Abu Dharr

Author(s): 
Publisher(s): 

Kitabu hiki kinahusu maisha ya sahaba mkubwa na mashuhuri; Abudhar (Jundab bin Junadah). Abudhar alikuwa mtu wa tano kuingia kwenya uislamu na upanga wake ulikuwa unafaa sana katika kuendeleza uislamu. Aliona mikengeuko mingi katika Uislamu tangu kuanza kwake, na baada ya kifo cha Mtukufu Mtume mambo hayakuwa mazuri.

Alishuhudia mitafaruku mingi wakati wa makhalifa watatu wa mwanzo kiasi kwamba hakuweza kuvumilia, na alianza kukemea maovu yanayofanywa na makhalifa wazi wazi na kwa ujasiri mkubwa sana mpaka ikafikia Khalifa wa tatu kuchukua hatua za kumhamisha na kumpeleka jangwani ambako aliishi maisha ya dhiki mpaka kifo kikamkuta huko.

Kwa bahati mbaya sana wanahistoria wengi wa Kiislamu na wasio wa Kiislamu hawakuzungumza habari zake kwa kina na kama inavyostahiki kuwa. Kwa hakika Abu Dharr pamoja na Masahaba wengine kama vile Amar bin Yasir, Mikidadi, Salman Farsy, halikadhalika na ami yake Mtukufu Mtume, mzee Abu Twalib na mke wa Mtume Bibi Khadija, alikuwa ni madhulumu wa historia.

Translator(s): 
Category: 
Topic Tags: 
Person Tags: 

Neno La Mchapishaji

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la: “Abu Dharr”

Kitabu hiki kinahusu maisha ya Sahaba mkubwa na mashuhuri; Abu Dharr (Jundab bin Junadah). Abu Dharr alikuwa mtu wa tano kuingia kwenye Uislamu na upanga wake ulikuwa unafaa sana katika kuendeleza Uislamu. Aliona mikengeuko mingi katika Uislamu tangu kuanza kwake, na baada ya kifo cha Mtukufu Mtume mambo hayakuwa mazuri.

Alishuhudia mitafaruku mingi wakati wa makhalifa watatu wa mwanzo kiasi kwamba hakuweza kuvumilia, na alianza kukemea maovu yanayofanywa na makhalifa wazi wazi na kwa ujasiri mkubwa sana mpaka ikafikia Khalifa wa tatu kuchukua hatua za kumhamisha na kumpeleka jangwani ambako aliishi maisha ya dhiki mpaka kifo kikamkuta huko.

Kwa bahati mbaya sana wanahistoria wengi wa Kiislamu na wasio wa Kiislamu hawakuzungumza habari zake kwa kina na kama inavyostahiki kuwa.

Kwa hakika Abu Dharr pamoja na Masahaba wengine kama vile Amar bin Yasir, Mikidadi, Salman Farsy, halikadhalika na ami yake Mtukufu Mtume, mzee Abu Twalib na mke wa Mtume Bibi Khadija, alikuwa ni madhulumu wa historia.

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu.

Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa luhga ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

Tunamshukuru ndugu yetu, Salman Shou kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu katika dini.

Mchapishaji:
Al-Itrah Foundation
S. L. P. 19701
Dar-es-Salaam.

Kuhusu Wachapishaji

Leo hii akili yenye hadhari inaona kiakili mabadiliko ya maisha ya mwanadamu. Sayansi na teknolojia na mafanikio yao ya kushangaza yanaonekana yamefika kwenye kilele chao. Mahitaji ya kidunia hisia kali za matamanio ya mamlaka na ukubwa, ni mambo ambayo yamemwelekeza mwanadamu kwenye muflisi wa maadili mema.

Katika hali hii ya kukatisha tamaa, mtu analazimika kutulia na kukadiria upya hatari zinazoweza kuwa tishio kwa mwanadamu kwa ujumla. Mwanadamu kwa mara nyingine tena ameelekeza macho yake kwa Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu kwani sasa ametambua kwamba ufumbuzi wa matatizo yake na hatima ya ukombozi wake ni mambo yaliyomo katika kufuata na kutekeleza.

Kuhama huku kutoka kwenye fikra ya mambo ya kidunia na kwenda kwenye mambo ya kiroho ni hali inayoafikiana kikamilifu na malengo na madhumuni ya seminari ya Kiislamu.

Miongozo ya kidini, iliyo sambamba na maendeleo ya wakati uliopo, yanatoa kimbilio linalohi- tajiwa sana na akili inayosumbuliwa na yenye wasi wasi. ni matokeo ya ongezeko la utambuzi, kwamba imeeleweka kwamba siri ya kuishi maisha ya uadilifu hapa duniani kuelekeza kwenye furaha kamili ya milele ya maisha ya Peponi. Huu ni ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu wote.

Jumuiya yetu ya Kiislamu inataka kunyanyua juu mwenge wa mwongozo wa kiroho na kusaidia kwa moyo wote kutangaza urithi wa kiroho wa mwanadamu. Inaonyesha njia ya maisha kwa mujibu wa Quran katika utukufu wake ulio safi kabisa. Inaonyesha hayo tu yenye mamlaka na yaliyothabiti. Uenezi wake umebuniwa kwa jinsi inayoweza kukidhi mahitaji ya kiroho katika wakati uliopo.

Itahudumia kama chemchem ya kudumu kwa wale wenye kiu ya ujuzi. Seminari ya Kiislamu ni taasisi ya kimataifa ambayo inajaribu kuleta udugu wa Kislamu. Inapata mchango mzuri sana kutoka kwa wanachuo, kama nyongeza ya kuwa na msaada wa kimataifa kwa ajili ya kutimiza lengo lake kubwa. Inayo vituo; Asia, Afrika, Ulaya, Amerika, Canada na Mashariki ya mbali.

Mpendwa msomaji.

Kitabu hiki kimechapishwa na Seminari ya Kiislamu. Uenezi wake umebuniwa kwa ajili ya kuhudumia mahitaji ya kiroho katika kipindi hiki ukiwa na msisitizo mahsusi kusafisha akili na fikra ya Muislamu.
Juhudi kubwa sana zimefanywa na Seminari kuweka katika machapisho yake yale ambayo yanaaminika na thabiti kweli katika Uislamu.

Unaombwa kwa ukarimu kukisoma kitabu hiki kwa moyo ambao umekusudiwa. Pia unaombwa uwe huru kuwasilisha kwetu maoni yako ambayo yatathaminiwa sana kuhusu uenezi wetu.

Kutangaza ujumbe wa Uislamu ni kazi inayotaka ushirikiano wa watu wote. Seminari inakukaribisha katika kazi hii ikikubaliana kwa furaha na Aya ya Quran Tukufu.

قُلْ إِنَّمَا أَعِظُكُمْ بِوَاحِدَةٍ ۖ أَنْ تَقُومُوا لِلَّهِ مَثْنَىٰ وَفُرَادَىٰ{46}

“Sema; Mimi ninakunasihini kwa jambo moja tu ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili wawili na mmoja mmoja.” (34:46).

Mwenyezi Mungu na akurehemu.
Wako katikaUislamu.

Utangulizi

Baada ya miaka kumi na tatu ya mfululizo wa mateso na mapambano, Mtume wa Uislamu aliondoka Makkah na kwenda Madina. Alihisi kwamba kipindi cha uvunjaji sheria na kutangazwa kwa siri kwa Uislamu kilikwisha na kwa msaada wa masahaba wake waaminifu na jasiri angeweza kujenga jumba kubwa la dola ya Kiislamu na kuweka msingi wa serikali ya kisiyasa kama anavyotaka Mwenyezi Mungu.

Mara tu baada ya kufika Madina, Mtukufu Mtume alijenga msikiti hapo. Alijenga nyumba yake iliyotazamana na msikiti, na alifanya mlango wake wa kuingia moja kwa moja msikitini. Hapakuwepo na mabadiliko ya maisha yake tangu mwanzo hadi mwisho. Tabia, mwenendo na maadili mema yalikuwa hivyo hata baada ya kuanzisha serikali ya Kiislamu katika Arabia yote.

Mfumo wa utawala mpya na dola mpya vilitokeza na kuanza kuwepo katikati ya dola mbili za wakati huo. Kwenye Serikali hii ya Kiislamu hapakuwepo na mtawala na mtawaliwa, hapakuwepo afisa na wa chini yake, na hapakuwepo na bwana na mtumwa. Wote walikuwa sawa mbele ya Mwenyezi Mungu.

Mwasisi wa mfumo huu mpaya wa utawala alitawafu na baada ya kunyang’anywa Ali urithi na kuundwa kwa vikundi vya kisiasa, mkengeuko wa kwanza ambao ulitikisa msingi wa Kiislamu ulitokeza kwenye jambo la Ukhalifa.

Mmojawapo wa masahaba waaminifu sana na jasiri sana wa Mtukufu Mtume alikuwa Abu Dharr. Alikuwa mtu wa tano kuingia kwenye Uislamu na upanga wake ulikuwa unafaa sana katika kuendeleza Uislamu. Aliona mikengeuko yote hii. Ali ambaye alikuwa mfano halisi wa wema na ukweli, alilazimika kuishi maisha ya upweke.

Maadui wa Uislamu waliopo na kwenye mfumo wa Ukhalifa na walikuwa wanauharibu Uislamu kwama mchwa. Abu Dharr alisumbuliwa sana na kushtuka na aliona kwamba hali ya Uislamu ya siku za usoni ilikuwa ya wasi wasi na kuogopesha. Hata hivyo pia aliona kwamba kwa hali yoyote ile msafara wa Uislamu ulikuwa unaendelea kwenye njia yake, ingawa haki haikutendeka. Kwa hivyo, ingawa alihuzunika na kufadhaika, alinyamaza kimya!
Mfumo wa utawala wa Uthman ulipopata uwezo kamili, haki za wafanya kazi na Waislamu wasio jiweza zilikiuka. Wala riba, wanao shughulika na watumwa, matajiri na makabaila, ambao walifika kwenye baraza la Uthman na Muawiyah.

Tofauti za matabaka na kuhodhi utajiri ni tabia zilizoanzishwa tena, na Uislamu uliotishiwa na hatari kubwa. Njia na tabia za Mtukufu Mtume ziliachwa. Maelfu ya dinari zilitumika kujenga Ikulu ya Muawiyah iliyoitwa (Green Palace) ya mtawala wa Kiislamu na utaratibu wa mabaraza ya Kifalme ulianzishwa. Umari aliendesha maisha yake kama mtu wa kawaida na Abu Bakr naye aliishi hivyo hivyo, ili kuendesha maisha yake, alikuwa anafanya kazi ya kukamua mbuzi wa Myahudi ambapo kidani cha mke wa Uthman, Khalifa wa tatu kiligharimu thuluthi moja (1/3) ya pato pote lililoletwa kutoka Afrika.

Akichukua nafuu isiyostahili ya kazi anayofanya baba yake, mtoto wa kiume wa mmojawapo wa maofisa wa ngazi ya juu sana katika utawala wa Umari alichukua farasi wa mtu kwa lazima. Kwa upande mwingine Uthman alimteua Marwan bin Hakam kama mshauri wake mtu ambaye alipewa adhabu ya uhamisho na Mtukufu Mtume na akampa zawadi ya kiunga cha Kheybar pamoja na malipo kutoka Afrika!

Abu Dharr alipochunguza shughuli hizi za kuaibisha hakuweza kuvumilia yote haya, aliamua kufanya upinzani dhidi ya mfumo huo wa kidikteta. Yalikuwa maasi ya kijasiri na ukakamavu ambayo yalisababisha Waislamu kufanya uasi dhidi ya Uthman; mawimbi yake yanayo rindima bado yanaweza kuonekana kwenye jamii nyingi za binadamu.

Abu Dharr alikuwa na shauku ya kuanzisha mfumo wa maadili ya Kiislamu, ambapo utawala wa Uthman ulikuwa unakiuka kwa kuhuisha utawala wa kitabaka. Abu Dharr aliona Uislamu kuwa ndio kimbilio la wasiojiweza, na mafakiri waliokuwa wanakandamizwa, na Uthman aliufanya utawala wake kuwa njia ya kuwafadhili jamii ya watu wakuu na wala riba. Ugomvi huu baina ya Abu Dharr na Uthman uliendelea, hatimayeAbu Dharr alipoteza maisha yake kwa sababu hii.

Abu Dharr alimtambua Mwenyezi Mungu Mweza wa yote; kwa hiyo kamwe hakutetereka katika njia Yake hata kwa nukta moja. Aligeuka kuwa mtu bora katika kundi la Uislamu na ndio jambo ambalo linatosha kuonyesha umashuhuri wake.

Abu Dharr ni mmojawapo wa wale viongozi na wakombozi wa uhuru mwanadamu anautaka leo hii. Hususan kwa vile utaratibu wa muda umefanyiza hali ya wasiwasi mkubwa katika ulimwengu wa uchumi na matatizo ya kiuchumi yanashughulikiwa kuwa ndio matatizo ya msingi zaidi ya maisha. Hali hiyo hiyo ya Syria na Madina kwa kuwakusanya wasiojiweza na kuwashawishi waasi dhidi ya wala riba na wanaohodhi utajiri, pia leo hii imejitokeza.

Waislamu hapa duniani wanakumbuka maneno yake ya kuvutia, maoni sahihi na hotuba kali. Inawezekana kwamba wanaweza kuona kwenye sehemu za mbali sana historia kwamba amewakusanya wanaokandamizwa na wasiojiweza kwenye msikiti na ana chokonowa hisia zao dhidi ya wale waishio kwenye ikulu na utaratibu mchafu wa Uthman na kutangaza hadharani:

وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَبَشِّرْهُمْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ{34}

“Watu hao wanao hodhi dhahabu na fedha na hawatumii katika njia ya Mwenyezi Mungu, wanapaswa kujua kwamba adhabu yao itakuwa mateso makali.” (Quran 9:34).

“Ewe Muawiyah! Endapo unajenga Ikulu hii kwa fedha yako mwenyewe ni ubadhilifu, na kama unajenga kwa kutumia hazina ya taifa, huko ni kuitwalia.”

“Ewe Uthman! Masikini wamekuwa masikini zaidi na matajiri wamekuwa matajiri zaidi. Yote haya yanasababishwa na wewe.”

Wachapishaji

Sura Ya Kwanza

Abu Dharr alikuwa mmojawapo wa hao masahaba wa Mtume wa Uislamu, Muhammad (s.aw.) ambao walikuwa wachaji Mungu na wapenda uhuru na walikuwa na tabia bora kwa mujibu wa maneno ya Mtukufu, Mtume: Pepo na wakazi wake wanawangojea kwa hamu. Alifaidika kuwa na Mtume katima uhalisi wake.

Abu Dharr mwenyewe anasema, “Jina langu halisi ni Jundab bin Junadah, lakini baada ya kuingia kwenye Uislamu, Mtume alinipatia jina la ‘Abdullah’ na hili ndilo jina ninalolipenda hasa.”

Abu Dharr ilikuwa Kuniyah yake (kutokana na mtoto wake wa kwanza aliyeitwa Dhar). Wanavyuoni wanakubaliana kwamba Abu Dharr alikuwa mtoto wa kiume wa Junadah bin Qays bin Saghir bin Hazam bin Ghafir na mama yake alikuwa Ramlah binti Wafiah Ghifariah. Alikuwa wa jamii ya Kiarabu na alikuwa wa kabila la Ghifar. Ndio sababu ya neno Ghifar; limeandikwa na jina lake.

Abdullah al-Subaiti ameandika, “Tunapoangalia wasifu wa Abu Dharr inaonekana kama vile ni nuru iliyopewa umbo la Binadamu. Alikuwa mfano halisi wa sifa za mtu mashuhuri. Alikuwa na sifa pekee ya akili, uelewa, busara na werevu.” Kwa maneno ya Imamu Jafar Sadiq: “Wakati wote alikuwa katika tafakuri na Swala zake ziliegemezwa kwenye mawazo kuhusu Mungu.” (Sahih Muslim).

Mwandishi maarufu wa Misri Abdul Hamid Jaudatus Sahar, kwenye kitabu ‘Al-Ishtiraki az-Zahid, ameandika: Wakati fulani ilitokea njaa kali. Watemi wa kabila la Ghifar walikusanyika kwa ajili ya kushauriana ili wapate ufumbuzi wa tatizo hilo kwa sababu ya ukame wa muda mrefu. Kwa hiyo hicho kilikuwa kipindi cha mateso makubwa. Wanyama walikonda na akiba kwenye maghala ilikwisha. Waliambizana wao kwa wao, ‘Hatujui kwa nini Mungu wetu (sanamu Manat) amekasirishwa na nini kutoka kwetu, ingawa tumeomba mvua, tumetoa sadaka ya ngamia na tumefanya kila linalowezekana ili atupendelee.

Msimu wa mvua sasa umekwisha. Hakuna hata dalili ya wingu angani. Hapajatokea mngurumo na rasha rasha ya mvua kipindi hiki, hakuna hata tone la mvua au manyunyu. Unafikiria nini? Tumekuwa wapotevu hivyo kwamba ghadhabu ya mungu wetu imetuangukia? Kwa nini ahisi amekosewa na sisi ambapo tumetoa sadaka nyingi kwa ajili ya kumfurahisha yeye?”

Watu walianza kutafakari juu ya jambo hili na kubadilishana mawazo. ‘Binadamu hawezi kuingilia mipango ya Mbinguni. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuleta mawingu ya mvua kutoka angani. Anayeweza kufanya hivyo ni ‘Manat’ tu. Kwa hiyo hatuna njia nyingine isipokuwa sisi, wanaume na wanawake, twende Hija huku tunalia kwa huzuni na kusali na kumwombea kwa huzuni na kusali na kumwomba Manat atusamehe.

Labda inawezekana akatusamehe na mvua ikaanza kunyesha na kuifanya ardhi kuwa kijani kibichi baada ya ukame, ili umasikini wetu ubadilike kuwa mafanikio, uchungu kuwa furaha na matatizo kuwa raha na starehe.”

Kwa hiyo, kabila lote lilianza matayarisho ya safari ya kwenda kumuona Manat. Wale waliokuwa wamelala waliamka na kuweza kuweka mito ya kukalia juu ya migongo ya ngamia wao. Unais (ndugu yake Abu Dharr) naye pia alipanda ngamia wake na kumwendesha, ili aungane na msafara, karibu na Pwani ya bahari, Mushalsal na Qadid sehemu zilizomo kati ya Makkah na Madina, ambapo ndipo Manat alipo.

Unais alitazama huku na kule lakini hakumuona kaka yake. Alimbembeleza ngamia akakaa chini. alikimbia kuelekea nyumbani. Aliingia ndani huku akiita ‘Jundab! Jundab! alipoona kwamba Jundab alikuwa amelala kitandani pake kwa raha mstarehe, alisema: Unais: “Hukusikia ‘wito’ wa kwenda safarini”

Jundab: “Ndio, nilisikia. Lakini nifanye nini ambapo ninahisi kuchoka na pia sitaki kwenda kwenye Hija ya Manat.”

Unais: “Nyamaza! Mwombe mungu akuhurumie. Huogopi kwamba endapo mungu atakusikia anaweza kukutesa.”

Jundab: “Wewe unaridhika kwamba Manat hutusikia sauti zetu na hutuona?”

Unais: “Nini kimekutokea leo? Kuna jinni lolote limekuzidi nguvu, au umeugua ugonjwa? Njoo jisikitikie. Labda Manat anaweza akakubali toba yako.”

Abu Dharr alipoanza kujibiringisha kitandani mwake, kaka yake alisema, “Amka msafara umekwisha ondoka na kabila linakwenda huko.”

Hawa ndugu wawili walikuwa wanaendelea na mazungumzo ambapo mama yao aliwasili hapo na walinyamaza.

Mama: “Wanangu! Nini maoni yenu?”
Unais: Kuhusu nini mama?”
Mama: “Kuhusu mvua.”
Unais: “Tunakubaliana na pendekezo lako.”
Mama: “Ninapendekeza twende kwa mjomba wenu (kaka yake mama yao Abu Dharr na Unais) ambaye ni tajiri.”
Unais: “Sawa! Tutafanya upendavyo. Mungu na aifanye hali yetu kuwa nzuri zaidi.”

Abu Dharr, Unais na mama yao walikwenda nyumbani kwa mjomba wao. Mjomba wao aliwakaribisha kwa ukarimu mkubwa. Waliishi hapo kwa muda mrefu. Matatizo yao yaligeuka kuwa raha ma machungu yao yakawa starehe. Watu wa kabila lao walipoona kwamba mjomba wao alikuwa mtu mwema kwa Abu Dharr na Unais na aliwapenda kama watoto wake mwenyewe, waliwaonea wivu na walianza kufikiria mipango ya kumfanya awadharau. Waliendelea kufikiria na kushauriana wao kwa wao, hadi hatimaye waliamua kutumia hila na walimchagua mtu kutekeleza njama yao.

Mtu huyo alikwenda nyumbani kwa mjomba wake Abu Dharr na akaketi chini, akiwa kimya na ameinama. Mjomba wake Abu Dharr alimuuliza huyo, ‘Ndio, waonaje hali?”

Mtu huyo alionekana na huzuni sana na alisema, Nimekuja kwako kwa shughuli muhimu! kama ingelikuwa kwa sababu ya kukupenda na kukuheshimu wewe nisingekwambia, lolote.

Lakini uaminifu wangu umenilazimisha kufanya hivi. Nataka kufichua jambo usilolijua, ili uone nini kinachoendelea kwa sababu ninaona kwamba upendeleo wako unaelekezwa mahali pasipofaa!”

Mjomba wake Abu Dharr alihisi kuna jambo lenye maudhi limetokea. Alihuzunika, sana na akasema, “Sema usifiche.” Mtu huyo alisema: “Nitakwambiaje kwamba unapotoka nje ya makazi yako, mpwa wako Unais, hukaa na mkeo na kuzungumza naye kwa siri sijui huzungumza nini naye?”

Mjomba wake Unais alisema, “Haya ni mashtaka ya uongo dhidi yake, na siwezi kuamini kwa jinsi yoyote ile!” Alijibu: “Sisi pia tulidhani kwamba ni uongo. Lakini ninajuta kusema kwamba ni kweli.”

Alimwambia atoe ushahidi. Mtu huyo alimwambia, “Kabila lote linaweza kutoa ushahidi kuhusu jambo hili. Wote wamemuona na wanazo hisia kama zako. Kama unataka ninaweza kuleta mashahidi wasio hesabika kutoka kwenye kabila langu.”

Aliposikia hivyo mjomba wake Unais alianza kufikiria heshima na hadhi yake. Alihisi heshima yake binafsi ilichafuliwa. Mtu huyo alitoka nje ya nyumba alipoona ametimiza kazi yake.

Mjomba wake Unais aliridhika kwamba taarifa aliyopewa ilikuwa kweli. Alifanya kila jitihada kupata utulivu wa kiakili, lakini alishindwa. Alisikitika sana na alihisi uchungu mkali na mateso moyoni mwake na kila siku. Wakati wowote ambapo wapwa zake walipofika mbele yake aligeuzia uso wake upande mwingine. Ukimya ulienea ndani ya nyumba yote.

Abu Dharr alipoona dalili ya huzuni kwenye uso wa mjomba wake, aliamua kumuuliza, “Mpendwa mjomba! Nini Kimekusibu? Nimekuwa nikichunguza mabadiliko ya hali yako kwa muda wa siku kadhaa sasa. Unatusemesha mara chache sana na muda mwingi unakuwa na mawazo mengi na kufadhaika.”

Mjomba wake alimjibu, “Hakuna tatizo lolote.” Abu Dharr akasema, “Hapana, hakika ipo sababu ya hali hii. Tafadhali niambie. Labda ninaweza kukufariji kuhusu huo wasi wasi wako au ninaweza kuwa pamoja na wewe kuhusu baadhi ya matatizo yako.”

Akasema, “Siwezi kueleza jambo ambalo watu wa kabila langu wamenieleza.”

Abu Dharr akasema; “Tafadhali nijulishe. Watu wa kabila lako wamekwambia nini?” Mjomba wake alijibu, “Wamesema kwamba, Unais huzungumza na mke wangu kwa siri wakati mimi sipo.”

Aliposikia hivi Abu Dharr aligeuka rangi na kuwa nyekundu iliyoiva kwa hasira na akasema, “Umeharibu msaada wako wote uliotupatia. Sasa tunaondoka, na hatutakuona tena!”

Hatimaye waliondoka hapo na walikwenda sehemu iitwayo ‘Batu Mari’, karibu na Makkah. Hapa ndipo Abu Dharr alipopata kujua kwamba Mtume alitokea huko Makkah.

Alipata shauku ya kutaka kujua kuhusu taarifa hii. Haraka sana alimwita kaka yake Unais na akamuomba aende Makkah na afanye utafiti wa habari kamili kuhusu Mtume.

Unais alikuwa hajaondoka kwenda Makkah, ambapo mtu alionekana anawasili hapo kutoka huko, na alikwenda moja kwa moja kuungana na watu wa nyumba ya Abu Dharr. Abu Dharr alimuuliza, “Unatoka wapi?” Akajibu; “Nimekuja kutokea Makkah?”

Abu Dharr aliuliza, “Hali ya huko ikoje?”
Akajibu, “Yupo mtu anayesema kwamba yeye ni Mtume na hupata ufunuo kutoka mbinguni.” Abu Dharr akasema; “Watu wa Makkah walimfanya nini?”

Mtu huyo akasema; “Walimkadhibisha, walimtesa, na waliwazuia watu wasiende kwake. Humtishia na kumuogopesha yeyote anayekwenda kumuona.”

Abu Dharr akauliza; “Kwa nini watu hawamwamini?” Watamwaminije, alisema mtu huyo, ambaye huwatukana miungu wao, huwaambia wapumbavu na wahenga wao wapotevu.”
Abu Dharr alisema; “Ni kweli kwamba husema hivyo? Ndio, husema hivyo kwamba Mungu ni Mmoja. Ona sasa! Sio jambo la kushangaza hili?” alisema mtu huyo.

Abu Dharr alianza kufikiria mtu aliyesema Mungu ni Mmoja. Aliendelea kufikiria kimya kimya kwa kipindi kirefu. Mtu huyo mgeni alimtazama na akamuona anayo mawazo mengi akamuaga akaondoka.

Baada ya kuondoka mtu huyo Abu Dharr alimwambia ndugu yake Unais, “Nenda Makkah na ufanye utafiti wa habari kamili za mtu huyu. Anasema kwamba hupokea ufunuo kutoka mbinguni! Uongeaji wake ukoje? Angalia kama kuna ukweli katika mazungumzo yake au hapana.”

Unais aliondoka kwenda safari ya kuelekea Makkah. Baada ya kupita vituo mbali mbali alifika Makkah na akaenda Ka’abah na kuzunguka. Alipotoka hapo, aliona kundi la watu. Alimuuliza mtu aliyekuwa anakuja mbele yake, “Kuna nini kinachofanyika hapo?” Akajibu, “Mwasi anawaita watu waende kwenye imani mpya!”

Mara tu Unais aliposikia hivyo, alikimbia kwenda huko. Alipofika hapo, alimuona mtu anasema, “Sifa zote zinastahiki kwake Mwenyezi Mungu. Ninamsifu Yeye na ninahitaji msaada Wake. Ninamwamini Yeye, ninamtegemea Yeye na ninashahidilia kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu na Hana mshirika.”

Katika nukuu ya Subaiti, Unais alimsikia mtu huyo akitangaza, “Enyi watu! Nimekuleteeni neema ya dunia hii na baada ya maisha haya. Semeni kwamba hapana mungu isipokuwa Allah ili muweze kupata ukombozi. Mimi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na nimekuja kwenu. Ninawaonya kuhusu adhabu ya siku ya Hukumu. Kumbukeni kwamba hakuna mtu atakayepata kuokolewa isipokuwa yule anayekuja mbele ya Mwenyezi Mungu kwa moyo wa unyenyekevu.

“Wala utajiri hautakuwa na manufaa kwake, wala watoto hawatawasaidieni. Mwogopeni Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atakuwa mwema kwenu. Enyi watu! Nisikilizeni!

Ninasema wazi kabisa kwamba mababu zetu walifanya upotovu kwa kuacha njia iliyonyooka na kuanza kuabudu masanamu haya na nyinyi mnafuata nyayo zao.

Kumbukeni kwamba masanamu wala hayawezi kuwaumizeni ama kuwanufaisheni. Wala hayawezi kuwazuieni ama kuwaongozeni.”

Unais aliposikia hotuba hii yenye ushawishi mkubwa alishangaa. Lakini katika kustajabu kwake aliona kwamba watu walikuwa wanasema mambo tofauti dhidi yake.

Aliposikia Mtume alisema, “Mitume hawasemi uongo. Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu mbali na Yeye, kwamba nimetumwa kwenu kama mjumbe. Kwa jina la Mwenyezi Mungu mtakufa kama mnavyolala na mtafufuka kama mnavyoamka. Mtaitwa kuhesabiwa matendo yenu. Halafu mtapewa Pepo au Jahanamu ya milele!”

Aliposema hivi watu walimuuliza Mtume, watafufukaje baada ya kuwa vumbi?

Wakati huu huu Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya zifuatazo:

قُلْ كُونُوا حِجَارَةً أَوْ حَدِيدًا {50} أَوْ خَلْقًا مِمَّا يَكْبُرُ فِي صُدُورِكُمْ ۚ فَسَيَقُولُونَ مَنْ يُعِيدُنَا ۖ قُلِ الَّذِي فَطَرَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ فَسَيُنْغِضُونَ إِلَيْكَ رُءُوسَهُمْ وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هُوَ ۖ قُلْ عَسَىٰ أَنْ يَكُونَ قَرِيبًا {51}

“Sema: Kuweni hata mawe, na chuma. au umbo lolote mnaloliona kubwa katika vifua. Watasema: Nani atakayeturudisha tena? Sema: Yule aliye kuumbeni mara ya kwanza! Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Lini hayo? Sema: Asaa akawa karibu!” (17:50-51).

Mara tu Mtume alipomaliza hotuba yake watu walinyanyuka. Wakati walipokuwa wanasambaa, mmoja wao alisema: “Huyu ni mtabiri?” Mwingine akasema, “Huyu ni mchawi.”

Unais alimsikiliza Mtume na watu. Aliinamisha kichwa chake kwa muda fulani na akanong’ona: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu maneno yake ni matamu. Hayo aliyoyasema ni kweli na watu wanaompinga ni wapumbavu.”

Halafu akapanda ngamia wake akaanza safari ya kuelekea kwao. Aliendelea kufikiria kuhusu Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu wakati wote wa safari yake, na alikuwa anashangaa kuhusu mazungumzo yake, hadi alipoonana na Abu Dharr.

Abu Dharr alipomuona Unais, alimuuliza kwa shauku kubwa, “Kuna taarifa gani? Uliona nini Makkah?”

Unais: “Wanasema kwamba mtu huyu ni mshairi, mchawi na mtabiri. Lakini nilipochunguza mazungumzo yake kulingana na wale wanaosema kuwa ni mshairi, niliona kwamba maneno yake si mashairi wala si utabiri kwani nimewahi kukutana na watabiri wengi, na mazungumzo yake si sawa na yale ya watabiri.

Abu Dharr: “Anafanya nini na anasema nini?”
Unais: “Ansema mambo ya ajabu.”
Abu Dharr: “Huwezi kukumbuka chochote katika yale aliyosema.”

Unais: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Hotuba yake ilikuwa tamu sana lakini sikumbuki chochote zaidi ya yale ambayo nimekwisha kwambia, lakini nimemuona anasali karibu na Al-Ka’abah, na pia nimemuona kijana moja mwenye sura ya kupendeza ambaye haja-balehe, akisali pamoja naye. Watu wanasema kwamba huyo ni binamu yake Ali. Pia niliona mwanamke anasali nyuma ya mtu huyu. Watu waliniambia huyo ni mke wake, Khadijah.

Sura Ya Pili

Baada ya kumsikiliza kaka yake, Abu Dharr alisema, “Sijaridhishwa na ripoti yako. Nitakwenda huko mimi mwenyewe, nimuone na nimsikilize mimi binafsi.”

Abu Dharr alifika Makkah, aliingia kwenye eneo la Ka’abah na akaanza kumtafuta Mtume, lakini wala hakumuona pale, ama kusikia akitajwa. Alikaa hapo hadi machweo ya jua. Ali aliwasili hapo na akapita karibu na pale alipoketi Abu Dharr. Alimuuliza, “Unaonekana kuwa msafiri. Ni kweli?”

Abu Dharr: “Ndio.”
Ali: “Njoo nifuate.”

Ali alimchukua nyumbani kwake. Wote wawili walikuwa kimya wakati wanakwenda nyumbani kwa Ali. Abu Dharr hakumuuliza Ali kitu chochote hadi walipofika nyumbani. Ali alitayarisha mahali pa kulala na Abu Dharr akalala. Kesho yake asubuhi alikwenda tena Ka’abah kumtafuta Mtume. Wala hakumuuliza mtu yeyote ama mtu yeyote kumwambia chochote. Abu Dharr aliendelea kungoja kwa hamu kubwa hadi mwisho wa siku. Ali alikwenda tena kwenye Al-Ka’abah kama kawaida yake na alipita mbele ya Abu Dharr: mara alipomuona Abu Dharr, alimuuliza: “Kwa nini? hujaenda nyumbani hadi sasa?”

Abu Dharr: “Hapana.”
Ali: “Vema! Sasa twende nifuate Mimi.”
Wote walili walikuwa wanakwenda kimya Ali alipouliza, “kwa nini! Umekuja hapa kwa sababu gani?”
Abu Dharr: “Ninaweza kukuambia sababu endapo hutamwambia mtu mwingine.”
Ali: “Sema wazi chochote unachotaka kusema. Sitamwambia mtu yeyote.”

Abu Dharr: “Nimekuja kumuona mtu baada ya kupata taarifa kwamba mtu huyu anajiita yeye Mtume. Nilimtuma kaka yangu azungumze naye. Aliporudi hakunipa taarifa ya kuridhisha. Sasa, nimeamua kumuona mtu huyu mimi mwenyewe.”

Ali: “Umefika. Sasa ninakwenda pale alipo. Nifuate. Ingia popote nitakapoingia. Endapo nitaona hatari yoyote nitaanza kukiweka sawa kiatu changu, nikiwa nimesimama karibu na ukuta, na nikianza kufanya hivyo, wewe rudi.”

Abu Dharr anasema, “Ali alinipeleka hadi ndani ya nyumba. Niliona nuru katika umbo la mtu inaonekana hapo. Mara tu nilipo muona, nilivutiwa kwake na nikahisi ninataka kubusu miguu yake. Kwa hiyo, nilimsalimia Assalamu Alaykum.” (Alikuwa mtu wa kwanza kumsalimia Mtume wa Uislamu kwa desturi ya Kiislamu, kabla ya kusilimu).

Alijibu salamu, akasema, “Waa Alaykum as Salam, wa Rahmatullah wa Barakatuh. Ndio Unataka nini?”
Nilijibu; “Nimekuja kuwako kwa moyo na imani.”
Alinielekeza mambo fulani muhimu na akanitaka nikariri Kalimah (Shahada) yaani (La ilaha illalah Muhammadun Rasulul lah) nilisoma hivyo, na kwa hiyo nikaingia kwenye Uislamu.

Baada ya hapo, aliondoka kwenda Ka’abah. Alipofika hapo alipoona kundi kubwa la makafiri wa kabila la Quraishi, alisema kwa sauti kubwa, “Sikilizeni enyi Maquraishi nina shuhudia kwamba Mwenyezi Mungu ni Mmoja na Muhammad ni Mtume Wake.”

Sauti hii iliwaogopesha Maquraishi. Hisia za Quraishi kwamba heshima ya masanamu yao imeshushwa iliwatia wasiwasi sana.

Hatimaye watu walimzunguka Abu Dharr wakaanza kumpiga sana hadi akazirai. Ilibakia kidogo afe lakini Abbas bin Abd al-Mutalib alifika hapo ghafla. Alipoona kwamba mfuasi wa Muhammad alikaribia kufa, alilazimika kumlalia Abu Dharr.

Akasema: “Enyi watu! Nini kimewatokea ninyi? Munataka kumuua mtu mkubwa wa kabila la Bani Ghifar. Mmesahau kwamba nyinyi hufanya biashara na Bani Ghifar na huwa mnatembelea huko mara kwa mara. Hamliogopi kabila lake kabisa!”

Baada ya kusikia hayo, watu hao waliondoka hapo na Abu Dharr ambaye alikuwa anatoka damu, alinyanyuka na kwenda kwenye kisima cha zam zam.

Alihisi kiu sana kwa sababu ya majeraha makubwa na kutoka damu nyingi. kwa hiyo, kwanza alikunywa maji halafu akasafisha mwili wake. Baada ya hapo alikwenda kwa Mtukufu Mtume huku akigumia. Mara tu Mtume alipomuona katika hali ile, alisikitika sana na akasema, “Abu Dharr! Umekula au kunywa chochote?”

Abu Dharr: “Bwana wangu! Nimeona nafuu kidogo baada ya kunywa maji ya Zam zam.”
Mtume: “Bila shaka maji hayo hutoa nafuu.”

Baada ya hapo alimliwaza Abu Dharr na akampa chakula. Ingawa Abu Dharr aliumia sana kwa sababu ya hotuba yake, bado hamasa ya dini haikumruhusu aondoke kwenda kwao kimya kimya. Imani yake ilimtaka awafanye Maquraishii waamini kwamba akili ya mwanadamu hudharau ushirikina wa uchaji masanamu.

Aliondoka hapo akaenda kwenye eneo la Al-Ka’abah tena. Alisimama sehemu iliyoinuka na akaita kwa sauti ya ushupavu imara. “Enyi watu wa Quraishii! Nisikilizeni! Ninashudia kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu na ninashuhudia kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu.”

Waliposikia hivyo wale wapotovu ambao waliona misingi ya miungu yao inatikiswa na ambao walikasirishwa sana na hotuba yake ya mwanzo, kwa mara nyingine waligutushwa na wakawa katika hali ya wasiwasi na wakageuka kuelekea upande inakotoka sauti na haraka sana walikusanyika na kumzunguka yeye. Walikuwa wanapiga kelele “Muueni huyu Ghifari haraka iwezekanavyo kwani yeye nia yake ni kuwatukana miungu wetu.”

Mkusanyiko wote ulisema kwa sauti moja, Mueni Abu Dharr.” Kwa hiyo walimpiga Abu Dharr hadi akazirai.

Abbas bin Abdul Muttalib alipoona hivi alijitokeza mbele na kumlalia Abu Dharr kama ilivyofanya jana yake, na akasema; “Enyi Quraishi! Nini kimewatokeeni kwamba mnamuua mtu wa kabila la Ghifari ingawa mnao uhusiano mzuri na kabila lake na biashara yenu inaendelea vizuri kwa msaada wa kabila lake. Msiendelee kumpiga.”

Baada ya kusikia haya, watu wote waliondoka na kumwacha Abu Dharr akiwa amepoteza fahamu. Alipopata fahamu, alikwenda kwenye kisima cha Zam zam! na baada ya kunywa maji alisafisha mwili wake uliokuwa umetapakaa damu.

Abdullah Subaiti ameandika kwamba ingawa Abu Dharr aliteseka sana kwa majeraha lakini hata hivyo aliwalazimisha Quraishi kuwa na maoni kwa mujibu wa hotuba zake kwamba Uislamu ulikwisha enea kwa watu na uliwavutia sana.

Kwa ufupi Abu Dharr alinyanyuka kutoka kwenye kisima cha Zamzam na kwenda kwa Mtukufu Mtume. Mtume alipomuona Abu Dharr katika hali hiyo alisema, “Ewe Abu Dharr! Ulikwenda wapi na kwa nini umekuwa katika hali hii?” Abu Dharr alijibu, “Nilekwenda kwenye Ka’abah tena. Nilitoa hotuba tena na nikatapakaa damu kwa kipigo. Sasa nimekuja kwako baada ya kuoga maji ya Zam zam.”

Mtume akasema; “Ewe Abu Dharr! Sasa ninakuamuru urudi nchini kwako mara moja. Nisikilize! Utakapofika nyumbani kwako, mjomba wako tayari atakuwa amekufa. Kwani hana mrithi mwingine isipokuwa wewe, wewe utakuwa mrithi wake na kuwa mmiliki wa rasilimali yake. Nenda ukatumie mali hiyo kwa kutangaza Uislamu. Baada ya muda mfupi nitakwenda na kuhamia Madina mji wa mitende. Wewe endelea kufanya kazi huko hadi nitakapohamia huko.” Abu Dharr alisema, “Ndio! Bwana wangu vyema sana. Nitaondoka hivi karibuni na kuendelea kutangaza Uislamu.” Sahih Bukhari, Sura ya Uislamu na Abu Dharr, chapa ya Misri, 1312 Hijiriya.

Sura Ya Tatu

Baada ya kuingia kwenye Uislamu, Abu Dharr aliondoka Makkah kwenda nchini kwake. Abdullah Subaiti ameandika kwamba Abu Dharr alipoondoka, alikuwa anabubujika imani, kamili, na alikuwa na furaha sana. Alifurahia sana kwamba Mwenyezi Mungu, alimwongoza kwenye imani ambayo imekubaliwa na waliotakasika na dhamira imeridhika nayo na akili inakaribisha kwa ukamilifu.

Aliendelea na safari hadi nchini kwake. Mtu wa kwanza kumsalimia alikuwa kaka yake Unais na pia alikuwa mtu wa kwanza kupata mwamko wa imani yake.
Unais alikwenda kubusu miguu ya kaka yake na kusema, “Ewe ndugu yangu! Umepitisha siku nyingi sana Makkah sasa niambie ulichopata huko.”

Abu Dharr alisema, “Unais! Nimefanya uamuzi wenye busara. Niliamua baada ya kutafakari sana kwamba lazima nikubali imani ya Muhammad! Ewe Unais! siwezi kukuambia kwamba nilipokutana na Muhammad na kumtazama uso wake, nilihisi kama vile kifua changu kilikuwa kinaongezeka. Moyo wangu ulijaa furaha na akili yangu ililewa imani.

Mara nikakariri kalimah-shahada na kukubali Utume wake nilimwomba anifundishe vipengele vya imani. Kwa hiyo alinieleza kanuni za Uislamu. Ewe Unais ninakuomba kwa kweli na kwa moyo safi na nia njema uinamishe kichwa chako kwa unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu na uache kuabudu miungu hii iliyotengenezwa na mikono ya watu yenye asili ya mawe.”

Aliposikia hivi, Unais alikaa chini huku akiwa ameinamisha kichwa chake na kuanza kufikiri. Alipatwa na hali kama vile umelewa. Unais alikumbuka mambo hayo yote aliyo yaona huko Makkah. Baada ya muda fulani alisema, “Ewe Ndugu! Akili yangu imethibitisha ukweli wako na mantiki yangu inanieleza nikutii wewe. kwa hiyo sikiliza! Ninashahidilia kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu na ninakiri kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.”

Abu Dharr alifurahi sana kuona Unais anaikubali imani. Alimwambia: “Sasa twende kwa mama yetu.” Wote wawili walikwenda kwa mama yao. Baada ya kumuamkia mama yao, Abu Dharr akasema, “Mama yangu mpendwa! Nakuomba unisamehe! Nimekuwa mbali na wewe kwa kipindi kirefu sana. Lakini, nimepata kitu cha nadra ambacho hakuna mtu aliye nacho hapa.”

Mama Akamuuliza, “Kitu hicho ni kipi?” Abu Dharr alisema, “Hii ni tunu ya imani mama. Nilikutana na mtu huko Makkah ambaye uso wake uling’aa nuru ya uadilifu, hana wa kumlinganisha kwa uzuri wa tabia yake na ukarimu wake. “Yeye husema kweli tupu. Yeye husema kilicho sahihi. Hutenda haki. Maneno yake yanayo busara. Mama! Maadui zake pia humwita mkweli na mwaminifu. Huwaita watu wamwelekee Mwenyezi Mungu ambaye ni muumba wa mbinguni na ardhi na mpangiliaji wa kuweza kudumu kwa ulimwengu huu.

“Nimekubali kumuamini mtu huyu kwa kuvutiwa na mwelekeo wake, maneno yake na semi zake, na Unais pia amekuwa Muislamu. Tumekubali Upweke wa Mwenyezi Mungu na Utume wa Muhammad.”

Mama yake Abu Dharr akasema: “Mwanangu, endapo ndio hivyo, mimi pia nina shahidilia kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na kukiri kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.”

Abu Dharr alitiwa moyo baada ya kaka yake na mama yake kuingia kwenye Uislamu na sasa alianza kutafakari jinsi ya kuwashawishi watu wa kabila lake na kuwavuta waelekee kwenye njia iliyonyooka.

Baada ya kufikiri sana Abu Dharr alitoka nje ya nyumba yake. Mama na kaka yake pia walikuwa naye. Baada ya kusafiri mwendo mfupi walipiga hema lao karibu na mahema ya watu wa kabila lao.

Usiku uliingia. Wasafiri hawa waliochoka walikuwa wamelala kwenye mahema yao walipohisi kwamba watu wengi wa kabila hilo waliokuwa pale walikuwa wanasimuliana hadithi wao kwa wao na kuelezea matukio mbali mbali. Walikuwa katika mazungumzo mfululizo.

Abu Dharr alipojaribu kusikiliza kwa siri walikuwa wanasema nini, alisikia kwamba walikuwa wanamsema yeye. Baada ya hapo watu waliondoka kutoka kwenye mahema yao na kwenda kwenye hema la Abu Dharr, akamwambia kaka yake, Unais, “Watu wa kabila letu wamekuja karibu na hema letu. Nenda nje ukawaone.”

Unais alitoka nje mara moja. Aliwaona vijana wa kabila hilo walikuwa karibu na hema. Walikwenda karibu na hema ili wajue endapo Unais na Abu Dharr walikuwa hapo. Walimsalimia. Baada ya Unais kujibu salamu yao, aliwauliza sababu ya wao kutembelea hapo. Wakasema, “Tumekuja tu kukuona wewe na Abu Dharr.”

Unais alirudi ndani na akamwambia Abu Dharr, “Vijana wa kabila letu wamekuja kutaka kujua hali ya safari.”

Abu Dharr alisema, “Waambie waingie ndani. Nitazungumza nao. Inawezekana labda nikawasilimisha waanze kumuabudu Mwenyezi Mungu, Aliye Pekee.”

Unais alitoka nje na akawaambia, “Ingieni ndani kwani kaka Abu Dharr anawaiteni.”
Wote walikwenda kwa Abu Dharr. Mmojawao akasema, “Ewe Abu Dharr! Hatujakuona kwa kipindi kirefu na matokeo yake ni kwamba tunasikitika sana.”

Abu Dharr akasema, “Wapendwa wangu vijana! Moyo wangu unayo mapenzi makubwa sana kwenu, na ninawahurumieni.”

Mtu mmoja: “Abu Dharr! Ulikuwa wapi kwa muda mrefu hivi? Tumeshindwa kukuona kwa kipindi kirefu.”

Abu Dharr: “Nilikwenda Makkah. Nilirudi siku chache zilizopita.” Mtu wa pili: “Tunafurahi kwamba ulikwenda Makkah.”

Abu Dharr: “Kama mambo yalivyo, nilikwenda Makkah, lakini sikutoa sadaka kwa Hubal wala sikuwasujudia Lat na Uzza. Vijana wangu! Kwa nini nifanye yote haya ambapo ninafahamu kwamba masanamu haya wala hayana uhai, ama kuweza kuumiza au kumnufaisha yeyote? Wala hayawezi kuona ama kusikia, ama kuzuia janga linaloweza kuwapata.

“Sikilizeni! Mimi nimekimbilia kwa Mwenyezi Mungu katika matendo yangu na mambo yangu yote. Hakika Yeye ni Peke yake, hana mfano wala mshirika, na ninakiri kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni Yeye peke yake anapaswa kuabudiwa, Yeye ni Muumbaji wa kila kitu na mwezeshaji wa kila kiumbe.

“Ninawaomba njooni kwangu tuwe pamoja katika mpango wetu wa utekelezaji na mshahidilie Upweke wa Mwenyezi Mungu kama sisi”

Waliposikia hivi, watu wote walianza kutetemeka. Mmoja wao alisema kwa mshangao, “Ewe Abu Dharr! Unasema nini?”

Abu Dharr: “Sikilizeni kwa yale ninayowaambieni ingawa siwezi kumuona Mwenyezi Mungu kwa macho yangu bado ninaweza kumuona Yeye kwa jicho langu la kiroho na sikilizeni! Inawezekanaje kitu chochote kinachotengenezwa na mikono ya mwanadamu kiwe na thamani ya kuabudiwa na binadamu? Si busara kuabudu masanamu yaliyotengenezwa kwa mawe na miti, na kuyaomba ili yatutimizie haja zetu.

“Watu wa kabila langu! mnajua kwamba masanamu haya hayana uwezo wowote. Wala hayawezi kuzuia uovu, ama kuwa na nguvu ya kupata manufaa?”

Baada ya kusikia ushawishi huu wa Abu Dharr, watu walianza kunong’onezana wao kwa wao.

Mmoja wao alisema; “Nimekwisha waambieni kwamba huko Makkah, mtu amejitokeza, anajiita yeye ni Mtume na anawaita watu kumwabudu Mwenyezi Mungu Mmoja. Abu Dharr amekutana na mtu huyu, na mahubiri ya mtu huyu yamesisimua sana hivyo kwamba fikra zozote anazozitoa Abu Dharr ni za mtu huyo.”

Mtu mwingine akasema; “Hali ni mbaya sana. Sasa tupo hatarini ambayo inatujia kupitia kwa Abu Dharr na mahubiri yake. Tunadhani kwamba endapo ataendelea kuhubiri namna hii, tofauti zitajitokeza kwenye kabila letu na maisha yetu yataharibika. Ni vema twende kwa mtemi wetu Khafaf, tumwelekeze hatari zote zinazoweza kujitokeza, na tumsisitizie na alipatie jambo hili kipaumbele ili tuweze kukabiliana nalo.”

Vijana wa kabila la Ghifari waliondoka nyumbani kwa Abu Dharr na walikwenda kumwona Khafaf. Wakati wapo njiani walibadilishana mawazo wao kwa wao. Mmoja wao alisema, “Abu Dharr ameanzisha ghasia kubwa.”

Mwingine akasema, “Itakuwa aibu kubwa sana kwetu kama tutaifumbia macho dhambi hii kubwa ya Abu Dharr. Anaifanyia ufisadi dini yetu waziwazi na kukebehi miungu yetu.” Mtu wa tatu akasema, “Ni wajibu wetu kumfukuza kutoka kwenye kabila letu bila kuchelewa hata kidogo, kwa sababu kama tukichelewa kumtenga katika kipindi kifupi tu, atawaelemea vijana wetu, wanawake zetu, watumwa wetu na kuwatia mawazo yake maovu akilini mwao. Endapo inatokea hivyo, tutapata hasara kubwa sana.”

Mtu wa nne akasema, “Maoni yako ni sahihi. Lakini, nani atamfunga paka kengele? Huyu ni mtu mashuhuri wa kabila na ni mzee wa kaya. Ninaona kwamba hata Unais anayo mawazo haya haya, na yeye pia ni mtu mwenye kuheshimiwa.”

Mtu wa tano akasema, “Hakuna haja ya wasi wasi. Njooni tukamtaarifu Khafaf. Tunao uhakika kwamba Khafaf na watu wengine waungwana wa kabila ndio watakao mfukuza kutoka kwenye kabila.”

Mtu wa sita akasema, “Ninatafakari kuhusu mawazo yao. Sina uhakika kama wataweza kuwabadili. Inawezekana kwamba wao ndio watakao badilika na kwenda kwenye njia iliyo nyooka tusijisumbue, lakini na tutafakari kuhusu dini yao. Nisikilizeni! Ninaona kuna ukweli kwenye imani yao. Hata hivyo karibu tutafika kwa mtemi Khafaf. Baada ya mazungumzo yetu na yeye, tunategemea kufikia uamuzi wenye msimamo.”

Kwa ufupi, wakizungumza pamoja, watu hawa walifika nyumbani kwa mtemi wa kabila la Ghifar na wakamwambia, “Tumetoka kwa Abu Dharr kuja kwako.”

Khafaf: “Abu Dharr amerudi kutoka safari yake ya kutoka Makkah?” Mtu mmoja akasema, “Bwana, Abu Dharr ameasi. Aliwabeza miungu wetu. Anasema kwamba yupo mtu ameteuliwa kuwa Mtume. Kazi yake ni kuwaita watu waende kumuabudu Mungu Mmoja na pia kufundisha mambo mazuri. Abu Dharr haridhiki bila kukubali utume wa mtu huyu na kuendelea na msimamo huo, lakini wakati wote anahubiri kwa watu na kuwaita wote wengine waende kwa Mtume huyo na Mungu wake.

Khafaf aliposikia, alisema, “inasikitisha kuona kwamba Abu Dharr, anawaacha miungu wote, na kutangaza kumuabudu Mungu Mmoja. Ni uovu mkubwa sana na kutia kinyaa. Ninaona kwamba jambo hili litachochea vurugu kubwa katika kabila letu, na matokeo yake kabila litaangamia. Enyi vijana wangu! Msifanye haraka lakini nipeni, muda wa kutafakari kuhusu jambo hili la Abu Dharr.”

Baada ya vijana hao kuondoka na kurudi makwao, Khafaf mtemi wa kabila, alianza kufikiri kwa nini wote walikuwa wanasema kwa kumpinga Abu Dharr. Aliendelea kutafakari usiku wote akiwa kitandani kwake. Hali ilimkanganya sana na hakuweza kufanya msimamo hasa. Lakini akili yake ilikuwa na fikra nzito kuhusu maneno yaliyosemwa na Abu Dharr. Saa nyingi zilipita bila kupata usingizi, na alikuwa anafumba macho yake.

Mtemi Khafaf pia alikumbuka hotuba ya mwanafalsafa wa Kiarabu, Qays bin Saidah, pale sokoni. Alisema kwamba Muumbaji wa ulimwengu bila shaka ni Mmoja na ni Yeye tu ndiye anaye stahiki kuabudiwa.

Aliunga mkono kikamilifu maoni ya Abu Dharr kwenye hayo mahubri yake ya kusifika na pia alitamka kwamba fikra za Warqa bin Naufal, Zayd bin Amr, Uthman bin Hoverath na Abdallah bin Hajash kuelekea kwenye imani ya Abu Dharr.

Alikuwa katika hali hii ya kustaajabisha ambapo akili yake ilimuongoza na akajisemea mwenyewe, ‘Naam! Abu Dharr yu sahihi kwa sababu Qays bin Saida amemuunga mkono na ninao uhakika kwamba Qays hawezi akashindwa kuelewa wala kukubali itikadi yoyote ya uongo. Bila shaka, lazima atakuwepo muongozaji wa dunia hii, na lazima pawepo na nguvu yenye uwezo wa kuendesha mpangilio wote wa ulimwengu na ni dhahiri kwamba miungu wetu wa mawe na miti hawana kabisa uwezo kama huu. Ee Mungu wa Abu Dharr! Tuongoze na utukomboe kutoka kwenye uovu huu na utuweke kwenye njia ya haki.”

Wakati ambapo Khafaf alikuwa anafanya uamuzi wake muhimu, siku ilipambazuka hadi jua lilionekana angani pamoja na kuenea kwa mwanga wa jua, pia habari zilizidi kuenea kwamba Abu Dharr, kaka yake na mama yake wote wamerudi kutoka Makkah na wamemuabudu Mungu Mmoja tu.

Pamoja na kuenea habari hizi hasira ilichochewa. Watu walianza kumlaani Abu Dharr na kusema, ‘Amepata kichaa na hawezi kuelewa kwamba haya masanamu yetu hutuponya maradhi, yanatupatia riziki na kutulinda. Abu Dharr ni mtu wa ajabu ambaye anatuita twende kwa mungu asiyeonekana! Inaonyesha kama vile Abu Dharr anataka kuanzisha vurumai na matatizo miongoni mwa vijana wetu na kuwapotosha watoto wetu na wanawake wetu. Hakika mtu huyu ni muongo na madai yake si sahihi. Lazima afukuzwe kutoka kwenye kabila.”

Mmojawao akasema, “Kwa nini! Unawezaje kuelezea wazo la kumfukuza mtu huyu? Itafanyikaje? Hapana , kamwe! Haiwezekani kutokea. Huyu ni mtu jasiri katika kabila letu.”

Baada ya mazungumzo haya watu hao waliamua kutaka wasikilizwe na wazee kuhusu suala hili. Kufuatana na uamuzi wao, waliwaendea wazee wao kushughulikia jambo hili. Wazee wao waliamua kulipeleka jambo hili la Abu Dharr kwa mtemi. Kwa hiyo, wote walikwenda kwa Khafaf.

Mtemi wa kabila alimtuma mtumwa wake haraka aende kumwita Abu Dharr. Mtumwa huyo alipofika nyumbani kwa Abu Dharr alisema, “Abu Dharr! Wewe na Unais mnaitwa na Mtemi.”

Abu Dharr akajibu kwamba alikuwa tayari kwenda kwa mtemi. Mtumwa alipoondoka, Abu Dharr alichukua upanga wake na kuhifadhi kwenye mkanda na alimwambia kaka yake, Unais, “Njoo; twende kwa Khafaf!”

Unais: “Ewe kaka! Nimesikia mambo mabaya yanazungumzwa na watu kuhusu wewe. Nina hofu huu mkutano wetu unaweza usiwe na manufaa, jambo lisilotegemewa linaweza kutokea badala ya mategemeo yetu.”

Abu Dharr: “Hapana, siyo. Namjua Khafaf vizuri sana. Ni mtu mwenye hekima. Mwenyezi Mungu amempa hekima. Ni mtu mwenye akili sana miongoni mwa kabila letu.”

Ndugu hawa wawili waliendelea kuzungumza hadi wakafika kwa Khafaf. Hapo waliona kwamba watu maarufu wa kabila hilo walikuwa wamekaa kumzunguka Khafaf. Akawaamkia wote Abu Dharr akasema, “Salaamu Alaykum” (Amani iwe kwenu).

Waliposikia maamkizi ya Abu Dharr kwa jinsi ya Kiislamu, wazee wa kabila hilo walikasirika na walisema kwa hasira; “Salamu gani hii ambayo hatujawahi kuisikia kamwe.” Halafu mmojawao akasema “Inasikitisha. Hatujui Abu Dharr anakoelekea.”

Mtu mwingine akasema, “Hebu mtazame. Amekaa na upanga wake, na hana heshima kwa mtemi.” Mtu wa tatu akasema, maneno yako ni sahihi. Lakini, huyu ni mpanda farasi wa kabila letu na watu jasiri wakati wote huwa tayari kwa lolote.”

Abu Dharr akasema, “Silikizeni! Ninawaheshimu nyinyi kwa sababu ni watu maarufu wa kabila letu, ambao mnastahili kujivuniwa na kuwaenzi. Salaamu niliyo wapeni ni Salamu ya Kiislamu.”

Baada ya haya, Abu Dharr na Unais waliketi kwenye nafasi zao wakitazamana uso kwa uso na mtemi, Khafaf. Khafaf alisema kwa sauti ya upole lakini kali, “Ewe Abu Dharr! Ninayo Taarifa kwamba wewe umekuwa na msimamo wa kumuabudu Mwenyezi Mungu Ambaye haonekani. Watu mashuhuri wa kabila letu wamekasirika na msimamo wako huu. Wanasema kwamba Abu Dharr amewatukana miungu yao na anawaita hawana hekima yoyote.

“Ewe Abu Dharr! Tunakuheshimu lakini haimaanishi kwamba tupo tayari kustahamili miungu yetu kubezwa. Ninakuomba uache hoja ya mawazo yako ya sasa na urudi kwenye imani ya wahenga wako, au vinginevyo unatakiwa uieleze imani yako kwangu ili niweze kuelewa ukweli wa imani yako. Pia, ninakuhakikishia kwamba nitafikiria kuingia kwenye imani hiyo endapo utathibitisha kwamba imani yako haina shaka zaidi kuliko ya kwetu.

Abu Dharr naye alijibu, “Ewe mtemi wa kabila! Tunakuheshimu na kustahi chochote unacho sema. Lakini, wakati huo huo tunataka kueleza kwamba Mwenyezi Mungu, wa Pekee Ambaye tumeamua kumuabudu na Ambaye tunamwamini, ni huyu huyu ambaye ameumba dunia na mbingu, Ambaye huruzuku viumbe vyote, Ambaye kudhibiti maisha ya viumbe vyote vyenye uhai na Ambaye uwezo wake hauna mipaka.

“Masanamu ambayo tumekuwa tunayaabudu hadi sasa, yametengenezwa na mikono yetu kwa kutumia patasi na nyundo. Akili inaweza kuamrisha kwamba yule ambaye ametengenezwa na mikono yetu anaweza kuwa muumbaji wetu, anaweza kuruzuku na tusikiliza dua zetu?

“Mwanadamu ni kiumbe bora zaidi kuliko viumbe vya muumbo wote. Inawezekana yeye na heshima yake astahili kuinamisha kichwa chake mbele ya jiwe? Mtemi wangu! Tafadhali tafakari bila upendeleo kuhusu haya ninayosema. Masanamu hayana hata uwezo wa kufukuza adui yao.

“Nisikilize, ewe mtemi! Wakati fulani nilikwenda kwa Manat na nikampa sadaka ya kikombe cha maziwa. Nilikuwa bado nipo eneo hilo ambapo mbweha alifika hapo na akanywa maziwa hayo yote na akamkojolea Manat. Tukio hili liliniathiri sana na nilifikiri kwa nini mungu anashindwa kujilinda mwenyewe?

“Jambo hili lilinidhihirishia kwamba sanamu haiwezi kuwa mungu. Nina uhakika na kila mtu mwenye akili ataamini kwamba Muumbaji wa mbingu ni bora zaidi kuliko mbingu na muumbaji wa dunia ni bora zaidi kuliko ardhi.
Kwa mujibu wa kanuni hii yenye mantiki, masanamu hayawezi kuwa ni bora kuzidi sisi, haina maana sisi kuyaabudu.

“Ewe mtemi wangu! Nimekuja kwenye imani ya kweli kwamba Mwenyezi Mungu ni Peke Yake Ambaye ni Mumbaji na mwenye kuruzuku ulimwengu, na Muhammad Mustafa ambaye alipelekwa Makkah ni Mjumbe Wake.

“Anazo sifa nzuri kama hizo hivyo kwamba hakuna afananaye Naye hapa duniani. Quraishi ambao ni maadui zake wabaya wanakubali ukweli wake na uwezo wake. hata wanapojua kuwa Muhammad ni mpinzani mkubwa wa miungu yao na dini yao, wamempatia jina la Sadiq na Amin, kama ambavyo, nimetambua hivi karibuni tu. Sikiliza! Uso wake unang’aa nuru na hekima inatiririka kutoka kwenye maneno yake.”

Mara tu Abu Dharr alipomaliza hotuba yake, kelele kubwa ilitoka sehemu zote, “Jinsi gani maneno ya Abu Dharr yalivyo matamu! Kwa hiyo, miungu yetu haisikii na haisemi! Abu Dharr ameidhalilisha imani yetu na anaitukana miungu yetu!”

Kundi moja lilisema kwa pamoja, “Rafiki zangu! Msizungumze mambo yasiyo na mantiki. Kwa uaminifu tunasema kwamba lolote alilosema Abu Dharr linaonekana kuwa sahihi na akili inataka kwamba lazima tukubali ukweli. Tunao uhakika kwamba hatuwezi kupata mwongozo mzuri zaidi kuzidi yale ambayo Abu Dharr ametuletea.”

Sauti nyingine ilitokeza: “Nchi ya Arabuni inahitaji muongozaji na inaonyesha kama vile hakuna mwongoaji bora zaidi kuliko huyu ambaye amedhihirishwa na Abu Dharr.”

Halafu sauti nyingine ilitokeza, “Hotuba ya Abu Dharr ni ya maana sana.” na baada ya hii sauti ya juu sana ilitokeza; kama vile ingetoboa masikio, Ewe Abu Dharr! Ninashahidilia kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu na ninakiri kuamba Muhammad ni Mtume Wake!”

Alipoona hivi, Khafaf, mtemi wa kabila, baada ya kufikiri sana alinyanyua kichwa chake na akawaambia watu wake: “Wapendwa watu wa kabila langu! Nisikilizeni kwa makini. Mmesikia yote hayo aliyoyasema Abu Dharr. Ni wajibu wetu kutafakari kuhusu hotuba yake kwa uangalifu sana na kwa makini sana na tuweze kuona inayo kiasi gani cha ukweli.

“Uamuzi wa haraka haufai. Si busara kutupilia mbali ushauri wa mtu bila kuchunguza. Rafiki zangu! Mnatambua kiasi cha machafuko yaliopo miongoni mwetu na jinsi uhalifu ulivyo zidi ambao sisi tunahusika. Matajiri wanawanyonya masikini na hakuna mipaka katika kufanya dhambi na maovu.

“Mimi nimeamua kwamba lazima nikubali na kuunga mkono yale anayoyasema Abu Dharr. Sasa ni juu yenu nyinyi kujiamulia wenyewe. Sikilizeni nyinyi nyote. Ninashahidilia kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wake!”

Mara tu Khafaf alipotamka Kalimah (la ila ha illalah Muhammadan Rasulillah) palitokea kelele kubwa ndani ya kabila, Khafaf amekuwa Muislamu. Khafah ameingia Uislamu!”

Haikupita muda mrefu baada ya Khafaf kuingia kwenye Uislamu, hali ya kabila ilibadilika kabisa. Watu walio wengi walisilimu na kuwa Waislamu hapo hapo, ambapo wengine walingojea kukubali kuwa Waislamu mbele ya Mtukufu Mtume baada ya kuwasili huko Madina.
Kwa ufupi, kwa juhudi kubwa ya Abu Dharr watu wengi wa kabila la Ghifar walikubali kuwa Waislamu na palitokeza ukelele wa “Mungu Mkubwa! na “Mungu ndiye Mwenye Kusifiwa!” na jina la Mtukufu Mtume likaanza kutangazwa mchana na usiku.

Baada ya kujaza moyo wa Uislamu kwenye kabila la Ghifari na kuwasilimisha watu na kuingia kwenye Uislamu, Abu Dharr alielekeza umakini wake Asfan. Alipofika huko alianza kuhubiri Uislamu miongoni mwa watu.

Kwa kuwa sehemu hii ilikuwa kwenye njia kuu iliyotumiwa mara nyingi na Quraishi na alijenga hisia dhidi yao kwa sababu ya mateso aliyofanyiwa nao alifanya zoezi la nidhamu kali katika kuwafanya kuwa Waislamu. Kundi la Quraishi lilipopita hapo, aliwaeleza habari ya Uislamu na kwa hiyo idadi kubwa ya Quraishi walikubali kuwa Waislamu.

Sura Ya Nne

Abdul Hamid Jaudatus Sahar wa Misri ameandika, Uislamu ulienea Madina kama moto wa mbuga ya majani makavu.” Kabila la Ghifar lilifurahishwa sana na hali hiyo. Waislamu walipongezana wao kwa wao kwamba makabila mawili ya Aus na Khazraj, ambao walikuwa wasemaji sana, wapiganaji wazuri sana na waunga mkono wazuri sana walikubali kuingia kwenye Uislamu, na pia kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikwisha ridhika kuinyanyua dini Yake na alinuia kumsaidia Mtukufu Mtume na kutimiza ahadi yake.

Unais alikwenda kwa kaka yake Abu Dharr akiwa na habari za kufurahisha na akasema “Uislamu umeenea Madina na Aus na Khazraj wamekubali Uislamu!”

Abu Dharr akasema, “Mtume wa Mwenyezi Mungu atakwenda na kuhamia huko baada ya kipindi kifupi.”

Unais alimwangalia kaka yake kwa mshangao na alisema,
“Umepokea habari zozote za aina hiyo?”

Abu Dharr, “Hapana, wala sina taarifa yoyote kuhusu habari hizi, ama kujua kwamba watu wa Yathrib wamekuwa waumini.”

Unais, “Vipi sasa ulijua kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu atahamia Yathrib?”

Abu Dharr, “Aliniambia siku hiyo hiyo nilipokutana naye, kwamba alitarajia kwenda kwenye mji wa mitende na nadhani sehemu hiyo ya Yathrib, Mtume alisema kweli.”

Unais, “Inawezekana kwamba kabila lake litamruhusu aondoke hapo akiwa na Waislamu, ili kwamba baada ya matayarisho kamili awashambulie?”

Abu Dharr, “Wanaweza wakamruhusu au wasimruhusu, lakini baada ya kipindi kifupi atahamia huko. Kama mambo yalivyo, ni Mwenyezi Mungu tu ndiye anaye jua ni vipi na lini itatokea.”

Abu Dharr alisilimisha kabila lake na kuingia kwenye Uislamu baada ya yeye kuwa muumini. Halafu akaelekeza shughuli hiyo Madina.

Tangu aliporudi kutoka Makkah hadi kuhama kwa Mtukufu Mtume, Abu Dharr alikuwa anashughulika na kuhubiri Uislamu na aliendelea kufanya juhudi kuipeleka dini ya Mungu kwa umma Mtukufu Mtume aliendelea kufanya kazi yake ya kuhubiri Uislamu na Quraishi waliendelea kufanya kazi yao ya kumtesa Mtume. Walimpa mateso makubwa sana hivyo kwamba hakuwa na uchaguzi mwingine isipokuwa kuondoka nyumbani kwake.

Kwa ufupi, kwa amri ya Mwenyezi Mungu Jibril alimwambia aondoke Makkah baada
ya kumwambia Ali alale kwenye kitanda cha Mtume. Alifanya alivyoagizwa.

Alimwambia alale kitandani pake na akaondoka, hivyo kwamba Quraishi hawangejua
kama hayupo kitandani pake. Baada ya kukaa siku tatu kwenye pango la Hira
aliondoka kwenda Madina.

Abu Dharr alikuwa anangojea uhamiaji Madina. Watu wa kabila lake pia walikuwa wanangojea na walikuwa wanauliza mara kwa mara habari za Mtukufu Mtume kwa mtu yeyote aliyetokea sehemu hiyo.

Kuanzia Makkah na baada ya kukaa kwa muda wa siku chache pangoni, Mtume aliondoka kwenda Madina. Kabila la Ghifar lilipopata taarifa kwamba alikuwa kati ya Makkah na Madina walifurahi sana. Abu Dharr alihisi wimbi la neema lilikuwa linakuja. Aliungana na kabila kungoja.

Watu walikusanyika na kumzunguka na walimuuliza kuhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu, mwenendo wake na umbile lake alijibu, “Mtamuona baada ya muda si mrefu. Yeye ni bora kuliko wote na anamzidi kila mtu kwa sifa.”

Watu walipongojea kwa kipindi kirefu, Abu Dharr alikuwa anaangalia njia, ili awe mtu wa kwanza kuwataarifu watu atakapo wasili Mtume na kutuliza nyoyo za watu na kuondoa hofu iliyokuwa inawaelemea kwa kungojea kwa kipindi kirefu hivyo.

Muda uliendelea kupita. Watu wa kabila la Ghifar walikuwa na shauku kubwa ya kumpokea Mtume. Abu Dharr alipotupa jicho aliona ngamia anakwenda hapo. Watu wote walikuwa wanaangalia macho ya Abu Dharr. Baada ya muda mfupi, Abu Dharr akasema kwa sauti ya kushangaa, “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mtume anawasili!”

Allamah Subaiti ameandika, “Uso wa Mtukufu Mtume ulikuwa unatoa nuru. Kwa ufupi watu wote walimfuata Abu Dharr, huku wakisema kwa sauti moja, “Mtume wa Mwenyezi Mungu amekuja! Mtume wa Mwenyezi Mungu amekuja!” Abu Dharr alikwenda mbele haraka na akashika hatamu ya ngamia wake.

Watu walianza kusema, “Allahu Akbar.” (Mwenyezi Mungu Mkubwa) huku wakimzunguka Mtume kwa hamu kubwa. Wanawake wote, vijana na vikongwe, wavulana na wasichana walikuwa wanashangilia kwa furaha kubwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu amewasili! Mtume wa Mwenyezi Mungu amewasili!”

Baada ya hapo watu wa kabila la Aslam walisema, “Pia na sisi tumekuwa Waislamu kama walivyo fanya ndugu zetu wa kabila la Ghifar.” Mtume wa Mwenyezi Mungu alifurahi sana na alinyanyua mikono yake kuelekea mbinguni aliomba, “Ee Mola wa ulimwengu! Wasamehe kabila la Ghifari na uwaweke kabila la Aslam salama.”

Baada ya hapo Mtukufu Mtume aliteremka kwenye ngamia na akaanza kukariri Quran. Sauti yake iliingia kwenye nyoyo za watu. Halafu akaanza kuhubiri. Watu walikwenda mbele kwa makundi na kutoa kiapo cha utii kwake. Abu Dharr alisimama kwa maringo karibu na Mtume akiwa amefurahi kupita kiasi.

Watu wa kabila la Ghifari walijitokeza mbele na wakasema, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Abu Dharr alitufundisha yote yale uliyomwambia. Tukasilimu na kuwa Waislamu na tukakiri kwamba wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.”

Baada ya hapo watu walifurahi sana na walikuwa wanaangalia uso wa Mtume mara kwa mara. Abdul Hamid Jaudatus Sahar ameandika, “Watu walianza kuangalia uso wa Mtume kwa makini, waliona kwamba alikuwa mtu mwenye uso unao ng’aa midomo inayo tabasamu na tabia njema kuhusu umbo lake, hakuwa mwembamba au aliye konda ama mnene. Alikuwa na sura nzuri ya kupendeza.

“Macho yalikuwa makubwa na meusi, kope za macho zilikuwa ndefu, nyusi zake nyeusi zilizojikunja mfano wa tao, nywele nyeusi, shingo ndefu na ndevu nyingi. Alikuwa Mtukufu wakati ametulia na alikuwa anatia moyo kwa heshima wakati anasema.

Mazungumzo yake yalikuwa matamu. Wala hakuwa mkimya au msemaji. Alikuwa na sura ya kupendeza sana akiwa mbali na mzuri sana akiwa karibu.

“Saizi ya umbile lake ilikuwa ya kati, wala hakuwa mrefu sana kiasi cha kutokupendeza kumwangalia, ama mfupi sana kiasi cha kufikiriwa kuwa mtu duni.

“Baada ya hapo Mtukufu Mtume aliondoka kwenda Madina na Abu Dharr aliendela kuishi na kabila lake.”

Kutoka hapo, Mtukufu Mtume aliondoka kuelekea Madina. Alipofika Madina, watu walimkaribisha kwa moyo mkunjufu. Mara tu baada ya kufika, alianza kuhubiri ujumbe wa Uislamu. Abu Dharr ambaye hakuweza kumsindikiza Mtukufu Mtume huko Madina aliishi mjini kwake kwa kipindi kirefu sana hivyo hakuwepo katika vita kuu tatu za Kiislamu (Ghazawat) vita vya Badr, mwaka wa 2, Hijiriya, Uhud mwaka wa 3 Hijiriya, na Ahzab mwaka wa 5/

Baada ya vita ya Ahzab, aya ya Quran Tukufu ilimlazimisha Abu Dharr kuondoka kwenda Madina. Siku moja alikuwa anashughulika na dua baada ya Swala ya jioni kwenye msikiti wa mjini kwake, ambapo alisikia mtu anasoma kwa sauti Aya (61:10)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَارَةٍ تُنْجِيكُمْ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ{01}

Enyi mlio amini! Nikuonyesheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iliyo chungu.”(61:10)

Baada ya kutafakari maana ya Aya hii alipata shauku ya Jihadi na akamwambia Unais, “Nitaondoka kwenda Yathrib kesho.”

Unais: “Sawa! Nenda. Mwenyezi Mungu na akufikishe huko Salama!”

Abu Dharr, “Sitarudi. Nitatumia maisha yangu yote katika kumtumikia Mtukufu Mtume.”

Unais, “Ewe ndugu yangu! Umekuwa muumini wa kweli na imani imepenya kwenye moyo na roho yako. Kabila lako na watu wako hapa wanakutaka sana. Patakuwepo pengo kubwa sana ukiondoka hapa. Nadhani ungeacha mpango wa kwenda Madina na uishi hapa hadi mwisho wa uhai wako.”

Abu Dharr; “Mtukufu Mtume ni bora zaidi kuliko watu hawa. Chochote ambacho kimetekelezwa kinatosha. Mtukufu Mtume alipigana Badr, Mimi sikuwa naye. Akapigana huko Uhud Mimi si kuwepo. Hadi lini nitaendelea kulitumikia kabila langu na nikose baraka za kufa shahidi. Yote hayo ambayo yamefanyika mpaka sasa yanatosha. Sasa sitakata tama hata kwa dakika moja kuhusu uamuzi wangu wa kwenda Yathrib.”

Unais, “Pendekezo langu ni kwamba wewe uendelee kuishi hapa nyumbani kama kawaida. Mtukufu Mtume atakuita yeye mwenyewe atakapokuhitaji. Wewe angalia walikuwepo watu wengi waliokuwa katika miji ya kwao na waliondoka kwenda Madina baada ya kuitwa na Mtukufu Mtume.”

Abu Dharr akasema: “muda wa kungojea umepita. Endapo Mtume hajaniita mimi pia nina wajibu. Sitaendelea kungoja, nitakwenda huko bila kuitwa.”

Unais: “Vema! Lakini usifanye haraka. Chukua mahitaji ya muhimu kwa safari.”

Abu Dharr; “Sihitaji chochote. Vipande vya mikate mikavu vinanitosha.”

Abu Dharr aliondoka nyumbani kwake na kuelekea Madina. Alipofika huko alipata heshima ya kukutana na Mtume na akawa naye.

Alikuwa na desturi ya kulala kwenye msikiti wa Mtume usiku na wakati wa mchana alikutana na watu. Alikula chakula pamoja na Mtume na akaiga maisha yake ya kidunia kwa uchaji Mungu na uadilifu. Alifanya bidii sana kujifunza hadithi za Mtume na kuzihifadhi katika kumbu kumbu.

Baada ya kufika Madina Abu Dharr aliugua kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa. Mtume alipata taarifa ya ugonjwa wake. Akaenda kumuona Abu Dharr na akamwambia; “Abu Dharr! Unatakiwa uishi nje ya Madina kwa muda fulani sehemu ambayo ngamia, kondoo na mbuzi huchungwa na uzingatie kwamba usile chochote isipokuwa maziwa wakati wote utakapo kuwa kule.”

Mara tu baada ya kupokea amri ya Mtume, Abu Dharr aliondoka kwenda mahali hapo alipoambiwa akiwa na mkewe.

Ugonjwa ulikuwa mkali sana kwa kipindi cha siku kadhaa lakini, ulipungua pole pole akapata afya nzuri hadi akaweza kutimiza tendo la ndoa na mke wake. Sasa, palijitokeza tatizo la upatikanaji wa maji kwa ajili ya josho kubwa la kuondoa janaba kabla ya Swala. Hadi hapo alikuwa hajajua Tayamamu. Kwa hiyo alikuwa hajui la kufanya kwa muda fulani.

Hatimaye akili yake ilimwongoza na akaenda kumuona Mtume kwa mwendo wa haraka sana wa ngamia. Mara tu Mtume alipomuona Abu Dharr alitabasamu na alisema kabla Abu Dharr hajasema, “Abu Dharr! Usiwe na wasiwasi. Maji yametayarishwa kwa ajili yako hapa na sasa hivi. kwa hiyo, msichana aliyekuwa mtumishi wa Mtume alitayarisha maji na Abu Dharr akaoga.

Baadaye alikwenda kwa Mtukufu Mtume na akafundishwa jinsi ya kutumia udongo kwa ajili ya kuchukua Wudhu (Tayamamu)- (Musnad Ahmad bin Hanbal).

Abu Dharr alikuwa anaendesha maisha yake ambapo Vita ya Tabuk ilitokea mnamo mwaka wa 9 Hijiriya. Waandishi wa historia wanasema kwamba Mtume alijua kwamba Wakristo wa Syria walifanya uamuzi thabiti wa kushambulia Madina na wapiganaji elfu arobaini kutoka kwa Harcules, Mfalme wa Roma. Kwa hiyo, Mtume aliamua kuondoka kwenda Syria kama hatua ya tahadhari akiwa na wapiganaji kati ya elfu thelathini hadi arobaini. Alimteua Ali kuwa mbadala wake Madina. Baada ya kutayarisha jeshi lake aliondoka Madina.

Baada ya kuondoka Mtume wanafiki walianza kumdhihaki Ali kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alimwacha ili kupunguza mzigo wake mwenyewe. Katika kuwathibitishia kwamba wanafiki ni waongo aliamua kwenda kwa Mtume.

Kwa kufuatana na Mtume mahali paitwapo Jaraf na akamtaarifu kuhusu dhihaka ya wanafiki.

Mtume akasema, “Wanafiki ni waongo. Nimekuja hapa baada ya kukufanya wewe kuwa kaimu wangu. Ewe Ali hufurahikii cheo chako cha juu zaidi. Uhusiano wako na mimi ni sawa na uhusiano aliokuwa nao Harun na Musa ila tofauti moja tu ni kwamba hapatakuwepo na Mtume baada yangu.

Maana yake ni kwamba Musa alipokwenda kwenye Mlima wa Tur alimteua Harun kuwa kaimu (wakili) wake na yeye (Mtukufu Mtume) alifanya namna hiyo hiyo.”

Aliposikia hivi Ali alirudi Madina na Mtume aliendelea na safari ya kwenda Tabuk sehemu iliyokuwa kwenye mpaka wa iliyokuwa Falme ya Roma katika urefu wa vituo kumi kutoka Madina na Dameski. Alipofika Tabuk, alikaa hapo kwa muda wa siku kumi. Wakati wa kuwepo yeye hapo, alimtuma Sariys (jeshi la Uislamu linaloongozwa na mtu mwingine na si Mtume) sehemu zote, na alisisitiza kuwaita watu waingie kwenye Uislamu. Hakuna jeshi lililofika hapo kutoka Roma kwa madhumuni ya vita. Kwa hiyo, alilazimika kurudi Madina.

Wakati wa safari hiyo, siku moja usiku wanafiki walitaka kumuua wakati anapita kwenye bonde la Aqaba Zi Fata, kwa kumuogofya ngamia wake, ambaye angeweza kumwangusha chini, lakini Hudhayfah bin Yaman na Ammar bin Yasir walimwokoa.

Baada ya Mtukufu Mtume kuvuka bonde, alimwambia Huzayfah bin Yaman majina ya wanafiki waliotaka kumuua kwenye giza, na akamuamuru kuwa majina hayo iwe siri yake. Masahaba maarufu walikuwemo kwenye orodha hiyo. (Madarijum Nuduwah uk. 302).

Kwa mujibu wa Tahzibut Tahzib, watu hao walijaribu kupata majina hayo kutoka kwa Hudhayfah lakini hakufichua.

Hatimaye mmoja wapo wa masahaba hao alikiri mwenyewe, “Uniambie ama usiniambie, kwa jina la Mwenyezi Mungu, mimi nilikuwa miongoni mwa wanafiki hao!” Kwa ufupi, Mtume alirudi Madina wakati wa mwezi wa Ramadhani.

Wakati wa kuondoka kutoka Madina kwa madhumuni ya Vita ya Tabuk, Abu Dharr alikuwa naye. Lakini kwa kuwa ngamia wake alikuwa dhaifu na kukonda, hakuweza kuwa katika msafara. Abu Dharr, hata hivyo, alibaki nyuma ya msafara kwa umbali wa muda wa safari ya siku tatu.

Alijitahidi sana kuwa karibu na Mtume lakini alishindwa. Alihuzunika sana alipotambua kwamba haingewezekana yeye kuwa ndani ya msafara.

Kwa mujibu wa maelezo mengine, alipobaki nyuma, watu fulani walimwambia Mtume kwamba ilikuwa vigumu sana Abu Dharr kuwa naye. Aliposikia hivi, Mtume akasema, “Mwacheni huyo hivyo alivyo. Atafika Inshallah. Kwa hiyo msafara uliendelea na Abu Dharr alizidi kubaki nyuma akiwa amefadhaika na wasi wasi. Wakati mwingine alifikiria kurudi Madina na halafu tena alishawishika kuendelea na safari hadi Tabuk kwa jinsi yoyote ile kwa sababu kuwa nyuma ya Mtume ni hali ambayo ilimtesa sana.

Aliendesha ngamia wake kwa msisimko mkubwa lakini hakuweza kwenda haraka kwa sababu ya udhaifu wake.

Alipogundua hivi, aliteremka kutoka kwenye ngamia na akachukua mzigo wake wote na kubeba mgongoni mwake na akaendelea na safari kwa mguu. Ulikua msimu wa joto kali. Kwa hiyo, ni jambo linalojulikana kwa wasafiri kiasi cha ukali wa kiu ambayo ingempata.

Alikuwa anatembea na mzigo mgongoni mwake wakati ambapo kiu ilikaribia kumwelemea. Tayari alikwisha choka na wakati huo kiu ilifanya hali yake kua mbaya zaidi. Abu Dharr akiwa na kiu kali, alitafuta maji huku na kule akaona maji ya mvua yaliyokuwa kwenye dimbwi.

Akafika kwenye dimbwi la maji ambapo alikuwa na kiu sana, na alitaka kunywa maji yaliyojaa kwenye kiganja chake, ambapo ghafla, aliwaza kwamba maji hayo yalikuwa baridi sana na haikuwa vema yeye kunywa maji hayo kabla ya Mtukufu Mtume. Kwa hiyo, baada ya fikra hii kuingia akilini mwake akayamwaga maji hayo na akajaza maji hayo kwenye gudulia.

Abu Dharr alikuwa peke yake huku akiwa na kiu kali sana na gudulia lililojaa maji hadi akafika Tabuk.

Mara tu alipofika Tabuk, Waislamu walimuona na wakamtaarifu Mtume kuhusu kuwasili kwa msafiri aliyedhikika. Mara moja alisema, huyu ni sahaba wangu, Abu Dharr. Kimbieni, enyi masahaba wangu, na mleteni kwangu. Waliposikia hivyo, masahaba walikwenda haraka kwa Abu Dharr na wakamfikisha kwa Mtume.

Baada ya Mtume kuuliza kuhusu afya yake, akasema, “Ewe Abu Dharr, unayo maji. Kwa nini basi unakiu kali namna hii?”

Abu Dharr; “Bwana wangu, kama unavyoona, maji yapo, lakini siwezi kunywa.”
Mtume; “Kwa sababu gani?”

Abu Dharr; “Bwana wangu! Nilipokuwa njiani. Kuja hapa niliona maji karibu na kilima, lakini dhamiri yangu haikuniruhusu kunywa maji haya kwa ajili yako. Mimi nitayaonja baada ya wewe kunywa.”
Aliposikia hivi Mtume alisema; “Ewe Abu Dharr! Mwenyezi Mungu Atakuhurumia. Utaishi peke yako na utaondoka hapa duniani peke yako. Utafufuka peke yako mnamo Siku ya Hukumu. Utaingia Peponi peke yako na kundi la watu wa Iraq watapata furaha kamili kwa sababu yako, ni kwamba watakuosha watakuvika sanda na kusalia maiti yako.”

Tukio hili si tu linaonyesha mapenzi makubwa ya Abu Dharr kwa Mtume lakini kupitia kwenye tukio hili Mtukufu Mtume kwa wazi kabisa alitabiri matatizo na majanga ambayo yangemfika Abu Dharr katika maisha yake. Amenukuu tukio kutoka kwa Bin Babway kutoka kwa Abbas kwamba siku moja Mtume (s.a.w) alikuwa ameketi ndani ya msikiti wa Quba na masahaba wake wengi walikuwa wamemzunguka.

Alisema, “Mtu ambaye atakuwa wa kwanza kuingia kwenye lango la Msikiti huu, atakuwa ametoka kwenye kundi la watu wa Peponi.” Baada ya muda mfupi Abu Dharr aliingia kupitia kwenye lango hilo. Alikuwa wa kwanza ambaye alitoka nje akiwa peke yake. Mtukufu Mtume akasema hapo hapo, “Ewe Abu Dharr! Wewe unatoka kwenye watu wa Peponi.” Aliendelea kusema, wewe utafukuzwa Makkah kwa sababu ya kuwapenda watu wa Nyumba yangu. Utaishi ugenini na utakufa katika hali ya upweke. Kundi la watu wa Iraq wataneemeka kwa kushughulikia maziko yako na utakuwa pamoja na mimi Peponi.”

Sura Ya Tano

Historia inashuhudia kwamba Abu Dharr alielimika sana baada ya kuwa Muislam hivyo kwamba hapakuwepo wa kumlinganisha naye miongoni mwa masahaba. Alipata utakaso ulio bora wa imani na unyofu wa moyo hivyo kwamba alihakikisha kwamba yeye ni nguzo ya nuru kwa watu wenye utambuzi. Alizirutubisha akili za watu kwa ushauri, baada ya kuja kwa Uislamu, aliwafundisha watu masomo ya usawa na upendo na aliwafundisha jinsi ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume.

Maisha yake ya Kiislamu yaliheshimika sana hivyo kwamba hapakuwepo na mtu wa kulingana naye miongoni mwa waumini. Abdulah Subaiti ameandika kwamba Abu Dharr alijipatia sifa sana miongoni mwa masahaba hao ambao walifanya vizuri kuzidi wengine katika uchaji Mungu, kujihini, kumuabudu Mwenyezi Mungu, ukweli, uimara wa imani na hakuna wa kumfananisha katika kujisalimisha kwa Radhi ya Mwenyezi Mungu.

Wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w) chakula chake cha kila siku kilikuwa kilo tatu za tende na aliendelea hivyo hadi mwisho wa maisha yake.

Anaendelea kuandika Abdullah Subaiti kwamba Abu Dharr alinyanyuliwa juu sana katika maadili na tabia yake hiyo kwamba Mtukufu Mtume alimjumuisha kwenye kundi la Ahlul-bait (watu wa Nyumba ya Mtume) kama alivyo mjumuisha Salman Farsi. Hafiz Abu Naim anasema kwamba Abu Dharr alikuwa msalihina, mtu mchaji Mungu, na alikuwa na moyo ulioridhika. Alikuwa mtu wa nne katika msululu wa kukubali Uislamu. Aliacha maovu yote hata kabla ya kuanza kutekeleza sharia ya Kiislamu.

Hili lilikuwa lengo lake alilolihifadhi, kukataa kuwatii watawala dhalimu. Alikuwa imara katika kuvumilia maumivu na huzuni. Alijipatia sifa ya juu katika kuhifadhi hadithi na nasaha za Mtukufu Mtume.

Abu Naim ameandika kwamba Abu Dharr alitoa huduma kubwa kwa Mtukufu Mtume na alipata ujuzi wa vipengele vya imani na utekelezaji akiwa naye, na alijiepusha na maovu. Sifa yake maalum ilikuwa kuuliza maswali kwa Mtukufu Mtume.
Alijifunza kuhifadhi maana na fahamu zilizotolewa na yeye (Mtume) na alikuwa na shauku sana kuhusu jambo hili.

Kwa ufupi, kwa kadiri alivyoweza, hakuridhika na kuuliza maswali tu lakini pia alikusanya hazina kubwa ya ujuzi wa Kiislamu kwa ajili ya wafuasi wa Uislamu.

Kitendo kingine maarufu cha maisha yake ni kwamba alifuata nyayo za Mtukufu Mtume alizozitilia maanani na kuzithibitisha, na ambazo aliziamuru zifuatwe.

Akaambatana na Imamu Ali baada ya Mtukufu Mtume na hakumkana hata kidogo. Alimfuata na alipata manufaa kutokana na ujuzi mkubwa wa Imamu Ali. Abu Dharr alihifadhi akilini ukarimu, maadili mema na tabia njema za Imamu Ali. Ndio sababu Mtume (s.a.w) alisema, “Abu Dharr ni Mtu mkweli zaidi katika taifa hili.”

Mahali pengine alisema, “Abu Dharr yu kama Mtume Isa katika ibada ya kujinyima anasa za mwili.” Kwa mujibu wa hadithi alisema, “Mtu anayetaka kuona mfano wa maisha na staha ya Isa amwangalie Abu Dharr.”

Ni dhahiri kwamba ibada ya dini kama alivyofanya Abu Dharr, haikuwekewa mpaka kwenye Swala peke yake. Alikuwa hodari kiutendaji katika aina zote za ibada. Ni jambo lisilo na upinzani kwamba, kutafakari kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na muumbo wake, pia ni ibada kubwa. Abu Dharr alifanikiwa katika ibada hii pia.

Waandishi wa historia na hadithi wanakubaliana kwa pamoja kwamba Abu Dharr alipata kiwango kikubwa cha ujuzi na hii ilikuwa kwa sababu alipata ujuzi kwa moyo ulionyooka wakati anafuatana na Mtukufu Mtume. Alimuuliza maswali Mtume kila wakati na alijifunza na kuhifadhi majibu yake. Alikuwa na uzoefu mkubwa wa ujuzi wakati anafuatana na Mtume.

Mwandishi wa Kitabu Darayatus Rafiah anasema kwamba Abu Dharr alihesabiwa katika safu ya wanachuo wakubwa na washikilia maadili na alikuwa na daraja la pekee la kitaalam. Alikuwa sahaba mwandamizi wa Mtume alikuwa miongoni mwa watu hao waliotimiza agano lao na Mwenyezi Mungu yaani, watu hao walitimiza ahadi ambayo waliahidiana Naye kuhusu wao kuwa wafuasi wa imani iliyokamilika, na alikuwa mmojawapo wa wale watu wanne ambao waumini wote wanawajibika kuwapenda.

Allamah Manazir Ahsan Gilani ametoa maelezo mafupi kuhusu utaalamu wa juu wa Abu Dharr, ameandika, Soma tamko la Ali, mbora wa majaji miongoni mwa masahaba, na lango la Ujuzi na uhitimishe mwenyewe kwamba anaposema, “Abu Dharr alikuwa na shauku na hamu kubwa ya kupata ujuzi;” anasema jambo lililo sahihi.

Je! Hivi ushahidi huu wa Imam Ali, hauhalalishi madai ya Abu Dharr? Wakati mwingine Abu Dharr mwenyewe alikuwa akisema kwa shauku kubwa, “Tumetenganishwa na Mtukufu Mtume wakati ambapo hakuna hata mmoja wetu ambaye anaweza kujitegemea mwenyewe, kwa sababu bado hatujajua mambo fulani maalum.” (Tabaqat bin Sad Juzuu ya 4, uk. 10).

Allamah Gilani ameandika kuhusu ujuzi wa Abu Dharr, “Mtu mmoja alimuuliza Imamu Ali, alimfikiriaje Abu Dharr.
Akamjibu kwamba ‘Yeye, Abu Dharr alihifadhi ujuzi ambao ulimuemea.’

Umesoma na kuona jinsi alivyo kuwa mwepesi kukubali fikira, na wewe mwenyewe unaweza kukisia kutokana na matukio. Ndio maana kila mara alikuwa tayari kutekeleza kwa mujibu wa vile alivyosikia kutoka kwa Mtukufu Mtume. Kama vile alivyo jaribu kusikia kutoka kwa Mtukufu Mtume, alitaka kutekeleza kwa vitendo bila kusita hata kidogo. Ilikuwa utashi wa dhati kuona kwamba tendo lake liliendana kwa ukamilifu na ujuzi.

Abu Dharr alinuia sana na alikuwa imara kuhusu kipengele hiki hivyo kwamba hakujali kamwe mamlaka yenye uwezo mkubwa kuliko zote hapa duniani kama ingekuwa kipingamizi chake. Hotuba na ushawishi hazikuweza kumtikisa kutokana na msimamo wake aliokuwa nao.

Akajivunia sifa hii wakati mwingine alisema, “Enyi watu! Mnaona siku ya Hukumu, mimi nitakuwa karibu sana na Mtume (s.a.w) na kundi lake, kwa sababu nimemsikia akisema kwamba atakayekuwa karibu sana naye mnamo siku ya Hukumu atakuwa mtu ambaye ataondoka katika dunia hii katika hali ile ile ambayo alimwacha. Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba sasa hapana yeyote aliyeachwa miongoni mwenu ambaye yumo katika hali ile ya wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume isipokuwa mimi na sijanajisiwa na kitu chochote kipya. (Tabaqat bin Sad na Musnad ya Ahmad bin Hanbal).

Hili halikuwa dai la haki peke yake tu, lakini pia kiongozi wa dunia na Mtume wa mwisho alishuhudia hivyo.

Allamah Subaiti amesema kwamba mifano ya uadilifu iliyowekwa na Abu Dharr inastahili pongezi. Msimulizi anasema, “Nilipomuona Abu Dharr amejifunika blanketi na amekaa kwenye kona ya msikiti, nilimuuliza kwa nini alikuwa amekaa peke yake hapo? Alisema kwamba alimsikia Mtukufu Mtume anasema, “Ni vizuri kukaa kwenye kona peke yako kuliko kuketi katikati ya kundi la watu wabaya na ni vema kuketi na watu wenye maadili mema kuliko kuketi peke yako. Kimya ni kizuri kuliko kusema jambo baya na kusema jambo zuri ni vema kuliko kunyamaza kimya.”

Abu Dharr alisema kwamba Mtukufu Mtume amemwambia mengi kuhusu maelekezo ya maadili mema. Yapo Saba:

1. Fanya urafiki na watu masikini na jaribu kuwa nao karibu.

2. Ili uweze kuboresha hali yako waangalie watu wenye hali ya chini kuzidi wewe na usijilinganishe na watu wenye hali nzuri kuzidi yako.

3. Usimwombe mtu yeyote msaada wa mambo ya kidunia na ujenge tabia ya kuridhika.

4. Wahurumie ndugu zako na wasaidie wanapohitaji msaada.

5. Usisite kusema kweli hata kama dunia itakugeukia wewe.

6. Usijali shutuma za Kafiri kuhusu Mwenyezi Mungu.

7. Kila mara sema. “La hawla wa la quwwata illa billah.” (Hapana mweza isipokuwa Mwenyezi Mungu). Kwa maneno mengine, ‘Mwenyezi Mungu ni Uwezo Usiowezwa.

Abu Dharr anasema, baada ya kusema mambo haya, Mtume alisema huku anashika kifua changu, “Ewe Abu Dharr hakuna busara nzuri zaidi kama kupanga mambo vizuri, hakuna uchaji Mungu ulio bora zaidi kama kujizuia na hapana kitu kizuri zaidi kama maadili mema.”

Allamah Gihani alikinukuu Musnad ya Ahmad bin Hanbal anataja madili mawili tu miongoni mwa maadili haya yaliyotajwa hapo juu, ambayo yanaendana na kufanya urafiki na watu maskini na kuwatazama watu wenye hali ya chini kuzidi ya kwako, na halafu ameandika:

“Kwa kweli, haya ndio marekebisho mazuri kuliko yote dhidi ya maradhi ya kupenda utajiri na kupenda anasa za dunia. idhaniwe kwamba yupo mtu ambaye analo shati la Muislamu na suruali ndefu kuvaa, mkate wa ngano na nyama ya kondoo kwa ajili ya chakula, na nyumba ya udongo wa mfinyazi iliyo pangwa vizuri na safi kuishi humo.

Sasa, endapo mtu huyu anajilinganisha na mtu ambaye hana kitu isipokuwa nguo iliyo duni. Mkate wa shayiri nyumba iliyoezekwa kwa mabua, atamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hali yake nzuri zaidi na hatateseka kisaikolojia, mateso ambayo angeyapata endapo angejilinganisha na mtu tajiri mwenye nguo za gharama zadi na chakula kizuri. Njia hii ndio bora zaidi kupata kujitosheleza kidunia na manufaa mengineyo ya kidunia.

Lakini wangapi miongoni mwetu wanatekeleza hivi leo? Kwa hakika mtu hatapata matatizo yoyote endapo anafuata kanuni hii. Hii peke yake ndio kanuni ya muhimu kwa ajili ya dunia hii na kwa ajili ya Peponi, ambayo imeelezewa katika sentenso ifuatayo` ya Sheikh Sa’d, bingwa wa mashairi wa Iran.

“Nilikuwa nalilia jozi ya viatu hadi nilipo muona mtu asiyekuwa na miguu.” Baada ya kupenda utajiri sehemu nyingine ya kupenda dunia ni kupenda daraja na uwezo. Hii inayo hatari zaidi na ni sababu ya uovu wa mpangilio wa dunia. Uharibifu unaendelezwa duniani na watumwa wa utajiri ni pungufu zaid kuliko ule unaosababishwa na watu wenye uroho wa cheo na uwezo.

Sababu halisi ya maradhi haya ni kwamba mtu anapohisi ubora wake katika fani fulani, husahau uwezo wa yule ambaye amemboresha, na hujifikiria yeye ni matokeo ya hivi hivi tu. Halafu hajaribu kuwafanya watu wengine, wako karibu naye, watambue umuhimu wake ambao amejipachika mwenyewe. Akiwa na hitimisho la fikra hii, hutayarisha mipango kwa mujibu wa uwezo wa akili yake.

Ni mara chache sana kuonekana kwamba mtumwa wa ulafi na uchoyo ashindwe kufanya kila awezalo kwa lengo la kutimiza kusudio lake. Hujaza akili yake unafiki na wakati wote hubakia kuwepo kwake kupitia njia za halali na mbaya sana. Ubora ambao Abu Dharr alipata au alikaribia kuupata, ulikuwa ule wa uchaji Mungu.

Palikuwepo hofu kwamba hali ile ingemfanya kuwa na majivuno na kupenda makuu, ambayo baadaye tamaa ya hadhi na heshima huvuruga amani ya hapa duniani na Peponi. Kwa hiyo Mtume alizuia hiyo mapema na akamwambia Abu Dharr, siku moja kwa maneno ya wazi.

Mwenyezi Mungu alisema: “Enyi waja wangu! Wote nyinyi mnazo dhambi isipokuwa hao ambao nimewapa kinga. Kwa hiyo wote lazima msali mkiomba msamaha kwa utaratibu unaokubalika. Nitawasameheni.

“Nitasamehe dhambi za mtu anayeniona Mimi kuwa ninao uwezo wa kutosha kumkomboa kutoka kwenye dhambi zake na kwamba ninawaokoa, na kwa mtu aliyeomba msamaha wa dhambi zake kupitia kwenye uwezo Wangu.

“Enyi waja wangu! Nyote nyinyi ni wapotovu isipokuwa hao Ninawaonyesha njia iliyonyooka. kwa hiyo lazima mniombe Mimi ili niwaongoze. Wote nyinyi ni masikini na wahitaji isipokuwa wale Ninao wafanya matajiri.

“Niombeni Mimi kwa ajili ya riziki yenu na kumbukeni kwamba endapo nyinyi nyote mlio hai na wafu, wazee na vijana, waovu na waadilifu, muungwana na kujizuia msiombe chochote kutoka kwangu hapataongezeka chochote kwenye milki Yangu.

Na endapo nyote nyinyi wafu na walio hai, wazee na vijana, waovu na waadilifu mnakusanyika pamoja na kuniomba Mimi niwatimizie mahitaji yenu na kuwatosheleza mahitaji yenu, hapatatokea upungufu wowote kwenye himaya yangu hata wa kulingana na tone la maji yaliyochukuliwa na ncha ya sindano mtu anapoitumbukiza baharini. Hii ni kwa sababu Mimi ni Mkarimu, Msamehevu, Mkuu, Anayetukuzwa na Aliyeko kila mahali.

Mtu yeyote anaweza kujivunia kuwepo kwake au mafanikio yake na utulivu wake baada ya kuamini ukweli wa Utulivu wa Mungu na Ufahari ambao unauona katika hali hii? Hivi mtu yeyote anaweza kuwa na kiburi hata kwa sekunde moja baada ya hapa? Mtu yeyote anayemwamini Mwenyezi Mungu anaweza kuchochea uhaini hapa duniani kwa ajili ya kituo chake cha maisha, heshima, kujionyesha na hudumu baada ya hao? Nani mwenye wazimu anayeweza kujivunia uchaji Mungu wake ambapo kila mmoja wetu ana dhambi?

Pale ambapo utajiri wa watu matajiri upo kwenye udhibiti na mamlaka ya Mwenyezi Mungu; yeyoye huyo anayeonyesha pesa si mpumbavu? Endapo ni sahihi kwamba makubwa na madogo yetu hayawezi hata kwa kuungana kuongeza hata nukta moja upana wa himaya ya Mungu, mtu ambaye ni vumbi la kujaa kiganja tu atajivunia nini? Inapokuwa hii ni hali ya uhuru wake kutokana na utashi hata katika mambo ya mwongozo na ukomavu wa akili anafikiria upendeleo na uwezo a Mwenyezi Mungu kuwa ndio wakala halisi, ni katika misingi gani mhudumu wa dini au mrekebishaji atafikia juhudi zake zikastahili kuthaminiwa?

Endapo kila kitu ni mali yake na sisi ni masikini na wahitaji, kwa nini basi kiburi hiki na kwa nini ufidhuli huu na majigambo haya?

Hizi zilikuwa amri na hotuba ambazo ziliiingiza maadili ya Mtume Isa kwenye moyo wa Abu Dharr. Hata hivyo, hali ilikuwa hiyo na hata zaidi ya Mtume alivyokuwa na desturi ya kuchokonoa tabia ya kujinyima ya Abu Dharr.

Lakini tunatakiwa kutazama kwa makini zaidi wa upande huo wa mafundisho yake na nasaha ambamo humo ndimo Uislamu umesimama na kutofautiana na dini zingine zote.

Lazima utajihisi unataka kujaribu kufikiria kwamba kama haya yalikuwa mafundisho ya Mtukufu Mtume, kwa nini Uislamu ulipinga maisha ya utawa na kuyafikiria kuwa ni bidaa zilizoendakezwa na watawa na wahudumu wa kanisa? Nitajaribu kuelekeza usikivu wako kwenye jibu la swali hili. kwa ujumla kujizuia na uchaji mungu maana yake ni kuondoka mijini na kwenda milimani na misituni kuabudu Mwenyezi Mungu katika hali ya upweke. Abu Dharr anaeleza ifuatavyo:

“Mtukufu Mtume alimwabia kwamba pia ni jambo zuri kuondoa mawe njiani, kuwasaidia wasiojiweza pia ni hisani na hata tendo la ndoa na mkeo ni kitendo cha fadhila.
(Musnad Ahmad bin Hanbal)

“Nilimuuliza Mtukufu Mtume kwa mshangao, pia ni sadaka kufanya tendo la ndoa na mke wake, ingawa anatosheleza tamaa yake kwa tendo hili? Endapo mwanamume anatosheleza tamaa yake, pia atapata fidia kwa tendo hilo? Mtume alisema, “Vema, niambie, haitakuwa dhambi endapo ungetosheleza tamaa kwa kufanya kitendo kisicho halali na kilicho harimishwa?” Nilijibu, “Bila shaka.”

Akasema, “Nyinyi watu mnafikiria kuhusu dhambi lakini si matendo mema. Kwa kawaida watu wanaoishi maisha ya kushikilia maadili kuacha kufanya kazi ili wajipatie riziki na baadaye pale ambapo mahitaji ya kidunia yanapowabana sana wanaanza kuomba.”

“Siku moja Mtume (s.a.w) aliniita na akasema, “Unaweza kutoa kiapo cha uaminifu kwamba baada ya hapo patakuwepo Pepo tu inakungojea wewe.” Nikajibu, “Ndio” Halafu nikanyosha mkono wangu. Mtukufu Mtume akasema, “Ninataka useme kwamba hutaomba kitu chochote kutoka kwa mtu yeyote?” Nikajibu “Sawa” akasema, “hata ule mjeledi unaoanguka kutoka kwenye farasi wako unatakiwa uteremke chini na kuchukua wewe mwenyewe.”

Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume alimwambia, “Usifikirie wema wowote na upendeleo kuwa ni kitu kisichokuwa na thamani na kidogo. Endapo hunacho kitu cha kumpa ndugu yako Muisilamu, angalau ni muhimu ukutane naye huku unatabasamau.”

Abu Dharr anasema, “Mpendwa wangu (yaani Mtume) ameniusia kwamba niendelee kuonyesha wema kwa ndugu zangu, hata kama siwezi kutimiza kikamilifu, (Musnad Ahmad bin Hanbal) kwa sababu ni vigumu sana. Hata hivyo mtu anatakiwa kuwafanyia wema watu wote kadiri iwezekanavyo.”

Tabia ya Abu Dharr inadhihiri ambapo tunaona kwamba kila mara yupo na watu fukara na wenye kuhitaji. Alikuwa makini sana kuhusu mafundisho ya Mtume na hakuna miongoni mwa masahaba wenye mioyo migumu ambao hawakuathiriwa na maadili ya Mtume. Alikuwa muungaji mkono madhubuti wa Imamu Ali hivyo kwamba alichota tabia ya kiwango cha juu cha desturi njema za Mtume.

Agizo la Mtume lilikuwa: “Wape watumwa wako na watumishi wako chakula unachokula wewe, na wape nguo unazovaa wewe.” (Musnad ya Ahmad bin Hanbal) Na Abu Dharr alifuata utaratibu huo huo. Kila siku aliwapa watumwa wake na watumwa wasichana chakula alichokula yeye na aliwapa nguo alizovaa yeye.

Kwa mujibu wa hadithi ya Mtukufu Mtume, Abu Dharr aliona ndoa ni jambo la muhimu. Alioa lakini kwake ndoa kamwe haikuwa na maana ya starehe na furaha. Alidhani kwamba ndoa ilikuwa ni jina la kufuata Hadith ya Mtukufu Mtume. Inaeleweka kwamba alifuatana na mke wake popote alipokwenda.

Kwa kuwa mke wake alitoka Afrika, wakati fulani watu walisema, “wewe unaye mke mweusi?” Alijibu, “Nafikiri ni bora zaidi kuwa na mke mweusi na mwenye sura mbaya kuliko mke wenye sura inayopendeza na watu wanitembelee kwa sababu tu ya uzuri wa sura ya mke wangu.” Abu Dharr alikuwa anamjali sana mkewe.

Ukarimu si tu ndio mojawapo ya sifa bora sana, lakini ni kiini cha ubinadamu. Jinsi mtu anavyozidi kutambua kanuni za Uislamu ndivyo anayozidi kujaa moyo wa huruma.

Naim Bin Qanat Riyath anasema, “Siku moja nilikwenda kumtembelea Abu Dharr na nikamwambia kwamba ninampenda na ninamdharau wakati huo huo.” Abu Dharr akasema, “Inawezekanaje hali hizi mbili zije pamoja?”

Nilisema, “Nimekuwa nikiwaua watoto wangu. Sasa nimetambua kwamba hicho ni kitendo kiovu. Kwa hiyo, kila mara ninapofikiria kuja kwako kukuuliza kuhusu vipi nitaokolewa na kusamehewa, hisia hizi kubwa zinapanda pamoja. Nilipofikiria kwamba ingekuwa bora kama ungeniambia kuhusu ufumbuzi wake hisia za mapenzi zilipanda juu sana, lakini nilipofikiria kwamba ningeumia daima milele endapo ungetangaza kwamba dhambi hiyo haisameheki, chuki dhidi yako ilizidi kuongezeka. Sasa nimekuja kutaka kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili.”

Abu Dharr alisema, “Sawa! Niambie endapo umefanya yote haya mnamo siku za ujahilia au baada ya kuingia kwenye Uislamu?

Nilisema, “Wakati wa ujahilia.” Abu Dharr akasema, “Dhambi yako imesamehewa. Uislamu ni ukombozi wa uchafu wa aina hiyo yote na dhambi zote.”

“Niliposikia hivi niliridhika. Baadae nilitaka kuondoka akasema, “Ngoja!” Na nilifuata maelekezo yake.

“Baadaye alimwambia mkewe kwa alama alete chakula ambaye alikwenda ndani na akarudi akiwa na chakula. Abu Dharr alisema, “Naim, Bismillah (maana yake kula katika jina la Mwenyezi Mungu).

Kabla sijaanza kula nilimwambia tule wote. Akasema, “Mimi nimo kwenye Swaumu.” Aliposema hivi akaanza kuswali. Mimi nikaanza kula na nilipokaribia kumaliza, naye akamaliza Swala na akaanza kula.

Nilisema, “kusema uongo ni dhambi kubwa katika Uislamu na hata kama nikimdhania mtu fulani kuwa ni mwongo inawezekana kwamba anaweza kuwa mwongo, lakini nikufikirie vipi wewe?”

Abu Dharr alisema, “Umekaa muda mrefu na mimi. Jambo gani limekufanya unifikirie mimi kuwa ni mwongo?”
Nikasema, “Muda mfupi uiliopita uliniambia kwamba unafunga Swaumu na sasa unakula na mimi.”

Aliniambia, “Sijakuambia uongo. Nimefunga Swaumu na wakati huo huo ninakula na wewe.”

Akasema, Mtukufu Mtume amesema kwamba yeyote anayefunga Swaumu terehe 13, 14, na 15 ya mwezi huu wa Shabani, kwa namna nyingine ni sawa kama amefunga Swaumu ya mwezi mzima. Kwa maneno mengine, atapata thawabu ya kufunga Swaumu ya siku thelathini yaani kila Saumu ya siku moja inabeba uzito wa Swaumu ya siku kumi.

Kwa kuwa nimefunga Swaumu katika siku hizi ninayo haki ya kusema kwamba ninafunga Swaumu ya mwezi mzima.” (Musnad Ahmad bin Hanbal na Hayatul Qulubi-Allamah Majlis).

Alamah Bayhaqi pia amesimulia tukio la aina hiyo hiyo. Muhtasari wake ni kama ifuatavyo:
Siku moja Abu Dharr na Abdullah bin Shafiq Uqaili walikwenda nyumbani kwa mtu kama wageni. Abu Dharr alikwisha sema kwamba yeye anafunga Saumu na chakula kilipoletwa alianza kula. Abdullah alidokeza, “Wewe unafunga Saumu.” Abu Dharr alisema, “Ninaikumbuka Swaumu yangu. Sijaisahau Saumu yangu. Kila mara nipo makini kufunga Swaumu katika hizo siku tatu za kila mwezi ambazo huitwa “Ayyam al-Beydh.” na kwa mujibu wa hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w), uelewe kwamba mimi ninafunga Saumu (Sunan Bayhaqi).

Sura Ya Sita

Shahidi Thalit Allamah Nurullah Shustari ameandika:
Abu Dharr alikuwa mmoja wa masahaba mashuhuri sana na anahesabiwa miongoni mwa masahaba wa mwanzo kabisa walioingia kwenye Uislamu. Katika kuukubali Uislamu alikuwa mtu wa tatu, hivyo kwamba, aliingia kwenye Uislamu baada ya mama wa Waumini Khadijahtul Kubra na Amiri wa Waumini Ali. Kwa mujibu wa mwandishi wa kitabu cha ‘Isti’ab’ alikuwa na sifa ya juu katika ujuzi, kushikilia maadili, uchaji Mungu na kuwa mkweli, miongoni mwa masahaba wote.

Ali amesema kwamba, Abu Dharr alifanikiwa nafasi hiyo katika kupata na kuelewa mafundisho ya kidini ambayo hakuna mwingine ambaye angeyafikia. Mtukufu Mtume alikuwa anasema, “Abu Dharr yu kama Mtume Isa katika umma wangu. Abu Dharr anashikilia maadili kama alivyofanya Mtume Isa.”

Kwa mujibu wa hadithi, mtu anayetaka kuona mfano wa Mtume Isa amuone Abu Dharr. Shaykh Saduq katika kitabu chake Uyumul Akhbar al-Ridha ameandika kwamba Imamu Ali al-Ridha amesema kutoka kwa mamlaka ya wahenga wake kwamba kwa mujibu wa Hadith ya Mtume, “Abu Dharr ni mtu mkweli wa umma huu.”

Ali anasema kwamba Abu Dharr ndiye mtu peke yake asiye jali kamwe kushutumiwa kwa sababu ya Mwenyezi Mungu maamrisho na maagizo yake, ni kwamba, yeye alisema lolote ambalo ni haki na atatekeleza kwa vitendo, na wala hatajali vitisho vyovyote kuhusu jambo hili, ama kuogopeshwa na uwezo wa serikali.

Wanavyuoni wameandika kwamba Abu Dharr alitoa kiapo cha uaminifu kwa Mtume kwa ahadi kwamba katika imani ya Mwenyezi Mungu hangejali mtu yeyote anayemshutumu na kwamba angesema ukweli hata ungelikuwa na athari ya aina yoyote ile.

Ukweli na ujasiri ni sifa ambazo hata watu mashuhuri sana hushindwa kushikilia. Mtukufu Mtume ameitabiri sifa hii ya Abu Dharr na akasema kwamba Abu Dharr angetoa mchango mkubwa katika jambo hili na ataendelea kushikilia hata katika mateso makali ambayo angeyavumulia.

Mtume alisema: “Hapana mtu mkweli zaidi ya Abu Dharr kati ya utando wa mbingu na ardhi.” (Mustadrak Hakim uk. 342 Isabah bin Hajar Asqalani, Juz. 2, uk. 622, Feheist Tusi, uk. 70).

Katika ufafanuzi wa hadithi hii Allamah Subaiti ameandika: “Mtukufu Mtume aliwahutubia masahaba wake alisema: “Enyi masahaba wangu! Ni nani miongoni mwenu ambaye atakutana na mimi mnamo siku ya Hesabu katika hali hiyo hiyo ambayo nitamwacha nayo hapa duniani?”

Waliposikia hivi, kila mmoja wao alinyamanza kimya isipokuwa Abu Dharr aliyesema kuwa mtu huyo ni yeye. Mtukufu Mtume akasema, “Bila shaka! umesema kweli.”

Baada ya hapo, aliongeza, “Enyi masahaba wangu! kumbukeni ninayowaambieni. Hakuna mtu kati ya mbingu na dunia ambaye ni mkweli zaidi kuliko Abu Dharr.” (Tazama Tarikhi Himmah uk. 251).

Allamah Majlis ameandika maelezo baada ya kunukuu hadithi hiyo hapo juu kwenye kitabu chake (Hayatul Qulub).

Bin Babwayh ameeleza kupitia mamlaka ya kuaminika kwamba mtu fulani alimuuliza Imamu al-Sadiq endapo Abu Dharr alikuwa bora zaidi ya Ahlul –Bait wa Mtukufu Mtume au vinginevyo. Imamu Alisema, “Mwaka mmoja una miezi mingapi?” Alijibu, “Kumi na miwili.” Imamu akasema, “Miongoni mwa miezi hiyo mingapi inaheshimika na kutakaswa?” Akasema, “Miezi minne,” Imamu aliuliza, “Mwezi wa Ramadhani umejumuishwa katika miezi hii minne?” Akasema, “Hapana.” Imamu aliuliza, “Mwezi wa Ramadhani ni bora zaidi au miezi hiyo ni bora zaidi.”

Akajibu, Mwezi wa Ramadhani ni bora zaidi.” Imamu Akasema, “Ndivyo ilivyo na sisi, Ahlul-Bait. Huwezi kumlinganisha yeyote na sisi.”

Siku moja Abu Dharr alikuwa ameketi katika kundi la watu ambao walikuwa wanaeleza maadili ya taifa hili. Abu Dharr alisema, “Ali ni bora kuliko wote katika taifa hili, na yeye ni mpaka wa Pepo na Jahanamu, ni Siddiq na Farooq wa Umma na utibitisho wa ujuzi wa mambo ya dini ya taifa hili.” Waliposikia maelezo haya kutoka kwake wanafiki hao waligeuza nyuso zao na kutazama upande mwingine na kukanusha tamko lake na kumwita muongo. Haraka Abu Amamah alinyanyuka na akaenda kwa Mtukufu Mtume na kumwambia alichosema Abu Dharr, na jinsi kundi hilo lilivyokataa kukubali. Mtukufu Mtume akasema, “Hapana mtu kati ya ardhi na mbingu ambaye ni mkweli kuliko Abu Dharr.”

Kitabu hiki hiki kimeeleza kupitia mamlaka nyingine kwamba mtu mmoja alimuuliza Imamu Jafar al-Saqiq endapo hadhithi hiyo ilikuwa sahihi ambamo Mtukufu Mtume ametangaza hivyo. Imamu alisema, “Ndio.” Akasema, “Kama ndio hivyo, Mtukufu Mtume, Ali, Imamu Hasan, na Imamu Husein na nafasi yao ni ipi?”

Imamu akajibu, “Sisi ni kama mwezi wa Ramadhani ambao ndani mwake upo usiku huo ambao ibada yake ni sawa na ile ya miezi elfu moja ambapo masahaba ni sawa na mwezi unao heshimika ikilinganishwa na miezi mingine, na hapana mtu anayeweza kulinganishwa na sisi, Ahlul-Bait.”

Ni dhahiri kama mwanga wa mchana kutoka kwenye hadithi hiyo hapo juu ya Mtukufu Mtume kwamba Abu Dharr alikuwa hana wa kumlinganisha naye katika ukweli.

Maelezo na ufafanuzi wa hadithi hii hii kama yalivyotolewa na Subaiti inaeleza kwamba Abu Dharr ataondoka hapa duniani akiwa katika hali ile ile ambayo Mtume alimwacha nayo, na atamuona akiwa katika hali hiyo hiyo huko Peponi.

Kama hadithi hii ikitazamwa kwa umakini zaidi, msimamo imara wa Abu Dharr kwenye njia ambayo iliimarishwa na Mtukufu Mtume unadhihirisha uadilifu wake.

Wanavyuo wanakubaliana kwenye mtazamo huu kwamba Abu Dharr hakutetereka hata nchi moja kutoka katika njia ya Mtukufu Mtume. Baada ya Mtume, hata sabaha kama Salman alilazimishwa kutoa kiapo cha utii na siku moja alipigwa sana ndani ya msikiti hadi shingo yake ikavimba. Lakini Abu Dharr kamwe hakunyamaza.

Allamah Subaiti ameandika: “Abu Dharr alikuwa mmojawapo wa wafuasi wa Mtukufu Mtume ambao walishika njia yao na walisimama imara kuhusu agano lao walilofanya na Mwenyezi Mungu, Ali, na Mtukufu Mtume kwa uaminifu, alifuata nyayo zake na kuiga mwenendo wake. Hakuachana na Imamu Ali hata kidogo, alimfuata hadi mwisho na akapata faida ya nuru ya ujuzi wake.”

Allamah Majlis ameandika: “Bin Babwayh anaeleza kupitia kwa mamlaka ya kuaminika kutoka kwa Imamu Ja’far al-Sadiq kwamba siku moja Abu Dharr alikuwa anapita karibu na Mtume wakati Jibril alikuwa anazungumza naye katika faragha katika umbile la ‘Dahyah Kalbi.’

Abu Dharr alirudi nyuma kwa kudhani kwamba Dahyah Kalbi alikuwa anazungumza na Mtume kwenye faragha. Aliporudi Jibril alimwambia Mtume, “Ewe Muhammad! Abu Dharr alikuja muda mfupi uliopita na akarudi bila kunisalimia.

Amini kwamba endapo angenisalimia, hakika ningejibu salamu yake. Ewe Muhammad! Abu Dharr anayo dua yake ambayo inajulikana kwa watu wa Peponi. Tazama! Nitakapoandoka kwenda mbinguzi muulize kuhusu taarifa hii. Akasema, “Vema.”

Jibril alipoondoka na Abu Dharr akarudi kwa Mtume, Mtume akasema; “Ewe Abu Dharr! Kwa nini hukutusalimia ulipokuja hapa muda mfupi uliopita? Abu Dharr alijibu, Nilipokuja, Dahyah Kalbi alikuwa ameketi na wewe na mlikuwa na mazungumzo. Nilidhani mnazungumza kuhusu mambo fulani ya siri na mimi sikuona vema kuingilia kati.

Kwa hiyo nikarudi. Mtukufu Mtume akasema, “Huyo hakuwa Dahyah Kalbi lakini huyo alikuwa Jibrili aliyenijia katika umbile la Dahyah Kalbi. Ewe Abu Dharr! Alikuwa ananiambia kwamba endapo ungemsalimia naye angejibu salamu yako.

Pia aliniambia kwamba unayo dua ambayo inajulikana sana miongoni mwa watu wa Peponi.” Abu Dharr aliondoka akiwa na haya sana na akaonyesha kujutia kitendo chake.

Halafu Mtukufu Mtume akasema, “Ewe Abu Dharr! Niambie dua unayosoma na ambalo linazungumziwa sana mbinguni” Abu Dharr akamwambia Mtume “Dua hiyo ni hii ifuatayo:

Allahumma inni Asalukal Amna wal Imana bika wat tasdiqa bi nabiyyika wal ‘Aafiyata min jami’il blaa’i’ washukra ‘alal ‘afiyat wal ghina’an shirarin naasi.” (Hayatul Qulub, Juz.1, uk. 166, Rabiyl Abrar, sura 23 iliyoandikwa kwa mkono, Mamba’us Sadiqin).

Zipo hadithi nyingi sana upande wa madhehebu ya Shia na Suni ambamo maagizo maalum yametolewa kuwapenda masahaba wanne. Wanavyuo wanasema kwamba masahaba hao wane ni Ali, Abu Dharr, Miqdad na Salman.

Umar Kashi ameandika kwenye Rijal yake, Abu Jafar Qummi kwenye Khasail, Abdullah Humayri kwenye Qurbul Asnad, Shaykh Mufid kwenye Iktisas, Ayashi kwenye maelezo yake, Saduq kwenye Uyun Akhbar al-Riza, Abdul Barr kwenye Istiab, Bin Sad kwenye Tabaqat na mwandishi wa Usudul Ghabah kwenye kitabu chake:

Mtukufu Mtume (s.a.w) amesema kwamba Mwenyezi Mungu amemuagiza kuwaweka masahaba wangu wanne kuwa marafiki zangu na niwapende, na pia nimeambiwa kwamba Yeye pia amewafanya marafiki masahaba hawa: Ali bin Abi Talib, Abu Dharr Al-Ghifari, Miqdad bin Al-Aswad na Salman Farsi (Mishkat Sharif uk. 572).

Hadithi inasema kwamba hao masahaba wanne ni Salman, Abu Dharr, Miqdad na Ammar. Wanachuo wanafikiria kwamba hawa masahaba wanne ambao Pepo na wakazi wa Pepo wanawapenda sana. Inasimuliwa kwenye hadithi kwamba mtangazaji atatangaza mnamo siku ya Hukumu, “Wako wapi hao masahaba wa Muhammad bin Abdullah ambao hawakuvunja ahadi yao ya kuwapenda Ahlul Bait al-Risalah, lakini walikuwa imara kuendelea nayo?” Salman, Miqdadi, na Abu Dharr watasimama.

Allamah Nuri ameandika kwa kumnukuu Raudhatul Waidhin cha Shaykh Shahia Muhammad bin Ahmad bin Ali bin Fital Naishapuri kwamba Imamu Muhammad al-Baqir amesema, zimo daraja kumi za imani. Miqdad amepata daraja nane, Abu Dharr amepata daraja tisa na Salman amepata zote kumi.

Dhamana ya udugu inakumbusha hilo tukio la kihistoria ambalo Mtukufu Mtume aliasisi udugu katika jozi moja ya masahaba wake kabla na baada ya kuhamia Madina.

Kabla ya Hijiriya aliasisi dhamana ya udugu baina ya kila masahaba wawili ili kwamba waweze kuhurumiana kwenye udugu huu alifikiria mfanano wa tabia wa masahaba wawili. Aliwafanya hao masahaba wawili kuwa ndugu wa kila mmoja kwa kuwa tabia zao zilikuwa zinafanana na kulingana kwa mwenendo. Kwa njia hii alitangaza udugu kati ya Abu Bakr na Umar, Talhah na Zubayr, Uthman na Abdur Rahman bin Auf, Hamza na Zayd bin Harith, Salman na Abu Dharr na Ali na yeye Mtume.

Halafu baada ya miezi mitano au minane, baada ya Hijiriya, Mtume (s.a.w) kwa mara nyingine aliasisi dhamana ya udugu kwa njia ile ile. Ilikuwa muhimu kuanzisha udugu baina ya wahamiaji na wenyeji wa Madina kwa lengo la kujenga misingi ya kuhurumiana baina yao. Mtume alianzisha udugu miongoni mwa masahaba hamsini.

Allamah Sahibli Nomani ameandika: “Kwenye himaya ya Uislamu yapo maadili na tabia safi sana. Ilikuwa ikizingatiwa kwamba masahaba ambao walipewa dhamana ya udugu baina yao walikuwa na mfanano wa upendo. Muungano huu wa upendo baina ya mwalimu na mwanafunzi ni muhimu kwa lengo la usilimishaji wa ujuzi. Baada ya kupima ilionekana kwamba muungano huu wa upendo wa watu hao wawili waliofanywa ndugu ulizingatiwa, tunaona kuwa ni vigumu kujua upendo wa mamia ya watu kwa muda mfupi, hivyo lazima tukubali kwamba uamuzi wa Mtukufu Mtume ulifanyika kwa sifa maalumu ya Utume. (Siratu Nabi, Juz. 1, uk. 112)

Juu ya hayo, hili pia linafaa kukumbukwa kwamba Mtume hakupata mtu mwenye upendeleo unaofanana na ule wa Ali ama miongoni mwa Muhajirina (wahamiaji) au Ansari. Ali akasema, “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu umeniunganisha na nani?” Akasema, “Wewe ni ndugu yangu hapa duniani na baada ya hapa duniani (Peponi)”

Ndio maana ya Ali alitangaza mara kwa mara kwenye mimbari ya Msikiti wa Kufa, “Mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu na ndugu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu.” (Tarikh Abul Fida, Juz. 1, uk. 127) Mtukufu Mtume pia alisema kuhusu Salman, “Salman ni mmoja wetu sisi Ahlul Bait.”

Kwa maoni yangu hii pia ni mojawapo ya sifa bora za Abu Dharr kwamba mtu mwenye uamuzi uliokomaa kama Mtukufu Mtume alimtangaza kuwa ndugu yake Salman. Allamah Subaiti amenukuu usemi wa Saleh al-Ahwal ambaye alimsikia Imamu Jafar al-Sadiq akisema kwamba Mtukufu Mtume alianzisha dhamana ya udugu baina ya Salman na Abu Dharr na alimwambia Abu Dharr asije akampinga Salman. (Abu Dharr al-Ghifar uk. 86, Kama ilivyonukuliwa na Usulul Kafi).

Hadith ya Abu Dharr ni ya juu sana hivyo kwamba aya za Quran Tukufu zimeteremshwa kwa ajili ya kumsifu yeye. Moja ya Aya hizo ni kama ilivyonukuliwa hapa chini:

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ نُزُلًا{071}

“Hakika wale walioamini na wakatenda mema mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo ya Firdausi.” (Surah 18:107).

Imamu Jafar al-Sadiq anasema kwamba Aya hii imeteremshwa kuhusu Abu Dharr, Miqdadi, Ammar na Salman.

Kwa mujibu wa hadithi, Mtume alisema kwamba Mwenyezi Mungu alimuamuru ampende Salman, Abu Dharr, Miqdadi na Ammar na akaongeza zaidi kwamba yeye mwenyewe aliwafanya marafiki zake.
Kwa mujibu wa hadithi nyingine Mtume alisema, “Pepo inayo shauku na watu hawa.” (Hayatul Qulubi, Juz.2)

Allamah Gilani ameandika kwamba heshima ya Abu Dharr na hadhi yake ni hali zilizoongezeka sana siku hadi siku katika mazingira ya Mtume, hivyo kwamba, Mtukufu Mtume alipokwenda kwenye Vita ya Zaat al-Ruqa1 alimfanya yeye kuwa mtemi wa Madina, na si yeye tu kuwa mtemi lakini kwa ajili yake wakati fulani Ghifari wengine pia walipata cheo hiki. Mathalani, Mtukufu Mtume alimteua Saya’ bin Urfah al-Ghifari kama Mtemi wa Madina wakati wa Vita ya Daumatul Jandal, (Zaadul Ma’ad).

Ilikuwa kawaida ya huko Arabuni kwamba wakati wowote ilipotokea mtu anapanda ngamia alimfanya mtu wake maalumu kuwa ‘sanjari’ wake. Sanjari alipoketi nyuma, alikuwa akishika hatamu kwa kuzungusha kiunoni. Kwa mujibu wa hadith hii ya kawaida Mtukufu Mtume pia alimfanya mtu kuwa Sanjari wake.

Wakati wa hija ya mwisho, Sanjari wake alikuwa Fazal bin Abbas bin Abdul Muttalib.

Masahaba waliona kuwa ni heshima kuwa Sanjari. Sanjari wa Mtume aliitwa ‘Radifun Nabi.’ Wasomi wanasema kwamba Mtume zaidi alimpa heshima hii Abu Dharr. Mtume alikuwa na desturi ya kupanda wanyama wengine wadogo.

Punda pia mara nyingi walitumika kumbeba Mtume. Alikuwa na tabia ya kumruhusu Abu Dharr kukaa nyuma yake na waliendelea na safari huku wanazungumza. (Tabaqat Ibn Sa’d).
Shah Walyullah Dehlavi, anapoelezea ghasia kwenye Uislamu, ameandika kuhusu tukio la Harrah. Abu Dawudi amemnukuu Abu Dharr ambaye alisema, “Siku moja niliketi nyuma ya Mtukufu Mtume tukiwa tumepanda punda.

Tulipokuwa nje ya Madina- sehemu isiyokaliwa na watu, aliniuliza hali yangu ingekuwaje wakati njaa itakapoikumba Madina, na ningeshindwa kuvumilia kabla ya kufika msikitini baada ya kutoka kitandani mwangu.” Nikasema, “Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanajua zaidi.”

Akasema, “Ewe Abu Dharr! Usije ukaenda kuomba wakati huo.” Halafu akasema, “Hali yako itakuwaje ambapo bei ya kaburi italingana na ile ya mtumwa kwa sababu ya kiasi kikubwa cha vifo?” Nikasema. “Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanajua zaidi.” Akasema, “Ewe Abu Dharr! Jizoeze uvumilivu.”

Halafu aliuliza tena, “Ewe Abu Dharr! Hali yako itakuwaje ambapo patatokea mauaji ya halaiki hapa Madina hivyo kwamba mawe na mchanga vitaloa damu?” Nikajibu, “Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanajua zaidi.” Alisema, “Wakati huo utatakiwa ukae nyumbani kwako.”

Nilimuuliza, “Itabidi nishike upanga wakati huo?” Alijibu, “Kama ukifanya hivyo utafikiriwa kuwa ni mshirika wao.” Halafu nilimuuliza, “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Nifanye nini wakati huo?” Alisema, “Hata kama unaogopa kwamba mng’ao wa upanga utafanya macho yako yasione vizuri, funika uso wako tu kwa kipande cha nguo yako na usipigane, lakini nyamaza kimya.”

Maelezo haya yapo ukurasa wa 176 kwenye Juzuu ya 5 ya Musnad Ahmad bin Hanbal iliyochapishwa Misri. Kwamba Mtukufu Mtume alikuwa na kawaida ya kumdokeza Abu Dharr siri zake na akasema kwamba alikuwa anamwamini sana. Abu Dharr naye pia, alikuwa mwangalifu sana kuficha siri hizo. Wakati wowote alipoulizwa kuhusu Hadith, alisema, “Isipokuwa mambo yale ambayo Mtukufu Mtume ameniambia kuwa ni siri, nipo tayari kukueleza kila kitu. Unaweza kuniuliza chochote unachotaka.”

Sura Ya Saba

Zipo nasaha nyingi ambazo Mtume alimpa Abu Dharr. Hapa tunadokeza kuhusu chache miongoni mwao. Muhammad Harun Zangipuri ameandika ka mujibu ya mamlaka ya ‘Amali’ ya Shaykh Tusi kwamba Mtume alimwambia Abu Dharr:

“Ewe Abu Dharr! Muabudu Mwenyezi Mungu kama vile unamuona Yeye, na Yeye Anakuona wewe na hata kama humuoni wewe.”

“Tambua kwamba kwanza kabisa ibada Yake ni kumtambua, yaani kuelewa kwamba Yeye ni wa kwanza kabla ya chochote. Yeye hana mshirika. Yeye ni wa Milele hana mwisho.”

“Yeye ni Muumbaji wa vitu baina ya ardhi na mbingu. Yeye Ametakasika na yumo kila mahali. Yeye hahusiki na dosari yoyote, na ni Muumbaji wa vitu vyote.”

“Baada ya kuelewa Upweke wa Mwenyezi Mungu ni muhimu kukubali Utume wangu na kuamini, kwamba Mwenyezi Mungu amenituma kama mjumbe wa habari njema, mwonyaji na taa nyeye nuru ya mwongozo kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu.”
“Baada ya kukubali Utume wangu, ni wajibu na muhimu kuwapenda Ahlil-Bait wangu ambao Mwenyezi Mungu ameweatakasa kutokana na uovu wote.

“Zingatia kwamba vimo vitu viwili vyenye neema: Afya njema na fursa ya kufanya ibada.”

“Vithamini vitu vitano kabla ya vitu vitano:

    • Thamini ujana kabla hujazeeka,

    • Afya njema kabla ya kuugua maradhi,

    • Utajiri kabla ya umaskini,

    • Starehe kabla ya kazi na

    • Uhai kabla ya kifo. Ishi duniani kama mgeni au pitisha siku zako

kama mpita njia.

“Unapoamka asubuhi, usiwe na matumaini ya kuiona jioni, na baada ya kupitisha usiku usiwe na tegemeo la kuiona asubuhi. Chukua nafuu ya afya yako njema (kwa ajili ya kuabudu kabla hujaugua na tumia maisha (katika njia ya Mwenyezi Mungu) kabla hujafa, kwa sababu hatujui watu watatuitaje kesho tukiwa hai au tumekufa”

“Uwe bahili kuhusu maisha yako kuliko pesa zako. Kwa maneno mengine, kama vile unavyotumia fedha zako kwa kujinyima na unajaribu hutaki kutumia kitu chochote isivyofaa kwa njia ile ile, unatakiwa kuwa bahili kuhusu maisha yako na jaribu kutofuja katika matendo ya uovu.”

“Mnamo siku ya Hesabu, Mwenyezi Mungu atawapia jicho baya kupita kiasi la kutoridhika hao Maulamaa ambao ujuzi wao haukuwanufaisha watu, au ambao wamepata ujuzi kwa lengo la kupata heshima ya kidunia bila kumnufaisha yeyote. Maulamaa wa aina hiyo, hawatanusa manukato ya Pepo”

“Wakati wowote unapoulizwa kuhusu kitu ambacho hukijui, kiri ujinga wako wazi wazi. Tazama usitoe uamuzi kuhusu jambo usilolijua.”

“Siku inakuja ambapo baadhi ya wakazi wa Peponi watawaambia baadhi ya wakazi wa Jahanamu, “T tumeingia Peponi kwa sababu ya mafundisho yako na nasaha, lakini wewe umeingia Jahanamu?” Watajibu kwa kusema, “Tuliwaagiza wengine kufanya wema lakini sisi hatukufanya hivyo sisi.”

“Mwenyezi Mungu anazo haki nyingi juu yako. Ili uweze kuzitambua unatakiwa kuomba msamaha wake wakati wa kulala na unapoamka asubuhi.”

“Kifo kinakutafuta wewe na kinaweza kuja wakati wowote. Kwa hiyo, unatakiwa kufanya mambo mema na uharakie kufanya hivyo, na sikiliza! Mtu huvuna anachokipanda. Ngano huzaa ngano na shairi huzaa shairi. Usisahau adhabu ya matendo yako.”

“Watu wanaojihini ni makamanda na wanasheria ni viongozi, kuna manufaa yasiyo na mwisho kuwa karibu nao.”

“Muumini anafikiria dhambi kuwa mzigo mkubwa kama mlima. Anahisi kama vile anakandamizwa na mlima.”

“Lakini asiye muumini anafikiria dhambi kama inzi kwenye pua yake.”

“Usiangalie udogo wa dhambi lakini angalia unafanya dhambi hiyo kinyume cha matakwa ya nani.”

“Mtu ambaye ni muumini anawasiwasi zaidi katika dunia hii kuliko ndege aliye nasa kwenye mtego wako. Anataka aondoke duniani haraka iwezekanavyo.”

“Si vema kuingilia katika kila jambo na unatakiwa kudhibiti ulimi wako kwa namna ile ile unavyo linda chakula chako.”

“Mwenyezi Mungu amezifanya Swala kuwa utulivu wa macho yako. Ewe Abu Dharr! Mtu mwenye njaa hula chakula hadi anashiba na mwenye kiu hunywa maji hadi anatosheka, lakini mimi sitosheki na Swala.”

“Almuradi unaswali, wewe ni kama vile unagonga mlango wa Mfalme kamili, unatakiwa utambue kwamba, kwa kugonga mlango huo mfululizo, hatimaye mlango huo hufunguka.”

“Usiifanye nyumba yako kama kaburi. Nyumba ambamo haisaliwi Swala imeenea giza kama kaburi. Unatakiwa kufanya mpango wa kuweka nuru kwenye kaburi lako kwa kusali ndani ya nyumba yako kwani unaposali ndani ya nyumba yako, unatia nuru kwenye kaburi lako.”

“Sala ni nguzo ya imani na sadaka hutakasa dhambi, lakini kudhibiti ulimi wako ni jambo la muhimu zaidi kuliko hayo mawili.”

“Mtu mwenye moyo mgumu hawezi kumkaribia Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, unatakiwa kuwa na moyo wa huruma.”

“Mkumbuke Mwenyezi Mungu Katika hali ya Khumul. Nilimuuliza, “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Khumul ni nini?” Akajibu, “Maana yake ni kumkumbuka mwenyezi Mungu katika faragha.”

“Mwenyezi Mungu anasema: “Mja wangu ni yule anayeniogopa. Nitamfanya mtu wa aina hii asiogope siku ya Hukumu, ikiwa ananiogopa Mimi. Hatakuwa na fadhaiko siku ya ufufuo badala yake atakuwa na amani.”

“Mwenye akili ni yule ambaye hunyenyekea na kufanya matendo kwa ajili ya kuingia Peponi; Na asiye na msaada na mpumbavu ni yule anayefuata matamanio ya kidunia na hajali Pepo.”

“Dunia na watu wa dunia wamelaaniwa. Ni vitu hivyo tu ambavyo vimetumika katika njia ya Mwenyezi Mungu, vinaweza kuwanufaisha watu wa dunia.”

“Mwenyezi Mungu alimfunulia ndugu yangu, Mtume Isa, “Ewe Isa! Usiipende dunia kwa sababu ni mahali pa marejeo. Kila mtu atarejea hapo na atatakiwa kutoa maelezo ya matendo yake hapo. Thawabu za matendo mazuri zitakuwa nzuri na adhabu itatolewa kwa matendo maovu.”

“Mwenyezi Mungu ataujaza busara moyo wa mtu anayejinyima. Ataupatia ulimi wake uwezo wa kujieleza kwa ufasaha, atamwonyesha maovu ya dunia na jinsi ya kuyaepuka na atamnyanyua kutoka hapa duniani kwa namna ambayo kwamba atafika kwenye nyumba ya amani (Darus-Salaam) kwa jinsi inayostahili.”

“Mwenyezi Mungu kamwe hakuamuru kukusanya utajiri. Badala yake Ameagiza Aabudiwe Yeye. Kwa hiyo, unatakiwa kuwa mchaji Mungu, rukuu mbele Yake na uendelee kumuabudu Yeye hadi mwisho wa uhai wako.”

“Mimi huvaa nguo za kawaida, huketi kwenye ardhi na hupanda punda asiye na mito ya kukalia. Sikiliza! Unatakiwa kuwa mfuasi wangu na ufuate Sunna zangu. Mtu anayekataa Sunna zangu, hata hesabiwa miongoni mwa watu wangu.”

“Nawapongeza watu wanao hiji ni ambao hawajali mambo ya dunia na wanaielekea Pepo; ambao hukaa chini kwenye ardhi, na huifanya ardhi kuwa zulia na maji yake kuwa safi; watu ambao wanacho kitabu cha Mwenyezi mungu Qurani Tukufu kuwa kigezo chao na maombi kuwa heshima yao, na hujitenga na dunia.”

“Bidhaa za dunia ni watoto na utajiri, na bidhaa za Peponi ni matendo mema.”

“Muogope Mwenyezi Mungu na usiwajali watu. Watu watakuheshimu wewe pia ikiwa utamuogopa Mwenyezi Mungu.”

“Nyamaza kimya unapoona maiti imebebwa, au unapokuwa na maiti. Pia nyamaza mapigano yanapoendelea na pia unyamaze wakati Quran Tukufu inaposomwa.”

“Chumvi huhifadhi kila kitu kisioze, lakini chumvi ikiharibika, hakuna marekebisho (Hadith hii inahusu wanavyuo na maana yake ni kwamba imani huharibika pale ambapo wanavyuo kuwa waovu).”

“ Swala mbili fupi zikisaliwa kwa uaminifu na tafakuri ni bora zaidi kuliko Swala za usiku moja zilizosaliwa bila uaminifu.”

“Jiite na ujifanye unahesabiwa matendo yako mnamo Siku ya Hesabu. Kusali bila matendo mema ni sawa na kutupa mshale bila lengo.”

“Mtu anaposali angalipo porini, Mwenyezi Mungu huwaamuru Malaika kusimama katika safu na kusali nyuma yake na kusema Amin baada ya Swala yake alimuradi Adhan imeadhiniwa na Swala imekimiwa kabla ya Swala.”

“Endapo mtu anasali Swala bila ya wito huo uliotajwa hapo juu, malaika wawili tu kuamuriwa kushiriki katika Swala hiyo.”

“Kumkumbuka Mwenyezi Mungu miongoni mwa watu wazembe ni sawa na kupigana kwenye uwanja wa vita. Kuwa na watu wazuri ni bora zaidi kuliko kukaa katika upweke na upweke ni bora zaidi kuliko kuwa miongoni mwa watu wabaya.”

“Kila wakati fanya urafiki na waumini, kula na kunywa na watu wanao jinyima.”

“Mwenyezi Mungu yu karibu na ulimi wa kila msemaji kila wakati. Kwa hiyo mfikirie Mwenyezi Mungu unaposema.”
“Kwa uwongo inatosha kwamba mtu husema chochote asikiacho. Ni muhimu kudhibiti ulimi moja kwa moja.”

“Mwenyezi Mungu humpenda mtu anayeheshimu ujuzi, wanavyuo, Waislamu wakongwe, wafuasi wa Qurani Tukufu, na mtawala mwenye haki.”

“Zilinde na uzifuate amri za Mwenyezi Mungu. Naye atakulinda na utamuona Yeye yu mbele yako. Mkumbuke Yeye wakati wa furaha naye atakukumbuka wakati wa shida na atakukomboa kutoka humo.”

“Kama unahitaji kitu, omba kutoka kwake tu. Hakuna atakaye kudhuru hata kama dunia yote itakuwa adui yako, almuradi Mwenyezi Mungu hana ugomvi na wewe. Hutaweza kunufaika hata kama watu wote kwa kuungana pamoja wanataka kukunufaisha wewe isipokuwa Mwenyezi Mungu aridhie hivyo. Mwenyezi Mungu hukusaidia wewe ukiwa kwenye uvumilivu. Ni Yeye ndiye anayekuondolea maumivu yako. Kila mara kuna faraja baada ya shida.”

“Mwenyezi Mungu haangalii nyuso zenu au utajiri wenu; Yeye hutazama nia zenu na matendo yenu.”

“Sifa za muumini ni kuwa na amani, kuonyesha staha na kumkumbuka Mwenyezi Mungu katika hali yoyote ile. Aliyelaaniwa ni yule anayesema uwongo kwa watu kwa madhumuni ya kuchekesha tu.”

“Epukana na usengenyi kwa sababu hilo ni tendo ovu zaidi ya zinaa. Nikauliza, “Vipi Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” Mtume alijibu, “Mzinzi akitubu, Mwenyezi Mungu hukubali toba yake lakini dhambi ya kuteta (kusenyenya) haisameheki hadi mtu ambaye ametetwa (amesengenywa) anaisamehe.”

“Mtu anayemtukana muumini ni mwovu na mtu anayepigana na muumini ni kafiri, na akimsengenya muumini maana yake ni kwamba anakula nyama ya anayemsengenya na kwa hivyo ni mwovu mkubwa; na mtu anaye linda mali ya muumini ni sawa kama vile analinda maisha yake.”

Mimi nilisema, “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Kusengenya ni nani?” Akasema, “Kumtaja ndugu yako kwa mabaya yake ambayo hangependa kutajwa kwayo.” Mimi nikasema, “Hata kama anazo sifa hizo?” Akasema, “Hiyo ni kusengenya, kwa kweli; lakini, kama ukimsingizia mambo asiyo kuwa nayo, hiyo ni usingiziaji ambao adhabu yake ni tofauti.”

“Mwenyezi Mungu atamzawadia thawabu ya kwenda Peponi endapo anamwondolea shida ndugu yake katika imani.”

“Qatat, hawataingia Peponi.” niliuliza, “Ni nani hawa Qatat?” Alijibu, “Hawa ni wasengenyaji.”

“Mtetaji hataweza kukwepa adhabu ya Mwenyezi Mungu huko Akhera.”

“Msaliti atakwenda Jahanamu.” kutoa siri ya rafiki yako ni usaliti. Endapo mtu anakufa kabla ya kuhisi toba baada ya kuonyesha majivuno hata mara moja tu, hatanusa harufu ya Pepo.”
“Mwenye mashati mawili, yeye atumie moja na la pili ampe ndugu yake ambaye hana shati.”

“Mtu anayeacha kuvaa nguo za gharama, pamoja na yeye kuwa tajiri, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, huko Peponi atapewa majoho kutoka kwa Mwenyezi Mungu.”

“Kabla ya majilio ya Mahdi. (Angalia ISP 1979,–The Awaited Saviour) watatokea watu watakaovaa nguo za sufi wakati majira ya joto na baridi, kuonyesha ubora wao kwa watu wengine. Mwenyezi Mungu atawalaani.”

“Dunia hii ni jela kwa muumini na Pepo kwa kafiri. Nia yako katika hali yoyote lazima iwe uaminifu. Hata kula na kulala kwako ni mambo ambayo unatakiwa uyafanye kwa makusudio ya uamifu.”

Kwa mujibu wa Hafidh Abu Naim, Kama inavyoelezwa kwenye kitabu chake, Huyatul Awlita Abu Dharr anasema: “Siku moja nilikwenda kwa Mtukufu Mtume alipokuwa amekaa msikitini. Nilikuwa hata bado sijaketi sawasawa, akiniambia, “Bado hujatoa heshima yako kwa msikiti.”

Nilimuuliza, “Kitu gani hicho bwana wangu!” Alijibu, “Rakaa mbili za Swala. Ewe Abu Dharr! Unapoingia msikitini haraka sana lazima swali Swala ya raka mbili.” Kufuatana na amri yake, mara moja nilisali Swala ya rakaa mbili.

Halafu niliuliza, “Nini msingi na dhamira ya Swala?” Alijibu, “Ni ibada bora kuliko zote.”

Halafu niliuliza, “Ni amali gani iliyo bora kuliko zote.” Alijibu, “kumwamini Mwenyezi Mungu na kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu hizi ni amali kuzidi zote.”

Nikauliza, “Ewe bwana! Ni waumini gani ambao imani yao inafikiriwa kuwa kamili?” Alijibu, “Ni hao ambao matendo yao ni mema na tabia zao ni nzuri.” akasema, “Ni hao ambao ndimi zao haziwasemi kwa ubaya na mikono yao haiwashambulii Waislamu wenzao”

Niliuliza, “Ni mambo gani mtu anatakiwa ayaepuke?” Alijibu, “Kujinyima na kuepuka kufanya dhambi.”

Nikauliza. “Ni Swala zipi zilizo bora kuliko zote?” Alijibu, “Ni Swala zile ambazo dua ndefu hukaririwa katika Qunuti,”

Nikauliza, “Ewe bwana! Kufunga swaumu ni nini?” Akajibu, “Ni ibada ya faradhi ambayo thawabu yake ni kubwa sana”

Niliuliza, “Ni jihadi ipi iliyo bora zaidi?” akajibu, “Ni hiyo ambayo miguu ya mnyama aliyepandwa hukatwa na aliyempanda mnyama huyo kuuawa.” Niliuliza, “Ni sadaka ipi iliyo bora zaid?”

Alijibu, “Ni sadaka ile iliyotolewa kutokana na malipo ya kazi ngumu.” Niliuliza, “Ewe bwana ni Aya gani miongoni mwa zile zilizofunuliwa na Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuzidi zingine?” Alijibu, “Ayat al-Kursi (aya za kiti cha enzi)

Nikasema, “Ewe bwana! Nipe nasaha zako.” Akasema, “Ninakushauri umwogope Mwenyezi Mungu kwa sababu huo ndio msingi wa amali njema.”

“Kariri Qurani Tukufu ambayo ni chanzo cha nuru kwako hapa duniani, na utajo wa upendeleo wako huko mbinguni.

“Usicheke sana, ukicheka sana moyo hukosa uhai na uso husinyaa. Uwe kimya kwa muda mrefu zaidi, kwani hali hii itakuepusha kwenye matatizo mengi.

“Uwe kipenzi cha watu fukara na uwe nao.

“Waangalie watu hao ambao kipato chao ni cha chini zaidi na usijilinganishe na watu ambao kiuchumi wapo juu zaidi.

“Wafanyie wema ahali zako, hata kama wanakudharau. Usijali lawama yoyote endapo tendo lako ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Sema ukweli hata kama unauma.

Kwa kuwa Mtukufu Mtume alikuwa na uwezo wa kubashiri mara kwa mara alitamka matukio na matatizo ambayo yangempata Abu Dharr katika maisha yake ya baadaye.

Imeandikwa kwenye Musnad ya Ahmad bin Hanbali kwamba siku moja Abu Dharr alikwenda msikitini na kulala baada ya mchoko wa mahubiri.

Mtume alikwenda msikitini kumliwaza na akaona kwamba alikuwa amelala. Mtume alimwambia kwa ishara ya kidole gumba chake na alisema: “Ewe Abu Dharr! Utafanya nini utakapofukuzwa kwenye msikiti?”

Abu Dharr alijibu, “Ewe bwana! Endapo hali inakuwa hiyo, nitachomoa upanga wangu na nitamkata kichwa chake mtu atakayefanya hivyo.”

Mtume akasema, “Ewe Abu Dharr! Usije ukafanya hivyo lakini uwe mvumilivu wakati huo; nenda popote utakapo pelekwa na uondoke uende huko utakapopelekwa.”

Allamah Muhammad Baqir Majlis ameandika kwamba siku moja Mtume alimwambia Abu Dharr, “Ewe Abu Dharr! Utaishi maisha ya upweke, na utakufa ukiwa peke yako.
Utafufuka mnamo siku ya Ufufuo ukiwa peke yako. Utafariki dunia ukiwa peke yako katika nchi ya ugenini. Baadhi ya watu wa Iraq wataikafini maiti yako, wataivisha sanda, na kukuzika.” (Anwarul Qulub).

Aidha ameandika kwamba siku moja Uthman na Abu Dharr walingia kwenye msikiti wa Mtume huku wakizungumza.

Hapo walimuona Mtume ameketi akiwa ameegemea kwenye mto. Wote wawili walikwenda kwake. Baada ya muda mfupi Uthman aliondoka hapo. Baadaye Mtume akasema, “Ewe Abu Dharr! Ulikuwa unazunguma nini na Uthman?” Abu Dharr alisema, “Tulikuwa tunazungumza kuhusu aya fulani ya Quran Tukufu.”

Mtume akasema, Ewe Abu Dharr! Haiko mbali siku ambapo wewe na Uthman mtatofautiana sana na wote nyinyi wawili mtakuwa wahasimu wakubwa. Wakati huo mmoja wenu atakandamizwa na mwingine atakuwa mkandamizaji. Abu Dharr! Usiache kusema kweli, hata kama ukifanyiwa udhalimu wa aina yoyote ile” (Hayatul Qulub).
Ilielekea zaidi kwamba aya iliyotajwa kwenye fungu la maneno hapo juu lilihusu suala la Zaka kwa sababu Allamah Subaiti akidokeza kwenye kitabu chake ameandika kwamba palitokea mazungumzo baina ya Uthman na Abu Dharr kuhusu suala la Zaka, ambalo lilisuluhishwa na Mtukufu Mtume (Hayatul Qulubi).

Waandishi wa historia na wahadithi wanakubaliana kwamba Abu Dharr alikuwa kwenye upeo wa uchaji Mungu. Alitumia maisha yake yote katika kuhubiri, na sababu ni kwamba alitoa kiapo cha utii kwa Mtukufu Mtume katika kipindi hicho hicho. Alisema kwamba hangemjali mtu yeyote mwenye kumshutumu kwa sababu inayohusiana na amri za Mwenyezi Mungu. Hotuba zake ni nyingi sana, baadhi ya hizo zimeatajwa hapa chini:

Kwa mujibu wa maneno ya Allamah Turayhi, Abu Dharr amesema mara nyingi kwenye mahubiri yake, “Enyi watu! Hata kama migongo yenu itajikunja na miguu yenu kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya kusali sana na huduma zingine za dini, haitawapeni manufaa isipokuwa muwapende Ahlul-Bait katika mioyo yenu.

Kwa hiyo mnatakiwa kwanza, muwapenhe watu wa nyumba ya Muhammad kwenye nyoyo zenu (kwa maelezo zaidi kuhusu “kuwapenda Ndugu” angalia Bwana na Ubwana, ISP, 1979, Majma’ul Bahrain uk. 356).

Allamah Subaiti ameandika kwamba siku moja Abu Dharr aliita kwa sauti kwenye mlango wa Al-Kaaba, “Enyi ndugu zangu! Njooni karibu yangu na msikilize kwa uangalifu.”

Waliposikia hivi watu walikusanyika karibu naye. Abu Dharr alisema, kila mmoja wenu hukusanya mahitaji kwa ajili ya safari yake na huanza safari yake baaada ya kukusanya mahitaji. Si rahisi kumuona mtu miongoni mwetu ambaye ataanza safari bila mahitaji. “Enyi ndugu zangu! Safari yenu kwenye siku ya Ufufuo ipo mbele yenu. Kwa hiyo, ni muhimu kwenu kukusanya mahitaji kwa ajili ya safari.”

Watu wakasema, “Ewe ndugu hapana shaka kuhusu safari ya kwenye Ufufuo, lakini hatujui tuchukue mahitaji gani?” Abu Dharr akasema, “Jambo linalohitajiwa katika safari hii ni Hija ya kutembelea Kaabah. Mahitaji yake ni kufunga Swaumu wakati wa siku za joto sana na kusali Swala ya rakaa mbili ili kuondoa hofu ya kaburi kwenye usiku wa giza.

“Enyi ndugu zangu! Fanyeni amali njema. Chunga ulimi wako usitamke maneno mabaya. Tumia utajiri wako katika kutoa Sadaka. Tumia siku za uhai wako katika kuitafuta Pepo, na tafuta njia za halali za kupata riziki. Ukipata dinari mbili, tumia moja kwa kumpa nduguyo na nyingine toa sadaka kwa ajili ya ustawi wa Pepo.

“Sasa sikilizeni! Maisha yenu yamegawanyika katika hatua mbili. Mojawapo ya hatua hizo imepita na nyingine inakuja. Fanyeni amali njema na jiepusheni na kutenda dhambi wakati huu uliopo kwa ajili ya hatua ijayo. Sikilizeni! Kama hamtafuata ushauri huu, bila shaka mtaangamia na mtalaaniwa huko Peponi.”

Mtu mmoja akamuuliza, “Vema! Tujulishe kwa nini hatupendi kifo?” akasema, “Kwa sababu mmeangamiza maisha yenu ya baada hapa duniani kwa sababu ya kupenda mambo ya kidunia. Mnajua kwamba hamkufanya lolote kwa ajili ya Pepo na mtapata matatizo huko.

Kwa hiyo inawezekanaje mtu apende kuondoka kwenda mahali, ambapo anajua kwamba haitakuwa vizuri yeye kufanya hivyo.”

Halafu akauliza, “Ni jinsi gani tutafikishwa mbele ya Mwenyezi Mungu?” Abu Dharr akajibu, “Wale waliofanya amali njema watakwenda Kwake kama msafiri ambaye amerudi nyumbani kwake, na wala waovu watafika huko kama mtoro aliyefikishwa hapo baada ya kukamatwa.”

Halafu, akauliza tena, “Hali yetu itakuwaje mbele ya Mwenyezi Mungu?” Abu Dharr alijibu, “Unaweza kuamua wewe mwenyewe. Yafanyie hukumu matendo yako kwa kuzingatia Kitabu cha Dini. Mwenyezi Mungu anasema: “Watu waadilifu watakwenda Peponi na waovu watakwenda Jahanamu.” Akauliza, “kama ndiyo hivyo, huruma Yake itatusaidiaje?” Abu Dharr alisema; “Mwenyezi Mungu tayari amekwisha sema kwamba, huruma Yake ni kwa ajili ya watu waadilifu.”

Mtu mmoja alimwandikia Abu Dharr, “Andika vitu vya ujuzi kwa ajili yangu.” Alijibu, “Mambo ya ujuzi ni mengi wala hayana mwisho. Ninaweza kukuandikia hadi wapi kuhusu ujuzi huo? Jambo moja tu la kuzingatia usimfanyie ubaya rafiki yako.”

Halafu aliandika, “Yupo mtu yeyote ambaye humfanyia ubaya rafiki yake?” Abu Dharr akaandika, “Ujipende wewe zaidi na usiwe na mtu mwingine yeyote ambaye utampenda kuliko unavyojipenda wewe mwenyewe. Kwa hali yoyote ile, ukimkosea Mwenyezi Mungu kwa kutenda dhambi, hakika utakuwa umejifanyia ubaya wewe mwenyewe.”

Pia, mahali pengine amesema, “Enyi watu! Mwenyezi Mungu amekuumbeni kama mwanadamu. Usijiteremshe daraja na kuwa hayawani na kuwa mnyama katili kwa kumkosea Yeye kwa kutenda dhambi.”

Allamah Shaykh Mufid ameandika; “Siku moja Abu Dharr alisema katika hotuba: “Utalipwa kufuatana na matendo yako. Utavuna kile ulichokipanda, yaani utapata thawabu kulingana na amali zako.

Ukifanya amali njema hapa duniani utapata thawabu nzuri Peponi na endapo unafanya matendo maovu utapata adhabu kulingana na hayo Ulimi wako ni ufunguo wa matendo mema na maovu.

“Unatakiwa kuuziba moyo wako kama unavyofunga pochi yako. Ni kwamba, kama unavyolinda utajiri wako, unatakiwa kuulinda moyo wako vivyo hivyo na jaribu kufanya kila uwezavyo usiruhusu uovu wowote usiingie humo. Mawazo yanayojikusanya humo lazima yawe safi.” (Amali, Shaykh Mufid)

Allamah Majlis ameandika: “Abu Dharr alikuwa na desturi ya kusema mihadhara yake na hotuba zake. Ewe mtafutaji wa ujuzi! Vitu vyote vya hapa duniani vinavyo hali moja katika hizi mbili. Uzuri wao unakunufaisha wewe au uovu wao unakudhuru wewe. Unatakiwa ukipende kitu chenye matarajio ya kukunufaisha.

“Ewe mtafutaji wa ujuzi! Upo uwezekano isije familia yako na utajiri wako vikufanye wewe usiwe mwangalifu wa maisha yako, kwa sababu ipo siku ambapo kwa hakika utatenganishwa na familia yako na rasilimali yako na utakapokaribia kuondoka, utakuwa kama mgeni ambaye ameishi na kundi la watu kwa usiku moja na kuondoka kesho yake asubuhi. Sikiliza! Umbali uliopo baina ya kifo na Ufufuo ni kama kuwa katika hali ya ndoto na kuamka haraka sana.”

“Ewe mtafutaji wa ujuzi! Peleka amali zako njema mapema kwa ajili ya siku hiyo ambapo utasimamishwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuhojiwa na kujieleza. Mnamo siku hiyo utapata thawabu za amali zako njema na utalipwa fidia kwa tendo lolote jema ambalo umelifanya hapa duniani.” (Hayatul Qulubi Juz. 2).

Sura Ya Nane

Masimulizi ya hadithi ni kitu chenye muhimu mkubwa. Wala si kila mtu anaruhusiwa kusimulia, ama kusikiliza simulizi zao. Ujuzi wa wahadithi ndio kipimo chake. Abu Dharr ni mmojawapo wa wasimulizi wa kuaminika, kutegemewa na wakweli ambao simulizi zao hazitiliwi shaka au kukataliwa. Amekuwa na Mtukufu Mtume kwa muda mrefu sana wa uhai wake. Kwa maelezo yake ni mengi sana miongoni mwa hayo, machache yameandikwa hapa.

Kuhusu Aya za Qurani Tukufu: Enyi mliamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, Mjumbe wake na “Ulil amr-i minkum,” Imamu Fakuddin Razi ametoa maelezo kwenye Tafsirul Kabir kwamba Aya hiyo inawazungumzia wale wasiokosea na Saiyid Ali Hamadani ameitaja katika Mawaddatul Kubra kwamba inawahusu wenye utakaso (Maimamu)Kumi na Wawili.

Lakini inahitaji kuthibitishwa na masahaba wa Mtume wenye kuheshimika kwamba Mtume mwenyewe alisimulia hadithi hiyo. Abu Dharr anasimulia kutoka kwa Mtume kwamba aya iliyotajwa hapo juu ilipofunuliwa, alimwomba Mtukufu Mtume amwambie majina ya Waku wa mambo ‘Ulil Amr. Aliwataja maimamu kumi na mbili. Baada ya kuwataja majina, Abu Dharr anatoa maelezo kwa ufupi kwamba mteule wa kwanza ni Ali na wa mwisho ni Imamu Mahdi.
(Yanabiul Mawaddah, Shaykh Sulayman Qandozy al-Hanafi na Riuzatul Ahbab).

Abu Ishaq Thalabi ameandika kwenye maelezo yake: “Siku moja Bin Abbas alikuwa anasimulia hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w) alipokuwa ameketi karibu na kisima cha Zamzam ambapo mtu mmoja aliyefunika uso wake alikuja hapo. Bin Abbas alinyamaza kwa muda. Mtu huyo alianza kusimulia hadithi ya Mtume Bin Abbas akasema, “Ewe mtu! Nina kuuliza katika jina la Mwenyezi Mungu uniambie kwa kweli wewe ni nani?”

Alifunua uso wake na akasema, “Enyi watu! Yule anayenijua mimi ananijua mimi, lakini yule asiyenijua mimi, anatakiwa anitambue kwamba mimi ni Abu Dharr Ghifari. Nimesikia kutoka kwa Mtukufu Mtume kwa masikio haya mawili ambayo yanaweza kupata maradhi na kuwa kiziwi kama sikukosea, na nimeona kwa macho haya mawili ambayo yanaweza kupofuka endapo mtasema uwongo kwamba Mtume alisema kuhusu Ali kwamba ni kiongozi wa watu waadilifu na muuaji wa watenda maovu. Mtu aliyemsaidia yeye alipata ushindi na yule aliye mtelekeza yeye naye alitupwa.”

Kufuatana na simulizi ya Abu Dharr Ghifari, Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Ali ni lango la ujuzi wangu mwongozo wa wafuasi wangu wa lengo lililosababisha nitumwe. Kumpenda yeye ni imani na kumfanyia uadui yeye ni unafiki na kuwa rafiki yake ni ibada.” (Arjahul Matalib uk. 604 kwa mamlaka ya Dailami).

Kwa mujibu wa simulizi ya Abu Dharr, Mtume alisema: “Mtu akiniheshimu mimi, anamheshimu Mwenyezi Mungu. Asiyeniheshimu mimi, hamheshimu Mwenyezi mungu.

Mtu anayemheshimu Ali, ananiheshimu mimi, na yule asiyemheshimu Ali haniheshimu Mimi.” (Arjahul Matalib Uk 606, kwa mamlaka ya Hakim).

Abu Dharr anasema; “Tulikuwa tunawatambua wanafiki kwa vitu vitatu: Kwanza kwa kumkana Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, mbili kwa kuacha kusali, na tatu kwa chuki yake dhidi ya Ali.” (Arjahul Matalib uk. 608 kwa mamlaka ya bin Shazan).

Ipo hadith ambayo imesimuliwa na Abu Dharr, kwamba Mtume alisema, “Ali ni lango la ujuzi wangu. Yeye ni msimulizi wa mambo hayo ambayo yamesababisha niteuliwe. Kumpenda Ali ni imani na kumchukia ni unafiki, na kumwangalia yeye ni ibada.”

Bin Abd al-Barr ameandika kwenye Istiab kwamba masahaba wengi wamesimulia hadithi hii ya Mtume: “Ewe Ali! Hapana yeyote atakaye kuwa rafiki yako isipokuwa muumini, na hapana yeyote atakayekuwa adui yako isipokuwa mnafiki.”
(Arjahul Matalid uk. 609 kwa mamlaka ya Dailami).

Abu Dharr amemnukuu Umm Salamah kwa kusema kwamba alimsikia Mtukufu anasema; “Ali yu mkweli na ukweli umo kwa Ali na Ali na ukweli hawatatengana hadi watakapofika kwenye Haudhi ya Neema (Arjahul Matalib uk. 699 kwa mamlaka ya Bin Marduyah)

Allmah Subaiti ameandika: “Abu Dharr amesema kwamba Mtume alimwambia yeye “Mtu anaye kubali imani kwa uaminifu huuweka moyo wake katika hali safi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, husema ukweli, huwa makini, anakuwa na tabia njema, hutumia masikio yake kusikiliza mambo mazuri, na hutumia macho yake kuona vitu vinavyostahili, atapata ukombozi.”

Abu Dharr anasema kwamba Mtume amesema: “Wafuasi wangu hawataneemeshwa endapo watafuturu kabla ya muda, na kuchelewa kula daku kabla ya alfajiri (muda wa kuanza kufunga wakati wa mwezi wa ramadhani).”

Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume anasema: “Furaha yangu ni kwamba dhahabu igawiwe kama sadaka hata kama ingekuwa kubwa kama Mlima Uhud.”
(Tafsir Bin Kathir uk. 61).

Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume amesema: “Ewe Ali! Mwenyezi Mungu ametufanya mimi na wewe kuwa mti mmoja. Mimi ni mizizi ya mti huo na wewe ni tawi lake. Mwenyezi Mungu atamtupa mtu Jahananu kwa kutanguliza uso wake, kama akikata Tawi Lake.” Aliendelea kusema, “Ali ni kiongozi wa Waislamu na Imamu wa wacha Mungu. Atawaua watakaovunja ahadi ya utiiifu kwake (watu wa Jamal), walio tengwa na jamii (makhawariji) na wakanushaji.” (Tafsir bin Kathir uk. 61).

Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume amesema; “Ali kwangu ni kama Harun alivyokuwa kwa Musa isipokuwa tofauti moja tu kwamba hapatakuwepo na Mtume badala yangu.” Hadithi hii imenukuliwa na masahaba wengine wengi, miongoni mwao wakiwemo Umar bin Khatab, Sa’d bin Abi Waqqas, Abu Hurayrah, Abdullah bin Mas’oud, Abdallah bin Abbas, Jabir bin Abdullah, Abu Said Khidri, Jabir bin Samrah, Malik bin Harith, Bara bin Azib, Zayd bin Arqam, Anas bin Malik, Abu Ayyub Al-Ansari, Aqil bin Abi Talib na kadhalika (Arjahul Matalib).

Allamah Abdul Mu’min Shablanji ameandika kwenye kitabu chake:‘Nurul Absar’ kwamba, Abu Dharr, ananukuu kutoka kwa Mtume ambaye alisema: “Kitendo kizuri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kumpenda yeye na kutofanya chochote kinyume na Ridhaa Yake..”

Abu Dharr anamnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w) akisema: “Unapokuwa na urafiki na mtu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mfahamishe.”

Abu Dharr anasimulia kwamba Mtukufu Mtume anasema; “Mtu anapokasirika, kama amesimama, ni vema aketi chini na endapo hasira haipungui, alale chini.” (Nurul Absar, Uk. 29).

Abu Dharr ananukuu hadithi ya Mtume kwamba Mwenyezi Mungu humpenda mtu anaye vumilia anapotendewa mabaya na jirani yake (Nurul Absar, uk. 32).

Abu Dharr anasema kwamba Mtume (s.aw.) ameagiza uchaji Mungu na kujinyima na alituomba tulinde dhamana, tusipite tunaomba kwa mtu yeyote, tusivunje uhusiano wa kimapenzi uliopo baina ya watu wawili, kumtendea wema mtu anayekutendea ubaya, na kumuogopa Mwenyezi Mungu kila mara katika jambo la wazi na siri (Nurul Absar, uk. 33).

Abu Dharr anasimulia hadith ya Mtume hivi: “Mwenyezi Mungu alifananisha Ahlul Bait na Safina ya Nuhu (Safinatu Nuh) kwa wafuasi wangu. Yeyote aliyepanda humo, aliokoka na yeyote ambaye hakupanda alikufa maji, yaani kwa usemi mwingine alikengeuka.

Pia Ahlul Bait wangu, wapo kama mlango wa kwendea toba (Hittab) kwa wafuasi wangu. Kuhusu wana wa Uyahudi ambao Mwenyezi Mungu aliwaambia kwamba mtu aliyeingia kupitia mlangoni, ataokoka kutokana na mateso ya dunia na Akhera. Vivyo hivyo, yeyote yule kutoka miongoni mwa wafuasi wangu akifuata njia ya Ahlul-Bait wangu na anaendelea kuwa imara katika kuwafuata, ataokolewa katika Siku ya Hesabu.” (Ainul Hayat).

Ali bin Shahab Hamadani anamnukuu Abu Dharr ambaye anasema kwamba alimsikia Mtukufu Mtume anasema; “Ewe Abu Dharr! Ali ni yeye ndiye atakayezigawanya Pepo na Jahanamu. Ewe Abu Dharr! Hakuna hata malaika moja aliyeweza kupata heshima ya kugawa Pepo kutoka kwenye Jahamanu. Tazama! Pepo ipo pale kwa ajili ya wanao muunga mkono yeye na amepewa ndugu kama mimi ambapo hakuna ndugu wa mtu yeyote kama mimi.”

Abu Dharr anamnuku Mtukufu Mtume akisema; “Mwenyezi Mungu ameimarisha Uislamu kupitia kwa Ali, Ali anatokana na mimi na mimi ninatokana na Ali, na Aya hii,

أَفَمَنْ كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِنْ رَبِّهِ وَيَتْلُوهُ شَاهِدٌ مِنْهُ وَمِنْ قَبْلِهِ كِتَابُ مُوسَىٰ إِمَامًا وَرَحْمَةً ۚ أُولَٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۚ وَمَنْ يَكْفُرْ بِهِ مِنَ الْأَحْزَابِ فَالنَّارُ مَوْعِدُهُ ۚ فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِنْهُ ۚ إِنَّهُ الْحَقُّ مِنْ رَبِّكَ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ{71}

“Basi mtu aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake Mlezi, inayofuatwa na shahidi anaye toka kwake na kabla yake kilikuwa Kitabu cha Musa kilicho kuwa mwongozi na rehema …” (11:17).
Imeteremshwa kuhusu yeye (Ali) mimi ninao uthibitisho katika Aya hii na Ali ni shahidi yangu” (Muwaddatul Qurba, uk. 78)

Kwa mujibu wa Abu Dharr, Mtume alimwambia Ali, “Ewe Ali! Mtu anayenitii mimi, anamtii Mwenyezi Mungu na mtu anayekutii wewe, ananitii mimi, na mtu asiyenitii mimi hamtii Mwenyezi na mtu asiyekutii wewe, hanitii mimi.” (Muwaddatul Qurba uk. 78 na Yanabiul Mawaddah, Shaykh Sulayman Qandozy).

Abu Dharr anasema kwamba siku moja alipokuwa kwenye Uwanja wa makaburi wa Baqi’ (Madina) na Mtume (s.a.w), ambapo alisema, “Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye anaoudhibiti wa maisha yangu kwamba yupo mtu miongoni mwenu ambaye atapigana kwa ajili ya fasiri iliyo sahihi ya Quran Tukufu, kwa namna ile ile niliyopigana mimi na wanao abudu miungu wengi wakati wa ufunuo wa Qurani, ingawa watakuwa wanakariri mfumo ya imani (Hapana Mungu ila Mwenyezi Mungu). Ambapo yeye (Ali) atapigana nao watu wataona si sahihi na watamkosoa rafiki ya Mwenyezi Mungu (yaani Ali) na watamkasirikia kwa sababu ya vita hii kama Mtume Musa alivyomkasirikia Khidhr kwa sababu ya kutoboa mashua, kumuua mtoto na kujenga ukuta, ingawa kutoboa mashua, kumuua mtoto na kujenga ukuta ni matukio yaliyotekelezwa kufuatana na amri ya Mwenyezi Mungu.” (Arjahul Matalib uk. 31).

Muhammad bin Yusuf Kanji Shafii amemnukuu Abu Dharr akisema kwamba Mtume alisema, Bendera ya Ali bin Abi Talib, kiongozi wa waumini, kiongozi mkuu wa wenye nyuso zing’arazo na mrithi wangu itanifikia mimi kwenye Haudhi ya Neema (kifay tut Talib).

Abu Dharr anasema kwamba alimuuliza Mtume, “Ni msikiti gani wa kwanza kujengwa hapa duniani? “ Akajibu, “Msikiti wa al-Haram ” Akasema, “Na baada ya huo?” Akajibu, “Msikiti wa Bayt al-Maqdis (Yerusalemu)” Halafu akasema, “Palikuwepo urefu gani wa kipindi?” Mtume alijibu, “Miaka arobaini.” (Tajrid Bukhari).

Imamu Bukhari amemnukuu Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume alisema, “Endapo kwa makusudi mtu anajihusisha na mtu mwingine kwamba ni baba yake ambapo sivyo, mtu huyo si muumini, na mtu, ambaye anajionesha kwamba yeye ni mtu wa jamii ambamo hana wazazi. Lazima ajitayarishe kufanya Jahanamu kuwa masikani yake.” (Tajrid Bukhari).

Sura Ya Tisa

Wataalamu wa historia na wahadithi wa madhehebu yote mawili (Shia na Sunni) wanakubaliana kwamba pale ambapo Mtume (s.a.w) alitaka kuanza safari yake ya kwenda kwenye hija yake ya mwisho, alitangaza waziwazi kwamba masahaba wote lazima wafuatane naye kwenye safari hiyo.

Baada ya tangazo hili, masahaba wa Mtume walianza kufika Madina kutoka sehemu zote. Pia aliwataarifu watu kwamba wale ambao hawangeweza kufika Madina, waende Makkah moja kwa moja ili wahiji pamoja naye.

Mtume aliondoka Madina tarehe 25 ya mwezi wa Zilqadah, mwaka wa 10 Hijiriya (Tarikh bin Alward). Masahaba wengi sana walianza safari naye tangu madina, pamoja na Salman, Miqdad, Abu Dharr na Ammar.

Alipofika Makkah, Mtume alitekeleza ibada zote za Hijja. Ahlul-Bait wake wote, wake zake na masahaba wote walikuwa naye katika Hijja. Alitoa hotuba wakati wa Hijja na akaorodhesha mambo yenye kuendeleza matumaini kwa wafuasi wake na akaeleza njia ambazo umma ungepita ili upate kukombolewa.

Alipomaliza Hijja Mtume aliondoka Makkah kwenda Madina. Kufuatana na masimulizi ya Muhadithi Dehlavi walikuwepo masahaba 124,000 au kwa mujibu wa taarifa ya Khawand Shah 125,000. (Izalatul Khifa, Juz. 1, uk. 514 na Rauzatus Safa, Juz. 2, uk. 215).

Alipofika sehemu iitwayo Ghadir Khum akiwa na masahaba wake, malaika Jibril aliteremsha ujumbe wa Mungu usemao:

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ مِنْ رَبِّكَ ۖ وَإِنْ لَمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ{67}

“Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu.” (5:67).

Baada ya amri hii ya wazi hapakuwepo na chaguo lingine sipokuwa yeye (Mtume) alifikisha ujumbe kwa watu.

Aliagiza mimbari itengenezwe kufuatana na hali halisi kwa kutumia mito ya kukalia kwenye ngamia! Baada ya hapo alimwambia Bilal wa Afrika, “Ewe Bilal! Waite watu na waambie masahaba wangu kwamba wale walioko mbele warudi na wale ambao bado wapo nyuma, wafanye haraka kuja mbele.”

Bilal aliita, Hayya ala Khairil Amal (Kimbilieni kwenye kitendo kilicho bora). Kundi lilikusanyika kuzunguka mimbari ya Mtume. Alipanda kwenye mimbari na baada ya hotuba ndefu sana alimwita Ali aende aliposimama. Halafu, akiwa ameshika mikono miwili ya Ali kwa mikono yake mwenyewe, alinyanyua mikono hiyo juu sana hivyo kwamba weupe wa kwapa za Ali ulionekana wazi. Halafu akasema; “Yeyote anayeafiki mimi kuwa mtawala na mlezi wake lazima pia amuafiki Ali kuwa mtawala na mlezi wake. Ee Mwenyezi Mungu! Uwe rafiki ya mtu ambaye ni rafiki yake Ali na uwe adui ya mtu ambaye ni adui yake Ali.”

Mara watu waliposikia taarifa hii walitamka kwa sauti kubwa kuonesha kumuuunga mkono. Mtukufu Mtume aliondoka kwenye mimbari na akamwamuru Ali kupokea hongera kutoka kwa masahaba kwenye hema la kijani.

Ali alipokea pongezi za kumrithi Mtume na aliwashukuru watu kwa kumpongeza. Imeandikwa kwenye Maarijun Nubuwwah kwamba, licha ya masahaba, wake zake Mtume pia walimpongeza Ali kwa kuwa mtawala na kiongozi wa umma wa Waislamu.

Kwa mujibu wa Tarikh bin Khalqami Mtume katika hotuba yake ya Ghadir iliweka wazi kuhuzu kuwa na sifa, fahari na kukubalika kwa Ali akasema kwamba Ali alikuwa na uhusiano sawa na yeye kama Harun alivyokuwa na Musa.

Ukifuatana na Mustadrak al-Hakim alisema, “Ninawaachieni vitu viwili vya thamani sana miongoni mwenu, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul Bait wangu. Hamtapotoka mkivishikilia vitu hivyo.” Maneno kama hayo yameandikwa kwenye Khasais an-Nasai. Kwa mujibu wa Rauzatul Ahbab, Mtukufu Mtume pia alisema, “Ee Mwenyezi Mungu!

Mfanye rafiki yako yule anayempenda Ali na uwe adui wa yule ambaye ni adui wa Ali na pia ielekeze kweli upande huo ambako Ali huelekeza uso wake.”

Imeandikwa kwenye Asbab al-Nuzul Tafsir Durrul Manthur, kwenye Tafsir Fatahul Bayan kilichoandikwa na Siddiq Hasan, kwamba Aya hii ‘Balligh’ imeteremshwa kuhusu Ali tu. Imeandikwa kwenye Sharh Bukhari Aini, Tafsir Gharaibul Qurani of Naishapuni, Tarikh bin Wazih, Kanzul Ummal na kadhalika, kwamba Aya ya ‘Balligh’ imeteremshwa kuhusu hadhi na ubora wa Ali.

Imeandikwa kwenye Tarikh Abul Fida kwamba baada ya kurudi kutoka Ghadir al-Khum, Mtukufu Mtume aliugua mwishoni mwa siku za Safar (Machi), 11, Hijiriya. Kwa mujibu wa Mishkat Sharif, sababu ya ugonjwa ilikuwa sumu ile ile iliyopelekwa huko Khaybar na ambayo ilionesha athari yake nyakati fulani. Imetaarifiwa kwenye Tarikh bin Alward kwamba aliwaomba masahaba wake wote kwenda na jeshi la Usmah bin Zayd na akasema kwamba alimteua Usamah kuwa ndiye kamanda wa jeshi.

Muhadithi Dehavi ameandika kwenye Madarij kwamba siku iliyofuata Mtukufu Mtume akiwa mahututi, alimkabidhi Usamah bendera ya vita na akamwomba aondoke aende kupigana na makafiri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Usamah alimpa bendera hiyo Buradah bin Khazib nje ya jiji na akamteua kuwa mbeba bendera ya jeshi. Akaanza safari yake kutoka Madina na akasimama ‘Jaraf’ sehemu ambayo ipo karibu na Madina hadi jeshi lilipokusanyika.

Pia Mtume aliagiza kwamba Muhajirina na Ansar isipokuwa Ali lazima wajiunge na jeshi la Usamah na kwenda naye. Baadhi ya masahaba walianza kulaumu kwamba Mtukufu Mtume alimteua mtumwa na kumweka juu ya Muhajirina na Ansari wenye vyeo vya juu.

Kwa hiyo walijiingiza katika ukosoaji wa wazi kuhusu suala hili. Taarifa hii ilipomfikia Mtukufu Mtume alihuzunika sana, na licha ya homa, alitoka nje ya nyumba yake akiwa amekasirika sana na alipanda kwenye mimbari. Hapo, aliwahutubia watu, “Enyi watu! Haya ni mazungumzo gani ambayo mmejiingiza kuhusu kuteuliwa kwa Usamah kama kamanda wa jeshi, kama mlivyofanya wakati wa Vita ya Motah ambapo baba yake Usamah aliteuliwa kuwa kamanda wa jeshi. Kwa jina la Mwenyezi Mungu Usamah anastahili kuwa kamanda kama alivyokuwa baba yake.”

Ni kwenye al-Milal wan Nahl kilichoandikwa na Shahristan na Hujajul Karamah kilichoandikwa na Sidiq kwamba Mtukufu Mtume aliwaambia masahaba kufanya matayarisho ya haraka kwa ajili ya jeshi la Usamah. “Alaaniwe mtu anaye pinga jeshi la Usamah!”

Kwa mujibu wa Madarijun Nubuwwah, Abu Bakr na Umar walibaki Madina na Usamah akaondoka na jeshi. Alipokaribia kuondoka mama yake alimwambia kwamba hali ya Mtume haikuwa nzuri. Alimshauri asiendelee na safari na hakwenda. Kwa mujibu wa Tarikhut Tabari, katika hali hiyo, Mtume aliagiza Ali aende kwake.

Aishah alimshauri amwite baba yake (Abu Bakr) badala ya Ali, na Hafsa alishauri jina la baba yake (Umar) badala ya jina la Ali. Wakati huo watu hawa walikusanyika hapo. Lakini Mtume alisema, “Rudini makwenu. Nitawaiteni mimi endapo nitawahitaji.” Waliposikia hivyo watu hao waliondoka.

Kwenye Sahih Muslim imetaarifiwa kutoka kwa Bin Abbas kwamba Mtukufu Mtume alikaribia kutawafu akiwa kitandani kwake, Umar bin Khatab na masahaba wengine walikuwepo hapo nyumbani kwake Mtume. Mtukufu Mtume akasema, “Niletee kipande cha karatasi na kalamu ili kwamba niweze kuandika kitu (kama wosia wangu) kwa ajili yenu msije mkapotoka baada yangu.” Umar akasema, “Mtume haya kwa sababu ya weweseko. Tunayo Quran Tukufu na hiyo inatosha.” Hapo hapo palitokea mzozo miongoni mwa watu waliokuwepo hapo.

Baadhi yao walisema, “Ni wajibu wetu kutii maagizo yake ili kwamba aweze kuandika chochote apendacho kutuandikia.” Baadhi yao walimuunga mkono Umar. Ilipotokea kelele kubwa kuhusu suala hili, Mtume alisema, “ondokeni hapa kwangu.” Ilikuwa kwa sababu hii kwamba Bin Abbas alikuwa akisema, “Ulikuwa msiba mkubwa na maafa kwamba Mtume hankuweza kuandika chochote kwa sababu ya kelele na mfarakano miongoni mwa watu.”

Abdullah bin Abbas amenukuliwa na anasema kupitia kwa simulizi ya Said bin Jubayr alieleza kwenye Sahih Bukhari. “Ni siku ya janga iliyoje siku hii ya Alhamisi!” Baada ya kusema hivi, alilia na halafu akasema, “Siku hiyo ya Alhamisi, ugonjwa wa Mtume ulizidi sana, akasema nileteeni kitu cha kuandikia ili niweze kuandika kitu kwa namna ya wosia wangu ambao mkiufuata hamtakengeuka baada yangu.”

Baada ya kusikia haya watu walianza kubishana na kupingana Mtume akasema: “Haifai kugombana mbele ya Mtume.” Watu wakasema, Mtume anasema katika hali ya kuweweseka. Mtume akasema, “Ondokeni hapa kwangu. Hali yangu ni njema hata iwe vyovyote vile. Si sahihi vyovyote vile mtakavyo sema. Niacheni peke yangu. Ondokeni hapa.”

Baada ya hapo Mtukufu Mtume alitamka wosia zake tatu kwanza kuwa fukuza kwa nguvu washirikina wote waliopo kwenye Rasi ya Uarabuni na pili, kuridhia ujumbe uliotoka sehemu za mbali. Msimulizi hakusimulia wosia wa tatu au alisahau.”

Imesimuliwa kutoka kwa Said bin Jubayr kwenye Musnad Ahmad Bin Hanbal na Sahih Muslim kwamba Abdullah bin Abbas alisema, “Ni siku iliyoje siku hii ya Alhamisi, akalia sana hivyo kwamba machozi yalitiririka kwenye mashavu yake kama nyuzi za lulu.

Baada ya hapo alielezea kwamba Alhamisi ni siku ambapo Mtukufu Mtume alisema, “Nipeni vitu vya kuandikia ili kwamba niweze kuandika kitu kwa ajili yenu ambacho kwa njia ya wosia wangu msije mkapotoka kwamwe baada yangu.” Lakini, pamoja na yote hayo, watu walisema, “Anasema akiwa katika kuweweseka.”

Shahabuddin Khafaji ameandika kwenye Nasimur Riyaz Sharah Shafa Qadhi Ayaz kwamba kufuatana na maelezo ya hadith zingine kuhusu tukio hili, Umar alisema, “Mtume anasema akiwa katika kuweweseka.” Shahristani ameandika katika kitabu chake al-Milal wan Nihal kwamba mabishano na tofauti ya kwanza wakati Mtume anaugua ni pale ambapo Muhammad Ismail bukhari amesimulia kutoka kwa Abdallah bin Abbas kwa mamlaka ya kwake kwenye kitabu chake- Sahih Bukhari kwamba wakati maradhi yaliyosababisha kifo cha Mtume yalipozidi, alisema, “Nipeni kidau cha wino na karatasi ili niweze kuandika kwa ajili yenu hati kwa njia ya uthibitisho msije mkapotoka baada yangu.”

Aliposikia hivi, Umar alisema, “Mtume anasema hivyo kwa sababu ya ukali wa maumivu ya ugonjwa. Kitabu cha Mungu kitafanya kazi hiyo.” Hivyo, palitokea mzozo, Mtume alisema, “Ondokeni niacheni mimi na msibishane na kuhojiana mbele yangu.”

Hii ndio sababu iliyomfanya Abdullah bin Abbas aseme baadae, “Ni balaa iliyoje iliyo sababishwa na mabishano hayo! Ilikuwa baina yetu na kuandika kwa Mtume na ilisababisha asiandike.”

Allamah, Shibli Nomani ameandika, “Lipo neno la Hayr kwenye hadith lenye maana ya kuweweseka. Umar aliifasiri hotuba ya Mtukufu Mtume kama kuweweseka.” (Al-Faruq, ul. 61) kwenye kamusi maana ya neno ‘Hizyan’ imeoneshwa kama mazungumzo ya upuuzi (Sirat Juzuu ya 2, uk. 522).

Nazir Ahmad Dehlavi ameandika, “Wale waliokuwa na njozi za Ukhalifa katika akili zao walitangua mpango huo kwa kutumia ugomvi wa kuhalalisha upinzani wao kwa kusema kwamba Qurani ilitosha kufanya yote na kwa kuwa Mtume alikwishapoteza fahamu hapakuwepo na haja ya kumpa karatasi na kidau cha wino au vinginevyo angetoa imla ya mambo yasio na umuhimu.” (Ummahatul Ummah, uk. 92).

Imamu Ghazali ameandika kwamba kabla ya kifo chake Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwaambia masahaba wake wampe kalamu, karatasi na wino ili aandike ni nani aliyestahili kuwa Imamu na Khalifa wao. Lakini wakati huo Umar, aliwaambia watu kumwacha mtu huyo kwani alikuwa anasema upuuzi. (Sirral Alamin, Sharah Muslim Navi, Juzuu ya 2).

Kwa ufupi, Mtume aliponyimwa kalamu na wino palitokea mzozo miongoni mwa wale waliokuwepo hapo. Ufahamu wangu wa kihistoria umesema kwamba wakati huo Abu Dharr, Salman, Miqdadi na bin Abbas na kadhalika walipinga kitendo cha kukataa na wanawake wakawaasa kutoka nyuma, “Nini kimewatokea! Kwa nini hamsikilizi kile anachosema Mtukufu Mtume? Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mpeni anachotaka.” Waliposikia hivyo Umar akasema, “Nyamazeni! Nyini ni sawa na wanawake wa Yusuf. Mnalia wakati Mtume mgonjwa na mnamghasi wakati anayo afya njema.” Mtume aliposikia sauti yake akasema, “Usiwakaripie kwani wao ni bora zaidi kuliko nyinyi.” (Tabrani).

Kwa mujibu wa Rauzatul Ahbab, wakati wa kifo chake, Mtume alimwambia mwanawe Fatimah Zahra awaite wanawe wa kiume. Aliwapeleka mbele yake. Wajukuuu hao wawili, waliketi karibu na babu yao baada ya kumpa heshima yake na walipomwona yupo katika maumivu makubwa ya ugonjwa, walilia sana hivyo kwamba watu waliowaona nao pia wakaanza kulia. Hasan aliweka uso wake kwenye uso wa Mtume na Husein aliweka kichwa chake kwenye kifua chake. Mtume alifungua macho na akawatazama kwa huba, akawapapasa kwa mahaba, na akaonesha utashi wake kwa watu kwamba wanastahili kuheshimiwa na kunyenyekewa.

Pia ipo Hadith kwamba baada ya kumsikia Husain analia, wote wale waliokuwa hapo walianza kulia na alipowasikia Mtume pia alianza kulia. Halafu akaagiza ndugu yake mpendwa, Ali aende kwake, Ali alikwenda na akaketi kuelekea kichwa cha Mtume. Aliponyanyua kichwa chake, Ali alikuwa anasogea karibu naye, alikiweka kichwa cha Mtume kwenye mkono wake.

Mtume akasema, “Ali! Nimekopa kiasi hiki cha deni kutoka kwa Myahudi fulani kwa ajili ya vifaa vya jeshi la Usamah. Mlipe kiasi hicho cha fedha. Ewe Ali! Utakuwa mtu wa kwanza kuja kwangu kwenye Haudhi ya Neema na utapata matatizo makubwa baada yangu. Yakabili matatizo hayo kwa uvumilivu na utakapoona kwamba watu wamechagua dunia, wewe shughulikia mambo ya akhera.” (Madarijun Nubuwwah, Juzuu ya 2, na Tarikhul Baghaad, Juzuu ya 11).
Pia imeandikwa kwenye Madarijun Nubuwah kwamba Fatimah Zahra alipata mshituko mkubwa kwa sababu ya kifo cha Mtume na alilia sana kwa uchungu. Muhadithi Dehlavi ameandika kwenye kitabu ‘Ma thabatabis Sunnah” kwamba matukio mengi ya hatari yalitokea baada ya kifo cha Mtume. Ameyataja kwenye shairi akisema kwamba endapo matatizo ambayo yalimpata, yangeipata mchana ungegeuka kuwa usiku wa giza. Mwandishi wa Rauzatul Ahbah anasema kwamba baada ya kifo cha Mtume hakuna mtu aliyemwona akicheka.

Tabaqat cha bin Sad ameandika kwamba kichwa cha Mtume kilikuwa kwenye paja la Ali wakati wa mwisho wa uhai wake. Hakim anasema kwenye Mustadirak kwamba Mtume kabla hajakata roho alipitisha siri kwa Ali na alitatua matatizo yake ya kimuujiza.

Abdul Barr kwenye kitabu chake, Istiab amemnukuu Abdullah bin Abbas akisema, “Ali anazo sifa nne za aina hiyo na hakuna miongoni mwenu aliye nazo. Kwanza, Alikuwa mtu wa kwanza kupata heshima ya kuswali na Mtukufu Mtume. Pili, alikuwa ndiye mshika bendera pekee wa Mtume katika kila vita. Tatu, ambapo wakati wa vita vitakatifu wakati mwingine watu walikuwa wanakimbia kutoka kwenye uwanja wa vita na kumwacha Mtume nyuma, Ali alikuwa imara kuwa pamoja na Mtume. Nne, Ali ni mtu aliyeiosha maiti ya Mtume na kuizika kaburini.”

Kwa mujibu wa imani ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, Mtukufu Mtume alifariki siku ya Jumatatu terehe 28 ya mwenzi wa Safar (machi), 11A.H. (Muwaddatul Qurba), uk. 49 kimechapishwa Bombay, 1310 A.H). Baada ya kifo chake palikuwepo na masikitiko na kilio miongoni mwa watu wa nyumba yake na masahaba walioheshimiwa.

Abu Dharr, Salman, Miqdad, Ammar na masahaba wengine waaminifu walikuwa wanalia sana. Kwa ufupi alikuwa kama rafiki mpenzi aliyekuwa na masikitiko kando yake. Historia inaonyesha kwamba Abu Dharr Ghifari alikuwa na maono ya kudumu kuhusu msiba huu.

Manazir Aksan Gilan ameandika, “Kwenye maelezo mengi ya maisha ya Abu Dharr japokuwa dalili za wazi zinaonekana za maumivu hayo ambayo bila ya kuwepo muumini anakuwa si muumini, hata hivyo yapo matukio kadhaa ya kutia moyo ambayo yanadhihirisha taswira nzuri ya uhusiano wa wote wawili yaani anayependa na anayependwa katika macho ya akili zetu.” (al-Ishteraki az-Zahid, uk. 90).

Wakati Mtukufu Mtume anakata roho, Abu Bakr alikuwa nyumbani kwake, Sakh, umbali wa maili moja kutoka Madina. Umar alizuia taarifa ya kifo isienee na Abu Bakr alipofika wote wawili walikwenda Saqifah Banni Saidah iliyopo maili tatu kutoka Madina, na pamoja nao pia alikuwa Abu Ubaydah bin Jarrah ambaye kazi yake ilikuwa mwosha. Vyovyote vile, masahaba wakuu wa Mtume walikwenda kuungana na kugombea Ukhalifa na kuacha maiti yake, na Ali alifanya mpango na akamudu mambo ya kuosha maiti ya Mtume na maziko.

Ali aliosha maiti, Fazal bin Abas alinyanyua kaptura yake, Abbas na Qathm walimgeuza na Usamah na Shaqran walimwagia maiti maji. Baada ya maiti ya Mtume kuoshwa, ilivishwa sanda. Abu Talhah alichimba kaburi. Ali, aliongoza Swala ya kumsalia maiti na yeye ndiye aliyeingia kaburini na kuilaza maiti inavyo stahili mahali pake.

Baadda ya hayo, alifukia kaburi kwa masikitiko makubwa. Abu Bakr na Umar na wengineo hawakushiriki matayarisho ya maziko yaani kuosha maiti, kuvisha sanda kusalia hadi kushusha maiti ndani ya kaburi, na kufukia kaburi la Mtukufu Mtume.
Kwa sababu waliporudi kutoka Saqifah, Mtume alikwishazikwa. (Kanzul Ummal, Juzuu ya 3, uk. 140 Arjahul Matalib, uk. 670, Fatahul Bari, Juz ya 6, uk. 4).
Mtukufu Mtume alikuwa na umri wa miaka 63 alipotawafu. (Abul Fida, Juz. ya 1, uk. 152).

Sura Ya Kumi

Baada ya kifo cha Mtume, wale masahaba ambao hawakuridhika kwa kitendo chake cha Ghadir Khum ambao walimpinga Ali, haraka sana walikusanyika Saqifah Bani Sadah mahali ambapo palitayarishwa maalumu kwa mashauriano yasiyofaa (Ghayathul Lughaat) na watu wachache wapatao 200 ambao walikuwemo Muhajirina na Ansar waliokubali na wasikubali walikuwemo, walianzisha msingi wa serikali ya mtu binafsi. Waliporudi Madina kutoka Saqifa, baada ya maziko ya Mtume, walianza kudai kiapo cha utii kutoka kwa watu kwa lengo la kupatia serikali hiyo ya kibinafsi sura ya pamoja na aina ya kidemokrasia. Ili kukamilisha lengo hili walionesha tabia ambayo katika ubinadamu wa kawaida inatetemesha si tu kwa masahaba wa kuheshimiwa lakini pia kwa Ahlul-Bait.

Kiini hasa cha hadithi hiii inayoumiza ya kipindi hiki ni kwamba, Ali alilazimishwa kutoa kiapo cha utii (Rauzatul Ahbab) na alipokataa, jeshi la Khalifa lilimpeleka mahakamani, huku shingo yake ikiwa imefungwa kwa kwamba (Bin Abil Hadid Motazali). Nyumba ya Fatimah ilichomwa moto (Tarikh Tabari, Tarikh al-Imamuah wa as-Siyasah Miratul Uqul) Mlango wa nyumba ulimwangukia Fatimah na kusababisha kuharibika kwa mimba ya mtoto wake wa kiume.(al-Milal wan Nahl of Shahristani).

Allamah Mukkah Muin Kashifi ameandika kwamba Fatimah aliugua kwa sababu ya mshtuko wa tukio hili, na hatimaye alifariki. (Maarij un-Nabuwwah Juz. 4, Sura ya 3, uk. 42). Halafu wale watu ambao walikataa kula kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr walilazimishwa kwa ukali, na wengine walipigwa sana. Salman Farsi ambaye Mtume alikwisha mjumuisha kwenye Ahlul Bait wake, pia alikuwa mmoja wapo wa majeruhi wa udikteta wao. Alipigwa sana hivyo kwamba shingo yake ilitenguka na hali hiyo ilidumu hadi kifo chake.

Majina ya wale waliokuwepo Madina na ambao walikataa kula kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr yameorodheshwa chini:

Imamu Ali, Abu Dharr, Salman Farsi, Ammar bin Yasir, Miqdadi bin al-Aswad Khalid bin Said, Burayda Aslami, Ubay bin Kab, Huzayma bin Thabit, Suhayl bin Harrif, Uthman bin Hanif, Abu Ayyub Al-Ansari, Hudhayfa bin al-Yamani, Sad bin Ubaydah, Qays bin Sad, Abdullah bin Abbas, Abbas bin Abdul Muttalib, Abdul Haytham bin Tayhan, Jabir bin Abdullah, Abdullah bin Thamit, Ubaydah bin Thamit, Abu Said Khidri (Tabsaratul Awam, uk. 24, Ainul’Hayat, uk. 5).

Imeandikwa kwenye ukurasa wa 43 wa kitabu hicho hicho (Tabsaratul Awam) kwamba baada ya siku chache Sad bin Ubaydah alipigwa mshale na akafa kwa sababu ya kukataa kwake kutoa kiapo cha utii.

Vyovyote vile uhuni huu wa kisiasa uliendelea baada ya kifo cha Mtukufu Mtume. Waandishi wa historia wameandika kwamba kiunga cha Fadak, rasilimali ya Ahlul bait kilinyang’anywa kwa sababu tu ya kukataa kutoa kiapo cha utii. Watu hawa walisema kwamba Ukhalifa ni haki isioondolewa kwa Ali na lazima apate. Maelezo marefu ya madai haya bado yapo kwenye hotuba ya Ali ya Shiqshiyyah iliyopo kwenye Nahjul Balaghah.
Ali amesema wazi kwamba Ukhalifa ilikuwa haki yake ambayo iliporwa kutoka kwake. Pia amesema jaribio lake la kuanzisha madai yake kama inavyoonekana kwenye ukurasa wa 231 katika kitabu cha an-Nihayah cha bin Athir.

Sasa tunanukulu kutoka kwenye Tarikhi Ahmadi kuhusu msiba wa tukio hili la maangamizi ambalo liliwatokea Ahlul-Bait na masahaba waaminifu baada ya kifo cha Mtukufu Mtume, hivyo kwamba msomaji aweze kujua nini kilitokea baada ya yote kwa uzao wa Mtume na masahaba wake waaminifu majuma mawili tu baada ya kifo cha Mtume na Abu Dharr aliwajibika vipi kwa hali mambo yalivyokuwa.

Kwa mujibu wa Tarikh bin Jasir, Umar alikuwepo wakati wa kifo cha Mtukufu Mtume lakini Abu Bakr hakuwepo. Alikuwa kwenye kijiji kiitwacho Sakh. Mtume alipokufa, Umar alisema, “Kufuatana na dhana ya wanafiki, Mtume amekufa, lakini ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba yu hai.”

Kwa mujibu wa al-Milal wan Nihal cha Shahristani, Umar alitishia kumuua kwa upanga wake endapo mtu anasema Mtume amekufa. Tukio hili pia limeandikwa kwenye vitabu vingine kama (Tarikh Abul Fida, Juz. 1, uk. 164, Tabaqatul Kubra Juz. Ya 2, uk. 271, Sunan bin Maja Juz. 1, uk. 571, Hadith ya 1618, Musnad Ahmad bin Hanbal Juz. 1).

Kwa mujibu wa Rauzatul Alhbab watu walianza kuwa na shaka kuhusu kifo cha Mtume waliposikia tishio hili la Umar. Wakati huo, Abu Bakr alikuwa nyumbani kwake Sakh. Alipopewa taarifa ya kifo cha Mtume haraka sana alikwenda Madina na alipofika kwenye msikiti wa an-Nabi aliona kwamba watu walikuwa katika ghasia nyingi.

Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, Abu Bakr alipoona hali hii ya watu, akakariri Aya ifuatayo:

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهِ الرُّسُلُ ۚ أَفَإِنْ مَاتَ أَوْ قُتِلَ انْقَلَبْتُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُم {144}

“Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume. Je, akifa au akauawa ndiyo mtageuka mrudi (Ukafirini)?” (Qurani 3:144).

Waliposikia hivi watu wakasadiki kuhusu kifo cha Mtukufu Mtume. Baada ya hapo watu wote waliondoka kwenda Saqifah Bani Sadah.

Kwa mujibu wa Tarikh Bin Khaldun, baada ya kufika Saqifah Abu Bakr alisema, “Sisi ni sahaba na ndugu wa Mtume na kwa hiyo tunastahili zaidi kudai Ukhalifa wa Mtume kuliko mtu mwingine yeyote.”

Kwa mujibu wa Tarikh Tabari cha Bin Jarir, Umar alimwambia Abu Bakr; “Nyoosha mkono wako ili niweze kutoa kiapo cha uaminifu kwako” Abu Bakr alisema, “Hapana; wewe ndiye unyooshe mkono kwa sababu katika kila hali wewe ni mwenye uwezo zaidi kuliko mimi.”

Pambano hili liliendelea kwa kipindi fulani. Hatimaye Umar aliunyoosha mkono wa Abu Bakr na akatoa kiapo cha uaminifu kwake na pia alisema, “Pia uelewe kwamba nguvu zangu zimeunganishwa.”

Kwa mujibu wa Tarikh Kamil cha Bin Athir, Umar na watu wengine waliapa kuwa waaminifu kwa Abu Bakr, lakini Ansar wote au baadhi miongoni mwao walisema, “Hatutatoa kiapo cha uaminifu kwa yeyote isipokuwa Ali.”

Kufuatana na Tarikh Khamis, wakati Abu Bakr alipomaliza kazi ya kupokea viapo, aliondoka Saqifa na kwenda Msikiti wa Nabi na akaketi kwenye mimbari. Hapa, pia, aliendelea kupokea viapo hadi mwisho wa siku na watu walishindwa kuhudhuria mazishi ya Mtukufu Mtume. Ilikuwa siku ya Jumanne usiku.

Kwa mujibu wa Kanzul Ummal imesimuliwa na Urwa kwamba Abu Bakr na Umar hawakuwepo kwenye mazishi ya Mtukufu Mtume, lakini walikuwepo kwenye kundi la Ansari (huko Saqifa bani Sadah) na Mtume alizikwa kabla ya kurudi kutoka huko.

Kwa mujibu wa Nihayah cha Bin Athir Jazari, Majma al-Bidar cha Mulla Tahir Qutni na al- Milal wa Nihal cha Shahristani, baadaye Umar alisema kwamba kutoa kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr ni jambo lisilotegemewa lakini Mwenyezi Mungu alitunusuru kutoka kwenye uovu wake.

Kufuatana na Tarikh Abu Fida kundi la Bani Hashim na pia Zubayr bin al-Awam, Miqdadi bin Amr, Salman Farsi, Abu Dharr, Ammar al-Yasir, Bara bin Azib na wengine waliokuwa upande wa Ali, walikaa pembeni wakati wa kutoa kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr.

Imeandikwa kwenye Istiab cha Abdul Barr kwamba wakati kiapo cha uaminifu kilikuwa kinatolewa kwa Abu Bakr, Ali hakuapa uaminifu kwake na alikaa nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa Muruj uz-Zahab cha Masudi, ambapo mnamo siku ya Saqifah kiapo cha uaminifu kilitolewa kwa Abu Bakr, Ali alimwambia Abu Bakr; “Umeharibu mambo yetu, ulituona kwa ushauri na hukufikiria haki yetu.” Abu Bakr akasema, “Lalamiko lako ni halali lakini nimefanya hivyo kwa kuhofia maasi.”

Kwa mujibu wa Rauzatul Ahbab, Abu Bakr alipomaliza kazi ya kutafuta kiapo cha uaminifu kwake, alimwita Ali kupitia kwa Wahajirina na Ansari kadhaa. Ali alikwenda na akauliza kwa nini nimeitwa? Umar akasema, “Umeitwa ili kutoa kiapo cha uaminifu kama ambavyo wengine wamekwisha fanya”. Ali akasema, “Ninaiweka mbele yako hoja ile ile, ambayo umewaambia Ansari kupata Ukhalifa. Niambie kwa uaminifu mtu ambaye yu karibu zaidi na Mtume.”

Umar alisema, “Hatutakuachia hadi hapo utakapotoa kiapo cha uaminifu.” Ali alisema, “Jibu swali langu kwanza halafu niambie suala la kutoa kiapo cha uaminifu.” Abu Ubaydah bin Jarrah akasema, “Ewe Abul Hasan! Ni wewe tu ndiye unayestahili Ukhalifa na utawala kwa sababu ya kutangulia katika Uislamu na ukaribu wako kwa Mtume, lakini kwa kuwa masahaba wamemkubali Abu Bakr, ni vema wewe pia uungane nao,” Ali akasema Abu Ubaydah! Unataka kuhamisha neema kubwa ambayo Mwenyezi Mungu ameipatia familia ya Mtume na kupeleka kwingineko. Tazama! Sisi ni mahali palipoteremshwa Wahyi, mahali ambapo ziliwasili amri na makatazo, chanzo cha uadilifu na maarifa, na mgodi wa akili na ustahamilivu.

“Aliposikia hivi, Bashir bin Said akasema, “Ewe Abu Hasan! Tulidhania kwamba kukaa kwako nyumbani ulikuwa tayari kujitoa katika kinyang’anyiro cha Ukhalifa.” Ali akasema, “Hivi nyinyi watu mnaona ni sawa kuacha maiti ya Mtume bila kukafiniwa, kuvishwa sanda na kuzikwa, na kwa hiyo ningejiingiza kwenye kugombania na kukirimu watu kwa kutafuta Ukhalifa?”

Imeandikwa kwenye Usudul ul-Ghibah kwamba Ali alimnukuu Mtukufu Mtume akisema, “Ewe Ali! Wewe ni kama Ka’abah ambapo kila mtu huenda kuzuru, ambapo yenyewe haiendi kuzuru mtu yeyote. Kwa hiyo, endapo watu wa kundi lako wanakuja kwako kutoa kiapo cha uaminifu kwako kubali. Usiende kwao hadi wao waje kwako.”

Kwa mujibu wa Rauzatul Ahbah, Abu Bakr aliposikia mambo haya na kuona kwamba kila sababu na hoja ya Ali, Ilikuwa haipingiki, thabiti na dhahiri kama hoja elfu moja, alisema kwa upole, “Ewe Abul Hasan! Nilidhani kwamba hungekataa kutoa kiapo cha uaminifu kwangu. Kama ningejua kwamba ungekataa, nisingekubali kuwa Khalifa. Sasa, kwa kuwa watu wametoa kiapo cha utii kwangu, nafikiri ni vema uungane nao, kama utapenda. Lakini, kama unasita kwa sababu hii, sitakulaumu.” Baada ya Ali kusikia haya alinyanyuka na kwenda nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa Iqdul Farid, cha Shahabuddin bin Abd Rabbihi Undlusi, watu waliokataa kutoa kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr walikuwa; Ali, Abu Dharr, Zubayr na Sad bin Ubadah. Miongoni mwao, Ali Abbas na Zubayr walikaa nyumbani kwa Bibi Fatimah hadi Abu Bakr alipomtuma Umar aende kuwatoa nje watu hao na kutumia upanga endapo wangekataa. Kwa hiyo, Umar alifika hapo akiwa na moto kwa lengo la kuchoma nyumba hiyo. Fatimah alipotambua nini kinachoendelea, alisema; “Ewe mwana wa Khattab! Umekuja kuchoma moto nyumba yangu!?” Umar alisema, Bila shaka nimekuja kwa nia ya hiyo, au vinginevyo, watu waliomo ndani ya nyumba hii watoke na watoe kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr.”

Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, Umar alikwenda na moto kwa nia ya kuchoma moto nyumba ya Fatimah. Fatimah alipotambua, alisema, “Ewe mwana wa Khatab! Umekuja kuchoma moto nyumba yangu!?” Umar akajibu, “Ndio, vinginevyo watu waliopo ndani watoe kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr.”

Kufuatana na Tarikhut Tabari cha bin Jarir, Umar alikwenda nyumbani kwa Murtaza (Imamu Ali) ambamo walikuwemo Talha, Zubayr na muhajirina kadhaa na akasema, “Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Nitachoma moto nyumba hii vinginevyo mtoke nje kwa ajili ya kutoa kiapo cha uaminifu.”

Imeandikwa kwenye Al-Imamah wa as-Siyasah cha bin Qutaybah Dinuri kwamba Abu Bakr alipogundua kwamba wale waliokuwa na Ali hawakuwepo wakati kiapo cha auaminifu kilipokuwa kinatolewa, alimtuma Umar awaite. Watu hao walikuwa ndani ya nyumba ya Ali. Walikataa kutoka nje. Umar aliagiza apewe kitita cha kuni zilizowashwa moto na akasema, “Tokeni nje au vinginevyo kwa jina la Mwenyezi Mungu nitawachoma watu waliomo ndani kwa moto!” Watu wakasema, “Fatimah, binti yake Mtukufu Mtume na yeye pia yupo ndani ya nyumba hii.”

Umar akajibu, “Haidhuru kitu,” Waliposikia hivi watu wote waliokuwa ndani ya nyumba walitoka nje isipokuwa Ali aliyekuwa anawapa maelezo watu ambao walitumwa wamwite, akasema; “Enyi kundi la Muhajirina! Ninayo haki zaidi ya kuchukua Ukhalifa kuliko nyinyi katika hali zote. Sitatoa kiapo cha uaminifu kwenu. Kwa usahihi zaidi, nyinyi mnatakiwa kutoa kiapo cha uaminifu kwangu.

“Tazama! Mmepata Ukhalifa kwa hoja mliyowapa Ansari kwamba nyinyi ni ndugu wa Mtume na jambo la kushangaza ni kwamba sasa mnajaribu kuchukua isivyo halali Ukhalifa kutoka kwa Ahlul-Bait wa Mtume.

“Hamweki madai yenu katika msingi kwamba nyinyi ni bora zaidi kuzidi Ansari kwa kisingizio kwamba Mtume alikuwa wa kabila lenu? Sasa nakupeni hoja hiyo hiyo ambayo mliwapa Ansari kwamba, uhusiano wetu na Mtume ni mkubwa na karibu zaidi kuliko wenu wakati wa uhai wake na baada ya kifo chake.

“Sasa mnatakiwa kutenda haki bila upendeleo endapo nyinyi mnamwanini Mwenyezi Mungu na kumwogopa Yeye.

“Kuhusu kundi la wahajirina! Mkumbukeni Mwenyezi Mungu na msichukue uongozi wa Mtume kutoka kwenye nyumba yake na kupeleka nyumbani kwenu.”

Baadhi ya hapo, Fatimah alisema akiwa kwenye ngazi za mlango wake, “Enyi watu! Mlituachia maiti ya Mtume, mkatatua jambo la Ukhalifa kwa kujipendelea nyinyi na hamkuzingatia haki yetu.”

Kwa mujibu wa Tarikh bin Qataybah Umar alipokwenda kwa Abu Bakr alisema, kwa nini hutoi amri ya kukamatwa Ali ambapo anapinga kutoa kiapo cha utii kwako?

Kwa mara nyingine Abu Bakr alimtuma mtumwa wake Qanfaz amwite Ali. Qanfaz alimwambia Ali, “Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu anakuita wewe.” Ali akasema, ‘Mmemkashifu Mtume haraka kiasi hicho nyie watu.”

Qanfaz alirudi kwa Abu Bakr na akarudia maneno aliyoambiwa na Ali. Baada ya kusikia Abu Bakr aliendelea kulia kwa kipindi fulani. Umar akamwambia Abu Bakr kwa mara ya pili, “Usimpe muda Ali ambaye hataki kutoa kiapo cha utii kwako.” Abubakr akamuagiza tena Qunfaz kwenda kwa Ali na kusema, Amiri wa Waumini anakuita ili utoe kiapo cha uaminifu. Qanfaz aliwasilisha ujumbe wa Abubakr kwa Ali. Ali akasema kwa sauti kubwa “Mwenyezi Mungu na asifiwe! Bwana wako amedai uhusiano huo ambao hana uwiano nao.”

Qafaz akaenda kwa Abu Bakr na kurudia maneno ya Ali. Baada ya kusikia hivi, Abu Bakr alianza kulia tena. Halafu Umar akasimama na akifuatana na kundi la watu, alikwenda nyumbani kwa Fatimah na akagonga mlango. Aliposikia kelele za watu, Fatimah alianza kulia kwa sauti kubwa, “Ewe Baba! Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni tatizo gani hili lenye uzito mkubwa ambao limeletwa kwetu na mwana wa Khattab na Abu Quhafah!” Watu waliposikia kilio cha Fatimah, wengi wao walirudi huku wanalia na wachache tu ndio waliobaki nyuma na Umar. Halafu Ali akatoka nje ya nyumba na akaenda nao kwa Abu Bakr. Ali aliambiwa atoe kiapo cha uaminifu kwa Abu bakr. Alisema, “Endapo sitatoa kiapo cha utii itakuwaje?” Akasema, “Endapo hutatoa kiapo cha uaminifu, kwa jina la Mwenyezi Mungu tutakuua.”

Ali alisema, Mtamuua mtu ambaye ni mja wa Mwenyezi Mungu na ndugu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Umar akasema, “Tunakiri kwamba wewe ni mja wa Mwenyezi Mungu, lakini hatujui kama pia wewe ni ndugu yake Mtume.” Abu Bakr alikuwa kimya wakati huo. Umar akamwambia, “Kwa nini hutoi amri, umekaaa tu?” Abu Bakr akasema, “Sitamlazimisha Ali wakati Fatimah bado hai.” Halafu Ali alinyanyuka na alikwenda kwenye kaburi la Mtume ambapo alilia, kwa uchungu na akasema, “Ewe ndugu! Watu wa kabila wamenitukana sana na walikaribia kuniua.”

Abu Dharr alikuwa anayaona mambo haya kwa macho yake. Alikuwa na kumbukumbu ya yele aliyoyaona humo Ghadir al- Khum. Alishangaa sana kuona yaliyokuwa yanatokea.

Akiwa bado yupo katika mshangao, ghafla imani yake ilitikisa hisia zake na alikimbia hadi kwenye Msikiti wa Nabi. Akili yake ilipatwa na fadhaa na kusumbuliwa na damu yake ilichemka kwa shauku. Alikuwa anangoja apate fursa ili atoe mawazo bila woga. Alipofika msikitini aliona kundi la masahaba wakiwemo Abu Bakr na Umar miongoni mwao.

Ujasiri wake wa kiume ulisisimuka na akaanza kutoa hotuba akiwa amesimama kwenye sehemu iliyoinuka.

Alisema: “Enyi watu wa Qurayshi! Nini kimetokea? Mmekuwa wazembe kiasi gani! Mmedharau kabisa ndugu wa karibu zaidi wa Mtume! Kwa jina la Mwenyezi Mungu kundi la Waarabu limeamua kuasi, na kutengeneza nyufa za mashaka katika imani. Nisikilizeni! Ukhalifa ni haki ya Ahlul Bait. Vurugu hii na ugomvi wa kelele ni mambo yasiyo na maana. Nini kimewapateni? Mnawaita wenye uwezo hawana uwezo na mnawasifu wasio na uwezo. kwa jina la Mwenyezi Mungu wote nyinyi mnatambua kwamba Mtume ametangaza tena na tena, ‘Baada yangu Ukhalifa na uongozi ni wa Ali, halafu Hasan halafu Husein na halafu uzao wangu ambao ni maasum ndio watakao shika nafasi hii.’

“Hamjali neno la Mwenyezi Mungu! Mlisahau mkataba ule na amri ile ambayo inawapa masharti. Mnaisujudia dunia hii ambayo inaandamia na mnauza Pepo ambayo inadumu milele, na ambamo vijana hawatazeeka na neema hazitapungua, na wakazi wake hawatapata huzuni au kufadhaika na ambamo malaika wa kifo hatafika. Mmeuza kitu cha thawabu kubwa sana kwa bei ndigo sana. Mmefanya kitu kile kile walichofanya watu wa Mitume wa zamani. Walivunja kiapo chao cha uaminifu na waliasi pindi Mtume wao alipokufa!

Walitangua mikataba yao, walibadilisha amri na kugeuza imani. Sasa mnathibitisha kwamba mpo sawa na wao. Kundi la Quraishii! Baada ya muda mfupi sana mtapata malipo ya makosa yenu na adhabu kwa maovu yenu. Kile mlichokichuuma kupitia na tabia yenu kitakuja kwenu kumbukeni! Vyovyote itakavyotokea itakuwa haki, kwa sababu Mwenyezi Mungu hawadhulumu waja Wake (al-Ishtiraki az-Zahis, uk. 113).

Ujasiri wa kiume wa Abu Dharr unaweza kudhihirishwa na hotuba iliyojaa ushawishi. Ni wazi kwamba alikuwa na moyo ulio mwepesi kuhisi na alijaalia kuwa shupavu na jasiri.

Abu Dharr alitoa hotuba hii wakati ambapo hakuna hata mtu mmoja ambaye angeweza kusema neno. Jeshi la Khalifa lilikuwa linawasonga masahaba wa Mtukufu Mtume. Yeyote aliyeonesha dalili za kukataa kutoa kiapo cha uaminifu aliuawa. Yeyote aliyesita kutoa kiapo cha Uaminifu alisongwa. Mtu jasiri kama Ali alifungwa kwamba shingoni na sahaba kama Salman alikabwa koo na kupigwa sana hivyo kwamba maumivu yake yalisababisha kifo chake.

Shaykh Abbas Qummi ameandika kwamba Fatimah binti yake Mtume baada ya kupata maumivu kwa kuangukiwa na mlango, aliugua kwa kipindi fulani na alifariki dunia. Kwa mujibu wa wosia wake, Ali hakutangaza kifo chake kwa watu walioshiriki katika kusababisha umateso yake. Baada ya kumaliza kuosha maiti, Ali alimtuma Imamu Hasan kumwita Abu Dharr ili aisalie maiti, na alikwenda akamwambia. (Safinatul Bihar, cha Shaykh Abbas Qummi, Juz. ya 1, uk. 483).

Hafidh Muhammad bin Ali bin Shahr Ashob (alifariki dunia mwaka 588 A.H) ameandika kwamba, maiti ya Fatimah ilisaliwa na Ali, Hasan na Husein, Aqil, Salman, Abu Dharr, Miqdad, Ammar na Buraydah.

Hadith nyingine imejumuisha majina ya Abbas bin Abdul Muttalib, Fazal, Huzayfah na bin Masud pia (Manaqib bin Shahr Ashob, Juz. ya 2, uk. 65 kimechapishwa Multan).

Sura Ya Kumi Na Moja

Abu Dharr, kwa sababu ya desturi yake, mwenendo wake, tabia na amri ya Mtume, alishindwa kunyamaza inapobidi alisema kweli na aliishi maisha ya kimya. Kazi kubwa zaidi ya kumuabudu Mwenyezi Mungu ilikuwa kukaa karibu na kaburi la Mtume na kuwasifu Aali Muhammad (Uzao wa Mtume).

Inaonekana na kwenye vitabu vingine vya historia kwamba Ali alimshauri afuate sera ya upole. (Nasikhul Tawarikh, Juz ya 2, uk. 803).

Baada ya muda kupita hadi mwaka wa 13. A.H., Abu Bakr alifariki dunia. Kwa mujibu wa Tarikh Tabari na Mujam Kabir ya Tabarani, Abu Bakr alisema kwa majuto na masikitoko; “Endapo nisinge fungua nyumba ya Fatimah hata kama ilifungwa kwa nia ya kupigana, na kama nisingekubali Ofisi ya Ukhalifa, lakini ni kwamba niliweka mkufu wa Ukhalifa kwenye shingo la Umar au Abu Ubaydah.”

Imeandika kwenye Tarikhi bin al-Wardi kwamba baada ya hapo alimteua Umar kuwa Mrithi wake. Kwa mujibu wa al-milal wan nahl cha Shahristani, Abu Bakr alipomteua Umar kuwa Khalifa muda mfupi kabla ya kifo chake, watu walipiga kelele, “Umemteua mtu mwenye hasira na moyo mgumu kama kiongozi wetu.”

Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, Abu Bakr alikufa mwezi wa Jamadiul ukhra tarehe 22, mwaka wa 13 A.H, kati ya muda wa Swala ya magharibi (jioni) na Isha (usiku) na siku hiyo hiyo kiapo cha utii kilitolewa kwa Umar. Abu Dharr hakushiriki Swala ya kumsalia maiti au taratibu zingine za mazishi ya Abu Bakr kwa sababu hakuna kitabu cha historia kinachotaja jina lake katika tukio hili.

Wimbi la ushindi lilijitokeza bada ya kifo cha Abu Bakr. Chini ya hali iliyojitokeza wakati huo, Abu Dharr aliamua kuondoka Madina na kwenda Syria na kuishi huko kwa kipindi chote cha uhai wake. Kwenye kitabu cha Musnad cha Ahmad, anasema kwamba Abu Dharr alipendelea kuishi Syria kwa sababu ya wasia wa Mtume ambapo unasema ifuatavyo; “Ewe Abu Dharr! Ondoka Madina uende Syria wakati idadi ya watu itaongezeka na kuenea hadi Mlima Sala.”

Kwa vyovyote vile, kwa mujibu wa wosia wa Mtume, Abu Dharr aliondoka kwenda Syria akiwa na mke wake na mtoto wa kike mmoja. Shah Walyullah Dehlavi, ameandika kwamba Abu Dharr aliondoka kwenda Syria baada ya kifo cha Abu Bakr na akaloea huko. (Izalatul Khiofa Juz. ya I , uk. 282).

Abu Dharr alikuwa mkali sana kuhusu ukweli. Kwa hali hii, kamwe hakujali ukali wa mtu yeyote, wala hakuogopa serikali ya mtu yeyote au uwezo wa mtu yeyote.

Baada ya Abu Dharr kuondoka kwenda Syria, Umar alikwenda huko kwa madhumuni mengine alipokutana na Abu Dharr ambaye alimsimulia hadith moja ya Mtume. Abu Dharr alisema; “Nina shuhudia kweli kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema; “Mtu ambaye anafanywa kuwa mtawala au kiongozi, ataamuriwa kusimama kwenye daraja la Jahanamu. Atapata ukombozi kama yeye ni muadilifu, lakini kama ni mwovu, daraja litavunjika na kuanguka na mtu huyo ataanguka ndani ya Jahanamu.”
Abu Dharr alikuwa anampenda sana Mtume (s.a.w). Mapenzi haya yaliongezeka zaidi baada ya kufa Mtume na alikuwa akilia sana. Wakati alipokuwa anaishi Syria, watu walimshinikiza Bilal aadhini Adhana kwa ajili ya Swala.

Bilal akasema, “Nimeacha kuadhini Adhana baada ya kifo cha Mtume (s.a.w). Wala sewezi kukariri Adhana sasa na siwezi kuivumilia.” Kwa hali yoyote Bilal alikataa na kwa shida sana akalazimishwa na kukubali. Bilal alisimama ili adhini Adhana na akaanza kuadhini kwa sauti yake kubwa ambayo kipindi fulani ilisikika kwenye mitaa ya Madina wakati wa uahi wa Mtume (s.a.w). Abu Dharr aliinamisha kichwa chake kuelekea mbele. Machozi yalianza kutiririka kwenye machavu yake. Fikra zake zilimkumbusha Madina na akamuona Mtume kwa macho yake ya kiroho, akiwa amezungukwa na masahaba wake.

Akakumbuka mambo yaliyopita akaanza kulia kwa sauti kubwa huku machozi yakimtoka machoni pake.” (al-Ishtiraki az-Zahid).

Abu Dharr aliishi nje ya Madina kwa muda wa miaka kumi huko Syria na alirudi Madina baada ya kupata taarifa kwamba Umar ameuawa.

Abdul Fida ameandika kwenye historia yake kwamba mtu aliyeitwa Abu Lulu alimshambulia Umar mnano mwezi wa Dhil Hijjah tarehe 24, mwaka wa 23 A.H Tarikh Kamil bin Athir ameonesha kwamba Umar alipojeruhiwa, mganga wa kabila la Bani Harith aliagizwa. Alimpa Umar divai ya tende, uliotoka kwenye jeraha bila mabadiliko. Halafu akampa maziwa anywe, pia yalitoka bila ya mabadiliko; “Ewe Amiri wa Waumini! Tayarisha wosia wowote unaotaka.”

Imesimuliwa kutoka kwa Abu Wajiz kwenye Kanzul Ummal kwamba Umar aliuliza watu, “Mnataka nani awe Khalifa baada yangu?” Mmoja wao alisema: “Zubayr bin al-Awam.”

Umar akasema, “Mtamfanya mtu huyo kuwa Khalifa wenu ambaye ni bahili na hana staha.” Mtu mwingine akasema; “Tutamfanya Talha awe khalifa wetu,” Umar akasema; “Mtapenda kumpa Ukhalifa mtu ambaye aliweka rehani kwa mwanamke wa Kiyahudi aridhi iliyotolewa wakfu na Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Baada ya kusikia hivi, bado mtu mwingine akasema, “Tutamfanya Ali kuwa Khalifa wetu.”

Umar akasema, “Kwa niaba ya uhai wangu! Hamtamfanya Ali kuwa khalifa na endapo kwa jina la Mwenyezi Mungu, mtamfanya Ali kuwa Khalifa wenu, hatajizuia kuwawekeni katika njia iliyonyoka hata kama nyinyi hampendi.” Walid bin Uqbah aliposikia hivyo, akasema, “Namjua mtu atakayekuwa khalifa baada yako,” Umar alinyanyuka na akamuuliza, “Nani?” Walid akasema; “Uthman”. Huzayfa bin al-Yaman anasimulia kwamba Umar aliulizwa, alipokuwa na afya njema, kama nani angekuwa khalifa baada yake. Akajibu, “Uthman bin Affan.”

Mulla Ali Qari ameandika kwenye‘Sharah I-iaqh Akbar’ kwamba wakati wa muda wa kifo cha Umar ulipokaribia shughuli za Ukhalifa zilianza kufanywa na Uthman, Ali, Talha, Zubayr, Abdul Rahman bin Auf na Sad bin Abi Waqqas, na akasema kwamba Ukhalifa usivuke hawa watu sita.

Imeandikwa kwenye Tarikh Kamil kwamba Baada ya hapo Umar alimlaumu Suhayb, “Waongoze watu kwenye Swala kwa kipindi cha siku tatu wafungie ndani ya nyumba hawa watu sita ambao wengine miongoni mwao wanatekeleza kazi za ukhalifa halafu uwaangalie.

Kama watano miongoni mwa watu hawa wanamkubali mtu mmoja na mtu mmoja anapinga, auawe endapo watu wanne wanakubaliana na wawili hawakubaliani, wawili wanakataa wauawe na kama watatu wanakubaliana na watatu wengine wanakataa, Abdullah bin Umar ateuliwe kuwa mwamuzi wa kuamua, na kama watu hawa wanamkataa Abdullah bin Umar kuwa mwamuzi, kundi ambalo Abdullah Rahman yupo lishinde na kundi lingine la watu liuawe.”

Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, Umar alikufa siku ya Jumamosi tarehe 30 mwezi wa Zil Hajjah. Kwa mujibu wa ‘Sharah Fiqh Akbar,’

Ambapo baada ya kifo cha Umar, na kufuatana na maagizo yake, kikao cha baraza la ushauri kilifanyika ndani ya nyumba ya Fatimah, dada yake na Ashath bin Qays. “Kwa mujibu wa Tarikh Aathama, uk. 112, watu wa kundi hilo la watu sita lilimpa Abdul Rahman bin Auf, haki ya kumteua khalifa.

Abdul Rahman akiwa amenyanyua mkono wa Ali aliuliza mara tatu, “Endapo tunakuteua wewe Walyyul Amir na Imamu upo tayari kufuata Kitabu cha Mungu, Hadith za Mtume na hadith za Shaykhain (Abu Bakr na Umar)?”

Ali alijibu, “Nitafanya hivyo, vyovyote vile itakavyokuwa, nitafuata Quran Tukufu na Suna ya Mtukufu Mtume (s.a.w) lakini (kuhusu suna za (shaikhain), nitapitia amri za kidini kufuatana na ujuzi wangu.” Baada ya kusikia hivi Abdul Rahman alimuuliza Uthman mara tatu, “Utafuata Kitabu cha Mungu, Suna za Mtume na Suna za Abu Bakr na Umar, endapo tunakuteua wewe kuwa Imamu?” Uthman alisema, “Ndio vyovyote vile itakavyokuwa, nitafanya.” Halafu Abdul Rahman alitoa kiapo cha uaminifu kwake na wengine wakafuata hivyo.

Imetamkwa kwenye Tarikh Kamil na Tarikh Abul Fida kwamba kiapo cha uaminifu kilipokuwa kinatolewa kwa Uthman, Ali alipoona hila katika jambo hili la kutoa kiapo cha uaminifu alisema, “Leo si mara ya kwanza kwamba mmepata ushindi kwa kutumia hila. Vema! Ni bora zaidi kuwa mvumilivu. Ewe Abdul Rahman! Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Umetoa kiapo cha uaminifu kwa Uthman ili ukhalifa ukuelekee wewe,” Abdul Rahman alisema; “ewe Ali! Usijali hili.” Halafu akatoka nje ya nyumba huku akisema; Ilitakiwa iwe hivyo. Miqdad akasema; “Ewe Abdul Rahman! Ulimwacha Ali pamoja na kwamba, kwa jina la Mwenyezi Mungu, yeye ni miongoni mwa watu wasio achana na kweli na hutoa hukumu zenye haki.”

Tarikh Kamil na Tarikh Tabari ni maandishi yanayosema kwamba, Miqdad iliendelea kusema, ‘nilikuwa sijaona kitendo cha ukorofi kama hiki wanafanyiwa watu wa Nyumba ya Mtume baada ya kifo chake. Ninashangaa kuona kwamba Qurayshi wamemwacha mtu ambaye ninamfikiria kuwa mwanachuoni bora kuliko wote (Alim-i Rabbani) na jaji muadilifu kuliko wote (Adil). Kwa jina la Mwenyezi Mungu, endapo ningepata wa kuniunga mkono na msaidizi!” Miqdadi alisema hivi tu ambapo Abdul Rahman aliingilia kati, “Ewe Miqdadi! Muogope Mwenyezi Mungu. Ninahofu vinginevyo waweza ukajikuta upo kwenye matatizo.”

Imeandikwa kwenye Murujuz Zahab cha Musudi kwamba Ammar Yasir alisimama kwenye Msikiti wa Nabi na akasema; “Enyi kundi la Waquraishi! Mlipopora Ukhalifa kutoka kwa Ahlul Bait wa Mtume wenu na mkauondosha na kuupeleka mara hapa mara kule, pia lazima tuwe na matumaini kwamba Mwenyezi Mungu atauchukua ukhalifa kutoka kwenu na kumpatia mtu mwingine kama ambavyo mmechukua kutoka kwa anayestahili.” Halafu Miqdadi akasimama na kusema, Sijapata kuona kamwe aina hii ya mateso na maudhi ambayo Ahlul Bait wanapewa baada ya kifo cha Mtume.” Abdul Rahman akasema, “Ewe Miqdadi! Unafanya nini?” Miqdad akasema, “Kwa nini nisiseme?

“Mimi ni rafiki wa Ahlul Bait wa Mtume kwa sababu mapenzi niliyonayo kwa Mtume na hakika wao hawaachani na kweli na ipo kwao peke yao. Ewe Abdul Rahman! Ninawashangaa Waquraishi ambao unajaribu kuwasaidia wapate kuwazidi wengine na ambao wamekula nyama kutaka kupora upendo na ukuu wa Mtume (s.a.w) kutoka kwa Ahlul Bait wake baada yake. Ewe Abdul Rahman! Tambua! Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Kama ningekuwa na watu wa kuniunga mkono na marafiki, ningepigana na Quraishii kama ambavyo nilivyofanya kwenye vita ya Badr.”

Kufuatana na Tarikh Tabari, Ammar Yasir alisema, “Enyi watu! Mwenyezi Mungu ametimiza jambo kubwa kwa kutupatia imani Yake na ametupatia ukuu kwa sababu ya Mtukufu Mtume. Mnataka kupeleka wapi Ukhalifa mnapowanyang’anya Ahlul-Bait wa Mtume wenu?”

Kwa mujibu wa Raudhatul Ahbab Abdul Rahman bin Auf alipotoa kiapo cha uaminifu kwa Uthman na wale waliokuwepo kwenye mkutano walifuata kufanya hivyo, Ali alisema baada ya kutua kwa muda, “Enyi watu! Ninawaulizeni mniambie kwa kiapo kama yupo hata mtu mmoja isipokuwa mimi miongoni mwa masahaba wa Mtume ambaye Mtume kwenye tukio la kutangaza ‘udugu’ baada ya kunitangaza mimi kuwa ndugu yake, kwamba mimi ni ndugu yake hapa duniani na Akhera.” Wasikilizaji wakajibu, “Hakuna.”

Ali akasema “Yupo mtu yeyote miongoni mwenu isipokuwa mimi ambaye Mtume angemteua kuitangaza Sura ya Baraat (Sura ya 9 ya Quran Tukufu) ikifuatiwa na tangazo kwamba kazi ya Utume wa Mwenyezi Mungu haiwezi kufanywa na yeyote yule isipokuwa na yeye au mojawapo wa Ahlul Baiti wake?” Wote walisema, “Hakuna.”

Ali akasema, ”Mnatambua kwamba kiongozi wa wanadamu, na mwombezi wa Siku ya Hukumu alinipeleka mimi kama kamanda wa Muhajirina na Ansari wote katika Siriyas (vita ambazo Mtume hakushiriki yeye binafsi) na akawaamuru wanitii na kamwe hakumteua mtu yeyote kama kamanda kunizidi mimi.” Watu wakasema, “Ndio, kwa vyovyote vile. Ni kweli.”

Ali akasema, “Mnatambua Mtukufu Mtume ametangaza elimu yangu kwa kusema; “Mimi ni jiji la elimu na Ali ni lango lake.” Watu wote walikiri, “Ndio tunajua.”

Ali akasema, “vita nyingi masahaba walikimbia na kuondoka kwenye uwanja wa vita na kumwacha Mtume ameelemewa katikati ya maadui lakini mimi kamwe sikumtekeleza kwenye vita yoyote ya hatari na nilibaki naye kujitolea maisha yangu kwa ajili ya maisha ya Mtume.” Watu wote walisema, “Ndio, hasa.”

Ali akasema, “mnajua kwamba mimi nilikuwa wa kwanza kuingia kwenye Uislamu.” Watu wakasema, “Ndio tunatambua.”

Halafu Ali akauliza, “Ni nani kati yetu ambaye yupo karibu zaidi na Mtume kwa sababu ya uhusiano wa undugu?” Wote kwa pamoja walisema, “Hapana shaka kwamba uhusiano wako wa nasaba na Mtukufu Mtume (s.a.w) unathibitishwa vema sana, rasmi na umeimarika kwa njia zote.”

Ali alipokuwa anazungumza hivyo naye Abdul Rahman bin Auf alisema, “Ewe Abul Hasan! Hakuna mtu anayeweza kukanusha sifa ambazo umezitaja na kuzieleza. Lakini, kwa kuwa sasa watu walio wengi wametoa kiapo cha utii kwa Uthman, na anayo matumaini kwamba wewe pia utaungana nao kwa jambo hili.” Ali akajibu, “Kwa Jina la Allah wewe unatambua vema sana ni nani aliyestahili Ukhalifa, lakini, inasikitisha kwamba umemwacha kwa kukusudia.”

Kwa mujibu wa Tarikh Tabari, Ali alikariri Ayah hii kutoka kwenyeQurani Tukufu:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا{1}

“Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaomba na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwaangalia.” (Sura 4:1).

Mazungumzo ya tukio la kuchaguliwa kwa Uthman pia yameandikwa katika Iqdul Farid, Juz. 3 uk. 75, kimechapishwa Misri na Sharah Maqasid Taftazani, uk. 296.

Mwandishi wa historia Muhammed bin Ali bin Athman Kufi ameandika kwenye kitabu chake mnao mwaka wa 204 A.H kwamba Ali bin Abi Twalib (a.s) aliongezea kwa kusema, “Enyi watu! Mnatambua kwamba sisi ni Ahli Bit wa Mtume na njia ya ulinzi wa umma dhidi ya kila janga na dhiki. Endapo hamtatupatia haki yetu, itajifikisha yenyewe kwenye mhimili wake, na kama hamtatupata haki yetu, tutakwenda popote tunapoona panafaa kwa kupanda ngamia, bila kujali muda utakaotumika, na saa ya ahadi ya kuonana, tutarudi.

Ninaapa kwa Utukufu wa jina la Mwenyezi Mungu kwamba kama Muhammad hakuchukua ahadi kutoka kwetu na kutuambia kuhusu jambo hili, nisinge acha kupigania haki yangu, na nisingesita kufanikisha lengo langu hata kama ingemaanisha kupoteza uhai wangu. (kwa kupigana).”

Kufuatana na Tarikh Abul Fida kiapo cha uaminifu kwa Uthman kilifanyika mwezi wa Muharram tarehe 3, mwaka wa 23 A.H.

Baada ya kuchaguliwa kwake kwa kazi ya ukhalifa, Uthman alifuata utaratibu unaotakiwa kutawala kwa muda fulani. Lakini, muda ulivyozidi kupita ndivyo alivyondeleza kugeuka, akaacha kutenda haki na kuwa dhalimu, matokeo yake ni kwamba ilitokea vurumai ya kusisimua miongoni mwa masahaba wa Mtukufu Mtume.

Muhammad bin Ali bin Atham Kufi, mwandishi wa historia wa Uislamu wa karne ya tatu A.H amesema kwamba lolote lile walilosema watu kuhusu Uthman na maneno na matendo yake yoyote yale yaliyovumiliwa nao, yalisimuliwa kutoka kwa wahadithi wa kuaminika kwa maneno na mitindo tofauti, lakini kwa kuwa kiini chao kimoja, ameyafupisha maneno hayo katika neno moja.

Wasimulizi wanasema kwamba baada ya kuwa khalifa Uthman aliendelea nao watendaji wa Umar kwa muda wa siku chache ambapo baadaye aliwafukuza kazi na akawapatia Bani Umayyah ambao walikuwa binamu na ndugu zake mikoa yote. Alimteua Abdullah bin Amir Kurbuz huko Basrah. Walid bin Atabah aliteuliwa gavana wa Kufah, Muawiyah bin Abi Sufyani aliendelea kuwa gavana wa Syria, alimteua Abdullah bin Sad bin Abi Sarah kuwa gavana wa Misri, na Umar bin Aas aliteuliwa kuwa gavana wa Palestina.
Sehemu ya ngawira ilipelekwa kwa Khalifa baada ya kutoka Khurasan, Sijistan, Pars, Kerman, Misr, Syria na visiwa vya Iraq. Pia Khalifa Uthman alikuwa na tabia njema hadi wakati huo na alizingatia utoaji wa haki. Lakini ofisi ya ukhalifa ilipoanza kupelekewa utajiri mkubwa na ngawira nyingi, tabia ya Uthman ilibadilika.

Aliweka utawala wote chini ya udhibiti wa Bani Umayyah, na aliwapatia ndugu zake miji yote. Aliwapa ndugu zake idadi kubwa ya fedha bila sababu za msingi kutoka hazina ya taifa. Alimpa Abdullah bin Khalid bin Asas bin Aas bin Umayyah dinari 100,000 mara tu alipomtaarifu kwamba yupo pale ingawa hakuwepo kwenye orodha, alimpa mwanae Abdullah, Harith dinari 100,000 na alimpa mwanae Harith bin Hakim kiasi hicho hicho.

Watu hawakukubaliana na ugawaji wa namna hii wa fedha, walilalamika kwa Abdul Rahman bin Auf na wakasema, “Utawajibika kwa matokeo yake. Tunapata hasara hii kwa sababu yako. Siku hiyo ulipomfanya Khalifa, hatukutoa kiapo cha uaminifu kwa matendo haya mabaya na uovu. Sasa tunataka kujua tufanye nini.”

Abdul Rahman akasema, “Bado sijapata taarifa ya hayo mnayoyasema.” Siku iliyofuata Ali alimuona Abdul Rahman na akamuuliza endapo alikubaliana na matendo kama hayo. Abdul Rahman akasema, “Mimi sijui endapo mambo haya ni ya kweli na tabia ya Uthman imebadilika kama hivi, chomoa upanga wako na mimi pia nitafanya hivyo.”

Watu, pia nao walipeleka taarifa hii kwa Uthman ambaye alikasirika na akasema, “Abdul Rahman ni mnafiki na yeye kuniua mimi halitakuwa jambo gumu kwake.” Abdul Rahman pia alisikia maneno haya, alikasirika na akasema, “Kamwe nisingedhani kwamba Uthman angediriki kuniita mimi mnafiki.” Halafu akaapa kwamba hatasema na Uthman hadi mwisho wa uhai wake. Sasa mambo haya yakajulikana na kila mtu akawa anamshutumu Uthman.

Taarifa zilikuwa zinamfikia Uthman pia. Siku moja aliagiza Waislamu wote wakusanyike msikitini. Watu walipokusanyika Uthman alipanda kwenye mimbari, akamsifu Mwenyezi Mungu na kukariri Salawat na Salam kwa ajili ya Mtukufu Mtume. Baada ya hapo akasema; “Enyi watu! Endeleeni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ukarimu Wake ili kwamba neema na utajiri unaweza kuongezeka. Mkumbukeni Yeye wakati wote, chukueni Jina Lake, na mzingatie haki Zake. Nyinyi ni Waislamu na muwe nacho Kitabu cha Mungu ambamo kila kitu kimeandikwa.

“Tambueni kwamba kuweza kukalia kiti cha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na kuendesha ukhalifa ni kazi ngumu sana. Pia cheo cha Ukhalifa kipo nje ya uwezo wenu wa kuelewa. Mwenyezi Mungu amewapa utawala Mawalii na Maamiri ili waweze kuamua ugomvi baina ya wanyonge na wenye uwezo na kuwazuia wenye uwezo wasiwakandamize wanyonge.

“Mjue kwamba ni amri ya Mwenyezi Mungu kumtii mtawala. Muwe na hofu kwa Mwenyezi Mungu. Mfuate maagizo Yake. Mjiepushe na upinzani na dhambi.

“Wapo wengi miongoni mwenu ambao wameona siku za Mtukufu Mtume, wamesikia mazungumzo yake matakatifu na wameshuhudia matendo yake. Zaidi ya hayo, Kitabu cha Mwenyezi Mungu kipo mikononi mwenu. Lazima mmezisoma amri zote na makatazo yote na matendo mema na maovu. Mwenyezi Mungu amekupeni tangazo Lake la mwisho, Ameahidi kuwazidishia neema wale watakao mshukuru Yeye kwa neema hizo. Watu waadilifu watapata thawabu na adhabu watapewa waovu.

“Tayari nimesikia ufahari na maonyesho na utukufu na uwezo wa wafalme na watawala. Wao walikuwa na uwezo zaidi kuzidi sisi na walikuwa na majeshi makubwa zaidi. Walikuwa na majiji makubwa na walikuwa wanaishi kwenye raha na starehe, lakini, kwa kuwa hawakutekeleza amri za Mwenyezi Mungu, walipenda zaidi dunia kuliko pepo, walipenda zaidi ugomvi na vurugu, na hawakutaka kumshukuru Yeye kwa ajili ya neema Zake. Aliwaweka kwenye uoza, na akawapeni nyinyi miji yao, nyumba zao na malisho yao na akawapeni neema zao zote. Neema zitabaki kwenu kama mkiendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu kwazo, au vinginevyo zitapunguzwa kwa sababu ya dhambi zako na kutokuwa mtiifu na hatimaye mtaangamia.

“Mwenyezi Mungu amenipa mimi Ukhalifa wa Mtume. Nina uwezo wa kufanya kazi hii leo. Nimechukua ofisi hii mkononi mwangu na ninafanya kazi muhimu na nzito.

“Mwenyezi Mungu huyu huyu ambaye amenipa Ukhalifa, hunipa uwezo unaolingana na ridhaa Yake, na pia nilitambua siri ya sentensi: Wote nyinyi ni walinzi na wote mtaitwa kuhesabu masuala yenu, na mmeelewa ukweli ulio wazi kwamba mtu ambaye amefanywa kuwa kamanda, amepewa dhamana kueleza kila tendo la watu wake na kuhesabu kila chembe na atomi.

“Watu wameniambia kwamba baadhi yenu waneweka pingamizi kuhusu fedha ninayotumia na wanaambizana kwamba ingelikuwa vizuri kama Uthman angeliwapa fedha hizi wapiganaji na watoto wao. Kwa vyovyote vile lingekuwa jambo la manufaa na lingekubaliwa na Mwenyezi Mungu. Ninakubali na nitaendelea kukubali siku zijazo. Nimewatuma watu wa kuaminika katika kila jiji na kuwagawia wapiganaji na watoto wao fedha nyingi kadiri watakavyokusanya na kuweka akiba zitakazobaki kwa matumizi wakati zitakapohitajika.

“Inshallah, nitakuwa ninawalipia haki zao wazee, fakiri, mayatima na wajane, nitataka ushauri wenu ninapokuwa na muda, kuhusu mambo yanayojitokeza na kuhitaji kufikiriwa na nitatekeleza kufuatana na ushauri wenu.

“Njooni kwangu mara kwa mara, zungumzeni na mimi matatizo na manufaa na nielezeni yale mnayoona yanastahili. Nitafanikisha kazi kama mnavyotaka na kufuatana na dharura itakayo kuwepo muda huo. Sina mlinzi mlangoni kwangu wa kuwakagua nyinyi. Mtu yeyote anaweza kuja wakati wowote na kuniambia lolote atakalo. Amani iwe kwenu!”

Baada ya kumsikia Uthman Waislamu wote walifurahi na walirudi kwao wakimsifu na kumwombea. Uthman alifuata njia ya haki, akazingatia usawa baina ya wapiganaji na raia, aliwafanya wema watu wote na aliwatimizia masikini na mayatima. Mwaka mmoja ulikwisha katika hali hii.

Kwa mara nyingine tabia yake ilibadilika kufuata taratibu ambazo zilikuwa kinyume na Sunna na uadilifu. Masahaba wa Mtume walikasirika sana. Walifanya mkutano na wakaamua kumuona Khalifa na wawasilishe kwake orodha ya maandishi ya mambo hayo ambayo yanachukiza katika Uislamu na ambayo yametokea tangu alipochukua cheo cha ukhalifa, kwa sababu mazungumzo ya mdomo yangeweza kusahaulika na hata kama wangekumbuka baadhi ya mambo muhimu lakini wangeshindwa kuyabainisha wazi wazi. Kwa hiyo ilionekena ni busara kuyaandika mambo hayo. Baada ya hayo, waloandika mambo yote matatu yanayopingana na dini ambayo yalitokea tangu mwanzo wa Ukhalifa wa Uthman hadi muda huo, na walitaka waende wote kwa pamoja kukabidhi Khalifa waraka huo.
Halafu, watu hawa walionana na Ammar bin Yasir, wakamwambia walichoandika na wakamwomba awasilishe waraka huo kwa Uthman.

Ammar akajibu kwamba alikuwa tayari kufanya hivyo. Halafu akaenda kwa Uthman na waraka ule. Wakati ambapo khalifa alikuwa anatoka nje ya nyumba yake, Ammar alikuwa amefika mlangoni na akamuuliza, “Ewe Abul Yaqzan! Unataka kuniona?” Ammar akajibu, “Sina jambo lolote la kibinafsi na wewe lakini masahaba wa Mtume kwa pamoja wameandika orodha ya matendo yako ambayo umeyafanya kinyume na sharia ya dini , ili ufafanue maoni yako.”

Uthman alichukua waraka huo akiwa amekasirika, alisoma mistari michache halafu akazitupa. Ammar akamwambia, “Usitupe kwa kuwa makaratasi haya yameandikwa na masahaba wa Mtume (s.a.w). Badala yake, soma kwa uangalifu na utoe jibu ipasavyo, ninakuambia mambo haya kwa maslahi yako.” Uthman akasema, “Ewe mwana wa Sumayyah! Unasema uwongo!” Akajibu, “Bila shaka mimi mtoto wa Sumayyah bin Yasir.”

Khalifa akakasirika. Akaamuru watumishi wake wampige Ammar, sahaba wa Mtume (s.a.w). Alipigwa sana hivyo kwamba alianguka chini na kupoteza fahamu. Halafu yeye mwenyewe Uthman alimpiga Ammar mateke kadhaa tumboni na sehemu za siri. Ammar akapoteza fahamu tena. Alipata mpasuko tumboni na kusababisha ngiri.

Watu wa bani Makhzum ambao walikwua ndugu zake Ammar, walikwenda na Hashim bin Walid bin Mughirah waliposikia habari hizo. Wakamchukua Ammar na kumlaza kitandani. Ammar alikuwa bado amepoteza fahamu ambapo watu wote waliapa kiapo kwamba endapo angekufa, kwa sababu ya kipigo wangemuua Uthman. Wakati Ammar bado hana fahamu, vipindi vya Swala vya adhuhuri na jioni vilipita. Alipopata fahamu wakati wa usiku aliamka, akatawadha na kusali Swala zake za vipindi vilivyopita.

Jambo hili la Ammar pia ni mojawapo ya matendo mabaya ya Uthman ambayo yalisababisha masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w) kuvunja kiapo cha uaminifu kwa hasira (Tarikh Aatham Kufi, uk. 126-130). Hili ni tukio moja tu ambalo limeandikwa kwenye vitabu vya historia. Ifuatayo ni mifano michache kutoka kwenye vitabu vya kuaminika na mashuhuri vya historia, ili ijulikane ni matendo gani aliyoyafanya wakati wa Ukhalifa wake na alifanya kwa umma na masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w).

Imeandikwa kwenye Tarikh Khulafa cha Suyuti, kwamba Uthmani alikuwa mtu wa kwanza kuanzisha Adhan ya kwanza kabla ya Sala ya Ijumaa. Kufuatana na ‘al-Wasail Fi Marifatul Awail’ Uthman alikuwa mtu wa kwanza kufanya hotuba itangulie Swala ya Idd. Kamwe haikufanyika wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w) na wakati wa utawaka wa khalifa wa kwanza na wa pili. Kwa mujibu wa taarifa ya Masoud iliyopo kwenye, Murujuz Dhahab, Uthman alipopata Ukhalifa, mjomba wake Hakam bin al-Aas, Marwan bin Hakam na wengineo kutoka Bani Umayyah (ambao walifukuzwa Madina kwa amri ya Mtume) walikusanyika kwa Uthman. Marwan alikuwa ni yule yule aliyetengwa na kutolewa Madina na Mtume na alikatazwa kusogea karibu na Madina.

Pia magavana walioteuliwa na Uthman, alijumuishwa kaka yake upande wa kikeni, Walid bin Uqbah ambaye Mtume alikwisha sema habari zake kwamba angekwenda Jahanamu. Walid bin Uqbah alikuwa na tabia ya kunywa kilevi na marafiki zake wapiga muziki na Malaya usiku kucha, na muadhini alikuwa akimwamsha kwa ajili ya Swala, naye (akiwa amelewa) alikwenda msikitini kuongoza Swala ya alfajiri, na baada ya Swala kusalisha rakaa nne badala ya mbili, alionesha kutaka kuendelea na rakaa zingine endapo watu walitaka kuendelea.
Pia imeandikwa kwamba Walid akiwa kwenye rukuu ya Swala alikawia kunyanyuka na kusema; kunyweni na mnifanye mimi ninywe. Kwa hiyo, mara mmoja ilitokea watu waliokuwa mstari wa mbele nyuma yake walisema, ‘Hatukushangai wewe lakini tunamshangaa yule aliyekuleta wewe hapa ili uwe kamanda wetu.” Taarifa ya ufisadi wa Walid na kulewa kwake ilipoenea kwa watu wote, kundi la Waislamu, akiwemo Abu Jundab na Abu Zaynab, walimzonga Walid msikitini. Wakamuona amelala na hana fahamu.

Watu walijaribu kumwamsha, lakini aliposhindwa kupata fahamu, walichukua pete yake ya alama kutoka kwenye kidole chake na haraka walikwenda Madina na kutoa taarifa ya ulevi wa Walid kwa Uthman. Uthman alimuuliza Abu Jundab na Abu Zaynab walijuaje kama Walid alilewa mvinyo. Walisema huku wanampa pete yake kama ushahidi wa ulevi wake. Alikunywa mvinyo huo huo tuliokuwa tunakunywa wakati wa siku za ujahiliya (kabla ya Uislamu). “Badala ya Uthman kusikiliza mazungumzo yao yote, alianza kuwalaumu na kuwasukuma huku akisema, “Ondokeni hapa.” Waliposikia hivi wote wawili walirudi haraka.

Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida Uthman alimfukuza Amr bin al-Aas kwenye ugavana wa Misri na badala yake akamteua kaka yake wa kuchangia ziwa Sad bin Ali Sarh na ni mtu huyu huyu ambaye Mtume alikwisha toa ruhusa ya kuuawa siku Makah ilipotekwa na Waislamu.

Kwa mujibu wa Tarikh Kamil, Uthman alikwenda Hija mwaka 26 A.H. Marwan bin Hakim anasimulia kwenye Musnad Abu Daud Tialisi. Nilimuona Uthman na Ali wakati wa Hija. Uthman alikuwa anawakataza watu kufanya Hija ya Mut’a (kutekeleza Hija na Umra). Ali alipoona hivi alikariri Tahlil (La ilaha illallah) ya Hija na Umra kwa pamoja na akasema; “Nipo hapa kwa Hija na Umra pamoja,” Uthman akasema, “Ewe Ali! Unafanya jambo lile ambalo nimekataza watu wasifanye,” Ali akajibu, ‘Sitaacha Sunna ya Mtume kwa ombi la mtu.” (Hadith hii inaweza kuonekana kwenye Sahih Bukhari pia).

Sura Ya Kumi Na Mbili

Abdul Hamid wa Misri na Allamah Abdullah Subaiti wameandika kwamba Abu Dharr alikaa Madina baada ya kifo cha Umar. Aliona kwamba Uthman alikuwa anawapendelea Bani Umayyah ambao mvuto wao ulipenya kwa kina kirefu katika serikali ya Kiislamu ambapo ilikwisha pata utukufu wa himaya. Watu waliendekeza ufahari na maonesho na waliishi maisha ya anasa sana. Watu walipendelea zaidi pato la dunia.

Aliona kwamba masahaba wengi walibadilika kabisa. Zubayr, Talha na Abdul Rahman bin Auf (wakawa wamepatana na serikali) walinunua ardhi na nyumba! Sad bin Abi Waqqas alikuwa na mawe magumu yaliyo kongomewa kwenye ikulu yake, aliinyanyua sana, akapanua na akajenga minara juu yake.

Kwa hiyo, Abu Dharr alisimama na akajitokeza wazi wazi. Hangevunjwa moyo na kamanda au Khalifa yeyote. Alianza kuwaita watu na kuwataka washikilia maadili na kumshambulia Uthman katika hotuba zake.

Siku moja alitambua kwamba Uthman alimpa moja ya tano ya ushuru kutoka Afrika Marwan bin Hakam, dinari 300,000 alimpa Harith bin al-As, Zayd bin Thabit alimpa dinari 100, 000, Abdullah bin Ali Sarah kaka yeke wa kuchangia ziwa, alimpa sehemu kubwa sana isiyo na idadi ngawira kutoka Afrika, na ardhi ya Fadak iliyoporwa kwa Fatimah alimpa Marwan alianza kukariri aya hii msikitini:

وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَبَشِّرْهُمْ بِعَذَابٍ أَلِيم{34}

“Na wanaokusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia za Mwenyezi Mungu.” (Quran Tukufu, 9:34).

Marwan akatambua kwamba Abu Dharr alimshambulia yeye na Uthman, akalalamika kwa Uthman ambaye alimuagiza mtumishi wake amwite Abu Dharr aende kwake. Abu Dharr alikwenda kwake. Uthman alipomuona akasema, “Abu Dharr! Acha hayo ambayo nayasikia, vinginevyo hutamuona mtu yeyote aliye na madhara kwako isipokuwa mimi.” Abu Dharr akasema, “Ewe kamanda! Umesikia ninasema nini?” Uthman akasema, “Nimetambua kwamba unawachochea watu dhidi yangu.”

Abu Dharr aliuliza, “Kwa vipi?” Uthman alisema, “Unakariri aya ‘Tangaza . . . mateso machungu . . . ndani ya msikiti.” Abu Dharr akasema, “Ewe kamanda! Unanikataza mimi nisikariri kitabu cha Mwenyezi Mungu na nisifichue dosari za wale ambao wameacha amri za Mwenyezi Mungu! Kwa jina la Mwenyezi Mungu, siwezi kumkosea Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Uthman. Hasira ya Uthman ni bora zaidi kwangu kuliko hasira ya Mwenyezi Mungu.”

Aliposikia hivi Uthman alimkunjia uso Abu Dharr lakini hakuweza kuamua ajibu vipi maneno ya Abu Dharr. Kwa hiyo, hakusema kitu na akanyamaza kwa muda fulani. Abu Dharr alisimama na akaondoka hapo, akiwa na azimio madhubuti la kuwakosoa wale ambao walikuwa wanafanya kinyume na amri za Mwenyezi Mungu kuliko kipindi chochote kile.

Abu Dharr alimshambulia Uthman mara nyingi zaidi. Kwa hiyo alikasirika sana na alingojea fursa ijitokeze amfukuze Abu Dharr aende uhamishoni. Siku moja alipata nafasi na akaitumia.

Kwa mujibu wa Bin Wazir mwandishi wa Tarikh Yaqubi, watu walimwambia Uthman kwamba Abu Dharr Ghifari alimdhihaki yeye msikiti na alitoa hotuba kwenye lango la msikiti ifuatayo:

“Enyi watu! Yule anayenijua mimi ananijua mimi, lakini yule ambaye hanijui mimi, ambaye hanitambui ajue kwamba mimi ni Abu Dharr Ghifari. Jina langu ni Jundab bin Junadah Rabazi.

Mwenyezi Mungu alimnyanyua Adam, Nuh, uzao wa Ibrahim na watoto wa Imrani, miongoni mwa watu wa duniani. Mtume Muhammad ni mrithi wa ujuzi wa Adam na maadili yote ambayo yaliwabainisha Mitume, na Ali bin Abi Twalib ni mrithi wa Mtume na mrithi wa ujuzi wake.

“Enyi watu mliokanganyikiwa! Endapo baada ya Mtume wenu mlimpenda yule ambaye Mwenyezi Mungu amempenda na alimweka nyuma yule ambaye Mwenyezi Mungu alimweka nyuma na amaeuwekea mipaka utawala na urithi miongoni mwa Ahlul –Bait, mungepata neema zisizo na hesabu kutoka juu ya vichwa vyenu na kutoka chini ya miguu yenu na hakuna rafiki yake Mwenyezi Mungu angekuwa masikini na fukara, na hakuna sehemu ya wajibu wa Dini ingepotezwa, na hakuna watu wawili ambao wangepambana kwa sababu ya amri ya Mungu kwa sababu wangepata taarifa kuhusu amri hiyo kwenye Kitabu cha Mungu na Sunna za Mtume, kwa mujibu wa Ahlul-Bait kuhusu Mtume wao.

Lakini kwa kuwa mmekusudia kufanya yale ambayo hamkufanya, lazima mtapata adhabu kwa sababu ya maovu yenu, na haikuchukua muda mrefu kabla ya hao ambao wamefanya uovu watajua watarudi kwa nani.”

Pia imeandikwa kwenye kitabu hicho hicho kwamba Uthman pia alipata taarifa kwamba alifanya mabadiliko ya Sunna za Mtukufu Mtume na Sunna za Abu Bakr na Umar kwenye msingi ambapo ndoto ya Ukhalifa wake ulitokeza, na kwamba Abu Dharr aliweka lalamiko hilo mbele ya Umma. Uthman aliposikia mambo haya, alimpeleka kwa Muawiyah, gavana wa Syria. Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, tukio hili lilitokea mwaka wa 30. A.H.

Wasomi wanasema kwamba kwa kuwa Abu Dharr aliendelea kumkosoa Uthman kwa matendo yake ambayo yalikiuka sheria za dini, Uthman alimwekea mipaka mikali. Uthman aliagiza kwamba hakuna mtu aliyeruhusiwa kuzungumza na Abu Dharr au kwenda naye au kukaa naye. Mikutano iliitishwa mara kwa mara kutangaza agizo hili.

Kwa mujibu wa maelezo ya Allamah Majlis na Allamah Subaiti, Ahnaf bin Qays mara nyingi alikuwa na mazoea ya kwenda msikitini na kuketi humo siku moja aliomba kwa Mwenyezi Mungu; “Ee Mola! Nibadilishie kutokuchangamana kwangu na watu niwe na upendo na upweke wangu na watu wa kuwa nao na nipe rafiki anayefaa asiye na mfano.”

Baada ya kumaliza Swala hii alimuona mtu amekaa na kufanya ibada kwenye pembe ya msikiti. Alinyanyuka kutoka alipoketi na akamwendea mtu huyo na kuketi karibu naye. Halafu akasema, “Wewe ni nani na jina lako ni nani?” Akajibu, “Jundab bin Junadah.” Aliposikia hivi akasema, Mwenyezi Mungu mkubwa! Mwenyezi Mungu Mkubwa.”

Abu Dharr akasema, “Kwa nini ulikariri Takbira?” Akajibu, “Nilipoingia msikitini leo nilimwomba Mwenyezi Mungu anipe rafiki mzuri sana. Ametimiza matakwa yangu haraka sana na amenipa mimi heshima ya kukutana na wewe.”

Abu Dharr akasema, “Ninamwita Mwenyezi Mungu, zaidi yako, kumtukuza Yeye kwa sababu niliamriwa anayefaa. Ewe binadamu! Nisikilize mimi. Mtukufu Mtume ameniambia kwamba wewe na mimi tutakuwa sehemu ya juu sana na tutabaki hapo hadi watu wote wamefanyiwa hesabu.”

Abu Dharr aliendelea kusema; “Ewe mja wa Mwenyezi Mungu! Kaa mbali na mimi vinginevyo utapata matatizo.” Akauliza, “Vipi hivyo rafiki?” Abu Dharr alimjibu, “Uthman bin Affan amenikataza nisikae na watu na ameagiza kwamba yeyote atakayekutana na mimi na kuzungumza na mimi ataadhibiwa.” (Hayatul Qulub, cha Allamah Majlis Juzu ya 2, na Abu Dharr bin Al-Ghifari, cha Allamah Subaiti).

Kwa ufupi, Uthman alikasirishwa na ukweli wa Abu Dharr. Naye aliendelea na kazi yake licha ya kuwekewa mipaka; na Uthman alipata taarifa kama kawaida. Hatimaye, alipochoshwa na Abu Dharr aliamua kumpeleka uhamishoni Syria.

Sura Ya Kumi Na Tatu

Waandishi wa historia wanasema kwamba Uthman alipochoshwa na kilio cha kutetea ukweli cha Abu Dharr alimfanyia kila aina ya ugandamizaji huko Madina. Amri yake ilikuwa hakuna ruhusa mtu yeyote kusema na kukaa naye. Alilazimishwa kunyamaza, lakini kilio chake cha kutetea ukweli kiliendelea.

Alipotoa hotuba kwenye msikiti wa Mtume, watu waliyasikia maneno yake. Alipozungumza kuhusu masuala yanayohusiana na makatazo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hotuba yake ilisisimua nyoyo za watu wa kawaida. Watu walizidi kuudhika kwa sababu ya matendo maovu na shughuli za Uthman zilikuwa kinyume na Uislamu. Kwa hiyo, kisiasa aliona inafaa kumtoa nje ya mji. Katika kutekeleza lengo hili alimpeleka Syria. Labda alidhani kwamba kwa kuwa Muawiyah alikuwa Gavana wa Syria na pia mwerevu sana, Abu Dharr angepooza kabisa huko.

Kufuatana na uamuzi wake, Uthman alimlazimisha Abu Dharr kwenda Syria.

Abu Dharr aliondoka na kuacha maskani yake akiwa na familia yake na akafika Syria. Kufika kwake Syria ni tukio liliolothibitisha utabiri wa Mtume (s.a.w) ambao alitamka mbele ya Abu Dharr walipokuwa katika mazungumzo siku za nyuma. Kufuatana na ushawishi wa Mtume alioonesha uvumilivu na alikubali uhamisho wake bila ubishi (al-Ghadir Allamah Amyn, Juz. 8, uk. 302).

Abu Dharr alikwisha choshwa na kuchukizwa na mwenendo wa Uthman uliokiuka mafundisho ya Kiislamu, lakini alipofikia Syria na kuona tabia ya Muawiyah ambayo ilikuwa inaharibu Uislamu, alishangaa sana na akajisemea peke yake kwamba mfumo wote wa utawala ulikuwa mbovu. Alilazimika kufikiria kuhusu mtindo wa maisha ya Muawiyah kwamba Uislamu kama ulivyo dhihirishwa na Mtume si tu ulikuwa unadhoofu lakini ulikuwa unazimwa.

Kufuatana na hali hii, hisia zake za kawaida zilisisimuka.

Alilazimika kuanzisha tena kilio cha ukweli kufuatana na sifa zake za uaminifu na kusema kweli. Kwa kuwa alikuwa jasiri sana, hakusita kusema kweli; kwa hivyo, bila kufikiria kwamba Muawiyah alikuwa ndiye mtawala wakati huo, alianza kufanya kazi zake za Kiislamu na akaanza kusema kwa lengo la kumzuia Muawiyah. Alimwambia wazi kwamba alikuwa anaendesha utawala kinyume na Uislamu kama ule wa Uthman bin Affan. Alamah Subaiti ameandika kwamba Uthman alipochukua hatua ya kumhamisha Abu Dharr na kumpeleka Syria ni uthibitisho wa uhakika wa kweli kwamba alikuwa anakwepesha msimamo wa ukosoaji wa Abu Dharr kutoka kwake kwenda kwa Muawiyah (Abu Dharr al-Ghifari).

Mwandishi wa historia Balazari, Allamah Majlis, Allamah Subaiti na Allamah Amyni wameandika kwamba Abu Dharr alipofika Syria Muawiyah alikuwa anajenga Ikulu yake ‘al-Khizra.’ Maelfu ya vibarua walikuwa wanafanya kazi hapo.

Siku moja Muawiyah alikuwa anaiangalia Ikulu hiyo kwa majivuno. Abu Dharr akamuona, akamkaribia, na akasema, “Ewe Muawiyah! Endapo Ikulu hii inajengwa kwa kutumia hazina ya Taifa ni uvunjaji wa uaminifu na endapo inajengwa kwa fedha yako binafsi ni ubadhirifu.”

Aliposikia hivi Muawiyah alinyamaza kimya, aligeuza uso wake na kutazama upande mwingine na hakujibu. Abu Dharr aliondoka na akafika msikitini. Alitafuta nafasi akaketi. Baadhi ya watu walilalamika kwa Abu Dharr kuhusu Muawiyah kwa kusema kwamba hawajapata chochote katika zawadi ambazo hutolewa na sasa mwaka umepita.

Abu Dharr aliinamisha kichwa chake kuelekea mbele halafu akasimama. Watu walimwangalia.
Akasema; “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, bidaa za namna hii zinaenea siku hizi kwani hazipo kwenye Quran Tukufu au Hadith za Mtume. Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, nimeona kwamba ukweli unadumazwa na uwongo unazidi kuwa na nguvu. Watu wakweli wanasingiziwa kuwa waongo na waovu wanapewa upendeleo kuzidi waadilifu.

Enyi watu wakuu! Ewe Muawuyah na magavana wake! Wasikitikie masikini. Wale wanaokusanya dhahabu na fedha na hawatumii katika njia ya Mwenyezi Mungu, wanajua kwamba nyuso zao, pande zote na migongo yao itapigwa chapa ya moto. Enyi mnaohodhi utajiri! Hamjui kwamba mtu anapokufa kila kitu hufarakana naye. Vitu vitatu tu hubaki naye; sadaka ya kudumu, elimu yenye manufaa, na mtoto mwema, ambaye humwombea yeye.”

Watu walisikia mhadhara wake wanaogandamizwa na masikini walikusanyika kumzunguka yeye na matajiri wakaanza kumuogopa. Habith bin Muslim Fahri alipoona kundi la watu karibu na Abu Dharr alisema, ‘Hali ni kero kubwa!” alikwenda kwa Muawiyah haraka na akamwambia; “Ewe Muawiyah! Abu Dharr atavuruga kabisa utawala wa Syria. Endapo unawahitaji watu wa Syria, lazima uzuie usumbufu huu kabla haujakomaa.Muawiyah alitafakari jambo hili peke yake.

“Nimshughulikie kwa ukali au kwa upole? Nikitumia ukali moto utawaka na kuenea. Je, Ni lazima nilalamike kwa Uthman? Lakini, Uthman atasema nini? “Atasema kwamba sikuweza kumfanya atengamae hata mtu mmoja miongoni mwa raia wangu. Kwa hiyo ni vizuri zaid kumwondoa Syria.”

Imekuwa ni mazoea ya kawaida kukandamiza kwa ukali maneno ya kweli ya watu wa kimungu kwa sababu ya uchungu wao. Ingewezekana wapenda dunia wanyamaze baada ya kusikia hotuba za Abu Dharr zenye hamasa ya kidini hilo ni la kawaida. Lakini inawezekanaje mtu ampende Muawiyah, baada ya ushauri wa Abu Dharr na angewezaje kuvumilia maneno yake makali?

Abu Dharr alitumia sauti ya kunasihi na alikuwa na desturi ya kukariri Aya ya Qurani:

وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَبَشِّرْهُمْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ{34}

“Na wanaokusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii kwa njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie habari ya adhabu iliyo chungu.” (Quran 9:34).

Na ilikuwa ni kawaida yake kwamba alikariri aya hii dhidi ya Muawiyah mwenye mitaa mingi zaidi na barabara za Syria. Kila alipokiariri Aya hii, masikini na wenywe kuhitaji wakimzunguka yeye na mara nyingi walimlalamikia kuhusu magavana wanaotafuta anasa za utajiri na umasikini wao.

Muawiyah alikuwa na kawaida ya kupata taarifa ya mahubiri yake mara kwa mara. Hatimaye alimwekea mipaka mikali na kumtesa kwa kila njia. Ilipoonekana kwamba hata hatua hii haikufaa, alimtishia Abu Dharr kwa kifo.

Abu Dharr aliposikia tishio hilo la kifo alisema, “Ufalme wa Muawiyah unanitishia mimi kwa umasikini na kifo. Ninapenda kuwaambia kwamba umasikini ni wa kutamanika zaidi kwangu kuliko utajiri, na ninapenda kuwa chini ya ardhi kuliko kuwa juu yake.

Wala siogopeshwi kwa tukio la kifo, ama kifo chenyewe.”

Allamah Majlisi ameandika kupitia kwa mamlaka ya Shaykh Mufid watu wa Syria walisema nini kuhusu hotuba nzito za Abu Dharr; “Uthman alipomhamisha Abu Dharr kutoka Madina kwenda Syiria, aliishi miongoni mwetu, na akaanza kuhutubia mlolongo wa hotuba ambazo zilitusisimua sana.

Alikuwa na mazoea ya kuanza hotuba yake kwa kumsifu Mwenyezi Mungu na Mtume na halafu alisema; “Kuwapenda uzao wa Mtume (s.a.w) ni wajibu wa kila mtu. Yule asiye wapenda hawa hatanusa hata ile harufu ya Pepo.”

Halafu aliongeza; “Enyi watu! Nisikilizeni. Nilikuwa na kawaida ya kuheshimu maagano yangu kabla sijakubali Uislamu, wakati wa ujahiliya kabla ya wahyi wa Quran na kabla ya kuteuliwa kwa Mtume. Alisema kweli, niliwafanyia wema majirani zangu, niliona kwamba ukarimu ni wajibu wangu, nilikuwa nawakirimu masikini, na niligawia utajiri wangu.

“Baadaye, Mwenyezi Mungu alipoleta ufunuo wa Kitabu chake na akamteua Mtume wake, niliulizia kuhusu mambo haya nikatambua kwamba ni namna na desturi zile zile tulizokuwa tunazitumia sisi, pia zilikuwepo kwenye nasaha za Mtume.

“Enyi watu! Inafaa zaidi Waislamu kuwa waadilifu. Ni kweli kwamba Waislamu walifuata mwenendo kufuatana na mafundisho ya Uislamu, lakini rafiki zangu! Tabia ya Waislamu ilikuwa njema kwa kipindi kifupi. Halafu ilitokea kwamba madhalimu walionesha matendo maovu ambayo tulikuwa hatujayaona kabla yake. Watu hawakuharibu Sunna za Mtume, walianzisha bidaa, walimpinga mtu aliyesema kweli, wakaungana na kundi la watu waovu na kuwaacha wale waliokuwa wacha Mungu na wanaofaa.

“Ewe Mwenyezi Mungu! Ichukue roho yangu endapo unayo mambo mazuri kwa ajili yangu kuliko haya yaliomo katika dunia hii, kabla sijapotosha imani Yako au kubadili Suna za Mtume Wako.”

‘Enyi watu! Shikamaneni na ibada ya Mwenyezi Mungu na mjiepushe na dhambi.” Halafu akaelezea sifa za Ahlul Bait ambazo alizisikia kutoka kwa Mtume na akawashauri watu waambatane na Ahlul Bait.

Watu wa Syria wanasema kwamba walisikiliza hotuba zake kwa umasikini sana na kundi kubwa la watu lilikusanyika kumzunguka yeye alipokuwa anahutubia, hadi Muawiyah akamtaarifu Uthman kuhusu matukio haya, kwa hiyo, alimwita Abu Dharr aende Madina.

Kwa kuwa Abu Dharr alimuudhi sana Muawiyah kwa mihadhara yake ya kidini, yeye, katika jitihada ya kumnyamazisha kwa vyovyote vile alifanya ujasiri wa kumpelekea mfuko wa fedha kwa sababu hakuweza kufikiria njia nyingine yoyote ya kufanya.

Wasomi na waandishi wa historia wanasema kwamba Muawiyah alimpelekea Abu Dharr mfuko wa dinari za dhahabu mia tatu zilizopelekwa na mjumbe ili kumnyamazisha. Alipoona hivi alisema, “Mwambie Muawiyah kwamba sihitaji fedha yoyote kutoka kwake,” na akarudisha mfuko huo. (al Ishtiraki az-Zahid, Tarikh Balazari, al-Ghandir, Juz. 8, uk. 293).

Abu Dharr aliona kwa macho yake baada ya kifo cha Mtume matukio yote hayo ya hatari ambayo Ale Muhammad (Uzao wa Mtume) walilazimishwa kupambana nayo.

Alisema wazi dhidi ya kuhodhi utajiri, kwani alikwisha elewa kwa ukamilifu, lengo la Hazina ya Taifa na madhumuni ya Qurani Tukufu, aliona namna ya utendaji wa Mtume na alikuwa anachunguza mwenendo wa maisha ya uzao wa Muhammad.

Alipoona tabia na namna ya maisha ya wale wenye madaraka ya Ukhalifa ni kinyume kabisa na Suna hizi, alihisi wasi wasi sana kwa sababu ya imani yake kuwa imara. Kamwe alikuwa hajafikiria yale aliyoyaona kwa macho yake. Mara tu baaada ya Uthman kushika hatamu ya serikali na Ukhalifa, alilazimisha hisia zake kutoka kwanye moyo wake na kuzipeleka mdomoni mwake na alilazimika kifichua kile alichokificha moyoni mwake kwa muda mrefu.

Aliona kwamba utajiri uliongezeka kuliko alivyofikiria, upendeleo na fadhila kwa ndugu ni mambo ambayo yalifika upeo wa juu sana, utajiri wa Hazina ya Taifa ulikuwa inagawiwa kwa ndugu, marafiki na wanaomunga mkono badala ya watu wanaostahili, bila hata kufikiria , na kwa sababu ya utajiri huu bida zilizokuwa zinatikisa misingi ya Uislamu, zilikuwa zinaongezeka bila ya kuzuizi.

Kwa hiyo, kufuatana na mkataba wa uaminifu aliofanya na Mtume, alianza kukataa na kuwakosoa wale wenye kuwajibika, ambayo matokeo yake alihamishwa Madina na kupelekwa Syria. Huko aliona bidaa nyingi za kutafuta starehe ambazo zilikuwa zinapingana na Uislamu na ambazo zilizidi hata njia za maisha ya anasa za Kaisari (wa Roma)na Khussoe (Shah wa Uajemi).

Kwa kuwa alilazimishwa na amri ya Mtume, na ahadi iliyofanywa kwake, na pia kwa uimara wake, wa kidini alianza pia kuhubiri huko. Alianza kuhadhiri huko Syria chini ya mwongozo wa Aya ile ile ya Quran ambayo ilikuwa kiini cha hotuba zake Madina. Katika uhusiano huu, alihutubia hotuba nyingi, baadhi ya hizo zimetajwa kwenye kurasa za nyuma.

Maelezo ya hotuba yake ya kushutumu kuhodhi utajiri ilikuwa Aya ifuatayo:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ كَثِيرًا مِنَ الْأَحْبَارِ وَالرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ وَيَصُدُّونَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ ۗ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَبَشِّرْهُمْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ{34}

“Enyi mlioamini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa batili na wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie habari ya adhabu iliyochungu. Siku zitapotiwa moto katika Moto wa Jahanamu, na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, wakaambiwa; Haya ndio mliyojilimbikizia nafsi zenu, basi onjeni mliyokuwa mkilimbikiza.” (Qurani 9:34).

Wasomi na waandishi wa historia wanasimulia kwamba alipokuwa anahutubia kundi huko Syria, alisema; “Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Ninaamini kwamba kweli utaangamia, udanganyifu unaendelezwa, watu wa kweli wanawekewa pingamizi na watu wanaendekeza uchoyo badala ya uchaji Mungu.” (al-Balazari, Juz. 5, uk. 56).

Aliendelea kusema; “Dhahabu na fedha zitageuka kuwa miale ya moto na zitawazunguka wale wanaoziweka kwa kuzifungia hadi wazitumie katika njia ya Mwenyezi Mungu.” Akisisitiza jambo hili alisema; “Vipande vilivyochomwa moto wa Jahanamu vitawekwa kwenye vifua vya wale wanaokusanya dhahabu na fedha, hadi vitoboe mbavu zao na mifupa ya mabega yao.” (Sahih Bukhari-Kitab az-Zakat).

Abdul Hamid, mwandishi wa Misri ameandika kwamba Abu Dharr alipowasili kwenye msikiti watu walikusanyika na kumzunguka na akawaambia; “Tumieni chochote ambacho Mwenyezi Mungu amewapeni. Tahadharini sana hivyo kwamba maisha ya dunia yasiwadanganye. Weka fungu la rasilimali yako liwe haki ya wasio nacho. Mtume amesema kwamba tama ya wingi wa rasilimali imefanya mzame kwenye kusahau.”

Mwanadamu anasema; “Mali yangu! Mali yanngu! Lakini mali yako ni ile ambayo umekula imeksisha au umetoa sadaka; kwa maana kwamba umeweka kwa lengo la kuhifadhi. Mwenyezi Mungu amezuia kuhodhi mali.

“Mtume amesema; “inasikitisha, inasikitisha dhahabu na fedha,” Ngawira ni haki ya Waislamu, lakini Muawiyah amehifadhi na kuitumia kwa watumishi na walinzi wake na kwa ufahari na maonesho yake. Muawiyah amesahau kwamba ni majoho mawili tu yanaruhusiwa kwake kutika kwenye hazina ya Taifa, moja kwa alili ya majira baridi na lingine kwa ajili ya majira ya joto. Zaidi ya hayo, anaweza kuchukua matumizi ya Hijja na familia yake tu kama ambavyo familia ya tabaka la kati ya Quraishii inaweza kuchukua.

“Ngawira lazima igawanywe kwa miongoni mwa Waislamu wote walio masikini. Lakini, sasa ardhi inatwaliwa, na nyumba zinajengwa, na maelfu ya dinari yanatumika katika kuziremba nyumba hizi na Waislamu walio masikini wanatelekezwa.”

Mtu alimnong’oneza sikioni mwake, “Tafadhali! Unasema nini kuhusu Muawiyah? Humuogopi?”

Abu Dharr alimjibu na kumwambia; “Rafiki yangu alinishauri niseme kweli, hata kama inaumiza, na bila kujali shutuma za anayeshutumu, ambapo nipo kwenye njia iliyonyoka. Ninamuomba Mwenyezi Mungu anilinde nisiwe na uoga, ubakhili na ujinga.” Halafu akaongeza, “Watu wameanza kupika vyakula vya aina tofauti, na wanatumia dawa ili visagwe.

Mtume wetu hakula chakula cha aina mbili kwa wakati mmoja hata siku moja hadi mwisho wa uhai wake. Kama alikula tende hakula mkate. Wazao wa Mtukufu Mtume kamwe hawakula mkate wa shayiri hadi kushiba kwa siku tatu mfululizo hadi mwisho wa uhai wao. Nyumbani kwa Mtume (s.a.w), mara nyingine ilitokea moto haukukokwa, ama mkate, ama chakula cha aina nyingine kilipikwa mfululizo kwa mwezi moja.”

Mtu mmoja aliuliza, “Aliwezaje kuwa hai Abu Dharr akajibu; “Mtukufu Mtume alikula tende na kunywa maji. Alisema kwamba hakuna mtu aliyeona chombo kibaya sana kuliko tumbo lake.

“Vipande vichache tu vinamtosha mtu kuwa hai. Endapo ni muhimu kula, theluthi moja ya tumbo liwe wazi kwa ajili ya chakula, theluthi moja kwa ajili ya maji na iliyobaki iwe kwa ajili ya hewa. Mtume ametushauri kwamba tusile chakula kupita kiasi kwa sababu hutengeneza ulegevu, huharibu mwili na kumhusisha mtu na magonjwa.

“Uwe na ulinganifu unaostahili katika mlo kwa sababu utaepukana na israfu, mwili utakuwa na nguvu na husaidia katika ibada. Mtume kamwe hakukusanya au kuhodhi kitu chochote. Kinyume chake, alikuwa akitoa sadaka chochote alichopata, hivyo kwamba hakuna kilichobaki kwa ajili ya mlo wake. Bila kuhusisha Hazina ya Taifa Mtume alikuwa anatoa hata mgao wake kama sadaka.”
Makabaila walimsihi Muawiyah na wakalalamika kuhusu propaganda ya Abu Dharr. Muawiyah alimwita na akamwambia kuhusu azimio imara la kuondosha tishio hili ambalo lilitikisa misingi ya serikali yake na kuvunja matumaini yake.

Abu Dharr aliingia kwenye baraza la Muawiyah akiwa na mwili mwembamba na mkondefu. Dalili za ushupavu na uimara zilionekana kwenye uso wake wa mviringo alisimama kumkaribisha na akamwonesha mahali pa kuketi karibu na yeye. Halafu akawaita watumishi na akawagiza walete chakula. Nguo ya chakula ilitandikwa na vyakula vya aina nyingi mbali mbali ambavyo vilizidisha ladha, vilitayarishwa.

Muawiyah akamwambia Abu Dharr, “Ndio, tafadhali.” Abu Dharr alikataa na akasema, “Mimi ninakula kilo mbili za ngano kwa juma moja. Haya yamekua mazoea yangu tangu uhai wa Mtume. Kwa jina la Mwenyezi Mungu sitafanya chochote kuzidi hapo hadi nitakapoungana naye.”

Halafu akamgeukia Muawiyah akamwambia, “Umebadili mwenendo wako chakula kinachotayarishwa kwa ajili yako sasa, sio kama kile cha zamani. Unakula mkate uliopikwa unga mzuri, unakula vyakula vya aina kadhaa kwenye mlo moja na unavaa nguo tofauti na ile ya jioni. Wewe hukuwa na tabia hii wakati wa uhai wa Mtume. Hali yako haikuwa tofauti na ile ya mtu masikini.” (Sahih Muslim, Sunan Nisai na Sunan Baihaqi).

Muawiyah; “Maafisa wangu wanalalamika kuhusu wewe. Wanasema kwamba unawachochea masikini wawachukie wao.”

Abu Dharr; “Ninawazuia wasihodhi.” Muawiyah; “Kwa nini unafanya hivyo?”

Abu Dharr: “Ninafanya hivi kwa sababu Mwenyezi Mungu amesema; “Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie bahari ya adhabu iliyochungu.” (Qurani 9:34).

Abu Dharr; “Ewe Muawiyah! Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sitaacha hadi hapo utajiri utakapowagawia masikini.”

Vyovyote vile, matatizo yalimzunguka Abu Dharr pande zote. Mateso makubwa yalimpata kutoka kwa Bani Umayyah. Aligandamizwa sana. Lakini hakuonesha udhaifu wowote na hakuacha kuhubiri. Sasa alianza mashambulizi makali zaidi.

Abdullah Subaiti, Abdul Hamid Misri na Manazir Ahsan Gilani wanasema kwamba Abu Dharr aliendelea kufanya kazi ya kuhubiri mara kwa mara na akiwaonya kuhusu adhabu kali kwa wanaohodhi. Hatimaye Muawiyah akaanza kufikiria mipango ya kujinasua kutoka kwenye michomo ya maneno yake na kuzuia utekelezaji wa malengo yake. Hata hivyo, aliamua kwamba pangeweza kuwepo fursa ya kuwa huru kutokana na mashambulizi endapo tabia ya kuhodhi mali inaweza kuthibitishwa na wale wanao ishambulia. Kwa hiyo, alipata mpango, na aliridhika kwamba mpango huo ungefanya kazi iliyokusudiwa.

Bin Athir baada ya kutaja Aya za Qurani, ameandika kwamba ilipoonekana si rahisi kumnyamazisha Abu Dharr kwa namna yoyote ile, Muawiyah alimtuma mtu na dinari elfu moja kwenda kwake wakati wa usiku. Abu Dharr alizichukua fedha hizo na akazigawa kwa masikini kabla ya alfajiri na hakubakisha hata sarafu moja kwa ajili ya matumizi yake.
Muawiyah, alimwita mtu aliyepeleka sarafu za dhahabu kwa Abu Dharr, baada ya Swala ya alfajiri, akamuamuru aende kwa Abu Dharr na amwambie kwa kujifanya anao wasi wasi, “Ewe Abu Dharr! Niokoe kutokana na mateso ya Muawiyah. Muawiyah aliniamuru nipeleke hizo sarafu za dhahabu kwa mtu mwingine lakini mimi nimekuletea wewe kwa makosa.”

Mjumbe wa Muawiyah alikwenda kwa Abu Dharr na kumwambia kama alivyoagizwa na Muawiyah. Abu Dharr akasema, “Ewe mwana! Mwambie Muawiyah kwamba fedha alizoniletea nilizigawa kwa watu wanaozihitaji kabla alfajiri leo. Sina hata sarafu moja sasa hivi na kama anataka fedha hizo zirudi kwake, atalazimika kunipa siku tatu, ambapo nitazipata fedha hizo kutoka mahali pengine ili nimrudishie.”

Mtu huyo alirudia taarifa hiyo kwa Muawiyah kama alivyoisikia kutoka kwa Abu Dharr, ambaye alisema, Bila shaka Abu Dharr hufanya yale ambayo huwaambia wengine wafanye.” (Tarikh kamil, Juz. 3, uk. 24, tafsir bin Kathir, sehemu ya 10, uk. 34).

Abdullah Subaiti, baada ya kunukuu tukio hili ameandika katika maelezo ya kifalsafa kwamba Abu Dharr alikuwa mtu mwenye tabia ya hali ya juu sana. Bani Umayyah walionesha kutokuwa na uwezo wa kuona mbali kiakili katika kumweleza yeye. Ndio sababu waliona umuhimu wa kufanya utapeli wa kisiasa.

Abdul Hamid Misri ameandika baada ya tukio hili. Muawiyah alielewa kwamba Abu Dharr alikuwa mkweli kwa maneno yake. Alitumia dinari zote kwa usiku moja. Muawiyah alishindwa kutimiza lengo lake. Alionesha huruma kwa Abu Dharr lakini haikufaa kitu. Halafu akatumia nguvu dhidi ya Abu Dharr lakini hakuathirika. Hatimaye akataka amnunue kwa dinari mia tatu, lakini hakufaulu. (Abu Dharr al-Ghifari, Uk. 133).

Kwa mujibu wa wasomi na waandishi wa historia, Abu Dharr alikuwa bado yupo Syria Muawiyah alipotuma jeshi kwa ruhusa ya Uthman kwa vita vya majini (Tarikh Abul Fida).

Abu Dharr alikuwa anashughulika na kazi yake. Baada ya vita hiyo kwisha, Muawiyah akamwagiza Abul Darda, Umar bin al-Aas, Ubadah bin Samit na Umme Hizam, ambao walikuwa masahaba wa Mtukufu Mtume waende kwake.

Walipofika, Muawiyah aliwaambia; “Nimechoka kumwonya Abu Dharr lakini hataki kunisikia. Inanisumbua. Nyinyi pia mmepewa heshima ya kuwa masahaba wa Mtume kama Abu Dharr alivyo. Nendeni kwake na mwambieni aache shughuli zake na aishi maisha ya kimya na utulivu. Nimechoshwa sana na mtu huyu na pia watu matajiri wa nchi hii.”

Watu hawa walikubali haraka sana kwamba wangekwenda kwa Abu Dharr na wangemwomba afanye kama ilivyoagizwa na Muawiyah. Kwa hiyo, walikubaliana kwa pamoja kuhusu mpango fulani na wakamtembelea. Wakamwambia Abu Dharr; “Tumekuja kwa niaba ya Muawiyah. Ametutuma tuje kwako na ombi kwamba uache mahubiri yako na uendeshe maisha yako kwa amani.”

Aliposikia hivi, Abu Dharr alikasirika. Alifikiria kwamba watu hao waliyaona mahubiri yake ni halali kabisa na walijua kwamba lolote alilokuwa anafanya liliendana na Radhi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na bado walikwenda kwake kwa amri ya Muawiyah.

Kwanza kabisa alimwambia Ubadah bin Samit; “Ewe Abul Walid Ubadah! Hapana shaka kwamba unanitangulia mimi kwa kila namna na unanizidi kwa ubora katika kila njia. Wewe ni mkubwa kwa umri na umekuwa pamoja na Mtume kwa kipindi kirefu zaidi. Unazo busara, akili, unajua sana mambo ya dini na utu wako ni bora. Lakini ninasikitika kusema kwamba licha ya kujua kila kitu sawa, umekuja kunishauriu mimi ombi la Muawiyah.

“Ewe Ubadah! Kwani sielewi mambo? Hivi nimepoteza akili ya kuhoji. Hutambui hali ya mambo? Haya ninayo si sahihi? Nasaha zangu haziendani na nia ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake? Ewe Ubadah! Iliniuma sana kwamba wewe ni mtu mwenye akili, unajua kila kitu sana, unakuja kwangu kunishauri mimi. Sikiliza! Ninayo chuki kubwa kwa sababu mtu mwenye kuelewa mambo kama wewe umejumuika kwenye ujumbe huu.”

Halafu akamgeukia Abu Darda na akasema; “Ewe Abu Darda! Umepewa neema ya kumpenda Mtume angalau kidogo. Ilikuwa wazi kwako kwamba endapo hungekubali haraka, hungepewa heshima ya usahaba kwa sababu ya kifo cha Mtume. Lakini uliikubali imani, ukapewa heshima ya usahaba, na ukafikiriwa kuwa sahaba mzuri. Lakini sikiliza! Wewe hukufaidika na usahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w) kama nilivyofaidika mimi. Wewe huwezi kuelewa malengo yake kwa kiasi ninachoelewa mimi. Ninayaelewa malengo ya Mtume na ninafanya kufuatana na utashi wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Kwa hiyo, huna haki ya kunishauri mimi.”

Halafu akaanza kuzungumza na Umar bin Aas kwa kumwambia kwa sauti ya ukali; ‘Ewe Umara bin Aas! Ninakutambua wewe vizuri sana. Umefanya nini zaidi ya kushiriki kwenye vita? Kama hali ilivyo, ulipewa heshima ya usahaba wa Mtukufu Mtume lakini kwamwe hukupata nafasi ya kuishi na yeye. Kila mara ulikuwa mbali na Mtume (s.a.w) kwa sababu ya vita. Wala huwezi kuelewa nia yake ama kuwa na uwezo wa kutosha kuunda maoni sahihi kuhusu matendo na tabia yangu. Ninajua kwamba wewe upo kwenye mvuto wa Muawiyah wakati huu ndio maana umekuja kuniona mimi bila kufikiria kwanza.”

Halafu akamgeukia Ummu Hizam na kusema; “Nikwambie nini wewe? Wewe ni mwanamke, kwa kiwango chochote kile, na unazo akili za kike.” Halafu akasema; “Nendeni mwambieni Muawiyah aone akili zake, aendeshe mambo kufuatana na ushauri wangu na asipoteze imani kwa ajili ya dunia.”

Waliposikia mambo yote haya, wote walinyamaza kimya. Baada ya muda mfupi waliondoka kwa Abu Dharr na kurudi kwa Muawiyah. Walimwambia kwamba walifikisha ujumbe kwa Abu Dharr. Aliwauliza walichosema na majibu waliyopewa na Abu Dharr. Ubadah bin Samit alirudia tukio lote na mwishowe akasema, “Kamwe sijawahi kukaa mahali ambapo shutuma kali kama hizo zinatolewa kwa wazi sana.” (Musnad bin Hanbal, Masanid Abu Dharr).

Abu Dharr alikuwa anashughulika na mahubiri huko Syria wakati wa Hija ulipofika. Aliomba ruhusa kutoka kwa Uthman na kusema alitaka kutoka nje ya Syria aende kuhiji na akae kwenye kaburi la Mtukufu Mtume (s.a.w) kwa muda wa siku chache.

Uthman akampelekea barua ya ruhusa kutoka Madina na Abu Dharr akaenda Hija. Alifanya ibada ya Hija na akaenda Madina. Alikaa karibu na kaburi la Mtume kwa siku chache na halafu akarudi Syria. Balazari pia amesimulia tukio hili kwa sentenso chache.

Aliporudi kutoka Hija akaanza tena shughuli yake ya kuhubiri. Kwa upande moja alikuwa anatumia nguvu zake zote katika kutoa nasaha na kwa upande mwingine maombi mengi sana yalikuwa ya watu matajiri yalikuwa yanamfikia Muawiyah kwamba akomeshe kelele za Abu Dharr. Kiini cha maombi haya ni kwamba watu walikuwa wanakariri mitaani na barabarani Aya ya Qurani ambayo inawaonya watu wenye fedha ambao wanapigwa chapa kwa dhahabu na fedha iliyochomwa moto, kwa hiyo inakuwa vigumu wao kupita kwenda Syria. Na matokeo yake ni kwamba Muawiyah alitangaza kwamba hakuna mtu yeyote kuwasiliana kwa namna yoyote na Abu Dharr (Tabaqati ya bin Sad uk. 176).

Abu Dharr alipopata taarifa ya kususiwa kijamii, yeye mwenyewe alianza kuwaambia watu wasiende kwake au kuketi naye. Hii ni kwa sababu alidhani kwamba endapo mtu alikwenda kwake angeteswa na serikali. Lakini kwa kuwa yeye ilimwia vigumu kuacha kuhubiri, yeye mwenyewe alikwenda kwenye mikusanyiko ya watu na akaanza kufanya kazi yake.

Kwa mujibu wa bin Khaldun, kundi la watu lilipokwenda kumuona baada ya amri ya kumsusa, Abu Dharr aliwaambia watu hao waondoke na yeye abaki peke yake. (Tarikh bin Khaldun uk. 27).

Inaonyesha kutoka kwenye taarifa ya Balazari kwamba watu hao waliofanya mawasiliano na Abu Dharr na kusikiliza hotuba zake, walishughulikiwa kwa ukali zaidi kuliko hata Abu Dharr mwenyewe (Tarikh Balazari, Juz. 5, uk. 65). Abu Dharr alikuwa jasiri kiwango gani! Hakuvumilia ukatili wowote kwa wale waliokuwa wanamwendea, na hakutaka watu hao wapate usumbufu wowote. Lakini almuradi hisia zake za moyoni zilimpa msukumo, alisisitiza kuendelea kuzisoma kwa watu kwa imani na hamasa kamili.

Yeye hakujali kuhusu mafanikio au hasara yoyote katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Sura Ya Kumi Na Nne

Abu Dharr alikuwa mtu mkweli. Alikuwa anawaonya watu wengine wafanye matendo mema. Muawiyah alikuwa mtu aliyependa mambo ya dunia. Kila mara Abu Dharr alikuwa anamwelekeza kufanya matendo mazuri hadi watu wa Syria walianza kuona aibu. Siku moja Muawiyah alimwambia Abu Dharr, “Wewe si muadilifu kiasi cha kunielekeza mimi kufanya matendo mema mbele ya umma.” Aliposikia hivi Abu Dharr akasema, “Nyamaza! Huoni hata aibu!”

Kwa ufupi, Muawiyah alipoona kwamba hangeweza kujirekebisha na hangemnyamazisha Abu Dharr, aliamua kumhamisha Syria. Kwa hiyo, aliamua kumpeleka Jabal al-Amul. Subaiti anasema kwamba Abu Dharr alipowaita watu wa huko kuwaelekea Ahlul-Bait, walikubali wito huo haraka sana! Kwa kuwa sehemu hiyo ilikuwa pana sana, wito wake haukubakia kwenye mipaka ya ndani ya Jabal al-Amul lakini ilifika hata kwenye sehemu za karibu.

Ni dhahiri kwamba Muawiyah alimpeleka Abu Dharr Jabal al-Amul kutoka Syria kwa sababu tu alidhani kwamba shughuli zake za kuhubiri miongoni mwa watu hao wageni zingesimama, lakini aliposikia kwamba Abu Dharr na hotuba zake kali aliwafanya watu wa Jabal al-Amul waelekee ukweli,1 alimwita arudi Syria haraka.
Abu Dharr alianza tena kazi yake alipofika Syria. Alikuwa na tabia ya kukaa mahali paitwapo Bab Damishq (lango la Dameski), baada ya Swala ya alfajiri na kila anapoona msururu wa ngamia uliobeba mali ya serikali aliita kwa sauti kubwa; “Watu! Msururu huu wa ngamia ambao unakuja haukubeba mali ile umebeba moto. Wamelaaniwa watu wanao waelekeza wenzao kufanya wema lakini wao hawafanyi hivyo, na iwaangukie laana watu wanaowakataza wengine wasifanye uovu lakini wao hufanya uovu.” (Tarikh Yaqubi, Juz. 2, uk. 148 na al-Ghadir, Juz. 8, uk. 299).

Halafu Abu Dharr aliondoka mahali hapo na kwenda kwenye lango la Ikulu ya Muawiyah na akatoa hotuba hiyo. Hili ilikwisha kuwa kawaida yake na alifanya hivyo mara kwa mara. Hatimaye Muayiyah alimkamata.

Abu Dharr aliizingatia hadith ambayo imenukuliwa na Khatib al-Baghdad na Almad bin Hanbal. Kufuatana na maelezo ya hadith hii Mtukufu Mtume aliwaambia masahaba wake; “Enyi masahaba wangu! Sikilizeni kwa makini.

“Baada yangu watawala wa umma wangu watakuwa kama makabaila. Wao hawatatofautisha haki na dhuluma na kweli na uwongo. Lakini, yeyote atakayekwenda upande wao na kuthibitisha uwongo wao na kuwaunga mkono katika udhalimu wao, hatakuwa na uhusiano na mimi, na hatakutana na mimi kwenye Haudhi ya Neema. Mtu ambaye hatakuwa na uhusiano nao, hatahalalisha uwongo wao, na hatawaunga mkono katika udhalimu wao, huyo atakuwa ametoka kwangu na mimi nitakuwa nimetoka kwake na atanikuta kwenye Haudhi ya Neema. (Tarikh al-Khatib al-Baghdad, Juz. 2, na Juz. 5, Musnad Ahmad bin Hanbal Juz.1)

Mtu yeyote mwenye akili ataelewa kwamba katika hali hiyo Abu Dharr hangejali mamlaka yoyote. Tabia ya Abu Dharr, zaidi ya kuwa mtu wa kawaida na wa hulka, yalikuwa matokeo ya mafundisho ya Mtukufu Mtume. Hakuna hata mfano moja uliotajwa kwenye historia za kuaminika kuonesha kwamba katika uhai wake Abu Dharr alisita kusema kweli.

Jalam bin Jandal Ghifari, Gavana wa Qiusarin anasema; “Wakati mmoja, wakati wa ukhalifa wa Uthman nilipokuwa Gavana wa Qiusarin nilikwenda kwa Muawiyah, Gavana wa Syria kwa shughuli za kikazi. Ghafla nilisikia mtu anasema kwa sauti kubwa kwenye lango la ikulu. Msururu wa ngamia unaokuja kwako umebeba Moto wa Jahanamu. Mwenyezi Mungu na awalaani wale wanao waambia wenzao kufanya matendo mema, lakini wao wenyewe hawafanyi hivyo. Mwenyezi Mungu na awalani wale wanaowakataza wenzao kufanya matendo maovu ambapo wao hufanya maovu.

“Wakati huo niliona kwamba uso wa Muawiyah ulibadilika rangi kwa sababu ya hasira. Aliniuliza kama nilikuwa humtambua mtu huyo, ambaye alikuwa analia. Nilimjibu hapana. Halafu Muawiyah akasema, ‘Huyu ni Jandab bin Janedah Ghifari. Huja kwenye lango la Ikulu yetu kila siku na kurudia maneno yale yale ambayo uliyasikia muda mfupi uliopita. Halafu akaamuru auawe.

“Ghafla nikamuona Yaqudunah anamleta Abu Dharr akimburuza na akamsimamisha mbele. Muawiyah akamwambia, ewe adui wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kila siku unakuja kwetu na kurudia rudia maneno hayo. Hakika ningekwisha kukuua kama ningeweza kumuua sahaba wa Mtume bila ruhusa ya Uthman. Sasa nitaomba ruhusa kuhusu wewe.”

“Nikataka kumuona Abu Dharr kwa sababu anatoka kwenye kabila letu. Nilipomtazama, nilimuona alikuwa amesinyaa, mwembamba na mrefu. Ndevu zake hazikuwa nyingi, na mgongo wake ulikunjika kwa sababu ya kuzeeka.

Abu Dharr alimjibu Muawiyah; “Mimi si adui wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake lakini wewe ndiye adui yake Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na baba yako pia alikuwa adui wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Nyinyi watu mlitangaza Uislamu kwa maslahi ya kibinafsi lakini katika nyoyo zenu mlikuwa makafiri. Mtume wa Uislamu alikulaani mara mbili na alikuapiza hivyo kwamba ule bila kushiba. Nimesikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba Umma wake utateswa na fitina ya mtu mwenye macho makubwa na koo pana, ambaye hatosheki chakula ingawa hula sana, pale atakapokuwa mtawala wa umma huu.

Aliposikia hivi Muawiyah akasema; “Mimi sio yule Mjumbe wa Mwenyezi Munu alimsema” Abu Dharr akasema; ‘Ewe Muawiyah! Haina maana kukanusha kwa hakika wewe ndio mtu yule yule na sikiliza! Mtume ameniambia kwamba mtu huyo alimaanisha wewe na wewe peke yako. Ewe Muawiyah! Siku moja ulipokuwa unapita mbele ya Mtume, nilimsikia akisema; Ee Mwenyezi Mungu! Mlaani huyo na ulijaze tumbo lake vumbi. Ewe Muawiyah! Nimemsikia Mtume akisema pia kwamba upande mmoja wa Muawiyah upo kwenye Moto wa Jahanamu. Aliposikia hivi, Muawiyah alicheka kicheko cha aibu, akaamuru Abu Dharr akamatwe, akapelekwa jela na akamwandikia barua Uthman kuhusu jambo hili. (Hayat al-Qulubi, Juz. 2, uk. 1043, al-Ghadir, Juz. 8, uk. 299 kama ilivyo nukuliwa kutoka kwenye Tarikh Yaqubi).

Baada ya kumpeleka Abu Dharr jela Muawiyah katika barua aliyo mwandikia Uthman alilalamika kuhusu Abu Dharr kwamba aondolewa Syria na kurudishwa Madina. Kufuatana na Barua hiyo Uthman alimrudisha Abu Dharr Madina. Kwa mujibu wa tafsiri ya Tarikh Atham Kufi Shafii (Majlisul Muaminin uk. 119) Maudhui yake ni kama yafuatayo:

“Baada ya heshima ipasayo kwako Muawiyah bin Sakhr kwa unyenyekevu kwa kusema kwamba Abu Dharr anawachochea watu wa Syria waasi dhidi yako. Anawahamasisha watu wakuchukie wewe. Anawakumbuka Umar na Abu Bakr kila wakati na anakumbusha kuhusu mwenendo na uadilifu wao mzuri. Hukutaja wewe kwa kutumia maneno mabaya na husema maneno yako na matendo yako ni maovu na yenye makosa. Haifai kumruhusu aishi Syria, Misri na Iraq kwa sababu watu wa nchi hizi ni wapenda fitina na huungana na watu wachochezi haraka na kusababisha ghasia. Nimekutaarifu kuhusu yaliyo jitokeza. Sasa vyovyote khalifa atakavyo amua ni bora. Wasalam.”

Mpanda ngamia aliondoka na barua ya Muawiyah na kuiwasilisha kwa Uthman huko Madina. Mara baada ya Uthman kupokea barua hiyo alirudisha majibu kwa Muawiyah mara moja. “Ninayo barua yako; nimekwisha elewa ulichoandika kuhusu Abu Dharr. Mara upatapo barua hii msafirishe Abu Dharr aje Madina kwa kutumia ngamia wa mwendo wa haraka ambaye ataendeshwa na mtu mwenye moyo mgumu ambaye atamkimbiza ngamia mchana na usiku ili Abu Dharr achoke na alale ili asahau kusema mambo yako na yangu.”

Baada ya kupokea barua hii, Muawiyah alimwita Abu Dharr na akamsafirisha kwenda Madina kwa kupanda ngamia asiye na tandiko la kukalia na ambaye ni mtundu na mwendeshaji mbaya. Muawiyah alimwagiza mwendesha ngamia kumfanya ngamia akimbie usiku na mchana bila kupumzika hadi Madina.

Abu Dharr alikuwa mrefu na mwembamba na wakati huo tayari alikuwa mzee sana hivyo kwamba nywele na ndevu zake zilikuwa kijivu. Zaidi ya haya alidhoofu sana, hapakutandikwa nguo au tandiko la kukalia kwenye mgongo wa ngamia huyo. Mshika hatamu wa ngamia hakuwa na huruma naye. Kwa sababu ya matatizo yote haya na majeraha, mapaja ya Abu Dharr yalipata majeraha na alihisi maumivu makali na kuchoka.

Waandishi wa historia wanakubaliana kwamba Abu Dharr alipelekwa Madina peke yake. Familia yake haikuwa naye. Labda inaezekana hakuruhusiwa kwenda nyumbani kwake kuchukua familia yake. Lazima aliitwa kutoka jela na kusafirishwa kwenda Madina moja kwa moja.

Kwa mujibu wa Allamah Majlis na Allamah Subaiti Abu Dharr alipokaribia kuondoka kwenda Madina, taarifa iliwafikia Waislamu ambao walikwenda kumuona na kumuuliza alikuwa anakwenda wapi. Abu Dharr akajibu; “Uthman ameniita Madina. Ninakwenda kuitika wito wake. Enyi Waislamu! Uthman alipohisi nimekosea, alinileta hapa kwenu. Sasa ninaitwa tena Madina. Ninatambua kwamba safari hii nimeitwa ili niteswe. Lakini ni muhimu mimi, kwenda, kwa vyovyote vile. Sikilizeni! Uhusiano wangu na Uthman utabakia hivi. Msisikitike na msiwe na wasi wasi kuhusu suala hili.”

  • 1. Vita hii ilitwa Zaat al-Ruqa (vita ya viraka vya nguo) kwa sababu njia ilikuwa na mawe mengi sana na mashimo, kwa sababu hiyo, miguu ya watu ilipasuka na kuifunga kwa vipande vya nguo. Zainul Ma’ad.

Sura Ya Kumi Na Tano

Abu Dharr alipokuwa anaondoka, watu walimsindikiza kumuaga hadi walifika Dair Maran sehemu iliopo nje ya jiji. Hapo aliswali Swala ya jamaa. Halafu akahutubia watu na tafsiri yake ni kama ilivyotolewa na Hayatul Qulub.

“Enyi watu! Ninawaachieni wasia wa kitu ambacho kitakuwa na manufaa kwenu.” Baada ya hapo aliwaambia wamshukuru Mwenyezi Mungu. Wote wakasema, “Sifa zote zinastahiki kwake Mwenyezi Mungu.” Halafu Abu Dharr akashuhudiaa Upweke wa Mwenyezi Mungu na Utume wa Muhammad na wote wakasema kama alivyosema. halafu akasema; “Ninakiri kuwepo kwa Ufufuo na Siku ya Hukumu na kuwepo kwa Pepo na Jahanamu. Ninaamini yale ambayo Mtume alileta kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ninawatakeni mshuhudie hii imani yangu.” Wote wakasema, “Tunashahudia yale ambayo umeyasema.”

Baada ya hapo akasema, “Yeyote miongoni mwenu atakaye kufa akiwa kwenye imani hii atapata habari njema za huruma na wema wa Mwenyezi Mungu almuradi yeye si msaidizi wa watenda dhambi anayeunga mkono matendo ya wagandamizaji, mshirika wa madhalimu.

“Enyi kundi la watu! Ghadhabu na msononeko iwe pia sehemu ya Swala zenu na kufunga Swaumu, mnapowaona watu wanafanya dhambi kinyume na matashi ya Mwenyezi Mungu. Msiwafurahishe viongozi wenu kwa vitu ambavyo ni sababu ya hasira ya Mwenyezi Mungu. Endapo watu hao wanaingiza vitu katika imani ya Mungu ambavyo ukweli wake hamjui, waacheni na mfichue makosa yao hadharani, hata kama watawatesa na kuwaondoeni kwenye makundi yao, hata kama watawanyang’anya zawadi zao, na kuwahamisheni kutoka kwenye miji, ili Mwenyezi Mungu apate kufurahishwa na nyinyi.

“Hakika Mwenyezi Mungu ametukuka mno na yuko Juu sana. Haistahili kumkasirisha Yeye kwa sababu ya kuwafurahisha viumbe Vyake Mwenyezi Mungu na waghufirie nyinyi na mimi. Sasa ninawaacheni kwa Mwenyezi Mungu na ninawatakia amani na huruma za Mwenyezi Mungu.”

Wote wakajibu; “Ewe Abu Dharr! ewe sahaba wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na akuweke salama na akuridhie neema Zake! Hungependa tukuchukue tena tukurudishe jijini kwetu na tukuunge mkono mbele ya maadui.” Abu Dharr akasema; “Mwenyezi Mungu na akupeni rehema! Sasa mnaweza kurudi. Hakika mimi ni msitahimilivu zaidi kwenye mabalaa kuliko nyinyi. Kamwe msifarakane na msiwe na wasiwasi na msitofautiane miongoni mwenu.”

Waandishi wa historia wanasema kwamba Abu Dharr alipofika Madina akiwa ameiacha familia yake Syria, akiwa amenyong’onyea na kuchoka sana alipelekwa mbele ya mfalme wa wakati huo, Khalifa Uthman. Wakati huo watu wengi walikuwepo kwenye baraza. Mara Khalifa Uthman alipomuona Abu Dharr, alianza kumshutumu bila kujali heshima yake mbele ya Mtukufu Mtume. Inaonekana kwenye wasomi wa histoira kama vile Uthman alisema chochote kilichokuwa akilini mwake akiwa kwenye hasira na ghadhabu. Hata alisema, “Ni wewe ndiye ambaye amefanya matendo yasiyostahili.”

Abu Dharr akasema, “Mimi sikufanya lolote isipokuwa nilikupa ushauri na ukauwelewa vibaya ushauri wangu na ukanihamisha na kunipeleka mbali na wewe. Halafu nikamshauri Muawiyah. Na yeye pia hakupenda ushauri wangu na amenihamisha na kunipeleka mbali na yeye .” Uthman akasema; “Wewe ni mwongo. Wewe unaendekeza uhaini akilini mwako. Unataka kuichochea Syria iniasi mimi.”

Abu Dharr akasema; “Ewe Uthman! Fuata nyayo za Abu Bakr na Umar tu na hakuna mtu atakayesema lolote dhidi yako.” Uthman akasema, “Kuna umuhimu gani mimi kufuata nyayo zao au nisifuate nyayo zao. Mama yako na afe!” Abu Dharr akasema; “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, huwezi kunishutumu mimi kwa lolote isipokuwa mimi ninawaelekeza watu wafanye matendo mema na kuwakataza wasifanye matendo mabaya.

Aliposikia maneno haya Uthman alijaa hasira na akasema, “Enyi wazee wa baraza! Nipeni ushauri nimfanye nini huyu mzee mwongo. Nimpe adhabu ya kumtandika viboko, nimfunge jela, auawe, au nimpeleke uhamishoni. Amesababisha wasiwasi katika jamii ya Waislamu.”

Baada ya kusikia hivi, Ali ambaye alikuwepo hapo, alisema; “Ewe Uthman! Ninakushauri wewe kama muumini wa taifa la Firauni umwache mtu huyo alivyo. Endapo yeye ni mwongo basi atapata malipo yake na kama yeye ni mkweli hakika wewe ndiye utakayeumia. Mwenyezi Mungu hamwongozi yule ambaye ni mbadhirifu na mwongo.” Hapa palitokea mabishano makali kati ya Uthman na Ali ambayo sitaki kuyaeleza hapa. (Tabaqati bion Sad al-Waqidi, alifariki mwaka 230 A.H. Juzu. ya 4, uk. 168).

Muhammad bin Ali bin Atham Kufi, Ameandika kuhusu mzozo huo: Ali alimwambia khalifa Uthman, “Usimsumbue Abu Dharr. Endapo yeye ni mwongo atateseka kufuatana na matokeo ya matendo yake, na kama ni mkweli, yale anayoyasema yatatokeza dhahiri.” Uthman hakukubaliana na usemi huu wa Ali. Alimwambia Ali kwa hasira, “Usiingilie jambo lisilokuhusu! Ali pia alirudia maneno hayo hayo.

Halafu Ali akasema; “Ewe Uthman! Unafanya nini sasa? Ni dhuluma iliyoje unaifanya sasa! Haistahili wewe kutamka maneno kama hayo kuhusu Abu Dharr ambaye ni rafiki yake Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya mambo yasiyojulikana ambayo Muawiyah ameyasema. Hivi huna habari kwamba upo upinzani, ugandamizaji, maasi na uovu wa Muawiyah? Aliposikia hivi Khalifa Uthman alinyamaza.” (Tarikh Atham. Kufi na Majalisul Muminin).
Sayed Nurullah Shustari ameandika kwamba mara tu Abu Dharr alipomuona Khalifa Uthman mbele yake alikuwa na desturi ya kukariri Aya ya Qurani; “Iogope siku ambapo Moto wa Jahanamu utaunguza nyuso zao na zitapigwa chapa.” Akimaanisha kusema kwamba, ‘Ewe Uthman! Ni kosa kwako unapoacha kuwapa masikini utajiri unao hodhi lakini unapotoa, huwapa ndugu zako. Siku hiyo ipo karibu ambapo pande zako na uso wako utapigwa chapa huko Jahanamu.” (Mjalisul Muminin, uk. 94).

Kwa mujibu wa Tabari ilitokea Ali alimwambia Uthman; “Umeacha kufuata nyayo za wale waliokutangulia na sasa kwa urahisi tu unazidisha kuwapa mali uzao wa Umayyah na ndugu zako. Umewasahau masikini kabisa unavyofanya si sawa hata kidogo. Umepata wapi haki ya kugawa rasilimali ya Waislamu kwa njia ya dhuluma?” Uthman akakasirika aliposikia maneno haya ya Ali na akajibu, “Wale walio tangulia waliwakosea ndugu zao. Mimi sitaki kufanya hivyo. Nitawapa ndugu zangu masikini kile nitakachoweza.” Ali akasema; “Ndio hao tu watu wenye haki ya kuwapa maelfu ya dinari kutoka kwenye Hazina ya Taifa ya waislamu? Hakuna masikini mwingine?” (Tarikh Tabari, Juz. 2, uk. 272).

Waandishi wa historia kama Abul Hassan Ali bin Husein bin Ali al-Masudi (alifariki mwaka 346 A.H) Ahmad bin Abi Yaqubi na Ishaq bin Jafar bin Wahhab bin Wazeh Yaqubi (alifariki mwaka wa 278 A.H), na Muhammad bin Sad al-Zahri al-Basri, Katib al-Abbasi al-Waqidi (alifariki mwaka 230 A.H) wamesimulia tukio hili hivi: Abu Dharr alipofikishwa kwenye baraza, Uthman alimwambia Abu Dharr; “Nimeambiwa kwamba umewaambia watu hadithi ya Mtume kwamba wakati idadi ya wanaume wa Bani Umaayah itafikia thelathini kamili, wataifikiria miji yote ya Mwenyezi Mungu kuwa ngawira yao na waja wa Mwenyezi Mungu watumishi wao wa kiume na wakike na wataifanya dini ya Mwenyezi Mungu kama udanganyifu.”

Abu Dharr akasema, “Ndio, nimemsikia Mtume anasema hivyo.” Uthman akawauliza wasikilizaji wa baraza, “Mlimsikia Mtume anasema hivyo?” Wakasema, “hapana!” Halafu akamwita Ali na akasema, “Ewe Abul Hassan! Unathibitisha hadith hii?” Ali akasema; “Ndio.” Uthman akasema; “Nini uthibitisho wa ukweli wa hadithi hii?” Ali akajibu, Usemi wa Mtukufu Mtume kwamba hakuna msemaji chini ya mbingu na juu ya ardhi, ambaye ni mkweli kuzidi Abu Dharr.”

Abu Dharr alikaa Madina kwa siku chache tu baada ya tukio hili ambapo Uthman alimpelekea ujumbe kwamba, “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, hakika utahamishwa kutoka Madina.” (Murujuz Dhahab al-Masud; Juz. 1, uk. 438 na Tarikh Yaqubi, Juz. 2, uk. 148).

Allamah Majlis ameandika kwamba baada ya kurudi kutoka Syria, Abu Dharr aliugua. Siku moja aliingia barazani akiwa na mkongojo. Alikuwa ndio amefika hapo ambapo maofisa wa serikali waliingia hapo wakiwa na dinari 100,000, ambazo walikusanya kutoka sehemu mbali mbali za nchi. Mara tu Abu Dharr alipoziona akasema, “Ewe Uthman! Rasilimali hiyo ni ya nani?” Akajibu, “Rasilimali ya Waislamu.”

Akauliza, “Itakuwa kwenye hazina hadi lini kabla haijawafikia Waislamu?” Khalifa akasema, “Fedha hii nitakuwa nayo hadi zitakapopatikana dinari zingine 100,000, kwa sababu wameniletea mimi utajiri huu. Kwa hiyo, ninangojea zingine zaidi, ili niweze kumgawia yeyote ninayemtaka, na kuzitumia ninapoona pana stahili.” Abu Dharr akasema, “Zipi nyingi, dinari nne au 100,000?” Uthman akasema; “100,000 ndizo nyingi.”

Aliposikia hivi Abu Dharr akasema: “Ewe Uthman! Hukumbuki ya kwamba siku moja wewe na mimi tulikwenda kwa Mtume usiku sana na tulipomuona amehuzunika tukamuuliza sababu ya huzuni yake, hata hakusema na sisi kwa sababu ya uzito wa majonzi yake. Halafu tuliokwenda kumuona tena asubuhi tulimkuta anafurahi na anacheka, tukamuuliza kwa nini usiku wa jana yake alisema na huzuni sana na kwa nini alifurahi sana asubuhi hiyo, Mtume akajibu “Usiku wa jana, baada ya kugawa rasilimali ya Waislamu zilibaki dinari nne tu, kwa hiyo nilifadhaika sana. Lakini nimempa mtu aliye na haki ya kuzipata. Kwa hiyo, sasa ninafurahi.”

Sura Ya Kumi Na Sita

Kama tulivoeleza kwa ufupi kwenye kurasa za nyuma, Uthman, alikua anagawa fedha ya Waislamu miongoni mwa ndugu zake tu huku anawanyima haki watu masikini. Abu Dharr, kwa ajili ya ushupavu wake wa kidini katika kufuatilia mafundisho matukufu ya Mtume, alilazimika kupiga kelele kukemea maovu hayo. Matokeo yake alipelekwa Syria. Halafu aliitwa kutoka Syria na kurudi Madina kwa namna ya kuadhibiwa. Akawekwa katika taabu nyingi. Kwa kuwa Abu Dharr alikuwa mtu mwenye msimamo na alikuwa makini katika kutimiza ahadi yake ya kuwa mkweli ambayo alimwahidi Mtukufu Mtume, aliendelea na kazi yake bila kujali mamlaka yoyote au shutuma kutoka popote pale. kamwe hakujali ama alikuwa anazungumza kwa mfalme au kwa mtu wa kawaida. Hakujali kama pale alipokuwa anasema ni mtaani, sokoni, msikitini au baraza. Mzigo na aina ya kilio chake cha ukweli ulikuwa ni ule ule.

Sasa tunataka kuandika kwa kina jinsi Uthman alivyofungua mlango wa Hazina ya Taifa kwa ajili ya washirika wake na jinsi ndugu wa wafuasi wake walivyotajirika kupindukia. Hapa tunaorodhesha majina ya watu waliohusika ile iwe rahisi wewe msomaji kuamua jinsi wale waliofuata nyayo za Mtume (s.a.w) yaani Ali, Abu Dharr, Salman, Miqdadi, Ammar, na masahaba wengineo wa Mtume, walivyokuwa wakijinyima na hawa waolifanya upinzani dhidi ya utendaji wa aina hiyo.

Tunanukuu mifano michache ya ubadhirifu na upendeleo wa Uthman. Lakini, kabla ya hapo tunataka kuelezea jinsi fikra ya kuionesha upendeleo kwa uzao wa Umayyah ilivyoanza akilini mwake na jinsi alivyovuka mipaka ya mwenendo mwema. Bin Asakir, mwandishi wa historia na mtoa maoni wa labda karne ya pili ya A.H ameandika:

“Kwa mujibu wa simulizi za Anas bin Malik, siku moja Abu Sufyani bin Harb, ambaye alikwishapofuka, alikwenda kwa Uthman na akauliza kama palikuwepo na mtu mwingine pale. Masahaba wake wakasema, ‘hapana.” halafu akasema, “Ewe Uthman! Ifanye serikali hii ya Kiislamu iwe ya kabla ya Uislamu; iache inchi iwe kama ile iliyonyakuliwa kutoka kwa mtu na uitunze iwe ya kudumu kwa ajili ya uzao wa Umayyah.” (Tarikh bin Kathir, Juz. 6, uk. 407).

Waheshimiwa wasomaji! Ni Abu Sufyani yule yule aliyemfanyia Mtukufu Mtume karaha zisizo na mfano kabla ya Uislamu, halafu akaingia kwenye Uislamu bila kupenda. Hakuheshimu Uislamu katika yakini ya moyo wake.

Uthman alikubali ushauri wake akawaunga mkono kwa ukamilifu Bani Umayyah, akawafanya kuwa matajiri na kufanya serikali kuwa nchi iliyonyakuliwa kutoka kwa mtu, akaanza kuwatendea matendo mabaya na kuwadharau wenyewe wa mwanzo. Ni dhahiri kwamba haki ya kumiliki utawala ulitakiwa uende kwa Ali na uzao wake. Kwa hiyo, Uthman kuwatendea uonevu kama alivyoshauriwa na Abu Sufyani haiendani na utaratibu uliowekwa.

Inathibitika kutoka kwenye maelezo ya kihistoria kwamba usiku huo alipofariki Umm Kulthum, Uthman alifanya tendo la ndoa na mwanamke mwingine bila kumjali yule anayeugua kwa sababu ya kwamba alikuwa na uhusiano wa kindugu na Mtume. (Tajul Urus Juz. 6, uk. 220, Tabaqat bin Sad Juz. 8, uk. 31; Musnad Almad Juz. 3, uk. 126; Mustadirak Juz. 4, uk. 47; Sunan al-Kubra Bayhaqi, Juz. 4, uk. 53, Nihaya bin Athir, Juz. 3, uk. 286; ilichapishwa Misri, Lisanul Arab, Juz. 11, uk. 8809, Isabah, Juz. 4, uk. 489).

Maelezo kuhusu sababu ya watu kuwa wapinzani wa Uthman waandishi wa historia wameandika kwamba Uthman alimpa Marwani bin Hakam, Fadak (Kiunga kilichoporwa kutoka kwa Fatimah wakati wa utawala wa Abu Bakr –Khalifa wa Kwanza).

Fadak ni rasilimali iliyobakia kwenye miliki ya Marwani na wazao wake hadi hapo Umar bin Abdul Aziz aliichukua kutoka kwake na akawarudishia Ahlul Bait ambao ndio walikua na haki ya kumiliki. (Maarif cha bin Qutayba, uk. 84, Tarikh Abul Fida, Juz. 1, uk. 168; Sunan al-Kubra Bayhaqi, Juz. 6, uk. 301, Iqdul Farid, Juz. 2, uk. 261).

Uthman hakumpa tu Marwan bin Hakam alikuwa binamu yake na mume wa bint yake, Umme Aban, umilikaji wa Fadak lakini alimpa pia sehemu ya tano (1/5) ya ngawira iliyopokelewa kutoka Afrika yaani dinari laki tano ambazo Abdul Rahman bin Hanbal al-Jamai al-Kindi wakati anazungumza na Khalifa alikariri aya za kejeli. Kwenye mojawapo ya Aya hizi anasema;

Ewe Khalifa! Ulimleta Marwan aliyelaaniwa karibu sana na wewe kinyume na walivyofanya wale waliokutangulia na ukamfanya kuwa mkwe wako, na halafu ukampa moja ya tano ya ngawira ya Afrika ukawadhulumu masikini.” (Maaeij uk. 84; Abul Fida, Juz. 1, uk. 160) Waandishi wa historia bin Kathir na Waqidi wanasimulia kwamba jumla ya thamani ya ngawira ya Afrika aliyopewa Marwan ilikuwa sarafu za dhahabu elfu ishirini. (Tarikh bin Kathir, Juz. 7, uk. 152) Tabari anasema kwamba ilikuwa dinari laki tano, sarafu aza dhahabu elfu ishirini (Tarikh Tabari, Juz. 5, uk. 50 Zaidi ya haya pia alipewa moja ya tano ya ngawira kutoka Misri. (Ansab al-Ashraf Balazari, Juz. 5, uk. 25; Tabari bin Sad, Juz. ya 3, uk. 44, ilichapishwa London)

Bin Abil Hadid ameandika, halafu alipomuoza mwanae kwa Marwan pia alimpa dinari laki moja kutoka kwenye Hazina ya Taifa. Kwa kitendo hiki, Zayd bin Arqam alimtupia Uthman funguo za hazina na akasema kwamba Marwan hakustahili kupewa hata dinari mia moja (Sharah bin Abil hadid, Juz. 1, uk. 67).

Waandishi wa historia wote, watoa maoni, wahadithi na wasimulizi miongoni mwao, Aishah anashika nafasi ya kutambulikana, wanasema wazi kwamba wote wawili Marwan na baba yake Hakam na pia uzao wao walilaaniwa na walichukiwa na Mtume. Aishah anasema kwamba Marwan alizaliwa kutokana na mbegu ya kiume iliyolaaniwa na Mtume ambaye hakuvumilia kuishi kwao hapa duniani. Mwenyezi Mungu aliwatangaza wao, wahenga wao na wazao wao mti wa nasaba iliyolaaniwa, na Mtume wa Mwenyezi Mungu alimhamisha Hakam kutoka Madina. Abu Bakr na Umar pia hawakuwaruhusu kurudi. Lakini Uthman aliwarudisha, akawapa zawadi na akamwoza binti yake Umm Aban kwa Marwan.

Kwa maelezo ya kina angalia kwenye Mustadrak Hakam, Juz. 4, 481, Tafsir Qurtabi, Juz. 16, uk. 197, Tafsir Khashashaf Juz. 3, uk. 99, ilichapishwa Misri.

Marwan bin Hakam aliporudi kwa kuitwa na Uthman alivaa matambaa na alipotoka ndani ya baraza lake alivaa nguo za hariri na josho. Khalifa alimpa laki tatu kutoka kwenye sadak ya Yemen. (Tarikh Yaqubi, Juz. 2, uk. 41) Ni mtu ambaye alihamishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu na Abu Bakr na Umar pia hawakumruhusu kuingia Madina. Lakini Uthman alimwita akampa zawadi ya dinari laki moja. (Maarif bin Qutaibah, uk. 83, Iqdul Farid, Juz. 2, uk 261, na Mahizirat al-Jinan Yafei, Juz. 1, uk 85).

Harith bin Hakim alikuwa ndugu yake Marwan na mume wa Ayesha bint yake Uthman. Uthman alimpa dinari laki tatu kutoka kwenye rasilimali ya Waislamu. Pia kama sadaka (Ansabul Ashraf Balazaqi, Juz. 5, uk 52). Uthman pia alimpa soko “Mahzuni, ambalo liliasisiwa na Mtume hapo Madina. (Maarif, uk. 84, Iqdul Farid, Juz. 2, uk. 261; Mahazarat Raghib Isafahan, Juz. 2, uk. 212). Zaidi ya hii, sehemu ya kumi (1/10) ya pato lililopokelewa kutoka kwenye masoko ya Madina pia ikitengwa kwa ajili ya Harith. (Sirat Halaabian, Juz.2).

Uthman alimpa Said bin Aas bin Umayyah dinari laki moja. (Abu Makhnaf na Waqidi) Aas baba yake na Said alikuwa mtu aliyekuwa na tabia ya kumtesa sana Mtume Ali alimua kwenye vita ya Badr. (Tabaqat bin Sad, Juz. 3, uk 301). Said mtu ambaye wakati moja alimwita Hashim bin Utabah mtu mwenye jicho moja kwa dharau wakati wa kuangalia mwezi. Mtu huyu alipoteza jicho moja katika vita ya Siffin. Matokeo ya kejeli ya Said masahaba waheshimiwa wa Mtume wakampiga na kuichoma nyumba yake. (Tabaqat bin Sad). Inaeleweka kwamba Ali, Talha, Zubayr na Abdul Rabman bin Auf alipinga kitendo cha Uthman kumpa Said dinari laki moja, lakini khalifa hakujali. (Ansabul Ashraf Balazari, Juz. 5, uk. 28).

Uthman alimpa kaka yake wa kambo Walid bin Uqbah bin Abi Muit bin Abi Umar bin Umayyah mkopo wa dinari laki moja kutoka kwa Abdullah bin Masud, mweka hazina wa Kufah. Baadaye, bin Masud alimwambia arudishe fedha hizo za Hazina ya taifa, alimwandikia barua Khalifa kwamba bin Masud alimwambia arudishe deni la fedha za Hazina ya Taifa ambazo yeye Uthman alimpa. Tukio hili lilimfanya Khalifa Uthman aandike barua kwa Abdullah bin Masud, “Wewe ni mweka hazina wangu. Ninakuamuru usimwambie Walid kurudisha deni ambalo amekopa kutoka Hazina ya Taifa, wala usikatae kutekeleza amri hii.”

Alipoona hali hii, Abdullah bin Masud alikwenda kwenye msikiti wa Kufah siku ya Ijumaa na akawaambia watu tukio hili la Walid na Uthman bila kuficha. Walid akamtaarifu Uthman kuhusu jambo hili ambapo matokeo yake Abdullah bin Masud alifukuzwa kazi. (Ansabul Ashraf Balazari, Juz. 5, uk. 30 na Iqdul Farid, Juz. 2, uk. 272).

Huyu Walid ni mtu ambaye baba yake, Uqbah alikuwa adui mbaya sana wa Mtukufu Mtume. Kwa mujibu wa simulizi ya Aishah, Mtukufu Mtume mara nyingi alikuwa akisema; “Nimechoshwa na majirani zangu wawili. Mmojawapo ni Abu Lahab na mwingine ni Uqbah bin Abi Muit. Wote wawili, zaidi ya fitina zingine, huacha lundo la uchafu na takataka, mlangoni mwangu.” (Tabaqat bin Sad, Juz. 1, uk. 186, chapa Misri). Waandishi wa historia wametengeneza orodha ya watu kama hawa ambamo majina ya Abu Lahab, Uqbah Abu Jahl, Hakam bin Abil, Aas bin Umayyah ni maarufu. (Tabaqat bin Sad, Juz. 1, uk. 186; na Sirah bin Hisham, Juz. 2, uk 25).

Watoa maoni na waandishi wa historia wanayomaoni kwamba Uqbah ni mtu aliye laaniwa ambaye alikwenda asi baada ya kuingia kwenye Uislamu. Aya hii iliteremshwa kwa ajili yake;

وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ{27}

“Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake.” (Surah al-Furqan, 25:27).

Kwenye Aya hii dhalimu maana yake ni huyu Uqbad aliye laaniwa kama ambavyo imeelezwa kwenye Tafsir, Juz. 9, uk. 25; Tafsir Baizawi, Juz. 2, uk. 161; Tafsir bin Kathir, Juz. 3, uk. 317; Tafsir Naishapuri kwenye maandishi ya pembeni Tabari, Juz. 19, uk 10; Tafsir Kabir Razi, Juz. 6, uk. 369).

Kwa ufupi, yapo maandishi mengi sana kwenye vitabu vya historia na hadith kuhusu tabia mbaya ya Walid na baba yake kwamba kitabu cha pekee yake kinaweza kuandika kuhusu watu hawa. Kwa ufupi ni kwamba Walid alikuwa mwasherati, mzinifu, fisadi, na mlevi ambaye alinajisi imani, hapa chini tunaorodhesha baadhi ya matukio muhimu ambayo yana dhihirisha tabia yake:

Kwenye Msikiti wa Kufah, Walid asali Swala ya rakaa nne wakati wa Swala ya alfajiri badala ya rakaa mbili kwa sababu alilewa.

Kwa amri ya Imamu Ali, Abdullah bin Jafar alimwadhibu Walid kwa kumchapa viboko thelathini kwa sababu ya kunywa mvinyo.

Walid bin Aas aliposhikanafasi ya Ugavana wa Kufah baada yake, alihakikisha mimbari ilisafishwa na alisema, “Ondoeni uchafu wa Walid kutoka humo.” (al-Ghadir na Allamah Amini, Juz. 1, uk 274).

Khalifa Uthman alimpa Abdullah bin Khalid bin Usayd bin Aas bin Umayah dinari laki tatu na dinari elfu moja kwa kila mtu wa kabila lake. (Iqdul Farid, Juz. 2, uk. 26) na Maarif cha bin Qutayba, uk. 84), Bin Abil hadid ameandika tarakimu ya laki nne (Sharah Nahju balaghah Juz. 1, uk. 66).

Yaqubi ameandika kwamba Uthman alimuoza binti yake kwa Abdullah bin Khalid na Usayd na akaamuru apewe dinari laki sita na kuhusu jambo hili alimwandikia Abdullah bin Aamir kwamba kiasi hicho cha fedha kichotwe kutoka kwenye Hazina ya Taifa ya Basrah (Tarikh bin Wazih Yaqubi, Juz. 2, uk. 45).

Kila mtu anajua tabia ya Abu Sufyani bin Harb, Uthman pia alimpa mtu huyu dinari laki mbili kutoka kwenye Hazina ya taifa fedha hii ilitolewa siku moja alipopewa Marwan bin Hakam dinari laki moja (Sharah Nahju Balagha, Juz. 1, uk. 67).

Khalifa Uthman alimpa Abdullah bin Sad bin Abi Sarah kaka yake wa kuchangia ziwa sehemu ya tano ya ngawira kutoka Afrika. Kwa mujibu wa Abul Fida thamani ya ngawira hiyo ilikuwa dinari laki moja (Usudul Ghaba, Juz. 3, uk. 173; na Tarikh bin Khathir, Juz. 7, uk. 152).

Bin Abil Hadid ameandika kwamba Uthman alimpa Abdullah bin Sad ngawira yote iliyopokewa kutoka Afrika ya Magharibi bila kupunguza hata sehemu ndogo kumpa Muislamu yeyote. (Sharah Nahju Balaghah, Juz. 1, uk. 67).

Sad bin Abi Sarah ndiye mtu aliyeingia kwenye Uislamu kabla Makkah haijatekwa. Halafu akahamia Madina na akaasi imani ya Uislamu.

Baada ya uasi wake, Mtume wa Mwenyezi Mungu akatangaza kwamba Sad bin Abi Sarah lazima auawe popote pale atakapoonekana hata kama alikuwa chini ya kifuniko cha Ka’abah takatifu. Katika kuangalia mambo haya, Uthman alimficha na akamwombea msamaha akasamehewa. (Sunan Abu Daud na Mustadrak Hakim).

Uthman alimpa Talha bin Abdullah dinari laki mbili (Sarafu za dhahabu). (Balazari, Juz. 5, uk. 7) na alimpa mifuko kadhaa ya dhahabu na fedha.

Mifano iliyotajwa hapo ju imeonesha upendeleo wa Uthman na jinsi alivyo watengeneza Bani Umayyah wanagalagala kwenye utajiri wa Waislamu. Sasa tunataka kueleza jinsi watu wengine ambao si masahaba walivyoanza kutafuta dunia baada ya kifo cha Mtume na sasa dunia imewashinda. Lakini kabla ya hapo tunataka kuonesha kwamba msukumo waliopewa ani Umayyah na Uthman ilikuwa kinyume na radhi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Mwenyezi Mungu amewaita ‘mti uliolaaniwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu amewaita watu walioapizwa na umma. Wasomi wanakubaliana kwa pamoja kwamba Bani Umayyah walikuwa na chuki dhidi ya Mtume.

Ali anasema kwamba kila umma ulikuwa na shida za namna moja au nyingine Balaa la uma huu ni Bani umayyah (Tathir al-Jinan kwenye maandishi ya pembeni Sawaiq Muhriqah, uk. 143, na Kanzul Ummah, Juz. 6, uk. 91).

Kwa mujibu wa maoni yaliyothibitishwa ya Mtume na uzao wake, Bani Ummayah walikuwa balaa la uma lakini msimamo wa Uthman kwao ni kwamba alijivunia kitendo cha kufungua hazina ya Taifa kwa ajili yao. Khalifa Uthman alikuwa akisema; “Hazina ya Taifa ni yetu. Tutatumia kama tupendavyo na hatutakubali ushauri wa mtu yeyote.” (Sahuh Bukhari, Juz. 5, uk 17 na Tarihut Tashrib, Juz. 7).

Sasa tutatoa maelezo kuhusu urithi kwa baba wa masahaba. Itahakikishw utajiri mkubwa wa Waislamu ulifujwa na Uthman na jinsi alivyowatajirisha ndugu zake.

Zubayr bin Awam alikuwa mkwe wa khalifa wa kwanza. Alichoacha baada ya kifo chake ni:

    • Nyumba kumi na moja –Madina

    • Nyumba mbili –Basrah Nyumba moja- Kufah.

    • Nyumba moja Misri. Alioa wanawake wanne.

Baada ya kutoa theluthi moja (1/3) ya utajiri wake, kila mke alipata robo (1/4) ya thamani ya utajiri wa rasilimali yake yote ilikuwa dinari laki nane. (Sahih Bukhari, Kitabul Jihad Baab Barakar al-Ghifani Fi-Malih, Juz. 5, uk 17 na 21; Irshad al-sare Undat al-Qari Shazarat Dhahab Juz. 1, uk 43, Tarikh bin Kathir Juz. 7 uk. 249 na Tarikh Khsanus, Juz. 2, uk 311).

Muhammad bin Sad al-Dhahri al-Basri, Kitab al-Abbasi al-Qaqidi (Alifariki mwaka 230 A.H), ameandika kwamba alikuwa na mashamba huko Alexandria, Misri na Kufah na nyumba kadhaa Basrah. Alipokea magunia mengi sana ya nafaka kutoka Madina (Tabaqat bin Sad Waqidi; Juz. 3, uk. 77 chapa –London) Abul Has Ali bin Husain bin Ali Masud alikufa mwaka 346 A.H) ameandika kwamba zaidi ya vitu hivi aliacha farasi elfu moja, watumishi elfu moja, watumishi wa kike elfu moja na sehemu kubwa ya ardhi. (Murujuz Zahab uk, 434).

Talha bin Ubaydullah Tamim pia alikuwa mkwe wa Khalifa wa kwanza. Alikuwa na nyumba Kufah iliyojulikana kwa jina la Kanaas. Pato lake la kila siku kutokana na mauzo ya nafaka ilikuwa dinari elfu moja. Alikuwa na nyumba za kulala wageni kadhaa ambazo zilikuwa kati ya Tahama na Taif. Alimiliki ikulu ya hali ya juu sana Madina. Alikuwa na rasilimali Iraq ambayo ilikuwa inazalisha pato la dinari 10,000 kila mwezi Musa bin Talha anasema kwamba aliacha dinari laki mbili fedha taslim. Pia aliacha ardhi ya kilimo. Zaidi ya hayo, aliacha magunia ya ngozi mia tatu yaliyojaa dhahabu na fedha. Bin Jauzi anasema magunia hayo yalitengenezwa kwa ngozi ya ngamia na yalikuwa makubwa sana (Tabaqat bin Sad, Juz. 3, uk 158, Ansabul Ashraf Balazari, Juz. 5, uk 7; Murujuz Zahab, Juz. 1, uk. 434, Iqbdul Farid, Juz. 2, uk 258, Duwalul Islam Zahabi, Juz. 1, uk 18 na Al-Khulasah Khazraji, uk. 152).

Abdur Rahman bin Auf alikuwa shemeji yake Uthman na ni mtu huyu ndiye wakati Umar alimfanya Uthman kuwa Khalifa badala ya Ali, kama ambavyo imekwisha simuliwa. Aliacha ngamia elfu moja, mbuzi elfu themanini na farasi mia moja na aliacha dhahabu nyingi sana hivyo kwamba ilibidi ikatwe kwa shoka ili igawanyike. Alikuwa na wanawake wanne wa ndoa. Kila mmojawao alikuwa na dinari 83,000. Alimtaliki mke mmoja wakati anaugua na alimpa dinari 83,000. Aliacha kondoo 10,000, wenye thamani ya dinari 84,000. (Tabaqat bin Sad, Juz. 3, uk 96, Murujuz Zahab, Juz. 1, uk 434; Tarikh Yaqubi Juz, 2, uk. 146; Safwatus Safwah bin Jauzi Juz. 1, uk. 138, Riazun Nazrah, Juz. 2, uk. 291; Istiab Abdul Barr Makki, Juz. 2, uk. 404 na Tuhfah Ithna Ashariyah na Muahadithi Dehlavi). Sasa kutokana na urithi aliooacha tunapata sababu iliyomfanya amweke Uthman kwenye Ukhalifa badala ya Ali bin Abi Talib.

Sad bibn Abi Waqqas aliacha dinari 250,000 na nyumba iliyojengwa mahali paitwapo Aqiq. Nyumba hii ilikuwa nzuri, kubwa yenye nafasi ndefu kwenda juu. (Tabaqat bin Sad, Juz. 3, uk 105, na Murujuz Zahab, uk 120 wa Tafsir ya kitabu cha Abdul Hamid Jaudatus Sahar kwamba Sad bin Abi Waqqas alikuwa amenakshi sehemu ya ndani ya ikulu yake kwa mawe magumu.

Yala bin Ummayah ambaye alikuwa gavana wa Yemen aliacha dinari 500,000, wadeni wake wengi na ardhi kubwa. Zaidi yake, aliacha rasilimali yenye thamani ya Dinari 100,000. (Murujuz Zahab, Juz. 1, uk 432).

Zaid bin Thabit ni mtu aliye msaidia Uthman kwa kila njia na alikuwa mnyenyekevu kwake. Alipokufa, aliacha dhahabu na fedha katika hali ambayo haingegawika isipokuwa kuikata kwa shoka na kishoka. Zaidi ya hayo, aliacha mali nyingine iliyokuwa na thamani ya dinari laki moja. (Murujuz Zahab Masud).

Huu ulikuwa ukarimu, upendeleo na fadhila za Uthman, Khalifa wa tatu kwa watu wake waliokuwa wanamtakia mema. Hakuna mfuasi wa Mtume ambaye angevumilia namna yake ya kugawa utajiri wa Waislamu miongoni mwa watu wake. Ndio sababu Ali, Salman, Abu Dharr, Miqdadi na Ammar walikuwa wanampinga wakati wote kuhusu tabia yake.

Inawezekana watu wakasema kwamba lolote alilofanya Uthman ilikuwa kwa ajili ya ndugu zake kama alivyosema yeye mwenyewe kwamba aliwafikiria kwamba walistahili na hakufanya lolote kwa maslahi yake. Jibu la maoni ya Uthman linaweza kuwa mtu asiyezingatia sharia ya dini katika masuala yahusuyo ndugu zake, kwa hakika hatakuwa muangalifu hata kwa mambo yanayomhusu yeye mwenyewe. Uthman alikuwa na meno kadhaa yaliyotengenezwa kwa dhahabu. Kivazi chake kilikuwa joho la hariri na manyoya ambalo thamani yake ilikuwa dinari mia moja.

Vazi la mkewe Nailah pia liligharimu dinari mia moja. (Tabaqat bin Sad Juz. 3, uk. 40; Ansad, Balazari Juz. 3, uk. 4, Istiab, Juz. 4, uk. 476).

Palikuwepo kasha kwenye Hazina ya Taifa huko Madina ambalo lilijaa dhahabu na fedha. Alitengenezesha urembo kwa ajili ya familia yake kutokana na madini hayo. Watu walimpinga sana kuhusu suala hilo, na alizozana na Ali pia, lakini hakujali lolote. (Ansah, Balaziri juz, 3, uk. 4). Alijenga ikulu Madina; jengo hilo liliimarishwa kwa mawe na marumaru na milango yake ilitengenezwa kwa mbao za mvule zenye ubapa unaoteleza. Alihodhi utajiri mwingi sana. Alimiliki chemchem kadhaa Madina. Waandishi wa historia wanasema kwamba baada ya kuuawa, aliacha dinari laki hamsini. Miongoni mwa mali zake na vitu vingine vilivyokuwa kwenye miliki yake, vile vilivyokuwa kwenye bonde la Qura na Hunayn peke yake thamani yake ilifika dinari laki moja. Zaidi ya hayo aliacha farasi na ngamia wengi. Kwa mujibu wa bin Sad thamani urith wa bonde la Qura na Khaybar ulikuwa dinari laki mbili. (Tabaqat bin Sad, Juz. 3, uk 53 na Masudi, Juz. 1, uk 433). Na kwa mujibu wa Jovji Zaydan uriti huo ulikuwa dinari laki 10. (Tamaddume Islam, Juz 1, uk 22, chapa Misri) Zaidi yake, aliacha watumishi elfu moja; (Bin Sad, Juz. 3, uk. 53).

Umar khalifa wa pili pia hakuweza kuepuka ladha ya ukabaila. Alikuwa na bustani Hijaz iliyokuwa inaingiza pato la dinari elfu 40 kwa mwaka ambalo alitumia yeye binafsi na familia yake Bani Adi. (Tarikh Tabari, Juz. 2, uk. 82, chapa Misri) kwa mujibu wa hadith ilioko sahih Bukhari, Umar aliuliza kiasi cha deni lake alilotakiwa kulipa Hazina ya Taifa. Watu walifanya hesabu na wakamwambia deni lake lilikuwa dinari elfu themanini na sita. Akawaamuru walipe deni hilo kutoka kwenye fedha ya ndugu zake mwenyewe. Ni kwamba, aliwaambia walipe deni hilo kutoka kwenye rasilimali yake. (Tarikh Tabari, Juz. 2, uk. 382). Naafe mtumishi wa bin Umar, amekanusha kwamba Umar hakuwa na deni na amesema ingewezekanaje Umar kuwa na deni ambapo mmojawapo wa warithi wake aliuza mgawo wa rasilimali kwa dinari laki moja. (Kitab Madina Umar bin Shaybah).

Akitoa maoni kuhusu usemi wa Naafe bin Hajaz alisema kwamba wakati mwingine hutokea kwamba mtu anakuwa na deni licha ya utajiri wake. (Tarikh Tabari, Juz. 3, uk. 383). Ndugu alimuomba Umar fedha. Mara ya kwanza alimdharau lakini baadaye alimpelekea dinari elfu kumi. (Tarikh Tabari, Juz. 5, uk. 19) Yakiwepo mambo kama haya tunapoangalia uzao wa Mtume na jinsi walivyoteseka, tunawasikitikia na tunashtuka sana tunapoona kwamba watu hawa waliwanyang’anya Ahlul-Bait hata ile haki yao ya khumus (Izatul Khifa, Juz. 2, uk. 256) na kuwapora fadak.

Sura Ya Kumi Na Saba

Ni ukweli ulio thabiti kwamba Abu Dharr alikuwa karibu sana na Mtukufu Mtume na Ahlul Bait wake na aliendelea kuwa msiri wao mkubwa. Aliona kwa uangalifu sana kila kipengele cha maisha yao, na alijifunza mengi kutokana nao. Ameona kwa macho yake si mara moja lakini mara nyingi kwamba Mtukufu Mtume alikuwa anajilaza msikitini akiwa na njaa na watoto wake nyumbani walikuwa na njaa. (Alaimun Nubuwwah, al-Mawardi, uk. 146 chapa Misri).

Abu Dharr pia alimuona Ali bin Abi Talib akifanya kazi ya kupokea ujira akiwa amevaa nguo zakukwaruza. Aliona majani ya mtende kwenye joho la bint yake Mtume.

Pia aliusikia Ali akimnasihi mtumishi wake wa kike wa Kiafrika Fizzah; “Ewe Fizah! Sisi Ahlul Bait hatukuumbwa kwa ajili ya dunia au kutafuta faida ya kidunia. Badala yake tumeumbwa kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu na kutangaza ujumbe wa Mwenyezi Mungu, Uislamu. Ni kazi yetu kuongoza thamani ya uadilifu wa mtu, kuwasha mwanga wa Upweke wa Mwenyezi Mungu kwenye mioyo ya watu na kuwapa njia na namna ya kuendesha na kustawisha maisha yao.”

Abu Dharr pia aliona kwamba Ali alikuwa na kawaida ya kula mkate mkavu wa shayiri na alificha mifuko unga wa Shayiri yake kwa ustadi mkubwa hivyo kwamba haingewezekana mtu kuweka samli. (Allamah Kashif al-Ghita, The Shia Origin and Faith, ISP 1982). Pia alimuona Ali kwamba alikuwa na desturi ya kubeba mfuko ya unga yeye mwenyewe kuwapelekea wajane masikini na mayatima. Pia alimuona Ali akiiambia dunia, “Ewe Dunia! Nenda ukawadanganye wengine. Nimekutaliki mara tatu!.” Pia alishuhudia kwa macho yake kwamba wazawa wa Muhammad walikuwa na tabia ya kula chakula pamoja na watumishi na watumwa wao. Alikumbuka vizuri kwamba wakati fulani ambapo dinari nne zilibaki baada ya Mtume kugawa fedha aliyokuwa nayo na kiasi hiki hakingemfikia mtu anayestahili, alisikitika sana. Alikuwa bado anakumbuka maneno haya ya Mtume aliyomwambia yeye, Ewe Abu Dharr! Hata kama nina miliki dhahabu yenye ukubwa sawa na Mlima Uhud sipendi ibakiea kwangu hata chembe.”

Katika hali kama hii, ingewezekanaje Abu Dharr anyamaze wakati Uislamu ulikuwa unageuzwa na mafundisho ya viongozi wa Uislamu yalikuwa yanadharauliwa? Mara tu Mtukufu Mtume alipofariki kila kitu kilibadilishwa. Dhuluma na udikteta ilishamiri, watu walilazimishwa kutoa kiapo cha uaminifu, nyumba ya Ahlul Bait ilichomwa moto, na mlango ulivunjwa na kumwangusha Fatimah, bint yake Mtukufu Mtume.(al-Milal wan Nahl Juz. 1, uk. 25 chapa ya Bombay).

Ali alifungwa kwamba shingoni na masahaba mashuhuri waliishi maisha ya upweke majumbani mwao. Katika kulazimishwa na hali halisi Abu Dharr alistahamili kwa kipindi fulani. Hatimaye akaondoka Madina na kwenda Syria na akakaa huko. Baada ya muda alipokwenda tena Madina aliona kwamba viongozi walifika kwenye kilele cha kuendelea mambo ya dunia.

Fahari na maonesho ya kifalme yalishika nafasi ya ucha Mungu aliyoishi Mtukufu Mtume. Fadhila na upendeleo ni tabia ambazo zilishamiri, na uaminifu na uchaji Mungu vilionekana kuwa vitu vya zamani. Utajiri wa Hazina ya Taifa ulikuwa unafujwa. Utajiri wa Waislamu ulikuwa unatumiwa kwa maslahi ya binafsi. Kila ndugu na anayemtakia mema khalifa alipata umilionea. Ukabaila ulipanuka. Palikuwepo na utajiri mwingi sana. Hakuna mtu aliyejali Zaka. Hakuna Mtu aliyejali mayatima na wajane.

Alipoona mambo mengi yasiyo na idadi kama haya, Abu Dharr alijaribu kumwonya Khalifa Uthman kwa ajili ya kuulinda umma wa Kiislamu na serikali ya Kiislamu na akamshauri kadiri alivyoweza, lakini Khatifa hakutilia maanani ushauri wake. Hatimaye kwa kuzingatia ahadi aliyoahidi kwa Mtukufu Mtume na ule uzio wa imani ambao Mwenyezi Mungu alihifadhi moyoni mwake, alijitokeza uwanjani na akaanza kutangaza dosari za Uthman. kuunganisha na hayo, pia alikemea tabia ya kuhodhi utajiri na ukabaila na alianza hotuba yake na zile aya za Qurani zinazokosoa kuhodhi utajiri.

Kwa kuwa Abu Dharr hakuvumilia kuona utajiri wa rasilimali ya taifa inatumika kwa kuwagawia ndugu zake khalifa tu na mayatima na wajane wanakufa kwa njaa, aliongeza kazi ya mahubiri yake, na kwa hiyo alikwenda sehemu nyingi mbali mbali.
Alihamishwa kutoka Madina na kupelekwa Syria na wakati mwingine alilazimishwa kuishi kwenye sehemu iliyokuwa tupu kama Rabzah.

Ni dhahiri kwamba kugawa utajiri miongoni mwa fukara ni muhinu, lakini pia ni muhimu kufikiria utajiri huo ugawiwe kwa kanuni gani kwa masikini na watu wengine wanaostahili. Ilikuwa ni kanuni ya Mtume kwamba aligawa utajiri bila upendeleo. Kuhusu ngawira ya kivita, alisema kwamba moja ya tano (1/5) ilikuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na sehemu nne ya tano (4/5) kwa ajili ya jeshi la Uislamu ambamo mashujaa wote wanapata mgawo sawa. Hakuna anayestahili kupata zaid ya mwingine (Sunan Baihaqi).

Inajulikana kutoka kwenye vitabu vya hadithi kwamba alikuwa na kawaida ya kugawa pato la ushuru miongoni mwa Waislamu siku hiyo hiyo ya kupokea pato hilo. Watu waliooa aliwapa mgawo mara mbili na mgawo moja kwa mseja. (Sunan Abi Daud, Juz. 1, uk 25; Musnad Ahmad bin Hanbal, Juz. 2, uk. 29 na Sunan Baihaqi Juz. 6, uk. 346).

Utaratibu huo huo ulifuatwa na Imamu Ali. Hafidh Baihaqi anasema kwamba wakati fulani alipata fedha na rasilimali kutoka Isfahan. Aligawa fedha na rasilimali hiyo katika sehemu saba za mgawo zilizo saw, mkate wa boflo moja ulibaki lakini aliugawa pia katika vipande saba vilivyo sawa na kuweka kipande kimoja kwenye kila mgawo katika hiyo migawo saba. Aliandika majina na alimpa mtu mgawo ambaye jina lake lilitokea kwenye kura. (Sunan Baihaqi juz, 6, uk 438).

Wakati fulani wanawake wawili walimwomba. Mmojawao alikuwa huru na mwingine alikuwa na asili ya utumwa. Alimpa kila mmoja ngano kidogo na dinari arobaini.

Mwanamke mwenye asili ya utumwa alikwenda na mgawo wake lakini yule mwanamke huru akasema, “Umenipa mgawo sawa na ule wa mtumwa, ingawa mimi ni mwanamke huru wa Kiarabu ambapo mwenzangu ni mtumwa na si Mwarabu.” Amiri wa Waumini akasema, Nimepekua kwa uangalifu mkubwa Kitabu cha Mungu lakini sikuona sababu yoyote ya ubora wako.”

Muhammad Razi Zangipuri ameandika kwamba wakati wa utawala wa Ali ambapo utaratibu wa Mtume alifuatwa na fedha iligawanywa katika misingi ya usawa, hali ya kutokuridhika chuki na kero ilionea miongoni mwa masahaba wa Mtume walio mashuhuri wakipinga mbinu hiyo. Ali akasema kuhusu kuonesha kwao chuki na kero; “Mtakuwa mnaniamuru mimi kwamba nitafute msaada wenu na kuniunga mkono kwa kufanya udhalimu kwa watu ambao kuwa ajili yao mimi nimewafanywa mtawala? Ni kwamba, niwapunje stahili yao ili nyingi niwazidishe mgawo na kwa hiyo kuwafanyeni nyinyi kuwa watu wanao niunga mkono?

“Kwa jina la Mwenyezi Mungu hadi hapo ambapo hadithi za usiku zinaendelea kusimuliwa na nyota inafuata nyingine yaani nyota zinakuwa kwenye mwendo, sitakaribia utaratibu kama huo. Hata kama ingekuwa rasilimali yangu binafsi, ningeigawa sawa kwa sawa miongoni mwa watu, lakini sasa inapokuwa hii ni mali ya Mwenyezi Mungu, kwa nini nisizingatie usawa. Lazima mtambue kwamba kugawa fedha na wema bila kuzingatia usawa ni ubadhilifu na ufujaji ambao unamnyanyua mgawaji juu hapa duniani na kumteremsha chini na kumfedhehesha huko akhera.” (Islam ka Maashi Nizam, toleo la lugha ya Urdu, uk 154).

Ni wazi kwamba kutokana na kanuni iliyotajwa kwenye kurasa za nyuma ya kugawa utajiri kwamba rasilimali zitagawanywa bila upendeleo miongoni mwa masikini, wasiojiweza na aina zote za watu wanaostahili. Mara tu Ali alipokalia kiti cha Ukhalifa alitangaza, “Nyingi ni waja wake Mwenyezi Mungu. Utajiri utagawanywa sawa sawa miongoni mwenu bila ubaguzi au kutofautisha.” (Nasikhut tawarikh, Juz. 2, uk. 21).

Endapo Waislamu wanafuata njia za Kiislamu, maisha ya umasikini hayatakuwa mzigo kwao.

Sura Ya Kumi Na Nane

Baada ya Abu Dharr kurudi Madina kutoka Syria, alijishughulisha na mahubiri yake ambapo tukio lingine la kupasua moyo lilitokea kwa mara nyingine na hilo lilikuwa la kuchomwa kwa Qurani.

Tayari alikwisha huzunika kuona Serikali ya Kiislamu ilikuwa inaharibiwa. Utajiri wa Waislamu ulikuwa unatumika kuwapa ndugu na jamaa wa Khalifa. Mlango wa Hazina ya Taifa ulifungwa kabisa kwa wanaohitaji, masikini, mayatima na wajane, lakini ulikuwa umefunguliwa wazi sana kwa uzao wa Umayyah. Watu masikini walikuwa wanateseka kwa njaa ambapo ndugu wa khalifa walikuwa wananunua nyumba, mabustani na ardhi. Ghafla akapata taarifa kwamba khalifa alikuwa na nakala tofauti za Qurani ambazo zilikusanywa kutoka sehemu mbali mbali na akazichoma moto. Kwa hiyo, tukio hili muhimu likawa lenye mahubiri yake. Mwandishi wa historia Abul Fida ameandika kwamba tukio hili lililotokea mwaka wa 30 A.H. (Tarikh Abul Fida, Juz. 2, uk. 100, chapa Amritsar, 1901 A.D).

Mwandishi wa historia Yaqubi (alifariki mwaka wa 278 A.H ) ameandika kwenye kitabu chake kwamba Uthman alikusanya Qurani na akazipanga kwa namna ambayo aliziweka sara ndefu pamoja na sura fupi pamoja mbali mbali, na akaagiza nakala kutoka kila sehemu, zikaoshwa kwa maji ya moto na siki na akazichoma moto. Matokeo yake ni kwamba hakuna nakala ya Qurani iliyobakia isipokuwa nakala iliyomilikiwa na Bin Masud ambayo alikuwa nayo Kufah. Abdullah bin Amir, gavana wa Kufah alipomuuliza bin Masud amwoneshe nakala yake akakataa. Uthman alipopata taarifa hii alimwandikia barua Amir amkamate bin Masud na ampeleke kwake Madina. Bin Masud alipoingia msikitini, Uthman alikuwa anatoa hotuba.

Alipomuona Bin Masud akasema; “Mnyama mbaya na katili amekuja.” Bin Masud naye alitoa jibu kali. Uthman aliposikia, akaamuru watu wampige. Kwa hiyo, watu wakampiga na kumburuza kwa namna ambayo kwamba mbavu zake mbili zilivunjika.

Imeandikwa kwenye tarjumi ya Kiajemi ya Tarikh Atham Kufi (imechapishwa Bombay, uk. 147 mstari wa 8) kwamba Uthman alipasua Quran na ikachomwa moto. Ni maelezo ya aina haya haya yapo kwenye kitabu ‘Successors of Muhammad’ (W. Iqving Uk. 160 chapa –London, 1850 A.D).

Kwa mujibu wa Majatul Mumin usemi wa Mulla Mohsin Kashmiri, Uthman akavunja mbavu za bin Masud na akamnyang’anya Quran na akaichoma moto. Kufuatana Raudhatul Ahad Juz. 2, uk. 229, chapa Luckanow), Uthman aliamuru Qurani yangu lazima ipewe nafasi ya kuenea kwenye utawala wangu na nakala zingine zichomwe moto. Kwa mujibu wa Tarikh al-Quran usemi wa Abdul Qadir Makki, uk. 36 chapa ya Jeddah, 1365 A.H Sahih Bukhari Juz. 6, uk. 26 chapa Bombay, Mishkar Shari chapa Delhi, uk. 150, na Tafsir Itqan Suyuti chapa Ahmads, Juz. 1, uk 84, Uthman alipeleka taarifa kwa Hafsah, mke wa Mtukufu Mtume, ili ampelekee Maandishi ili aweze kunakili na halafu amrudishie. Hafsah alimpekea nakala alizokuwa nazo na Uthman akamteua Zayd bin Thabit, Abdullah bin Zubayr, Said bin As, Abdul Rahman bin Harith kukusanya na kunakili maandiko hayo, na aliwataka watu hao wote watatu wa Quraishii kuandika Qurani kwa kutumia mazungumzo ya Quraishi endapo pangetokea tofauti fulani katika mambo kadhaa, kwa sababu Qurani iliteremshwa katika lugha yao. Watu hao watatu walifanya kufuatana na walivyoagizwa hadi mwisho na Uthman akayarudisha Maandiko hayo kwa Hafsah kama alivyoahidi na akampelekea nakala iliyotayarishwa upya. Sasa, nakala ya Qurani iliyobakia ni hiyo tu iliyotayarishwa na Uthman iliendelea kuwepo na nakala zingine zote zilichomwa moto. Kwa mujibu wa Fathul Bari, usemi wa bin Hajar Asqalani Juz. 4, uk 226, Uthman alirudisha Qurani ya Hafsah lakini Marwan alichukua kwa nguvu na akaichoma moto. Kwa mujibu wa Tarikh Khamis uk. 270, Istiab uk. 73 na Sawaiq Muhrizah uk. 68 Uthman alihakikisha nakala zote za Qurani zimechomwa moto isipokuwa ya kwake na aliamuru Abdullah bin Masud apigwe sana hivyo kwamba alipata maradhi ya henia (ngiri). Halafu akamfunga jela na akafia huko. Kwa mujibu wa Tuhfah Ithna Ashariyah, usemi wa Abdul Aziz, Ubayy bin Kab alimpa Uthman Qurani yake na hakupigwa. Qurani hiyo pia ilichomwa moto.

Kwa hali yoyote ile imeandikwa kwenye vitabu vingi sana kwamba Uthman alichoma maandiko matakatifu. Hizi ni nakala za Qurani zilizokusanywa wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr. Aishah Ummul Muminin alipopata habari ya Qurani kuchomwa moto alikuwa na wasi wasi. Akasema, “Enyi Waislamu! Muueni mtu huyu ambaye anachoma Qurani! Amefanya udhalimu mkubwa sana.”(Anwarul Qulub, Muhammad Baqir Majlis uk. 313).

Aishah hakuridhika na jambo hili alifululiza kudhihirisha kero dhidi ya Uthman. Alisema tena na tena; “Muueni Yahudi huyu, Na’thal. Mwenyezi Mungu na amuue. Amekuwa asi.” Rauzatul Ahbab, Juz. 3, uk. 12). Kwa mujibu wa Tazkirab Khawasul Ummah uk. 38, 40, 41 bin Athir Jazari alikwua akisema, “Muueni Na’thal huyu. Mwenyezi Mungu na amuue.” Kwa matamshi haya alikuwa anamaanisha khalifa Uthman. Halafu bin Athir anaeleza kwa nini Aishah alimuita Uthman Na’thal. Sababu ni kwamba Na’thal alikuwa yahudi wa Misri na ndevu zake zilifanana na zile za Uthman. Halafu tena anasema kwamba kufuatana na matamshi ya Shaykh ilimaanisha mpumbavu. Anaendelea kusema kwamba baadae Aishah alikwenda Makkah (Nihayah bin Athir).

Mwandishi wa historia Ibn Taqtaqi ameandika kwamba Uthman aliuawa kwa matokeo ya amri ya Aishah, ‘muueni Na’thal huyu.” Siku hiyo hiyo nyumba yake ilipozingirwa, Aishah alikwenda Makkah. (Tarikh Fakhri, uk. 62 chapa Misri).

Inaeleweka wazi kwamba Aishah akiwa mwanamke alishtushwa na tukio hili, kwa nini Ali asingeshtushwa na tukio hili la kutisha? Imejulikana kutokana na maandishi ya wasomi wa kuaminika kwamba Ali alishtushwa sana na tukio hili la kuchomwa Qurani. Kwa hiyo, aliona umuhimu wa kutaka ushauri wa Abu Dharr kuhusu suala hili. Allamah Majlis ameandika kwamba baada ya tukio hili Ali alimuomba Abdul Malik, mtoto wa Abu Dharr ampeleke baba yake kwake. Alipofika, alibadilishana mawazo naye kuhusu tukio hili, alionesha kuhuzunika kwake na akasema jambo hili limenyoshwa na kupasuliwa vipande vidogo. Inawezekana Mwenyezi Mungu atalipa kisasi kwake kwa jinsi ile ile. Abu Dharr akasema , “Ewe Ali! Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema kwamba wafalme dhalimu watawaua watu wa nyumba yake.” Ali akasema, “Ewe Abu Dharr! Unataka kunikumbusha kuhusu kuuawa kwangu?” Abu Dharr akasema, “Hapana shaka, hilo litatokea na wewe utakuwa mtu wa kwanza miongoni mwa uzawa wa Mtume kuuawa.” (Hayatul Qulubi, Juz. 2, uk. 104).
Kwa ufupi, inaonesha wazi kwamba Abu Dharr aliathirika sana na tukio hili la kuogofya. Pia aliongeza maudhui moja zaidi kwenye hotuba zake na kuliita tukio hili njia isiyo ya Kiislamu. Na itambulike kwamba kwa kuwa kitendo cha kuchoma Qurani kinatia jeraha moyo wa Kiislamu kwa baadhi ya waandishi wa siku hizi, wamebadilisha neno kuchoma pale ambapo maelezo ya kuchomwa Qurani yanatolewa. Shah Walyullah Dehlavi, kwenye matukio katika maisha ya Uthman ameandika. “Aliyaondoa maandiko mengine ambayo yalifikiriwa kusababisha migongano. (Izalatul Khifa Juz. 1, uk 274).

Sura Ya Kumi Na Tisa

Waandishi wa historia wanasema kwamba Abu Dharr alitoa hotuba zake kuhusu mada maalum. Msikitini, nje ya msikiti, kwenye baraza, kwenye viwanja vya maonyesho ya michezo, mitaani na mahali popote alipopata fursa ya kufanya hivyo. Hakuogopa kuuawa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu alikwisha mwambia kwamba hakuna mtu ambaye angeweza kumua au kumfanya aache imani yake wala hakuogopa shutuma kwa sababu aliapa mbele ya Mtukufu Mtume kuhusu suala hili. Alikuwa na uhakika kabisa kwamba lolote alilofanya ilikuwa linakubaliana na utashi wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Ndio sababu alikuwa anashughulika wakati wote katika kutekeleza kazi yake kwa ujasiri na hamasa kubwa.

Kwa upande moja mahubiri ya Abu Dharr yalizidi kupamba moto na kwa upande mwingine Uthman alikuwa anaendelea na zoezi la kuipima dhamiri yake kwenye kioo cha tabia yake mwenyewe. Alitaka ushauri kutoka kwa Marwan ili aweze kujua Abu Dharr angenyamazishwa kwa njia gani na shutuma zake kuhusu tabia ya Uthman na upinzani wake kuhusu kuhodhi utajiri ungesitishwa.

Marwan akasema, “Ipo njia moja tu ya kuweza kufanikiwa ni kwamba, kiasi fulani cha fedha kipelekwe kwa Abu Dharr. Labda anaweza akakubali na kunyamaza.” Uthman alisikia jibu hili la Marwan na akanyhamaza. Sababu ya kimya chake ni kwamba alikuwa anatambua tabia ya Abu Dharr. Alijua kwamba Abu Dharr alikuwa hana tama ya fedha. Marwan aliwaita watu wawili, akawapa mfuko wenye dinari mia mbili na akasema, “Mpelekeeni Abu Dharr na mwambieni kwamba Uthman anamtakia kila la kheri na amemwomba akubali kuchukua mfuko huo wa fedha na atumie apendavyo.”

Watu hao walikwenda kwa Abu Dharr usiku wakiwa na huo mfuko wa fedha. Wakati huo alikuwa anasali msikitini. Labda alikuwa anakaa kwenye msikiti wa Mtume wakati huo kwa sababu Uthman alimuita kwa lazima kutoka Syria ambapo familia yake ilikuwa bado huko.

Akiwatazama wageni, Abu Dharr aliwauliza wao walikuwa nani na walikuwa na madhumuni gani? Wakampa mfuko wa fedha na wakasema, “Khalifa Uthman amekupa salamu zake na anakuomba ukubali kuchukua hizi dinari mia mbili kwa ajili ya matumizi yako.” (Kashkol Bahai).
Abu Dharr akasema, “Je! Amegawa kiasi kama hiki kwa Muislamu mwingine pia?” Wakajibu, “Hapana, hajampa yeyote. Huu ni ukarimu wa Khalifa kwako peke yako.

“Tafadhali rudusha.”Abu Dharr akasema, “Mimi pia ni mmojawapo wa Waislamu ambapo Khalifa hajampa Muislamu yeyote, mimi peke yangu siwezi kukubali kuchukua. Mimi sihitaji fedha ambapo Waislamu wengine masikini hawakupata. Nendeni, mrudishieni na mwambieni kwamba mimi ninatosheka na ngano kidogo tu, mimi hupata ujira wa riziki yangu. Nifanye nini na dinari hizi?” (Abu Dharr Ghifari, uk. 126, na Hayatul Qulub Juz. 2, uk 1039).
Marwan alikosea kufanya uamuzi huo kuhusu Abu Dharr. Yeye alidhani kwamba kama vile watafutaji wengine wa dunia hawakujali imani na itikadi kwa ajili ya utajiri, Abu Dharr naye angefanya hivyo. Hakujua kwamba Abu Dharr alikuwa kwenye daraja la juu zaidi kulinganishwa na watafutaji wa dunia.

Tukiliangalia tukio hili kwa uangalifu, Abu Dharr alifuata kwa karibu sana nyayo za Mtukufu Mtume na Ali kwa kurudisha fedha na kwa kusema, “Maana yake nini kunipelekea fedha peke yangu na kutowajali Waislamu wengine?” Hawa (Mtume na Ali) ni watu ambao walijali kuwatumikia Waislamu zaidi kuliko kutumikia nafsi zao. Wao hawakutaka wawe wanabilingika kwenye utajiri ambapo masikini waendelee kuwa masikini. Wao hawakupenda kuwepo na hata ile tofauti ndogo baina yao na watu masikini. Kwa uthibitisho tunaweza kutoa mfano wa tukio la kufuturu kwa Ali kama ilivyosimuliwa na Ahnaf bin Qays mbele ya Muawiyah barazani kwake.

Kwa mujibu wa Mansur bin Husein Abi alikufa 422 A.H) kwenye kitabu chake Nass ud-Duras, kama ilivyo nukuliwa na Shaykh Muhammad husayn Ale Kashiful Ghita; Ahnaf bin Qays alisema, “Wakati fulani nilikwenda kwa Muawiyah. Aliweka mbele yangu vyakula vya aina nyingi mno. Nilikuwa bado ninashangaa ambapo aliweka mbele yangu chakula maalum ambacho sikuweza kukitambua. Nikamuuliza hicho kilikuwa chakula gani.

“Akajibu kwamba huo ulikuwa utumbo wa bata uliojazwa ubongo na kukaangwa kwenye mafuta na kunyunyiuzia viungo. Niliposikia hivi nilianza kulia. Muawiyah akaniuliza sababu ya kulia, nikamwambia kwamba nilimkumbuka Ali wakati huo.

“Siku moja nilikuwa na Ali ambapo muda wa kufturu ulifika. Aliniomba nisiondoke. Wakati huo huo mfuko ulio zibwa vizuri uliletwa. Nikamuuliza mfuko ulikuwa na nini. Akajibu kwamba huo ulikuwa unga wa shayiri iliyokaushwa . Nikamuuliza kwa nini mfuko huo ulizibwa kwa uangalifu kiasi hicho, ilikuwa ni sababu ya kuzuia usiibwe au matatizo ya kiuchumi. Akajibu kwamba haikuwa sababu yoyote kati ya hizo mbili zilizotajwa. tahadhari hiyo ilikuwa kuwazuia wanawe wasije wakachanganya unga huo na mafuta ya samli au michikichi.

“Niliendelea kuuliza endapo mafuta ya samli au mchikichi yaliharamishwa. Akajibu kwamba hayakuharamishwa. Bado, ilikuwa muhimu kwa viongozi wa umma kujiweka katika hali iliyo sawa na ile ya watu masikini, ili kwamba ukosefu wa njia za kujikimu isije ikawa sababu ya tabaka la watu masikini kugeuka kuwa waasi. Muawiyah akaniambia kwamba nilimkumbuka mtu ambaye uadilifu wake si rahisi kukanusha.”

Hata hivyo, wale waliopeleka mfuko wa dhahabu kwa Abu Dharr walirudi kwa Uthmani na wakamwambia alivyowaambia Abu Dharr. Uthman akamwambia Marwan, “Nilijua kabla kwamba Abu Dharr hangekubali kuchukua fedha hiyo.”

Abu Dharr aliendelea na shughuli yake ya kuhubiri kama kawaida. Kila alichosema haikuwa upinzani ulioelekezwa kwa mtu fulani pekee. Hakika, alitaka watu wasimsahau Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kuhodhi fedha lakini kuimarisha kanuni za Uislamu kwa kuwahurumia masikini. Abu Dharr hakuweza kuvumilia kuona utajiri wa Hazina ya Taifa unatumika kwa kupewa watu wasiostahili bila sababu yoyote ambapo watu wanaohitaji wanateseka njaa.

Hakuvumilia hata kupasuliwa na kuchomwa Quran. Hakuchoka kuwashutumu wale ambao walikuwa na hatia kwa kufanya uhalifu kama hao.
Alikuwa nazo amri za Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Alikuwa anazingatia kanuni za Uislamu. Alitaka watawala Waislamu kufuata njia ya Uislamu.

Kwa ufupi, kwa upande moja Abu Dharr alikuwa anashughulika na kazi yake ya kuhubiri na kwa upande mwingine, Uthman alikuwa na shauku ya kupata njia ya kumnyamazisha.Katika kutimiza lengo hili alijaribu kushauri kila aina ya mpango lakini hakuweza kufaulu. Hatimaye alitoa amri katika tangazo la jumla, “Hakuna ruhusa mtu yeyote kukaa na Abu Dharr, wala kusema naye.” (al-Masud).

Agizo la mtawala lilitakiwa kutekelezwa bila masharti. Mara tu tangazo hili lilipofanywa watu waliacha kuwasiliana naye na wakaacha kusema naye. Watu waliondoka popote pale Abu Dharr alipopita kuepuka wasije wakashtakiwa kwa khalifa. Hakuna mtu aliyemsikiliza Abu Dharr wala kufika mahali alipokuwa. Lakini Abudhar alikuwa mtu jasiri aliyoje. Hakujali mambo haya. Alikuwa anasadiki kwamba lolote alilofanya lilikuwa linalingana na Radhi ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, alikuwa anaridhika kabisa na yale aliyokuwa anayafanya na hakuna sharti lolote ambalo lingefaulu.

Subaiti anasema kwamba licha ya tangazo, Abu Dharr aliendelea kuwapa nasaha watu kama kawaida. Kwa bidii sana hivyo kwamba humo Madina watu wa ukoo wa Umayyah ambao walikuwa waunga mkono wa Uthman, walichoshwa naye na wakalalamika kwa Uthman, kwamba Abu Dharr alikuwa hajaacha kuhubiri. “Sasa ametuchosha sana, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na ufanywe mpango mwingine.”

Aliposikia hivi, Uthman aliamuru Abu Dharr apelekwe kwenye baraza lake.

Kwa amri ya Uthman watu wakamkamata Abu Dharr na kumpeleka kwa Uthman ambaye alisema, “Ewe Abu Dharr! Nimekuonya kwa kila njia lakini hutaki kuzingatia ushauri wangu. Nini kimekutokea?” Abu Dharr akajibu, “Laana iwe juu yako, ewe Uthman! Je, Mwenendo wako ni sawa na ule wa Mtukufu Mtume, au sawa na ule wa Abu Bakr bin Quhafa na Umar bin Khatab? Wewe unafanya mambo miongoni mwetu yale ambayo madhalimu hufanya.” Uthman akasema, “Sijui lolote. Toka nje ya jiji langu!”

Abu Dharr, “Mimi pia sitaki kukaa karibu na wewe. Sawa, niambie niondoke nielekee wapi?”

Uthman, “Nenda popote unapotaka lakini ondoka hapa!”
Abu Dharr, “Naweza kwenda Syria?”

Uthman, “Hapana, nimekuita na ukaburuzwa kutoka huko. Umewafanya watu wa Syria wanione mimi ni mkosaji kwao. Ninaweza kukupeleka huko tena?”
Abu Dharr, “Labda niende Iraq?”

Uthman; “Hapana, unataka kwenda ambako watu hawashutumu watawala wao?”
Abu Dharr, “Kama hivyo, niende Misri?” Uthman, “Hapana!”
Abu Dharr; “Niende Kufah?” Uthman, “Hapana.”
Abu Dharr, “Sasa niende wapi? Niende Makkah?” Uthman, “Hapana!”
Abu Dharr; “Ewe uthman! Hutaki mimi niende kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu! Kuna tatizo gani kwako endapo mimi ninakwenda huko na kumuabudu Mwenyezi Mungu hadi kifo changu?”

Uthman, “Hapana, kwa jina la Mwenyezi Mungu, kamwe!”
Abu Dharr, “Basi niambie niondoke niende wapi. Niende porini.”

Uthman, “Hapana”
Abu Dharr; “Basi nirudi kwenye siku zangu kabla ya Uislamu na niende kuishi Najd. Kwa vyovyote vile niambie mahali pa kwenda.”
Uthman, “Ewe Abu Dharr! Niambie ni sehemu gani unapenda zaidi zaidi.”
Abu Dharr, “Madina au Makkah au Jerusalem.”
Uthman, “Huwezi kuishi huko kwa vyovyote vile. Sasa niambie sehemu unayo ichukia kuliko zote.”

Abu Dharr, “Rabzah”
Uthman, “Vema, ninakuamuru uondoke uende Rabzah!”
Aliposikia hivi, Abu Dharr akasema; “Mwenyezi Mungu Mkubwa! Mtukufu Mtume alisema kweli kwamba yote haya yatatokea.” Uthman, “Mtume alisema nini?”

Abu Dharr, “Alisema Mtume kwamba, ningehamishwa kutoka Madina, ningezuiwa kwenda Makkah ningelazimishwa kuishi sehemu mbaya sana Rabzah ambapo ningeuawa na ningezikwa na kundi la watu wa Iraq ambao wangekuwa wanakwenda Hijaz.”

Aliposikia hivi Khalifa Uthman kwa mujibu wa Athan Kufi, alisema, “Nyanyuka ondoka kwenda Rabzah. Kaa huko na usiende popote.” Kwa mujibu wa Damah Sakibah Juz. 1, uk 194, aliteswa na kujeruhiwa sana. Halafu Khalifa akamuagiza Marwan ampeleke Rabzah akiwa amepanda ngamia asiye na tandiko la kukalia, na atangaze kwamba hakuna mtu atakaye ruhusiwa kumuona wakati anaondoka! (Murujudh Dhahab- Masud Juz. 1, uk. 438; Tarikh Yaqubi, Juz. 2, uk. 148; Tabaqati bin Sad, Juz. 4, uk 169. Hayat Qulubi, Juz. 2, uk. 1033; Majalisul Mumin, uk. 94, Tarikh Atham Kufi, uk. 131; Kitab al-Sufiyania, Abu Uthman Jahiz.

Haiwezekani kukanushwa kwamba kuhamishwa kwa lazima ni sawa na kuuawa. Wale wanaofukuzwa kutoka nchini kwao hupendelea zaidi kuuawa kuliko kuhamishwa. Matukio yanajieleza yenyewe kwamba watu waliofukuzwa kutoka kwenye nchi ya uzalendo wao kila mara walilia sana. Uzalendo ni zawadi ya viumbe vyote. Hadith zimeiita hali hiyo ni sehemu ya imani. Mtume Yusufu alikuwa na kawaida ya kulilia kwao alikozaliwa wakati ameketi kwenye kiti cha ufalme wa Misri.

Bila kutaja Mitume wengine, na tutafakari matukio ya Mtume Muhammad (s.aw). Alilazimika kuhama Makkah na kwenda Madina. Lakini kila alipokumbuka Makkah au alipowaona wakazi wa jiji hilo, macho yake yalijaa machozi. Loo! Abu Dharr alikuwa anafukuzwa kutoka kwenye mji wa nyumbani. Fikiria jinsi ambavyo alijihisi hususan alipokuwa anaondoka na kuacha kaburi la Mtume. Lakini hapakuwepo na uchaguzi wowote kwa sababu aliondolewa na kuhamishwa kwa mujibu wa mwandishi wa historia Tabari, ilikuwa ni utendaji wa Uthman kwamba alimfarikisha mtu kutoka watu, aliye kuwa kero kwake na alikuwa na kawaida ya kusema kwamba hakuna adhabu iliyokuwa kali kama hiyo. (Tarikh Tabari, Juz. 4, uk. 527).

Amri zilitolewa kwa ajili ya kuhamishwa kwa Abu Dharr na pia kwamba hakuna mtu aliyeruhusiwa kumuaga au hata kusema naye au kumtembelea.

Abdullah bin Abbas anasema kwamba Abu Dharr alipohamishwa Madina kwenda Rabzah tangazo lilitoka kwamba hakuna mtu aliyeruhusiwa kusema na Abu Dharr au kumuona anaondoka. (Saqifah Ahmad bin Abdul Aziz Janhari, Murujuz Zahab, Juz. 1, uk. 438; Sharh bin Hadid). Hili ni agizo ambalo lilifadhaisha watu na kuwazuia makwao. Hakuna mtu aliyeweza kuwa jasiri kutoka nje ya nyumba yake kwa madhumuni ya kumuona sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w) mwenye kuheshimiwa kama Abu Dharr isipokuwa Imamu Ali, Hasan, Husein, Aqil, Abdullah bin Jafar, Abdulah bin Abbas na Miqdadi bin al-Aswad.

Ingawa masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w) hawakuweza kutoa maoni yao dhidi ya agizo la Uthman kuhusu uhamisho wa Abu Dharr, bado walipata wasi wasi sana. Si tu masahaba waliokuwa pale ambao walisumbuliwa na tukio hili lakini pia wale ambao walikuwa nje ya Madina lakini walisikia habari ya kufukuzwa kwa Abu Dharr Madina.
Mathalan Abdullah bin Masud1 ambaye alikuwa Kufah na pia watu wa kabila lake walipatwa na fadhaa.

Abdullah bin Masud aliposikia habari hizi akiwa Kufah, alipata wasi wasi na akahutubia kundi la watu ndani ya msikiti wa Kufah, “Enyi watu! Mmewahi kuisikia Ayah hii? “Bado, ni nyinyi ndio mnao waua watu wenu, na mnawafukuza baadhi yao nje ya makazi yao.” Alipinga khalifa kwa kukariri ayah hii.

Walid, gavana wa Kufah alimtaarifu Khalifa Uthman kuhusu tukio hili. Khalifa alimjibu barua yake kwa kumuagiza ampeleke bin Masud kwake. Abdullah bin Masud alipofika Madina, Uthman alikuwa na hutubia. Alipomuona, Uthman alimuamuru mtumishi wake Aswad ampige bin Masud. Alimvuta na kumtoa nje ya msikiti na kumtupa chini na akamcharaza sana, akamzuia nyumbani mwake na akasitisha ruzuku yake kwa maisha yake yote. (Abu Dharr Ghifari, uk. 146, Musnad Ahmad bin Hanbal, Juz. 5, uk 197).

Lazima ieleweke kwamba Ali pia ameonesha masikitiko yake kuhusu kufukuzwa kwa Abu Dharr kwa maoni ya ‘Zammul Quraysh.” (Sahifah Alawiyah).

Kwa ufupi, kufuatana na agizo la Uthman, Marwan alimpeleka ngamia ambaye hakuwekewa tandiko la kukalia kwa lengo la kumsafirisha Abu Dharr kusiko julikana ambapo ghafla Ali, Hasan, Husein, Aqil, Ammar, Abdullah bin Jafar, Miqdadi bin al-Aswad na Abdullah bin Abbbad walifika hapo na kusema; “Wewe Marwan uliye laaniwa! Acha!
Usimkalishe kwenye ngamia. Lazima tumpe kwa heri.”

Halafu Imamu Ali akawaambia wanawe waagane na mjomba wao. Baada ya kusikia hivyo, Imamu Hassan akasema, “Ewe mpendwa wangu mjomba Abu Dharr! Mwenyezi Mungu na akuhurumie. Nyoyo zetu zinateseka. Usiwe na wasi wasi. Mwenyezi Mungu ndiye kiongozi wako na ni Yeye unatakiwa umweke mbele yako. Ewe Mjomba! Hakuna kitu kizuri kama uvumilivu. Mwamini Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye mpangaji wa mambo yako.”

Ammar alisema kwa hasira, “Mwenyezi Mungu na asimhurumie mtu ambaye amekupa taabu kubwa sana na ampe wasi wasi mtu ambaye anakusumbua. Ewe Abu Dharr, kwa jina la Mwenyezi Mungu, endapo ungeikumbatia dunia ya watafutaji wa dunia, hawangekufukuza na endapo angekuwa umekubali tabia yao, wangekufanya wewe rafiki yao. Uliposimama kidete kwenye imani yako, wapenda mambo ya dunia wamechoshwa na wewe. Usiwe na wasi wasi kwa sababu Mwenyezi Mungu yupo pamoja na wewe.

Watu hawa ni wale wenye bahati mbaya ambao mawazo yao yanatamani dunia na wamo kwenye hasara kubwa sana. Vivyo hivyo, watu wengine pia walisema na kumliwaza Abu Dharr kwa maneno tofauti.

Baada ya kusikia hotuba hizi Abu Dharr akalia sana na akasema, “Enyi Watu wa familia ya Mtukufu Mtume mlio neemeshwa! Nilipowaoneni, nilimkumbuka Mtukufu Mtume (s.a.w) na neema zikanizunguka. Enyi watu ninaowaenzi! Ni nyinyi peke yenu mlikuwa njia ya kupita faraja hapa Madina! Wakati wowote nilipowaoneni nilipata hali ya kuridhisha moyo wangu na utulivu wa akili yangu.

“Enyi wazee wangu! Kama ambavyo nilikuwa mzigo kwa Uthman hapa Hijaz, nilikuwa mzigo kwa Muawiyah huko Syria, kwa sababu anaye kaka yake wa kuchangia ziwa Abdallah bin Sarah kama gavana wa Misri, na mtoto wa kiume wa mama yake mdogo, Abdullah bin Amir kama Gavana wa Basra. Sasa ananipeleka mahali ambapo ni jangwa ambapo sina anayeniunga mkono mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, natambua kwamba ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye msaidizi wangu na kwa ajili Yake peke Yake sitajali upweke wa nyika.”

Kwa mujibu wa Allamah Subaiti, baada ya haya, Abu Dharr ambaye alikwisha kuwa mzee na dhaifu, alinyanyua mikono yake kuelekea mbinguni na akasema, “Ee Mwenyezi Mungu! uwe shahidi kwamba mimi ni rafiki yao Ahlul Bait na kila mara nitakuwa rafiki yao kwa ajili yako na kwa ajili ya Akhera, hata kama nitakatwa vipande kwa ajili ya mapenzi yangu kwa vitu hivi viwili.”

Baada ya haya Ali (a.s) akasema, “Ewe Abu Dharr! Mwenyezi Mungu na akuhurumie. Tunatambua sana kwamba sababu pekee ya wewe kufukuzwa kutoka sehemu moja na kupelekwa nyingine ni mapenzi yako kwetu, wazao wa Mtukufu Mtume (s.a.w).2

Hata hivyo, watu hawa mashuhuri waliporudi Madina baada ya kuagana na Abu Dharr kwa huzuni, Uthman alikasirika sana.
Atham Kufi ameandika, Abu Dharr alianza safari ya kwenda Rabzah na masahaba wengine na Ali wakarudi. Khalifa akaagiza Ali aende kwake na akamuuliza sababu ya kutoka nje ya Madina na kumuaga Abu Dharr na kwa nini alichukua kundi la masahaba kwenda naye, bila kujali amri yake. Ali alimuuliza Khalifa endapo ilikuwa wajibu kwake kufuata amri za Uthman hata pale ambapo zilipingana na utii kwa Mwenyezi Mungu na ukweli. Halafu akaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba kamwe hangefanya hivyo.” (Tarikh Atham Kufi, uk. 131, chapa Delhi).

  • 1. Allamah Subaiti anasema kwamba masahaba wa Mtume walionesha kukasirika kwao kwa sababu ya kufukuzwa Abu Dharr kutoka Madina na kupelekwa Rabzah. Kwa mujibu wa Mustadirak wa Hakim, Abu Darda aliposikia habari za kufukuzwa kwake alisema kwa mshangao, “Inna Lillahi wa inna illahe rajiun!” (Sisi tumetoka kwa Mwenyezi Mungu na tutarudi Kwake) Alirudia maneno haya mara kumi Ali akasema; “Ewe Abu Dharr! Usiwe na wasi wasi. Watu walikuogopa kwa sababu ya tamaa ya mambo ya dunia, na wewe hukuwaogopa kwa sababu ya imani yako hadi wakati walipofukuza. Abu Dharr! Mchamungu hupatwa na kila aina ya matatizo, lakini kumbuka kwamba Mwenyezi Mungu ni stadi wa kutengeneza njia za ajabu za ukombozi kwa wacha mungu. Hakuna kitu kinachoweza kukupatia maliwazo isipokuwa ‘ukweli’. Ukweli’ ndio utakao kuwa sahaba wako huko kwenye upweke. Najua kwamba wewe unaweza kupata mshtuko wa hofu kutokana na uwongo na hali hiyo haiwezi kuja karibu na wewe.
  • 2. Abu Dharr alitambua kwamba kuwapenda Ahlul Bait ndio msingi wa Uislamu. Kwa mujibu wa Jazairi, Imamu Jafar al-Sadiq amemnukuu Mtukufu Mtume akisema, "Kama ambavyo kila kinacho msingi, msingi wa Uislamu ni kutupenda sisi, Ahlul -Bait (Anwar Nomaniah

Sura Ya Ishirini

Abu Dharr alikuwa anaona siku zinapita akiwa Rabzah katika hali ya upekee na upweke. Hapakuwepo na mtu wa kumtunza na kujua hali yake. Alikuwa hana njia ya kufarijika. Kama familia yake ingekuwepo naye, hangehisi uchungu wa upweke kiasi hicho. Familia yake ilikua bado ipo Syria na Abu Dharr akafukuzwa na kupelekwa Madina na halafu akafukuzwa kupelekwa Rabzah.

Abdul Hamid Jaudatus Sihar ameandika kwamba Muawiyah alipopata taarifa kwamba Uthman amemfukuza Abu Dharr na kumpeleka Rabzah, akamsafirisha mkewe na (wengineo) kwenda huko. Mke wa Abu Dharr alipotoka nje ya nyumba yake, alikuwa na sanduku tu. Muawiyah akawaambia watu, “Tazameni vitu anavyo miliki mhubiri wa maadili.” Baada ya kusikia hivi mke wa Abu Dharr akasema, Ndani ya begi hili zipo sarafu chache na si dinari na hizo pia zinatosha kwa matumizi tu.” Mkewe alipofika Rabzah aliona kwamba Abu Dharr alikwisha jenga msikiti.

Waandishi wa historia wengi wameandika kuhusu Abu Dharr kujenga msikiti huko Rabzah. Tunaona kutajwa kwa msikiti huo kwenye vitabu vya Tabari bin Athir na bin Khaldun. Kwenye nakala ya Kiarabu ya Tabari ipo sentensi isomekayo, ‘Abu Dharr alikuwa ameweka alama za msikiti, na mahali hapo ndipo ambapo alikuwa akisali, kama vile ilivyo leo, watu hukusanya udongo porini na kuuita msikiti, wala haingewezekana yeye kujenga msikiti kama wa siku hizi. Kwa mujibu wa Abdul Hamid, siku za Hija watu walipopita Rabzah walisali kwenye msikiti wa Abu Dharr.

Maana yake ni kwamba, sehemu hiyo haikuwa na watu. Endapo pangekuwepo na watu, ingeandikwa kwenye msikiti huo, kama vile ambavyo imetamkwa kwamba mahujaji walikuwa wanaswali kwenye msikiti huo.

Allamah Subaiti ameandika kwamba Abu Dharr alikuwa katika hali ya upweke na alikuwa akipitisha siku zake Rabzah katika hali ambayo hakuna binadamu angeonekana hapo isipokuwa mara chache ambapo mpita njia alipita hapo. Hapakuwepo sehemu yoyote ambapo angejihifadhi. Aliishi chini ya mti. Hapakuwepo na mpango wowote wa chakula chake, palikuwepo na majani yenye sumu sehemu yote iliyozunguka hapo na hayo ndio yaliyo sababisha kifo chake na cha mkewe.” (Abu Dharr al-Ghifari, uk. 165, chapa Najaf, 1364 A.H).

Baada ya hapo, mwandishi anaongeza kwamba, sababu ya kumpeleka Abu Dharr mahali kama hapo ilikuwa kusitishwa hotuba zake, ili pasiwepo na mtu wa kumsikia kwani alikuwa na ucheshi kwenye ulimi wake. Wakati wote aliposema, alisema ukweli, ambao ulitikisa misingi ya serikali.

Kwa ufupi, Abu Dharr alikuwa anaishi maisha yake na familia yake katika hali ya dhiki sana. Hapakuwepo na mtu wa kumliwaza huko.

Lakini wale watu waaminifu ambao walikua wanampenda na kumheshimu katika nyoyo zao walikuwa na desturi ya kwenda kumuona.

Kwa mujibu wa mwandishi wa historia, Waqidi, Abul Aswal Duayli anasema; “Nilikuwa nataka kumtembelea Abu Dharr kwa moyo wangu wote na kumuuliza kwa nini alifukuzwa. Kwa hiyo, nilikwenda kwake Rabzah na nikamuuuliza kama aliondoka Madina kwa chaguo lake mwenyewe au alifukuzwa kwa lazima. Akasema; “Ndugu yangu! Namna ya kukuambia kwamba nilipopelekwa Syria nilidhani kwamba nimekwenda mahali ambapo ni muhimu kwa Waislamu.

“Nilifurahi kuwa kule, lakini sikuruhusiwa kukaa huko na nikaitwa tena Madina. Nilipofika huko nilijiliwaza mwenyewe kwa fikra kwamba hiyo ilikwua ni sehemu ambayo ilikuwa nimehamia na ambapo nilipata heshima ya usahaba wa Mtukufu Mtume. Lakini, loo, pia nilifukuzwa kutoka hapo na nipo hapa unaponiona.” Baada ya hapo akasema, “Ewe Abul Aswad! Sikiliza, nikuambie. Siku moja nilikuwa nimelala kwenye msikiti wa Mtume.

Kwa bahati tu Mtukufu Mtume aliingia msikitini. Akaniamsha na akasema, “Ewe Abu Dharr! Kwa nini unalala msikitini?”

Abu Dharr, “Usingizi ulinizidi na ghafla nikalala.
Mtume, “Niambie utafanya nini utakapofukuzwa kwenye msikiti huu?

Abu Dharr, “Nitakwenda Syria, kwa sababu zipo ishara za Uislamu, huko. Pia sehemu hiyo ni mahali pa Jihadi.

Mtume, “Utafanya nini utakapofukuzwa huko pia?”

Abu Dharr, Wakati huo nitachomoa upanga wangu na kumuua mtu atakaye nifukuza.”

Mtume, “Ninakupa ushauri mzuri sana.” Abu Dharr, “Ushauri gani huo?”

Mtume, “Toa ruhusa ya kuburuzwa utakapoburuzwa, na kwamba ukubali kila unaloambiwa, na usipigane.

Ewe Abul Aswad! Kufuatana na ushauri wa Mtume, nilisikiliza nilivyoambiwa nao na nikakubali yale waliyoyasema. Bado ninaendelea kusikiliza wanayoyasema. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Atalipa kisasi kwa Uthman kwa yale ambayo amenifanyia na atathibitishwa kuwa mtenda dhambi mbaya kuzidi, kuhusu hili tatizo langu atakapofika kwenye mahakama ya Mwenyezi Mungu.”

(Sharh bin Abil Hadid, Juz. 1, uk 214; Murujuz Zahab Musudi, Juz. 1, uk. 238; Tarikh Yaqubi, Juz. 2, uk 148, Mustadirak Hakim, Juz. 3, uk. 343; Hulyah Abu Naima, Juz. 1, uk 162; Tabaqatul Kubra bin Sad, Juz. 1, uk. 166; Musnad Ahmad, Juz. 5, uk 156 na 180; Sunan Abi Daudi, Juz. 3, uk 213; Umdatul Qari Sharh Sahih Bukhari 8, Juz. 4, uk 291).

Wasimuliaji wa hadithi hii ya kuaminika ni watu wa kuaminika sana na kutegemewea kama ilivyo andikwa na Allamah Amini kwenye kitabu chake ‘al-ghadir.’

Mtu alimuuliza Abu Dharr wakati alipokuwa anaishi Rabzah, “ewe Abu Dharr unao utajiri wowote?” Akasema, “Utajiri wangu ni matendo yangu.”
Pia akasema, Ninaposema utajiri nina maana utajiri huu wa hapa duniani na ninataka kujua endapo unao utajiri wa kidunia au hapana.” Abu Dharr akasema; “Kamwe sijawahi kuwa na utajiri wa kidunia hata kwa siku moja au usiku moja nikiwa na hazina au tajiri wa kidunia na mimi. Nimesikia kutoka kwa Mtukufu Mtume kwamba utajiri wa mtu ni kaburi yaani utajiri wa kidunia haufai lolote, lakini mwenendo wa mtu lazima uwe mzuri kwa sababu utamtumikia kila mahali hususan Kaburini. Utajiri wa dunia hubaki duniani, na tabia njema hukunufaisha wewe huko Peponi.” (Hayatul Qulubi, Juz. 2, uk. 1046).

Allamah Majlis akimnukuu Shaykh Mufid anasimulia kutoka kwa Abu Ammah Bahili1 kwamba Abu Dharr baada ya kufika Rabzah alimuandikia mambo ya hatari yaliyo mpata Huzayfah bin al-Yaman,2 sahaba wa Mtukufu Mtume ambaye labda alikuwa Kufah. Kwenye barua hiyo, ametoa, ushauri wa aina mbali mbali na akaeleza kuhusu shida zake na matatizo yake. Ameandika’ Nuorullah Shustari kwamba wakati moja Huzayfah alimtembelea Abdullah bin Umar ambaye hakumheshimu. Wakati huo Huzayfah alimwambia kwamba wale ambao walikuwa bora zaidi yeye (bin Umar) walimhesabu kama mnafiki. Tukio la Uqbah lilitokea wakati watu wanarudi kutoka Vita ya Tabuk. Ali hakuwa na Mtume. Hatamu ya ngamia wa Mtume ilishikwa na Huzayfah na Ammar alikuwa anamwendesha ngamia. Ngamia alipofika kwenye mpasuko wa hatari baadhi ya wanafiki walijaribu kumuua Mtume kwa kumuogofya ngamia. Lakini aliokolewea na ujanja wa Ammar na Huzayfah. Huzayfah alikwenda kuishi Kufah siku arobaini baada ya kutoa kiapo cha uaminifu kwa Ali. Alikuwa anamuunga mkono kwa uaminifu. (Majalisul Monimi).

“Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu. Mpendwa Huzaifah, Ninakuandikia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu kwamba kilio chako kimechupa mipaka. Ewe ndugu! Ikatae dunia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Usilale usiku kucha, ukeshe unamuabudu Mwenyezi Mungu na uweke mwili wako na roho yako katika taabu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Haya ni mambo yafaayo kufanya.

“Ewe Ndugu! Ni muhimu kwa mtu akatambua kwamba mtu ambaye amekasirikiwa na Mwenyezi Mungu atadumu Jahanamu, ili uondokane na starehe za dunia, kesho usiku kesha katika kumuabudu Yeye na uteseke kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Ewe Ndugu! Ni muhimu kwa mtu anaye tambua kwamba furaha ya Mwenyezi Mungu ni ujumbe kuishi Peponi, kujaribu kutafuta radhi Yake mfululizo ili upatikane ukombozi na kufuzu.

“Ewe Ndugu! Mtu asijali kufarakana na familia yake kwa ajili ya radhi ya Mwenyezi Mungu. Ni radhi ya Mwenyezi Mungu tu ndio usalama wa Peponi. Endapo Mwenyezi Mungu anaridhika mambo yetu yote yatatimia na Pepo itakubalika. Lakini, endapo Mwenyezi Mungu haridhiki ni vigumu sisi kuwa na mwisho wenye furaha.

“Ewe Ndugu yangu! Mtu anayetaka kuwa pamoja na Mtume na watakatifu huko Peponi, lazima abadili maisha kama ambavyo nimefanya na kama ambavyo nimesema hapo juu. Ewe Hudhayfah! Wewe ni mmojawapo wa watu ambao ninao furaha kuwaelezea kuhusu machungu na mateso yangu. Kwa kweli mimi ninajiliwaza kwa kukutaarifu wewe yale yanayonipata au yaliyonipata.

“Ewe Hudhayfah! Nimeona dhuluma ya madhalimu kwa macho yangu, na nimesikia maneno yao ya kuchukiza kwa masikio yangu. Kwa hiyo, ninalazimika kutoa maoni yangu kuhusu mazungumzo hayo karaha na kuwaambia wao kwamba vyovyote walivyo kuwa wanafanya haikuwa sahihi kabisa. Nilifanya kwa kutimiza wajibu na kwa hiyo watu hao dhalimu wakaninyang’anya haki zangu zote. Wakanifukuza kutoka jiji hadi jiji na kuniswaga kutoka sehemu hadi sehemu na wakaniweka mbali na ndugu na jamaa zangu. Ewe Hudhayfa! Walisababisha vurugu kubwa na baya zaidi kuliko yote, walinizuia hata kwenda kutembelea kaburi la Mtume.

“Ewe Hudhayfa! Ninakuelezea kuhusu mateso yangu, lakini nina hofu isije maelezo yangu haya yakageuka kuwa malalamiko dhidi ya Mwenyezi Mungu. Hudhayfah! Ninakubali kwamba uamuzi wowote wa Mola wangu Mlezi na Muumbaji atakao ufanya kuhusu mimi ni sawa. Ninainamisha kichwa changu mbele ya amri Yake. Maisha yangu na yawe mhanga katika njia Yake. Ninatamani kupata radhi Yake. Ninayoandika yote haya kwako ili uniombee na Waislamu wanaojitolea kwa Mwenyezi Mungu. Amani iwe kwako.” Abu Dharr.

Haijulikani Abu Dharr alipelekaje barua hii kwa Huzayfah bin al-Yamah. Huzayfah aliposoma barua hii macho yake yalijaa machozi. Akazikumbuka hadith za Mtume (s.a.w) kuhusu Abu Dharr. Kilichomshangaza yeye zaidi ni kufukuzwa kwa Abu Dharr na kupelekwa kwenye upweke. Alishika kalamu kwa uchungu mwingi na akaandika jibu la barua hii:

“Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye kuneemesha.

Mpendwa wangu Abu Dharr,

Niliipokea barua yako na nikajua yanayokusibu. Umeniogofya kuhusu kurudi kwangu siku ya Hukumu na umeshawishi nifanye mambo fulani, kwa ajili ya kujitengeneza na kujiboresha mimi mwenyewe.

“Ewe ndugu! Wewe umekuwa ukinitakia mema mimi na Waislamu wote kila mara na umekuwa na huruma na mwema kwa wote. Kila mara ulikuwa na shauku ya ustawi wa wote. Kila mara uliwaonesha watu njia ya uadilifu na ukakataza wasifanye uovu. Mambo kama yalivyo, uongozi ni haki ya pekee ya Mwenyezi Mungu. Humwokoa amtakaye na ukombozi unategemea radhi Yake. Ninamuomba Mwenyezi Mungu Atoe msamaha kwa jumla na neema nyingi kwangu, kwa wateule na watu wa kawaida wa umma wote.
“Ninafahamu hayo mambo ya kushangaza, ambayo umeyataja kwenye barua yako, ni kwamba, ule uhamisho wako wa kufukuzwa kutoka mji wa nyumbani kwako na kuachwa kwenye nchi ya kigeni bila marafiki na wanao kuunga mkono, na kule kutupwa nje ya nyumba yako.

“Ewe Abu Dharr! habari kuhusu mateso yako zimevunja moyo wangu kabisa kabisa na mateso ambayo unayapata sasa yanasikitisha sana. Lakini ninasikitika kusema kwamba siwezi kufanya lolote nikiwa hapa. Kama ingekuwa inawezekana kununua mabalaa yako yote kwa fedha yangu yote, ningefanya hivyo. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, kama ingewezekana ningejitolea kila kitu changu kwa ajili yako. Ewe Abu Dharr! Umo katika dhiki na siwezi kufanya lolote.

“Kwa jina la Mwenyezi Mungu kama ingekuwa inawezekana mimi na wewe kugawana matatizo yako hakika ningefanya hivyo. Nina hisi uchungu ulioje kwamba siwezi kukutana na wewe. Ni vigumu kufika pale ulipo. Endapo watu hawa katili wakinifanya mimi mshirika sawa na wewe katika matatizo yako, nipo tayari kuchukua matatizo yako. Lakini, loo, haiwezekani iwe hivyo.

“Ewe Abu Dharr! Usiwe na wasi wasi. Mwenyezi Mungu ndiye anayekuunga mkono. Anayaona mambo haya yote. Ndugu! Ni muhimu kwetu sisi, mimi na wewe, kumwomba Mwenyezi Mungu na tumsihi Yeye ili atuzawadie thawabu nyingi na atuokoe kutoka kwenye adhabu. Ewe ndugu! Muda unakaribia sana ambapo mimi na wewe tutaitwa mbele ya Mwenyezi Mungu na tutaondoka kuelekea huko hivi karibuni. Ewe Ndugu! Usiwe na wasi wasi kwa matatizo ambayo umekuwa unayapata na usistaajabu. Mwombe Mwenyezi Mungu akupatie malipo yake.

“Ewe ndugu! Ninafikiria kifo ni bora zaidi kwetu sisi kuliko kuishi hapa. Sasa ni muhimu sisi kuiacha dunia hii ya kupita kwa sababu baada ya muda si mrefu ghasia3 zitatokea kwa mfuatano moja baada ya nyingine. Ghasia hizi zitaendelea kuongezeka na zitawagandamiza watu waadilifu wa dunia. Panga zitachomolewa kwenye vurugu hizi na kifo kitawazunguka watu pande zote. Yeyote ambaye atanyanyua kichwa chake kwenye vurugu hizi hakika atauawa.

“Ewe Abu Dharr! Ninakuombea wewe wakati wote. Mwenyezi Mungu na atuweke chini ya huruma Yake na atulinde tusiwe na kiburi wakati wa ibada. Mpangaji mkubwa wa mambo yetu. Siku zote sisi hutegemea ukarimu Wake. Amani iwe kwako.” Hudhayfah

(Shifa’us Sudur, Abu Dharr Gihfari, uk. 105 al-Fusul kilichoandikwa na Murtaza Alamul Huda).

Wasomi wanasema kwamba Abu Dharr aliishi na familia yake huko Rabzah ambapo ghafla mtoto wake wa kiume, Dhar aliugua. Hapakuwepo na daktari wa kumwendea huko jangwani kwa ajili ya tiba isipokuwa kumwamini Mwenyezi Mungu. Hatimaye maradhi yalizidi hadi wakati wake wa kufa ulikaribia. Mama mwenye huzuni alinyanyua kichwa cha mwanae kutoka kwenye mchanga na kukiweka juu ya goti lake.
Dhar alifariki. Mama na dada yake Dhar walianza kulia. Abu Dharr alishtuka sana lakini imani yake kwa Mwenyezi Mungu ilimliwaza. Alijizuia na hakulia. Kwa kuwa ilikuwa jangwa hapakuwepo na matayarisho kwa ajili ya mazishi.

Historia haituambii Abu Dharr alivyomzika mwanae, lakini inajulikana kutoka kwa chanzo cha kuaminika alichofanya baada ya hisia zake kwa maneno muhadithi Yaqubi Kulayni ameandika; “Wakati mtoto wa kiume wa Abu Dharr, Dhar alipokufa Abu Dharr aliweka mkono wake juu ya kaburi lake na akasema; “Ewe mwanangu! Mwenyezi Mungu na akuhurumie. Ulikuwa mtoto anaye jiweza sana. Umekufa wakati mimi nina furaha na wewe. Utambue kwamba, kwa jina la Mwenyezi Mungu, sikupata hasara yoyote kutokana na kifo chako na simhitaji mwingine yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu.

“Ewe mwanangu! Endapo hapangekuwepo na kufikiria mshtuko baada ya kifo ningefurahi kutamani kuchukua nafasi yako kaburini. Lakini sasa kwa kuwa mimi ninaomboleza kifo chako, hutaomboleza kifo changu. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sikulia kwa ajili ya kifo chako lakini mateso yako ndio yamenifanya nilie. Natamani ningejua nini ulichoulizwa na majibu yako. Ee Mwenyezi Mungu! Nimesamehe haki zangu ambazo nilikuwa ninamdai. Ee mstawishaji wangu! Ninakuomba umsamehe haki zozote ambazo ulikuwa unamdai. Mola wangu Mlezi! Wewe ni msamehevu zaidi kuliko mimi.” (Usudul Kafi).

Shaykh Abbas Qummi ameandika kwenye kitabu chake Safinatul Bahar Juzuu ya 1, ukurasa wa 438 kwamba maneno yaliyotamkwa na Abu Dharr juu ya kaburi la mwanae Dhar, pia yalitamkwa na Imamu Jafar Sadiq juu ya kaburi la mwanane Ismail.

Abu Dharr alikuwa hajasahau kifo cha mwanae kijana ambapo mke wake pia alipatwa na mauti na hakumuona tena hadi milele.

Kwa mujibu wa Allamah Abdul Hamid, Abu Dharr na watu wa familia yake walikuwa wanaishi katika hali ambayo haikuwa na mpango unaostahili kuhusu chakula isipokuwa walikuwa wanapata kipande kidogo cha nyama ya ngamia aliyechinjwa kwa ajili ya maafisa wa serikali. (Tabari, Juz. 5, uk. 67). Kwa kawaida walikula majani kama chakula chao kikuu au vitu vingine kipindi hicho. Siku moja mke wa Abu Dharr alikula majani yenye sumu ambayo yalisababisha apate maradhi ya hatari na alifariki dunia. (Hayatul Qulubi, Juz. 2, uk. 1049) Abu Dharr naye akaugua.

Baada ya kifo cha mke wake, Abu Dharr alihisi kuwa mpweke mno. Alibaki yeye na mwanae wa kike. Watu waliokuwa wanaishi Rabzah walipojua kuugua kwa Abu Dharr, baadhi yao walimtembelea na kumtaka hali. Kwa mujibu wa usemi wa mtoto wa kike wa Abu Dharr, watu hao walimwambia; “Ewe Abu Dharr!Unaumwa na nini na unalalamika kuhusu nini?”

Abu Dharr akajibu; “Nina malalamiko kuhusu dhambi zangu.” Watu hao wakasema, “Unatamani kitu chochote?” Akasema, “Ndio natamani huruma za Mwenyezi Mungu” Wakasema, “Kama unataka tunaweza kumwita daktari wa tiba.” Akasema, “Mwenyezi Mungu ndiye mganga wa uhakika. Maradhi na tiba yake vyote vimo kwenye uwezo Wake. Mimi sihitaji mganga wa tiba.” (Hayatul Qulubi) Alikuwa na uhakika wa kifo chake.

Majlis, kwa mamlaka ya Sayyid bin Taus, amemnukuu Muawiyah bin Thalabah anasema: Hali ya Abu Dharr ilipozidi kuwa mbaya huko Rabzah na tukapata taarifa, tuliondoka Madina kwenda Rabzah kwa lengo la kumuona yeye. Baada ya kuulizia kuhusu hali yake tulimsihi atengeneze wasia wake.

Akasema kwamba alikwisha tayarisha wasia wake, vyovyote itakavyo kuwa, mbele ya Amiri wa Waumini.

Tukauliza, “Kwa Amiri wa Waumini unamaanisha Khalifa Uthman?” Akasema, “Kamwe! Kwa Amiri wa Waumini maana yake ni kwamba yule ambaye ndiye anayestahili kuwa Amiri wa Waumini. Ewe bin Thalabah! Nisikilize! Abi Turab, (Baba wa Ardhi) Ali ndiye yeye ambaye ni maua ya dunia. Yeye ni msomi wa dini wa umma huu. Sikiliza! Utaona mambo mengi ya kuchukiza sana hapa duniani baada ya kifo chake.” Nikasema; “Ewe Abu Dhar! Tunaona kwamba unafanya urafiki na watu ambao Mtume aliwapenda.”

Sasa tunataka kusema kitu kuhusu mahali, Rabzar ambapo Abu Dharr alizuiliwa na hakuruhusiwa kuvuka mipaka yake.

Wasomi na waandishi wa historia wanakubaliana kwamba Rabzah ipo umbali wa maili tatu kutoka Madina karibu na Zate Araq kufuata njia ya kuelekea Hijaz na wakati huo huo haikuwa zaidi ya sehemu iliyotekelezwa na pweke maoni ukurasa wa 17 wa Juz. 2, ya Nahjul Balagha kwamba Rabzah ni sehemu iliopo karibu na Madina ambapo kaburi la Abu Dharr lipo. Bin Abil Hadid anasema kwamba Kufukuzwa kwa Abu Dharr na kupelekwa Rabzah ilikuwa sababu moja wapo ambayo iliwachochea Waislamu kumuasi Uthman.

Hapana shaka kwamba Abu Dharr alipata daraja la juu zaidi la imani. Alizingatia hadi dakika za mwisho za uhai wake kwamba aliapa kwa Mtume kusema kweli na bila kujali shutuma yoyote kwa ajili ya ukweli. Shah Walyullah Dehlavi ameandika kwamba katika utekelezaji kwa Mtume (s.a.w) ni kwamba alichukua viapo vya uaminifu vya aina mbali mbali kutoka kwa watu mbali mbali yaani kwenda Jihad, kukataa bidaa, kuanzisha sheria za Kiislamu, na kusema kweli. (Shifau alil).

Kiapo alichochukua kutoka kwa Abu Dharr ni kusema kweli. Abu Dharr alifanya kwa mujibu wa kiapo cha uaminifu baada ya kutambua vema maana yake na kwamba asingefanya hivyo, ambapo alikwisha sadiki sana hali ambayo iliondoa shaka kwake, kwamba chochote alichofanya kililingana na Ridhaa ya Mwenyezi Mungu na nia ya Mtukufu Mtume (s.a.w) (Futunatul Makkiyah bin Arabi, Sura ya 269).

Kuhusiana na hilo, kamwe hakujali nguvu za serikali wala kuogopa kupata matatizo. Alistahamili kila aina ya ukandamizaji na alibeba kila aina ya usumbufu lakini hakuacha kusema kweli, hadi akafukuzwa na kupelekwa uhamishoni mara mbili. Uhamisho wa Abu Dharr wa mara ya mwisho hauna mfano wake.

Alijitolea mhanga kwa kuzuiliwa kwenye jangwa ambalo ni pweke. Bila kuzungumzia habari za nyumba ya kuishi, alifanya kivuli cha mti kuwa makazi yake. Hakuwa na mpango wowote wa chakula na makazi ambapo angepumzika au kulala. Lakini kwa ujasiri wake wa hali ya juu na azima aliokuwa nayo, Abu Dharr aliyachukua matatizo yote kwa uchangamfu kwa sababu ya kumridhisha Mwenyezi Mungu. Mke na mtoto wake wa kiume walipokufa sasa muda ulikaribia ambapo alikuwa anangojea kifo chake mwenye we akiwa kwenye sehemu pweke kama hiyo akiwa na mtoto wake wa kike tu.

Loo! Siku ya mwisho ya uhai wa Abu Dharr kwenye sehemu hiyo pweke ilikaribia. Alikuwa anasali mara nyingi na binti yake alikuwa na wasi wasi na shauku kuhusu hali ya baba yake na mwisho wake uliokuwa unakaribia. Hapakuwepo na mtu. Hapakuwepo na hata mnyama. Muda wa kuwasili malaika wa kifo ulikaribia.

Muda ambao binadamu hulia na mtoto wa kike kunyang’anywa mapenzi ya baba yake.

Si tu kwamba alikuwa anaangalia kwa makini kwa kutokuwa na msaada kwa baba yake ambaye mapenzi yake yalisababisha mshtuko mara kwa mara.4

Hapa tunatoa maelezo ya historia ya hatari ya kifo cha Abu Dharr kama ilivyosimuliwa na binti yake kama ilivyoandikwa na Majlisi. Binti huyu anasema; “Siku zetu zilipita katika mateso yasiyo elezeka kwenye upweke. “Siku moja ilitokea kwamba hatukuweza kupata chochote chakula. Tulijitahidi kutafuta lakini hatukufanikiwa. Baba yangu aliyekuwa taabani akaniambia, “Binti yangu kwa nini una wasi wasi sana leo?”

Nikasema, “Baba, mimi nina njaa sana na wewe unazidi kudhoofika pia kwa sababu ya njaa. Nimejaribu kujitahidi kila nilivyoweza kupata chakula ili niweze kuhisi ninaheshimika kwako lakini sikufanikiwa.” Abu Dharr akasema, “Usiwe na wasi wasi. Mwenyezi Mungu ndiye mpangaji mkuu wa mambo yetu.” Mimi nikasema, “Baba! Ni sawa lakini hakuna kitu chochote sasa ambacho kinaweza kukidhi mahitaji yetu.”

Akasema; “Binti yangu! Nishike bega langu na unipeleke hapa na pale. Labda tunaweza tukapata chochote huko.” Nilimshika mkono wake na tukaanza kwenda kuelekea upande alikonielekeza. Wakati tupo njiani baba yangu aliniambia nimkalishe chini. Nikamketisha kwenye mchanga wenye joto. Akakusanya mchanga na akalaza kichwa chake juu ya mchanga huo.

Mara tu alipolala chini, macho yakaanza kuzunguka na akahisi uchungu wa kifo. Nilipoona hivi nikaanza kulia kwa sauti kubwa sana. Akajikaza kidogo na akasema, “Kwa nini unalia, binti yangu?” Nikasema, “Nitafanya nini baba yangu? Hapa ni jangwa na hakuna mtu yeyote. Sina sanda ya kukuvesha na pia hakuna mtu wa kuchimba kaburi hapa. Nitafanya nini mauti yakikufika hapa kwenye sehemu hii pweke.”

Akalia baada ya kuona jinsi nilivyokuwa sina jinsi ya kuwa na msaada wowote na akasema, “Binti yangu! Usiwe na wasi wasi. Huyo rafiki yangu ambaye kwa ajili ya kumpenda yeye na watoto wake ninavumilia matatizo yote haya, aliniambia kuhusu tukio hili mapema, Sikiliza, Ewe bint yangu mpendwa, alisema mbele ya kundi la masahaba wake wakati wa Vita ya Tabuk kwamba mmojawao angekufa lakini jangwani na kundi la masahaba wangekwenda kwenye maziko na mazishi yake.

“Sasa hakuna hata mmoja wao aliyehai isipokuwa mimi. Wote wamekufa wakiwa kwenye sehemu zenye watu. Ni mimi tu niliye baki na pia nipo kwenye upweke wa pekee.

Kamwe sijapata kuona jangwa la aina hii ambapo nimelala sasa na mwenye uchungu wa kifo. Binti yangu mpendwa! Nikifa nifunike joho langu na ukae kwenye njia inayoelekea Iraq. Kundi la watu waumini watapita hapo. Waambie kwamba Abu Dharr sahaba wa Mtume (s.a.w) amekufa. Kwa hiyo tafadhalini tayarisheni mazishi yake.”

Alikuwa anazungumza na mimi wakati malaika wa kifo alipofika na kumtazama uso wake. Baba yangu alipomtazama uso wake ukawa mwekundu na akasema, “Ewe Malaika wa Kifo! Umekuwa wapi hadi sasa? Nimekuwa ninakungojea wewe. Ewe rafiki yangu! Umekuja wakati ambapo mimi ninakuhitaji sana. Ewe Malaika wa kifo! Na asiokolewe mtu asiyefurahi kuonana na wewe. Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nichukue haraka sana na unipeleke kwa Mwenyezi Mungu mwenye Huruma sana ili niweze kupumzika na matatizo ya dunia hii.”

Baada ya hapo alimwambia Mwenyezi Mungu, “Ee Msitawishaji wangu! Ninaapa Kwako Wewe, na Unajua kwamba ninasema kweli kwamba kamwe sikuchukia kifo na kila mara nilitamani kukutana na wewe.”

Baada ya hapo jasho la kifo likatoka kwenye uso wa baba yangu na aliponitazama, aligeuza uso wake na kuiaga dunia daima milele. Sisi tunatoka kwa Mwenyezi Mungu na Kwake tutarejea.”5

Binti yake Abu Dharr aliendelea, “Baba yangu alipokufa nilianza kulia huku ninakimbia kuelekea kwenye njia inayoelekea Iraq. Nilikuwa nimeketi pale nikangojea kundi la watu linalokuja. Ghafla nilikumbuka kwamba maiti ya baba yangu ilikuwa haina mtu wa kuiangalia. Kwa hiyo, nilikimbia hadi ilipokuwa maiti. Tena nikarudi kwenye njia isije kundi likapita bila kulitaarifu. Kwa hiyo, ikawa ninakwenda kwenye maiti na kurudi njiani, mara kadhaa.

Sasa, ghafla nikawaona watu wanakuja wakiwa wamepanda ngamia. Walipokaribia, nikawaendea huku nikilia na kutokwa na machozi na nikawaambia; “Enyi masahaba wa Mtume! Sahaba wa Mtume amekufa.” Wakaniuliza sahaba huyo ni nani?” Nikajibu; “Baba yangu, Abu Dharr Ghifari.”

Mara waliposikia waliteremka kutoka kwenye ngamia na wakafuatana na mimi huku wakilia. Walipofika hapo wakalia sana kuhusu kifo chake cha kuhuzunisha na wakashughulikia ibada ya mazishi yake.

Mwandishi wa historia Atham Kufi, amesema kwamba kundi la watu waliokuwa wanakwenda Iraq, alikuwepo; Ahnaf bin Qays, Tamimi, Sasaah bin Sauhan al-Abdi, Kharijah bin Salat Tamimi, Abdulah bin Muslimah Tamimi, Halal bin Malik Nazle,
Jarir bin Abdullah bajali, Malik bin Ashtar bin Harith na wengineo. Watu hawa walimkosha Abu Dharr na wakafanya mpango wa kumvisha sanda. Baada ya mazishi Malik bin Ashtar alisimama pembeni mwa kaburi na akatoa hutuba ambapo ilirejea mambo ya Abu Dharr na kumwombea yeye. Baada ya kumsifu Mwenyezi Mungu Mweza wa yote akasema”

“Ee Mwenyezi Mungu! Abu Dharr alikuwa sahaba wa Mtume Wako na muumini wa Vitabu Vyako na Mitume Wako. Alipigana kishujaa sana katika njia Yako, alikuwa, mfuasi imara wa sheria Zako za Kiislamu na kamwe hakubadilisha au kugeuza amri yoyote miongoni mwa amri Zako.

“Ee Mola wangu Mlezi! Alipoona ukinzani unafanywa dhidi ya Kitabu na Sunna akapiga kelele na kuwatahadharisha wahusika kwa umma ili wajirekebishe, matokeo yake wakamtesa, wakamhamisha kutoka sehemu moja hadi nyingine, wakamfedhehesha, wakamhamisha kutoka katika nchi ya Mtume Wako mpendwa na kumweka kwenye matatizo makubwa sana, hatimaye amekufa akiwa katika hali ya upweke kabisa sehemu ambayo hawaishi watu.

“Ee Mwenyezi Mungu! Mpe Abu Dharr sehemu kubwa ya hizo neema za mbinguni ambazo Umewaahidi waaminio na umlipe kisasi yule ambaye amemfukuza kutoka Madina na umpe adhabu kamili anayostahiki.”6

Malik Ashtar alimwombea Abu Dharr kwenye hotuba yake na wote wale ambao walikuwepo hapo na akasema, “Amini” (Na iwe hiyo). Hata hivyo, walipokamilisha ibada ya mazishi ilikuwa jioni na wakawa hapo hadi asubuhi. Wakaondoka asubuhi siku iliyofuata.” (Tarikh kamil, Juz. 3, Izalatul Khifa Juz. 1, Tarikh Tabari, Juz. 4).

Hata hivyo bint yake Abu Dharr ambaye aliendelea kukaa hapo Rabzah kwa muda wa siku chache zaidi. Siku moja usiku alimuona Abu Dharr kwenye ndoto ameketi na anakariri Qurani Tukufu.

Akasema, Baba! Nini kimekutokea na umerehemewa kwa kiwango gani na Mwenyezi Mungu ambaye ni Mwingi wa Rehma? Akasema, Ewe binti yangu! Mwenyezi Mungu amenizawadia upendeleo usio na mipaka, amenipa starehe zote na amenipa kila kitu. Ninafurahia sana ukarimu Wake. Ni wajibu wako kujishughulisha na kumuabudu Mwenyezi Mungu kama kawaida na usiruhusu aina yoyote ya maringo na kiburi kuja kwako.” (Hayatul Qulubi, Juz. 2,).

Wasomi na waandishi wa historia wanakubaliana kwamba Abu Dharr alikufa tarehe 8, Zilhajjah, 32 A.H, Rabzah. Alikuwa na umri wa miaka 85.

  • 1. Jina lake alikuwa Sadi bin Ajlan Zaidi hujulikana jina lake la utani, Bahilah ni jina la kabila lake. Hadith nyingi zimesimuliwa na yeye. Aliishi Homs (Syria) ambako alikufa akiwa na miaka 91. Watu wengine husema kwamba huko Syria alikuwa sahaba wa mwisho wa Mtume (s.a.w) kufia huko. Lakini ukweli ni kwamba huko Syria sahaba wa mwisho kufa alikuwa Abdallah bin Bashir (Izalatul Khifa, Juz. 1, uk 285).
  • 2. Huyu alikuwa sahaba aliyeheshimiwa. Jina halisi la baba yake, Yaman lilikuwa Asal au Umail. Alikufa shahidi kwenye vita ya Uhud. Hudhayfah aliambiwa majina ya wanafiki na Mtume wa Uislamu. Kila mara Umar alikuwa akimuuliza Hudhayfah majina ya wanafiki. Hudhayfah pia alikuwa mtawala katika Madain wakati wa khalifa wa pili (Izatul Khifa, Juz. 1, uk. 282). Tabarsi anasema kwamba wanafiki walitayarisha njama ya kumuua Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenye bonde la Uqbah, lakini mpango huo ulivurugwa na Ammar yasir na wengineo. Mara tu baada ya tukio hilo, Mtukufu Mtume akafichua majina ya wanafiki kwa Hudhayfa. . . Kwa mujibu wa maandishi ya Abu Dharr orodha ya majina yaliyofichuliwa kwa Hudhayfa pia ilijulikana Ashrah Mubashirah (Masahaba kumi wa Mtume ambao walijulikana kwa cheo hiki baada ya kifo cha Mtume. Maandishi ya pembeni ya Ethtijaj Tabarsi, uk. 29).
  • 3. Labda anataja rejea ya utawala a Bani Umayyah na Bani Abbas. Hakuna Kabila la makabila yote ya miji na majangwa ya Arabuni ambalo halitaathiriwa. Wakati huo, watu katili watafikiriwa kuwa ndio wa kuheshimiwa, na wachamungu watadharauliwa. Mwenyezi Mungu na atunusuru kutokana na uovu a kipindi hicho.
  • 4. Waandishi wengi wa historia wamehusisha tukio la kifo cha Abu Dharr kwa mke wake Umm Dhar, lakini haioneshi kuwa sahihi kwa sababu waandishi wa historia kama vile Masudi na Yaqubi, wameandika kwamba mke na binti yake Abu Dharr walikwisha fika huko Rabzah. Majilisi ametoa maelezo ya kifo cha mke wake huko Rabza kama alivyoeleza bint yake. Tabari amesema kwamba mtoto wa kike alipelekwa Madina baada ya kifo cha Abu Dharr. Bin Athir pia amekiri kuwepo kwa mtoto wa kike (Kufuatana na Tarikh Kamil, Juz. 3, uk. 51) na hakuna hata mwandishi yeyote wa historia mwenye kuaminika ambaye ametamka kuhusu kuwasili kwa mke wa Abu Dharr Madina.
  • 5. Imetamkwa kwenye masimulizi ya kwamba Abu Dharr hakuhisi uchungu wowote wa kifo, na uhalali wake ulithibitika kwa sababu uchungu wa kifo anauhisi yule tu ambaye matendo yake yalikuwa ya kuchukiza au ambaye amefanya kitu ambacho kumbukumbu yake katika maisha husababisha kizuizi kwa roho kutoka. Mathalani Aishah alipohisi mateso makubwa alipokuwa kwenye uchungu wa kukata roho na alianza kupumua kwa nguvu sana watu wakamuuliza, Ewe Mama wa Waumini! Kwa nini imekuwa hivi? Nini kinachokusumbua" Akajibu, Vita vya Ngamia vinasonga roho (Rauzatul Akhyar anasimulia kutoka kwenye Rabiul Abrar).
  • 6. Upo uwezekano kwamba matokeo ya laana hiyo Uthman aliuawa baadaye kwa mfano wake. Historia inasema kwamba mwili wake ulilala juu ya lundo la kinyesi kwa muda wa siku tatu na mbwa walikula mguu wake mmoja. (Tarikh Atham Kufi). Baada ya mazishi ya Abu Dharr watu waliondoka Rabzah lakini mwanae wa kike aliendelea kukaa hapo kufuatana na wasia wake. Baada ya siku kadhaa, khalifa Uthman alimwita na akampeleka kwao. (Tarikh Tabari Juz. 4, uk 527)

Sura Ya Ishirini Na Moja

Baada ya kupata mateso ya kugandamizwa na matatizo mfululizo na mfuatano wa kuhamishwa kutoka kwa watu wenye fikra za kidunia, Abu Dharr aliiacha dunia hii ya muda mfupi akiwa Rabzah. Lakini hadith ya mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu bado inaendelea kuishi hadi daima milele. Historia imejaa mifano, ukweli na hotuba zake zilizowazi na kuaminika zitaendelea kusikika kwenye nyoyo za waumini. Abu Dharr bado yu hai kupitia kwa tabia yake hata baada ya kifo chake; na ataendelea kuwa hai kupitia kwa kanuni alizozishikilia sana.

Dunia inatambua kwamba Abu Dharr alikufa katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Aliteseka kwa matatizo na dhiki kwa ajili ya kutetea ukweli na kuanzisha na kutangaza kanuni za Uislamu katika Nchi za Kiislamu. Lakini inasikitisha kuona kwamba dhalimu hataki kutubu kwa udhalimu wake. Tunatoa maelezo ya tukio hili hapa kwa maneno ya mfasiri wa ‘Hitoria’ yaliyoandikwa na Muhammad bin Ali bin Atham Kufi, mwandishi wa historia wa karne ya 3 Hijiriya. Ameandika:

Habari za kifo cha Abu Dharr zilipomfikia Uthman, Ammar bin Yasir alikuwepo hapo. Ammar akasema; “Mwenyezi Mungu amhurumie Abu Dharr. Mwenyezi Mungu! Uwe shahidi kwamba tunaomba kwa nyoyo na roho zetu umhurumie yeye. Ee Mwenyezi Mungu umsamehe.”

Mara tu khalifa aliposikia akakasirika na akasema, “Ewe mpumbavu! Na wee utakutana na hatima ya aina hii hii. Nisikilize! Sioni aibu kwa sababu ya kumhamisha Abu Dharr na kifo chake cha upwekeni.” Ammar akasema, “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, hii haitakuwa sababu ya mwisho wangu.”

Khalifa aliposikia hivi akaagiza wafanya kazi wake wa baraza, “Msukumeni nje, mhamisheni hapa Madina na mpelekeni sehemu hiyo hiyo ambako Abu Dharr alipelekwa Yeye pia aendeshe maisha ya aina ile ile na msimruhusu arudi Madina almradi bado nipo hai.”

Ammar akasema, “Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Napenda zaidi kuwa jirani na mbwa mwitu na mbwa kuliko kuwa karibu na wewe.” Baada ya kusema hivyo alinyanyuka na kuondoka hapo na akaenda kwake.

Khalifa alipoamua kumpeleka Ammar huko Rabzah na taarifa ikalifikia kabila lake la Bani Makhzum, wakakasirika. Wakasemezana wao kwa wao kwamba Uthman alikwisha chupa mipaka ya uadilifu. Baada ya hapo walikaa kikao cha baraza na wakafikiria kwamba ingekuwa bora endapo kabla ya kuchukua hatua yoyote jambo hili lisuluhishwe kwa maelewano. Wakiwa na lengo hili katika maoni yao, walikwenda kumuona Ali.

Ali akawauliza, kwa nini nyinyi wote mmenijia wakati kama huu? Wakasema, “Lipo tatizo kubwa linatukabili, khalifa ameamua kumfukuza Ammar kutoka Madina kwenda Rabzah. Uwe mwema kiasi cha kutosha, uende kwa khalifa na umsihi kwa maneno yenye busara amwache Ammar kama alivyo na asimfukuze kutoka jijini, vinginevyo ghasia ya aina hiyo inaweza kuanzisha vurugu ambayo itakuwa si rahisi kuizima.”

Imamu Ali aliwasikiliza, akawaliwaza na akawaomba wasifanye haraka. Akawaambia, “Nitakwenda nijaribu kusuluhisha jambo hili. Ninao uhakika litasuluhishwa kwa makubaliano. Ninatambua vema hali hii. Nitamfikisha pale kwenye fikra yenu.”

Baada ya mazungumzo haya, Ali alikwenda kwa khalifa Uthman na akasema, “ Ewe Uthman! Kuna mambo mengine unayafanya haraka na unadharau ushauri wa marafiki na washauri. Wakati fulani ulimfukuza Abu Dharr Madina. Alikuwa Muislamu Muadilifu sana, sahaba mashuhuri wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na muhajirina bora sana. ulimpeleka Rabzah ambako alifariki katika hali ya upweke.

“Kwa sababu ya tukio hili, Waislamu sasa tayari wamekugeuka, hawako na wewe. Sasa ninasikia kwamba umeamua kumfukuza Ammar kutoka Madina. Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu usiwape usumbufu wa aina hii masahaba wa Mtume (s.a.w) na waache waishi kwa amani.”

Uthman aliposikia hivi akamjibu Ali kwa hasira; “Wewe ndiye unayetakiwa kufukuzwa kwanza kutoka hapa jijini kwa sababu ni wewe ndiye unayemharibu Ammar na wengine.”

Ali aliposikia maneno haya yasiyofaa, akassema; “Ewe Uthman! Unawezaje kudiriki kunifikiria mimi namna hii? Hutaweza kufanya jambo hili hata kama unatamani kulifanya na kama unatilia mashaka maneno yangu, jaribu kufanya hivyo. Hapo ndipo utakapotambua hali halisi ya mambo na ndipo utakapotambua ni nani hasa unaokabiliana nao. Na sasa unasema kwamba mimi ninamharibu Ammar na wengine.

“ Kwa jina la Mwenyezi Mungu, vurugu hii inatoka upande wako. Sioni kama watu hawa wana dosari yoyote. Unafanya matendo ambayo ni kinyume cha dini na maadili mema. Watu hawatayavumilia, na sasa wanaanza kukupa kisogo, na wewe huwezi kuvumilia mambo haya. Unahisi unakosewa na kila mtu na halafu unawasababishia matatizo. Msimamo huu upo mbali sana na vile walivyofanya wazee wetu.” Baada ya maneno haya akanyanyuka na kuondoka hapo.

Watu wa Bani Makhzum walipokwenda kwa Ali kutaka kujua khalifa alimwambia nini kuhusu suala lao, Ali aliwaambia, “Mwambieni Ammar asitoke nje ya nyumba yake. Mwenyezi Mungu atamkomboa kutoka kwenye mbinu za hila.” Khalifa pia alipata taarifa ya mazungumzo haya kupitia kwa mtu mwingine na akaacha kumfukuza Ammar.

Zayd bin Thabit akamwambia Uthman, “Endapo khalifa anataka hivyo tunaweza kwenda kwa Ali na kubadilishana mawazo naye kwa lengo la kuondoa hali ya kutoelewana ambayo imejitokeza na uelewano uendelee kama kawaida.” Khalifa akasema; “mnao uhuru wa kufanya hivyo.”

Zayd bin Thabit na Mughyrah bin Ahnas Thaqafi walikwenda kwa Ali, wakamsalimia na wakaketi. Halafu Zayd bin Thabit alianza kumsifu Ali na akasema, “Hapana mtu yeyote hapa duniani ambaye anao ukaribu huo, undugu, daraja na heshima kwa Mtukufu Mtume kama wewe ulivyo. Hapana mtu yeyote anaweza kulingana na wewe katika kuunga mkono Uislamu na kuwa mtu wa kwanza kuwa Muislamu. Wewe ni chemchem ya uadilifu na chanzo cha ukarimu.”

Baada ya wasifu huu Zayd bin Thabit akasema lengo lake hasa lililompeleka kwake na akasema; “Ewe Ali bin Abi Talib! Tulikwenda kwa khalifa Uthman. Ametoa aina fulani ya malalamiko dhidi yako, na amesema kwamba wakati mwingine unapinga matendo yake na unaingilia mambo anayotaka kuyafanya. Kwa hiyo, ili maudhi na kero zilizopo kati yenu ziondolewe kwani hiyo itakuwa ni furaha na shangwe kwa Waislamu wote.”

Ali akasema, “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwa kadiri nilivyoweza. Sikupinga kitu chochote wala sikuingilia jambo lolote. Lakini, sasa, mambo yamekuja kwenye kiwango ambacho haiwezekani kuonesha uvumilivu au kunyamaza. Nilimwambia ukweli kuhusu Ammar jambo ambalo lilimaanisha ustawi wake Uthman, uswalama na manufaa yake mwenyewe. Nilifanya kazi yangu na sasa shauri yake kufanya apendavyo.”

Aliposikia hivi Mughyrah bin Ahmad akasema; “Ewe Ali! Unatakiwa kukubaliana na hayo anayoyasema au anayoyataka kufanya Khalifa hata kama unasadiki moyoni mwako au hapana. Unatakiwa kufikiria kwamba utiifu kwa amri zake ni muhimu kwa sababu yeye anaoudhabiti juu yako na wewe huna udhibiti juu yake. Ametutuma kwako kwa sababu anataka tu tushuhudie yale unayoyasema na baada ya hapo, anaweza akasema lolote kuwa kosa.”

Aliposikia maneno ya Mughyrah, Ali alikasirika na akasema, “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, yule mnaye muunga mkono, kamwe hataheshimiwa na yule ambaye mnamfukuza kamwe hatapumzika. Ondoka nenda zako.”

Mughyrah alipatwa na bumbuwazi kwa yale aliyoyasema Ali na kusema, “Ewe Ali! Mughyrah amesema upuuzi. Amesema mambo haya kufuatana na anavyotaka mwenyewe. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, hatukuja kwako kwa ajili ya kushuhudia wala si nia yetu kukukosoa wewe au kupinga yale unayoyasema. Tulitaka tufungue mlango wa maelewano na mapatano na kwamba hiyo ndio sababu iliyotuleta hapa. Tunakuomba ufikirie jambo hili.” Ali akaonesha ridhaa yake na Zayd bin Thabit akarudi.

Imesimuliwa hapo juu jinsi Ali alivyopinga mwenendo wa Uthman. Bila shaka kuchupa mipaka kwa Uthman, iliwafanya masahaba wa Mtume (s.a.w) kuwa na wasi wasi na kusumbuka sana. Tayari walikwisha mkasirikia Uthman waliposikia mateso ya Abu Dharr. Mkasa huu ulisababisha hasira kubwa miongoni mwa Waislamu wa matabaka yote. Kwa hiyo, watu walianza kumkosoa Khalifa kibinafsi na kwa makundi.

Kuhusu suala hili, Zubayr bin al-Awam, sahaba wa Mtume alikwenda kwake na akasema, “Hivi Umar alichukua ahadi kwako kwamba hungewapachika watoto wa Abi Muit kwa watu?” Khalifa akasema, “Ndio, alichukua ahadi hiyo kutoka kwangu.” Zubayr akasema, “Kwa nini ulimteua Walid bin Uqbah Gavana wa Kufah?”

Khalifa akasema, “Nimefanya hivyo kama Umar alivyompa Ugavana wa Kufah Mughayrah bin Shubah. Kama mambo yalivyo, nilikwisha mteua kuwa gavana wa kufah lakini tabia yake ilipogeuka na kuwa kinyume na Uislamu, yaani akaanza kunywa mvinyo na kuzini, nilimwondoa na kumweka mtu mwingine kushika nafasi yake.”

Halafu Zubayr akasema, kwa nini ulimteua Muawiyah kuwa Gavana wa Syria kwa mujibu wa maoni ya Umar bin Khatab kwa sababu kabla yangu ni yeye ndiye aliyemteua Muawiyah kuwa Gavana wa Syria.” Tena akauliza, “Kwa nini uliwakemea masahaba wa Mtume, ingawa wewe si bora kuliko wao kwa namna yoyote ile?” Uthman akasema, Sikukusema wewe kwa ubaya. Kwani unajali nini ikiwa niliwakaripia wengine?”

Halafu akauliza, Kwa nini ulisema kwamba kukariri nakala ya Quran Tukufu ya Abdullah bin Masud ni vibaya, ambavyo alijifunza kukariri Qurani Tuklufu kutoka kwa Mtume Zaidi ya hayo, kwa nini ulimgandamiza? Ukaagiza apigwe hadi akapoteza fahamu.” Khalifa akasema, “Alikuwa na desturi ya kusema maneno ambayo hayangevumiliwa.”
Akauliza tena, “Kwa nini ulimpiga mateke Ammar bin Yasir na kwa agizo lako akapigwa sana hadi akapata maradhi ya henia?” Uthman akasema, “Kwa sababu alikuwa na desturi ya kuwachochea watu waniasi mimi.”

Zubayr akamuuliza tena, kwa nini ulimhamisha Abu Dharr na ukamtupa mahali ambapo penye upweke na hakuna hata mti. Mtu alikufa katika hali ya kukata tamaa kwa kutokuwa na msaada.

“Ewe Uthman! Hukuwa unatambua kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alimfanya kuwa rafiki yake mkubwa, na akasema kwamba hapana mtu aliye mkweli zaidi ya Abu Dharr kati ya mbingu na dunia? Hukuwa unajua kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu hakuwa anastahamili kuwa mbali naye na wakati wowote walipokuwa hamuoni alitoka kwenda kumtafuta Abu Dharr?”

Uthman bin Affan akajibu, “Alikuwa anawachochea watu wa Syria waniasi, alikuwa ananikashifu na alikuwa anafichua mapungufu yangu kwa watu.” Halafu Zubayr akauliza, “Kwa nini ulimfukuza Malik Ashtar na masahaba wake kutoka Kufah na kwa nini uliwatenganisha na familia zao?”

Uthman akasema, “Walikuwa wanasababisha vuruga Kufah na hawakumtii Gavana wangu Said bin Aas.” Zubayr bin Awam akasema, “Ewe Uthman matendo yako si halali. Hukuwa unafikiri na kujua ni nani hao uliokuwa unawachukulia hatua kama hizo. Mambo uliyoyataja hayakuwa sababu ya kuwafanyia mateso kama hayo masahaba wa Mtume walio heshimiwa sana.

“Ewe Uthman! Endapo utaniruhusu, nitakutajia matendo yako yaliyokiuka mafundisho ya imani. Ninasisitiza kwamba umuogope Mwenyezi Mungu na usijitenge kwa sababu ya serikali ya Kiislamu ambayo wewe ni kiongozi, vinginevyo siku utakapopata malipo ya matendo yako hapa duniani, wala haipo mbali. Adhabu hii itakuwa nyongeza ya adhabu utakayopata Akhera.”

Baada ya kifo cha kutisha cha Abu Dharr ambapo watu mashuhuri wa Misri walikwenda Madina kutafuta marekebisho ya malalamiko yao na wakaingia kwenye msikiti wa Mtukufu Mtume , humo waliona mkusanyiko wa Muhajirina na Ansar. Wakawasalimia na wao wakaitikia. Waislamu waliokusanyika hapo wakawauliza watu wa Misri, “Kwa nini mmekuja hapa kutoka Misri,” Wakawaelezea sababu ya safari yao ndefu kama hiyo. Walisema kwamba Gavana wa Misri aliyeteuliwa hakuwa na uwezo wa kazi kabisa na katili.

Hata hivyo watu wa Misri walikwenda mlangoni kwa khalifa Uthman na wakaomba wamuone. Wakapata ruhusa na wakaingia bada ya kupeana salamu, wakasema, “Ewe Uthman! Tumeteswa na Gavana wako. Matendo anayoyafanya yanararua moyo, yanatia uchungu na kusikitisha. Ewe khalifa! Mwenyezi Mungu amekupatia utajiri mwingi.

“Umshukuru Mwenyezi Mungu, uwe mchunguzi na mkali kwa watendaji wako na lengo lako liwe kusitawisha umma. Si tu kwamba tumeleta malalamiko dhidi ya Gavana wako, lakini pia mambo ambayo unayafanya wewe yana udhia.”

Uthman akasema, “Niambieni mambo hayo ni yepi.” Wakasema; “Ulimwita Hakam bin Aas arudi Madina tena, ingawa Mtume alikwisha mfukuza kutoka Madina na akampeleka Taif milele na Abu Bakr na Umar waliheshimu uamuzi wake wakati wa uongozi katika serikali zao.
“Ulipasua Qurani na kuichoma. umewapa udhibiti wa maji ya mvua ndugu zako ambapo yanatakiwa yatumiwe na watu wote na watu wamenyang’anywa manufaa yake. Umewafukuza baadhi ya masahaba wa Mtukufu Mtume kutoka Madina. Unataka watu wakufuate wewe kwa hali yoyote ile hata kama yale unayoyafanya yanaendana na sheria za imani au vinginevyo.

“Ewe Uthman! Sikiliza; tunakwambia wazi wazi kwamba tutakufuata wewe endapo utafuata njia iliyo sahihi na kama uking’ang’ania kuendeleza mwenendo ulio nao sasa, tutawajibika kutupilia mbali kiapo cha uaminifu kwako na kwa hiyo pande zote mbili kwa hakika zitaharibika.

“Ewe Uthman! Mwenyezi Mungu anatambua hali ya kila mtu. Kila Muislamu lazima amuogope yeye, sikiliza Uhusiano baina ya mtawala na mtawaliwa ni dhaifu sana. Mtawala lazima amuogope Mwenyezi Mungu na aache kufanya vitu ambavyo ni kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu na mtawaliwa lazima wamtii yeye. Mtu ataitwa kuhesabu hata matendo madogo kiasi chochote kile mbele ya Mwenyezi Mungu. Tumesema tulichotaka kusema. Sasa ni shauri lako kufanya unavyotaka.”

Baada ya kusikia haya Uthman aliinamisha kichwa chake kuelekea mbele na baada ya kuwa kimya kwa muda fulani akasema, kwa hali ilivyo sasa sitatoa maelezo yoyote kuhusu upinzani wenu kwa sababu mojawapo ya haya ni mengi sana, lakini ninachosema kuhusu Hakam bin Aas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu hakukosewa naye kwa sababu ya matendo yake mabaya na yasiyo stahili na ndio sababu alimfukuza kutoka hapa jijini. Sasa, niliposhika kazi ya Ukhalifa nilimwita arudi kwa sababu ya kuzingatia undugu wetu. Niambieni ikiwa watu wa Madina wanayo malalamiko yoyote yake, kwa hakika nitamwita ili ajieleze.

Waandishi wa historia wanasema kwamba watu walipompelekea Uthman mfululizo wa kipingamizi kuhusu mambo kadhaa, aliamua kuyafikiria mambo hayo na kuhusiana na hilo aliwaandikia barua magavana wote wa utawala wake kuwaambia watu waende Madina na kulalamika moja kwa moja kwake dhidi ya magavana. Mara tu barua hizi zilipowafikia magavana, malalamiko kutoka kila sehemu ya utawala yalianza kupelekwa Madina mfululizo.

Malalamiko ya kwanza kuwasili yalikota Kufah, Basra na Misri. Kutoka Kufah, Malik bin Ashtar Nakhai akifuatana na watu mia moja. Kutoka Basra Hakam bin Heil akifuatiwa na watu mia moja hamsini. Kutoka Misri watu mia nne wakifuatiwa na Abu Umar bin Badil, Wahhab bin Waraqa Khuzai, Kanana bin Shir al-Hamni na Saidi bin Hamran Muradi walifika Madina.

Baada ya watu hawa kufika Madina, Muhajirina na Ansari waliokasirishwa na tabia ya Uthman na walikuwa wamehuzunika sana kwa sababu ya matendo yake mabaya, waliungana nao na wote wakaamua kukubaliana endapo Uthman atafikiria kuhusu mambo hayo ambayo walimpa na akatoa majibu sahihi na ya kuridhisha, walikuwa tayari kumfuata lakini kama hakutoa majibu yaliyo sahihi na ya kuridhisha, wangempindua na kumpa Ukhalifa mtu mwingine aliye bora badala yake.

Mjumbe alipowasilisha habari hizi kwa Uthman, alitubu na kukiri kwamba alifanya kosa kubwa la kipumbavu kwa kuwaita watu hao Madina. baada ya kutafakari kwa kina sana kuhusu jambo hili, hata hivyo, alifanya uamuzi kwamba hatakutana nao. Huu ulikuwa uamuzi wake usio sahihi, lakini aliamua hivyo.
Akajificha ndani ya nyumba yake na milango mikubwa yote ilifungwa kwa ndani.

Watu walipofika kwenye lango la ikulu ya Uthman, alianza kufanya mazungumo nao kutoka kwenye paa la nyumba. Akasema, Ni jambo gani ambalo nimelifanya linalowakera? Kuweni na uhakika kwamba nitakubali madai yenu yote na nitafanya kama mnavyotaka. Msiwe na wasi wasi. Sitawakasirisha kwa namna yoyote ile.”

Watu hao wakassema, “umeyafanya maji ya mvua kwamba si sheria watu wote kuyatumia isipokwua ndugu zako.” Khalifa akasema, Msiwe na wasi wasi. Nisikilizeni kwa makini, nimesitisha matumizi ya maji kwa sababu nimeyahifadhi kwa ajili ya ngamia ambao nimewapokea kwa njia ya sadaka lakini endapo mnataka niruhusu yatumiwe na watu wote sina kipingamizi kwa hilo.”

Watu wakasema, “Umepasua nakala nyingi zisizohesabika za Qurani na ukazichoma moto. Huu ni ukiukaji wa sheria ya Kiislamu.” Khalifa akajibu, “Kwa kuwa palikuwepo na matokeo mengi ya Qurani moja, nilikusanya maandishi kwenye nakala zingine zote kwenye ardhi badala ya kuzichoma?”

Kwa nini hukufuatana na Mtume kwenye Vita ya Badr na kwa nini hukushiriki?” Akajibu, “Wakati huo mke wangu alikuwa mgonjwa kwa hiyo nilishughulika kumtunza.” Wakasema, “Kwa nini hukushiriki kwenye Bayatus Rizwan (Kiapo cha ahadi kwa Mtume kilichofanyika Rizwan)?” Akajibu, “Nilikuwa nimetoka nje wakati huo,” Wakauliza, “Kwa nini ulikimbia na kumwacha Mtume peke yake kwenye Vita ya Uhud?” Akajibu, “Nilikimbia kama mambo yalivyotokea, lakini hii ni dhambi yangu ambayo nilisamehewa. Kwa hiyo hakuna haja ya kuhoji jambo hili sasa.”

Wakasema, “Umewafukuza masahaba wengi wa Mtume ambao waliteseka kwa matatizo mengi huko uhamishoni. Baadhi yao walikuwa wanaheshimiwa sana na wenye hadhi. Uliwafukuza kutoka nyumbani kwao na ukawaweka kwenye dhamana ya vijana wasio na uzoefu na watu waovu ambao alijihalalishia umwagaji damu na utajiri ulikatazwa. Ewe Uthman! Miongoni mwa wale waliofukuzwa alikuwepo pia sahaba ambaye alikuwa kipenzi cha Mtume na Mwenyezi Mungu alimuamuru Mtume ampende.

“Unatambua kwamba Abu Dharr alipokwenda mahali Mtume mwenye alikuwa anatoka kwenda kumtafuta. Ulimpeleka kwenye jangwa lililo na upweke huko alikufa kwa njaa na kiu. Unayo maelezo gani kuhusu kitendo chako hiki kiovu.”

Uthman akasema, “Niliwafukuza watu hawa kutoka kwenye miji ya masikini walipoanza kuwashawishi watu kutoniamini. Nilihofu kwamba wangesababisha mgogoro na kutokuelewana. Mwachieni Mwenyezi Mungu kama mnafikiria kuwa ni dhambi yangu. Sasa, kuhusu wale watu ambao bado wapo kwenye uhamisho ninasema kwamba kuanzia sasa mnaweza kuwaita kupitia kwa mtu mwingine kama mnataka hivyo. Sina kipingamizi.”

Wakasema, “Dhuluma uliyomfanyia Ammar haisameheki. Kwa nini uliagiza apigwe sana hivyo kwamba akapata maradhi ya henia na bado mgonjwa hadi sasa.” Khalifa akasema, “Alinikosoa mimi na akatangaza mapungufu yangu hadharani.”

Wakasema, Kwa nini uligawa fedha ya Hazina ya Taifa kwa ndugu zako na kuwafanya kuwa matajiri? Masikini wanateseka na njaa na ndugu zako wanaishi maisha ya anasa.?”

Akajibu; “Umar bin Khatab pia alitumia mtindo huu. Alikuwa anampa zaidi mwenye kujiweza.” Wakasema, “Hakufanya upendeleo kama unavyofanya wewe. Uligawa fedha yote kwa ndugu zako. Hivi sifa zimewekewa mipaka kwa nduguzo tu? Salman, Miqdad, Ammar, Abu Dharr hawakuwa na sifa hadi wakanyang’- anywa mgao wa ruzuku na msaada? Umetumia fedha yote kwa ubadhilifu na kupoteza utajiri wa Waislamu.”

Uthman akasema, “Kama mnadhani hivyo, fanyeni hesabu fedha ninazolipwa. Nitalipa fedha hiyo polepole na kuziweka kwenye Hazina ya Taifa.”

Baada ya hapo khalifa alizungumza kwa maneno laini na kunyenyekea mbele yao, na wakati huo watu hao walikwenda zao. Khalifa hakuridhika hata walipokwisha ondoka.

Alitambua kwamba watu hao wangemshambulia baada ya muda mfupi. Kwa hiyo akamwita Abdullah bin Umar na akataka ushauri wake. Alimshauri amwite Ali ili amwombe aende kuwapooza watu hao. Alikuwa na uhakika kwamba wangefuata ushauri wa Ali.

Khalifa akamwita Ali kupitia kwa mjumbe maalum na akamweleza jambo lote na jinsi alivyotakiwa kuwatuliza watu hao. Ali akamuahidi kufanya kufuatana na ombi la Khalifa na alipokwenda kwa watu akawaambia, “Ni bora zaidi kuwa na moyo mtulivu.” Walikasirika sana; wakasema; “Tunakuchukulia katika heshima ya juu, lakini hatuwezi kuvumilia jeuri na kujiachia hadi kuchupa mipaka kwa Uthman.”

Kwa mujibu wa Athan Kufi, Ali aliwahakikishia na akasema, “Msiwe na wasi wasi, maelewano ni bora zaidi kuliko ugomvi.” Baada ya hapo Ali akaenda kwa Uthman akifuatana na viongozi wa makundi hayo. Baada ya mabishano marefu walihitimisha kwa kukubaliana na Uthman aliandika mkataba wa makubaliano ambao tunaunukuu hapa kwa maneno ya mfasiri wa Tarikh Atham Kufi:

“Kwa niaba ya Uthman, waraka huu umetolewa kwa maandishi kwa watu wa Basra, Kufah na Misri ambao amepinga vitendo vyangu, na ninategemea kwamba kuanzia sasa na kuendelea nitafanya kazi yangu kwa kufuata Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Suna za Mtume.

“Sitadharau ridhaa ya watu na nitaepuka ugomvi. Nitawaita watu niliowafukuza warudi makwao na nitawarudishia watu misaada ya fedha walio nyang’anywa. Nitamwondosha Abdullah bin Sad bin Abi Sarah kwenye Ugavana wa Misri na nitamteua mtu ambaye angependwa na watu wa Misri.”

Watu wa Misri wakasema; “Tunamtaka huyo Muhammad bin Abi Bakr bin Abi Quhafah ateuliwe kuwa mtawala wetu.” Uthman akasema; “Ndio, hilo litafanyika.” Kwa ufupi, Ali ndiye aliyekuwa dhamana katika mambo yote haya na ushahidi wa Zubayr bin al-Awam, Talha bin Abdullah bin Umar, Zayd bin Thabit Suhayl bin Hanif na Abu Ayyub bin Zayd, waliandikwa na alama zao zilibandikwa. Maneno ya mwisho yalikuwa, “Waraka huu uliandikwa mwezi wa Ziqadah 35 A.H.” Baada ya hapo Ali na watu wote waliondoka hapo.

Waandishi wa historia wanasema kwamba Uthman alitoa waraka wa maandishi kuhusu Ugavana wa watu wa Misri, wakaondoka Madina wakiwa wamefurahi na kuridhika.

Wakiwa amefuatana na Muhammad bin Abi Bakr (mtoto wa kiume wa Khalifa wa kwanza), walikuwa wamesafiri hatua kwa hatua hadi walipokuwa wamesafiri hatua tatu au walikuwa wamekwenda umbali wa siku tatu, kwa mujibu wa bin Qutaybah na Atham Kufi, wakamuona mtu amepanda ngamia akienda mwendo wa haraka kuelekea Misri.

Muhammad bin Abi Bakr aliamuru mtu huyo akamatwe na apelekwe kwake. Watu walimwendea mtu huyo haraka na wakamkamata na kumfikisha kwa Muhammad. Muhammad akamuuliza; “Unatoka wapi na unakwenda wapio?” Akajibu; “Ninatoka Madina na ninakwenda Misri.” Wakamuuliza kwa nini alikuwa anakwenda Misri? Akajibu kwamba alikuwa na shughuli zake binafsi. Kwa kuwa walikwisha mtilia shaka walimuuliza kama alikuwa na barua yoyote.

Akakataa. Muhammad bin Abi Bakr aliamuru apekuliwe. Alipopekulia, hakuna barua yoyoite iliyoonekana.

Muhammad akasema, “Pekueni kiriba chake cha maji.” Maji yaliyokua kwenye chupa yalipomwagwa, waliona barua ambayo ilihifadhiwa kwa kuzungushia nta. Walipoifungua, waligundua kwamba barua hiyo iliandikwa na Uthman na ikagongwa muhuri wake na ilikuwa inapelekwa kwa Gavana wa Misri, Abdullah bin Sad bin Abi Sarah:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu.

Mimi, mtumishi wa Mwenyezi Mungu, Uthman ninakuagiza wewe (Abdullah bin Sarah) kwamba mara tu Umar bin Badil Khuzai akifika kwako umkate kichwa na ikate miguu ya Alqamah bin Adis, kananah bin Bashir na Urwaisi ili wafe wakiwa wanabilingika na kugaragara kwenye damu yao. Halafu itundike miili yao kwenye miti karibu na njia panda. Utekeleze amri zilizoandikwa kwa mkono wangu, ambazo Muhammad bin Abi Bakr anazo anakuletea wewe, na ikiwezekana muue kwa kutumia mbinu zozote. Endelea kuwa gavana bila wasi wasi. Usiogope kitu chochote na uitawale Misri.”

Muhammad bin Abi Bakr na watu wengine mashuhuri wa Misri walishtuka baada ya kusoma barua hiyo na wakasema, “Mkataba mzuri ulioje ambao ameuhitimisha! Kwa uaminifu wa jinsi gani kiapo kimetolewa na kwa uaminifu kiasi gani ahadi imetimizwa! Ingekuwaje kama tungefika Misri baada ya kuwasili mtumwa wa Uthman!!”

Kwa ufupi walimshukuru Mwenyezi Mungu kwamba waliikwepa hatari, na wakarudi Madina waliwakusanya masahaba wote wa Mtume na wakaisoma barua ya Uthman bin Affan mbele yao.

Baada ya kusikia yaliyokuwa kwenye barua hiyo na kugundua ukweli halisi, hakuna hata mkazi moja wa Madina aliyekuwa na huruma kwa Khalifa. Msisimko wa uasi mkubwa ulikuwa unatokeza pole pole na watu wote wakaanza kuzungumza wazi wazi shutuma dhidi ya khalifa.

Nyoyo zilijaa shauku na kwa sababu ya hila hii kila mtu alikasirikia utawala wa Khalifa. Watu hao –kwa mujibu wa al-Fakhri ambao waliwahi kusikia sentenso ya Aishah ‘Muueni yahudi huyu Uthman” na watu hao ambao kwa mujibu wa Atham Kufi walikirahishwa na kuhuzunishwa sana, kwa sababu wazee wao waliteswa, walikuwa tayari kupigana.

Bani Salim walikasirishwa kwa sababu ya Abdullah bin Masud, BaniMakhzum walikwua na wasi wasi kwa sababu ya tukio la hatari lililomtokea Ammar bin Yasir na Bani Ghifar walikasirishwa kwa sababu ya yale aliyofanyiwa Abu Dharr Ghifari. Kwa maneno mengine, makabila haya yaliasi kwa sababu ya tabia ya Uthman kuhusiana na viongozi wao na walikasirika sana hivyo kwamba hawakuwa wanafikiria jambo lingine isipokuwa kumuua Uthman.

Katika hali hi makala yote pamoja na watu wa Misri waliazimia kumuona Ali Kwanza, kwa sababu yeye alikuwa dhamana yao katika mkataba wao na walitia sahihi hati ya mkataba kwa cheo hicho. Kwa hiyo watu wote walikwenda kwa Ali na wakampa barua hiyo ya Khalifa iliyozuiwa njiani. Ali alipoisoma barua ile na kufahamu yaliyoandikwa humo, alishtuka sana. Alisema kwa mshangao mkubwa, “Mimi nimeshangaa sana. Uthman amefanya nini?”

Baada ya hapo Ali alikwenda kwa Uthamn akiwa na barua hiyo na akaiionesha mbele yake, alisema, “Soma barua hii!” Uthman aliposoma hadi mwisho, Ali akasema, “Mimi sijui nifanye nini kuhusu wewe. Umecheza mchezo wa uharibifu. Niliwafanya watu hawa wakubaliane na wewe. Sasa umefanya yasiyofikiriwa kufanywa na Muislamu. Ninasikitika kwamba hata hukutambua ugumu niliopata katika kuondoa uadui wao kwako.

“Unatambua kwamba, watu hawa walikwishaondoka kwenda kwao wakiwa wameridhika na kufurahi kikamilifu kwa sababu ya imani yao kwangu. Ewe Uthman! Nilidhani jambo hili lilikwisha suluhishwa moja kwa moja. Nilidhani kwamba uadui uliondolewa na Waislamu walikwisha maliza ugomvi huu. Lakini loo! Niambie hii ni barua ya aina gani? Nani mwandishi wa barua hii? Hiki ni kitendo cha aina gani? Kutumia itakuwa maoni gani kuhusu udanganyifu hu na njama hii?”

Uthman akasema, “Ewe Abul Hasan! Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sikuandika barua hii, wala sikumwambia mtu yeyote kuandika, wala sikumwambia mtumishi wangu kwenda Misri. Mimi sijui lolote kuhusu tatizo hili!”

Ali akauliza; “Huyu ni ngamia wako?” Akajibu; “Ndio.” Ali akauliza tena, “Muhuri wako?” Akajibu, “ndio” Ali akasema; “Mwandiko huu unafanana na ule wa mwandishi wako. Muhuri wa kwako. Mtumwa wa kwako na ngamia ni wa kwako; hata hivyo unasema kwamba hujui lolote!”

Khalifa akasema; “Inawezekana kwamba sikutaarifiwa, na barua ikaandikwa na kusafirishwa.” Hata hivyo, Ali aliondoka hapo baada ya mazungumzo haya.

Hatimaye, Khalifa alihutubia kwenye Msikiti wa kati na alijaribu kutoa mmaelezo kuhusu msimamo wake kuhusu barua . Watu wakasema, “Sawa! Tunadhani kwamba hukuandika barua hii. Lakini imethibitishwa kwamba imeandikwa na mkono wa mwandishi wako, Marwan. Muhuri ni wako. Ngamia ni wako. Mtumwa ni wako. Sasa tunakuomba urudi kwenye ikulu yako na utuletee Marwan.”

Khalifa akasema, “Hapana, kamwe haitawezekana!”

Ghasia kubwa zilitokea baada ya mazungumzo haya. Kwa mujibu wa Tham Kufi mapigano yalianza na msikiti ukageuka kuwa uwanja wa vita, hali hiyo iliendelea kuwa mbaya zaidi hivyo kwamba Uthman alipoteza fahamu kwa sababu ya kupigwa mawe. Halafu akaondoshwa hapo na kupelekwa kwake.
Sasa muda ulikaribia ambapo wale watu ambao waliagizwa na Uthman kuwa huko Misri waliamua kutekeleza amri ya Ummul Muminina, mfululizo wa maneno, “Muueni Yahudi huyu! Amekua asi!” Kwa hiyo watu wakaizunguka nyumba ya Khalifa. Al-Fakhi ameandika kwamba mara tu nyumba ilipozungukwa na waasi, Aishah aliondoka Madina na akaelekea Makkah na khalifa Uthman akauawa na watu, chini ya uongozi wa Muhammad bin Abi Bakr:

Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, Uthman aliuawa tarehe 18, Zilhajjah 35 A.H. Ukhalifa wake ulidumu kwa muda wa miaka kumi na tatu. Mwili wake ulidumu siku tatu bila kuzikwa kwa sababu maadui zake walizuia asizikwe. Kwa mujibu wa bin Jarir Tabari, maiti ya Uthman ilidumu siku mbili na hakuna mtu aliyediriki kuuzika. Mwandishi wa historia, Atham Kufi, ameandika kwamba maiti ya Uthman haikuzikwa mpaka baada ya siku tatu na haukupata ulinzi hadi mbwa walinyofoa mguu wake mmoja. Baada ya hapo, Hubayr bin Mutia Taujeer bin Mutim na Hakim bin Hizam walikwenda kwa Ali na wakasema, “Tafadhali jaribu kupata maiti hiyo izikwe.” Kufuatana na vitisho vya Ali, mpango ulifanywa kuzika maiti hiyo. Lakini watu hawakukubali maiti hiyo izikwe kwenye uwanja wa makaburi ya Waislamu! Hatimaye mwili wake ulizikwa Hash Kaukab uwanja wa makaburi ya Wayahudi.

Baada ya hapo mwandishi wa historia huyo huyo ameandika kwamba tukio hili lilitokea tarehe 17, Zilhajjah, 35, A.H. siku ya Ijumaa baada ya Sala ya Alasiri. Uthman alikuwa na umri wa miaka 82. Taarifa ya tukio hili ilipomfikia Aishah, mama wa Waumini huko Makkah alipojua kwamba Uthman aliuawa na masahaba mashuhuri wa Mtume, alifurahi sana na akasema, “Mwenyezi Mungu amempa malipo kwa ajili ya matendo yake. Ninamshukuru Mwenyezi Mungu, Amemwadhibu kama ilivyo stahili.” (Tarikh Atham Kufi, Tarikh al-Imamuah vas Siyasah, Juz.1; Tarikh al-Fakhii, Tarikh Abul Fida, Tarikh Tabari).

Kwa ufupi, Uthman aliuawa miaka mitatu tu ya kifo cha kutisha cha Abu Dharr. Ukitafakari kwa uangalifu, mauaji yake yalihusiana na matendo hayo ambayo Abu Dharr alimwambia aache kufanya. Kama Uthman angekubali ushauri wa mheshimiwa Abu Dharr, hangekutana na siku kama hii, na mabalaa kama hayo hayangemfika na Abu Dharr pia hangetupwa huko upwekeni Rabzah ambako alikufa kifo cha kutisha.

Sura Ya Ishirini Na Mbili

Jaun bin Huwi alikuwa mtumwa wa Abu Dharr ambaye historia ya maisha yake yanaonekana jinsi alivyofundishwa na Abu Dharr. Kwa mujibu wa Mama qani, nasaba ya Jaun ni kama ifuatavyo:

Jaun bin Huwi bin Qatadah bin Awar bin Saidah bin Awf bin Kab bin Huwi Habashi (Tanqihul Maqal Juz. 1)

Imeandikwa kuhusu mtu huyu kwamba alikuwa wa jamii ya Kiafrika na alikuwa anamilikiwa na Fadhl bin Abbas bin Abdul Muttalib, ambako Ali alimnunua kwa sarafu za dhahabu 150 na akamtoa kama zawadi kwa Abu Dharr. Ali alitaka Jaun amtumikie Abu Dharr.

Kama ilivyotarajiwa, Jaun alifanya kazi inayostahili sifa kwa Abu Dharr ambaye alikuwa akifurahi sana kuwa anaye. Jaun alimtumikia Abu Dharr na pia alipata faida ya kuwa naye. Alichunguza kila kipengele cha tabia ya Abu Dharr kwa uangalifu mkubwa na alipendezwa sana nayo.
Kwa mambo yalivyokuwa, Jaun alimtumikia Abu Dharr kwa kila jinsi alivyoweza. Pia hakuna mahali ambapo alikosa heshima ya kuwa na Abu Dharr isipokuwa huko Rabzah ambako kuwepo kwake huko hapatajwi na mwandishi yeyote wa kuaminika wa historia.

Hata hivyo, Jaun alimtumikia Abu Dharr kwa ufanisi kwa kadiri alivyoweza. baada ya Abu Dharr kuondoka kwenda Rabzah yeye alibaki na kuendelea kumtumikia Ali. Baada ya Ali kufa kishahidi aliendelea kumtumikia Imamu Hasan naye alipokufa kishahidi mwaka wa 50 A.H alianza kumtumikia Imamu Husein.

Kwa ufupi, aliwatumikia kwa uaminifu watu waadilifu maisha yake yote. Imamu Husein alipoondoka Madina na kwenda kwanza Makkah na halafu Karbalah wakati wa mwezi wa Rajabu, mwaka wa 60 A.H. Jaun alikuwa naye kwenye safari hii.

Allamah Majlisi na Allamah Samawi wameandika kupitia kwa mamlaka ya Sayyid Razi daudi kwamba mapigano yalipoanza Karbala tarehe 10, Muharram, mwaka wa 61, A.H. Jaun alikwenda kwa Imamu Husain na akaomba ruhusa apigane. Imamu Husain akasema unaruhusiwa.

”Lakini ewe Jaun! Umeishi na mimi kwa kipindi kirefu katika amani na sasa unataka kuuawa!” Aliposikia maneno haya, Jaun alianguka miguuni mwa Imamu Husain na akasema, “Ewe bwana wangu, mimi si mmojawapo wa wale wanaokudanganya wakati wa amani na na furaha, na kukuacha wakati wa dhiki. Ewe bwana wangu! Hapana shaka kwamba jasho langu hunuka harufu mbaya, nasaba yangu si ya watu bora na rangi yangu nyeusi, lakini ukiniruhusu, jasho langu litanukia harufu nzuri, nasaba yangu itakuwa bora na rangi yangu itakuwa nyeupe huko peponi. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sitakuacha hadi hapo damu yangu itakapo changanyika na damu yako.”

Hatimaye Imamu Husain alimpa ruhusa. Jaun akaingia kwenye uwanja wa vita, akaanza kupigana na akakariri rajaza ifuatayo:

“Enyi mliolaaniwa! Mliwahi kuona mtumwa Mwafrika anavyopigana? Angalieni anavyopigana akiwaunga mkono uzao wa Mtukufu Mtume!”

Baada ya kukariri ‘rajaz’ Jaun alifanya shambulizi kali kwa adui na aliendelea kupigana mfululizo hadi akawaua maadui ishirini na tano na yeye mwenyewe alikufa kishahidi (Muntahul Amal).

Muhammad bin Abi Talib Makki ameandika kwamba Jaun alikufa kishahidi, Imamu Husain alikwenda kwenye maiti yake, akaweka kichwa chake kwenye maiti yake, akaweka kichwa chake kwenye paja lake na akamwombea Mwenyezi Mumgu;

“Ee Mwenyezi Mungu! Tia nuru uso wa Jaun, fanya jasho lake liwe na harufu ya kupendeza na mpe mahali awe na waadilifu wa huko Peponi, ili aweze kuwa na Muhammad na uzao wake (Ahlul-Bait).”

Wasomi humnukuu Imamu Muhammad Baqir ambaye humnukulu baba yake Imamu Zaynul Abidin akisema kwamba siku chache baada ya Bani Asad kuzika maiti ya mashahidi na kuondoka, waliona maiti ya Jaun ambayo uso wake ulikuwa unang’ara na maiti yake ilitoa harufu nzuri ya manukato. (Absanul Ainu uk. 165; chapa Hyderabad Deccan, 1357 A.H Biharul Anwar, Juz 1).

Kwa ufupi, mtumwa huyu mwaminifu wa Abu Dharr aliyeweka mhanga maisha yake kwa ajili ya bwana wake, Imamu Husain, aliyekuwa anapigana na Yazid bin Muawiyah Dikteta wa Umayyad, kwa ujasiri ushujaa na ushupavu na akafa shahidi.

Ni ukweli uliothibitishwa kwamba mara tu baada ya kufariki Mtukufu Mtume, mafundisho yake yote na maonyo hayakutiliwa maanani na wanafiki, ambao lengo lao moja tu lilikuwa kupata manufaa ya kidunia na wakayadharau mafundisho ya Mtume.

Baadhi ya masahaba wa Mtukufu Mtume walikuwa waumini imara wa Uislamu na mapenzi yao kwake na Ahlul Bait wake yalijaa kwenye mioyo yao, walinyanyuka kupigana kufa na kupona na hizo nguvu za uovu. Walikuwa wafuasi wa kweli wa Mtume Muhammad na Ahlul-Bait wake na walichukua mwongozo kutokana na yale waliyoyasema na kuyatenda. Pia walipata masahaba wengine ambao walipata uwezo na mamlaka kwa jina la Uislamu. Lakini badala ya kutumikia njia ya Uislamu, wakalitumia vibaya jina la Uislamu na utajiri kwa maslahi yao binafsi na kujiongezea kifamilia.

Walifuja utajiri wa taifa kama vile ulikuwa rasilimali yao. Miongoni mwa masahaba alikuwepo mmoja ambaye alithubutu kutamka; “Kwa jina la Mwenyezi Mungu hadi hapo nitakapolifuta jina la Mtume Muhammad kutoka kwenye uso wa ardhi sitapata amani”. (Murujuz Zahab Andalus Press) Matokeo yake ni kwamba mfumo mpya wa utawala ulijitokeza yaani ufalme ambao ulisababisha matisho miaka iliyofuata. Kupotoshwa kwa Uislamu kwa namna hiyo haikuvumiliwa na masahaba wa kweli ambao hawakujizuia kusema kweli hata kama ilimanisha kupoteza maisha.

Abu Dharr ni mfano wa wazi wa kubeba dhiki za kila aina na uimara na ujasiri ambazo ni sifa alizozionesha alipokuwa anateswa na mateso hayo yalikuwa makali kiasi cha kusababisha kifo chake kama ambavyo ilikwisha tabiriwa na Mtukufu Mtume (s.a.w). Mfano wake ulifuatwa na mtumwa wake Jaun ambaye naye pia alijitoa mhanga kwenye mchanga wa Karbala ambapo aliamua kuutetea Uislamu bega kwa bega na mjukuu wa Mtukufu Mtume, Husein. (a.s).