7. Zaka Zilizo Sunnah

Vitu saba vina Zaka Sunnah :

• Mali ya biashara au mtaji

• Mali ambayo mtu anataka kuitumia katika kufanyia bishara

Aina za nafaka :

• Mfano mchele, dengu, dengu iliyoparazwa. Lakini mbogamboga kama vile biringanya, matango, matikimaji, maboga hayana Zaka.

• Farasi jike

• Vito vya dhahabu na mawe

• Vitu vilivyotengezwa vya kuvaa na mawe kama almasi n.k.

• Mali iliyozikwa au kufichwa

Iwapo mtu atakuwa na mali aliyoizika au aliyoificha ambayo hawezi kuitumia basi kwa misingi ya uwezo inambidi kutoa Zaka ya mwaka mmoja.

Kukwepa kutoa Zaka, iwapo mtu atauza sehemu ya mali kiasi fulani kabla ya kuisha kwa mwaka kwa misingi ya kukwepa kulipa Zaka, basi itambidi uanzapo mwaka mpya, alipie Zaka sehemu hiyo aliyokuwa ameuza kwa ajili ya kukwepa Zaka yake.

Mali ya kukodisha, mtu anayepokea malipo kutokana na kukodisha majumba, maduka, mashamba, mabustani au hamaamk (mabafu yanayotoza malipo kwa kutumia).