read

Utangulizi

Hapa nitapenda kuzungumzia machache kuhusu sadaqah
• Sadaqah inalipia madeni na kuongezea neema kwetu,

• Sadaqah inatuepusha na mauti katika hali mabya

• Siku ya Qiyama kutakuwa na jua na joto kali mno, lakini Mumin atakuwa katika kivuli, nacho ni sadaqah aliyokuwa akiitoa.

• Toeni sadaqah asubuhi na mapema, ili balaa na matatizo yasiwafikieni katika siku nzima.

• Muwatibu wagonjwa wenu kwa kutoa sadaqah

• Kutoa sadaqah ni afadhali kuliko kumnunua mtumwa na kumfanya huru

• Mtu mmoja alifiwa na watoto wawili, alibakia mmoja. Akashauriwa kutoa sadaqah.Toeni sadaqah kwa mikono yenu wenyewe kwani hamtakuwa kifo kibaya na balaa zaidi ya 70 zitaepukwa na kujiepusha na mitego 70 ya Shaitani, kwani Shaitani yupo anasema, “Usitoe sadaqah.” Je tutamwitikia Shaitani?

• Toeni sadaqah hata kama ni tonge moja ya tende na kama hiyo pia hamuwezi basi toeni punje moja ya tende.

• Sadaqah inatuepusha na balaa 70 ambamo kuna magonjwa, madhara ya moto, kuzama maji, kuangukiwa na kufunikwa na majumba yanayoporomoka na kubomoka na kutokuwa masikini,

• Unapokuwa na hofu ya kuibiwa, kuugua n.k. bali toa sadaqah.