alikwisha ona kwamba muda wa kuacha maisha ya kufikiri na kutafakari ulifika, na kwamba baada ya muda mfupu alikuwa anatumbukia kwenye utekelezaji wa vitendo na mapambano.

Sura Ya Sita: Kutangazwa Kwa Uislamu

Kipindi kirefu cha matayarisho aliyotakiwa kuyafanya Muhammad ili aje kusimamia kazi zake na wajibu wake kama Mtume Mkubwa wa Mwisho wa Mungu hapa duniani kilikwisha.

Usiku wa upagani, makosa na ujinga vimekuwa vya muda mrefu, vyenye giza nene, vyenye kutia huzuni na majonzi. Mwanadamu alik­wisha fika katika hali ya kutokutambua kama kweli ingewezekana kuonekana hali ya kuleta matumaini.

Ilikuwa ni kwa sababu ya huruma za Mungu zisizo na kipimo ndizo zili­zo kumbusha shauku ya muda mrefu isiyotamkwa. Katika kutoa jibu kwa ombi lake (mwanadamu) la kimya, kimya "Jina" la Uislamu lili­chomoza kutoka kwenye bonde la Makka kushinda giza la ushirikina hapa duniani, na kutangaza ushindi wa imani ya Tauhid (Kumpwekesha Mwenyezi Mungu).

Muhammad alikuwa na umri wa miaka 40 alipoamriwa na Mwenyezi Mungu, kupitia kwa malaika Wake Jibril kutangaza Upweke Wake Tauhid, kwa watu wanaoabudu masanamu na washirikina wa ulimwen­gu wote, na kufikisha ujumbe wenye matumaini mapya na amani kwa jamii ya binadamu iliyokuwa inajihami wakati wote.

Kwa kukubali amri hii ya Mbinguni, Muhammad aliasisi mpango wa maana sana uitwao - Uislamu, ambao ulibadilisha majaliwa ya binadamu daima milele. Msingi wa madhumuni ya Uislamu, kama alivyoupokea kutoka kwa malaika Jibril, ulikamilishwa mbinguni, na sasa alitakiwa aufikishe kwa Jamii ya kibinaadamu.

Kabla hajapokea Ujumbe wake wa kiutume, Muhammad alikuwa akitu­mia mchana na usiku katika kusali na kutafakari wakati mwingine nyumbani kwake na wakati mwingine kwenye pango la jabali Hira, (kama ambavyo imeelezewa hapo kabla) kwa muda wa siku nyingi.

Siku moja, saa za jioni alipokuwa kwenye pango la Hira Malaika Mkuu Jibril alimtokea, na alimpa habari kwamba Mwenyezi Mungu alimteua yeye kuwa mjumbe wake wa mwisho hapa duniani, na alimwamuru afanye kazi ya kumwondoa mwanadammu kutoka kwenye vurugu ya dhambi, makosa na ujinga na kumleta kwenye mwanga wa Mwongozo, ukweli na ujuzi. Halafu Jibril alimwambia Muhammad "asome" Aya zifuatazo:

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ {1}

خَلَقَ الْإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ {2}

اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ {3}

الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ {4}

عَلَّمَ الْإِنْسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ {5}

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

“Soma kwa Jina la Mola wako Mlezi aliyeumba,
“Amemuumba binadamu kwa pande la damu,
“Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!
“Ambaye amefundisha kwa kalamu.
“Kamfundisha mtu aliyokuwa hayajui."
(Qur'an Majid 96: 1-5).

-Aya hizi tano zilikuwa ndio ufunuo wa kwanza kabisa, na ziliteremsh­wa kwa Muhammad Mustafa kwenye Usiku huo Mkuu "au" "Usiku Uliobarikiwa" mnamo mwezi wa Ramadhani (Mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu) ya mwaka wa 40 wa Ndovu.

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ{185}

"Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa Qur'an kuwa ni mwongozo kwa watu, na hoja zilizowazi za uwongofu na upam­banuzi kati ya wema na Ubaya." (Qur'an Majid 2: 185)

إِنَّا أَنْزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ {1}

"Hakika sisi tumeiteremsha Qur'an katika Laylatul Qadri, Usiku wa cheo Kitukufu..."
(Qur'an 97:1)

وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ {2}

إِنَّا أَنْزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُبَارَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنْذِرِينَ {3}

"Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha,
"Hakika tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa..."
(Qur'an Majid 44:2-3)

"Usiku wa Cheo Kitukufu" "au" "Usiku Uliobarikiwa" hutokea wakati wa kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhani, na inawezekana kuwa mwezi 21 au 23 au 25 au 27 ya mwezi huo. Kwa mujibu wa Hadithi. Na kwa mujibu wa kalenda ya Gregory, ufunuo wa kwanza uliteremshwa kwa Mtume tarehe 12, Februari, 610 kama anavyotaarifu

Mahmud Pasha al-Falaki wa Misri. Aya hizi tano zimo mwanzoni mwa Sura ya 96 ya Qur'an Majid. Jina la sura ni Iqraa (soma) au Alaq (Tone la Damu).

Katika maelezo yao kuhusu Muhammad Mustafa kupokea Ufunuo wa kwanza, Suni na Shia hawakubaliani. Kwa mujibu wa hadithi za Sunni, kutokea kwa Jibril ni jambo ambalo lilimshangaza Muhammad, na malaika alipomwamuru asome alisema "Siwezi kusoma."

Hii ilifanyika mara tatu, na kila mara Muhammad alipotamka kutokuwa na uwezo wa kusoma malaika alimbana tumbo. Hatimaye aliweza kukariri hizo Aya 5 kisha ndipo malaika naye alimwachia na kutoweka.

Malaika Jibril alipotoweka Muhammad ambaye alikwisha "tangazwa" kuwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alishuka kutoka kwenye majabali ya Hira na alikwenda nyumbani kwake akiwa na wasiwasi sana. Ni dhahiri, malaika Jibril kuingia ghafla pangoni ilisababisha kiwewe.

Alikuwa anatetemeka kwa sababu ya baridi, na alipofika nyumbani kwake alimwambia mkewe Khadija amfunike blanketi na alifanya hivyo. Baada ya hali ya woga kumtoka, alimwelezea mkewe kuhusu mkutano wake na Malaika Jibril ndani ya pango la Hira.

Maelezo ya Hadithi ya Sunni kuhusu tukio hili ipo kwenye makala iliyoandikwa na sheikh Ahmad Zaki Hammad, (Ph. D.) Chini ya kichwa cha habari; "Uwe na Matumaini" iliyochapishwa kwenye gazeti la Islamic Horizons of the Islamic Society of North America Plain field, Indianic Mei-June, 1987, kama ifuatavyo:

"Mtume (s.a.w.) katika hatua zake za mwanzo mjini Makka, alihofia kwamba kuteremshwa kwa ufunuo ilikuwa ni mguso wa kishetani ili kusumbua mawazo yake, kumchezea kiakili, kuvuruga utulivu na amani ya akili yake. Alihofu kwamba jini mojawapo lilimwingia. Alimuelezea haya Khadija. Hofu yake ilizidi kiasi kwamba... (na tafad­hali usishangazwe na taarifa sahihi iliyopo kwenye sahili Bukhari) Mtume (S.a.w.w.) alitaka kujiua ili asije akaguswa na shetani, apotosh­we, avurugwe na kuharibiwa."

Lakini kwa mujibu wa maelezo ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, ni kwamba; Muhammad Mustafa, mbali na kutokushangazwa, hakuhofish­wa na tukio la kukutana na Malaika Mkuu Jibril. badala yake alimkaribisha kama vile alikuwa anamtazamia. Malaika Jibril alileta habari njema kwamba Mwenyezi Mungu alimteua yeye kuwa Mjumbe wake wa mwisho kwa binadamu, na alimpongeza kuchaguliwa kuwa mpokeaji wa heshima kubwa kuliko zote kwa kiumbe wa hapa duniani.

Muhammad alikubali bila kusita ujumbe wa utume wala hakupata shida kukariri Aya za Ufunuo wa Mwanzo. Alizisoma au alizikariri aya hizo bila shida wala bila kuongozwa.
Kwa hakika Jibril hakuwa mgeni kwake, na pia alitambua kwamba yeye akiwa mtumishi wa Mwenyezi Mungu, wajibu wake ni kutekeleza ujumbe aliopewa na Mwenyezi Mungu. Muhammad alikwisha tayarishwa kuuendeleza ujumbe huo hata kabla Jibril hajamtembelea. Jibril alimpa tu ishara za kuanza.

Waislamu wa madhehebu ya Shia pia wanasema kwamba kitu kimoja ambacho Jibril hakufanya ni kutumia nguvu za kimwili kumbana Muhammad na kumwambia asome. Kama alifanya, kweli ingekuwa mtindo wa kioja wa kumfundisha Muhammad, uwezo wa kusoma -kwa kumbana au kumkaba. Pia Shia wanaendelea kueleza kwamba Muhammad Mustafa hakufikiria kujiua hata mara moja katika maisha yake, hata alipokuwa amehuzunishwa sana, na haikupata kutokea kwamba angeingiwa na "shetani" au "angepotoshwa, kuvurugwa au kuchafuliwa."

Katika mazingira haya, Waislamu wa madhehebu ya Shia wananukuu Aya mbili za Quran Majid ambazo zinaonekana kuwa na uhusiano wa kimantiki kuhusu kisa hiki: (Mwenyezi Mungu alimwambia Shetani) "Hakika wewe huna mamlaka juu ya waja wangu. Na Mola wako Mlezi anatosha kuwa ni wa kutegemewa."(Qur'an Majid 17:65)

Mwenyezi Mungu mwenyewe huwalinda waja wake waaminifu na wa kweli kutoka kwenye mfumo wa Shetani; hawezi kuwa na mamlaka juu yao, na hawawezi kubadilishwa, au kuvurugwa au kuharibiwa.

وَيُنَجِّي اللَّهُ الَّذِينَ اتَّقَوْا بِمَفَازَتِهِمْ لَا يَمَسُّهُمُ السُّوءُ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ{61}

"Na Mwenyezi Mungu atawaokoa wenye kujikinga kwa ajili ya kufuzu kwao. Hapana Uovu utakaowagusa, wala hawatahuzuni­ka".(Qur'an Majid 39:61)

Hakuna uovu ambao ungemgusa Muhammad, mteule wa Mwenyezi Mungu Mwenyewe. Chini ya ulinzi wa Mungu alikuwa salama, hivyo kwamba haguswi na ouvu wowote.

Aliishi chini ya mamlaka ya kishe­ria ya Mungu wakati wote. Hata hivyo, Muhammad alikuwa na wasi­wasi kuhusu ukubwa wa kazi iliyokuwa mbele yake.

Alielewa kwamba katika utendaji wa kazi yake, angekutana na upinzani mkubwa, wenye kuogofya na uliodhamiria kutoka kwa wapagani dunia nzima.

Hali ya shauku yake ilikuwa dhahiri. Kwa hiyo alikuwa na mawazo ya huzuni alipoondoka pangoni kwenda nyumbani kwake. Na kweli alimwambia Khadija amfunike blanketi alipoketi na kumwelezea yaliyo tokea huko pango la Hira.

Khadija aliposikia habari aliyoambiwa na Muhammad Mustafa, alimli­waza na kumhakikishia kwa kumwambia "Ewe mwana wa ami yangu, uwe na matumaini mema. Mwenyezi Mungu amekuteua wewe kuwa Mjumbe wake. Mara nyingi wewe ni mkarimu kwa jirani zako, unawa­saidia ndugu zako, unawapa yatima, wajane na masikini na mwema kwa wageni. Mwenyezi Mungu kamwe hatakutelekeza."

R.V.C,Bodley

"Mungu ni ulinzi wangu, Ewe Abul Qasim" Khadija alisema: "Furahi na uwe na matumaini mema. Yeye ambaye mikononi mwake maisha ya Khadija yanategemea, ni Shahidi wangu kwamba wewe utakuwa Mjumbe wa watu Wake!"

(Messenger, The Life of Mohammad, 1946).

Inawezekana kwamba Muhammad mara moja alizidiwa na fikira ya kuwajibika kwa Mwenyezi Mungu katika kutekeleza mzigo mkubwa mno wa kazi yake mpya, lakini, aliposikia maneno ya Khadija ya kumpa matumaini, haraka sana alijisikia mfadhaiko unapungua.

Khadija alimhakikishia na kumshawishi kwamba, pamoja na msaada wa Mwenyezi Mungu alio nao, atasimama kidete katika utendaji wake na atashinda vizuizi vyote.

Muhammad alikubali. Tangu wakati huo alitambua kwamba Khadija alikuwa "chombo" ambacho kingeimarisha ujasiri wake endapo ungetetereka, na angekuwa tegemeo la imani yake endapo angelegalega.

Aya ifuatayo pia inaunga mkono maoni ya dhehebu la Shia:

"Na tulipochukua ahadi kwa Manabii na kwako wewe, na Nuhu na Ibrahim na Isa mwana wa Mariamu na tulichukua kwako ahadi ngumu, ili (Mwenyezi Mungu) awaulize wakweli juu ya ukweli wao. Na amewaandalia makafiri adhabu chungu." (Qur'an Majid 33:7­8)

Maoni ya Mfasiri

“Kuna dokezo za mkataba juu ya kila kiumbe kufuata Sheria ya Mungu, nayo ni sheria ya kuwepo kwao. Lakini kuna dokezo la mkataba maalu­mu na Mitume, uliotongolewa sawasawa na makini, kwamba mitume watatekeleza ujumbe wao, watatangaza kweli ya Mungu bila woga au upendeleo, na kuwa tayari wakati wote kufanya kazi yake katika hali yoyote. Hiyo inawapa mitume nafasi yao na hadhi na madaraka yao makubwa sana kuhusu watu ambao wamekuja kuwaelekeza na kuwaon­goza kwenye Njia iliyonyooka.” (A. Yusufu Ali).

Waislamu wa madhehebu ya Shia wanasema kwamba Mwenyezi Mungu alichukua mkataba kutoka kwa Muhammad wa kufikisha Ujumbe Wake wa Mwisho kwa Mwanadamu.

Kwa hiyo, hawakubaliani na wanahistoria ambao hudai kwamba Muhammad alishangaa, alishtu­ka na kuogopa alipotembelewa na Jibril. Wanasema, maonyesho kama hayo ya hisia, hayaafikiani na mwenendo wake, na hayalingani na tabia ya Mkataba wake ulio makini.

Baada ya muda mfupi, Jibril alimtokea tena Muhammad alipokuwa kwenye pango la Hira, na alimpa Ufunuo wa pili ambao unasomeka kama ifuatavyo:

"Ewe uliyejigubika! Simama uonye! Na Mola wako Mlezi Mtukuze!" (Quran Majid 74:1-3).

Amri kutoka Mbinguni ya "simama na uonye" ilikuwa ishara kwa Muhammad (aliyejigubika blanketi) kuanza kazi yake. Jibril alimweleza waziwazi kazi zake mpya na ya kwanza kabisa ilikuwa kuharibu ibada ya miungu ya uongo, na kusimika bendera ya Tauhid ­imani ya Upweke wa Muumba - hapa ulimwenguni, na alitakiwa kuwaita wanadamu kwenye Imani ya kweli - Uislamu. Uislamu maana yake ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na kukubali kwamba Muhammad ni mtumishi Wake na Mjumbe Wake.

"Alif Lam. Hiki ni kitabu tulicho kiteremsha kwako ili uwatowe watu kwenye giza uwapeleke kwenye nuru, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe kwenye Njia ya Mwenye nguvu, Msifiwa." (Quran 14: 1).

Muhammad alitakiwa kuwaongoza wanadamu kutoka kwenye kina cha giza nene na kuwaleta kwenye nuru.

"Muhammad angewaongozaje wanadamu kutoka kwenye kina cha giza nene na kuwaleta kwenye nuru” Swali hili linajibiwa na Quran Majid kwenye aya ifuatayo:

"Kama tulivyo mtuma Mtume kwenu, anayetokana na ninyi, kukutakaseni na kukufundisheni Kitabu na hekima na kukufundisheni mliyokuwa hamyajui." (Qur'an Majid 2:151).

Qur'an iko sahihi na bayana katika kufafanua dhana ya kazi yake kwa ajili ya Muhammad Mustafa. Alitakiwa kuwaongoza wanadamu kutoka kwenye "dimbwi la giza" na kuwapeleka kwenye nuru, kwa:

1. Kukariri Aya za Mwenyezi Mungu,

2. Kuwatakasa wanadamu

3. Kuwafundisha wanadamu yale yaliyomo kwenye maandiko na hekima, na

4. Kuwapatia wanadamu ujuzi mpya.

Jibril na Muhammad walitoka nje ya pango. Jibril alimfundisha kutawadha (matendo ya kujitakasa kabla ya sala). Muhammad alitawadha, na halafu waliswali pamoja na Jibril akiongoza swala, ilipoisha Jibril aliagana na Muhammad na kupaa
Jioni hiyo, Muhammad alirudi nyumbani kwake akiwa anafahamu zake na makini kwa kazi yake mpya ya "kusimama na kuonya."

Alitakiwa kuhubiri Uislamu, Dini ya Mwenyezi Mungu, duniani pote, na alitakiwa kuanza kuifanya kazi hiyo nyumbani kwake kwa kuhubiri kwa mkewe.

Muhammad alimwambia Khadija kuhusu Jibril kumtembelea kwa mara ya pili, na kazi aliyo amriwa na Mwenyezi Mungu kuifanya ya kumlin­gania yeye kwenye Uislamu.

Kwa Khadija, uadilifu na unyofu uliotangulia wa mumewe, ulikuwa uthibitisho usiopingika kwamba yeye alikuwa mjumbe wa Mungu, na tayari aliukubali Uislamu.

Hakika, "uhusiano wa kiitikadi" kati yake na Uislamu, ulikwisha kuwepo. Kwa hiyo, Muhammed Mustafa aliupele­ka Uislamu kwa Khadija mara moja "aliutambua", na aliukubali kwa matumaini makubwa. Aliamini kwamba Muumba alikuwa Mmoja na Muhammad alikuwa Mjumbe Wake, na akatamka:

"Nashahadia kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu; nanashahadia kwamba Muhammad ni mja na Mjumbe Wake."

Muhammad, mjumbe mpya wa Mwenyezi Mungu, alimpata mfuasi wake wa kwanza wa Uislamu Khadija - mkewe. Alikuwa wa kwanza, wa kwanza kabisa kuthibitisha imani ya Tauheed (Upweke wa Mwenyezi Mungu) na alikuwa wa kwanza kabisa kukubali kwamba, Muhammad ni Mjumbe wa Mungu kwa watu wote duniani. Alikuwa Mwislamu wa kwanza.

Muhammad "aliutambulisha" Uislamu kwa Khadija. Alimweleza maana ya Uislamu, na alimwingiza kwenye Uislamu. Alimwambia kwamba utiifu na upendo kwa Mwenyezi Mungu ndio msingi wa mfumo wote wa Uislamu.

Halafu Muhammad alimuonesha Khadija jinsi ya kutawadha na kusali. Khadija alitawadha na wote wawili wakasali, Muhammad akiwa Imamu. Baada ya sala, wote walimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwapa neema ya dini ya Uislamu. Pia walimshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema za sala ambayo kwayo Aliwahudhurisha Kwake.

Khadija aligundua kwamba, Sala ndio "lango" la kuingia kwenye Baraza ya Mwenyezi Mungu ya Rehema na neema Zake, na huruma Zake.

Watumishi wanyenyekevu wa Mwenyezi Mungu wanatakiwa kupita kwenye "Lango" hili ili wafike kwenye Baraza Yake na waweze kupata Rehema na Neema na Huruma kutoka Kwake. Pia alijua kwam­ba Sala katika wakati wote ilisababisha upya na utakaso.

Khadija ni Mwislamu wa kwanza - wa kwanza kabisa kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu - baada ya mumewe. Sasa basi yeyote atakaye orod­hesha majina ya watu wa mwanzo kusilimu, jina lake litakuwa la kwan­za. Sasa haidhuru ni nani anaorodhesha orodha ya watu wa mwanzo kabisa kuingia Uislamu, Siku zote jina lake litakuwa la mwanzo.

Hapana mwanahistoria mla rushwa anayeweza kubadilisha jambo hili. Heshima ya kuwa Mwislamu wa kwanza ni ya Khadija, na itakuwa ya kwake daima Milele.

Baada ya kuingia kwenye Uislamu, Khadija alifuata imani ifuatayo:

Sema: "Kwa hakika, Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia iliyonyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliyekuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina."

Sema: "Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote. Hana mshirika. Na hayo ndiyo niliyoamrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu." (Qur'an 6:161-163)

Washington Irving

Baada ya Muhammad kukutana na Jibril kwa mara ya kwanza, alikuja kwa Khadija akiwa anatetemeka na kufadhaika. Khadija aliona kila kitu kwa jicho la imani. "Ni habari njema ulizozileta", alisema kwa mshangao, "kwa Jina Lake, ambaye roho ya Khadija ipo chini ya uwezo wake, kuanzia sasa ninakutambua wewe kama Mtume wa taifa letu." Aliendelea kusema, "Furahi, Mwenyezi Mungu hakupi usumbufu wa kuanguka kwenye fedheha Je, hukuwa wewe kipenzi cha ndugu zako, mwema kwa jirani zako, mpaji kwa masikini, mkarimu kwa mgeni, mwaminifu kwa neno lako, na wakati wote ni mtetezi wa kweli.?"

(Life of Muhammed)

A. Yusufu Ali

Katika umri wa miaka 25 Muhammad aliunganishwa katika mkataba mtakatifu wa ndoa na Khadija Mkubwa mwanamke mwenye daraja kubwa ambaye alimfanya kuwa rafiki yake wakati ambapo hakuwa na utajiri wowote, Alimwamini wakati umashuhuri wake ulikuwa hauju­likani, Alimtia moyo na alimwelewa katika bidii zake za kiroho, Alimwamini ambapo miguu yake ilikuwa inatetemeka, Aliitika wito na kupigana na upinzani, mateso, matusi, vitisho na maumivu, Na alikuwa msaidizi wake wa maisha kwa kipindi kirefu hadi kufa kwake, na kuju­muishwa na watakatifu wakati akiuwa na umri wa miaka 51. Mwanamke bora, mama wa wale waaminio.”

(Introduction to the translation and Commentary of the Holy Qur'an).

Wakati Muhammad alipoamriwa kuwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, binamu yake Ali bin Abu Talib aliyekuwa bado mdogo, alikuwa na umri wa miaka kumi, pamoja na umri wake kuwa mdogo, alionyesha uwezo mkubwa wa kushika mambo yake, na alipewa uwezo mwingi wa kuju­muika kwenye shughuli za kidini za mlezi wake.

Kwa hiyo, alitangaza kwa shauku kubwa kile alichokiamini kwamba Mungu ni Mmoja, na Muhammad alikuwa mjumbe Wake.

Na baada ya muda mfupi, alianza kusali pamoja na Muhammad na Khadija. Alitaka kwenda mbele ya Mwenyezi Mungu akiwa amefuatana na mjumbe Wake Mwenyewe.

Muhammad Mustafa alimfundisha Ali namna ya kutawadha na kusali, kuanzia hapo, Muhammad hakuonekana anasali bila ya Ali kuwepo.

Mvulana huyu pia alikariri Aya za Quran hapo hapo zilipoteremshwa kwa Muhamad. Katika hali hii, Ali alikua pamoja na Quran. Hakika, Ali na Quran "walikuwa" pamoja kama "mapacha" nyumbani kwa Muhammad Mustafa na Khadija Bibi Mkuu.

Ali aliishi kwenye mazingira ya kusisimua ya maadili ya Kiislamu.

Kwa kitendo cha unyonyaji huu (wa elimu), Uislamu ukawa sehemu ya damu ya Ali bin Abu Talib, mfuasi mdogo wa Muhammad. Uislamu ukawa umbile kabisa la utu wake.

Muhammad, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alimpata Khadija kuwa Mwislamu wa kwanza mwanamke na alimpata Mwislamu wa kwanza mwanamume - Ali bin Abi Talib.

Muhammad bin Ishaq

"Ali alikuwa mwanamume wa kwanza kumwamini Mtume wa Mungu, kusali naye na kuamini ujumbe wake wa dini, alipokuwa na umri wa miaka kumi. Mungu alimpendelea kwa kulelewa na Mtume kabla ya kutangazwa Uislamu."

(The Life of the Messenger of Allah)

Muhammad Husayn Haykal

Wakati huo Ali alikuwa kijana wa kwanza kuingia Uislamu, alifuatiwa na Zayd bin Harithah, mteja (mtumwa aliyeachwa huru) wa Muhammad. Uislamu ukakomea kwenye kuta nne za nyumba moja. Baada ya Muhammad mwenyewe, waliosilimu na kufuata hiyo imani mpya walikuwa mke wa Mtume, binamu ya Mtume na mteja wa Mtume.

(The life of Muhammed, Cairo, 1935).

Maumaduke Pickthal

Wa kwanza kabisa miongoni mwa wafuasi wa Muhammed walio silimu ni mkewe, Khadija; wa pili binamu yake Ali, ambaye alikuwa mtoto wa kupanga, wa tatu mtumishi wake Zayd bin Harith aliyekuwa mtumwa wake.

(Introduction to the Translation of Holy Qur'an. 1975).

Abdullah Yusuf Ali

Kwa binamu yake Muhammad, Ali, aliyependwa sana, alizaliwa, alipokuwa na umri wa miaka thelathini, alionekana kama mfano wa mtu bora. Alikuwa mpole na mwenye hekima na mkweli na imara. Mtu ambaye alitumia nguvu zake zote na ustadi wake wote alipotakiwa kuweka ulinzi, Aliyachukulia maisha yake kuwa kitu kisicho na thamani alipotakiwa kuunga mkono jambo kubwa lenye kuthaminiwa sana, na ujasiri wake, akili yake, kujifunza kwake na upanga wake katika kum­tumikia huyu Mjumbe mkuu wa Mwenyezi Mungu.

Khadija aliamini, akitukuka katika imani kuliko wanawake wote; Ali, aliyependwa sana, kisha alikuwa mtoto wa miaka kumi, lakini mwenye moyo kama wa simba ( kwa ujasiri ), alitoa ahadi kwa imani yake, na tangu hapo alikuwa Msaidizi Mkuu wa Uislamu.

(Introduction to the Translation and Commentary of the Holy Quran).

Shahidi wa tatu aliyeukubali Uislamu alikuwa Zayd bin Haritha, mtumwa aliyeachwa huru na Muhammad, na kuwa sehemu ya familia yake.

Tor Andre

Zayd alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kukubali Uislamu, kwa hakika alikuwa wa tatu baada ya Khadija na Ali. (Muhammed, the Man and his Faith, 1960).

Ali bin Abu Talib alikuwa mwanamume wa kwanza kukubali Uislamu, na kutangulia kwake kukubali Uislamu hakuna shaka. Dk. Maulana Muhammad Jabal, mwana falsafa wa mashairi wa India na Pakistani, anasema mtu huyu hakuwa wa kwanza, bali "Mwislamu bora wa mwan­zo kabisa."

Ali alikuwa Mwislamu wa mwanzo kabisa kwa kuzingatia wakati. Hakuna mtu aliyemtangulia katika kukubali Uislamu. Lakini pia alikuwa wa mwanzo kabisa katika kuutumikia Uislamu na Mjumbe -Mtume wake kama ambavyo miaka iliyofuata ilivyokuja kuonyesha.

Muhammad bin Ishaq, mwandishi wa maisha ya Muhammad Mustafa anataarifu ifuatavyo kwenye kitabu chake -Sira:

"Ilipokewa kutoka kwa Yahya bin Ash'ath bin Qays al-Kindi kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake Afiif: Al-Abbas bin Abdul Muttalib alikuwa rafiki yangu aliyekuwa na desturi kwenda Yemen mara kwa mara kununua manukato na kuuza wakati wa maonyesho ya biashara.

Nilipokuwa naye Mina, alikuja mtu mkubwa kwa umri na alifanya kwa ukamilifu vitendo vyote vya kutawadha na baada ya hapo alisimama na kusali. Halafu akaja mwanamke kutoka ndani naye akatawadha na akasali.

Halafu alitokea kijana aliyekuwa anakaribia kuwa mtu mzima alitawadha, akasimama karibu naye akasali. Nilimuuliza Abbas wali­chokuwa wanafanya watu hao, na alisema kwamba alikuwa mpwawe, Muhammad bin Abdullah bin Abdul Muttalib, ambaye anadai kwamba Mwenyezi Mungu amemtuma yeye kuwa Mtume; mwingine ni mtoto wa kaka yangu, Ali bin Abi Talib, ambaye amemfuata yeye kwenye dini yake; wa tatu ni Khadija ambaye ni mkewe, mtoto wa Khuwaylid ambaye pia anamfuata yeye kwenye dini yake.”

Baada ya kuwa Mwislamu na Uislamu ulikwisha jikita moyoni mwake, Afiif alisema, "Lau vile ningekuwa wa nne." Mtu wa nne kushahidilia na kuukubali Uislamu, alikuwa Abu Bakr, mfanyabiashara wa Makka.

Mwanzoni, Muhammad alihubiri Uislamu kwa siri. Aliwalingnia kwenye Uislamu watu hao tu aliowaamini na ambao walikuwa marafiki zake binafsi. Wachache katika wale waumini wapya aliowasilimisha "hawakujionyesha" hapo Makka."

(Sira-Muhammad Ishaq)

Muhammad Husayn Haykal

Wakihofia kuamsha uadui na migogoro kutoka kwa Quraysh kwa sababu ya kuacha ibada za masanamu, Waislamu wapya hawakutaka kujulikana kwamba wamesilimu.

(The life of Muhammed, Cairo, 1935).

Miongoni mwa waliosilimu mwanzoni kabisa walikuwa Yasar, mke wake, Sumayya; na mtoto wao Ammar. Wao wanajulikana sana kwa sababu familia yao yote ilikubali Uislamu kwa pamoja, hivyo, wao walikuwa familia ya kwanza ya Kiislamu iliyo nje ya ile ya Mtume wa Uislamu.

Mwingine aliyesilimu mwanzoni ni Abu Dharr el-Ghiffari wa kabila la Ghiffar, ambaye alijulikana miaka iliyofuata, kwa kupenda mno haki na kweli.

Kwa juhudi za Abu Bakr, mtu wa nne kusilimu, wakazi wengine wachache wa Makka walikubali kuwa Waislamu.

Miongoni mwao walikuwemo Uthman bin Affan, aliyekuja kuwa khalifa wa Uislamu; Talha; Zubayr; Abdur Rahman bin Auf; Sa'ad bin Abi Waqqas; na Ubaidullah Aamir bin al-Jarrah.

Abu Abdullah Arqam bin Abil Arqam alikuwa kijana wa miaka ishirini. Alikuwa wa ukoo wa Makhzum wa kabila la Quraysh, na alikuwa mfanyabiashara aliyefuzu. Aliishi kwenye nyumba kubwa yenye nafasi kwenye bonde la Safa. Yeye pia alisikia wito wa Uislamu na aliukubali, na aliweka nyumba yake - Dar-al-Arqam kwa matumizi ya Mtume wa Uislamu.

Mwanzoni Waislamu walikuwa wachache sana kwa idadi kiasi kwamba hawakuweza kusali sala zao ndani ya Al-Ka'aba au hadharani. Mtume alikubali na kumshukuru Arqam kwa kujitolea kwake, na Waislamu walikusanyika nyumbani kwake na kusali sala za jamaa. Dar-al-Arqam ikaitwa jina Dar-al-Islam taasisi ya ujumbe wa Uislamu, na ndio ilikuwa mahali pa kwanza walipokuwa wanakutana Waislamu.

Miaka mitatu ilipita katika hali hii lakini mnamo mwaka wa nne wa wito, Muhammad aliamriwa na Mwenyezi Mungu kuwaita ndugu zake kwenye Uislamu waziwazi.

"Na uwaonye jamaa zako wa karibu Quran 26:214.

Ndugu wa Muhammad walikuwa watu wote wa ukoo wa Bani Hashim na Bani al-Muttalib. Alimwamuru binamu yake, Ali, awaalike wazee wote kwenye karamu. Watu arobaini walihudhuria.

Wageni walikusanyika kwenye ukumbi wa nyumba ya Abu Talib, na baada ya kumaliza kula chakula, Muhammad, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alisimama na kusema nao. Miongoni mwa wageni waalikwa, alikuwepo Abu Lahab, ami yake Muhammad. Labda, Abu Lahab alik­wishasikia alichokuwa anafanya mpwawe kwa siri, na alihisi sababu ya wao Bani Hashim kualikwa kwenye karamu. Muhammad alipoanza tu kusema, Abu Lahab aliingilia kati kifedhuli, na yeye mwenyewe akahutubia mkutano huo:

"Ndugu, binamu na ami, msisikilize yanayosemwa na "msaliti" huyu na msiache dini ya wahenga wenu, endapo atawaita muingie kwenye dini mpya.

Kama mtakubali, basi kumbukeni kwamba mtaamsha hasira ya Waarabu wote na mtagombana nao. Hata hali ilivyo ninyi ni wachache sana. Kwa hiyo itakuwa kwa faida yenu kuendelea na dini ya jadi yenu."

Kwa hotuba yake fupi, Abu Lahabu alifaulu kuutumbukiza mkutano kwenye vurugu. Kila mtu alisimama na kurandaranda hapa na pale na kupigana vikumbo wao kwa wao. Halafu wakaanza kuondoka, na baada ya muda mfupi ukumbi ulibaki wazi.

Jaribio la kwanza la Muhammad la kusilimisha ukoo wake lilishindwa. Lakini hakustushwa na tatizo hili la mwanzo, alimwamuru binamu yake, Ali, awaalike tena wageni walewale kwenye karamu.

Baada ya siku chache, waalikwa walikwenda, na baada ya chakula cha jioni Muhammad aliwahutubia kama ifuatavyo:

"Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa huruma zake. Sifa zote anastahi­ki Mwenyezi Mungu na namwomba mwongozo wake. Namwamini Yeye, na ninaweka matumaini yangu Kwake. Yeye ni mwingi wa Neema na Mwenye kurehemu; Yeye ni Mwema na Mwenye Huruma."

Baada ya kumsifu Mwenyezi Mungu, Mtume aliendelea kusema "Nina shuhudia kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu; Yeye hana mshirika, na mimi ni mjumbe wake. Mwenyezi Mungu amenia­muru niwaite kwenye dini Yake Islam- kwa kusema: ‘Na onya ndugu zako wa karibu.’

Kwa hiyo, nawaonyeni kwamba acheni ibada za uongo, na ninawaiteni kushuhudia kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi mungu, na kwamba mimi ni mjumbe Wake. Enyi wana wa Abdul Muttalib, hakuna mtu yeyote ambaye amekuja kwenu na kitu kizuri kuzidi hiki ambacho nimewaleteeni. Kwa kuikubali (dini hii) mtakuwa na uhakika wa hali njema hapa duniani na Akhera. Ni nani basi, miongoni mwenu ambaye ataniunga mkono kufanya kazi hii kubwa mno? Nani atakaye nisaidia mzigo wa kazi hii? Nani atakaye kuwa naibu wangu, makamu wangu na waziri wangu?"

Walikuwepo wageni arobaini kwenye ukumbi. Muhammad alinyamaza ili atathmini matokeo ya maneno yake kwao. Lakini hakuna hata mmoja wao aliye jibu. Hakuna hata mtu mmoja miongoni mwa wasikilizaji aliyeonyesha kutikisika. Hatimaye, wakati kimya kilikwisha elemea mkutano, kijana Ali alisimama na kusema kwamba angemuunga mkono Mjumbe wa Mwenyezi Mungu; angegawana naye mzigo wa kazi yake; na angekuwa Naibu wake, Makamu wake na Waziri wake.

Lakini, Muhammad alimpa ishara Ali aketi chini, na alisema: "Ngoja! Labda mtu mwengine anayekuzidi umri atasimama."

Muhammad alitoa tena wito wake lakini hakuna aliyejibu, na kimya chenye kuleta mashaka kilizidi kutanda. Kwa mara nyengine Ali aliji­tolea lakini Mtume aliendelea kusubiri kwamba labda mtu mwenye umri mkubwa kuzidi wake angetokeza, alimwambia azidi kungoja. Halafu akatoa wito kwa mara ya tatu, lakini hakuna aliyeitika. Hakuna hata mtu mmoja kwenye mkutano aliye onyesha kupendelea wito wake.Alitupa macho kwenye kundi lote na kuwatazama kila mmoja kwa makini laki­ni hakuna hata mmoja aliyetikisika. Baada ya muda mrefu alimuona Ali ananyanyuka na kutangaza kujitolea kumtumikia yeye kwa mara ya tatu.

Safari hii Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikubali kujitolea kwa Ali. Alimsogeza karibu naye sana, na akauambia mku­tano. “Huyu ni Waziri wangu, Mrithi wangu, na Naibu wangu. Msikilizeni na mzitii amri zake."

Edward Gibbon

Katika kipindi cha miaka mitatu, watu kumi na wane walisilimu, matun­da ya mwanzo kabisa ya ujumbe wa Muhammad; lakini mnamo mwaka wa nne aliingia kwenye kazi yake ya kiutume, na aliamua kuionyesha familia yake nuru ya dini ya kweli, alitayarisha karamu ya watu arobai­ni wa ukoo wa Hashim. "Marafiki na ndugu."
Muhammad aliwaambia watu wa mkutano. Nawapa zawadi, na ni mimi pekee ninayeweza kuwapa zawadi hii yenye thamani kubwa sana, hazina ya hapa duniani na dunia ijayo. Mungu ameniamuru niwaite nyinyi kwenye kumtumikia Yeye. Nani miongoni mwenu atanisaidia mzigo wangu? Nani miongoni mwenu atakuwa Sahaba wangu na Naibu wangu?

Hakuna jibu lililo­tolewa, hadi hapo kimya cha kustajabisha na wasiwasi, na kebehi ilivun­jwa na ujasiri wa Ali uliokataa kuvumilia, mwenye umri wa miaka kumi na mine. “Ewe Mtume mimi hapa ni mtu huyo, yeyote atakayepigana na wewe nitamn'goa meno yake, nitayararua macho yake, nitavunja miguu yake, nitapasua tumbo lake. Ewe Mtume, mimi nitakuwa Naibu wako."

Muhammad alikubali kujitolea kwa Ali kwa msisimko wa furaha na Abu Talib kwa shingo upande alilazimika kukubali heshima kubwa ya mwanaye.

(The Decline and Fall of Roman Empire)

Washington Irving

"Enyi wana wa Abd al-Muttalib", aliita Muhammed kwa shauku, "kwenu ninyi, kwa watu wote, Mwenyezi Mungu amewapa zawadi hizi za thamani sana. Kwa jina L ake, nawapa neema za hapa duniani na furaha ya milele ya kesho Ahera.

Nani miongoni mwenu atanisaidia mzigo wa kazi yangu? Nani atakuwa ndugu yangu, Naibi wangu, Waziri wangu?" Wote walinyamaza kimya; baadhi walikuwa wanashangaa; wengine walikuwa wanatabasamu kwa mshangao na kejeli.

Baada ya muda mrefu Ali, alianza kuzungumza kwa ari ya ujana, alijitolea kumsaidia Mtume ingawaje kwa kiasi fulani alikiri kwamba yeye bado mtoto na hana nguvu za musuli. Muhammed alimkumbatia kijana huyo mwema na alimsogeza zaidi kifuani mwake. Tazama ndugu yangu, Naibu wangu, Waziri wangu", alisema kwa sauti ya juu, sik­ilizeni maneno yake, na mheshimuni yeye."

(The life of Muhammed)

Bwana Richard Burton

"Baada ya kipindi kirefu cha kutafakari, ikiwa imechochewa na ushabi­ki wa kipumbavu wa Wayahudi, ushirikina wa Wakristo wa Syria na Uarabuni, na ibada za masanamu za kuchukiza zinazofanywa na wananchi wenzake wasioamini, pia mwenye shauku. na kuna roho ipi mashuhuri ambayo haijawa na shauku? Yeye (Muhammad) alidhamiria kuyarekebisha maonevu hayo ambayo yalisababisha ujumbe uliokuwa unateremshwa kuchukiwa na watu wenye ujuzi na kutokupendelewa na wafedhuli.

Alijitambulisha kama mtu aliyetiwa moyo miongoni mwa ndugu zake na watu wa ukoo wake. Hatua hii haikufaa, isipokuwa ilim­silimisha muumini mmoja mwenye thamani ya wapiganaji elfu moja, naye ni Ali, mwana wa Abu Talib.

(The Jew the Gypsy and El-Islam, San Francisco, 1898)

Ali alijitolea kumtumikia Muhammad, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na alikubaliwa. Kwa wazee wa kabila la Qurayish, tabia ya Ali ilionekana kama ya kuharakisha mambo na kutokuwa na adabu lakini baada ya muda mfupi alithibitisha kwamba alikuwa na ujasiri wa kufanikisha mambo kinyume na vile wengine walivyofikiri. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alikubali kujitolea kwa Ali si tu kwa maneno ya kushukuru na furaha lakini pia alitangaza kwamba Ali alikuwa kuanzia muda ule Naibu na Waziri wake.

Tangazo la Muhammad lilikuwa la kweli na lisilo na shaka. Ni upumbavu kukwepa jambo la msingi kama watu wengine wafanyavyo, kwamba Unaibu wa Ali kwa Muhammad ulikomea kwenye ukoo wa Bani Hashim, kwa sababu mkutano huo ulikuwa wa Bani Hashim. Lakini Muhammad hakuweka mipaka kwa unaibu wa Ali. Ali alikuwa Naibu kwa Waislamu wote duniani na wakati wote.

Karamu ambapo Muhammad, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alim­tangaza Ali kuwa naibu wake inajulikana kihistoria kama "Karamu ya Dhul-Asheera." Jina hili linatoka ndani ya Qur'an (26:214).

Katika hali isiyo ya kawaida Sir William Muir amelitaja tukio hili la kihistoria kama "lisilothibitishwa."
Lakini nini kisichothibitika au kisi­cho cha kweli? Kuna kitu gani ambacho kingekuwa cha mantiki zaidi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kuliko kuanza kazi ya kutangaza Uislamu nyumbani kwake, na watu wa familia yake na ukoo wake, hususan, baada ya kuamriwa kwa hakika na Mwenyezi Mungu kuwaonya "ndugu zake wa karibu sana?"

Karamu ya Dhul-Asheera pale ambapo Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu, alimteua Ali bin Abi Talib kuwa Naibu wake, ni tukio la kihistoria na ukweli wake umethibitishwa na wanahistoria wa Kiarabu, baadhi yao ni hawa wafuatao:

1. Tabari, History , Juzuu ya pili uk. 217

2. Kamil bin Athir, History, Juzuu ya pili uk. 22

3. Abul Fida, History Juzuu ya pili uk. 116.

Alipoandika kuhusu Ali, wakati huu Sir, William Muir anasema: "Binamu yake Muhammad, Ali, akiwa na umri wa miaka 13 au 14, tayari alikwisha onyesha ishara za hekima na uamuzi tabia ambazo zimempatia sifa ya maisha ya akhera. Ingawa alikuwa na moyo thabiti, alikuwa hana msisimko wa nguvu ambao ungemfanya yeye kuwa mtangazaji wa Uislamu mwenye kuathiri. Tangu utoto wake alikua kati­ka imani ya Muhammad, na mahusiano yake ya mwanzoni yaliimarisha imani ya miaka ya utu uzima...”

(Life of Muhammed, London, 1877).

Tuna mashaka mengi kuhusu usemi wa Bwana William Muir kwamba Ali alikuwa hana msisimko wa nguvu ambao ungemfanya yeye kuwa na uwezo mkubwa wa kutangaza Uislamu. Ali hakupungukiwa nguvu au chochote.

Kwenye matatizo yote ya Uislamu, Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alimteua yeye kutekeleza majukumu ya hatari sana, na bila kusita aliyatekeleza.

Kama mhubiri, Ali alikuwa hana kifani. Hapakuwepo na yeyote mion­goni mwa masahaba wote wa Mtume ambaye alikuwa na uwezo wa kutangaza Uislamu kumzidi Ali. Alizitangaza Aya za mwanzo 40 za Sura Baraa (kinga), Sura ya 9 ya Qur'an, kwa wapagani wa Makka, akiwa kama mhubiri wa kwanza wa Uislamu, na kama mwakilishi wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Ali ndiye aliyeyaingiza makabila yote ya Yemen kwenye Uislamu.

Muhammad, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alimlea Ali kama mtoto wake wa kumzaa, na kama alikuwa amepungukiwa na chochote ange­jua. Alimtangaza Ali kuwa waziri wake, wasii wake na naibu wake wakati ambapo hakuna mtu ambaye angeweza kutabiri hatima ya Uislamu. Hii inaonyesha jinsi Mtume wa Uislamu alivyojiamini sana katika kipindi cha miaka 14.

Ali alikuwa alama ya matumaini na malengo ya Uislamu. Kwenye mapinduzi yaliyofanyika wakati wa karamu ya Dhul-asheera, Muhammad, Mtume wa Mungu, alikusanya nguvu na mawazo, bidii, juhudi ya vijana; Ali alikuwa nazo tabia zote hizo. Mambo mawili yali­tokea kwenye Karamu. Jambo la kwanza ni kwamba Mtume aliudhi­hirisha Uislamu hadharani; halikuwa jambo la kuficha; Uislamu "uliji­tokeza."

Kwenye Karamu ya ndugu zake. Muhammed "alivuka Rubicon - (kivuko ambacho haingewezekana kurudi nyuma tena)". Wakati ulikwishafika kwake yeye kuufikisha Uislamu nje ya ukoo wake kwanza kwa Quraysh wa Makka, halafu kwa Waarabu wote na mwisho, duniani pote. Jambo lingine ni kwamba alimpata Ali ambaye alikuwa ngome ya ujasiri, kujitolea na thabiti, na alikuwa na thamani kubwa kuzidi "wapiganaji" elfu moja ."

Imeelezwa kwamba baada ya siku kad­haa baada ya karamu ya pili ya Dhul-Asheera, Muhammad Mustafa ali­panda kwenye kilima cha Safa karibu na Kaaba, na aliita: "Enyi wana wa Fihr; Enyi wana wa Loi, Enyi wana wa Adi, na Quraysh wengine wote. Njooni huku na mnisikilize. Nina jambo muhimu sana la kuwaambia."
Wakazi wengi wa Makka waliposikia sauti yake, walikwenda kumsik­iliza. Aliwaambia; "Je, mngeniamini kama ningekuambieni kwamba jeshi la adui limejificha nyuma ya milima hiyo, na lilikuwa linawataza­ma ili lije kuwashambulia haraka sana kama mkilala au mkijisahua?" Walisema wangemwamini yeye kwa sababu walikuwa hawajamsikia akisema uongo.

Muhammad alisema: "Kama ni hivyo, hasi sikilizeni kwa makini. Mola wa mbingu na dunia ameniamuru kuwaonya ninyi kuhusu kipindi kibaya kijacho. Lakini kama mkizingatia, hamtaangamia…" Abu Lahab ambaye alikuwepo aliingilia kati kwa mara ya pili na kusema: "Kifo kiwe juu yako. Umepoteza muda wetu kutuambia hili tu? Hatutaki kukusikiliza. Usituite tena."

Tangu hapo Abu Lahab aliifanya ni desturi kumghasi Mtume popote alipokwenda. Kama alianza kusoma Qur'an au kusema jambo fulani, Abu Lahab alimkatiza au alimbabaisha. Chuki ya Abu Lahab kwa Muhammad na Uislamu pia ilifanywa na mkewe (Abu Lahab) Umm Jameel. Wote wawili walilaaniwa na Mwenyezi Mungu, kwa ukaidi wao, kwenye Sura ya 111 ya Kitabu Chake.

Sura Ya Saba: Wapagani Waliwatesa Waislamu

Ingawa Abu Lahab mara kwa mara alifaulu kuwasambaza watu waliokusanyika kusikiliza ujumbe wa Uislamu, taarifa hiyo ilienea Makka. Watu walizungumza habari za ujumbe wa Uislamu. Wenye mawazo mazuri miongoni mwao waliuliza: "Hii ni dini gani ambayo Muhammad anatuita tuingie?" Swali hili lilionyesha udadisi na baadhi yao walitaka kujua zaidi kuhusu Uislamu.

Katika siku zilizofuata, Muhammad, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alijaribu mara nyingi kuhubiri kwa wakazi wa Makka. Abu Lahab na mwenzake Abu Jahl, walifanya kila walivyoweza kuhujumu kazi yake lakini hawakuweza kumpoteza kutoka kwenye lengo lake.

Huu ulikuwa ujumbe mpya ambao Muhammad aliuleta kwa Waarabu, na ulikuwa wa pekee. Hakuna mtu yeyote ambaye alipata kusikia mfano wake kabla ya hapo.

Kama Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Muhammad aliwaambia wasiabudu vitu visivyo kuwa na uhai ambavyo wao wenyewe walivichonga, na ambavyo havikuwa na uwezo wa kuwapa wao kitu chochote au kuwaondolea kitu chochote, na ambavyo wao walivipa hadhi ya miungu wa kiume na wa kike. Aliwaambia badala yake waelekeze mapenzi na utii wao kwa Mwenyezi Mungu, Mola Aliye Pekee wa ulimwengu wote. Pia aliwaambia kwamba mbele ya Yeye-Muumba - wote walikuwa sawa, na kama wote wangekubali kuwa Waislamu, wote wangekuwa ndugu wa kila mmoja wao. Lakini ibada ya masanamu ilikuwa ni "tamaa kuu" ya zamani kwa Waarabu na hawakuwa tayari kuyatupa masanamu yao. Hawakupenda karipio la Muhammad dhidi ya masanamu, na walimwonyesha hasira zao waziwazi.

Pia Muhammad aliwaambia Waarabu matajiri kugawana utajiri wao na mafukara na wasiojiweza. Alisema, masikini walikuwa na haki ya kugawiwa mafungu wanayostahiki kutoka kwa matajiri. Aliendelea kusema kwamba mgao huo, ungekuwa dhamana ya kila mtu kupata mgao sawa katika jamii.

Waarabu wengi wa Makka walikuwa wakopeshaji wa pesa. Walitajirika kwa sababu ya kukopesha masikini kwa kuwatoza riba ya juu sana.

Masikini hawakuweza kulipa madeni yao kwa hiyo walikuwa watumwa wa kudumu wa kiuchumi. wakopeshaji hawa walineemeka kwa riba kama wanyonya damu wanavyoneemeka kwa damu. Kugawana utajiri uliopatikana kwa njia haramu na watu hao hao waliowanyonya, kwao ilikuwa "kufuru." Kwa kuwashauri kwamba wagawane utajiri wao na masikini, Muhammad amewachokoza maadui.

Pia Muhammad alitaka kuiweka jamii ya Kiarabu kwenye mpangilio mwingine. Imani mpya ambayo aliifundisha kwa madhumuni hayo, ili­fanya Imani badala ya damu, kuwa "kiungo muhimu" kwa jamii. Lakini Waarabu walilelewa kwenye desturi na mila za kipagani; waliamini kati­ka misingi ya kikabila na mpangilio wa undugu. Kwao "Damu" uny­onyaji ulikuwa ndio njia pekee inayofaa kuwa msingi wa kupangilia jamii. Kwa utambuzi wao, kama Imani iliruhusiwa kushika nafasi ya Damu katika mfanano huu, ingeharibu mpangilio mzima wa jamii yote ya Kiarabu.

Lakini Muhammad alikuwa hapendelei sana katika mfumo wa "jamii ya Kiarabu". Lengo lake ilikuwa kuanzisha na kuimarisha "jamii ya Kiislamu", ambayo kiungo chake ni Imani si Damu. Kwa hiyo, kwa uan­galifu aliendeleza na kupanga ukombozi, uwezo wa miujiza ya Imani.

Philip K. Hitti

Kwa kuifanya dini iwe ndiyo mbadala kwa muunganisho wa damu wa karne nyingi, kama msingi wa mshikamano wa jamii, kwa kweli ulikuwa ni ujasiri wa ukamilishaji wa kwanza wa Mtume nchini Arabuni.

(Islam, A way of Life).

Kwa Waarabu, mawazo haya yote yalikuwa mapya na yasiyojulikana; hakika yalikuwa ya kimapinduzi. Kwa kuhubiri fikira za kimapinduzi kama hizi, Muhammad aliikasirisha serikali ya zamani. waliokasirika sana, na imara sana katika serikali hiyo ya zamani, ni ukoo wa Banu Umayya wa Quraysh. Wajumbe wake (wa serikali hiyo) walikuwa wanaongoza katika ualaji riba na Mabepari wakubwa wa Makka, na hao walikuwa makuhani wakuu wa mahekalu ya kipagani.

Walimwona Muhammad na ujumbe wa Uislamu kama tishio kwa mfumo wao wa kijamii ambao uliendeshwa katika misingi ya upendeleo, kitabaka na mabavu. Kwa hiyo, fikira zake zilichukiwa sana na wao, na waliamua kumzuia asibadili hali kama hiyo.

"Quraysh hususani ukoo wake wa Umayya, ambao ndio waliokuwa waangalizi wa Kaaba na kisima cha Zamzam, wamiliki wa misafara ya biashara na mabwana wa serikali ya wachache ya jiji la Makka, walikuwa na sababu maalum kumkabili Muhammad.

Mahubiri mapya labda yangeharibu hija kwenye Al- Kaaba, ambayo ilikuwa chanzo chao cha mapato baada ya biashara. Aidha, (Muhammad) aliyewahi kuwa yatima anaanzisha itikadi hizi hatari za kiuchumi kama haki ya madai ya ombaomba na fukara kwenye mgao wa utajiri wa matajiri.

Kwa nyongeza, Muhammad alitetea itikadi ya hatari, ambayo itakuwa mbadala wa imani kwa damu kama mfungamano wa kijamii wa uhai wa jumuiya. Kama 'Kwa hakika waumini wote ni ndugu” ...' (Q. 49:10) ilikuwa inaathiri juu yao, familia yote, ukoo, na umoja wa kika­bila ungedharauliwa na mahala pake kuwekwa umoja wa kidini..."

(Islam - A Way of Life).

"Uadui wa Banu Umayya kwa Muhammad na Uislamu ilionyeshwa kwa ukali usio na simile, kwa upande mwingine, kwa sababu ni kitu kili­choibuka, ambacho hakikuzoewa na vizazi vingi vilivyopita. mabadiliko hayo hayakutokea kwa vizazi vingi.

Fikira zao ziliishia kwenye vizazi vya upagani. walionyesha upinzani mkubwa kwa Muhammad alipokuwa Makka, na walianzisha vita isiyo suluhishika dhidi ya Uislamu alipohamia Madina." "...kiini cha upinzani, Banu Umayya, waliendelea kuwa wakaidi kwa Muhammad..."

(Islam, A Way of Life).

Lakini pia walikuwepo watu wachache ambao waliona mvuto imara kwenye mawazo mapya ambayo Muhammad alikuwa anauanzisha, kwa pamoja unaoitwa Uislamu. Kwa hakika waliyaona mawazo haya kuwa ya kuvutia sana, hivyo wakayaamini. Waliacha masanamu yao na walianza kumwabudu Mwenyezi Mungu - Muumba.

Uislamu ulishikilia mwito maalum kwa ajili ya tabaka za chini mjini Makka; kwa ajili ya wale waliokuwa "masikini na dhaifu." Watu wa tabaka hizi walipoanza kuingia kwenye Uislamu, pia walitambua kwamba walipokuwa Wapagani walidharauliwa na kukataliwa na taba­ka za juu za Makka, lakini Uislamu uliwapa heshima mpya. Kwenye Uislamu waliona fahari mpya nafsini mwao.

Watu wengi waliosilimu mwanzoni walikuwa "masikini na wanyonge." Lakini walikuwepo pia Waislamu wachache ambao walikuwa matajiri kama Hudhayfa bin Utba na Arqam bin Abil-Arqam. Na watu wote wale ambao Abu Bakr aliwaleta kwenye Uislamu, kama vile Uthman, Talha, Zubayr Abdur Rahman bin Auf, Sa'ad bin Abi Waqqas na Abu Ubaidah Aamir bin al-Jarrah, pia walikuwa matajiri. Walikuwa katika koo mbalimbali za Quraysh.

Tunaweza kufikiria kwamba, mwanzoni, wapagani makabaila wa Makka walishuhudia juhudi za Uislamu ulivyokuwa unatambuliwa, kwa shangwe zaidi na si kwa maudhi, bila kutaja chuki na jazba iliyowaingia baada ya muda mfupi. Lakini; jinsi harakati ilivyozidi kupataa kasi, walihisi kwamba fikira ambazo Muhammad alikuwa anazitangaza kwa hakika zilikuwa za "hatari" na kwamba sio mchezo. Walihoji kwamba babu zao waliabudu masanamu, vizazi na vizazi, kwa hiyo ibada ya masanamu ilikuwa sahihi, na walikataa kuiacha kwa sababu Muhammad aliishutumu.

Lakini Muhammad hakutosheka na kushutu­mu tu ibada yao hiyo, bali jambo la hatari na kuogofya kwa ukoo wa Umayya, ilikuwa zile fikira zake za kiuchumi na haki sawa kwa jamii ambazo ndizo zilizotishia kuvunja ngome ya wao kujipendelea; na kuvunjika kwa mfumo wao wa utendaji dhambi wa ukiritimba, kubo­moa muundo wa zamani wa mamlaka na utawala msonge; na kuvunjil­ia mbali taasisi zote za zamani. Kwa hiyo, waliweka wazi kwamba fursa ya upendeleo ni kitu ambacho kamwe hawatakiacha - iwe vyovyote iwavyo.

Lakini wazo moja ambalo mamwinyi waliojitawalisha wenyewe wa kabila la Quraysh waliloliona la kuchukiza mno ilikuwa ni ile "dhana" iliyoendelezwa na Muhammad; kwamba watu wanaokandamizwa, kud­harauliwa, walikuwa sawa nao -usawa wa hali ya juu na ukubwa wa Maquraysh! Na lilo la kuchukiza zaidi kwao ni wazo la kwamba, mtumwa anapokubali Usilamu, kwa hakika anakuwa bora zaidi kuliko wakuu wote na mamwinyi wa Quraysh. Kawaida ya maisha yao ilikuwa ni kiburi na fahari; na usawa na watumwa wao wenyewe, waliokuwa watumwa na wateja, ni jambo ambalo halifikiriki kwao. Walijazwa na wenda wazimu wa utukufu wao wenyewe na "ubora" kuliko wanadamu wote. Usawa na udugu wa watu, kwao ilikuwa fikira ngeni na ya kuchukiza kwao.

Kwa kutangaza itikadi ya usawa; imani yenye kufuatwa tofauti na wingi wa watu - usawa wa mtumwa na bwana wake, masikini na tajiri, na Waarabu na wasio Waarabu na kukataa madai ya ubora wa undugu wa damu. Muhammad ametenda uhaini dhidi ya Maquraysh!

Maquraysh waliabudu masanamu mengi sana na utaifa ilikuwa mojawapo.

Lakini, ufahari wa kitaifa haukubaliwi na Quran Tukufu ambayo inatamka kwamba mwanadamu alitokana na Adamu na Adamu alikuwa konzi mmoja tu ya vumbi. Ibilisi (Shetani) amekuwa mlaaniwa kwa usahihi kwa sababu alihoji kuhusu ukuu wa kuumbwa kwake kinyume na alivyo fikiri kwamba chanzo cha kuumbwa Adamu ni cha daraja la chini. Alisema: "Mtu aliumbwa kutokana na udongo ambapo mimi nil­iumbwa kutokana na moto." Tabia hiyo yakibaguzi ambayo pia ime­wakumba binadamu kwa sababu ya utashi wa kudai ubora wa damu, umekataliwa na Uislamu.

"Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo. Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika."

قَالَ أَنَا خَيْرٌ مِنْهُ ۖ خَلَقْتَنِي مِنْ نَارٍ وَخَلَقْتَهُ مِنْ طِينٍ {76}

قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ {77}

وَإِنَّ عَلَيْكَ لَعْنَتِي إِلَىٰ يَوْمِ الدِّينِ {78}

"Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo.” (Qur'an 38:76-78).

Uislamu umeivunja hoja ya umuhimu wa rangi ya ngozi, utaifa na upen­deleo, na unawakataza Waislamu kuwagawa watu kwenye makundi katika misingi ya damu, na au ujirani wa kijiografia au upendeleo fulani ambao wanaweza kudai. Quran imemsifu mtu ambaye ni Muttaqi ­yaani mja anayempenda na kumtii sana Mwenyezi Mungu. Katika Uislamu, mtihani pekee wa ubora wa mtu, ni mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu. Mitego mingine yote ya maisha ya mtu binafsi haina maana yoyote.

"Enyi watu! Hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye Mcha Mungu zaidi katika ninyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari." (Qur'an 49:13).

Lakini kama ilivyoonyeshwa hapo juu, Maquraysh wa Makka hawakuwa katika hali ya kuzipokea fikira kama hizo. Labda hawakuwa na uwezo wa kiakili kuweza kuzielewa. Walizifikiria kama maneno ya kukufuru. Ndipo walipoamua kumpinga Muhammad, Mtume wa Uislamu (S.a.w.w.) na kuangamiza "uasi" ulioitwa Uislamu, kabla ya kuimarika na kuwa na nguvu.

Uamuzi wao haukueleweka vizuri kwa ukaidi, tamaa ya mali, wazimu wa kujiona wanaonewa kila wakati, na utambuzi wa upofu. Walisukumwa na majivuno yao - fahari ambayo yenyewe hushinikiza nje ya mipaka ya vipimo vya ubinadamu na kwa kupenda kwao sana mali kuweza kufikia uamuzi wa namna hiyo dhidi ya Muhammad na Uislamu.

Baada ya kufanya uamuzi huu, Maquraysh walitangaza nia yao ya kupi­gana kwa lengo la kutetea masanamu na miungu ya uongo, mpangilio wao wa kiuchumi na kijamii ambao ulikuwa unawahikikishia hali ya wao kuendelea kupendelewa.

Makka ilikuwa katika hali ya vita!

Maquraysh walianza kampeni dhidi ya Uislamu kwa kuwanyanyasa na kuwatesa Waislamu. Mwanzoni mateso dhidi ya Waislamu yalikuwa matusi, kuzomewa na dhihaka, lakini baada ya kupita muda, Maquraysh waliacha kuwatesa Waislamu kwa maneno - walianza mateso ya viten­do. Walidhani kwamba kutumia nguvu wangeangamiza au angalau wangeidhoofisha imani ya Waislamu.

Hawakutaka kumjeruhi Muhammad binafsi kwa kuogopa kisasi cha Waislamu lakini hawakuwa na vipingamizi katika kudhuru safu ya Waislamu. Kwa kipindi kirefu, walikuwa ni Waislamu ambao walichoshwa na nguvu kuu ya chuki kubwa na hasira kubwa ya Maquraysh.

Muhammad bin Ishaq

"Halafu Maquraysh waliwachochea watu wawatese Masahaba wa Mtume ambao walisilimu. Kila kabila liliwapiga Waislamu na kuwashawishi warudi kwenye upagani.

Mungu alimpa ulinzi Mtume Wake kwa kumtumia (Abu Talib), ambaye baada ya kuona vurugu za Maquraysh aliwaita Bani Hashim na Bani Al-Muttalib kusaidiana naye katika kumlinda Mtume. Walikubali isipokuwa Abu Lahab."

(Life of the Messenger of God).

Miongoni mwa waathirika wa mateso walikuwa:

• Bilal, Muethiopia (Mhabeshi) aliyekuwa mtumwa wa Umayya bin Khalaf. Mtu huyu aliteswa hadharani na Bwana wake akiwa na waabudu masanamu wenzake, walimtesa kuzidi kiwango cha kuvu­miliwa na binadamu. Lakini alitiwa nguvu na imani na hakutetere­ka. Kwa sababu ya kumpenda Mwenyezi Mungu na mjumbe Wake, Bilal alivumilia maumivu ya mateso kwa matumaini. Abu Bakr alimnunua Bilal na akamwacha huru. Wakati Mtume wa Mungu na wafuasi wake walipohamia Madina, alimteua Bilal kuwa muadhini wa kwanza katika Uislamu. Sauti yake nzito na nyenye nguvu ilivu­ma kwenye anga ya Madina iliyosema: Allahu-Akbar (Mungu Mkubwa). Baada ya ushindi wa rasi (ya Arabuni) kukamilika, Mtume alimteua Bilal kama katibu wake wa hazina.

• Khabab bin el-Arat Alikuwa kijana wa miaka 20 aliposilimu. Alikuwa mmoja wapo wa ukoo wa Bani Zuhra. Maquraysh wal­imtesa mara nyingi hadi alipoamua kuhamia Madina pamoja na Mtume wa Uislamu.

• Suhaib bin Sinan. Suhaib alikuja Makka kama mtumwa. Aliposilimu, Bwana wake alimpiga sana lakini hakuivunja imani yake.

• Abu Fukaiha, aliyekuwa mtumwa wa Safwan bin Umayya. Alisilimu pamoja na Bilal. Kama alivyo fanyiwa Bilal yeye pia alifungwa kamba miguuni mwake na kuvutwa kwenye mchanga wenye joto. Abu Bakr alimnunua na kumpa uhuru. Alihamia Madina lakini ali­fariki dunia kabla ya vita ya Badr.

• Lubina alikuwa mtumwa mwanamke wa Bani Mumil bin Habib. Amin Dawidar anaandika katika kitabu chake: "Pictures from the life of the Prophet" (Cairo, 1968,) kwamba Umar bin Khattab, aliyekuja kuwa Khalifa wa Waislamu, alimtesa, kila alipopumzika, alisema: "Nimeacha kukupiga si kwa sababu ya kukuhurumia, isipokuwa ninapumzika." Alipotosheka kupumzika aliendelea kumpiga tena. Abu Bakr alimnunua na alimuacha huru.

• Zunayra alikuwa mtumwa mwingine wa kike. Alipotangaza kwam­ba amesilimu, Umar bin al-Khattab na Abu Jahl walimtesa kwa zamu. Waliendelea kumtesa hadi akawa kipofu.

Amin Dawidar anasema kwamba miaka michache baadae alianza kuona tena, na Maquraysh walilihusisha tukio hili na "uchawi" wa Muhammad. Abu Bakr alimnunua na alimuacha huru.

• Nahdiyya na Umm Unays walikuwa watumwa wengine wa kike ambao waliteswa na mabwana zao kwa sababu ya kusilimu. Yasemekana Abu Bakr aliwanunua na kuwaacha huru.

Muhammad Husayn Haykal

Abu Bakr aliwanunua watumwa na wateja wengi ambao walikuwa wanateswa na makafiri. Miongoni mwao, Abu Bakr alimnunua mtumwa mwanamke kutoka kwa Umar bin Khattab kabla hata haja sil­imu. Mwanamke mmoja aliteswa hadi kufa kwa sababu ya usilimu.

(The Life of Muhammed, Cairo 1935)

Walikuwepo Waislamu wengine ambao ingawa hawakuwa watumwa lakini walikuwa "masikini na wanyonge" na kwa hiyo, walikutana na mateso ya Maquraysh waovu. Mmojawapo alikuwa Abdallah bin Masud. Alikuwa mashuhuri miongoni mwa Masahaba wa Mtume. kwa sababu alikuwa na ujuzi wa mambo mengi. Inawezekana alikuwa na uzoefu mkubwa wa maadili ya Kiislamu na sheria za Kiislamu kuliko sahaba wengine wengi.

Abdullah bin Masud alikuwa miongoni mwa watu waliohifadhi Quran katika Uislamu. Kila ilipoteremshwa Aya, yeye aliihifadhi na kuten­geneza nakala yake ya Qur'an. Nakala hii ilichukuliwa kwa nguvu na kuchomwa na Uthmani bin Affan, khalifa wa tatu, wakati wa utawala wake.

Inasemekana kwamba ilipoteremshwa Sura ya 55 (Sura ya Rahman), Mtume wa Mungu aliwauliza sahaba wake kama nani miongoni mwao ambaye angekwenda Ka'aba na awasomee makafiri. Masahaba wengine waliduwaa lakini Abdullah bin Masud alijitolea. Alikwenda ndani ya Al­Ka'aba na akaisoma sura hiyo mpya kwa sauti.

Akifuatiwa na Muhammad Mustafa, Abdullah bin Masud, alikuwa mtu wa kwanza kusoma Quran ndani ya Al-Ka'aba mbele ya kundi la waabudu masana­mu waliokuwa wamechukia. Walimuumiza mara kadhaa lakini hawakuweza kumnyamazisha kwa kutumia vitisho.

Muhammad bin Ishaq.

Yahya bin Urwa bin al-Zubayr aliniambia kuwa na yeye alihadithiwa na baba yake kwamba mtu wa kwanza kusoma Quran kwa sauti kubwa Makka baada ya Mtume alikuwa Abdullah bin Masood.

(The Life of Messenger of God)

"M. Shibli mwanahistoria kutoka India, anasema kwenye kitabu chake "Seera" kwamba Abu Bakr alikuwa sawa na wakuu wengine wa Maquraysh kwa hadhi na utajiri, lakini hakuweza kusoma Quran kwa sauti ndani ya Al-Ka'aba.

Miongoni mwa Masahaba wa mwanzo kabisa wa Muhammad Mustafa alikuwa Abu Dharr al-Ghiffari. Alitokea kwenye kabila la Ghiffar ­ambalo lilijitafutia riziki yake kwa unyang'anyi. Alisikia kutoka kwa wasafiri kwamba ametokeza Mtume Makka ambaye alihubiri imani mpya iitwayo Uislamu na aliwashawishi watu kuacha kuabudu masana­mu na kuanza kumcha Mungu Mmoja tu, kuwapa chakula wenye njaa, kutowakashfu wanawake, na kuacha kuwazika watoto wao wa kike wakiwa hai.

Abu Dharr alikwisha tengwa na waabudu masanamu hata kabla hajasikia ujumbe wa Uislamu na kazi ya Muhammad. Kwa haki­ka aliishi kama mtu anayejinyima anasa, na hakushiriki kwenye vitendo vya uvamizi wa misafara ya biashara na ya mahujaji vilivyofanywa na watu wa kabila lake. Aliishi kama mchunga kondoo.

Abu Dharr alimtuma kaka yake kwenda Makka ili athibitishe taarifa ali­zozisikia kuhusu Muhammad. Kaka yake alikwenda Makka, akakutana na Muhammad akazungumza naye na akamuuliza maswali mengi, alim­sikiliza anasoma Qur'an, alirudi kwao na kumtaarifu Abu Dharr yale aliyoyaona na kusikia. Alimwambia Abu Dharr: "Tayari unafanya mambo mengi ambayo Muhammad anafanya kwa vitendo na kuhubiri."

Kama vile nondo anavyovutiwa na mwanga wa taa ndivyo Abu Dharr alivyo vutiwa na nuru ya Imani iliyokuwa inawaka Makka. Alipata shauku ya kumuona Mtume kwa macho yake na kuisikia Qur'an iki­somwa naye aliamua kwenda Makka.

Abu Dharr alikuwa mgeni. Kaka yake alikwisha mwambia kwamba Makka ilijaa chuki dhidi ya Mtume mpya. Kwa hiyo, bila kujua nani rafiki ya Mtume na nani adui ya Mtume, hakutaka kumuuliza mtu yey­ote kuhusu yeye. Kwa muda wa siku nzima alikaa kwenye kivuli cha Ka'aba akiwatazama wapita njia.

Wakati wa jioni, Ali Abi Talib alipita sehemu hiyo, aligundua kwamba alikuwa mgeni hapo, alimkaribisha aende naye nyumbani kwake wale chakula cha jioni. Abu Dharr alikubali mwaliko huo na baadaye alimfahamisha Ali madhumuni yake ya kutembelea Makka, kwamba alikuwa na nia ya kumuona Mtume wa Uislamu. Kama iliyvo kawaida yake, Ali alifurahi sana kumpeleka rafi­ki mpya kwa Bwana wake, Muhammad Mustafa.

Abu Dharr alisalimiana na Mtume. Baada ya muda mfupi, Abu Dharr alikubali kwamba mtu huyo alikuwa mjumbe wa kweli wa Mungu. Alisikia ujumbe wa Mungu, Qur'an, kutoka kwa mjumbe wa Mungu na alifundishwa maana ya Uislamu. Aliona kwamba, mjumbe na ujumbe ni vitu visivyopingika. Alipendezwa sana na mvuto wa Uislamu. Hakika, alishangaa, angeishije bila Uislamu. Alisahau maisha yake ya zamani aliyoishi bila Uislamu.

Baada ya kusilimu, jambo la kwanza alilofanya Abu Dharr, alionyesha ujasiri waziwazi dhidi ya makafiri wa Makka. Aliingia ndani ya Al­Ka'aba na kusema kwa sauti kubwa: "Hapana Mungu ila Mwenyezi Mungu, na Muhammad ni Mjumbe wake."

Kama ilivyotazamiwa, makafiri hawakukawia kumwandama, walianza kumpiga. Abbas bin Abdul Muttalib ami yake Mtume, ndiye aliyem­nusuru Abu Dharr kwenye ghasia hii. Aliwaambia Maquraysh kwamba Abu Dharr ni wa ukoo wa Ghiffar ambao makazi yao yapo sambamba na njia ya misafara upande wa kaskazini na kama wangemuumiza, watu wa kabila lake wangefunga njia inayokatiza nchini mwao kwenda Syria.

Abu Dharr el-Ghiffari ni mtu anaye sifika sana katika historia ya Uislamu. Alionesha waziwazi kuchukizwa kwake kwa Maquraysh na kiburi chao cha madaraka. sio tu Makka walipokuwa wanaabudu masanamu, lakini pia hata kule Madina baada ya kuukubali Uislamu, lakini walirejesha tena mfumo wa ubepari wa kabla ya Uislamu. Alikuwa mzungumzaji sana asiye na woga miongoni mwa Masahaba wote wa Muhammad Mustafa ambaye aliwahi kusema: "Wingu halita­mfunika mtu yeyote atakaye kuwa mkweli zaidi ya Abu Dharr."

Abu Dharr alikuwa kama nguvu ya asili iliyokuwa inatafuta lengo kati­ka maisha na ililipata ndani ya Uislamu. Alikuwa sauti ya Dhamira ya Uislamu.

Hofu ya ghasia za Maquraysh hazikuzuia hizi roho jasiri na adilifu kuukubali Uislamu, na kila moja iliacha alama za kujitolea kwake mhanga.

Vilevile mwingine aliyejulikana sana miongoni mwa Waislamu wa mwanzo alikuwa Mas'ab bin Umayr, binamu ya baba yake Muhammad Mustafa. Miaka mingi baadaye katika Kiapo cha kwanza cha Aqaba, raia wa Madina walimwomba Mtume kuwapelekea mwalimu wa Qur'an na uteuzi ulimwangukia yeye. Hii ilimfanya yeye kuwa ofisa wa kwan­za katika Uislamu. Pia alikuwa mbeba bendera wa jeshi la Uislamu kwenye vita ya Uhud lakini aliuawa katika mapigano.

Kama mtu wa familia ya kipagani alisilimu, alitengwa moja kwa moja, bila matumaini ya kurejesha uhusiano tena. Wakazi wengi wa Makka waliuona Uislamu kama "jambo linalowagawa watu" ambalo lilikuwa linavunja familia zao, na baadhi miongoni mwao walifikiria kuikome­sha hali hiyo ya "kugawika" isiendelee kuenea. Lakini, zaidi ya tishio la kutumia nguvu kwa lengo la kuusambaratisha Uislamu, hawakuweza kufikiria njia nyingine ambayo ingefaa zaidi kuzuia usiendelee.

Pia walifikiri kwamba kama hawakuchukua hatua zozote haraka na zilizo thabiti, dalili zilikuwa zinaonyesha kwamba kila nyumba huko Makka ingegeuka kuwa uwanja wa vita ambapo viongozi wa imani za zamani na mpya wangeingia kwenye umwagaji wa damu kwa kushambuliana wao kwa wao. Wapo watu wengine walidhani kwamba Muhammad ali­chochewa na tamaa ya kukanusha na kushutumu ibada za wahenga wao na masanamu yao.

Wote kwa pamoja walijaribu kutafakari na kupata jibu kwa kutumia njia isiyo ya kawaida. Baada ya mazungumzo marefu, waliamua kumtuma Utba, mmoja wapo wa wakuu wa Maquraysh, kumuona Muhammad, kujaribu kumsihi aache mpango wa ujumbe wake. Utba alikuwa anajulikana kwa uwezo wake wa kushawishi.

Utba alikwenda kwa Muhammad Mustafa na kumwambia: "Ewe Muhammad! usilete mfarakano na kutokuelewana miongoni mwa Waarabu, na usilaani miungu ya kiume na kike ambayo wahenga wetu wamekuwa wanaiabudu kwa karne nyingi na tunaiabudu leo hii. Kama lengo lako kufanya hivyo unataka kuwa kiongozi wa kisiasa, tupo tayari kukutambua wewe kuwa mtawala wa Makka. Ukitaka utajiri, wewe sema tu na tutakupa kila kitu tuwezacho. Na endapo unataka kuoa mke mzuri sana kutoka kwenye familia mashuhuri, wewe sema, sisi tutafanya mpango."

Utba alimaliza hotuba yake kwa matumaini kwamba angepata jibu la kupendeza. Alistaajabu alipoona Muhammad haonyeshi dalili ya kutaka ukubwa au utajrii au uzuri wa mwanamke. Badala yake alimsomea Sura Sajda (Sura 32 ya Quran) ambayo katika siku hizo hizo ndio ilikuwa imeteremshwa kutoka mbinguni.

Muhammad kamwe hakuruhusu makubaliano yenye msingi wa kud­hoofisha mamlaka yake ya kiroho.

Utba alisikia, hakusema kitu, na alirudi kwa Maquraysh na kutoa taari­fa kuhusu kazi aliyotumwa. Aliwashauri Maquraysh wamwache Muhammad aendelee na mambo yake bila kubughudhiwa. Pia inase­mekana kwamba aliwaambia Maquraysh kwamba kama Muhammad akishindwa kwenye ujumbe wake, wao hawatapata hasara, lakini kama angefaulu, wangegawana utukufu na mamlaka na yeye.

Lakini Maquraysh hawakukubali ushauri wa Utba kwa kujizuia na kupunguza makali dhidi ya Muhammad na wafuasi wake.

Maquraysh waliendelea kumnyanyasa Mtume na kuwatesa Waislamu. Lakini pia waliendelea kujaribu kubuni vigingi vipya katika kampeni dhidi ya Uislamu ambavyo vingeweza kuleta matokeo mazuri zaidi kuliko yaliyofanywa na vurugu zao hadi hapo.

Muhammad Mustafa alipewa ulinzi na ami yake na mlezi wake, Abu Talib. Wapagani hawakuweza, kumuonea mpwa wa Abu Talib wakati wa uhai wake. Baadhi yao walileta fikira mpya kwamba labda wange­lazimika kujaribu kumshawishi Abu Talib mwenyewe aache kumpa ulinzi Muhammad kwa jina la umoja wa kikabila. Umoja wa kikabila ni msingi wa kuendeleza maisha jangwani. Wazo hili lilionekana zuri sana na liliwapendeza viongozi wote wa kikabila. Kwa vyovyote vile, umoja wa kikabila ulikuwa jambo la muhimu sana hivyo kwamba haungestahili kufanyiwa masihara hata na Abu Talib, bila kujali mapen­zi ya mpwa wake.

Maquraysh waliamua kutuma ujumbe kwa Abu Talib. Waliteuwa watu wa ujumbe huo kwa uangalifu sana na walimuona na wakamwomba kwa ajili ya kudumisha umoja wa kikabila asitishe ulinzi wake kwa Muhammad ambaye alikuwa "anauharibu" umoja huo.

Hata hivyo, Abu Talib hakuwa na nia ya kusitisha ulinzi wake au kuacha kumuunga mkono Muhammad.

Lakini aliwaridhisha wajumbe wa Maquraysh kwa maelezo ya uchaji Mungu na kutuliza na akawaambia warudi.

Wajumbe hao pia walitambua kwamba walirudi nyumbani kutoka kwenye kazi ya "kufukuza zimwi" kazi ngumu isiyo tekelezeka. Lakini hawakushtushwa na kushindwa kwao na baada ya muda kidogo, wali­fanya jaribio lingine lakumlaghai Abi Talib amkimbie Muhammad. Ujumbe mwingine tofauti na ule wa kwanza ulikwenda kumuona na safari hii walimpelekea kijana wa kiume mwenye sura nzuri jina lake Ammara bin Waleed, ambaye walimpa Abi Talib awe mtoto wake wa kufikia kama angekubali kumsalimisha Muhammad kwao.

Abi Talib aliwacheka makafiri kwa ujinga wao. Hivi waliamini kabisa kwamba angewapa mtoto wake wamuue, na angemlea mtoto wao kama mwanae? Wazo hili lilikuwa la kipuuzi sana lakini kwa mara nyingine Abu Talib alitumia busara kubwa kulitatua tatizo hili kwa kutumia werevu wake, wakaondoka kwenda zao.

Jaribio la pili la viongozi wa Quraysh kumshawishi Abu Talib aachane na Muhammad halikufaulu. Maana ya kushindwa jaribio lao la pili ilipo­tua akilini mwao, walihoji kwamba njia zote za amani zimeshindikana, na sasa kwa kweli lazima wajaribu kuchukua hatua kali.

Katika hali ya ghadhabu na kukata tamaa, Maquraysh wenye madaraka ya kutengeneza sera, waliamua kuchukua "hatua kali" na waliutuma ujumbe wa tatu na wa mwisho kumuona Abu Talib. Lengo la ujumbe ilikuwa kumlazimisha awaruhusu wamchukue Muhammad. Viongozi wa ujumbe huo walimkabidhi Abi Talib sharti la mwisho; ama awaruhusu wamchukue Muhammad au mambo yange mgeukia yeye mwenyewe.

Abu Talib alikuwa na tabia ya uchangamfu na siku hiyo jua liliwaka lakini ilikuwa majonzi kwake. Maquraysh wale aliokuwa anawajua, hawakuwa na masihara, kwa hiyo alimuita Muhammad, akamwelezea kuhusu azma ya Maquraysh na kuongezea: "Lo! Maisha ya ami yako! Usinibebeshe mzigo ambao utanishinda kuubeba."

Muhammad alijibu: "Ewe ami yangu! kama Maquraysh watanipa jua nilibebe kwa mkono wangu wa kulia na mwezi mkono wa kushoto, sitaacha kutangaza Upweke wa Mungu.

Katika kutekeleza kazi hii, ama nitafaulu na Uislamu utaenea, au, kama nikishindwa, nitaangamia nikiwa ninajaribu kuifanya kazi hiyo."

Abu Talib hakuwa na nia ya kumwambia mpwawe aache kuhubiri Uislasmu. Alikuwa anajaribu kuona uamuzi wake ulikuwa thabiti kiasi gani. Baada ya kusikia jibu la Muhammad alikubali na kutosheka kwamba mpwawe hangetetereka, akamwambia: "Mwanangu nenda, na ufanye uonavyo sawa. Hakuna mtu atakayethubutu kukuumiza wewe."

Sir William Muir

“Lakini fikira ya kukimbiwa na mlinzi wake mwema (Abu Talib) ilimuelemea Muhammad. Alilia sana na alirudi na kuondoka. Halafu Abu Talib alimuita kwa sauti kubwa: 'Mtoto wa kaka yangu! Rudi! Alirudi. Na Abu Talib akasema:

"Ondoka nenda kwa amani, mpwa wangu, na useme chochote kinachokupendeza. Kwa Jina la Mola wangu, kwa vyovyote vile, sitakutoa kwamwe kwa watu hao."

(The Life of Muhammed, London, 1877).

Muhammad Husayn Haykal

Abu Talib akasema: 'Nenda haraka mpwa wangu, na sema lolote unaloweza kwa Jina la Mungu yule yule ninaapa sitakusaliti wewe kwa maadui zako.'

"Abu Talib aliwasilisha uamuzi kwa Bani Hashim na Bani al-Muttalib na alizungumza nao kuhusu mpwawe kwa kumsifu sana na kupendeze­wa sana kuhusu utukufu wa daraja la Muhammad. Aliwaomba wote wamlinde Muhammad asishambuliwe na Maquraysh.

Wote walikubali isipokuwa Abu Lahab ambaye alitangaza waziwazi uadui wake kwa Muhammad na akajitoa na kuingia kwenye kambi ya upinzani.

"Maquraysh waliwafanyia Masahaba Muhammad kila aina ya maumivu ambayo aliokolewa tu kwayo kwa ulinzi wa Abu Talib, Banu Hashim na Bani al-Muttalib."

(The Life of Muhammed, Cairo, 1935).

Abu Talib alijitahidi kuwazuia mara nyingi Maquraysh wasiwatese sahaba wa Muhammad, uvumilivu wa wapagani ulifika mwisho. Ukali wao ulijilimbikiza kwa miaka mingi. Baada ya jaribio lao la tatu kushindwa, walianza kukata tamaa na wasiojali, na wakaanza kuwa fed­huli na tishio kwa Waislamu.

Waliamua kuwaangushia Waislamu ambao hawakuwa na ulinzi hasira zao zote, na kuiangamiza imani mpya kwa vitisho na ukatili. Ilionekana kama vile Maquraysh walipagawa!

Wahanga wa kwanza kutokana na msuguano na uvamizi wa wapagani walikuwa Waislamu wote ambao hawakuwa na uhusiano wowote na makabila ya Makka. Yasar na mkewe, Sumayya na mtoto wao wa kiume, Ammar hawakuwa na uhusiano wa kikabila kwa hiyo, walikuwa "wageni" hapo Makka, na hapakuwa na mtu wa kuwalinda. Wote watatu waliteswa na Abu Jahl akisaidiwa na wapagani wengine.

Sumayya, mke wa Yasar alikufa alipokuwa anateswa. Kwa hiyo mke wa Yasar akawa shahidi wa kwanza wa Uislamu. Baada ya muda si mrefu, mumewe, Yasar naye aliuawa wakati anateswa, naye akawa shahidi wa pili wa Uislamu.

Katika hali hii mke na mume walifanya uchaguzi wa mgongano usioisha baina ya nuru na giza, wema na uovu, ukweli na uongo, haki na batili na Uislamu na upagani. Uchaguzi huo ulikuwa mgumu lakini hawakuwa na jinsi nyingine kuhusu jambo hilo, na kwa furaha walitoa maisha yao kwa ajili hiyo! Waliyafanya maisha yao kuwa kafara kwa Uislamu.

Maquraysh walichafua mikono yao kwa damu isiyokuwa na hatia!

Katika orodha tukufu ya mashahidi, Sumayya na mumewe, Yasar wana daraja miongoni mwa walio juu. Waliuawa si kwa sababu nyingine isipokuwa kwa kujitolea kwa Mwenyezi Mungu na kuupenda Uislamu na Muhammad Mustafa. Waislamu wale waliouawa kwenye vita vya Badr na Uhud walikuwa na jeshi la kuwalinda na kuwakinga mkono wao. Lakini, Sumayya na mumewe Yasar, hawakuwa na ulinzi wowote.

Hawakuwa na silaha, na walikuwa Mashahidi ambao hawakuwa na ulinzi kabisa, katika historia ya Uislamu. Kwa kujitoa mhanga, wali­sisitizia ukweli wa Uislamu na waliimarisha muundo wake.

Kujitolea kwao muhanga ilikuwa ni ushindi wa imani dhidi ya mali. Marafiki na maadui zao walishangaa kuwaona hawajali kifo. Kujitolea na kuwa muhanga wa Uislamu ilifanywa kuwa desturi na kitengo cha muhimu katika maadili ya Uislamu.

"Wapo watu miongoni mwa walioamini waliotimiza ahadi walioahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha mal­iza umri wao, (wamekwisha kufa), na baadhi yao wnangoja (siku yao kufika), wala hawakubadilisha (ahadi yao) hata kidogo.”(Qur’an 33:23)

Maelezo ya Mutarjumi

"Katika kupigana kwa kweli, wengi walijitoa mhanga na wanaendelea kufanya hivyo kwa kutumia mali zao, ujuzi wao, maongezi yao, uhai wa maisha katika njia ya Mwenyezi Mungu na hawakutetereka wakati huo hadi sasa. Kama walishinda taji la kujitolea muhanga walineemeka." (A. Yusuf Ali)

Mapema kabisa, Sumayya, Yasar na Ammar walipata ushindi wa heshi­ma ya kuwa Familia ya kwanza ya Kiislamu. Sasa wamepata ushindi wa heshima nyingine. Sumayya na Yasar walikuwa Mashahidi wawili wa kwanza wa Uislamu. Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ambaye alifahamu vipi na kwa nini walikuwa wanateswa, ali­waliwaza; aliwashauri wawe na subira ya muumini wa kweli, na ali­waambia kwamba Mwenyezi Mungu alikwisha wajengea Ikulu huko Peponi. Mtoto wao Ammar taji la ushahidi lilikuwa linamngojea ingawa itakuwa hapo baadaye.

Kama familia ya Yasar walikuwa Familia ya kwanza ya kiislamu, vile viles walikuwa Familia ya kwanza ya Mashahidi. Kila mmoja wa famil­ia hii iliyo barikiwa alikufa kwa ajili ya kuthibitisha misingi ya haki na kweli iliyomo kwenye Uislamu. Mungu alifurahishwa kwa kuwapa hes­hima mbili kuu, ubora katika imani na ubora katika ushahidi.

Kama ilivyoonyeshwa kwenye kurasa za nyuma, Bilal, Khatab bin el-Arat, Suhaib Rumi na Waislamu wengine masikini na ambao hawakuwa na ulinzi, walilazimishwa kusimama kwenye mchanga wenye joto kali na walichapwa viboko na wapagani.

Walinyimwa chakula na maji kwa matumaini yasiyokuwa na matokeo ya kuwafurahisha wao kwamba njaa na kiu ingewalazimisha wao kutengana na Muhammad na Uislamu. Katika kuwatesa Waislamu, wapagani walikuwa na msimamo, nia ya kuendeleza mpango huo na kuvumbua njia za kuendeleza mpango huo.

Kama Maquraysh walimkuta Muhammad yuko peke yake, walipata fursa ya kumsumbua. Kwa vyovyote vile walitamani lakini ilibidi waizuie tamaa hiyo. Kama wangemuua, wangekuwa wameanzisha kulipizana visasi au hata kuanzisha vita vya kikabila.

Mnamo mchana wa siku moja Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alikwenda kwenye Al-Ka'aba kusoma Qur'an. Wakati anaendelea kusoma Qur'an ghafla alijikuta amezuungukwa na waabudu masanamu.

Walimfanyia ghasia, na inawezekana wange­muumiza vibaya lakini aliingilia kati Harith bin Abi Hala mpwa na mtoto wa kufikia wa Khadija, ambaye alibahatika kufika hapo. Harith aliingia kwenye vurumai hiyo na akafanikiwa kumpa ulinzi Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ambaye alinusurika kutoka kwenye vurugu za waabudu masanamu na wapagani wa Makka.

Harith bin Abi Hala aliwapiga ngumi wapagani. Inawezekana sana kwamba Harith alikuwa na upanga au jambia lakini hakutaka kuutumia kwa kuwa hakutaka damu imwagike ndani ya Al-Ka'aba. Lakini wakati tafrani hiyo inaendelea, mmojawapo wa waabudu masanamu alitoa jam­bia na kumchoma Harith mara kadhaa. Alianguka kwenye dimbwi la damu yake, na akafariki kutokana na majeraha makubwa kifuani mwake, kwenye bega na uso. Alikuwa Mwislamu wa kwanza kuuawa kwenye eneo la Al- Ka'aba.

Harith alikuwa kijana mwenye umri wa miaka kumi na saba, na aliyatoa maisha yake kwa sababu ya kuokoa maisha ya Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Kwa kufanya hivyo alijinyakulia ushin­di wa taji la Ushahidi. Alikuwa Shahidi wa Tatu. Kifo chake ambacho kilimjia mapema sana katika maisha yake, kilimsikitisha sana Mtume. Kwa Khadija, kifo cha Harith kilikuwa hasara yake binafsi. Alimlea Harith kama mwanae wa kumzaa. Lakini Khadija alisahau huzuni yake ili aweze kumliwaza mume wake katika huzuni hiyo.

Ingawa wanahistoria wa Kiarabu hawasemi lolote kuhusu jambo hili, lazima palifanyika mapigano makali sana Makka baina ya Waislamu na Wapagani kabla Mtume wa Uislamu hajahamia Madina. Abu Talib, alimlinda mpwa wake kipindi chote cha uhai wake, na baada ya kifo chake, mwanawe Ali, aliendelea kumlinda Mtume.

Alikuwa bado hajafika miaka ishirini alipojiteua mwenyewe kuwa mlinzi wa Muhammad Mustafa. Baada ya mauaji ya Harith bin Abi Hala, ndani ya Ka'aba yaliyofanywa na wapagani, Ali alianzisha mpan­go wa kufuatana na Mtume wakati wowote alipotoka ndani ya nyumba yake na popote alipokwenda na alikuwa anasimama katikati yake na maadui zake.

Kama mhuni alimwendea Muhammad kwa lengo la kumtishia, haraka Ali alimkabili mtu huyo, na alipambana naye. Akiandika kuhusu kipindi hiki cha historia ya Uislamu, mwanahistoria Muingereza, D.S. Margoliouth, anasema:

"Watu ambao kuingia kwao kwenye Uislamu kulifurahiwa sana walikuwa ni watu wenye nguvu za kimwili, na mapigano mengi hasa lazima yatakuwa yametokea huko Makka kabla ya kukimbia,; vinginevyo utayari ambao kwamba ungetolewa na Waislamu baada ya kukimbia (kutoka Makka) kutokana na idadi ya mabingwa wao wakutegemewa isingeelezeka. Mabingwa wa kutegemewa lazima wangejaribiwa mahali fulani; na hakuna mapigano ya nje yaliyotaarifi­wa au hata suala la dokezo kwa kipindi hiki."

(Muhammed and the Rise of Islam, London, 1931).

Hapakuwepo na mapigano ya nje hapo Makka kabla ya Hijira (kuhama kwa Mtume kutoka Makka kwenda Madina); lakini yalikuwepo mengi mitaani na sehemu za wazi ndani ya jiji la Makka. Vijana wahuni wa Makka walimtupia Mtume mawe au tende kavu alipokuwa katika shughuli zake, na Ali aliziumiza pua zao, alingoa meno yao na alivunja miguu yao.

Ilikuwa kwenye 'viwanja hivi vya mapigano" ambamo ndimo Ali, mpiganaji jasiri kijana alipata ustadi wa kivita. "Vita" hivi hapo Makka vilikuwa "mazoezi" ya kazi aliyotakiwa kuifanya miaka michache baadaye huko Madina kwenye mapambano ya Uislamu na upagani. Pia ilikuwa ni wakati huu wa mwanzo, kabla ya Hijira ndipo Ali alipata kuwa "msitari wa mbele wa kutetea Uislamu." Kwa hakika wakati huo huo, pia alikuwa msitari wa pili na wa mwisho wa kutetea Uislamu. Yeye alishika nafasi hizo peke yake, aliendelea hivyo hadi mwisho wa uhai wake.

Maquraysh waliitesa miili ya Waislamu ambao hawakuwa na ulinzi jiji­ni Makka kwa matumaini kwamba wangewalazimisha kuukana Uislamu lakini walishindwa. Hakuna yeyote miongoni mwa hawa Waislamu "fukara na wanyonge" aliye ukana Uislamu kamwe. Hali mbaya inaweza kukatisha tamaa hata watu madhubuti, na kwa Waislamu, hali haingekuwa na nafuu yoyote. Lakini, kwa vyovyote hali ilivyokuwa haikuweza kuwavunja moyo. Uislamu uliwaunganisha pamoja.

Kwa hawa Waislamu "fukara na wanyonge," Uislamu ulikuwa ume­wakolea kiasi cha kulewa. Uislamu uliwaunganishia maisha yao, uliwa­pa maana ya maisha; ukiwafanya watambue makusudio yao katika maisha na uliweza kuwafanya wajue upeo wa fikira zao. Kwa hiyo, walidharau usalama, starehe na raha za maisha; na baadhi yao kama Sumayya na mumewe Yasar, walidharau uhai wao; lakini walishikilia imani. Walikufa baada ya kuteswa sana na maadui wa Uislamu lakini hawakukubali uwongo.

Mwenyezi Mungu na aziridhie roho hizi jasiri na adilifu na Azineemeshe. Imani zao na mioyo yao ilikuwa, kama Maquraishi walivyogundua, haishindiki.. kama ilivyokuwa imani na moyo wa Bwana na kiongozi wao, Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Hawa walikuwa almasi ambazo zilipatikana kutoka kwenye majabali ya dunia. Kwa idadi walikuwa wachache lakini thamani yao haina kiwango, ambayo ingeweza kuelezewa si kwa uwingi ila kwa ubora tu; na ubora huo ulikuwa wa hali ya juu sana.

Sura Ya Nane: Kuhama Mara Mbili Kwa Waislamu Kwenda Abyssinia (Ethiopia) (615-616)

Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alishiriki katika huzuni zote na huzuni na maumivu ya mateso ya wafuasi wake ambao walikuwa wakiteswa kwa sababu ya kuamini Tauheed (Upweke wa Mungu) lakini hakuwa na namna ya kuwalinda. Ilipoonekana kwamba vurugu na mateso hayangepungua dhidi ya Waislamu toka kwa wapa­gani, aliwashauri waondoke Makka, wakimbilie Abyssinia nchi iliyokuwa inatawaliwa na mfalme Mkristo, aliyejulikana sana kama mtu muadilifu na mchamungu.

Baada ya ushauri huu, kundi la Waislamu; wanaume kumi na moja na wanawake wanne, waliondoka Makka na wakaenda Abyssinia. Kundi hili lilijumuisha watu kama Uthman bin Affan (Baadaye akawa Khalifa wa Waislamu) na Zubyr bin al-Awwan, binamu ya Mtume. Mtume alim­teua mmoja wa Masahaba wake wakuu, Uthmani bin Mazoon, kama kiongozi wa kundi hili.

Muhammad bin Ishaq

Mtume alipoona mateso ya Masahaba wake na kwamba ingawa yeye aliyakwepa kwa sababu ya msimamo wake kwa Mwenyezi Mungu na ulinzi wa ami wake, Abu Talib, hakuweza kuwapa ulinzi, aliwaambia: "kama mngeondoka kwenda Abyssinia (ni bora zaidi kwenu), kwa sababu mfalme (wa kule) hatavumilia uonevu, na nchi hiyo ni rafiki, hadi hapo Mwenyezi Mungu atakapo waondolea dhiki."

Bila kukawia Masahaba wake walikwenda Abyssinia, wakiogopa wasije wakamkana na kumkimbia Mungu na dini yao. Hii ilikuwa hijira ya kwanza katika Uislamu.

(The Life of the Messenger of God).

Hijra ya kwanza ilikuwa mnamo mwaka wa tano wa Wito (Kutangazwa Uislamu) yaani, 615 A.D.

Mfalme wa Abyssinia aliwakaribisha wakimbizi Waislaamu kutoka Makka kwenye himaya yake. Aliwapa hifadhi, na wakapata amani na salama, na walifurahia uhuru wa kuabudu.

Inasemekana kwamba baada ya kama mwaka mmoja, Waislamu wakim­bizi waliokuwa Abyssinia walisikia tetesi kwamba Maquraysh wa Makka waliukubali Uislamu. Kama ilikuwa hivyo, basi hapakuwepo na sababu ya wao kuendelea kuishi uhamishoni, na wakatamani sana kwenda kwao.

Kwa hiyo, walirudi Makka. Lakini walipokuwa Makka waligundua kwamba si tu kwamba taarifa za kusilimu Maquraysh zilikuwa za uongo bali waliongeza kasi ya kutesa Waislamu. Kwa hiyo, kwa mara nyingine waliondoka Makka lakini si wao tu. Safari hii Waislamu wengine wengi walikwenda nao Abyssinia. Kundi hili jipya lilikuwa na jumla ya watu themanini na tatu (wanaume) na wanawake kumi na nane, wakiwemo wakimbizi wa zamani na wapya; miongoni mwao akiwemo Abdur Rahman bin Auf, Abu Salma Makhzumi na Abdullah bin Masud.

Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alimteua Binamu yake Jaafar bin Abu Talib, kaka mkubwa wa Ali, kuwa kiongozi wa kundi hili.

Hijira ya pili ya Waislamu kwenda Abyssinia ilikuwa mnamo mwaka wa sita baada ya Wito (Kutangazwa kwa Uislamu). Yaani, 616 A.D.

Kuhama kwa Waislamu na kupokewa kwao Abyssinia, kuliwashtua Maquraysh. Walihofia kwamba Waislamu huko Abyssinia labda wangekusanya nguvu ya kupigana au wangepata washirika wapya, na halafu, wangerudi Makka na kuwakabili. Kwa hiyo, ili kuzuia tishio hili lenye nguvu, kama ambavyo waliona, waliamua kutuma ujumbe kwenye baraza la mfalme wa Abyssinia kumuomba awarudishe Waislamu Makka.

Wakimbizi wa kiislamu ambao walitegemea wangeachwa katika hali ya amani, walishangaa na kukasirika kuona ujumbe kutoka Makka unafika Abyssinia ambao uliongozwa na Amr bin Ass. Amr alimletea mfalme na watumishi wake zawadi za thamani ili ajipendekeze nazo kwao.

Mfalme alipowapa nafasi ya kuongea, kiongozi wa ujumbe wa Maquraysh alisema kwamba, Waislamu waliopo Abyssinia hawakuwa wakimbizi waliokimbia mateso lakini walikuwa watoro waliotoroka haki na sheria; na alimuomba awarudishe Makka.

Hata hivyo, mfalme, alitaka kusikiliza maelezo kutoka upande wa pili kabla ya kutoa uamuzi, na alimwita Jaafar bin Abi Talib, kiongozi wa wakimbizi, kujibu mashitaka dhidi ya Waislamu.

Jaafar alitoa utetezi usio sahaulika. Ifuatayo ni hotuba yake ikijibu maswali yaliyo ulizwa na mfalme Mkristo wa Abyssinia.
"Ewe mfalme! Tulikuwa watu wajinga na tuliishi kama hayawani wa msituni. Wenye uwezo miongoni mwetu waliwanyonya wanyonge. Hatukutii sheria yoyote na hatukutambua mamlaka yoyote isipokuwa ile yakutumia nguvu.

Tuliabudu masanamu ya mawe na miti iliyochong­wa, na hatukujua lolote kuhusu hadhi ya binadamu. Halafu Mwenyezi Mungu kwa huruma zake alituletea mjumbe wake ambaye alikuwa mmoja wetu. Tulikuwa tunafahamu kuhusu ukweli wake na hadhi yake.

Tabia yake ilikuwa mfano wa kuigwa, na alikuwa mzawa aliye bora wa Waarabu. Alitukataza kuabudu masanamu na alituita na kutuambia tumwabudu Mungu Mmoja. Alitushauri kusema kweli, na kuwapa ulinzi wanyonge, fukara, wanyenyekevu, wajane na yatima.

Alituamuru kuonyesha heshima kwa wanawake, na kamwe tusiwasengenye. Tulimtii na tulifuata mafundisho yake. Nchini mwetu, wapagani bado wapo wengi sana na walitukataza tusisilimu na kufuata imani mpya. Walianza kututesa, na ilikuwa kwa sababu ya kukwepa mateso kutoka kwao, hivyo kwamba tukatafuta na kupata hifadhi hapa kwenye himaya yako."

Jaafar alipomaliza kuhutubia, mfalme alitangaza kwamba aliridhika na ukweli wake, na aliongeza kusema kwamba Waislamu waliruhusiwa kuishi bila woga wowote. Usemi ambao ulimkasirisha sana Amr bin Al-As.

Lakini Amr bin Ass alipata fikira nyingine, ambayo alikuwa na uhakika ingemridhisha mfalme ambaye alikuwa Mkristo. Kama ingekubalika, alikuwa na uhakika kwamba ingebadilisha hali dhidi ya Waislamu, na wangerudishwa Makka.

Kwa hiyo siku iliyofuata, alirudi barazani na akamwambia mfalme kwamba lazima asitishe ulinzi kwa Waislamu kwa sababu walikana uungu wa Yesu (Isa) na walidai kwamba yeye ni binadamu kama wengine. Mfalme alipomuuliza Jaafar kuhusu jambo hili, alisema: "Uamuzi wetu kuhusu Yesu (Isa) ni kama alivyo funuliwa Mtume wetu, kwamba Yesu (Isa) ni mtumishi wa Mungu na Mtume wake, Roho Yake na Amri yake iliyotolewa kwa Mariam, bikira mtakatifu."

Mfalme alimwambia Jaafar: "Yesu (Isa) yu vilevile ambavyo umesema na hakuna zaidi ya hapo." Halafu akawageukia Waislamu na kusema: “Nendeni nyumbani kwenu na muishi kwa amani. Kamwe sitawaruhusu maadui zenu wawakamate."Alikataa kuwarudisha Waislamu Makka, alimrudishia Amr bin Al-As zawadi alizokwisha mpa na kuwaambia warudi walikotoka.

Washigton Irving

"Miongoni mwa wakimbizi waliokwenda Abyssinia, alikuwepo Jaafar, mtoto wa Abu Talib na kaka wa Ali, binamu wa Muhammed. Alikuwa mtu mwenye uwezo wa kujieleza na umbo la kupendeza sana. Alisimama mbele ya mfalme wa Abyssinia, na akamweleza imani ya Uislamu kwa hamasa na nguvu.

Mfalme ambaye alikuwa Mkristo wa dhehebu la Nestorian, aliona imani hizi zinafanana sana katika mambo mengi na kwa hiyo alikataa kabisa imani ya kuabudu masanamu iliyokuwa inakumbatiwa na Maquraysh hivyo kwamba, hadi hapo, badala ya kuwafukuza watoro, aliwakubali zaidi na kuwapa upendeleo na ulinzi maalum na akimrudishia zawadi alizokwisha mpa Amr bin Al-Ass na Abdullah na kuwafukuza hapo mahakamani."

(The Life of Muhammed).

Waislamu waliishi miaka mingi Abyssinia. Baada ya miaka kumi na tatu, walirudi Madina, si Makka - mnamo mwaka wa saba Hijiria (A.H.) (628 A.D.).- miaka saba baada ya Mtume wa Mungu kutoka Makka kwenda Madina. Kufika kwao Madina iligongana na ushindi wa Waislamu huko Khybar.

Jaafar bin Abi Talib alikuwa kiongozi wa Waislamu wote waliokwenda Abyssinia mwaka wa 615 na 616 A.D. inaonyesha kama vile alikuwa peke yake kutoka ukoo wa Bani Hashim aliyeondoka Makka kwenda Abyssinia na wakimbizi wengine. Watu wengine wote wa ukoo wa Bani Hashim walibaki Makka.

Sura Ya Tisa: Hamza Aukubali Uislamu - 615 A.D.

Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), ingawa alikuwa salama kutokana na ulinzi wa ami wake Abu Talib, si kwamba yeye hakufanyiwa fujo na makafiri. Kila walipopata fursa ya kumnasa, hawakumkosa. Ilitokea wakati fulani, Abu Jahl alimkuta akiwa peke yake na alitumia lugha ya matusi machafu kumtukana Mtume.

Jioni hiyo hiyo, ami wake, Hamza bin Abdul Muttalib alirudi nyumbani kuto­ka safari ya kuwinda, mtumwa wake wa kike alimweleza kuhusu tukio la Abu Jahl kumtukana Muhmammad, na jinsi Mtume alivyo vumilia na kwamba yeye alishuhudia hayo kwa macho yake.

Hamza alikuwa shujaa, mwindaji na mwana michezo, na hakuwa anapendelea kujua yanayo tokea mjini Makka kila siku. Lakini, tabia ya Abu Jahl kwa mpwa wake ilimkasirisha mno hivyo kwamba alichukua upinde wake na kwenda kwenye mkusanyiko wa Maquraysh ambapo Abu Jahl alikuwa anatoa maelezo kuhusu matukio ya siku hiyo kwa wenzake, alimpiga kichwani kwa upinde na kuanza kutoka damu na akasema kwa sauti ya juu sana "Mimi pia nimesilimu na kuukubali Uislamu."

Hii ilikuwa changamoto kwa Abu Jahl lakini aliona kwamba ukimya ulikuwa sehemu muhimu sana ya ushujaa, na hakugombana (hakupam­bana) na Hamza, pia akawazuia marafiki zake ambao walitaka kuamka kwa ajili ya utetezi wake.

Hamza akawa Mwislamu wa dhati na shujaa wa Uislamu. Akawa rafiki mkubwa wa mpwa wake mwengine Ali bin Abi Talib, na ilikuwa ni wao wawili walioua wapiganaji wa jeshi la Makka kwenye vita ya Badr - vita ya kwanza ya Uislamu ambayo ilipiganwa miaka michache baada ya Hamza kuwa Mwislamu.

Vita ya Uhud ilikuwa vita ya pili ya Uislamu. Kwenye vita hiyo, Hamza alimuua mbeba bendera mmoja wa jeshi la wapagani wa Makka.

Walipo shambulia safu ya Waislamu, Hamza aliingia kati yao. Alikuwa anawakatakata miongoni mwao, huku akisonga mbele ambapo Wahshi mtumwa kutoka Abyssinia alitupa mkuki na kumchoma Hamza tumboni, alianguka na kufa hapohapo. Wahshi aliajiriwa na Hinda, mke wa Abu Sufyan na mama wa Muawiya kwa lengo la kumuua Hamza.

Kwenye vita ya Uhudi Waislamu walishindwa. Baada ya ushindi wao Hind, na wakatili wengine aliokuja nao kutoka Makka, waliikatakata miili ya Waislamu waliouawa. Hind alipasua tumbo la Hamza, akachukua ini na kulitafuna. Muhammad bin Umar Waqidi, mwanahis­toria, anasema kwamba, Hind alikoka moto kwenye uwanja wa vita, na akachoma moyo na ini la Hamza akala.

Hakutosheka na hilo, alikata miguu, masikio na pua ya Hamza akavitunga kwenye kidani chake na akaingia Makka akiwa amevaa kama alama ya ushindi.

Hamza alimuua Utba, baba ya Hind, kwenye vita ya Badr. Kwenye vita ya Uhud alikuwa na hamu ya kulipiza kisasi jambo ambalo lilikuwa linamnyima raha tangu vita ya Badr.

Muhammad Mustafa, Mtume wa Mungu, alisikitishwa sana na kifo na kukatwakatwa vipande mwili wa mkereketwa wa Uislamu kama Hamza. Alimpa vyeo vya "Simba wa Mungu" na "Mkuu wa Mashahidi."

Hamza alisilimu mnamo mwaka wa tano baada ya kutangazwa kwa Uislamu. Mwenyezi Mungu na Amridhie na Amneemeshe.

Sura Ya Kumi: Umar Kusilimu Kwake Kuwa Muislamu - 616 A.D

Tukio lililokuwa kubwa mnamo mwaka wa sita baada ya Wito (Tangazo la Uislamu) ilikuwa kusilimu kwa Umar bin al-Khattab, Khalifa wa baa­daye wa Waislamu. Huyu alikuwa adui mkubwa wa Uislamu, na Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na alikuwa mte­saji mkubwa wa Waislamu. Mwanahistoria wa zama za sasa, Amin Dawidar, anasema kwenye kitabu chake.
Pictures from the Life of the Prophet, kwamba chuki ya Umar kwa Uislamu, na uadui wake kwa Muhammad Mustafa, ililinganishwa tu na chuki na uadui kwao na ule wa mjomba wake, Abu Jahl.

Inasemekana kwamba siku moja Umar aliamua, kwa ghadhabu kali, kumuua Muhammad Mustafa, na kuzima kabisa mwale wa Uislamu. Aliondoka nyumbani kwake akiwa na nia hiyo.

Kama ilivyoonyeshwa huko nyuma, Waislamu wakati huu (mwishoni mwa mwaka wa sita) bado walikuwa ndani ya nyumba ya Arqam bin Abil Arqam wakisali sala ya jamaa. Ndio kwanza walianza kukusanyi­ka wakati mmoja wao alichungulia dirishani, alimuona Umar anakuja akiwa ametoa upanga wake kwenye ala. Katika hali ya mshangao, ali­waambia wenzake alichokiona. Bila shaka, na wao pia walishtuka.

Lakini Hamza ambaye naye alikuwepo ndani humo, aliwahakikishia, na akasema kwamba kama Umar alikua anakuja kwa nia njema, basi haku­na tatizo, vinginevyo, yeye (Hamza) angemuua kwa upanga wake mwenyewe.

Lakini, ilitokea kwamba Umar alikuja kwa lengo la kusil­imu, na alifanya hivyo.

Hadithi inasimuliwa kwamba Umar alikuwa anakwenda Dar-ul-Arqam kwa lengo la kumuua Mtume ambapo mpita njia alimsimamisha, na akamtaarifu kwamba dada yake mwenyewe na mume wake walisilimu, na alimshauri ajisafishe yeye mwenyewe kwanza nyumbani mwake kabla ya kufanya jambo lolote litokanalo na dhana.

Muhammad Husayn Haykal

"Umar alikwenda Dar-ul-Arqam mwenye nia ya kumuua Muhammad na kuwapunguzia Maquraysh mzigo, kurejesha mshikamano wao ulioteketezwa, na kuanzisha tena heshima ya miungu ambayo Muhammad aliikemea vikali. Alipokuwa njiani alikutana na Nuaym bin Abdullah. Baada ya kufahamu madhumuni ya Umar, Nuaym alisema, "Kwa Jina la Mungu, umejidanganya mwenyewe, Ewe Umar! Unadhani kwamba Bani Abd Manaf watakuruhusu uwe hai mara baada ya kumuua Muhammad. Dada yako ni Mwislamu sasa. Kwa nini usirudi nyumbani kwako na kuiweka sawa?"

(The Life of Muhammed, Cairo, 1935)

"Umar alikasirika aliposikia hivyo. Haraka sana alibadili njia na kuelekea nyumbani kwa dada yake ili apeleleze kama madai hayo ni ya kweli. Katika kumjibu, dada yake alimpa jibu la moja kwa moja lakini la werevu."

Muhammad bin Ishaq

Umar alikwenda kwenye mlango (wa nyumba ya dada yake) na wakati huo huo Khabbab (sahaba wa Mtume) alikuwa anasoma Sura: Taha na pale jua litakapopinduliwa. Wapagani walikuwa na desturi ya kuyaita maandishi haya "uchafu." Umar alipoingia ndani, dada yake aling'amua kwamba alitaka kufanya madhara na walificha maandishi hayo waliyokuwa wanayasoma. Khabbab aliingia ndani haraka. Umar ali­uliza maneno gani ya kipuuzi aliyosikia wanasema? Dada yake alijibu kwamba hayo yalikuwa mazungumzo ya kawaida tu kati yao...”

(The life of the Messenger of God)

Umar alipandwa na hasira kwa kile alichodhani ni uwongo, na alimpiga dada yake usoni. Pigo hilo lilisababisha damu kutoka mdomoni mwa dada yake. Umar alitaka kumpiga tena lakini alipoona damu aliacha. Mara alionekana hana hasira, na halafu kwa sauti tofauti kabisa alim­womba dada yake amwonyeshe kile alichokuwa anasoma.

Dada yake aliona mabadiliko kwa kaka yake lakini alisema: "Wewe ni mwabudu masanamu mchafu, na siwezi kukuruhusu wewe kushika neno la Mwenyezi Mungu."

Haraka Umar alikwenda nyumbani kwake, akaoga, akarudi nyumbani kwa dada yake, akasoma maandishi ya Qur'an na halafu akaenda nyum­bani kwa Arqam ambako alishahadia Upweke wa Muumba na Utume wa Muhammad.

Sir William Muir anasema kwamba Umar alisilimu mwishoni mwa mwaka wa sita baada ya kutangazwa kwa Uislamu.

Sir William Muir

Umar alisilimu wakati wa Dhul Hijja, mwezi wa mwisho wa mwaka. Inasemekana wakati huo waumini walifikia wanaume 40 na wanawake 10, au kwa hesabu nyingine; wanaume 45 na wanawake kumi na mmoja.

(The Life of Muhammed, London, 1877)

Umar alikuwa na miaka zaidi ya thelathini aliposilimu.

Muhammad Husayn Haykal

"Wakati huo, Umar bin al-Khattab alikuwa mtu mzima mwenye umri wa miaka kati ya thelathini na thelathini na tano."

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935).

Sura Ya Kumi Na Moja: Kuzingirwa Kwa Bani Hashim - A.D. 616 - 619

Mwaka wa sita baada ya kutangazwa kwa Uislamu ulikuwa unaelekea kwisha. Wapagani wa Makka walikwisha tumia miaka mitatu kufanya kampeni dhidi ya Uislamu.

Walifaulu kusababisha machungu mengi na uadui dhidi ya Waislamu lakini hawakuwa na lolote la kuonyesha dhidi ya Waislamu, walitumia kila aina ya silaha ikiwa ni pamoja na kushaw­ishi, kupotosha, kutukana na kudhihaki.

Waliishia kutumia nguvu na kwa hakika walitumia nguvu kuzuia Uislamu au angalau kwa kiwango fulani kuudhibiti, lakini juhudi zao zote zilishindwa. Waislamu wali­himili mashambulizi yao. Nguvu ya imani ya Waislamu viliwashangaza watesaji wao.

Kushindwa huko mara kwa mara kuliwalazimisha Maquraysh, hasa zaidi ukoo wa Umayya, kutathmini upya hali ya Muhammad na Uislamu na baadhi yao walijaribu kuliona tatizo lao kwa namna nyingine. Wakati wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa tatizo la kuchukiza walianza kuele­wa pole pole kwamba, adui yao alikuwa si kundi la Waislamu ambao ni masikini sana hapo Makka.

Adui yao halisi - adui wa waabudu masana­mu na washirikina - alikuwa Abu Talib! Kwa vyovyote vile ni Abi Talib ndiye aliyekuwa anamlinda Muhammad na Uislamu kwa msimamo na ushupavu. Kwa upande mwingine, Waislamu walikuwa hawana uwezo wa kumlinda Muhammad. Hakika wao nao walikuwa wanahitaji sana ulinzi.

Uzoefu wa muda mrefu uliojaa mambo machungu kwa Quraysh, uli­wathibitishia kwamba mtu anayekwamisha vita yao dhidi ya Uislamu si mwengine isipokuwa Abu Talib.

Kwa hiyo, waliamua kwamba hawangeweza kukivunja kipingamizi kilichowakabili, kwa kuwawinda au kulitesa kundi la Waislamu wakazi wa Makka ambapo adui halisi ­Abu Talib - alikuwa huru na kuranda randa miongoni mwao, na kama vile anawakejeli.

Hatimaye Maquraysh walifaulu kumtambua adui yao halisi.

Kufaulu huku "kumtambua adui" kulikuwa na athari ya ufunuo juu ya viongozi wa Maqurysh. Na waliamua kutengeneza mkakati mpya kati­ka vita yao dhidi ya Muhammad na Uislamu.

Abdul - Al-Rahman Azzam

"Hatimaye, utawala wa Makka uliamua katika hali ya kukata tamaa kumchukulia hatua Abi Talib. Kwa mawazo yao, alikuwa mlinzi halisi wa kufuru, ingawa bado alikuwa ana heshimiwa kama mtetezi wa taa­sisi za Makka na hajawa mfuasi wa imani ya Muhammad. Walikubaliana kumpelekea kauli ya mwisho…"

(The Eternal Messege of Muhammad, London, 1964)

Siku za nyuma Quraysh walijaribu mara nyingi "kumtenga" Muhammad kutoka kwenye kabila lao, na walikuwa na matumaini kwamba wangeweza ama kumshawishi au kumdanganya Abu Talib asiendelee kumuunga mkono na kumpa ulinzi mpwa wake na Uislamu. kama wangemtenga Muhammad kutoka Bani Hashim, waliridhika kwamba, wangeweza kutatua tatizo ambalo liliwakera kwa njia rahisi ya "Kummaliza."

Lakini Abu Talib hakuwaruhusu Maquraysh "kumtenga" Muhammad. Si tu kwamba alikuwa anamlinda mpwa wake, alikwisha unganisha koo za Bani Hashim na Bani al-Muttalib na kuwa naye. Hizi koo mbili zilikuwa imara katika kumuunga mkono Muhammad, na makafiri wali­jikuta hawana uwezo dhidi yake.

Baada ya mjadala mrefu na mashauriano, Maquraysh walikubaliana kwamba kutotii na kutokukubali maafikiano kwa Bani Hashim palihita­jika kutumia hatua kali zaidi dhidi yao, na waliamua kumtenga si Muhammad tu lakini mlinzi wake, Abu Talib, pamoja na koo za Bani Hashim na Bani al-Muttalib.

Ilikuwa ni jambo lenye mantiki kudhani kwamba jaribio lolote la kuwa­chokoza Bani Hashim lingesababisha mkingamo katika mshikamano wa makundi jijini Makka.

Kila mtu Makka angetangaza ama kuwa pamoja au dhidi ya Bani Hashim. Lakini haikuchukuwa muda mrefu, ilijulikana wazi kwamba katika mapambano haya, Bani Hashim wangejikuta Arabia yote inawapinga.

Muhammad Husayn Haykal

Ni karibu ya kutowezekana kwetu sisi kufikiria nguvu na kiwango cha juhudi ambacho Maquraysh walitumia katika jitihada zao dhidi ya Muhammad au uvumilivu wake katika kipindi cha miaka ya juhudi hiyo. Maquraysh walimtishia Muhammad na ndugu zake, hususan ami zake. Walimkejeli yeye na ujumbe wake, na walimtusi yeye halikadhalika na wafuasi wake. Waliwaagiza washairi wao wamuigize kwa kubeza kwa werevu wao na waelekeze miba yao mikali dhidi ya mafundisho yake. Ilimsababishia madhara na maumivu juu yake na wafuasi wake.

Wali­jaribu kumpa rushwa ya fedha, ya ufalme na utawala, kwa hakika, kati­ka yote yale ambayo yangemtosheleza mgumu aliye mgumu kabisa wa kuridhika miongoni mwa watu. Waliwafanya kuwa masikini Waislamu kwa kuharibu biashara zao, waliwafukuza na kuwatawanya kutoka nchi­ni mwao. Walimtahadharisha Muhammad na wao kwamba vita hiyo pamoja na matokeo yake ingewapata wao. Waliishia kwanza kuwasusa kama njia ya kuwashindisha na njaa.

(The Life of Muhammed, Cairo, 1935).

Siku chache kabla ya kuanza mwaka wa saba, viongozi wa koo mbal­imbali za Maquraysh walikutana katika baraza la siri lenye umakini, kwenye ukumbi wa jiji la Makka, na waliandika na kutia saini zao kati­ka mikataba ambayo ilisema kwamba, hadi hapo ambapo ukoo wa Bani Hashim utakapomwasilisha Muhammad kwao, wangeususa ukoo huo kiuchumi na kijamii. Waliahidi kutokununua chochote au kuuza cho­chote kwa watu wa Bani Hashim na walizuia kuoana.

Makubaliano haya yalipelekwa kwa makabila mengine kwa uthibitisho, na baada ya makabila mengine kukubali, mikataba hiyo ilitundikwa kwenye ukuta wa Al-Ka'aba kwa utaratibu wa mila yao.

Uthibitisho wa makabila mengine wa makubaliano haya lilikuwa tendo la uchokozi!

Abu Talib aliitafakari hali hiyo. Aliona waziwazi kwamba mpangilio wa tatizo kubwa ulikuwa unawazunguka Bani Hashim.
Baada ya maka­bila mengine kuthibitisha makubaliano ya kuwasusa Bani Hashim, hali huko Makka ilibadilika dhahiri, hali ilikuwa ilipuke wakati wowote hivyo kwamba walijikuta kwenye dhiki kubwa mno.

Abu Talib alitam­bua kwamba ingekuwa ni hatari sana kwa ukoo wake kuishi jijini Makka ambapo wakati wowote adui angechoma moto nyumba zao. Kwa hiyo, kwa usalama wa ukoo huo, alitangaza kuondoka Makka, na kutafuta usalama wake pembezoni mwa jiji mahali penye korongo. Korongo lilikuwa na usalama wa kutosha katika hali yoyote ile. Hapo ilikuwepo salama ya Bani Hashim kuishi, kuliko kuishi kwenye nyum­ba zao ambazo zingeshambuliwa kwa urahisi.

Mnamo siku ya kwanza ya mwaka wa saba tangu Wito au Kutangazwa kwa Uislamu, koo mbili za Bani Hashim na Bani al-Muttalib, zilitoka nje ya Makka, na walianza kuishi kwenye korongo ambalo baadaye lilipewa jina - Shi'b Abu Talib. Sasa walikuwa katika hali ya kuzingir­wa! Hali hii ingeendelea kwa kipindi kirefu.

Muhammad Husayn Haykal

Mkataba ambao uliwekwa na koo za Maquraysh kwa kumsusa Muhammmad na kuwakwamisha Waislamu uliendelea kutekelezwa kwa miaka mitatu mfululizo.

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935).

Marmaduke Pickthall

Kwa kipindi cha miaka mitatu, Mtume alikuwa amezuiliwa (amefungi­wa) pamoja na ndugu zake katika ngome yao ambayo ilikuwepo katika moja ya mabonde membamba yateremkayo mpaka mjini Makka.

(Introduction to translation of Holy Quran 1975)

Maelezo kuhusu kuzingirwa kwa Bani Hashim ni hali inayotisha katika historia ya Uislamu, na imeelezewa na kila mwanahistoria kuhusu jambo hilo, miongoni mwao ni Muir na Margoliouth.

Sir William Muir

Maquraysh walisaini mkataba dhidi ya Banu Hashim - kwamba hawan­geoa wanawake wao wala hawangewaruhusu wao kuoa wanawake wao, kwamba hawangewauzia chochote wala kununua chochote kutoka kwao, na kwamba shuguli za aina yoyote na wao lazima zisitishwe.

Kikwazo hiki kiliandikwa kwa uangalifu sana na kupigwa mihuri mitatu. Wakati wote walipofungamana na mkataba huo, maandiko hayo yalining'nizwa juu ya Al-Kaaba na hivyo adhabu ya kidini kupatiwa kibali chake Banu Hashim hawakuweza kuvumilia maneno ya watu ambayo yalian­za kuenea kwa fujo dhidi yao na kuelewa kwamba labda huo ulikuwa ni mwanzo wa mashambulio halisi yaliyo kuwa yanakuja na yangekuwa makali zaidi, walikwenda kuishi mahali pembezoni mwa mji wa Makka palipoitwa Shib Abu Talib. Ilikuwa ni sehemu ya korongo, ambapo majabali ya Abu Kubeis yalichomoza nje kidogo ya Makka.

Mnamo usiku wa kwanza wa Mwezi wa kwanza wa mwaka wa saba baada ya kutangazwa ujumbe wa Muhammad, Banu Hashim, pamoja na Mtume na familia yake, walikwenda kwenye makazi ya Abu Talib, na pamoja nao pia walifuata wazawa wa Al-Muttalib, ndugu wa Hashim. Mtafaruku wa kutengwa ulisimamiwa kikamilifu. Banu Hashim wali­jikuta wamezuiwa kupata mahitaji ya nafaka na vitu vingine vya muhimu na uhaba mkubwa wa vitu uliwakumba, akiba ya Banu Hashim ilikuwa inaongezewa tu mara kwa mara kwa njia za kichinichini na hatari, hali ambayo iliwafanya wawe watu walioishiwa na mahitaji. Raia wa Makka waliweza kusikia kilio cha watoto wenye njaa huko Shi'b. Miongoni mwa ndugu wa kundi lililotengwa, walionekana wakihatar­isha maisha yao kwa kupeleka chakula kwa siri kwenye makazi ya Abu Talib ingawa walitishiwa na Maquraysh.

Hakimu, mjukuu wa Khuwayled, alikuwa na mazoea ya kupeleka chakula kwa shangazi yake Khadija, ingawa ilikuwa hatari.

(The Life of Muhammed, London, 1877)

D.S. Margoliouth

Mpango uliofahamika kwa wapagani wa Kiarabu ulikuwa kuwatenga, madhumuni ambayo yalifanya kuanzishwa kwa ushirikiano maalum. Hati za kukunja (scroll)1 ilikuwa katika matumizi ya kawaida mjini Makka.

Mapatano na mkataba makini ulifanywa, uliandikwa kwenye hati ya kukunja na kutundikwa ndani ya Kaaba, ambao ndani yake vion­gozi wa Makka waliapa kuwatenga bani Hashim na Bani Muttalib ili wasipate haki hizi hadi hapo Muhammad atakapotangazwa kuwa ni mhalifu na akakabidhiwa kwenye mamlaka husika na kulipa kisasi.

(Muhammed, and the Rise of Islam, London, 1931).

Idadi ya watu wa ukoo wa Hashim na al-Muttalib, wateja wao na watumwa wao ambao waliondoka Makka kwenda kutafuta makazi kwenye korongo walikuwa mia nne. Mara tu walipotulia kwenye makazi yao, waliangalia mandhari ya ardhi ya hapo, waliweza kuona kwamba walikabiliwa na changamoto ya hali ngumu isiyoelezeka kwa urahisi. Ambapo siku za nyuma walikuwa wanapambana na uadui wa binadamu, sasa walishindana pia na uadui wa maumbile.

Waligundua pia kwamba makazi yao mapya hayakuwa na mpangilio unaofaa kutege­meza maisha. Kwa hiyo, walifahamu tangu siku ya mwanzo kabisa kwamba wangewajibika kwa kutumia ujasiri wao, ustadi wao, ubunifu wao na uamuzi wao kukubali mazingira mapya. Walijua kwamba uhai wao ungetegemea uwezo wao wa jinsi ya kutumia makazi hayo.

Khadija alizaliwa kwenye familia ya kiungwana na alilelewa katika raha na starehe. Kwa hiyo alikuwa mgeni kabisa kwenye maisha magumu na ya upweke. Lakini ilipotokea dharura, aliambiwa aache nyumba yake yenye nafasi kubwa mjini, aende kuishi ndani ya korongo lenye hali ngumu, alifanya hivyo kwa hiyari yake mwenyewe akiwa na furaha.

Korongo lilikuwa linatia majonzi hivyo kwamba roho ya mtazamaji ilikata tamaa lakini Khadija hakuonyesha dalili ya kufadhaika alipoingia humo. Ingawa makazi mapya yalikuwa si mazuri, alijizoesha haraka sana kuishi humo. Aliangalia mateso mbele yake, akajikaza na kuvu­mila na kutumia uhodari wake. Uimara wa roho yake, kweli ulis­hangaza.

Mwanzoni mwa kuzingirwa, Ali alikuwa na umri wa miaka kumi na sita. Alikabiliwa na kazi ngumu na hatari ya kukusanya akiba ya chaku­la kwa ajili ya koo mbili. Alifanya kazi hii katika hali ya hatari kwa maisha yake; alileta maji na nafaka kutoka popote.

Kiriba kimoja cha maji walinunua kwa kipande kimoja cha dhahabu, na alijihisi anayo bahati kama alifaulu kufikisha kwenye makazi mapya. Juhudi zake, zilileta nafuu kidogo kwenye koo zilizozingirwa.

Abu Talib alikuwa halali usingizi usiku. Kwake yeye usalama binafsi wa Muhammad ulipewa kipaumbele. Muhammad alipolala, Abu Talib alimnyanyua na akamweka kwenye kitanda cha mmoja wa watoto wake wanne na akamuamuru alale kwenye kitanda cha Muhammad. Baada ya muda kidogo akamweka kwenye kitanda cha mmoja wa watoto wake. Usiku wote Abu Talib alifanya kazi ya kumyanyua Muhammad kutoka kitanda hiki na kumpeleka kitanda kingine.

Hakutaka kudanganyanyi­ka kuhusu maadui zake, alitambua kwamba walikuwa wang'ang'anizi sana, wasaliti, fisadi, wapenda kulipa kisasi. Kwa hiyo hakufanya kosa la kudhani wangeshindwa. Kama mmoja wao angetambaa chini na kuingia kwenye makazi yao kwa nia ya kumuua Muhammad, basi uwezekano mkubwa ungekuwa kwamba, angemuua mmojawapo wa watoto wake Abu Talib akidhani kwamba ni Mtume. Abu Talib na mkewe walikuwa tayari kujitolea maisha ya watoto wao kwa ajili ya kumwokoa Muhammad.
Kwa hakika wangefurahi sana kujitolea maisha yao wenyewe kwa sababu ya Muhammad kama ingekuwa lazi­ma. Si tu kwamba walimlinda Muhammad, walihakikisha kila mtu mzima kwenye makazi hayo mapya anawajibika kumlinda Mtume.

Kuna wakati ambapo Ali, pamoja na ujasiri wake, alishindwa kupata mahitaji yoyote au kama alipata chochote hakuweza kuleta hapo kwenye makazi, kwa kushindwa kuwakwepa Maquraysh. Nyakati kama hizo, watoto na wakubwa walisumbuliwa na njaa na kiu.

Lakini njaa na kiu hapo kwenye korongo ilikuwa hali ya kawaida. Wanawake walichemsha majani na magamba ya miti na kuwapa watoto wanywe ili watulize njaa. Kilio cha watoto wenye njaa kilisikika nje ya makazi hayo ya muda na Maquraysh walijibu kwa kicheko cha kejeli. Walichekelea na huku wakiwabeza kuhusu ushindi wao wa kuwafanya watoto wa Bani Hashim walie kwa sababu ya njaa na kiu. Maquraysh walidhamiria kufanya makusudi ili Banu Hashim waathirike.

Zawadi yenye thamani kubwa sana kwa koo zilizozingirwa katika kipin­di cha miaka mitatu ilikuwa maji. Watu wa koo hizi; wateja wao na watumwa, walipata maji kutoka kwa Khadija. Alimpa Ali vipande vya dhahabu ambavyo alitumia kununua maji. Kuhusika kwake kwa watu waliokuwa pale kulijionyesha kwa namna nyingi. Alimwomba Mwenyezi Mungu Awahurumie. Sala ilikuwa shughuli ya muhimu sana kwake, na ilikuwa ni lengo lake la kuhimili dhiki. Baada ya muda mfupi alitambua kwamba ilikuwa lengo rahisi na lenye umuhimu.

Sala ilimwezesha Khadija kukabiliana na changamoto zisizoepukika kila siku wakati wa kuzingirwa, na alifaulu. Alikuwa malaika kiongozi wa kabila, na kila mmoja alihisi tabia ya kupendeza ya kuwepo kwake na kuungwa mkono na uwezo wa nguvu yake ya kiroho.

"Enyi mlioamini! Jisaidieni ( katika mambo yenu) kwa subira na Sala; Bila ya shaka Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri"(Qur'an 2 : 153)

Khadija alitafuta msaada wa Mwenyezi Mungu kwa uvumilivu na sala. Aliposali, hakupata msaada tu bali, ujasiri, nguvu, amani na utulivu na kutosheka.

"(Nao) ni wale walioamini na zikatulia nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Sikilizeni! Kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu nyoyo hutulia. Wale walioamini na kufanya vitendo vizuri raha itakuwa yao, na marejeo mema." (Quran 13:28,29)

A.Yusufu Ali amefafanua "kuneemeshwa" kama ifuatavyo: "Kuneemeshwa: hali ya kutosheka katika nafsi, furaha ya ndani ambayo hujionyesha katika maisha ya mtu mzuri, bila kujali raha na taabu. Na halafu, kila mara huwa kuna lengo la mwisho ambako macho ya mhusika huelekea, Makazi mazuri ya kupumzika huko Peponi, baada ya shughuli za maisha haya (hapa duniani) kwisha. Lengo ni Mwenyezi Mungu Mwenyewe."

Katika kumkumbuka Mwenyezi Mungu, Khadija, mtumwa Wake mwenye imani kali, walipata kutoshelezwa na kuneemeshwa.

Mara kwa mara, wale marafiki wachache waliokuwa nao Bani Hashim Makka, walijaribu kupeleka chakula kwa siri kwenye makazi ya muda ya Banu Hashim, lakini wapagani waliwanyang'anya endapo wali­waona.

Mmoja wapo wa marafiki wa Banu Hashim huko Makka alikuwa Hashim bin Amr al-Amiri. Alikuwa anawapelekea chakula na maji mara nyingi kadiri alivyoweza. Alijua kwamba kupeleka mahitaji huko kwenye Makazi ni shughuli iliyotakiwa kufanywa kwa siri - tahadhari kubwa, usahihi na bila vurugu. Kwa hiyo, muda aliochagua wa kupele­ka chakula na maji kwa Waislamu waliozingirwa, ulikuwa saa chache kabla ya alfajiri.

Lakini siku moja wapagani walimkamata na wal­imtishia kumuua kama angeendelea kuwapelekea Bani Hashim mahita­ji.

Rafiki mwingine wa Banu Hashim huko Makka alikuwa Hakim bin Hizam, mpwa wa Khadija. Yeye na rafiki yake, Abul Bukhtari, walipeleka mahitaji muhimu kwa Bani Hashim.
Siku moja, wote waw­ili walikuwa wanapeleka chakula na maji na nguo kwa Banu Hashim ambapo Abu Jahl aliwashtukiza na aliwaambia kwamba alikuwa anawanyang'anya ngamia na mahitaji. Abu Bukhtari alijaribu kuele­wana naye lakini hakutaka kusikia lolote. Aliwazuia wasifike kwenye Makazi Mapya ya Waislamu. Abu Bukhtari alijaribu kumpita kwa nguvu. Walipigana ngumi. Ugomvi wa namna hii ulitokea mara kwa mara karibu na makazi lakini marafiki wa Banu Hashim wa Makka hawakukata tamaa, na walijitahidi kila wawezalo kupeleka msaada.

Hashim bin Amr al-Aamiri, na Hakim hawakuwa Waislamu lakini hawakutaka kuona mtoto au hata mtumwa yeyote wa Banu Hashim anaangamia kwa njaa au kiu na walihatarisha maisha yao mara kwa mara kwa kupeleka mahitaji huko Shib Abu Talib. Pia walifurahi kuli­pa gharama za shuguli za kuhami kama hizo kwa miaka mitatu, na wali­chotaka wao ni usalama wa koo zilizozingirwa.

Lazima ieleweke kwamba katika kipindi hiki mahsusi, chuki na hasira za ukoo wa Umayya wa Quraysh hazikuelekezwa kwa Waislamu tu, bali zilielekezwa kwa ukoo wa Banu Hashim. Lengo lao ilikuwa kuangamiza Uislamu bila kumuua Muhammad.

Walijaribu mara nyingi kumuua lakini walishindwa kwa sababu hawakuweza kumfikia. Alikuwa salama na mwenye furaha akiwa na ulinzi wa ukoo wake -Banu Hashim.

Kama ilivyo andikwa kwenye kurasa za nyuma, Banu Umayya kwa uhakika walimlenga Abu Talib mkuu wa Banu Hashim, kuwa yeye ndiye aliye sababisha kushindwa kwa vita yao ya kipumbavu dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mjumbe Wake, Muhammad. Kamwe hawakum­samehe kwa yale aliyokuwa anayafanya kwenye jitihada hiyo.

Kwa Waislamu ambao hawakuwa wa ukoo wa Banu Hashim, walikuwa wengi na wote walikuwa wanaishi mjini Makka. Baadhi yao wali­tangazwa kuwa wenye ushawishi, uwezo na tajiri, na wote walidai kwamba walikuwa wanampenda Mtume wao. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba hakuna hata mmoja miongoni mwao aliyekwen­da kumuona Mtume au hata kumpelekea msaada wowote. Walifurahia starehe na usalama wa nyumba zao kwa miaka mitatu ambapo Mtume wao, Muhammad Mustafa, aliishi, na aliowapenda, akiyumbayumba, kama ilivyokuwa, kwenye makali ya upanga, akiwa amezungukwa na maadui ambao walikuwa na kiu ya damu yake na wafuasi wake.

Inaweza ikaonekana kama vile familia ndogo ya Khadija yenye mume wake Muhammad Mustafa, mtoto wake mdogo wa kike, Fatima Zahra na mtoto wake wa kambo, Ali bin Abi Talib, waliishi katika hali ya wasi­wasi wakati wote kama watu wengine kwenye ukoo huo, bila kujua kabisa vitisho vya siku iliyofuata au usiku huo. Kila siku ilisongwa na hatari. Lakini hata kidogo hakukosekana kuwa na akiba mpya katika Imani yake na Tabia, kuiimarisha kama kitu kamili. Aligundua kwam­ba hakuna kitu kingine alichokitaka zaidi ya kujihisi yu karibu na Mwenyezi Mungu. Kwa kujihisi kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, ali­weza kuondoa wasiwasi.

Kwa Khadija, chanzo cha dukuduku kilikuwa njaa na kiu ya watoto. Pale Ali au Hakim bin Hizam au Hashim bin Amr alipokuwa akileta mahitaji kwenye Makazi, yeye (khadija) aliwaangalia. Watoto wal­imzunguka na aliwapa chakula na maji. Walimtazama kwa furaha na mshangao. Aliyapa kipaumbele mahitaji ya watoto halafu ya wazazi wao, na alishughulikia mahitaji ya wazazi wa watoto kabla ya kwake. Alikuwa na kipaji cha kupanua familia hadi kwenye kabila lote.

وَمَنْ أَرَادَ الْآخِرَةَ وَسَعَىٰ لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَٰئِكَ كَانَ سَعْيُهُمْ مَشْكُورًا {19}

"Na anayetaka akhera na akazifanyia jitihada amali zake, na hali ya kuwa ni Mwislamu, basi hao jitihada
yao (hiyo) itakuwa ni yenye kushukuriwa."( Quran 17: 19 )

Usalama wa koo zilizozingirwa hapo Makazi ya Waislamu haukutishi­wa na Banu Umayyad tu, na si tu na tishio la njaa na maji, lakini pia na joto na baridi kali. Wakati wa siku ndefu wa majira ya kipupwe, anga ilitema cheche duniani, na majabali na miamba ya korongo yalizirudisha zilikotoka, hivyo kufanyiza kitu kama tanuru. Khadija aliwapa maji wenye kiu mara kwa mara kwa kadri alivyoweza ( kujaaliwa). Wakati wa majira ya baridi, usiku mrefu ulikuwa na baridi kali sana.

Mama wenye watoto walifanya jitihada nyingi sana bila matumaini kuwalinda watoto wao wasiumizwe na baridi kali. Khadija aliwagawia nguo na kuni.

Hali hiyo ya muda mrefu ilivuruga mwenendo wote wa maisha ya watu wa ukoo wa Hashim na al-Muttalib. Kila siku ilileta mateso ya kutisha au hatari mpya kwao. Lakini hawakukata tamaa. Kwa hakika, walifu­rahi. Kuwepo kwa Muhammad, kipenzi cha Mwenyezi Mungu, mion­goni mwao ilitosha kuwafanya wasahau hofu yao na kuwapa furaha. Walitambua kwamba Mwenyezi Mungu aliwateua wao kwa kazi ya kumlinda Muhammad, Mtume Wake, kutoka kwa maadui zake. Ilikuwa ni heshima ambayo hawangetaka kubadilisha hata kwa kupewa utawala. Khadija aliwatia moyo kwa mfano wake. Utukufu na uwezo wa Imani yake uliwapa msukumo, na walipita kwenye shida nzito za miaka ya uhamishoni kwa heshima na kujiamini.

Khadija alikuwa na furaha kutoka mwanzo wa kuzingirwa hadi mwisho. Roho ya Kweli na Ukarimu ilikuwa maajabu ya utu wake. Alitambua ulinzi wa Mwenyezi Mungu kwa kabila la Banu Hashim, kwa hiyo, lilikuwa salama. Siri ya utulivu wake ipo kwenye aya za Qur'an zifuata­zo:

فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ مِنِّي هُدًى فَمَنْ تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ {38}

"Basi watakaofuata uongozi wangu huo haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika" (Quran 2 : 38)

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ {62}

"Sikilizeni! Vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na khofu (siku ya Kiyama) wala hawahuzuniki" (Quran 10: 62)

إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ{13}

"Hakika wale waliosema: ";Mola wetu ni Mwenyezi Mungu," kisha wakatengenea, hawatakuwa na khofu ( siku ya kufa kwao wala baa­daye) wala hawatahuzunika."(Quran 46: 13)

Maelezo ya Mfasiri

"Kujitolea na kufanya kazi ya Mwenyezi Mungu husababisha roho kuwa huru na huondoshewa woga na huzuni, kuhusu yaliyopita, yaliy­opo na yajayo, kama tukichukua mfano wa kulinganisha na wakati wa hali isiyo na wakati. Kujitolea huko na kufanya kazi, huonyeshwa na (1) Kuamini Dalili za Mwenyezi Mungu, ikimaanisha kuelewa na kukubali Radhi Yake na (2) kwa kushikamanisha utashi wetu moja kwa moja na Utawala Wake wa ulimwengu, maana yake: kuwa katika mlingano pamoja na hali isiyo na ukomo, na kutenda katika mambo yote ili kuen­deleza Ufalme Wake." (A. Yusuf Ali).

Kwa upande wa Khadija hapakuwepo na woga na huzuni. Alionyesha namna Ujumbe wa Mungu ulivyo ndani ya kazi zake za kila siku.

Imani ya Khadija, wema na kutoa sadaka ni mambo yaliyojulikana na kila mtu. Hakuna mtu aliyejua kiwango cha uvumilivu wa mateso na uwezo wake wa kuvumilia hadi hapo alipoanza kuishi uhamishoni. Khadija alivumilia usumbufu kwa ukakamavu, na alipambana na hali ya kukata tamaa na kufa moyo, na alishinda.

Maisha ya Khadija yalishikamanishwa na matumaini kama msokoto wa kamba. Matumaini yangetoweka kutoka kwenye mazingira aliyoishi Khadija. Lakini hali hiyo haikumhusu yeye. Matumaini yake yalikuwa hayaonekani lakini yalikuwa yanaambukiza." Yaani yaliwatia moyo watu ambao walikuwa wanakata tamaa.

"Wanashangilia neema ya fadhila za Mwenyezi Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wanaoamini" (Quran 3 : 171)

Khadija alifurahia kwenye Rehema na neema za Mungu na Ukarimu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Alibarikiwa nazo kwa wingi.

Yafuatayo ni maelezo mafupi yaliyokusanywa kutoka vyanzo mbalim­bali, kuhusu kisa cha Muhammad Mustafa na Khadija, na Banu Hashim na Bani al-Muttalib, walipokuwa wamezingirwa huko Shib Abu Talib mwaka 616-619. Mambo mengi muhimu hayakusimuliwa kikamilifu.

Lakini yapo matumaini kwamba utafiti wa wataalamu wa historia na wasomi wenye kujitolea kwa dhati utadhihirisha mambo mapya. Mambo haya mapya yatawawezesha wataalamu wa historia ya Uislamu wa siku zijazo kuandika historia iliyokamilika na kueleweka zaidi kuhusu kipindi ambapo Uislamu ulikuwa umezingirwa.

Kuzingirwa kwa Bani Hashim na Bani al-Muttalib kulidumu hadi mwaka wa A.D. 619. Mnamo mwaka huo, koo zote zilirudi jijini Makka. Kuzingirwa kwao na Quraysh hakukufanikisha lengo lililotara­jiwa.

Watu wa Banu Hashim hawakujali kabisa na ari yao ilikuwa imara. Kwa upande wao, ilikuwa ni jambo lisilofikirika, katika mwisho wa kipindi cha kuzingirwa, kama ilivyokuwa hapo mwanzoni, kumtoa Muhammad - kipenzi chao kwa maadui zake..

Kama Abu Jahl na Banu Umayya walisitisha (waliacha) mpango wa kuwazingira Banu Hashim, haikuwa kwa sababu ya badiliko la moyo lolote lile kwa upande wao; walikuwa makafiri na azma yao mbovu isiy­ojenga, ya kuangamiza Uislamu.

Walijaribu kuendeleza mzingiro huo na kuyazunguukia magofu ya Bani Hashim. Lakini walilazimika kusitisha mpango huo kwa sababu palikuwepo na nguvu nyingine inayofanya kazi dhidi yake.

Yafuatayo ni maelezo yaliyotolewa katika kitabu cha mwanzo kabisa kilichopo mpaka leo, katika wasifu wa Mtume na Muhammad bin Ishaq, kuhusu matukio ya kilele katika kurudi kwa Banu Hashim na Bani al-Muttalib kutoka Shi'b Abu Talib, baada ya miaka mitatu ya uhamishoni.

Nukuu: "Kusitishwa kwa Mpango wa Kuwasusa Bani Hashim."

Bani Hashim na Bani al-Muttalib waliishi mafichoni kwenye mlima baada ya Maquraysh kufanya mapatano ya kuwatenga wao. Halafu, baadhi ya watu ndani ya kundi la Maquraysh walichukua hatua za kuyapinga na kuyakataa mapatano yale. Miongoni mwao, hakuna aliye­jitahidi kumzidi Hisham Bin Amr katika jambo hili kwa sababu alikuwa mtoto wa kaka yake Nadla b. Hashim b. Abd Manaf upande wa kikeni, na alikuwa karibu sana na Bani Hashim. Alikuwa ana heshimiwa sana na watu wake.

Wakati koo hizi mbili zilipokuwa uhamishoni, Shi'b mara nyingi alikuwa anawapelekea mahitaji wakati wa usiku kwa kutu­mia ngamia, alipofika mwanzo wa uchochoro aliondoa hatamu na aliusukuma mzigo ambao uliporomoka hadi kwenye makazi. Mara nyengine aliwapelekea nguo kwa kutumia njia hiyohiyo.

Hisham alikwenda kumuona rafiki yake, Zuhayr bin Abu Umayya bin al-Mughira ambaye mama yake alikuwa anaitwa Atika mtoto wa Abdul Muttalib, na alisema; "Wewe unaridhika kula chakula na kuvaa nguo nzuri ambapo unajua hali walionayo wajomba zako? Hawawezi kununua au kuuza au kuoleana.

Kwa Jina la Mungu, kama wangekuwa wajomba wa Abul Hakam bin Hisham (Abul Jahl) na ukamwomba afanye kile ambacho amekuambia wewe ufanye, kamwe hangefanya."

Zuhayr alisema "Inashangaza, wewe Hisham, nifanye nini? Mimi nipo peke yangu. Kwa jina la Mungu kama ningekuwa na mtu mwengine wa kuniunga mkono, ningesitisha mgomo huu."Alisema "Nimekutafutia mtu kwa ajili yako" (mimi mwenyewe)." "Tafuta mwengine;' Zahyr alisema. Hivyo Hisham alikwenda kwa al-Mutim bin Adiy na akamwambia "Wewe unaridhika kwamba koo mbili za Bani Abd Manaf ziangamie ambapo wewe unaafiki kuwafuata Maquraysh? Baada ya muda watakufanya hivyohivyo." Mutim alitoa jibu kama la Zuhyr na akadai mtu wa nne.

Hisham alikwenda kwa Abul Bukhtari bin Hisham na akamuomba mtu wa tano na halafu kwa Zamaa bin Al-Aswad bin Al-Muttailb bin Asad, na akamkumbusha kuhusu uhusiano wao wa kindugu na kazi zao. Alimuuliza endapo wengine walikuwa tayari kushirikiana katika kazi hii, na alimpa majina ya wengine. Wote walisema wangekutana usiku karibu na Hujun nje ya Makka na walipokutana, walikubaliana kutafakari kati ya mkataba na kusitishwa kwake.
Siku iliyofuata, wahusika walipokutana pamoja, Zuhary alivaa kanzu na aliizunguuka Al-Kaaba mara saba.
Halafu akawageukia wenzake, akasema: "Enyi watu wa Makka, tutaku­la na kuvaa ambapo Banu Hashim wanaangamia, hawawezi kununua au kuuza? Kwa jina la Mungu sitapumzika hadi hapo uovu huu wa mkata­ba wa mapatano ya Maquraysh kuwasusa Banu Hashim na Bani al-Muttalib umeharibiwa."

Abu Jahl aling'aka: "Umekosea. Hautaharibiwa kamwe." Zama'a alimjibu kwa ukali: "Wewe ndiye unayekosea.

Mkataba huu wa udhalimu utaharibiwa. Hatukuutaka hata hapo ulipotayarishwa na kusainiwa."

Abul Bukhtari alisema: "Zama'a yuko sahihi. Hatukuupenda mkataba huu tangu ulipoandikwa na hatuutaki hivi sasa."

Al-Mutim aliongeza: " Wote Zamaa na Zuhayr wako sahihi, na yeyote anayesema vinginevyo, anakosea. Tuna mtaka Mwenyezi Mungu awe Shahidi wetu kwamba sisi tunajitoa kwenye jambo hili, na yale yaliy­omo ndani ya mkataba huo." Hisham pia alisema, na aliwaunga mkono marafiki zake.

Halafu Al-Mutim alikwenda kuuchukuwa ule mkataba na kuuchana vipande vipande. Alikuta mchwa ulikwisha kula sehemu kubwa isipokuwa maneno: "Kwa jina Lako Ee Mwenyezi Mungu." Huu ulikuwa utaratibu wa desturi na mila za Maquraysh za kuandika mambo yao. Mwandishi wa mkataba alikuwaa Mansur bin Ikrima.

Ifuatayo sio nukuu: Al-Mutim Bin Adiy aliupasua mkataba wa Quraysh vipande vipande. Vipande hivyo vilipeperushwa na upepo na hakuna alama iliyobaki. Kitendo hiki kilikuwa cha imani na ujasiri - imani kwamba Banu Hashim hawakuwa na hatia ila walikuwa wahanga wa dhuluma; na ujasiri kwa kuwadharau Maquraysh. Kitendo chake cha ushupavu ilikuwa dalili kwamba huo ulikuwa mwisho wa kuwasusa Banu Hashim, na kwamba wahusika walikuwa huru kurudi jijini Makka. Mutima yeye mwenyewe na vijana mashujaa wa ukoo wake waliovalia kijeshi walik­wenda kwenye korongo.

Walimsindikiza Muhammad Mustafa, Khadija na watu wote wa koo mbili za Banii Hashim na Bani Al-Muttalib, kurudi Makka, na hadi majumbani mwao.

Dr. Muhammad Hamidullah ameandika kwenye ukurasa wa 10 wa kitabu chake: Mafunzo ya Awali ya Uislamu. (Introduction to Islam) kilichochapishwa na International Islamic Federation of Student Organizations, Salimiah, Kuwait (1977).

"Baada ya miaka mitatu, watu wanne au watano wasio Waislamu, ambao walikuwa na ubinadamu zaidi kuliko wengine na waliotoka kwenye koo tofauti, walitangaza hadharani kukataa mkataba wa ususaji."

Dr. Hamidullah amehusisha kushindwa kuendelea kwa mkataba wa ususaji wa koo mbili na ubinadamu wa watu wasio Waislamu wanne au watano. Anasema watu hao walikuwa na "ubinadamu zaidi kuliko wengine." Anasema kweli. Watu hao walikuwa na ubinadamu zaidi kuliko wengine ambao hawakuwa Waislamu hapo Makka. Lakini walikuwa na ubinadamu zaidi kuliko hata Waislamu ambao walikuwa wakazi wa Makka?

Inashangaza na maajabu," jibu la kihistoria la swali hili lenye kero ni "ndio." Ni hali yenye kejeli. Hata hivyo, zaidi ya hawa watu watano ­wote wasio Waislamu - ubinadamu haukumlazimisha mkazi yeyote wa Makka asiye Mwislamu au Mwislamu - kuwadharau Maquraysh na kuwasaidia Banu Hashim!

Kuna swali moja zaidi: kwa nini Zuhayr alihisi yupo peke yake?

Hisham alipoanzisha mada ya kusitisha Mkataba wa wapagani kwa mara ya kwanza kwa rafiki yake Zuhayr, alimsuta kwa kutokufikiria matatizo yao, na alimlaumu kwa kushindwa kusitisha tatizo hilo. Zuhayr alisema: "Inashangaza wewe Hisham, nifanye nini?

Mimi nipo peke yangu. Kwa Jina la Mungu, kama ningekuwa na mtu mwengine wa kuniunga mkono, ningesitisha mgomo huu."

Jibu la Zuhayr ni fumbo. Kwa nini alijihisi hana mtu wa kumsaidia? Hakujua kwamba walikuwemo Waislamu wengi Makka? Kwa nini hakujaribu kuwashawishi ili waondoe tatizo hili? Ilikuwa muhimu kwake kuomba msaada wao. Hata kama wangekataa, hapangeharibika jambo.

Kwa mujibu wa wanahistoria, baadhi ya Waislamu wa Makka walikuwa watu wenye hadhi na mashuhuri na walikuwa na ushawishi katika jamii ya Maquraysh. Lakini kwa sababu zisizoeleweka, haikutokea kwa Zuhayr au rafiki yake yeyote kuwahamasisha Waislamu. Waliamua kuwapuuza Waislamu. Waliendelea na mpango na kuchukuwa hatua za upande mmoja kusikitisha ususiaji kwa Banu Hashim.

Zuhary na marafiki zake walifaulu katika juhudi zao za kuwarudisha Banu Hashim mjini Muhammad Mustafa, Khadija, Ali, Abu Talib na jamaa wengine wote wa Banu Hashim na Bani al-Muttailb, walirudi kwao. Lakini kwa kitendo chao, Zuhayr na marafiki zake walionyesha kwamba Waislamu wa Makka, hawakuwa watu wa lazima kwa Muhammad na Uislamu.

Ni moja ya mafumbo makubwa ya historia ya Uislamu kwamba mkono ambao ulifikia ukuta wa Al-Kaaba na kuung'oa mkataba wa Maquraysh wa kuwatenganisha Banu Hashim, na kuupasua vipande vipande, haukuwa mkono wa "Mumin" bali ulikuwa mkono wa "asiyeamini" -Mutim bin Adiy! Wala hakuna yeyote katika marafiki zake aliyekuwa Mwislamu yaani; Hisham bin Amr, Zuhayr bin Abu Umayya, Abul Bukhtari bin Hisham na Zamaa bin al-Aswad. Lakini wote watano walikuwa watu waliojaa ubinadamu ambao hawakukubali kuonewa kwa Banu Hashim.

Hawakupunzika hadi hapo haki ilipotendeka huko Makka.

Hawa watu watano wenye msimamo mkali hawakuwa Waislamu kama ilivyo onyeshwa hapo juu. Lakini wao peke yao waliokuwa na ujasiri na busara za kuunga mkono na kutetea kanuni ambazo ni za Kiislamu, yaani; kanuni ya Haki. Walitetea haki na kwa tendo lao la kijasiri wal­ifuzu kupata uzima wa milele katika nyanja za Uislamu.

Kwa upande mwengine si tu kwamba Waislamu hawakuchukuwa hatua yoyote; hata ile ya kupinga dhidi ya ubezi na ukiburi wa Maquraysh. Walidumisha kwa muda wa miaka mitatu mtengo makinifu na ukimya usioshawishika. Wote walikuwa watu wenye busara. Kwa hiyo, yote hayo waliyo yafanya ilikuwa ni kukawiza mambo na kuangalia mwelekeo wa matukio.

Bani Hashim walisuswa kwa muda wa zaidi ya siku elfu moja. Kinacho shangaza katika tukio hilo la kugomewa ni kwamba uimara wa Bani Hashim na al-Muttalib haukuonyesha ufa wowote ingawa wakati wote walikuwa kwenye mfadhaiko na wasiwasi kutoka mwanzo hadi mwisho. Quraysh hawakumpata hata msaliti mmoja kwenye koo, hata mtumwa aliyekuwa radhi kuwasaliti mabwana zake; wala hawakuona dalili yoyote ya mtu mwenye moyo mwepesi, hata kwa mtoto mdogo.

Kule Shi'b Abu Talib walikuwepo watu mia nne: wanaume, wanawake na watoto. Watu hao walikuwa wanapata uzoefu wa kuishi uhamishoni wakiwa na Muhammad na Khadija, na hakuna hata mmoja wao aliye­fanya utoro, ama kuokoa maisha yake au kutosheleza njaa na kiu au kuepuka joto na baridi kali au kuepuka kizuizi kisichokuwa na mwisho.

Hawakuwa na njia ya kujua vipi na lini, kama ingetokea mwisho wa mgomo huo, na kama ingetokea wao warudi makwao. Uhamishoni siku zilipita kuwa majuma, majuma yalipita kuwa miezi, na miezi kuwa miaka. Kulikuwa hakuna kabisa kitu cha kupoteza matumaini. Na bado matumaini ndicho kitu kilicho waendeleza hadi mwisho.

Inaonyesha kwamba uamuzi wa pamoja, lakini wa kimya kimya wa hawa mashujaa "Mia Nne" ulikuwa ni wa "kuzama au kuogelea" (yaani, kuangamia au kunusurika) pamoja na Muhammad. Waliamua kuwa wafungwa lakini wawe naye Muhammad kuliko kuwa huru lakini asi­wepo. Kwa maoni yao ni kwamba, maisha bila Muhammad hayangekuwa na thamani ya kuishi kabisa.

Abu Talib na watu wengine wa Banu Hashim na Bani al-Muttalib wali­uona mgomo kama mtihani wa kuwapima kama kweli wanampenda Muhammad. Mgomo ulikuwa pia mtihani kwa hamasa yao, ujasiri wa kimwili na ujasiri wa kimaadili, uthabiti wao, uvumilivu wao usta­hamilivu wao kwenye matatizo, na nguvu zao. Walifuzu mitihani yote.
Mwenyezi Mungu alikabidhi usalama binafsi wa Muhammad Mustafa-Mjumbe Wake, kwao. Walikuwa na msimamo wa kumlinda yeye na walileta utukufu na heshima kwenye msimamo wao.

Katika miaka mitatu ya uhamishoni, utajiri mwingi wa Khadija ulik­wisha. Sehemu kubwa ya utajiri huo ulitumika kununua maji. Alifurahi kwamba utajiri wake ulikuwa njia ambayo Mwenyezi Mungu aliokoa maisha yenye thamani sana katika Uumbaji wote - maisha ya Muhammad Mustafa na Ahlul Bayt - na alimshukuru kwa kumpa yeye heshima hii.

Katikati ya misukumo na mabadiliko yaliyomzunguka Khadija, imani ilibakia katika kiwango hichohicho na iliendelea kuwa chanzo cha nguvu isiyo shindwa kwake na wale aliokuwa nao.

Imani yake ilien­delezwa na sala kama ilivyoonyeshwa huko nyuma. Imani ya Khadija ilikuwa kitu kinachoonekana na kuguswa. Wakati wote alikuwa anawasiliana na Mwenyezi Mungu - kwa njia ya sala ambayo ndio chan­zo cha Imani. Pia sala ilikuwa ndio siri ya ujasiri wake wa kimya kimya. Tabia yake ya amani na utulivu popote alipo, haikuruhusu imani ya kabila kudhoofika wakati wote wa mgomo. Alikuwa kama nanga ya meli ya kabila lote katika miaka yote ya fujo na majonzi.

Kushindwa kwa kugomewa Banu Hashim na Bani al-Muttalib, na wapa­gani wa Makka, na kurudi kwa koo mbili majumbani mwao, ilikuwa njia panda katika historia ya Uislamu. Ilikuwa uthibitisho wa uhakika na nguvu ya imani mpya.

Mwanzoni mwa mgomo, wapagani walikuwa na uhakika kwamba wal­iumaliza Uislamu na kwamba sasa ulitegemea huruma yao. Juhudi zao za kufutilia mbali Uislamu hazikuwa nusu nusu au za hapa na pale, na hawakutaka kubahatisha. Walining'iniza tishio la njaa mbele ya koo zilizosuswa. Walidhani kwamba wakati wa mabalaa mawili kwa wakati mmoja unaoendelea, yaani njaa na kiu, na hali ya hatari inayoendelea, upinzani wa koo zilizogomewa nao, ungelazimika kumuwasilisha Muhammad kwao (wapagani).

Bila shaka, uvumilivu wa binadamu una upeo wake, njaa na kiu isiyo na mwisho ni njia rahisi ya kudhoofisha imani ya mtu, hata kama angekuwa jasiri namna gani. Lakini wapagani hawakujua kwamba imani ya Banu Hashim kwa Mwenyezi Mungu ilikuwa na nguvu zaidi kuliko woga wa njaa na kiu na kwa hakika ilikuwa na nguvu zaidi kuliko woga wa kifo.

Watu wa ukoo wa Banu Hashim hawakuwa na woga wa kifo. Wakati Muhammad Musatafa aliposimamisha Bendera ya Tauhid na kuwasha Taa ya Imani humo Arabuni, mara moja alipewa changamoto na waabuduo masanamu.

Waabudu masanamu walichukia kuona Bendera ya Tauhid inapepea hadi upeo wa macho na walipeleka vikosi vyao kwa msongamano ili waing'oe. Lakini vikosi hivyo vilikuta Bendera imezunguukwa na kulindwa na wana wa Banu Hashim. Bendera ilizunguukwa na walinzi na katika kuilinda ilibidi wadharau kifo kila sekunde! Vikosi vilifanya mashambulizi makali mara nyingi dhidi ya Bendera lakini wapiganaji hao walirudishwa nyuma. Wana wa Banu Hashim waliwashinda na kuwafukuza maadui.

Taa ya Imani iliyowashwa na Muhammad Mustafa ilitishiwa na dhoru­ba ya upagani na ushirikina. Lakini wana wa Banu Hashim walifaulu kuilinda taa hiyo. Upagani ulitumia nguvu zake zote kuizima taa hiyo na ulishindwa.

Katika kulinda Bendera ya Tauhid na Taa ya Imani wapiganaji wengi wa Banu Hashim walikufa. Lakini kama ambavyo imeandikwa kwenye kurasa za nyuma, askari wa Banu Hashim hawakuogopa kifo. Tauhid na Imani ni vitu vilivyokuwa na thamani zaidi kwao kuliko uhai wao. Walijivunia kifo wakiwa wanailinda Tauhid na Imani. Waliamini kwamba bendera na Taa vyote vilikuwa urithi wenye thamani kubwa, na ilikuwa ni kazi yao ya kuheshimiwa sana kuvilinda vitu hivyo, na wali­fanya hivyo.

Abu Jahl na Banu Umayya walifanya majaribio yasiyohesabika kuuzi­ma mwanga wa Uislamu. Lakini walishindwa. Mwanga wa Uislamu uliangaza zaidi wakati wote. Wangewezaje kuuzima ambapo ulikuwa na walinzi wanao onekana na wasio onekana. Kama Banu Hashim walikuwa walinzi wa mwanga wa Uislamu walioonekana, Mwenyezi Mungu alikuwa Mlinzi wake. Asiye onekana. Kama tunavyosoma kwenye aya zifuatazo za Qur'an 9:32,33

"Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, lakini Mwenyezi Mungu amekataa isipokuwa kuitimiza nuru yake ijapokuwa makafiri wanachukia." (Quran 9 : 32)

"Yeye ndiye aliyemleta mtume wake kwa uongofu na Dini ya haki ili ajaalie (dini hii) kushinda dini zote; ijapokuwa watachukia hao washirikina." (Quran 9:33)

  • 1. Aina ya vitabu na makaratasi ya kuandikia ya zamani

Sura Ya 12: Kifo Cha Khadija-Tul Kubra Na Abu Talib - A.D. 619.

Mashujaa watano wa Makka waliukanyaga mkataba wa Maquraysh wa kuwasusia Banu Hashim. Shukurani kwa uungwana na ushujaa wao, Bani Hashim wameweza kurudi mjini, na kuishi kwenye nyumba zao kwa mara nyingine tena. Lakini, kabla hata hawajatulia na kuanza kusa­hau ugumu wa maisha ya maficho ya milimani kwa miaka mitatu, Khadija, mke, sahaba na rafiki wa Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mfadhili wa Uislamu na Waislamu aliugua. Ugonjwa wake ulikuwa wa muda mfupi lakini wa kufisha. Maisha yake yote aliyoishi katikati ya maisha ya kujitosheleza na ya anasa, lakin miaka mitatu aliyoishi uhamishoni ulikuwa wakati wa kushikilia sana maadili kwake ambao bila kuepukika uligharimu maisha yake.

Kama ambavyo imeandikwa kwenye kurasa za nyuma, Khadija alikuwa mwanamke wa kwanza kutangaza kwamba Muumbaji ni Mmoja na kwamba Muhammad alikuwa Mjumbe Wake.

Utukufu na heshima ya kuwa Muumini wa Kwanza duniani pote, ni yake daima.

Wakati Uislamu ulipoanza kupata upinzani mkali kutoka kwa maadui zake, Khadija alijitolea kwa kusahau raha zake zote, utajiri na familia yake ili auhami Uislamu, na sasa ilionyesha kama vile alikuwa tayari kuyatoa mhanga maisha yake. Bila shaka kama angeishi kwenye nyum­ba yake ya starehe Makka, akiwa amezungukwa na watumishi wake, labda angeishi kwa miaka mingi. Lakini alipendelea kumsaidia mume wake na ukoo wake na kushiriki maisha machungu pamoja nao.

Kipindi cha kuzingira Waislamu, si tu kwamba alivumilia uchungu wa njaa na kiu, bali na joto kali la kiangazi na baridi ya majira ya kipupwe, hata hivyo hakulalamika kwa mumewe kwa hayo yote. Ima hali iwe nzuri au mbaya; mahitaji ya kutosha au hakuna kabisa kitu, wakati wote alikuwa na furaha. Hali mbaya ya maisha na ufukara kamwe havikumkatisha tamaa. Mwenendo huu ndio ulikuwa chanzo imara cha raha, ujasiri, umadhubuti wa mume wake wakati mbaya sana katika maisha yake.

Katika kipindi cha kuzingirwa Waislamu. Khadija alitumia utajiri wake wote kwa kununua mahitaji muhimu kama chakula na maji kwa ajili ya ukoo wa mumewe. Aliporudi nyumbani kwake Makka, senti yake ya mwisho ilikwishatumika na alipofariki dunia hapakuwepo hata hela ya kununua sanda. Joho la mume wake lilitumika kama sanda.

Muhammad Mustafa kamwe hakuoa mke mwingine wakati wa uhai wa Khadija, na kama asingekufa, uwezekano ni mkubwa kabisa kwamba hangeoa kabisa.

Edward Gibbon

Katika kipindi cha miaka 24 cha ndoa yao, mume wa Khadija ambaye alikuwa bado kijana aliepusha na haki ya mitala, na fahari au upendo wa mjane kamwe haukufedheheshwa na jamii ya upinzani. Baada ya kifo chake, Mtume alimweka kwenye daraja la wanawake wanne ambao ni bora zaidi, dada wa Musa, mama wa Isa (Yesu) na Fatima, binti yake aliyependwa sana.

(The Decline and Fall of the Roman Empire)

Muhammad bin Ishaq, mwandishi wa maisha ya Mtume, anasema kwamba wakati Wahyi kutoka kwa Mungu uliponza tena baada ya kuko­ma kwa muda baada ya kutembelewa mara mbili na malaika Jibril kati­ka pango la Hira, Khadija alipokea sifa na salamu za amani kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Ujumbe uliwasilishwa na malaika Jibril kupi­tia kwa Muhammad, na alipoufikisha ujumbe kwa Khadija alisema: "Mwenyezi Mungu ni Amani (as-Salaam), na Amani yote hutoka kwake na amani iwe kwa Jibril."

Muhammad alimkumbuka Khadija katika uhai wake kwa hisia za mapenzi, shukrani na upendo. Wakati Khadija anaugua, usiku kucha hakulala kwa kumuuguza, kumliwaza na kumwombea. Mumewe alimwambia kwamba Mwenyezi Mungu alimuahidi furaha kamili ya Milele na alikwisha mjengea kasri ya kifalme yenye kuta za lulu huko Peponi. Ilipokaribia asubuhi mwili wake uliodhoofika haukuweza kuhimili mauvivu ya homa na roho yake iliyotakaswa na uadilifu ilion­doka hapa duniani na kuelekea kwenye kituo chake - Mbinguni ambapo iliingia kwenye kundi la walio hai milele.

Kifo chake kilimhuzunisha Muhammad sana.

Khadija alifariki tarehe kumi mwezi wa Ramadhani mnamo mwaka wa kumi baada yakutangazwa Uislamu.

Khadija alizikwa Hujun sehemu ilioko jirani na Makka. Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, aliteremka ndani ya kaburi na kulala humo kwa dakika chake. Halafu akawasaidia waombolezaji wengine kuuteremsha mwili kaburini. Baada ya maziko alisawazisha ardhi juu ya Kaburi lake (Khadija).

Kwa hiyo, Khadija alikufa akiwa mwanamke wa kwanza kuamini Upweke wa Muumbaji.

Amani iwe kwa Khadija ambaye alipelekewa salamu za amani na Mwenyezi Mungu (s.w.t).
Amani iwe kwa Khadija ambaye alijengewa kasri ya kifalme yenye kuta za lulu huko Peponi.
Amani iwe kwa Khadija, mbora sana miongoni mwa wanawake, na mkuu wa wanawake wote.

Khadija alifariki mwaka wa 619 A.D. Mwezi mmoja baada ya kifo chake, Muhammad Mustafa alipata mshtuko mwengine wa kifo cha Abu Talib, ami yake na mlezi wake na ngao ya Uislamu. Kifo cha hawa marafiki wawili-Khadija na Abu Talib - kilikuwa mshtuko mkubwa zaidi ambao Mtume wa Mungu alitakiwa avumilie katika miaka hamsi­ni ya maisha yake. Taa mbili za maisha yake zilizimika. Alizidiwa na huzuni. Aliuita mwaka wa vifo vyao "Mwaka wa Huzuni."

Mwaka wa 619 uligeuka kuwa mwaka wa huzuni kwa Muhammad Mustafa katika maana mbili. Kifo cha mpendwa wa wastu kwa kawaida ni tukio la huzuni. Lakini kwa hali ya Muhammad, kifo cha hawa marafiki wawili haikuwa tu tukio la huzuni kwake. Haikupita muda mrefu alifanywa atambue maana ya vifo vyao, kwa mfululizo wa matukio tofauti tofauti.

Muhammad bin Ishaq.

Khadija na Abu Talib walikufa mwaka mmoja, na kwa kifo cha Khadija matatizo yalikuja kwa haraka moja baada ya lingine. Alikuwa muumini wa kutegemewa naye katika Uislamu, na alikuwa anamsimulia kuhusu matatizo yake. Pamoja na kifo cha Abu Talib alipoteza chanzo cha nguvu ya maisha, ulinzi wa kabila lake. Abu Talib alifariki miaka mitatu kabla ya Muhammad hajahamia Madina, na hapo ndipo Maquraysh walipoanza kumfanyia mambo mabaya ambayo hawangeyafanya wakati wa uhai wa ami yake. Kijana baradhuli alimtupia Mtume mchanga kichwani.

Hisham kutoka kwa baba yake, Urwa, aliniambia kwamba Mtume aliin­gia nyumbani mwake na alikuwa anasema: Maquraysh kamwe hawaku­nifanyia hivi kabla Abu Talib hajafa."

(The Life of the Messenger of Allah)

Washington Irving

Baada ya kipindi kifupi, Muhammad alitambua hasara aliyopata kutokana na kifo cha Abu Talib. ambaye hakuwa tu ndugu mwenye upendo bali mlinzi madhubuti mwenye nguvu, kutokana na ushawishi wake mkubwa kule Makka.

Baada ya kifo cha Abu Talib hapakuwepo mtu ambaye angezuia uchokozi wa Abu Sufian na Abu Jahl.

Mafanikio ya Muhammad yalianza kufifia pale Makka. Khadija, mfad­hili wa kwanza, swahiba wake aliyejitolea katika faragha na upweke wake, muumini mkereketwa wa imani yake, alikufa; vivyo hivyo Abu Talib, ambaye alikuwa mlinzi wake mwaminifu na makini.
Kwa kukoseshwa kinga yenye ushawishi ya Abu Talib, Muhammad katika hali hiyo, alikuwa kama mtu mhalifu mjini Makka, aliwajibika kujificha na kuwa mzigo wa wema wa watu ambao imani yake mwenyewe ili­waingiza kwenye mateso (sic1). Kama manufaa ya dunia yangekuwa ndio lengo lake, aliweza vipi kufanikiwa?

(The Life of Muhammed)

Washington Irving amekosea kwa kusema kwamba Muhammad "alikuwa mzigo wa wema wa watu ambao imani yake mwenyewe ili­waingiza kwenye mateso." Kamwe Muhammad hakuwa mzigo kwa yeyote. wakati wowote. Watu wa ukoo wake Bani Hashim waliona fahari na upendeleo kumlinda yeye na kuutetea Uislamu, vyote hivi vilikuwa hazina yao kubwa mno.

Walitambua kwamba akiwepo Muhammad miongoni mwao, walikuwa wapokeaji wa neema za Peponi na hawakuwa na nia ya kuzipoteza neema hizo kwa jinsi yoyote ile.

Ni nani mwengine isipokuwa ukoo wa Banu Hashim ambaye angemlin­da Muhammad na Uislamu? Muhammad alikuwa musuli na damu yake, na Uislamu ulikuwa uhai na mapenzi yake.

Kosa lingine ambalo mtaalamu huyu mashuhuri wa historia amelifanya lipo ndani ya swali ambalo ameliuliza: "Kama manufaa ya dunia yangekuwa lengo lake, aliweza kuyapata jinsi gani?"

Manufaa ya dunia hayakuwa madhumuni ya Muhammad. Quraysh walikuwa tayari kumpa yeye manufaa ya dunia; walitaka kumpa utajiri, utawala na starehe. Vyote hivyo wangempa kama angevitaka. Lakini alivikataa katakata. Je, wangeweza kumpa chochote kingine zaidi ya hivyo?

"Muhammad alikuwa na lengo moja tu, nalo ni kufanya kazi aliyoamri­wa na Mwenyezi Mungu (S.w.t.), yaani kutangaza Uislamu - Dini ya Mwenyezi Mungu"

Sir William Muir

Kujitoa muhanga ambako Abu Talib na familia yake walifanya kwa ajili ya mpwa wake, ingawa bado hajasadiki ujumbe wake, ameikiri tabia yake kuwa ni nzuri ya kipekee na ni mkarimu si mchoyo na mbinafsi. Hapo hapo wanadiriki kuhoji uthibitisho madhubuti wa uaminifu wa Muhammad. Abu Talib hangefanya hivyo kwa mpenda uwongo; na alikuwa na njia nyingi za kuchunguza.

(The Life of Muhammed, London, 1877)

Sir William Muir anasema kuhusu jambo hili: "Kama kweli isingekuwa kwa sababu ya ushawishi na ulinzi mkali wa Abu Talib, ni dhahiri kwamba nia ya uchokozi wa Maquraysh inge­hatarisha uhuru na pengine uhai wa Muhammed."

(The Life of Muhammed, London, 1877).

Turji Zaydan

Sababu iliyomfanya Abdul Muttalib amshawishi Abu Talib kufanya kazi ya kumlea Muhammad, ilikuwa, Abu Talib na Abdullah walikuwa wato­to wa mama mmoja. Bila shaka, ulinzi wa Abu Talib ulikuwa sababu kubwa, si tu kwa ushindi wa ujumbe wa Muhammad lakini pia kwa sababu ya usalama wake mwenyewe.
Abu Talib alikuwa na hadhi kwa Maquraysh, na mtu mwenye kuheshimika sana. Muhammad aliishi ndani ya nyumba yake kama mmojawapo wa watoto wake…

(Complete Works, published by Dar. ul-Jeel, Beirut, Lebanon, Volume 1 page 91, 1981).

Luteni Generali Sir John Glubb ameandika kwenye kitabu chake, the Life and Times of Mohammad.
Kwamba Abu Talib hafikiriwi na Waislamu kuwa shujaa kwa sababu alikufa kabla hajasilimu. Lakini anaongezea, "Hata hivyo, kama isingekuwa kwa ujasiri wa kumlinda mpwa wake, inawezekana Uislamu ungesambaratika ukiwa katika siku zake za mwanzo.

Wote wawili, Sir William Muir na Sir John Glubb na wataalam wengine wengi wamejiingiza katika kusema kwamba Abu Talib alikufa kabla hajasilimu. Kama wakitakiwa kuthibitisha madai yao wangekimbilia kwenye maandishi ya Imam Bukhari. Bukhari anasema kwenye "hadithi" yake kwamba; wakati Abu Talib alipokuwa taabani kitandani, Mtume alimsisitizia asilimu, lakini alisema kwamba kufanya hivyo kungemuaibisha yeye na rafiki zake Maquraysh.

Waandishi wa "hadithi" hii walisahau kitu kimoja. Abu Talib alikuwa anakufa na alijua kwamba hangewaona tena rafiki zake, Maquraysh.

Alitambua kwamba alikuwa anakwenda kukutana na Muumba wake. Kwenye kipindi kama hiki hangewajali Maquraysh. Shauku yake wakati wote ilikuwa kufuzu kumfurahisha Mwenyezi Mungu. Alithibitisha hilo kwa vitendo vyake zaidi kuliko mtu mwingine yeyote ambaye angeweza kuthibitisha kwa maneno yake kwamba imani yake kuhusu Upweke wa Mungu na kwenye ujumbe wa Muhammad kama mjumbe Wake, ilikuwa imani imara thabiti na ngumu kama mwamba usiotikisika.

Amin Dawidar, mtaalam wa historia wa zama za sasa wa Misri, anase­ma kwamba Abu Talib alikuwa kama ngome ya Muhammad ambayo ilimhifadhi yeye (Muhammad) kutokana na joto lote na baridi yote na shutuma na ukaidi wa walimwengu. "Na Abu Talib alipofariki," anase­ma: "Muhammad alijikuta ana kwa ana na adui kwa mara ya kwanza katika maisha yake. Bila shaka, kifo cha Abu Talib kilikuwa msiba kwake."

Hakuwa na lingine la kufanya ila Abu Talib aliamua kuwa Mwislamu na Muumini. Hakuna mtu anayeweza kumpenda Muhammad na masana­mu kwa wakati mmoja; mapenzi haya mawili hayaendi pamoja hata kidogo. Na hakuna mtu anayeweza kumpenda Muhammad na auchukie Uislamu. Kumpenda Muhammad na kuchukia Uislamu ni vitu visivy­oweza kuwekwa pamoja.

Yeyote anayempenda Muhammad, lazima apende Uislamu. Kama kuna kitu chochote kisichokuwa na shaka kati­ka historia ya Uislamu, ni mapenzi ya Abu Talib kwa Muhammad. Kama ambavyo imeandikwa kwenye kurasa za nyuma, Abu Talib na mke wake, walimpenda Muhammad zaidi ya walivyowapenda watoto wao. Mapenzi hayo yalikuwa na chemchem moja tu - yaani kukubali kwamba Uislamu chanzo chake cha asili ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Abu Talib alijivuna kwamba Mwenyezi Mungu alimteua Muhammad mtoto wa ndugu yake, Abdullah, katika Uumbaji wote, kuwa awe mjumbe Wake wa mwisho na Mjumbe mkubwa kabisa kwa watu wote. Muhammad alikuwa pendo kubwa kabisa na fahari kubwa kabisa ya ami yake, Abu Talib.

Kwenye Kitabu Chake, Mwenyezi Mungu (s.w.t) alitambua mwenyewe ulinzi ambao Abu Talib alimpa Muhammad Mustafa, kama ulinzi wake mwenyewe kama isemavyo Aya ifuatayo: "Je! Hakukukuta yatima akakupa makazi (mazuri ya kukaa)" (Quran 93: 6)

Mwenyezi Mungu alimpa ulinzi na ulezi (uangalizi) Mtume Wake Muhammad Mustafa, kupitia kwa mtumishi Wake Abu Talib.

Abu Talib alifanya kazi Makka kwa ajili ya Utukufu na Uwezo wa Uislamu na alikuwa mlezi wa maadili.

Kwa muda wa miaka 10 alikien­desha chombo cha Uislamu wakati wa ujinga na matatizo mbali mbali kwa ustadi, akiona mbali na imani ambayo iliwakasirisha walezi wa masanamu ya wapagani wa Arabuni. Matendo yake ni sehemu muhimu ya simulizi ya Uislamu, pia ni uthibitisho usiopingwa wa imani yake kwa Mwenyezi Mungu na mjumbe Wake - (imani ) ya Uislamu.

Mwenyezi Mungu na awabariki waja wake wapendwa, Khadija na Abu Talib. Wote wawili waliuweka utii kwake Yeye mbele kuliko kitu cho­chote kingine katika maisha.

  • 1. Sic- Japo kwa makosa. Maana yake ni kukataa maneno ya mwandishi aliyenukuli­wa

Sura Ya 13: Khadija - Mama Wa Waumini

Kabla ya Uislamu, Khadija alikuwa Malkia wa Makka. Wakati jua la Uislamu lilipochomoza juu ya upeo wa macho, Mwenyezi Mungu ali­furahi kumfanya pia Malikia wa Uislamu. Mwenyezi Mungu pia alifu­rahishwa kumfanya yeye Mama wa Waumini, kama Asemavyo kwenye Kitabu chake.

"Nabii yu karibu zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao wenyewe, na wakeze ni mama zao.
(Quran 33 : 6)

Maelezo ya mfasiri

"Sura hii ya (33) inathibitisha hadhi na nafasi ya wakeze Mtukufu Mtume, ambao walikuwa na ujumbe maalum na wajibu kama Mama wa Waumuini. Hawakutakiwa kuwa kama wanawake wa kawaida: wali­takiwa kuwaelekeza wanawake katika mambo ya kiroho, kuwatembelea na kuwasaidia wagonjwa au wenye dhiki, na kufanya mambo mengine mema katika kusaidia ujumbe wa Mtume." (A.Yusuf Ali)

Cheo cha Mama wa Waumini kinaonyesha kutayarishwa hususani kwa ajili ya Khadija. Bila Khadija, cheo hiki hakina maana. Yeye na yeye peke yake alionyesha mapenzi ya dhati ambayo yanatolewa na mama tu kwa waumini. Mama anaweza kuwa anahisi njaa lakini kama watoto wake wana njaa, atawapa chakula watoto wake kwanza. Kwa hakika, kama ni muhimu katika hali ya dharura atawalea na njaa huku akifurahi.

Hali hii imetokea mara nyingi katika historia, hasa zaidi wakati wa vita na njaa. Ni jambo la uhakika kwamba watoto walioshiba na kutosheka, inatosha kumfanya mama afurahi na kutosheka, inatosha kumfanya yeye (mama) asahau njaa na kiu yake.

Mapenzi ya mama hayana shar­ti; yanalenga hali zote na kujumuisha wote.

Waislamu walio wengi Makka walikuwa masikini. Hawakuwa na vyan­zo vya mapato, na walikuwa hawana namna ya kuwawezesha kujipatia riziki kwenye jiji ambalo uchumi wake ulikuwa mikononi mwa makun­di ya siri ya waubudu masanamu. Wanachama wa makundi ya siri wal­itoa agizo kwamba Mwislamu asilipwe ujira wowote kwa kazi yoyote atakayofanya na ni marufuku kununua kitu chochote kutoka kwake.

Walitambua kwamba ufukara wa mali uliathiri vibaya mwili na roho na walidhani kwamba wakati upinzani wa Waislamu utakaposhindwa, kutokana na kudhoofika kiuchumi, wangeukana Uislamu, na wangemkataa Muhammad. Lengo la sera hii ilikuwa ni kuwanyima chakula Waislamu.

Lakini Khadija aliwalisha Waislamu masikini kila siku, hivyo kwamba hakuna hata mmoja miongoni mwao aliyedhikika kwa njaa, na aliwapa mahali pa kukaa. Kwake yeye, utoaji wa sadaka halikuwa jambo jipya lakini kipimo na uwezo wa msimamo ilikuwa kama ifuatavyo: alitumia fedha nyingi mno kwa ajili ya masikini na Waislamu wa Makka wasiokuwa na nyumba, hivyo alikwamisha mpan­go wa matajiri wa Makka waabuduo masanamu.

Msaada ambao Khadija aliutoa kwa jamii ya Waislamu wa Makka, ulikuwa muhimu kwa uhai wa Uislamu. Msaada wake kwa jamii ya Waislamu ulihakikishia uhai wa Uislamu wakati ulipokuwa katika hali ya mkwamo. Katika hali hii, alikuwa mtengenezaji wa historia - histo­ria ya Uislamu.

Wake zake Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wote ni kina Mama wa Waumini; lakini kuna tofauti kubwa kati yao na Khadija. Wanawake wote walioolewa na Mtume Muhammad huko Madina walipokea ujira kutoka Hazina ya Umma. Baadhi yao walidai haki maalumu na marupurupu kutoka kwake. Walisema kwamba haki maalum zilizolipwa zilikuwa hazitoshi kwa mahitaji yao.

Kwa upande mwengine, Khadija kamwe hakuomba kitu chochote kuto­ka kwa mume wake. Khadija aliamua mali yake iwe Hazina ya Umma kwa ajili ya Waislamu. Hapo Makka hapakuwepo Hazina ya Umma, ilikuwa ukarimu usio na mpaka na utajiri mwingi wa Khadija ambao ndio uliiokoa Jamii ya Waumini.

Alikuwa anajihusisha sana na ustawi wa wafuasi wa mume wake, hivyo kwamba aliridhika kutumia fedha zake zote kwa madhumuni haya. Mwenyezi Mungu ambariki mtumishi Wake, Khadija, Mama wa Waumini zaidi na zaidi.

Khadija kama Mama

Dk. Sir Muhammed Iqbal (d. 1938) alikuwa Mshairi Mwana falsafa wa Indo-Paksitan. Pia alikuwa kichocheo cha mwamko wa Waislamu karne ya 20.

Anasema kwamba, mama anashika nafasi ya pili baada ya Mungu Mwenyewe. Mama analeta maisha mapya hapa duniani, yaani anaumba; na tendo hilo - tendo la kuleta maisha mapya hapa duniani au tendo la kuumba, linamtaka mtu ajitolee muhanga. Katika kuleta maisha mapya hapa duniani, mama huyaweka maisha yake hatarini. Kwa hiyo, mama anastahili hadhi na heshima kubwa sana.

Kinachomfanya mama ayatoe muhanga maisha yake ni mapenzi­mapenzi kwa mwanawe. Mapenzi kwa mwanawe ni mapenzi yaliy­otakasika. Kwenye utakatifu, mapenzi ya mama kwa mwanae yanashika nafasi ya pili baada ya mapenzi ya Mungu Mwenyewe.

Khadija alikuwa mama aliyejivunia watoto watatu - watoto wanaume wawili na mwanamke mmoja, kama ilivyokwisha onyeshwa huko nyuma. Watoto wawili wa kiume - Qasim na Abdullah walifariki dunia wakiwa wachanga. Mtoto wake wa mwisho na ndiye tu aliyebaki kati­ka kuishi alikuwa Fatima Zahra.

Kama Khadija alikuwa mama bora, Fatima Zahra alikuwa binti bora.

Fatima Zahra, binti bora wa Muhammad Mustafa na Khadija, naye pia alipata kuwa mama bora. Alikuwa mama wa watoto wa kiume wawili -Hasan na Husain - na mabinti wawili- Zainabu na Umm Kulthum.

Khadija na Fatima Zahra - mama na bintiye - walikuwa wawili miongo­ni mwa wanawake wanne walio bora hapa duniani. Wote wawili wali­fanya umama utakasike. Waliufanya umama utukuke na kuheshimiwa.

Kama ambavyo imesemwa huko nyuma, katika kitabu hiki wanawake hawakuwa na hadhi kabla ya Uislamu huko Arabuni. Kwenye jamii iliy­otawaliwa na mfumo dume walikuwa wana dhulumiwa kikatili na wal­ifanyiwa mambo kama wanyama. Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alikomesha dhuluma ya wanaume kwa wanawake, na aliwapa hadhi ambayo wanawake walikuwa hawajapewa katika nchi yoyote na wakati wowote. Kuhusu wakina mama alisema:"Pepo ya mtu ipo chini ya miguu ya mama."

Maana yake ni kwamba hakuna mtu anayeweza kuwa na matumaini ya kupata pepo kama amemkasirisha mama yake. Mtu kuipata pepo lazi­ma awe na uwezo wa kufuzu kuupata wokovu, na hakuna mtu ambaye amemkasirisha mama yake akaupata wokovu.

Hivyo Mtume wa Uislamu amefanya mtu kufuzu kupata radhi ya mama -mwanamke - sharti linalo tanguliwa kabla mtu hajapata wokovu na kuingia peponi.

Sura Ya 14: Khadija, Mwanamke Mkamilifu

Kumekuwepo na wanawake wengi katika historia ya ulimwengu huu ambao walipata kuwa wakubwa na maarufu kwa sababu ya matendo yao makubwa. Jamii ya kibinaadamu inaweza kujivunia kwa haki kabisa kutokana na (wanawake) hawa. Lakini katika historia ya ulimwenguni wote, wako wanawake wanne tu ambao wangeweza kufikia vipimo vya daraja ya juu vya ukubwa wa kweli na ukamilifu uliowekwa na Uislamu. Walifikia kwenye vipimo hivi kutokana na huduma zao kubwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Muhammad Mustafa, Mtume wa Uislamu, Mpokeaji wa Ufunuo (Wahyi) kutoka mbinguni, na Mfasiri wake, aliwatambua. Nao ni:

1. Asiya, mke wa Firauni,

2. Maryam, mama wa Isa, (Yesu)

3. Khadija, binti wa Kuwaylid na

4. Fatima Zahra, binti ya Muhammad Mustafa (s.a.w.w)

Muhammad Mustafa aliwaona wanawake wanne tu walio bora katika jamii ya dunia nzima. Baina ya hao wanne, wawili wa mwisho wanato­ka nyumba moja; wao ni Khadija, mama wa Fatima, na binti yake, Fatima. Khadija alikuwa mfano kwa roho iliyo bora na iliyokamilika.
Katika jamii iliyosalia hapa duniani, wanawake wengine tu ambao wanaweza kufuzu kuwa wanawake wenye sifa ya ubora, wangekuwa ni wake zake wengine wa Muhammad Mustafa. Lakini yeye mwenyewe alitoa hukumu kuhusu jambo hili, na hukumu yake haifutiki haibadili­ki. Alimtaja Khadija tu miongoni mwa wake zake kwamba ni mwanamke bora, na kwa hiyo aliwatenganisha - kwa amri wake zake wengine kutoka kwenye kundi la wanawake bora.

Khadija alikusanya katika utu wake sifa zote hizo zinazo mfanya mtu kuwa bora. kama angepungukiwa na yoyote katika sifa hizo, mume wake hangemweka kwenye kundi la walio bora. Na hakuna ushahidi wowote kwamba alikuwa na kasoro hizo, ambazo zinasemekana kwa kanuni kuwa ni tabia za kimaisha ya wanawake.

Tabia mojawapo ya udhaifu wa wanawake ni wivu. Khadija hakuwa na wivu wa aina yoyote. Alikuwa mwanamke aliyeona ukamilifu, furaha na kutosheka katika kutoa msaada. Alikuwa mlezi karimu wa masikini. Alikuwa anajisikia mwenye raha wakati anawapa chakula wenye njaa na huzuni. Matendo ya kuwalisha na kuwaliwaza wenye njaa na huzu­ni haikulazimu juhudi ya dhamira kwa upande wake; kwake matendo hayo yalikuwa kawaida yake.

Kama vile ambavyo Khadija alivyokuwa hana wivu, pia alikuwa habezi. Kitu kimoja ambacho kamwe hakukifanya, ni kuumiza hisia za mtu. Hakumtania mwanamke yeyote, hakujaribu kumdhalilisha mtu yeyote; kamwe hakumdharau mtu yeyote; kamwe hakukasirika na kuchukia na hakujiingiza katika kutoa maamuzi. Hakutamka neno baya au neno la kashfa dhidi ya mtu yeyote. Alikuwa na moyo wa kuelewa, alikuwa mtu wa kujihusisha sana na hisia za wanawake wanyenyekevu na masikini sana, na alidhikika kwa sababu ya dhiki ya wengine.

Kuna wakati ambapo Khadija aliitwa Binti wa Wafanyabiashara na Binti wa Makka. Halafu kuna wakati ambapo aliamua mali yake nyingi imi­likiwe na Uislamu.

Alikuwa tajiri sana lakini baadaye akawa masikini kwani hakuwa na kitu. Alibadilisha mfumo wa maisha ya starehe na kuendesha maisha ya dhiki. Lakini hakuna kilichobadilika katika tabia yake. Alikuwa mwenye furaha, karimu, mkamilifu kama mwanzo. Alitumia muda mwingi sana kujitolea kumtumikia Mwenyezi Mungu, na Mjumbe Wake, na kama ilivyo kawaida, kamwe hakusahau ustawi wa umma wa Waumini. Aya ifuatayo inatoa maelezo kuhusu alivyo:

ثُمَّ أَوْرَثْنَا الْكِتَابَ الَّذِينَ اصْطَفَيْنَا مِنْ عِبَادِنَا ۖ فَمِنْهُمْ ظَالِمٌ لِنَفْسِهِ وَمِنْهُمْ مُقْتَصِدٌ وَمِنْهُمْ سَابِقٌ بِالْخَيْرَاتِ بِإِذْنِ اللَّهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَضْلُ الْكَبِيرُ {32}

"Na wako wanaokwenda mbele kabisa katika mambo ya kheri, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo fadhila kubwa." (Qur'an 35 : 32)

Khadija, aliyemkamilifu, alikuwa mstari wa mbele kufanya "Matendo mema." Alikuwa na hali ya msukumo wa utakatifu ndani mwake. Kupitia "matendo yake mema" akawa mpokeaji wa neema za hali ya juu kutoka Mbinguni.

Khadija alikuwa mwanamke aliyekamilika, mke aliyekamilika wa Muhammad Mustafa, Mama aliyekamilika wa watoto wao, na Mama aliyekamilika wa Waumini.

Imani kwamba Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma ilikuwa kama springi ambapo ndipo Khadija alipata majibu ya mafanikio ya maisha yake. Yeye aliyepewa kile Quran inachokiita Qalb Salyim (moyo mtulivu) aya ya 89 kwenye Sura ya 26. Qalb Salyim au moyo tulivu,

A. Yusuf Ali mfasiri na mfafanuzi wa Quran Majid ametoa maana ifu­atayo: "Moyo uliotakasika, na usio athiriwa na maovu yanayotesa wengine. Kwa sababu kwa lugha ya Kiarabu moyo unaeleweka kama kiini cha hisia maono na akili, na matokeo ya tendo, ina jumuisha tabia yote."

Ulinganifu wa tabia ya Khadija ilikuwa ishara ya Qalb Salyim yake. Khadija alizaliwa na "Qalb Salyim" (moyo mtulivu) kama vile tu wale wateule wa Mwenyezi Mungu wanavyo zaliwa nayo. Ni moyo uliokuwa unabubujika imani, kuutumikia Uislamu. Mapenzi na shukurani kwa Mwenyezi Mungu.

Sura Ya 15: Ukarimu Wa Khadija

Khadija Bint wa Arabuni, na Muhammad Mustafa, walioana mwaka wa A.D. 595. Miaka kumi na tano baadaye, Muhammad aliteuliwa na Mwenyezi Mungu kuwa Mjumbe Wake. Kama Mjumbe wa Mungu, kazi yake ilikuwa kutangaza Uislamu hapa duniani. Kuanzia hapo, kila kitu kilibadilika kwa Khadija.

Alitoa wakfu utajiri wake wote kwa ajili ya Uislamu. Wakfu huo ulipatikana katika kipindi mwafaka kwa Uislamu. Khadija alimwambia mumewe kwamba utajiri wake wote umekuwa mali yake, na atumie utajiri huo kwa jinsi apendavyo.

Ukarimu wa Khadija ulikuwa mng’aro wa kiwenyewe.

Muhammad Mustafa “aliwekeza” utajiri wa Khadija kwenye Uislamu. Hapajafanyika “uwekezaji” mzuri kama huo katika historia ya binadamu. “Uwekezaji” huu ulikuwa hakikisho kwamba mwendo wa Uislamu hautsimamishwa au hata kudumazwa kwa sababu ya kusefu wa matumizi muhimu na msaada. Ulikuwa ni uwekezaji ambao, mpaka hii leo, unalipa “migawanyo” mingi na utalipa “migawanyo” kwa kila kizazi cha Waislamu, mpaka mwisho wa muda.

Lakini nyenzo ya utajiri haikuwa ya uwekezaji pekee ambao Khadija alifanya kwa ajili ya Uislamu. Vilevile aliwekeza muda wake, kipaji, nguvu na juhudi na moyo katika Uislamu, uwekezaji unaojulikana vinginevyo kama msimamo wa kujituma. Alitambua ndoto na matu­maini ya mume wake na alishiriki yote pamoja naye.

Nia ya Khadija kusaidia Uislamu ilikuwa dhahiri mno hivyo kwamba Mwenyezi Mungu (S.w.) alifurahi na kuuita utajiri huo wa Kwake Mwenyewe katika aya ifuatayo:

وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَىٰ {8}

"Na akakukuta fakiri akakutajirisha" (Qur'an 93: 8)

Maelezo ya mfasiri:

"Mtukufu Mtume hakurithi utajiri wowote na alikuwa masikini. Mapenzi ya kweli, safi, na ya dhati ya Khadija si tu kwamba yalimwon­dosha na kumweka juu ya tamaa ya kupata, bali yalimfanya ajitegemee kwa mahitaji ya kidunia, mnamo siku za usoni za maisha yake, yal­imwezesha yeye kutumia muda wake wote kumtumikia Mwenyezi Mungu." (A.Yusuf Ali).

Mwenyezi Mungu alimtajirisha mtumishi wake, Muhammad, kwa mali ya Khadija.

Khadija na makundi mawili ya Wahamiaji Waislamu kwenda Abyssinia (Uhabeshi)

Makundi mawili ya Waislamu yaliondoka Makka mwaka wa 615 na 616 kuepuka mateso ya Maquraysh na walitafuta hifadhi Abyssinia. Jumla ya idadi ya wanaume na wanawake katika makundi yote mawili ilikuwa takriban mia moja.

Wakitolewa wachache katika kundi kama Uthmani na Zubayr, wakim­bizi wengine wote walikuwa masikini mno kiasi cha kushindwa kumudu gharama za usafiri kwenda Abyssinia. Nani aliyefanya mipango yote ya misafara kuipatia vifaa muhimu ikiwa ni pamoja na chakula na maji na gharama nyengine zote za kuwezesha kusafiri? Wataalamu wa historia hawajatoa jibu la swali hili.

Lakini kuna uwezekano mkubwa kwamba Khadija aliipatia misafara vifaa na kulipa gharama za usafiri, na Waislamu wakawa na uwezo wa kukimbilia Abyssinia. Hapa Makka ni Khadija peke yake ndiye aliyekuwa na uwezo wa kudhamini uhamaji wa Waislamu wa kiwango hicho.

Sura Ya 16: Khadija Na Muhammad Mustafa

Katika kipindi cha miaka kumi na tano ya mwanzo wa ndoa yake, kazi za Khadija zilikuwa zile hasa za mke na mama wa nyumbani.
Mwaka wa A.D. 610 Mwenyezi Mungu (S.w.) alimteua Muhammad kuwa Mjumbe Wake, na tangu hapo kazi za Khadija ziliongezeka. Zaidi ya kuwa mume wake, Muhammad alikuwa kiongozi na mlezi wake kati­ka malimwengu yote mawili hapa duniani na Akhera. Khadija alikuwa makini sana katika utendaji wa kazi zake kama mke na mama; na pia, sasa akajitambua katika kazi zake kama Mwislamu na Muumini wa kweli.

Alifurahi kwamba Mwenyezi Mungu alimteua mume wake kuto­ka miongoni mwa viumbe wote kuchukua ujumbe wa Uislamu kuufik­isha duniani, na yeye alijitolea nafsi yake, kwa moyo, akili na roho, kuhakisha kwamba kazi hiyo inatekelezeka ipasavyo na kuleta mafanikio

Wazazi wa Khadija, kama wale wa Muhammad Mustafa, walifariki akiwa bado mdogo sana. Kwa hiyo hakuwa nayo mapenzi ya huruma na upole wa wazazi kama ilivyokuwa kwa Muhammad. Khadija na mume wake walikuwa mayatima lakini hatimaye wote wawili wangekuwa watu wa kuwapa mapenzi na huruma mayatima wa dunia yote.

Kile walichopoteza kutoka kwenye mapenzi na huruma ya wazazi wao, walifanikiwa kupata mapenzi na huruma kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe (s.w.t) za milele na milele.

Khadija alipoingia nyumba ya Muhammad baada ya kuolewa, hakuonyesha kupenda kujikwatua kwa kutumia vipodozi, kuvaa mapambo ya gharama kubwa yaliyoingizwa kutoka nchi za nje na kad­halika. Baada ya ndoa yake, alikuwa na mapenzi ya kufanya kitu kimo­ja tu, nacho ni kumpa mume wake starehe na furaha.

Aliweza kufanik­isha hayo kwa kutumia nguvu zake zote kwa uthabiti. Alistarehe pale ambapo mume wake alikuwa na starehe na alifurahi tu ikiwa mume wake alikuwa na furaha. Furaha ya mume wake ilikuwa furaha yake. Alipewa kipaji hicho adimu na ule mkono stadi uliofanya nyumba ya mume wake kufana kama Pepo hapa duniani.

Wajibu aliofanya Khadija baada ya mume wake kutangaza ujumbe wake kama mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ulikuwa muhimu sana katika his­toria ya Uislamu.

Mara alipotoka nyumbani mwake, alipambana na matatizo. Wapagani walimtesa kwa matusi na walimuumiza kwa mikono yao. Kazi yake ilijaa matatizo, ugomvi na jirani wasio na adabu waliifanya kuwa ngumu zaidi. Lakini mara alipoingia nyumbani mwake, Khadija alimsalimia kwa tabasamu iliyomfanya afurahi. Alisema maneno ya kuchangamsha yenye matumaini na starehe na wasiwasi na woga wake wote ulitoweka.

Tabasamu na maneno ya Khadija yalikuwa kama kitulizo cha mateso aliyofanyiwa Muhammad na waabudu masanamu kila siku. Na kila siku Khadija alimtia moyo na kurejesha ari yake. Uchangamfu wake ulipun­guza shinikizo baya lililosababishwa na matukio wakati wa shughuli zake, na aliweza kupambana na maadui zake tena akiwa mwenye kuji­amini.

Khadija alikuwa ndio chanzo pekee cha furaha yake wakati wa vitisho na hofu. Huzuni na majonzi yalikuja kwa mfululizo kama maw­imbi, yakimtishia kumshinda, lakini mke wake alikuwepo wakati wote na kumwezesha apate ujasiri na ushupavu zaidi kuendelea na kazi yake. Kwake yeye mke wake alikuwa ngao ya kisaikolojia dhidi ya vurugu za Maquraysh zilizokuwa zinaongezeka mara kwa mara.

Khadija alikuwa na uelewa sawa ujumbe huu kama Muhammad alivy­ouelewa, na yeye alikuwa na shauku ileile aliyokuwa nayo mume wake kuona Uislamu unashinda upagani. Zaidi ya kuwa na shauku ya kuona Uislamu unashinda, yeye aliongeza msimamo na uwezo. Alifanya hivyo kwa kuhakikisha mume wake anafanya kazi ya kutangaza Uislamu tu, na kazi ya kutafuta riziki alifanya yeye. Kwa hiyo Khadija alimwezesha mume wake kuelekeza uangalifu wake wote, nguvu zake zote na muda wake wote katika kuendeleza Uislamu. Huu ni mchango wake muhimu alioufanya katika kazi ya mume wake kama mjumbe wa Mungu. Khadija alikuwa tegemeo ambalo alihitaji, kwa maneno yake A. Yusuf Ali, "miaka yote ya matayarisho yake."

Miaka ile kabla ya kutangazwa Uislamu, ilikuwa "miaka ya matayarisho" kwa utume wake.

(A.Yusuf Ali)

Mchana na usiku Muhammad alikuwa ndani ya pango la Hira na Mola wake Mlezi. Matatizo magumu aliyoyatafakari akilini mwake, magumu zaidi kuliko jiwe la kito jekundu litokanalo kwenye jabali lililomzungu­ka, matatizo ambayo si yake, lakini matatizo ya watu wake, ndio, na ya hatima ya mwanadamu, ya huruma ya Mungu na mgongano wa miaka mingi ya uovu na wema, dhambi na Rehema nyingi.

(The Holy Qur'an Introduction)

Inawezekana sana kwamba Muhammad, Mtume - Mteule, aliupangilia na kuuwekea msimamo Uislamu ndani ya pango la Hira. Sura ya Uislamu ilikuwa dhahiri na kuonekana wazi ndani ya maisha yake binafsi muda mrefu kabla hajatangaza kwamba alikuwa mjumbe wa Mungu. Hatujui kwa ufasaha "miaka ya matayarisho" ilidumu kwa muda gani hadi hapo alipofikisha umri wa miaka 40, msingi wa Uislamu ulikuwa akilini mwake.

Muda ulikuwa jambo la msingi katika mpangilio wa Uislamu, na Khadija alijua umuhimu wake kwa mume wake katika kazi yake kwa hiyo Khadija alitengeneza mazingira bora ambamo mume wake angepa­ta mafaniko ya muda, na kusababisha matokeo mazuri. Khadija alikuwa na kipaji cha kusoma hisia za mtu mwengine. Alikuwa anategemea matamshi yasiyotamkwa kutoka kwa mume wake na alien­delea kufanya kile alichotaka kufanya. Miaka ishirini na tano ya maisha ya ndoa, aliyafanya mawasiliano sahihi kabisa na ya karibu sana baina yake na mume wake.

Mnamo mwaka wa 10 baada ya Tangazo la Uislamu, Khadija alifariki dunia. Kifo cha mpendwa huonyesha jinsi mapenzi ya binadamu yanavyoathiriwa na tukio hilo lakini mapenzi ya Muhammad na Khadija hayakuwa ya kusitishwa na kifo; yalikuwa mapenzi ya milele daima. Khadija alipofariki, mapenzi ya Muhammad kwake hayakukatika.

Kwa hakika, mapenzi yake kwa Khadija yaliendelea kuongezeka hata baada ya kutoweka duniani. Hata kuwapo kwa wake zake tisa haikuwa sababu ya kuzuia ongezeko la mapenzi kwa Khadija, na mapenzi yake kwa marehemu, wakati wote yalikuwa yanatafuta namna ya kujionyesha.

Kama Khadija alimfanyia wema mtu wakati fulani na hata kama ali­fanya hivyo mara moja tu, Muhammad Mustafa alikumbuka na aliji­tahidi kuonyesha wema wa aina ileile kwa mtu huyo hata baada ya kifo chake, na alifanya hivyo mara nyingi iwezekanavyo.

Huko Madina, ilitokea Bibi kizee alikuja kumuona Muhammad Mustafa na akampa maombi fulani. Alimsalimia kwa upole, na alionyesha kuhusika sana na tatizo lake, na alimtimizia ombi lake hapohapo.

Alipoondoka Bibi kizee huyo, Aisha ambaye alikuwa mmojawapo wa wake zake, alitaka kujua mtu huyo ni nani. Alisema: "Wakati Khadija na mimi tulipokuwa Makka, mwanamke huyu alikuwa na mazoea ya kuja kumuona mara kwa mara."

Wakati wa uhai wake, Khadija alionyesha ukarimu na wema kwa watu wengi sana. Baada ya kifo chake, Muhammad Mustafa hakuwasahau watu hao waliokuwa wanapokea ukarimu na wema kutoka kwa Khadija, baada ya kifo chake, waliendelea kufanyiwa hayo na mume wake.

Kuhusu haya Aisha alisema: "Wakati alipochinjwa mbuzi au kondoo (nyumbani kwa Mtume), mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliamuru nyama ipelekwe kwa wanawake ambao walikuwa marafiki zake Khadija. Siku moja nil­imuuliza kwa nini alifanya hivyo na alisema: Nawapenda watu wote ambao walimpenda Khadija."(Isaba, Vol. 4, P. 283)

Mwenyezi Mungu (s.w.t) Alimpa heshima mtumishi wake ampendaye, Khadija, kwa kutokuchangia mapenzi ya mume wake na wake wengine. Kipindi chote cha robo karne cha maisha ya ndoa, ni Khadija pekee ndiye alikuwa sahaba na rafiki wa mume wake, Muhammad Mustafa. Kila mmoja aliishi kwa ajili ya mwenzake na walipata machungu na matamu ya maisha wote pamoja.

Mwenyezi Mungu alimpa mtumishi Wake Khadija nafsi na tabia yenye sifa nyingi. Kama alivyoneemeshwa kwa wingi mno kupewa sifa hizo, yeye aliziimarisha kwa kuutendea wema Uislamu.

Khadija alizipamba sifa hizo kwa kumpenda Mwenyezi Mungu kwa kumtii mume wake na kuutumikia Uislamu. Upendo na kutumika kwake ni sifa zilizo mnyanyua Khadija na kumweka kwenye nafasi ambayo hakuna mke mwingine wa Muhammad Mustafa aliyeweza kuifikia. Khadija peke yake, kwa kemikali ya tabia yake aliifanya nyumba ya Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kuwa kama kisi­wa cha amani, kutosheka na furaha katika bahari ya mapambano na ugomvi.

Iliamriwa huko Mbinguni kwamba Muhammad Mustafa lazima aoe mwanamke mwenye malezi mazuri na mwenye kuelewa sana katika Arabu yote.

Hapakuwepo mwanamke wa aina hiyo isipokuwa Khadija. Mwenyezi Mungu alikuwa na madhumuni ya pekee ambayo yange­timizwa na Khadija. Kwa hiyo, ndoa yao ilitengenezwa Mbinguni.

Abbas, Mahmud al-Akkad wa Misri anasema kwenye kitabu chake, “Aisha”: "Ilikuwa amri maalumu ya Mwenyezi Mungu kwamba mke wa mjumbe wake anatakiwa awe mwanamke mpole sana, mwema na aliyetakasika kama Khadija."

Khadija alikuwa mfano halisi wa uchaji Mungu, utakatifu na alikuwa mlezi wa ukamilifu wa kiwango cha juu na maadili ya juu sana. Inaelekea kwamba kama Muhammad Mustafa hakutokea, Khadija angeishi maisha ya pekee bila mume. Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wakati fulani alisema kuhusu binti yake Fatima Zahra, kwamba hakuna mtu mwengine ambaye angemuoa isipokuwa Ali bin Abi Talib: Ingekuwa kweli kabisa kusema kwamba hapana mtu mwengine ambaye angestahili kumuoa Khadija isipokuwa Muhammad.

Kuhusu suala hili, A. Yusuf Ali, mfasiri na mfafanuzi wa Qur'an Majid anasema: Ilikuwa baina yake na Hadhrat Khadija, mwanamke na mke bora kuliko wote.

Alimuoa miaka kumi na tano kabla ya kupewa Utume; maisha yao ya ndoa yalidumu miaka ishirini na tano, na mapen­zi yao yalikuwa ya kiwango cha juu sana, yakilinganishwa katika kipi­mo cha kiroho na kijamii. Wakati wa uhai wa Khadija mume wake hakuoa mke mwingine, jambo ambalo si la kawaida kwa mtu mwenye hadhi kama yake miongoni mwa jamii yake.

Mkewe alipokufa, yeye alikuwa na umri wa miaka hamsini (50), na kwa sababu mbili tu, inaelekea kamwe hangeoa tena, kwa kuwa alikuwa anajiepusha sana katika maisha ya kidunia.

Mambo mawili yaliyotawala ndoa zake zilizofuata ni:

1. Aliwaonea huruma na kuwaonyesha upole wajane walio na dhiki na hawangesaidiwa kwa namna nyingine yoyote katika hali ya jamii ile, baadhi yao, kama Sauda, walikuwa na watoto katika ndoa zao za zamani, hivyo walihitaji ulinzi;

2. Msaada katika kazi yake ya uongozi, kutoka kwa wanawake ambao walipewa maelekezo na kuwekwa pamoja katika familia kubwa ya Waislamu, ambapo wanawake na wanaume walikuwa na haki sawa za kijamii.

Muhammad Mustafa, Mtume wa Mwenyezi Mungu, alitumia fursa zote kuonyesha kuvutiwa kwake na mapenzi kwa Khadija na kutambua ukubwa wa kiwango alicho utumikia Uislamu. Alifanya hivyo, kwanza kabisa kutii amri ya Mwenyezi Mungu kama Kitabu chake kinavyose­ma kwenye Aya zifuatazo:

"… Na kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu…." (Sura Al-Baqara 2:231)
" ...Na neema za Mola wake Mlezi zisimulie..." (Sura 93:11 ).

Muhammad Mustafa mtumishi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alipokea upendeleo na ukarimu mwingi kutoka Kwake kupitia kwa Khadija - alizikariri na kuzitangaza.

Halafu, pili, Muhammad Mustafa alipenda kutaja matendo mema, makubwa ya Khadija aliyoyafanya katika kumtumikia Mwenyezi Mungu na Uislamu, kwa sababu ya kuonyesha mapenzi kwake (Khadija). Hii ilikuwa njia mojawapo ya kuonyesha mapenzi. Ilikuwa pia namna nyingine ya kujikumbusha muda waliyotumia yeye na Khadija wakiwa pamoja Makka.
Mtu anaweza akaona waziwazi kwam­ba katika kumbukumbu zake, fikra zake zilikuwa zinayatembelea maisha yake ya zamani; na pia mtu anaweza kugundua humo dalili za mambo aliyozoea zamani. Palikuwepo na muda katika maisha ya kila mtu ambapo alizidiwa na kumbukumbu ya mambo aliyoyazoea.

Waandishi wa vitabu viwili mashuhuri, Isaba na Istiab, wamemnukuu Bi Aisha akisema: "Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu akiondoka kwenda popote, alimkumbuka, alimsifu na kumrehemu Khadija."

Jinsi muda wa maisha ya ndoa ulivyopita, mapenzi ya Muhammad na Khadija yalizidi kupenya kwenye mioyo yao kwa nguvu zaidi. Kwa mapenzi yake, aliondoa wasiwasi wake wote, woga na huzuni kama ilivyoelezwa hapo kabla. Kwa kutumia istiari ya mashariki: Khadija aling'oa miba yote katika maisha ya Muhammad Mustafa, badala yake, alipanda maua ya waridi ya mapenzi.

Maua hayo kamwe hayakunyau­ka; rangi, harufu na ubichi wao ulikuwa wa daima milele. Kama palikuwepo na ndoa iliyopendeza wakati wote, ndoa hiyo ilikuwa ni ile ya Muhammad na Khadija; ndoa hiyo ilikuwa mpya siku ya mwisho wake kama ilivyokuwa siku ilipoanza.

Khadija alikuwa hai moyoni mwake daima milele. Jina la Khadija lilikuwa mdomoni mwake wakati wote, na mapenzi ya Khadija yalijaa moyoni mwake. Hata kuzungumza juu yake na kumsifu kulimfanya Mtume afurahi.

Kila neno na tendo la Khadija lilidhihirisha busara zake. Katika kuch­agua mume wake, alionyesha uwezo wa kushangaza na wepesi wa kuelewa wa hali ya juu. Lakini uwezo na wepesi wa kuelewa ni vipaji ambavyo wanawake wengine vile vile wanaweza kuwa navyo, na Khadija hakuwa mwanamke pekee aliyepewa vipaji hivi. Maelezo kuhusu uamuzi wenye msukumo wa kimungu uliofanywa na Khadija kukubali kuolewa na Muhammad Mustafa ni kwamba kulifanywa chini ya mwongozo wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Mwenyewe. Kwa hiyo, hangeamua vibaya. Alipokutana na Muhammad, Mtume mteule, Khadija aliona Utukufu kwa mbali sana ndani yake, na alikabidhi hati­ma yake kwenye mikono yake iliyobarikiwa. Mikono hiyo ilinyanyua hatima yake, na kuifanya tukufu.

Sura Ya 17: Khadija Na Wake Wenza Wa Mtume (S.A.W.W)

Jambo la kushangaza ni kwamba wanawake wote wa nyumba ya Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, walikuwa na udhaifu kama ilivyo kwa wanawake wengine. Wake zake wengine wal­isumbuliwa na wivu, na hawakuwa na haya kabisa kuuonyesha (huo wivu). Tukio kuhusu “asali” litadhihirisha jambo hili.

Mmojawapo wa wake zake Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikuwa Zainabu binti Jahash. Alijua kwamba mume wake alikuwa anapenda asali. Kwa hiyo alifanya mpango wa kuwa nayo aina hiyo ya asali. Ilitokea kwamba Zainabu alikuwa na sura nzuri kuliko wake wengine wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Alimtilia maanani sana. Hali hii ilis­ababisha wasiwasi kwa Bi Aisha binti Abu Bakr, mke mwingine wa Mtume. Aisha aliogopa isije mapenzi ya mume wake yakaelekezwa yote kwa Zainabu na kuwabagua wake wengine. Kwa hiyo, Aisha binti Abu Bakr na Hafsa binti Umar, mke wa tatu wa Mtume, walifanya mpango ambao madhumuni yake ilikuwa kumfanya mume wao achukie asali.

Sehemu nyingine ya Hadithi anasimulia Aisha mwenyewe. Imam Bukhari amemnukuu kwenye Kitabu chake cha Talaq (Talaka) na Kitabu cha Tafsiri (ya Sura ya Tahreem) kama ifuatavyo:

"Mimi na Hafsa tulibuni mpango huu kwamba wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu akimtembelea yeyote kati yetu, amwambie kwamba mdomo wake unanuka uvundo wa maghafir (Maghafir ina ladha tamu lakini inayo harufu mbaya. Muhammad Mustafa alikuwa hapendi jambo hili. Alikuwa hapendi harufu kali).

Ilitokea kwamba Hafsa alikuwa mke wa kwanza kutembelewa baada ya kubuniwa mpango huu. Mara Mtume alipoingia chumbani kwake alisema: "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Mdomo wako unanuka harufu ya Maghafir, "Alisema: "Sijala Maghafeer. Lakini nilipokuwa na Zainabu, alinipa asali nikala. Inawezekana kwamba asali ilikuwa na harufu ya maghafeer. Lakini, sitakula asali tena."

Hapa wake wa Muhammad Mustafa Aisha na Hafsa wanaonekana wanafanya hila dhidi ya mke wa tatu - Zainabu. Zainabu alikuwa hajafanya lolote baya kwa Aisha na Hafsa. Alikuwa binamu wa Mtume, Zainabu akimuona Mtume ni mtoto wa mjomba wake (anayezaliwa na mama yake).

Zainabu alimpenda mumewe naye mume alimpenda mke wake. Mke alijua vitu avipendavyo na avichukiavyo mume wake; kati­ka hali hiyo, alikuwa na aina fulani ya asali chumbani kwake ambayo alijua ni kitu anacho kipenda.

Mapenzi ya Muhammad kwa Zainabu yaliwasha miale ya wivu moyoni mwa Aisha. Ili kutuliza wivu huo, alitumia mpango akiwa pamoja na Hafsa dhidi ya Zainabu na kuutimiza. Ni dhahiri kwamba hawa wanawake wawili hawakumwamini mume wao katika kuwatimizia haki zao jinsi inavyopasa. Walifikiri kwamba Zainab anapendelewa na wao wanasahauliwa. Kama wangekuwa wanamwamini, hawangebuni mpango huo.

Abul Kalim Azad anasema kwamba wivu ni silika ya wanawake, na inaweza kuzielemea silika zingine zote walizo nazo. Anasema, Aisha, aliongozwa na silika hii ya kibinadamu kwa lengo la kutunga hila hara­ka haraka ambayo ingemfanya mume wao atumie muda mfupi kuwa na Zainabu kuliko alivyokuwa anafanya.

Muhammad Mustafa aliwaambia Aisha na Hafsa kwamba hangekula asali tena. Tamko hili liliwafurahisha wote wawili kwa sababu labda waliamini kwamba mpango wao ulikwisha fuzu. Lakini, hapohapo Ufunuo uliingilia kati na kulikemea jambo hilo kwa aya ifuatayo:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ ۚ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ {1}

"Ewe Nabii! Kwa nini unaharamisha alicho kuhalalishia Mwenyezi Mungu? Unatafuta kuwaridhisha wake zako. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.” (Qur'an 66:1).

Hadhrat Aisha na Hafsa hawakutaka mume wao ale asali, na alikubali kwamba hangefanya hivyo, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t) Mwenyewe alimkumbusha yeye kwamba ni halali kabisa kula asali na kwamba asi­jinyime raha ya kula kitu hicho.

Muhammad Mustafa kama ilivyokuwa kawaida, alirudi chumbani kwa Zainabu na alifurahia kula asali kama alivyofanya kabla ya tukio hilo.

Maria Mkipt

Mnamo mwaka wa 10 A.H. gavana wa Misri, alimpeleka mtumwa mwanamke aitwaye Mariya Mkipt, kwenda Madina kama mjakazi kum­tumikia Muhammad Mustafa. Baada ya muda mfupi Mariya alipata fursa ya kupendwa na kukaa nyumbani mwake Mtume. Alimpenda na yeye alimpenda. Mary alizaa mtoto wa kiume aliyeitwa Ibrahim. Ibrahim alizaliwa wakati wa mwisho wa uhai wa baba yake. Baba yake, alimpenda sana.

Ibrahim alikuwa zawadi maalum ambayo Mwenyezi Mungu aliwapa watumishi wake, Muhammad Mustafa na Maria Mkipt.

لِلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ يَهَبُ لِمَنْ يَشَاءُ إِنَاثًا وَيَهَبُ لِمَنْ يَشَاءُ الذُّكُورَ {49}

أَوْ يُزَوِّجُهُمْ ذُكْرَانًا وَإِنَاثًا ۖ وَيَجْعَلُ مَنْ يَشَاءُ عَقِيمًا ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ قَدِيرٌ {50}

"Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; anaumba apendavyo, anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anam­tunukia amtakaye watoto wa kiume na wakike na akamfanya amtakaye tasa." (Qur'an 42: 49-50).

Muhammad Mustafa na Maria Mkipt walibarikiwa na Mwenyezi Mungu kwa kuzaliwa mtoto wa kiume, Ibrahim. Walimshukuru yeye kwa baraka kubwa iliyojaza furaha maisha yao na nyumba yao.

Lakini kuzaliwa kwa Ibrahim halikuwa tukio la kufurahisha kwa wake wengine wa baba yake.

D.S. Margoliouth

Miaka ya mwisho ya uhai wake, Mtume ilichangamshwa kwa kipindi fulani kwa kuzaliwa mtoto wa kiume ambaye mama yake alikuwa Maria Mkipt ambaye alimuita kwa jina la Ibrahim muasisi wa kubuniwa (sic) wa dini yake. Mama huyu baada ya kufanyiwa wivu mkubwa sana na wake zake wengine ambao walikuwa hawana watoto, tukio hili lenye kheri liliwasababishia maumivu makali ndani ya mioyo yao, ambayo yalipunguzwa haraka na kifo cha mtoto Ibrahim (ambaye aliishi miezi kumi na moja tu).

(Muhammad and the Rise of Islam, London)

Mmojawapo wa wake zake Mtume ambaye kuzaliwa kwa Ibrahim kulimuumiza sana moyo wake, alikuwa Bi Aisha. Bi Aisha bila shaka alikuwa na wivu dhidi ya Maria -mke mwenza mpya, na alimchukia.

Bahati mbaya chuki yake haikuelekezwa kwa Maria peke yake; chuki hiyo ilivuka mpaka na kuelekezwa kwa mtoto wake mchanga. Aisha alimchukia Ibrahim. Haikupata kutokea kwamba angempenda Ibrahim, si tu kwamba alikuwa kipenzi cha Mtume, lakini pia kwamba alikuwa mtoto mchanga. Lakini kama Aisha alikuwa hawezi kujizuia kuona wivu na chuki na alishindwa kuonyesha mapen­zi kwa mtoto huyo, angalau angejifanya kumpenda, kumfurahisha tu baba yake. Lakini Aisha hakuweza hata kufanya hivyo.

Aisha hakuweza kuonyesha mapenzi yoyote kwa Ibrahim, hata kwa ajili ya kujionyesha tu. Lakini kuna jambo moja ambalo angeweza kulifanya na hilo ni kujizuia kuonyesha hasira kwa mtoto huyo.

Ni jambo la kushangaza kwamba ambapo Aisha alikuwa amejaa hisia za chuki, wivu na kumkataa mtoto huyo, anaonyesha alikuwa hana upole ambao ni tabia ya wanawake duniani pote. Hakuonyesha upole wowote.

Kwa jambo la watoto, na hasa zaidi watoto wachanga hata mwanamke katili huonyesha upole kwao. Lakini si Aisha. Pamoja na kwamba hakuonyesha upole kwa mtoto mpendwa wa mume wake, alimtolea maneno ya kashfa. Hata hivyo Ibrahim hakuishi muda mrefu. Alifariki akiwa mchanga.

Muhammad Husayn Haykal.

"Wakati Maria alipomzaa Ibrahim, tukio hilo lilileta furaha kubwa kwa Muhammad, mtu ambaye umri wake ulizidi miaka sitini. Kwa sababu ya kuzaliwa kwa mtoto, nafasi ya mama yake - Maria pia ilipanda dara­ja. Muhammad sasa alimuona Maria kama mke mweye uhuru, hakika kama mtu anayefurahia nafasi iliyopendelewa sana.

"Ilikuwa ni kitu kisichoepukika kwamba kuzaliwa kwa Ibrahim kunge­washa moto kubwa wa wivu kwenye mioyo ya wake wengine wa Muhammad ambao wote walikuwa wagumba. Pia ilikuwa jambo la kawaida kwamba mapenzi ya Mtume kwa mtoto mchanga na mama yake, yaliongeza nguvu za wivu.

Muhammad alimkarimu kwa kumpa zawadi Salma, mke wa Abu Rafi, na yaya wa Ibrahim. Pia aligawa nafa­ka kwa fukara wote Madina. Alimpa Umm Sayr kazi ya kumlea Ibrahim. Mlezi huyu alikuwa na mbuzi saba na alitakiwa kumpa mazi­wa mtoto.

Muhammad alikwenda nyumbani kwa Maria kumuona mwanae kila siku na kumpakata mikononi mwake. Yote haya yali­chochea wivu miongoni mwa wake wengine waliokuwa wagumba. Swali ni kwamba hadi lini hawa wake wenza wa Maria wangeendelea kuvumilia machungu hayo.

"Siku moja, baba mpya mwenye fahari, Muhammad Mustafa aliingia chumbani kwa Aisha akiwa amembeba mtoto wake wa kiume mikononi mwake ili amwonyeshe Aisha. Alimwambia Aisha jinsi mtoto huyo alivyofanana naye mno. Aisha alimwangalia mtoto na alisema kwamba hakuona mfanano wowote naye. Mtume alipoonyesha furaha jinsi mtoto wake alivyokuwa anakua, Aisha alijibu kwa ukali kwamba mtoto yeyote akipewa kiasi cha maziwa anayopewa Ibrahim, angekuwa na mwili mkubwa na mwenye afya nzuri na nzito kama alivyo Ibrahim. Kweli kuzaliwa kwa Ibrahim ilikuwa sababu ya wake wenza wa Maria kuumia mioyo yao, hivyo kwamba walizidi kutoa majibu yenye kuumiza.
Hali hii ilifika kiwango ambacho Qur'an iliingilia kati kulaani. Bila shaka suala lote hili lilitia doa maisha ya Mtume pamoja na histo­ria ya Uislamu.

"Kwa kuwa Mtume alikuwa anawapa wake zake haki maalum na upen­deleo, wakati ambapo wanawake wa Arabuni walikuwa hawana thamani kabisa katika jamii, ilikuwa ni jambo la kawaida kwao kutumia vibaya uhuru ambao wenzao hawakupata kufurahia kabla yao.

Uhuru huu uli­wafanya baadhi yao kumlaumu Mtume mwenyewe kwa ukali sana, kiasi cha kuvuruga mipango yake ya siku nzima. Mara nyingi hakuwajali baadhi ya wake zake, na aliwaepuka wengine kwa lengo la kuwazuia wasiendelee kutumia vibaya upendeleo waliopewa. Hata hivyo, mmoja wao alisongwa sana na wivu wake hadi akavuka mipaka yote ya staha. Lakini, Maria alipojifungua mtoto, Ibrahim, hawakuwa watulivu na walishindwa kujizuia.

Ilikuwa kwa sababu hii Aisha alikataa kwamba mtoto Ibrahim hakufanana na baba yake, kukataa ambako ni sawa na shutuma ya zinaa kwa masikini Maria asiye na hatia."

(The Life of Muhammed, Cairo, 1935)

Mwenyezi Mungu alimwokoa mtumishi Wake mpendwa, Khadija kuto­ka kwenye maudhi ya kulazimishwa na mila na desturi za nchi, kushirikiana kumuangalia na mapenzi kwa mume wake na wake zake (Mtume) wengine. Lakini kama alikuwa na mke mwenza angemfanya­je? Angekuwa na wivu dhidi yake? Kamwe. Kwa Khadija, wivu ulikuwa mbali sana naye kama ambavyo nguzo huachana. Hangewachukia wake wenzake au mke mwenzake. Wakati wa uhai wake hakumchukia jirani yake, mtumishi au mtumwa. Hakuwachukia hata wanyama, wala binadamu yeyote. Khadija alipita kwenye maisha akiwa ameneemeshwa sifa za kimalaika.

Baada ya kifo cha Khadija, Muhammad Mustafa alioa wanawake wengi. Lakini hakuna hata mmoja wao ambaye angeweza kulingana na Khadija kwa ubora. Miongoni mwao walikuwepo wanawake wenye historia tofauti tofauti, na walitoka kwenye tabaka mbalimbali za tabia. Inaonyesha baadhi yao kamwe hawakujua kwamba mume wao ni mteule wa Mungu Mwenyewe, na alikuwa na daraja na hadhi isiyoweza kufikiwa na binadamu mwingine yeyote.

D.S. Margoliouth

Ukaaji wa wake zake Mtume nyumbani mwake ulikuwa wa muda mfupi, kwa sababu ya tabia mbaya, ilitokea mara moja au zaidi ambapo wake zake Mtume wapya walifundishwa na wake wenzao wenye wivu misemo ya Mtume ambayo kwa ujinga wao waliitamka vibaya, jambo ambalo lilimfanya awafukuze (awataliki) bila kukawia. Mmoja wao ali­talikiwa kwa sababu ya kutangaza baada ya kifo cha Ibrahim kwamba kama baba yake angekuwa Mtume, hangefariki - matumizi ya ajabu ya "uwezo wa kuhoji".

(Muhammed and the Rise of Islam, London)

Kwa Muhammad Mustafa, tabia ya baadhi ya wanawake aliowaoa huko Madina, ilionekana kama vile ni utumbuizo mgeni kwa mwenendo wa Khadija. Mwenendo wa Khadija ulikuwa mzuri na mwepesi. Kila neno na tendo lake limepatana na lengo lake la kujaza furaha kwenye nyum­ba ya mume wake, na aliweza kufaulu kutambua hilo.

Muhammad Husayn Haykal wa Misri na Abul Kalam Azad wa India wamewanukuu wakusanyaji na wafafanuzi wa Hadithi ile isemayo kwamba Hadhrat Abu Bakr na Hadhrat Umar wakati fulani waliomba ruhusa ya kumuona Mtume.

Walipoingia nyumbani kwake walimkuta amekaa kimya, na kuzungukwa na wake zake. (wanawake hawa walikuwa wanadai fedha nyingi zaidi kutoka kwa mume wao, kwani walisema kwamba hawangeweza kuishi kwenye umasikini). Umar alisema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kama binti yangu alionekana au alisikika ananiomba fedha, kwa hakika ningezivuta nywele zake. "Mtume alicheka na kusema: "Hawa hapa wake zangu wamenizunguka na wananiomba fedha." Haraka Abu Bakr alinyanyuka na kuzivuta nywele za binti yake, Aisha; na Umar naye alifanya vivyo hivyo kwa binti yake Hafsa. Wote wawili Abu Bakr na Umar wali­waambia mabinti zao: "Mnathubutu kumuomba Mtume wa Mwenyezi Mungu kile ambacho hawezi kuwapeni?"
Walijibu: "La! Kwa jina la Mungu sisi hatumuombi kitu cha namna hiyo."

"Ilikuwa ni kuhusu mazungumzo haya baina ya Abu Bakr na mabinti zao;" anasema Muhammad Husayn Haykal, "kwamba Aya zifuatazo ziliteremshwa."

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لِأَزْوَاجِكَ إِنْ كُنْتُنَّ تُرِدْنَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَيْنَ أُمَتِّعْكُنَّ وَأُسَرِّحْكُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا {28}

وَإِنْ كُنْتُنَّ تُرِدْنَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَالدَّارَ الْآخِرَةَ فَإِنَّ اللَّهَ أَعَدَّ لِلْمُحْسِنَاتِ مِنْكُنَّ أَجْرًا عَظِيمًا {29}

"Ewe Nabii! Waambie wake zako: Ikiwa mnataka maisha ya duni­ani na pambo lake, basi njooni, nitakupeni kitoka nyumba, na kukuacheni mwachano mzuri." (Qur'an 33: 28, 29)

Ingawa inawezekana wake zake Mtume waliungana katika kudai fedha zaidi kwa ajili ya chakula na mahitaji mengine muhimu kutoka kwake.

Aisha na Hafsa walikuwa wanadai kwa nguvu zaidi. Abdullah bin Abbas anasema kwamba wakati fulani alimuuliza Umar ibn al-Khattab ni nani kati ya wake zake Mtume ambao walikuwa wanasisitiza kudai fedha kutoka kwa mume wao, na alisema: "Aisha na Hafsa."

Mtume mwenyewe aliishi maisha ya kujinyima.Mara nyingi aliwahudu­mia kwanza masikini na wenye njaa ndipo akajihudumia yeye. Mfumo wa maisha yake waliokuwa wanaujua zaidi kuliko mwengine yeyote ni wake zake.

Kwa hiyo, walipomwambia kwamba maisha yalikuwa magumu kwa upande wao na kwamba alikuwa anatakiwa kupunguza ukali wake kwa kuwaongezea fedha, alishangaa. Alidhani labda wake zake wangemuiga yeye, na wangeishi maisha ya kujinyima sana kama yeye. Kwa hiyo aliona kwamba madai yao ya pamoja yalimshtua sana; alidhani labda yalichochewa na tamaa kubwa ya chakula na anasa zitokanazo na mali.

Abu Kalam Azad anasema kwamba, wake zake Mtume, hata hivyo, walikuwa binadamu, na wao pia walikuwa na mahitaji na matamanio ya kibinadamu. Kwa hiyo madai yao, yanaeleweka.

Hata hivyo, Mtume, hakufurahishwa na walivyofanya wake zake kwa hiyo alijitenga nao kwa mwezi mmoja.

Muhammad Huseyn Haykal

"Muhammad alijitenga na wake zake kwa mwezi mmoja na hakutaka kusema chochote kwa yeyote kuhusu wao. Wala hakuna mtu yeyote aliyethubutu kusema lolote kwake kuhusu wake zake.

Abu Bakar, Umar, na wakwe zake wengine pia walikuwa na wasiwasi sana kuhusu hatima yao ya kusikitisha iliyokuwa inawangojea "Mama wa Waumini" kwa kuwa sasa walijionyesha kwenye ghadhabu ya Mtume, na matokeo ya kuadhibiwa na Mungu. Hata hivyo ilisemekana kwamba Muhammad alimtaliki Hafsa, binti ya Umar, baada ya kutoa siri aliyoahidi kutoi­fichua.

Habari zilienea kwenye soko la Madina kuhusu kutalikiwa kwa wake zake Mtume. Kwa upande wao wake zake walitubu na kujaa hofu. Walijuta kwamba kuoneana wivu wao kwa wao iliwaelemea na kwam­ba walimtukana na kumkasirisha mume wao. Muhammad alitumia muda wake mwingi akiwa ndani ya nyumba ya stoo aliyokuwa anaimi­liki, ambapo alimweka mtumishi wake Rabah mlangoni kwa muda wote aliokuwa ndani. Ndani ya stoo alikuwa analala juu ya kitanda kigumu sana cha matawi makavu ya mtende.

(The Life of Muhammed, Cairo, 1935).

Baadhi ya wake zake Mtume walijionyesha wenyewe kuwa na wasi wasi sana. Wasiwasi wao usingemfanya kuwa na furaha sana katika maisha yake ya ndoa.

Profesa Margoliouth amenukuu Musnad ya Imam Ahmad bin Hanbali (Vol. IV, P. 221) kuhusiana na jambo hili, kwenye kitabu chake "Muhammad and the Rise of Islam kama ifuatavyo":

"Wakati wa usiku wa manane, yasemekana Mtume alitoka na kwenda makaburi ya Al-Baqi, na akawaombea msamaha wafu waliozikwa pale. Ni kweli kwamba aliwahi kufanya hivyo siku za nyuma; ambapo Aisha alimfuata nyuma kama mpelelezi alipoanza safari yake, akidhani kwam­ba alikuwa ameshawishiwa na baadhi ya mapenzi; lakini aliona kwam­ba mwisho wa safari yake ilkuwa ni makaburini."

Sura ya 66 ya Quran Majid iitwayo Tahrim, inazungumzia zaidi suala la tabia za wake zake Mtume. Mojawapo ya Aya zake imenukuliwa hapo juu kuhusu tukio la "asali." Aya zake za 4 na 5 zinasomeka ifuatavyo:

"Kama nyinyi mtatubia kwa Mwenyezi Mungu (Basi inataka mfanye upesi upesi) kwani nyoyo zenu zimemili upande kidogo. Na kama mtasaidiana juu yake (Mtume kumuudhi kwa mambo ya nyumbani, Mwenyezi Mungu atakuwa naye juu yenu.) kwani Mwenyezi Mungu ni kipenzi chake na Jibrili na waislamu wema wote; na zaidi ya hayo malaika pia watasaidia. (Mtume) akikupeni talaka, Mola wake atampa, badala yenu, wake wengine walio bora kuliko nyinyi;…. (Quran 66:4-5)

Hakuna makubaliano ya wafafanuzi wa Qur'an Majid na wanataaluma wa historia kuhusu tukio mahsusi linalorejewa kwenye Aya hizi mbili. Wengine wanasema kwamba Mtume alimwambia Hadhrati Hafsa jambo la siri kwa sharti kwamba hangelifichua. Hata hivyo, hakuweza kuificha siri hiyo na aliitoa kwa Hadhrati Aisha. Kukiukwa kwa uaminifu ndiko kuliko sababisha kemeo lililopita juu ya mmoja wao kwa ajili ya "kusal­iti amana, na juu ya wengine kwa ajili ya kuutia nguvu usaliti," Hivyo, "kusaidia kosa la kila mmoja wao."

Akizielezea aya za Sura ya 66 ya Qur'an Majid, A. Yusuf Ali, mfasiri na mfafanuzi wake anaandika ifuatavyo: "Nyumba ya Mtume haikuwa kama nyumba nyingine. Wake wenza watakatifu walitakiwa kuwa na kiwango cha juu zaidi cha tabia na unya­mavu kuliko wanawake wa kawaida, kwani wao walikuwa na kazi kubwa ya kufanya.

Lakini, hata hivyo, wao walikuwa binadamu na walikuwa na udhaifu wa jinsia yao, na wakati mwingine walishindwa kufikia kiwango cha kuridhisha.

Ujinga wa Hadharti Aisha wakati fulani ulisababisha matatizo: Akili ya Mtume iliudhika mno na hakuta­ka kukutana na wake zake kwa kipindi fulani.Hafsa, binti ya Hadhrati Umar wakati mwingine alikuwa mwepesi wa kutumia vibaya nafasi yake, na hao wawili walipokutana na kushauriana kwa siri, na kuzungumza na kufichua siri zao, walisababisha huzuni kubwa kwa Mtukufu Mtume ambaye moyo wake ulikuwa mwema na aliyeifanyia familia yake yote matendo mema kwa uvumilivu na huba ya mfano wa kuigwa.

Sura Ya 18: Khadija Na Aisha

Hadhrat Aisha hakuwaonea wivu wake wenzake aliokuwa anaishi nao tu nyumbani kwa Muhammad Mustafa, bali pia mke mwenzake ambaye alikwisha fariki muda mrefu - yaani Khadija. Hakika alikuwa ana­muonea wivu zaidi Khadija, kuliko mke mwenzake yeyote aliye hai. Alimuonea Khadija wivu mwingi mno hivyo kwamba alikuwa na des­turi ya kutamka makaripio makali dhidi ya jina lake.

Abbas Mahmud al-Akkad anasema kwenye kitabu chake, "Aisha":

"Aisha hakuonyesha hisia kali kiasi hicho cha wivu kwa mke mwenza­ke yeyote isipokuwa Khadija. Sababu yake ni kwamba Khadija alik­wisha jitengenezea nafasi yake moyoni mwa mume wake ambayo haku­na yeyote awaye angeweza kuichukua. Muhammad Mustafa alikuwa anazikumbuka sifa za Khadija usiku na mchana.

Muhammad Mustafa wakati wote alikuwa anawasaidia masikini na wagonjwa. Wakati fulani, Aisha alimuuliza mume wake sababu ya kufanya hivyo, alisema: "Khadija aliniambia niwafanyie wema na mapenzi watu hawa. Hili lilikuwa tamanio lake la mwisho."

Aisha aliposikia hivi, alilipuka kwa hasira na kung'aka: "Khadija! Khadija! Inaonyesha kama vile kwako wewe hakuna mwanamke mwengine hapa duniani isipokuwa Khadija."

Mtume alikuwa mtu mwenye uvumilivu mwingi mno. Lakini baada ya Mtume kusikia kauli ya ukali ya Aisha, aliacha kuzungumza naye.

Kama tukio hili linaonyesha jinsi Khadija alivyokuwa anawapenda masikini na wagonjwa, inaonyesha pia jinsi Mtume alivyokuwa anam­tukuza. Muhammad Mustafa alifanya kufuatana na matakwa yake (Khadija) bila kujali chuki ya wazi ya Aisha kwa mke mwenzake. Kwa hakika, alifanya mambo kufuatana na matakwa ya Khadija kipindi chote cha uhai wake. Je! Hakujua kwamba kumbukumbu yoyote ya Khadija ilimkasirisha Aisha? Bila shaka alijua.

Kwa hiyo alipomuuliza, kwanini alikuwa anawalisha masikini, anawapa nguo wasio na nguo na kuwali­waza wenye huzuni, angempa jibu la "tahadhari kubwa" ambalo halingechochea hasira zake. Lakini Mtume hakufanya hivyo. Alitoa jibu la kweli. "Ninatekeleza matakwa ya Khadija."

Je, hii ilikuwa ni sadfa kwamba fikira ya mwisho aliyokuwa nayo Khadija hapa duniani ilikuwa ustawi wa masikini, wagonjwa, mayati­ma, wajane na wasiojiweza? Hapana. Hakuna sadfa kuhusiana na hilo. Kila kitu alichofanya au alichosema Khadija, ilikuwa mpango uliok­wisha tayarishwa kwa lengo la kumfurahisha Mwenyezi Mungu. Na ali­tambua kwamba angefuzu kupata radhi ya Mwenyezi Mungu kwa kuwapenda na kuwatumikia wenye kuhitaji msaada miongoni mwa waja wake wanyenyekevu.

Zawadi ya Khadija ilikuwa kuwafikia wenye njaa, masikini na wag­onjwa hata baada ya kifo chake. Msaada wake haukukoma wakati alipokuwa hai na alipofariki!

Jina na sura ya "Khadija vilichorwa moyoni mwa Muhammad Mustafa, na wala si mwenendo wa wakati au ghadhabu za Aisha zingeweza kufu­ta.

Hadhrat Aisha alitambua kwamba hangeweza kumshawishi Muhammad Mustafa asiendelee kumsifu Khadija na kuzungumza habari zake. Lakini utambuzi huo haukuwa kizuizi cha kumfanya Aisha aache desturi yake ya kumuonea wivu mke mwenzake (Khadija).

Abbas Mahmud al-Akkad wa Misri, anatoa maelezo kuhusu tukio lingine kwenye kitabu chake, "Aisha," kama ifuatavyo:

Siku moja Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikuwa anamsifu Khadija ambapo Aisha alisema: "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Kwa nini wakati wote unazungumza habari za yule mwanamke mzee ambaye ana ufizi uliovimba? Hata hivyo, Mwenyezi Mungu amekupa wanawake wazuri zaidi kuliko yeye." Muhammad Mustafa alisema: "Hapana Aisha! Mwenyezi Mungu kamwe hajanipa mke bora zaidi ya Khadija. Aliniamini wakati ambapo watu wengine walinikana. Alinipa utajiri wake wote ambapo watu wengine hawakufanya hivyo. Na zaidi ya hayo, Mwenyezi Mungu alinipa watoto kupitia kwa Khadija tu."

Inaonyesha kwamba chuki ya Aisha kwa Khadija ambaye aliidhihirisha mno ilimrudia yeye.Mume wake alimwambia kwamba Mwenyezi Mungu alinipa watoto kupitia kwa Khadija tu ambapo wake zake wengine hawakuweza kumpa mtoto yeyote yule.

Kuishi bila mtoto ni hali inayomuumiza sana mwanamke. Lakini aki­ambiwa kwamba yeye ni mgumba, maumivu yale hugeuka kuwa mate-so. Na kama ni mume wake mwenyewe ndiye anayemdhihaki kuhusu ugumba wake, basi maumivu hayo yanakuwa machungu.

Lakini Aisha hakuweza kuacha kumchukia Khadija. Yeye mwenyewe alisema wakati fulani; "Sijamwonea wivu mwanamke yeyote kwa kiwango ambacho nina muonea Khadija." Alionyesha wivu wake mara kwa mara na kila alipofanya hivyo alishawishi hasira ya aina ile ile kuto­ka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Mtoto wa mwisho wa Muhammad Mustafa na Khadija alikuwa binti yao, Fatima Zahra. Alizaliwa mnamo mwaka wa tano wa tangazo la Uislamu na miaka minane kabla ya Hijiriya. Kaka zake, Qasim na Abdallah, walifariki kabla yake. Ilikuwa ni ridhaa ya Mwenyezi Mungu kwamba nasaba ya Mjumbe Wake na rafiki, Muhammad Mustafa, ianzie kwa binti yake, Fatima Zahra. Fatima alikuwa furaha ya moyo wa baba yake, na mwanga wa macho yake. Alimtunza binti yake na wototo wake kama hazina zake kubwa sana. Kwake yeye, walikuwa, mfano wa fura­ha iliyotakasika - hapa duniani na Akhera.

Mara kwa mara Muhammad Mustafa alisafiri nje ya Madina kwa ajili ya kutangaza Uislamu. Ilikuwa ni kawaida yake kutanguliza jeshi lake, na yeye alikuwa wa mwisho kuondoka jijini.

Pia ilikuwa ni kawaida ya Muhammad Mustafa kwamba jambo la mwisho alilolifanya kabla ya kutoka Madina ilikuwa kwenda kwa binti yake, Fatima Zahra, aliye barikiwa na watoto wake. Alimkabidhi Mungu awape ulinzi na kuwaaga.

Kitu cha kwanza alichofanya Muhammad Mustafa aliporudi Madina, ilikuwa kwedwa nyumbani kwa binti yake. Alimuomba Mungu ambari­ki yeye na familia yake. Wakati wa safari zake nje ya Madina, hakuna alichokikosa mno kama watoto wa binti yake. Alipowaona, alisalimiana nao, aliwabusu, aliwabeba na kucheza nao. Siku moja alikuwa nao, basi uchovu kutokana na mwendo mrefu kwa miguu kwenye vumbi na joto la Arabia, ulitoweka, na hali yake kurudi kuwa ya kawaida.

Huu ulikuwa mpangilio wa maisha ya Muhammad Mustafa, na kamwe hakubadili. Maisha ya hisia zake yalizunguka nyumba ya binti yake.

Hadhrat Aisha hakushiriki kumpenda binti ya Mtume kama alivyofanya baba yake. Abbas Mahmud al-Akkad anasema kwenye kitabu chake, "Aisha":

Kwanza kabisa, Fatima alikuwa mtoto wa Khadija; na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alimpenda Khadija sana hivyo kwamba wakati wote alikuwa anamsifia na kumpongeza. Aisha hakupenda hivyo. Kwa upande wa pili Aisha alikuwa hana mtoto. Wakati wowote alipomuona mume wake anacheza na watoto wa Fatima, alizidi kupata uchungu wa maumivu ya kukumbushwa kwamba yeye alikuwa mgumba. Uhusiano wa Aisha na Fatima haukuwa na huba.

Sura Ya 19: Khadija Na Uislamu

Leo hii Uislamu ni jeshi lenye nguvu kubwa kabisa duniani. Maadui wake hawawezi kufanya lolote. Uislamu ni kama gogo la mti mkubwa, ambalo dhoruba za duniani zimeshindwa kuling'oa. Hata hivyo, kuna wakati ambapo gogo hili kubwa sana lilikuwa mti mchanga, ambao uli­hitaji mtu wa kuulinda kutoka kwenye vimbunga vya waabudu masana­mu na ushirikina ambavyo vilitishia kuung'oa.

Waislamu wanaweza wakasahau lakini Uislamu hautasahau kwamba wakati wa uchanga wake, ilikuwa Abu Talib na Khadija walioulinda. Waliufanya Uislamu usidhurike. Abu Talib aliulinda uchanga wa Uislamu usidhuriwe na tufani ya wasioamini na upagani; na Khadija aliumwagilia Uislam maji ya utajiri wake. Khadija hakuruhusu Uislamu mchanga ufe. Hakika Khadija hakutaka hata kuruhusu Uislamu udhoofike kwa sababu ya uzembe. Kwa Abu Talib na Khadija, kazi yao kubwa sana ilikuwa kuulinda Uislamu. Walipenda Uislamu, na wali­yarithisha mapenzi hayo kwa watoto wao.

Kama Abu Talib na Khadija waliulinda Uislamu usidhuriwe na maadui wakati wa uhai wa Muhammad Mustafa, na wakauimarisha kwa kutumia dhahabu na fedha nyingi, watoto wao na wajukuu wao waliulinda usidhuriwe na maadui baada ya kifo chake, na waliuimarisha kwa kumwaga damu yao. Damu yao ilikuwa Takatifu sana kuzidi yeyote katika Uumbaji wote. Hata hivyo, hiyo ilikuwa damu ya Muhammad Mustafa mwenyewe - Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wa Mwisho na Mkubwa kuliko Mitume wote.

Khadija alikuwa shahidi aliyeona kwa jicho lake Uilsamu ulipozaliwa. Aliutunza katika kipindi chake cha uchanga, wakati wa matatizo makubwa sana, na wakati wa ukuaji wake. Uislamu ulipewa umbo na sura ndani ya nyumba yake. Kama kuna nyumba yoyote inayoweza kuitwa mtoto mchanga wa Uislamu, basi ni nyumba yake.

Aliulea Uislamu. Kama nyumba yoyote ile ingeitwa chimbuko la Uislamu, basi ni nyumba yake. Nyumba yake ilikuwa makazi ya Qur'an Tukufu kitabu cha Allah, na chenye Sheria za Kiislamu, za kidini na za Kisiasa.

Ilikuwa ndani ya nyumba yake Hadija ambayo Malaika Jibril alikuwa anamletea Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) ufunuo kutoka Mbinguni kwa kipindi cha miaka kumi.

Khadija amekusanya alama za kwanza nyingi zaidi katika historia ya mwanzo wa Uislamu kuliko mtu mwingine yeyote. Alikuwa mke wa kwanza wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Alikuwa Muumini wa kwanza. Alikuwa binadamu wa kwanza kushahadia kwamba Muumba ni Mmoja tu, na kwamba Muhammad ni mjumbe Wake. Baada ya mume wake alikuwa mtu wa kwanza aliyesikia sauti ya Ufunuo.

Alikuwa mtu wa kwanza kusali sala ya Mwenyezi Mungu akiwa na mume wake. Wakati wowote alipokwenda kumsikiliza Mwenyezi Mungu, Khadija alikuwa karibu naye. Alikuwa wa kwanza kuwa Mama wa Waumini. Alikuwa ndiye mke pekee wa Muhammad Mustafa ambaye hakuishi maisha ya uke wenza. Mapenzi yote na urafiki wote wa mume wake, alipewa yeye peke yake.

Wakati Muhammad Mustafa alipotangaza ujumbe wake kuwa yeye ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na kuwaambia Waarabu waache kuabudu masanamu na aliwaita wakusanyike chini ya bendera ya Tauhid, dhoruba ya mawimbi ya huzuni ilimkabili. Washirika walitaka kumuua. Waligundua namna mpya za kumtesa yeye na walijaribu mara nyingi kumnyamazisha milele. Wakati huo wa shida na dhiki, Khadija alikuwa ngome yake. Ilikuwa kwa sababu tu ya Khadija na Abu Talib, washirikina hawakufanikiwa kuvuruga kazi yake ya kuhubiri na kutangaza Uislamu. Katika hali hii alifanya mchango wake muhimu sana kwa uhai na kutangazwa kwa Uislamu.

Khadija aliiwekea misingi viwango ambavyo vilifanikisha kuwepo kwa amani, uelewano, furaha na utimilifu ndani ya nyumba, na sifa hizo alizishikilia na kuonekana katika maisha yake alitoa mfano kwamba, ufunguo wa nguvu na furaha ya familia ni kiwango cha ukaribu wa huba baina ya wahusika wa familia.

Alionyesha haki na kazi za waume na wake. Viwango vilivyowekwa na yeye vilikuwa ndio rasimu ya maisha ya familia katika Uislamu. Muhammad Mustafa na Khadija walikuwa pamoja kwa miaka ishirini na tano, na katika kipindi hicho walitunga sheria zinazo yafanya maisha ya ndoa kuwa na mafaniko na yenye fura­ha. Tangu hapo dunia imeshindwa kupata sheria bora zaidi ya hizo, hata za kutumia kwa muda mfupi. Uislamu ulijumuisha sheria hizo katika mpango wake.

Khadija aligeuza mawazo ya dhana na kuyaweka katika hali halisi. Maisha yake na Muhammad ni ushahidi madhubuti wa kweli hiyo. Kile alichokipatia dunia haikuwa mpangilio wa misingi au fikira za kinad­haria bali ni uzoefu wa hali halisi yenye nyakati nyingi za furaha iliy­otakasika, ndani ya Uislamu, miitikio stadi ya kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.

Kama ilivyotajwa huko nyuma, Waarabu wapagani walijihisi wame­poteza heshima yao yote. Heshima hiyo ilikuwa ile iliyowalazimisha kuua mabinti zao pindi wazaliwapo. Uislamu ulikataza desturi hii ya kishenzi kwa kuifanya dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu, na kosa la jinai dhidi ya ubinadamu. Mbali ya kukataza kuua watoto wa kike, Uislamu pia umetoa hadhi, heshima na haki kwa wanawake na kud­hamini haki hizo.

Mwenyezi Mungu alitaka kuonyesha kwamba sheria za Uislamu zinatekelezeka. Kuonyesha utekelezwaji wa sheria hizo, na kuonyesha "Mfumo wa Maisha" ya Kiislamu, Aliteua nyumba ya waja Wake, Muhammad na Khadija. Bila Khadija, sheria za Kiislamu zingekuwa hazina maana. Hakika, inawezekana pia kwamba Muhammad Mustafa hangeweza kuzianzisha sheria hizo bila Khadija.

Moja ya Neema kubwa sana Muhammad Mustafa na Khadija waliy­oipata kutoka kwa Mwenyezi Mungu (S.W.) ni binti yao Fatima Zahra. Kama ilivyo onyeshwa kwenye kurasa za nyuma, Fatima alizaliwa baada ya kufa kaka zake Qasim na Abdullah.

Fatima alikuwa na umri wa miaka mitano tu mama yake alipofariki. Baada ya kifo cha mama yake, Muhammad Mustafa, mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alikuwa baba na mama wa Fatima. Katika kumlea na kumkuza binti yake, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikuwa anaonyesha jinsi sheria za Kiislamu zitumikavyo. Kwa kuwa yeye ni kigezo cha Waislamu wote, wanatakiwa kumuiga katika matendo yake yote. Aliweka upendo mkubwa sana juu yake, na alionyesha heshima kubwa mno kwa binti yake.

Kote Makka na Madina, watu wengi mashuhuri kama vile watoto wa wafalme na viongozi wa makabila yenye nguvu, walikuja kumuona Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Alikuwa hasimami wakati wa kusalim­iana na watu hao.

Lakini kama alisikia kwamba binti yake Fatima Zahra alikuwa anakuja kumuona, alinyanyuka na kwenda kumsalimia, alim­sindikiza na kumuonyesha sehemu ya heshima inayostahili kuketi yeye. Hakupata kuonyesha heshima hiyo kwa mtu yeyote wakati wote kati­ka maisha yake, si kwa mwanaume au mwanamke!

"Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu anayompa amtakaye; na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kuu. (Quran 62:4)

Mwenyezi Mungu alimpa Fatima Zahra Ukarimu Wake, binti ya kipen­zi chake na Mjumbe Wake, Muhammad Mustafa.

Alikuwa tu binti wa Khadija, Fatima Zahra, ambaye alipata kupokea sifa kuu za Mbinguni kama isemavyo Qur'an Majid, Sura ya 76 Sura Dahr. Kwa hakika, Sura yote inasema habari zake na familia yake pamo­ja na mume wake Ali bin Abi Talib, watoto wake Hasan na Husain, na mtumishi wake Fizza.

Pia amekuwa fasili ya maandiko yaliyomo kwenye Sura Kauthar (108) "Mwenyezi Mungu alimpa Khadija mkwe ambaye ni Ali bin Abu Talib aliyeitwa baadaye Simba wa Mwenyezi Mungu; "Mkono wa kuume wa Uislamu;" na ngao na kikingio cha Muhammad Mustafa; na Alimpa wajukuu kama Hasan na Husein ambao walikuwa “Wapanda mabega ya Mtume wa Mwenyezi Mungu", na "Viongozi wa Vijana wa Peponi."

Bila shaka Uislamu unamaanisha matendo ya nyumba ya Khadija, na bila shaka Qur'an Majid ni lugha ya familia yake. Binti yake, Fatima Zahra na wajukuu zake, Hasan na Husain, katika kukua kwao wanazungumza Qur'an Majid. Alikuwa na uhusiano ulio sawa kwa Uislamu na Quran kama vile mwanga ulivyo kwa macho, mng'aro kwa lulu na harufu nzuri kwa ua waridi.

Hata lugha yenye msamiati wa kiwango cha juu hushindwa kuzisema au kuzisifia sifa za Khadija. Lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameahidi zawadi zake kwa wapendwa watumishi wake kama Khadija kwenye Aya zifuatazo za Kitabu Chake:

" Hakika wale walioamini na kutenda wema, basi hao ndiyo wema wa viumbe. Malipo yao kwa mola wao ni mabustani ya daima ambayo mito inapita mbele yake, wakae humo milele; Mwenyezi Mungu amewaridhia, nao wameridhika. (malipo) hayo ni kwa yule anayemuogopa Mola wake." (Quran 98:7-8)

Sura Ya 20: Khadija Na Wana Historia Wa Kiislamu

Kwenye vitabu vyao vya historia, sifa ya juu sana ambayo wanahistoria wa Kiislamu wamempa Khadija, ni kwamba aliuimarisha Uislamu kwa utajiri wake. Wanampa sifa hii halafu wana endelea na mambo mengine. Ni kweli kwamba ni utajiri wa Khadija ulioufanya Uislamu kuwa na uwezo wa kukua na kuendelea kuwepo; lakini hii ni sehemu tu ya ukweli. Kama kuna uthibitisho uliotolewa na wanahistoria kuhusu mchango wa Khadija kwa Uislamu, ni mdogo sana. Mbali na kukiri huduma nyingi kubwa kubwa alizozitoa Khadija kwa ajili ya Uislamu. Lakini wengi wa wanahistoria ama wameupotosha ukweli au wameu­ficha ukweli au wameunda maneno (maelezo) yao wenyewe, na kuya­toa kama ndiyo ukweli wa historia.

Siyo historia yote ya Uislamu ya zama za kale ni taarifa ya kweli; sehe­mu fulani ya historia hii ni "tungo." Historia hii bunifu iliandikwa kwa ajili ya au na makundi fulani yenye mwelekeo maalum, Hadithi nyingi za uwongo zilipata nafasi na kuingizwa kama historia ya Uislamu kwa jinsi hiyo na ukweli ulizikwa kimyakimya.

Kutunga hadithi za uwongo, kuziingiza kwenye mzunguuko wa waso­maji na kuuzika ukweli ilikuwa hila ambayo kwayo viongozi wa sala za jamaa, wahubiri kwenye mimbari misikitini, waalimu shuleni, wasaidizi wa wafalme, masultani na makhalifa, maprofesa wa vyuo, wanafalsafa wa sheria, majaji wa mahakama, wafalme, wote walisaidia. Wanahistoria walikuwa na haki au nafasi ndogo sana ya kuchagua kuhusu jambo hili. Hata kama alikuwa mtu mwenye kuheshimika na mwenye msimamo, hakuthubutu kuupaa changamoto msimamo wa chama.

Kama alijaribu kufanya, alihatarisha maisha yake mwenyewe. Kama aliandika historia yenye taarifa ya kweli, aliuawa. Kwa hiyo ali­fuata mwenendo wa vitendo. Aliacha ukweli na kuandika historia ban­dia (za kubuni)

Maulana Shibli Numani, mkuu wa kitengo cha historia ya Uislamu, huko India, ameandika kwenye kitabu chake "Life of the Prophet", Vol. 1 (Azamgarh, India, 1976) kwamba wakati wa utawala wa Khalifa Muawiya (D. A.D. 680), na Waumayya wa baadaye, maelfu na makumi ya maelfu ya Hadith ( I ) zilizalishwa na watengenezaji wa hadithi na ziliingizwa kwenye mzunguko.

Wanataaluma wanahistoria walioko kwenye orodha ya wapokea mshahara wa serikali, waliunganisha pamoja uwongo baada ya uwongo na kuuingiza kwenye vitabu vya his­toria. Na kwa miaka 90, majina ya Ali bin Abi Talib, na watu wengine wa Bani Hashim walilaaniwa kwenye kila mimbari katika dunia ya Uislamu kutoka Sind huko India hadi Hispania - Ulaya. Watoto waliza­liwa, walikua na walikufa, wakisikia laana hizi na kamwe bila kujua ukweli.

Mnamo A.D. 750, ukoo wa Abbas ulichukua ukhalifa, na kuung'oa utawala wa ukoo wa Umayya. Lakini hata huo ukoo wa Abbas haukuwa na nafuu yoyote katika chuki yao kwa familia ya Muhammad Mustafa kwama ulivyokuwa ukoo wa Umayya. Hakika, baadhi yao waliwazidi Waumayya katika kuwafanyia mateso watoto wa Mtume na wafuasi wake. Tabia moja ambayo koo hizi mbili zilikuwa nayo ni ile chuki ya kinyama waliyokuwa nayo dhidi ya familia na watoto wa Muhammad Mustafa.

Edward Gibbon

Watesaji wa Muhammad walipora urithi wa watoto wake; na mabingwa wa waabudu masanamu wakawa ndio viongozi wakuu wa dini yake na himaya.

(The Decline and Fall of the Roman Empire)

Robet Payne

…Tena na tena tutaona wafuasi wa Muhammad (yaani, waislamu) kwa ukatili kabisa wanaangamiza kizazi cha Muhammad bila huruma. (uk. 84 - 85)

Kwa miaka 350, kizazi cha Abu Sufyan na wale waliodai kwamba wana nasaba na ukoo wa Abbas walipigana vita na kizazi cha Muhammad. (uk. 193).

Kipindi chote cha karne za Uislamu, mateso ya kushangaza yalikizun­guka zunguka kizazi cha Muhammad. Ilikuwa kama vile sehemu ile ya dunia ambayo kwa bidii iliukubali Uislamu na Mtume wa Mungu, iligeuka adui wa kizazi chake kiishicho daima milele. (uk. 306).

(The Holy Sword (Upanga mtukufu), 1959)

Kampeni ya makhalifa wa ukoo wa Abbas dhidi ya watu wa nyumba ya Mtume au watoto wake, pia ilidumu kama ulivyo dumu ukhalifa wao ­miaka 500.

Ilikuwa wakati wa ukhalifa wao ndipo historia ya Uislamu ilipoandikwa na hadithi zilikusanywa, zikahaririwa na kuchapishwa. Majaribio yasiyo madhubuti yalifanywa na wasomi makini ambao walitenganisha taarifa zenye ukweli na kuacha taarifa za uwongo, laki­ni kwa mafanikio madogo sana.

Vitabu vingi vya historia na Hadithi siku zote vimebebeshwa mizigo ya "ukweli" au "Hadith" ambazo zimepandikizwa humo.

Historia imesemwa kiusahihi kwamba, ni propaganda ya upande ulioshinda. Makundi yaliyoshinda katika historia ya Uislamu, kwanza yalikuwa, ni Banu Umayya na halafu Banu Abbas ambayo yalifaulu, kwa kunukuu maneno ya Gibbon: katika "uporaji wa urithi wa watoto wa Muhammad." Mara walipochukua vyombo vya dola, walikuwa huru kuandika au kupotosha historia ya siku za mwanzo za uislamu jinsi walivyopenda..
Kwa vile vitabu vingi vya historia ya Uislamu vilipewa "msukumo" na kile wakomunisti wakiitacho "watu wenye mamlaka ya dola" nitawatambulisha waandishi wake kama "wanahistoria wa mahakama." Wanahistoria hawa waliwahadaa wasomaji wao juu ya ngano tatu zifu­atazo kwa kulinganisha na maisha ya Hadhrat Khadija, Mwenyezi Mungu na amuwie radhi na amrehemu.

1. Alikuwa na miaka 40 alipoolewa na Muhammad Mustafa.

2. Alikwisha olewa mara mbili kabla ya kuolewa na Muhammad Mustafa.

3. Yeye na Muhammad Mustafa walizaa watoto sita wa kiume wawili na wakike wa nne.

Tutauzungumzia uwongo huu moja baada ya mwingine.

1. Umri wa Khadija

Wanahistoria wengi wa kiiislamu wanasema kwamba Khadija alikuwa na umri wa miaka 40 alipoolewa na Muhammad Mustafa. Tarakim hii imerudiwa mara nyingi zaidi na wanahistoria hivyo kwamba sasa inaminiwa kama jambo la kweli kabisa. Lakini bado tarakimu hii ina maswali ya wazi kwa sababu zifuatazo:

Hakuna mtaalamu yeyote wa historia anayejua tarehe ya kuzaliwa kwa Khadija, tarakimu "40" ni makadirio tu, na ni makadirio ya juu sana. Ambapo ni kweli kwamba Khadija alikuwa na umri mkubwa kuliko Muhammad Mustafa, hakuwa anamzidi umri kwa miaka 15 kama ambavyo inadaiwa na wanahistoria wengi, lakini anamzidi miaka michache tu.

Bara Arabu ni nchi yenye joto sana, na wasichana wa Kiarabu hubalehe haraka zaidi kuliko wasichana wa nchi zenye baridi au joto la wastani. Hadhrat Aisha inasemekana aliolewa akiwa na umri wa miaka 11. Wasichana wengine wa Kiarabu pia waliolewa mapema sana.

Kwenye nchi kama Arabia, mwanamke hangekaa miaka 40 ya maisha yake akingojea kuolewa. Katika umri wa miaka 40, miaka mizuri kwa maisha ya mwanamke itakuwa imekwisha pita - katika Uarabuni au kwingineko popote. Lakini hata kama akiolewa akiwa na miaka 40, hawezi kufikiria kuzaa watoto. Hata kwenye nchi za baridi na joto la wastani, mara nyingi, mwanamke kupita umri wa kutokuzaa ni 40.

Arabuni hali hii pengine hutokea mapema zaidi. Khadija aliishi miaka mingi katika hali ya upekee bila mume. Kama ambavyo imeonyeshwa hapo kabla, alipokea posa nyingi kutoka kwa mamwinyi na watoto wa wafalme wa Arabuni, lakini alikataa.

Hawakuweza kumshawishi kwa utajiri wao. Kama walikuwa matajiri, yeye Khadija alikuwa tajiri sana kuliko yule aliyewazidi wao. Na kati­ka sifa za mtu binafsi kama sifa za kichwa mkono na moyo wote walikuwa kama vumbi ya miguu yake. Yeyote aliyejaribu kumshawishi kwa kutumia utajiri wao au mamlaka yao angeonekana mpumbavu kama sio mjinga hasa. Kwa hiyo, alitulia hadi hapo alipojitokeza mwanamume ambaye kweli alipendeza - Muhammad Mustafa na alikubali kuolewa naye.

2. Madai ya ndoa zingine za Khadija

Khadija hakuolewa kamwe kabla ya kuolewa na Muhammad Mustafa. Ndoa yake na Muhammad Mustafa ilikuwa ya kwanza na ya mwisho. Wanahistoria hao hao ambao wamedai kwamba Khadija aliolewa mara mbili kabla ya kuolewa na Muhamad Mustafa, wameeleza kwamba mamwinyi wote wa Maquuraysh na watoto wa matajiri wa Waarabu, walimposa, lakini alikataa. Kama angekuwa ameolewa mara mbili kabla, hangesita kuolewa mara ya tatu.

3. Watoto wa Khadija

Imedaiwa na wanahistoria ya mahakama ya Banu Umayya kwamba Khadija na Muhammad walizaa watoto sita na wanatoa orodha ya maji­na yao kama ifuatavyo:

1. Qasim

2. Abdullah

3. Zaynab

4. Rukayya

5. Umme Kulthum

6. Fatma Zahra

Muhammad Mustafa na Khadija walizaa watoto watatu si sita. Nao walikuwa:

1. Qasim

2. Abdullah

3. Fatima Zahra

Miongoni mwa hawa watoto watatu, wawili wa kwanza kuzaliwa -Qasim na Abdullah - walikuwa wanaume, na wote walifariki dunia wakiwa wachanga kama ambavyo imeonyesha huko nyuma. Mtoto wa tatu na wa mwisho alikua binti yao Fatima Zahra. Ni nani hawa watoto wengine watatu wa kike-yaani Zaynab, Rukayya na Umm Kulthum? Swali linajibiwa baadaye kwenye sura hii.

Madai haya yote matatu yamepata kuenea kama ya "ukweli" lakini hata hivyo ni ngano za uwongo. "Mng'ao" wa zama umeyafanya "yaheshimike" hivyo kwamba Waislamu wengi wameyaamini (mada hayo) kuwa ya kweli. Lakini hizi sio kwa namna yoyote, ngano pekee ambazo Waislamu wengi wamezipatia hadhi ya ukweli. Kuna ngano nyingine nyingi ambazo "zimefuzhu" kama za ukweli.

Mifano ifuatayo, itaonyesha kwamba hii inaweza kutokea hata kama hakuna nia ya makusudi ya kuupinda ukweli au kuharibu ukweli.

1. Waislamu wengi wanaamini kwamba mhusika anayetajwa kwenye aya 83 na 94 kwenye sura ya 18 ya Quran Majid (Kahf au pango), kama Zul-Qarnain alikuwa Alexander the Great (Alexander Mkuu) wa Macedonia. Hata Abdallah Yusufu Ali anaunga mkono maoni haya.

Anasema: "Binafsi, sina shaka kwamba huyu Dhul-Qarnain ni, Alexander the Great, Alexander wa kihistoria, na si Alexander wa hadithi za kale…

Na tena, Zul-Qarnain angeweza kuwa yeyote, lakini sio Alexander the Great, Zul-Qarnain alikuwa mteule wa Mwenyezi Mungu, labda alikua Mtume. Alexandaer kwa upande mwengine alikuwa mpagani. Aliwaabudu miungu ya kiume na kike, si tu ya Kigiriki bali pia ya Misri, Babylon na Ajemi.

Harold Lamb

Alexander aliabudu miungu ya ajabu -si Zena tu, bali hata Ammon-Re wa jangwa la Misri, Marduk wa minara ya Babylon, na Anura mlezi wa mahekalu ya Ajemi.

(Alexander wa Macedon, New York, 1946)

Alexander alifanya makosa mengi pamoja na kuua marafiki zake waw­ili wa siku nyingi na majenerali waliokuwa watiifu, Cleitus na Parmenion. Na alipanga mauji ya Baba yake mwenyewe Philip.

R.D.Milns

Hapana shaka kwamba Alexander alipata ufalme kwa kumuua baba yake.

(Alexander the Great, New York, 1969)

Wakati wa vita alizopigana, Alexander aliua maelfu ya watu wasio na hatia waume kwa wake bila sababu ya msingi. Labda alielemewa na uchu wa kumwaga damu.

Mwana historia wa kisasa anasema kwamba kabla hajafa, alirukwa na akili. Na utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kwamba alikufa baada ya kuwa mzoefu wa kupindukia wa kunywa mvinyo.

2. Jina halisi la Abdul Muttalib, babu yake na Muhammad Mustafa, Mtume wa Mwenyezi Mungu lilikuwa Shaiba. Alipokuwa kijana, siku moja alisaidiwa usafiri na ami yake, Muttalib, kutoka Yathrib ( Madina) kuingia Makka. Watazamaji walisema: "Ohoo angalia! Muttalib amemnunua mtumwa mpya"; Muttalib alikasirika ali­posikia kauli hiyo na alisema: "Mlaaniwe ninyi. Huyu si mtumwa wangu. Ni mtoto wa kaka yangu , Hashim." Lakini jina la "Abdul Muttalib" "Mtumwa wa Muttalib" lilimganda huyo kijana. Anajulikana kwenye historia kwa jina lake la kupanga la kupachik­wa -Abdul Muttalib, Jina lake halisi Shaibu limesahauliwa.

3. Mfano huu unatoka kwenye kisa cha Mtume Yusuf. Aya ifuatayo imo kwenye sura ya 12 ya Qur'an Majid (Sura Yusuf)

إِذْ قَالُوا لَيُوسُفُ وَأَخُوهُ أَحَبُّ إِلَىٰ أَبِينَا مِنَّا وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّ أَبَانَا لَفِي ضَلَالٍ مُبِينٍ {8}

"Hakika Yusufu na nduguye (yule aliye baba mmoja na mama mmoja naye) wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi hali sisi ( watoto wa mama mwingine) ni kundi lenye nguvu. Hakika baba yetu yuko katika upotofu uliyo dhahiri. Quran (12:8)

A.Yusuf Ali ameielezea Aya hii ifuatavyo: "Ndugu kumi hawakuwaonea wivu na kuwachukia wadogo zao Yusuf na Binyamin tu, walimdharau na kutomtiii baba yao kama mzee mjinga mwenye kupungukiwa akili.

Katika hali halisi. Yakuub alikuwa na hekima ya kuhakikisha kwamba watoto wake wadogo wasio na hatia walihitaji ulinzi na alitambua Utukufu wa kiroho wa mwanae Yusuf.

Lakini, hekima zake kwao zilikuwa ujinga au kichaa, au kupungukiwa akili, kwa sababu iligusa kujipenda kwao, kama ufanyavyo ukweli mara kwa mara. Na walitegemea juu ya ukatili wa nguvu ya idadi - dhidi ya mzee Yakub, kijana mdogo Yusuf na mvulana Binyamin."

Aya nyingine katika muktadha huo huo, inasomeka kama ifuatavyo:

قَالُوا تَاللَّهِ تَفْتَأُ تَذْكُرُ يُوسُفَ حَتَّىٰ تَكُونَ حَرَضًا أَوْ تَكُونَ مِنَ الْهَالِكِينَ{85}

"Wakasema: "Wallahi! Hutaacha kumkumbuka Yusufu ( na kulia) hata utakuwa mgonjwa au utakuwa miongoni mwa wenye kuangamia."(Quran 12 : 85)

Mfasiri anaifafanua aya kama ifuatavyo: "Wakasema" lazima watakuwa watu wa karibu na Yakuub kabla ya nduguze (Yusuf) kuwasili ( kutoka Misri). Ndugu hawa hawa kwa bidii walipanga uzushi kwamba baba yao alikuwa mzee katili aliyepun­gukiwa na akili, na kila mtu aliamini hilo, hata baada ya watunzi wake kuliacha hilo. Hivyo uwongo haufi kiurahisi, mara unapoanzishwa. (A.Yusuf Ali)

Ipo mifano mingine mingi kwenye historia ya Waislamu na na wsio Waislamu, ya udanganyifu kugeuzwa kuwa kweli. Hivi ndivyo ilivy­otokea kuhusu hizi taarifa za uwongo zilizo husishwa na hadithi ya maisha ya Khadija. Taarifa hizi zilipata kukubalika miongoni mwa Waislamu. Mara uwongo uanzapo, hukataa kufutika.

Pia inawezekana kwamba wanahistoria ambao walikuwa wakikusanya taarifa ili waandike historia ya Uislamu wa siku za mwanzo, waliweza kupata tu visa ambavyo "vilipandikizwa" kwa uhodari kabisa na "taba­ka la watawala" kwenye vyanzo vya mwanzo kabisa. Walishawishiwa kwamba taarifa zinazopatikana kwenye vyanzo hivyo, zilikuwa sahihi, na waliziingiza kwenye vitabu vyao. Madai kuhusu umri, ndoa na watoto aliozaa Khadija, yalichochewa na sababu mbili , ambazo ni:

1. Khadija alikuwa mama wa Fatima Zahra; na alikuwa mama mkwe wa Ali bin Abi Talib; na bibi wa Hasan na Husein. Kwa hiyo, hangeepuka chuki ambayo Banu Umayya na Banu Abbas walikuwa nayo dhidi ya watu wa familia ya Muhammad Mustafa, hasa zaidi Ali, Hasan na Husain.

Hata waandishi wa historia, kwa sehemu kubwa walikubali kuingia kwenye kundi la wale waliokuwa wanawalipa wakati wanaandika historia, lakini kama wangekataa, wangekosa malipo na pengine hata kuuawa.

Kwa hiyo hawakuwa na jinsi isipokuwa kutunga "ukweli" fulani ambao utapunguza umuhimu wa Khadija.
Katika kuchagua "ukweli" ambao wameutunga wao au wenzao waliotangulia, hujiona wako huru kutekeleza busara zao - ushabiki wao. Lakini katika kuyafanya maele­zo yao yakubalike, iliwabidi wawe werevu sana vinginevyo chuki yao ingedhihirika kuwa ya wazi mno. Na thamani ya kazi yao ya historia ingekuwa haiaminiki.

2. Wanahistoria mamluki walitaka kuwaambia wasomaji wao kwam­ba miongoni mwa wake wa Mtume, walikuwepo ambao walikuwa mashuhuri au hata kumzidi Khadija, na kwamba mwanamke huyo ni Aisha. Ilibidi waanze kumtukuza Aisha na si Khadija.

Wanahistoria hawa hawakuwa na hofu na tasnifu ambazo walikuwa wanajaribu kuzikuza kutoka kwa mke mwingine yeyote wa Muhammad Mustafa, lakini walikuwa hawana uhakika kama juhudi zao za kum­wonyesha Aisha kama mke bora kuliko Khadija zingefanikiwa.

Lakini watu hawa walikuwa wanabahatisha na wakatengeneza "tungo" kwam­ba Khadija alikuwa na miaka arobaini na aliolewa mara mbili kabla ya kuolewa na Muhammad. Ni tungo ambayo kwa maoni yao ingeweza kumpinga Khadija. Kwa upande mwingine walidai kwamba Aisha si tu kwamba alikuwa mdogo wa umri na mzuri wa sura bali pia alikuwa bikira.

Kwa matumizi haya ya mantiki za kiholela, wanahistoria wamejenga tasnifu zao za ubora kwa mke mmoja kuwazidi wake wenzake. Lakini, Je Mtume alimuoa Aisha kwa sababu ya ujana wake, uzuri wa sura na ubikira? Abbas Mahmud Ali Akkad, anajibu swali hili kwenye kitabu chake. "Aisha" kama ifuatavyo: Kwa kadiri tujuavyo, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakuoa kwa sababu ya kupata watoto. Kwa ujumla alioa kwa sababu mbili, yaani:

1. Wanawake wengine walikua wanahitaji msaada baada ya kufiwa na waume zao. Walikuwa hawana ndugu wa kuwasaidia. Mtume aliwaoa ili wawe na nyumbani kwao.

2. Mtume alitaka kuvunja upinzani wa makabila ya Waarabu dhidi ya Uislamu. Njia mojawapo ya kufanya kwake yeye ni kuoa wanawake wa makabila hayo.

Pia palikuwa na sababu nyingine ya tatu kuhusu ndoa nyingine za Mtume, yaani, kama yeye alikuwa mwalimu wa wanaume wa Kiislamu, wake zake walikuwa walimu wa wanawake wa Kiislamu, katika mambo yote ya imani za dini. Waliwapa maelezo wanawake wa Kiislamu maana ya Quran na waliwafundisha jinsi ya kuzitumia sheria za Kiislamu kwenye maisha yao binafsi.

Ukimuondoa Khadija, Mtume aliwaoa wanawake wengine wote kwa sababu moja au zaidi ya zile sababu zilizotajwa. Ndoa yake na Khadija ilikuwa ndio pekee iliyo tua kwenye huba, mapenzi na urafiki; na kwake yeye, ilitimiza malengo yote ya ndoa.

Khadija naye pia aliwafundisha sharia za Uislamu kwa wanawake wa Kiislamu, lakini alifanya hivyo zaidi kwa kuonyesha mifano na kwa maadili kama ilivyoonyeshwa mwanzo.

Wanahistoria wa mahakama wamekuwa wakirudia rudia baadhi ya uwongo na nusu ukweli kwa karne nyingi, na kwa marudio hayo wamefaulu kuushawishi Umma wa Waislamu kwamba Khadija aliole­wa mara mbili kabla ya kuolewa na Muhammad Mustafa.

Akiandika juu ya suala la ndoa ya Khadija, Mwandishi wa "Raudhatus-Safa" anasema:

"Watu wakubwa wa kabila la Quraysh walitaka kumuoa Khadija na walipeleka posa zao lakini hakukubali kuolewa na yeyote yule katika wao." (Volume 2, P. 271).

Na mwandishi wa Raudhatul-hbab" anaandika kama ifuatavyo:
"Watukufu wote wa kabila la Quraysh walitaka kumuoa Khadija lakini hakumfikiria yeyote yule katika wao." (Volume1. P. 105)

Kwa mujibu wa wanahistoria wala rushwa, wanasema kwamba wakati Khadija anaolewa na Muhammad Mustafa, alikwisha olewa mara mbili; na alikuwa na umri wa miaka 40.
Kama hii ni kweli, basi ina maanisha kwamba Khadija alikuwa mwanamke aliyefika umri wa kuelekea uzeeni, au labda, kwenye nchi kama Arabuni alikwisha kuwa na umri wa kati ambapo uzuri wake wa ujana ulikwisha toweka. Kwa nini basi mamwinyi wa kabila la Quraysh na watoto wa familia mashuhuri wa Arabuni walitamani sana kumuoa? Hata hivyo, kuwa tajiri na uwezo kama walivyo kuwa, wangeweza kuwapata wanawake wengine vijana na wazuri wa sura, miongoni mwao wengine wangekuwa mabikira, ili wafunge ndoa nao.

Kwa nini basi wakimbilie na kung'ang'ania kumuoa mjane ambaye hata hivyo alikuwa anaelekea uzeeni kiumri? Pia haitakuwa sahihi kusema kwamba wachumba hao waliokataliwa na Khadija walivutiwa na utajiri wake, kwa sababu wachumbiaji wenyewe walikuwa matajiri.

Allama Ali Ahmed Abul Qasim al-Kufi anahoji uthabiti wa hadithi ya ndoa mbili za Khadija kabla ya kuolewa na Muhammad Mustafa. Anaandika ifuatavyo kwenye kitabu chake -Al-Istighatha"

"Khadija hakuolewa na mtu yeyote kabla ya kuolewa na Muhammad Mustafa. Waandishi wote wa historia wamekubaliana kwa pamoja kwamba wakuu wote wa kabila la Quraysh walimposa Khadija, kila mmoja kwa wakati wake lakini aliwakataa wote.

Hatimaye aliolewa na Muhammad Mustafa. Hali hii iliwafanya wanawake mashuhuri wa Maquraysh kumkasirikia. Walisema kwamba wakati watukufu wakub­wa na watoto wa familia mashuhuri jijini Makka walipomposa ali­wakatalia na kuwabeza. Na halafu, wakati anatokea kijana wa ukoo wa Bani Hashim ambaye hakuwa na utajiri wowote, au mamlaka, alipom­posa, alimkubali. Hawa wanawake mashuhuri wa Makka hawakuelewa kwa nini Khadija alidharau maombi ya posa ya watu matajiri na wenye mamlaka katika jamii ya Arabuni, na mwishowe alikubali kuolewa na mtu asiye na kitu wala mamlaka.

Huu ni uthibitisho kwamba Khadija hakuolewa na mtu yeyote kabla ya kuolewa na Muhammad Mustafa.

Watu wengine huuliza swali kwamba kama inadhaniwa kwamba Khadija aliolewa mara mbili kabla ya kuolewa na Muhammad Mustafa, na kwamba alikuwa na umri wa miaka 40 wakati wa ndoa yake ya tatu, kuna jambo lolote la kulaumika hapa? Hapana! Kama mwanamume au mwanamke anaoa au anaolewa zaidi ya mara moja au anakuwa na umri, wa miaka 40 wakati wa kuoa au kuolewa, hakuna jambo lolote la kulaumu hapa. Suala ni kwamba, kama ni kweli au uwongo kama Khadija aliolewa zaidi ya mara moja au kama alikuwa na miaka 40 wakati anaolewa wakati wa ndoa yake ya mwisho.

Swali lenyewe ni je, ni ukweli wa kihistoria kwamba Khadija aliolewa mara tatu; au kwamba alikuwa na miaka 40 wakati wa ndoa yake ya mwisho. Hapana. Sivyo hivyo. Kama mtu anakubaliana na waandishi wa historia mamluki kwamba Khadija aliolewa mara tatu, na kwamba alikuwa na miaka 40 wakati wa ndoa yake ya tatu, hakuna kinachopungua kutoka kwenye hadhi yake. Yeye anaendelea kuwa Mtukufu. Lakini kwa vyovyote vile si kweli kwamba alikuwa mjane wa miaka 40 alipoolewa na Muhammad Mustafa, na, kwa hiyo, si uadilifu kusingizia uwongo kwenye hadithi ya maisha yake, au maisha ya mwanamme au mwanamke yeyote, kuhusu suala hili.

Kila mtu anayo haki ya kutoa mawazo yake lakini si kwa taarifa za mambo yahusuyo ukweli wake. Kama mtafiti wa ukweli anataka kutenganisha mambo yaliyo tokea kutoka kwenye dhana, anaweza kufanya hivyo kwa msaada wa kutu­mia akili na mantiki katika kupata mchanganuo ulio sahihi. Utafiti wake wa kuelewa kutoka kwenye misingi isiyobadilika utampa matokeo mazuri ya uzoefu wa hali halisi.

Zainab, Rukaiya na Ummu Kulthum

Kabla Khadija hajaolewa na Muhammad Mustafa, walikuwepo wasichana watatu waliokuwa wanaishi naye nyumbani mwake mjini Makka. Majina yao yalikuwa Zainab, Rukaiya, na Ummu Kulthum. Hawa walikuwa mabinti wa marehemu dada yake. Baba yao alifariki mapema zaidi, na mama yao alipofariki, Khadija aliwachukua na kuan­za kuishi nao nyumbani kwake.

Baada ya kuolewa Khadija, wasichana wote watatu waliendelea kuwa naye kama wasaidizi wake . Inawezekana walimwita Khadija mama yao na Muhammad Mustafa baba yao. Na kufuatana na mila za Kiarabu, walijulikana kama watoto (mabinti) wake kwa sababu waliishi nyumbani mwake, na alikuwa mlezi wao kisheria.
Zainab alikuwa ndiye mkubwa kwa umri kuzidi wengine. Aliolewa na mtu aliyeitwa Abul-As bin er-Rabi. Mnamo mwaka wa 624 A.D alikuja na jeshi la wapagani wa Makka na alipigana na jeshi la Muhammad Mustafa kwenye vita vya Badr. Alikamatwa kama mateka lakini ali­fidia uhuru wake, na alirudi Makka, baadaye, alisilimu.

Wasichana wengine wawili - Rukayya na Ummu- Kulthum waliolewa na Utba na Utayba watoto wa Abu Lahab na Umm Jamil. Wasichana wote watatu waliolewa kabla ya kutangazwa Uislamu, waume wao wote watatu, kwa hiyo, walikuwa waabudu masanamu.

Baaada ya kutangazwa kwa Uislamu, Abu Lahab na mke wake, Umm Jameil, wote walikuwa maadui wakubwa wa Uislamu, wakafanywa kuwa viumbe walio laaniwa katika sura ya 111 ya Qur'an Majd. Hali hii ilichochea hasira zao na waliwamuru watoto wao - Utba na Utayba kuwataliki wake zao na kuwarudisha kwao. Wasichana wote wawili-Rukayya na Ummu Kulthum walipewa talaka, na walirudi nyumbani kwa Khadija.

Baada ya muda, Rukayya aliolewa na Uthman bin Affan mtu wa ukoo wa Ummayya wa kabila la Quraysh, na miaka mingi baadaye alikuwa Khalifa wa Waislamu. Alikufa mwaka 624 A.D. huko Madina. Baada ya kifo chake, dada yake Ummu Kulthum, naye pia aliolewa na Uthman bin Affan.

Muhammad Huseyn Haykal

Muhammad aliwaoza Rukayya na Ummu Kulthum kwa Utba, na Utaybah, watoto wa ami yake, Abu Lahab. Ndoa hizi hazikudumu, kwa sababu mara tu baada ya kutangazwa kwa Uislaumu, Abu Lahab ali­waamuru watoto wake wawili wawataliki wake zao. Uthman ndie aliye­waoa baadaye mmoja baada ya mwengine.

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Wanahistoria wa Umayya "walitiwa moyo" na Muawiya bin Abu Sufyan, mwasisi wa ukoo wa Ummaya, na warithi wake, walidai kwam­ba Rukayya na Umm Kulthum walikuwa watoto wa Muhammad na Khadija. Hawa mabinti walipoolewa na Uthman aliyetoka ukoo wa Umayya walimwita Dhun-Nurayn, yaani, "mwenye nuru mbili," Rukayya na Umm- Kulthum. Lakini kipindi kifupi kabla ya hapo, "nuru" zote hizi mbili zilikuwa za waabudu masanamu wawili wa Makka. Kila mmoja wa hawa waabudu masanaumu, kwa hiyo, alikuwa mmiliki wa "nuru" moja ambayo baadaye ilikwenda kwa Uthuman. Hata hivyo, "nuru" hiyo au hizo zilibakia hivyo bila mabadi­liko, isipokuwa ni umilikaji tu ndio uliobadilika.

Je, mabinti hawa walikuwa watoto wa Muhammad Mustafa na Khadija kama wasemavyo wanahistoria mamluki? Jibu la swal hili litafutwe (A) katika Qur'an Majid na (B) ushahidi wa historia. Jibu lake litolewalo hapa chini, ni la dhahiri:

A. Ushahidi wa Qur'an Majid

Kama nuru ya mwongozo wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu ina maana yoyote kwa Waislamu, basi hawa mabinti watatu: Zaynab, Rukayya na Umm Kulthum hawakuwa, na hawangekuwa mabinti wa kuzaliwa na Mtume wa Mungu na Khadija. Hawa walikuwa mayatima. Uhusiano wao na Muhammad na Khadija ulikuwa kwamba waliwahi kuishi nyumbani mwao. Khadija alikuwa mlezi wa yatima ( na wajane) hata kabla ya kuoliwa.

Kama Muhammad Mustafa na Khadija wangekuwa wazazi wa hawa mabinti, watatu - Zaynab, Rukayya na Umm Kulthum- hawangewaoza kwa waabudu masanamu kama walivyo kuwa waume watatu wa mabinti hawa. Ni kweli kwamba mabinti wote watatu waliolewa kabla ya Uislamu haujatangazwa, lakini hata hivyo,

Muhammad hakuvunja amri yoyote ya Qur'an Majid, wakati wowote, kabla au baada ya kufanywa mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Muhammad Mustafa haku­fanya kosa lolote la kipagani wakati wowote maishani mwake. Na Qur'an inaeleza wazi wazi kuhusu kukatazwa kwa ndoa ya mwanamke Mwislamu na mpagani.

Amri ya kukataza ndoa ya mwanamke Mwislamu na mshirikina iliteremshwa katika Aya zifuatazo zilizomo kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu.

وَلَا تَنْكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ"{221}

"Wala msiwaoze (Wanawake wenu) kwa Wanaume washirikina mpaka waamini (Qur'an 2:221)

"(Wanawake hawa) waumini si halali kwao hao (makafiri wa kiume), wala wao (wanaume makafiri) si halali kwao" Quran 60 : 10

Zimo aya nyingine ndani ya Quran ambazo ingawaje hazisemi moja kwa moja kuhusu ndoa, zina mfanya Mwislamu asiweze kumwoza au kuwaoza mabinti zake kwa muabudu masanamu. Baadhi ya aya hizo ni:

فَلَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى الْكَافِرِينَ {89}

"Basi laana ya Mwenyezi Mungu iko juu ya makafiri hao (Qur’an 2: 89)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ{28}

"Enyi mlioamini! Hakika washirikina ni Najisi" (Qur'an 9: 28)

فَإِنَّ اللَّهَ عَدُوٌّ لِلْكَافِرِينَ {98}

"……..Mwenyezi Mungu ni adui kwa Makafiri (Quran 2:98)

Hakuna Mwislamu ambaye angekuwa mzembe kiasi hicho, hivyo kwamba, angedhani kwamba Muhammad Mustafa alivunja makatazo ya Qur'an kwa kuruhusu mabinti zake waolewe na wanaume ambao Mwenyezi Mungu amewalaani, ambao adui wao ni Yeye na ambao ni najisi.

Kwa Mwislamu, Aya za Qur'an Majid zilizonukuliwa hapo juu, zinathibitisha kikamilifu kabisa kwamba Zaynab, Rukayya na Umm Kulthum, wote watatu, wakati fulani waliolewa na waabudu masanamu, hawakuwa watoto wa Muhammad Mustafa na Khadija.

Mwislamu-yeyote - hata yule ambaye yuko pembeni au anafuata mkumbo wa Uislamu atashangaa kama atashawishiwa kumuoza binti yake au binti zake kwa muabudu masanamu au hata kwa Ban Israel au Mkristo.

Lakini Mwislamu huyo huyo na hali inanuka uvundo wa kejeli- ataamini, bila kuumwa na dhamira yake, kwamba Mtume wake mwenyewe, Muhammad Mustafa-mfafanuzi na mwenezaji wa Qur'an ­aliwaoza mabinti zake watatu kwa waabudu masanamu watatu mjini Makka.

B. Ushahidi wa Historia

Muhammad Mustafa alikuwa anawapenda sana watoto. Hasa zaidi alikuwa anawapenda watoto wa binti yake Fatima Zahra. Watoto wake Hasan na Husain walikuwa nembo za macho yake. Aliwaendekeza. Watoto hao walikuwa wanapenda kucheza na babu yao hata wakati anaongoza sala ya jamaa. Hata aliingilia kati wakati anatoa hotuba na kuanza kucheza nao kama waliingia msikitini. Walipokuwa na yeye; alisahau matatizo yote ya nchi na serikali. Walimpa furaha kubwa sana nyakati zile walipokuwa naye.

Na inaonyesha kama vile hangeweza kuwapa sifa za juu zaidi wao na mama yao. Kwa hiyo, hili ni jambo la udadisi wa kihistoria kwa nini hakuwataja Zaynab, Rukayya, na Ummu Kulthum wakati wowote ule. Wazazi huwapa watoto wao wote mapen­zi hayo hayo, na hawafanyi ubaguzi wa aina yoyote. Lakini ikiamuli­wa kwa kupitia hadithi na maandishi ya historia ya wakati huo, Mtume wala hakuwa na habari kwamba palikuwepo na wanawake watatu wait­wao Zaynab, Rukayya na Umm Kulthum wakiishi.

Kwa upande wa mjumbe wa Mwenyezi Mungu, miaka ya huko Makka baada ya kutangazwa kwa Uislamu, ilijaa hatari. Kila siku ilikuwa na hatari zake na changamoto mpya kwake. Na bado, Rukayya na Umm Kulthum kamwe hawatajwi kama walimtumikia baba yao wakati wowote ule. Kwa upande mwingine, binti yake, Fatima Zahra, alim­saidia yeye, Makka na Madina, kwenye dharura mbalimbali.
Wote wawili, Rukayya na Umm Kulthum walimzidi Fatima kwa umri. Wangelazimika kumliwaza baba yao pale alipoonewa na wapagani Mjini Makka au alipoumizwa vitani Madina. Lakini kamwe hawaku­fanya hivyo.

Ukweli uliofanywa udhihirike kwa njia zote mbili kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu na kwa mantiki ya historia, ni kwamba, Zaynab, Rukayya na Umm Kulthum hawakuwa watoto wa Muhammad Mustafa na Khadija.

Suala la umri, madai ya ndoa tatu na idadi ya watoto wa Khadija, si jambo ambalo humo imani ya Uislamu inategemea, sivyo kabisa. Lakini Mwislamu lazima awe na msimamo kuhusu ukamilifu wa histo­ria. Khadija alikuwa mfadhili mkuu wa Uislamu na Waislamu.

Kiasi angalau kidogo ambacho Waislamu wanaweza kufanya katika kuthibitisha shukurani zao kwake, si kupindisha ukweli na kusingizia mambo ya historia. Ukweli lazima ushikiliwe kwa gharama yoyote ile, ama iwape faida au iwaumize rafiki na maadui.

Mtu anaweza kuwa na yoyote ya kuonyesha utii wake kwa mashujaa wake, na kupenda kufanya hivyo kwa mashujaa, kunaweza kumshawishi kuwatukuza wao. Lakini kama yeye ni Mwislamu, lazima ajizuie kufanya hivyo kwa sababu atavuruga ukweli.

Kama akifanya, atastahili kupambana na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ambaye anasema kwenye kitabu chake:

وَلَا تَلْبِسُوا الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُوا الْحَقَّ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ {42}

"Wala msichanganye haki na batili, mkaficha haki, na hali mna­jua."(Quran 2 : 42)

وَلَا تَكْتُمُوا الشَّهَادَةَ ۚ وَمَنْ يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ ۗ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ {283}

" Wala msifiche ushahidi. Na atakayeficha basi hakika moyo wake ni wenye kuingia dhambini. Na Mwenyezi Mungu huyajua (yote) mnayoyatenda."(Qur'an 2:283)

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنْ كَتَمَ شَهَادَةً عِنْدَهُ مِنَ اللَّهِ ۗ وَمَا اللَّهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ{140}

" Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule afichaye ushahidi alio nao utokao kwa Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu si Mwenye kughafilika na hayo mnayoyafanya" (Qur'an 2: 140).

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنْزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِنْ بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ {159}

"Hakika wale wanaoficha tuliyo yateremshanazi ni hoja zetu zilizo wazi na uongozi baada ya sisi kuzibainisha kwa watu kitabuni ­hao anawalani Mwenyezi Mungu na wanawalaani (kila) wenye kulaani. (Qur'an 2: 159).

Mwenyezi Mungu amewaamuru Waislamu kuthibitisha na kuonyesha shukrani kwa kutendewa fadhili Naye.

وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ {11}

"Na neema ya mola wako isimulie (kwa kushukuru na kwa kufanya amali njema.)" (Qur'an 93: 11)

Kama Waislamu ni waaminifu katika kuonyesha shukurani zao kwa Khadija, ni lazima waharibu uwongo, yaani hadithi ya maisha yake. Uwongo huu umekuwa ukisambaa kwa muda mrefu mno. Hakuna njia bora zaidi ya Waislamu kukariri na kutangaza ukarimu wa Mola kama kuheshimu ukweli-kweli yenyewe. Kwa kuheshimu Ukweli, pia wata­fuzu kupata radhi za Mwenyezi Mungu (s.w.t)

Khadija alikuwa mtumishi aliye pendwa sana na Mwenyezi Mungu, na alikuwa mke wa kwanza wa rafiki yake na mjumbe, Muhammad Mustafa. Alikuwa wa pekee, hangeweza kulinganishwa na yeyote, na alikuwa maalum kwa Mwenyezi Mungu ambaye alipeleka salaamu zake kwake kupitia kwa malaika mkuu Jibril!
Mwenyezi Mungu na amridhie Mtumishi wake, Khadija.
Aya zifuatazo za Qur'an Majid zimeelekezwa kwa watumishi wa Mwenyezi Mungu waaminifu na wapenzi, ambao hutanguliza radhi Zake kabla ya zao. Na wote ambao hutafuta radhi Zake katika kujitoa kumtumikia Yeye na Uumbaji Wake.

Khadija alikuwa mmoja wa wale waliokuwa mstari wa mbele kabisa miongoni mwa watumishi wa Mwenyezi Mungu. (Kwa nafsi ya mtu mwema itasemwa)

يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ {27}

ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَرْضِيَّةً {28}

فَادْخُلِي فِي عِبَادِي {29}

وَادْخُلِي جَنَّتِي {30}

"Ewe Nafsi yenye kutua rudi kwa mola wako, hali ya kuwa utarid­hika (kwa utakayopata), na (Mwenyezi Mungu) aridhike na wewe. Basi ingia katika (kundi la) waja wangu (wazuri), uingie katika Pepo yangu.(Qur'an 89:27-30)

Mwenyezi Mungu Amrehemu Khadija na aweze kumnyanyua na kumpa daraja la juu zaidi katika wote wenye mamlaka miongoni mwa watumishi wake wa kweli na rafiki waaninifu.

Mwenyezi Mungu na Amrehemu Muhammad Mustafa na Ahlul-Bayt. Kupitia kwake mwanadamu alipokea neema ya nuru ya Uislamu.

Kujitolea mhanga kwa Khadija katika kuutumikia Uislamu si rahisi kulinganishwa. Kujitolea huko kuliingiliana na misingi ya Uislamu. Kujitolea huko kuliimarisha umbo la Uislamu hivyo kwamba haikuwa rahisi kuuharibu.

Kujitolea kwa Khadija kumepewa sifa bora na nyingi kushinda za mtu mwengine yeyote ambaye alifanya kitu chochote kwa ajili ya Uislamu. Aliufanya Uislamu uweze kujitegemea kwa kujitolea kwake mno. Kuna uwiano wa wazi baina ya kumuunga mkono mume wake na ushindi wa Uislamu kijamii, kiuchumi na kisiasa. Hapana yeyote ambaye anaweza kuwajibika kwa ustadi, mapenzi, uthabiti, wepesi wa kuelewa na kugun­dua. Kujishughulisha, na kipaji kwa kiwango hicho alichofanya yeye.

Kujitolea kwa Khadija kulileta mafanikio mazuri baada ya kifo chake. Uislamu ulipata ushindi baada ya mapambano na upagani ya muda mrefu. Maadui wa Uislamu waliangamizwa, wakana Mungu wenye kiburi wa ukoo wa Umayya walidhalilishwa na itikadi yao ya kipagani ilivunjwa.

Khadija alikuwa miongoni mwa watu muhimu walio fanikisha imani ya kumpwekesha Mungu kushinda ushirikina, imani ya kiroho kushinda tamaa ya mali, na Uislamu kushinda upagani hata pamoja na kwamba historia ya yale aliyo yafanya wakati wa migongano, kwa kipindi kire­fu, imekuwa haifahamiki. Historia hiyo imebakia inaeleweka nje ya dhamira za Waislamu walio wengi.

Mwaka A.D. 630 Muhammad Mustafa. aliingia Makka kama mshindi. Yeye na binamu yake, Ali bin Abi Talib, waliingia ndani ya Al- Kaaba wakiwa na nembo ya Amri za Mungu alizompa Ibrahim na Ismail.

نَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ أَنْ طَهِّرَا بَيْتِيَ {125}

"……Na tulimwusia Ibrahimu na Ismaili (tukawaambia) "itakaseni Nyumba Yangu…" (Quran 2:125.)

Muhammad na Ali waliikuta Nyumba ya Mungu katika hali mbaya sana; ilikwisha kuwa nyumba ya masanamu; kwa hiyo, ilibidi itakaswe. Kwa hiyo, kwa kuwaiga Ibrahim na Ismaeli - mitume waliotangulia ­Muhammad na Ali waliyavunja masanamu yote na kuharibu mapicha yote ndani ya Al-Kaaba. Waliitakasa nyumba ya Mungu na wakarudisha utakatifu humo.

Khadija angelilinganisha tendo hili la kurejesha utakat­ifu kwenye Kaaba, lililofanywa na mumewe na mkwe wake, kwa kutimia kwa matumaini na ndoto zake, na angefurahi na kujivuna.

Na ni kiasi gani Muhammad Mustafa alilazimika kuhisi kwamba mke wake angekuwa naye, akiwa amesimama karibu naye, akaona na kushiriki kupata msisimko wa siku hiyo iliyoneemeshwa ambapo Al-Kaaba ilire­jeshwa kwenye wakfu wa matumizi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, baada ya kupita karne nyingi ikiwa mikononi mwa wasioamini.

Tangu wakati Khadija aliposhahadia kwamba Mungu ni Mmoja, na Muhammad alikuwa Mjumbe Wake, aliyaweka maneno, matendo, maisha na kifo chake katika usawa wa mwelekeo mmoja kuafikiana na Radhi na utashi wa Mwenyezi Mungu, alipata Ushindi wa Juu Kabisa wa utakatifu wa maisha yake.

Back cover Khadija-tul-Kubra

Khadija alikuwa mke wa kwanza wa Mtume Mkubwa wa mwisho wa Mungu kwa wanadamu wote - Muhammad Mustafa (saww). Wakati Mtukufu Mtume alipoanzisha harakati itwayo Uislamu, alijipatia sifa ya kuwa Mu'umin na Mwislamu wa kwanza.

Maisha ya Khadija yamejaa utajiri wa mwongozo wa kimungu. Sifa yake kubwa katika maisha yake ya kiutakatifu, ilikuwa ni imani yake isiyo na kifani katika Uislamu. Imani yake ilikuwa kama jabali katika bahari iliyochafuka.

Imani za watu wachache kamwe hazikuwekwa katika mtihani mkali kama ile imani ya Khadija. Imani yake ilijaribiwa kwa njaa, kiu, uhamisho na hatari kubwa katika maisha yake na kwa wapendwa wake. Kusema kweli, wakati wa kwanza wa mika kumi ya Uislamu, maisha yake yalikuwa ya mfululizo wa mitihani isiyo na mwisho.

Khadija alifuzu katika mitihani yote. Ufunguo kwenye mafanikio yake ilikuwa ni upendo wake kwa Mungu, mapenzi kwa mume wake na kuji­tuma kwake ili kuufanya Uislamu ufanikiwe.

Khadija aliweka mfano ambao wanawake katika Uislamu wanaweza kuuiga mpka mwisho wa dunia. Wanawake wanweza kuona katika maisha yake vipi mu'mun wa kweli anavyoweza kufanya tabia ya maisha yake kuwa bora sana na ya utukufu.

MWENYEZI MUNGU AMBARIKI KHADIJA NA FAMILIA YAKE