Table of Contents

Utangulizi

Qayamat -i- Sughra ni kitabu ambacho kinazungumzia mambo mengi hasa kuhusiana na ubashiri wa kuja kwa Imam MahdiError: Reference source not found a.s. , jambo ambalo linakubaliwa na Waislamu wa Madhehebu zote kwa pamoja kuanzia mwanzoni hadi siku hii ya leo. Waandishi wa Kishiah wamefanya kazi kubwa mno katika swala hili na vile vile juhudi za waandishi wa Kisunni pia zinastahili pongezi kwani wao wamechangia kwa kiasi kikubwa katika kuthibitisha waziwazi kuja kwa Imam Mahdi a.s. .

Hivyo hapa chini munaletewa marejeo ya maandiko kutoka vitabu vya Kisunni:

1. Jame' Sahih Muhammad ibn Ismail Bukhari Ahadith 13
2. Jame' Sahih Muslim ibn Hajjaj. Ahadith 11
3. Jame' Sahihain Hamidi Ahadith 2
4. Jama bain Sihah Sitta Zaid ibn Muawiya Abdari Ahadith 11
5 Fadhail-us-Sahaba Abdul Aziz Abkari Ahadith 7
6. Tafsir Tha'labi Ahadith 5
7. Gharib-ul-Hadith Ibn Qataiba Ahadith 6
8 Al-Firdous Ibn Shirwiyah Dailami Ahadith 4
9. Musnad-i-Fatimah Hafidh Abul Hasan Darqutni Ahadith 6
10 Musnad-i-Ali Hafidh Abul Hasan Darqutni Ahadith 3
11 Al-Mubtada KIssai Ahadith 3
12 Al-Masabih Husain ibn Masud Atra Ahadith 5
13 Al-Malahim Abul Hasan Manadiri Ahadith 34
14 Kitab Hafidh Ibn Mutayyan Ahadith 3
15 Ar-Riaya-li-Ahlir Riwaya Muhammad Ismail Farghani Ahadith 3
16 Khabar-i-Soteh Hamidi Ahadith 2
17 Istiab Yusuf ibn Abdul Aziz Numairi Ahadith 2

Katika karne hizi kumi na tatu kumeweza kutokea watu wachache ambao wanakanusha kabisa swala hili la kuwapo kwa Imam MahdiError: Reference source not found a.s. na idadi yao ni ndogo mno. Hapana shaka kuwa kuna watu ambao wanadai kuwa Yazid bin Muawiya bin Abi Sufiyan kuwa khalifa halali. Kunaweza kuwapo sababu mbili tu za kukanusha kuwapo kwa Imam Mahdi a.s. Moja, iwapo wao watakubali na kuthibitisha kuwapo kwa Imam Mahdi a.s. , basi kutakuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua shakhsiyah yake na nasaba yake, maisha na mienendo yake, n. k. hivyo mambo yote kama hayo yangalijitokeza mbele yao ambavyo wao wasingaliweza kufanya hila za kuzikubalia taarifa hizo.

Sababu ya pili ni kwamba kumewahi kutokezea watu waongo na ambao walijiita MahdiError: Reference source not found, hivyo watu walikwisha choshwa na wazushi hao kiasi kwamba hawataki kumkubalia Mahdi a.s. wa kweli. Na hii ni mbinu ya kukwepa tu ambavyo hoja kama hizi hazikubaliki katika Islam.

Kwa hakika sisi hatuwajali wale wote wanaomkanusha MahdiError: Reference source not found a.s. kwa hoja zao zisizo na misingi wala faida. Lau hoja zao zingalikuwa halisi na za kimsingi basi kusingalikuwapo na Mahdi wazushi na wafuasi wao. Hapa sisi tunazingatia wale ambao wamejivika Umahdi katika miili yao isiyo toharifu. Kumekuwapo na Mahdi katika Banu Abbas, Banu Fatima,n. k. vile vile mabara yote ya Indo-Pak na Afrika imeshirikiana katika kupatikana kwao. Lakini historia imewakanyaga Mahdi wengi waongo na wazushi.

Tabia na desturi ya mwanadamu imekuwa daima ikivutiwa na mitindo na mambo mapya, vivyo hivyo ndivyo hao MahdiError: Reference source not found waongo ndivyo walivyoweza kufaidi na kuwavutia watu. Imesemekana kuwa wale wotakaomkimbilia Mahdi kwa pupa bila ya kuwa na maarifa kamili, basi wamepotoka - Halakal Mustaji'un!

Kwa hakika zipo Ahadith nyingi mno zilizo sahihi na kutegemewa kuhusu Imam MahdiError: Reference source not found a.s. na hivyo hakuna mwanya wowote ule wa kutokezea Mahdi waongo. Lakini hao wazushi huwa watu wenye hila ambazo wao hujihusisha na ubashiri fulani na huweza kujitangaza kuwa wao ni Mahdi. Kwa bahati mbaya, wale wote wenye elimu ndogo wamekuwa daima wakiwakubali Mahdi kama hao na wakiwazunguka hadi kufa kwa Mahdi mzushi. Hivyo itakuwa ni vyema kwa kuchapisha habari kamili kuhusu Mahdi wa kweli ili mwanya wowote wa upotofu ufungwe kabisa. Faida ya pili ya uchapishaji kama huo utasaidia kuwapambanua Mahdi wazushi bila hata ya kutokezea magomvi na mafarakano.

Kwa mfano, kumekuwapo na kikundi kimoja ambacho kimedai kuwa Mtume Issa a.s. na Imam MahdiError: Reference source not found a.s. ni mtu mmoja tu. Katika swala hili, iwapo mtu atakuwa akijua kuhusu ubashiri wa kuja kwa Imam Mahdi a.s. na kwamba Mtume Issa a.s. atamsaidia na atasali nyuma yake, basi swala hili litajitatua lenyewe bila ya kuzusha ubishi wowote. Vile vile itakuwa vyema iwapo tutajihusisha zaidi katika swala hili. Kuna hoja mbili katika wazo hili:

1. Masiha aliyeahidiwa hatakuwa Mahdi bali atakuwa akilingana naye

2. Ipo Hadith moja isemayo kuwa 'La Mahdi illa Masih' yaani hakutakuwapo na Mahdi illa ni Masihi.

Inawezekana kuthibitisha habari yoyote kama ni kweli kwa kutoa maelezo ya kimantiki. Popote pale panapozungumziwa ubashiri wa Mtume Issa a.s. katika Hadith, basi tujue waziwazi kuwa yeye atakuwa Issa bin Maryam na wala si mtu mwingine kama yeye. Na wala haipatikani Hadith kama hiyo katika maandishi ya Mashia.

Hadith kama hizo zinapatikana katika maandishi ya Masunni ambapo Wanazuoni wao wamezipuuzia na kusema kuwa walioziripoti ni watu dhaifu. Kinyume na hivyo, zipo Hadith nyingi mno ambazo zinaelezea na kuthibitisha kuwa Mtume Issa a.s. atakuwa Mwisraili na MahdiError: Reference source not found a.s. atatokana na kizazi cha Mtume Muhammad s.a.w.w Hivyo imetuwia dhahiri kuwa Mahdi na Masihi ni watu wawili walio tofauti kabisa.

Hao MahdiError: Reference source not found waongo wameleta hasara kubwa miongoni mwa jamii zetu na hivyo halitakuwa jambo la ajabu iwapo Mahdi a.s. wa kweli atapata upinzani. Hivyo inatulazimu kuwa na elimu kamili ya Mahdi a.s. wa kweli. Kwa hakika ulimwengu kwa hivi sasa umejaa matatizo na misiba, na hivyo kumjua mtetezi wetu moyoni mwetu ni jambo la kutufariji mno. Kitabu hiki ni kiungo kimoja cha elimu juu ya Imam Mahdi a.s.

Maandiko ya Mashia yamejaa kwa Ahadith kuhusu Imam MahdiError: Reference source not found a.s. na kijitabu hiki sio cha kwanza kwa aina yake bali kina habari ambazo zitatuongoza kwa njia haki. Vile vile jambo la kututia moyo ni kwamba habari nyingi mno zimetolewa na Ahli Bayti a.s. ya Mtume s.a.w.w ambapo haziwezi kuwa ni habari za uzushi. Wanazuoni wa Kisunni wamethibitisha usahihi wa Ahadith hizo na wamekana wale wote ambao wanajaribu kupotosha ukweli na usahihi wa Ahadith na riwaya hizo.

Si kazi ngumu kukusanya Ahadith bali kazi iliyo ngumu kabisa ni ile ya kuthibitisha usahihi na ukweli wake hivyo ni vyema kuwadokezea mambo machache kuhusu hayo:

1. Maandiko mengi ya watu wa mji wa KufaError: Reference source not found yamepitia mabadiliko kabla ya kutufikia sisi. Wao wamekuwa na utaratibu tofauti wa maandiko yao na katika kuleta mabadiliko ya maandishi,kumeweza kutofautiana katika maana na maelezo. Mfano 'maberamu yatachomwa motoError: Reference source not found katika mitaa ya Kufa' au inapatikana hivi 'maberamu yatachanwa katika mitaa ya Kufa'. Mfano wa pili, ipo Hadith inayomzungumzia Auf-Salmi, ambaye makazi yake yanajulikana kama ni Tikrit na kwa mujibu wa maandiko ya Kufa inawezekana pia kupatikana kuwa ni Kuit. Miji yote hiyo miwili ipo Saudi Arabia na ni vigumu kuamua uhakiki wake. Kwa kuchukulia mojawapo ni lazima lakini uasili wa Maandiko ya Kufa yatapotea.

2. Katika riwaya na mapokezi, majina ya miji na mahala pengine yanatumika majina ya kale ambayo kwa sasa hayatumiki tena. Hivyo ni vyema kupata majina yanayotumika kwa sasa sambamba na majina ya kale ili Hadih hizo zieleweke vyema.

3. Taarifa kamili ya kimsingi ya Hadith itolewe, nani aliyeiripoti, mbele ya nani iliripotiwa, mahala pa kuripotiwa, n. k. , ili taarifa hizo ziweze kutambulisha vyema kuhusu Hadith hiyo.

4. Ahli Bayt a.s. ya Mtume Mtukufu s.a.w.w wamerekebisha kipindi katika nyanja mbalimbali za jamii ,maadili, kiuchumi, n. k. Hivyo Ahadith zinazozungumzia mambo ya ubashiri hayatakuwa na mushkeli kueleweka na kukubalika. Vile vile kuna mambo mengine manne pia, nayo ni:

    a. Uhakiki,

    b. Isiyo na uhakiki

    c. Makhsusi,

    d. Kawaida.

Ubashiri wowote ule ambao ni wenye uhakiki, basi hayo yatatokea tu katika hali yoyote ile. Na Mabashiri yale yasiyo na uhakiki yanaweza kutokea, inategemea. Mabashiri ya kawaida yanaweza kupatikana kila mahala. Na mabashiri makhsusi yamefungamanishwa na muda na mahala maalum. Ni matumaini kuwa mafungu haya ya uchambuzi yatasaidia kutambua matatizo na mabishano yoyote yatakayotokea.

5. Ahadith za ubashiri hazihitaji tafsiri au maelezo. Ama hayo yamekwishatokea au yatatokea kama vile yalivyoelezwa. Kwa watu kujaribu kuchambua kwa kuongezea chumvi na pilipili kutaongezea kuleta hali ngumu ya kueleweka na kufahamika.

Ninayo furaha kuwaelezea kuwa kitabu hiki cha Qayamat-i-Sughra kimejaribu kutimiza mahitaji na masharti kama hayo. Ni jambo la kuvutia kuona kuwa Qayamt-i-Sughra kinazungumzia mabashiri ambayo hayajatokea bado mfano uasi utakaoongozwa na Hasan Sayyed, Uchokozi wa SufianiError: Reference source not found, kuteketezwa kwa baadhi ya sehemu za Mashariki ya Kati ,n. k. mabashiri ambayo bado Mahdi wazushi hawajaweza kuzibashiri.

Kwa kumalizia mazungumzo haya, ninawaomba wasomaji wote wakisome kitabu hiki kwa makini sana na wala si kwa kuupoteza muda tu bali waweze kuzingatia makusudio ya kuandika kitabu hiki. Imethibitika kwa mamlaka ya QuranError: Reference source not found Tukufu na vile vile Ahadith kuwa ni lazima kuwepo na kiongozi wa Kidini katika ulimwengu na kwamba mtu yeyote yule atakayekufa bila ya kumjua Imam wa zama zake basi atakufa kifo cha ujahili. Hivyo elimu na maarifa ya Imam ni swala la Aakhera pia na ambapo ni faradhi kwa wanawake na wanaume wote kwa pamoja.

Mwishoni mwa kitabu hiki nimejaribu kuongezea makala juu ya uthibitisho wa kuwapo kwa Imam MahdiError: Reference source not found a.s. kwa mujibu wa Wanazuoni wa Ahli Sunna ili msomaji aweze kutambua umuhimu wa Imam Mahdi a.s. katika madhehebu mengine ya Islam.

Amiraly M. H. Datoo
Bukoba, 5 Januari 1996