read

1. Kutokulipa Zaka

Katika Madhambi makuu, dhambi la thelathini na saba ni kule kutokulipa Zaka zilizofaradhishwa na kama vile ilivyoelezwa katika Sahifa ya ‘Abdul ‘Adhim kwamba Maimamu Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s), Imam Musa al-Kadhim (a.s) na Al Imam Muhammad at-Taqi (a.s) wamesema kuwa hili ni dhambi kubwa kabisa kwani amesema Allah (swt) katika Quran: Surah al –Tawbah, Ayah 34 – 35:

“Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika moto wa Jahannam , na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, “Haya ndiyo (yale mali) mliojilimbikia nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya) yale mliyokuwa mkikusanya.” (9:34-35)

Imeelezwa katika riwaya kuwa neno lililotumika katika Ayah hii kanz inamaanisha mali yoyote ile ambamo Zaka na haki zinginezo zilizofaradhishwa hazijatolewa.

Vile vile Amesema Allah (swt) katika Qur'an Tukufu, Surah Ali-Imran, 3, Ayah 180:
“Wala wasione wale ambao wanafanya ubakhili katika yale aliyowapa Allah (swt) katika fadhila Zake kuwa ni bora kwao. La ni vibaya kwao. Watafungwa kongwa za yale waliyoyafanyia ubakhili – Siku ya Qiyamah.” (3:180)

Yaaani wale ambao wanamiliki mali kwa kipindi kifupi tu ambayo hatimaye watakufa na hakuna shaka kuwa hakuna kitakachobakia kingine isipokuwa Ufalme wa Allah (swt). Hivyo inatubidi sisi tutumie mali hii vyema iwezekanavyo katika njia ya kutuletea baraka na uokovu Siku ya Qiyamah, kabla mali hii haijatutoka na tukaiacha humu humu duniani. Imeandikwa katika Minhaj-us-Sadiqiin kuwa imeelezwa katika Hadith kuwa

‘Yeyote yule aliyebarikiwa na Allah (swt) kwa mali na utajiri, lakini kwa sababu za ubakhili wake hakutoa Zaka na malipo mengine yaliyofaradhishwa kwake, basi Siku ya Qiyamah mali hiyo itatokezea kwake katika sura ya nyoka, ambaye atakuwa mwenye sumu kali kwani hatakuwa na unywele wowote juu ya kichwa chake na atakuwa na alama mbili za rangi nyeusi chini ya macho yake na hii ndiyo dalili ya kutambulisha kuwa nyoka huyo ni mkali sana na hatarikabis. Basi nyoka huyo atajiviringisha shingoni mwa mtu huyo kama mnyororo na kujivingisha shingoni mwake. Katika hali ya kumsuta, nyoka huyo atasema: ‘Mimi ni mali yako ile ambayo wewe ulikuwa ukijivuna na kujifakharisha duniani.’

Al Imam Muhammad al-Baqir (a.s) amesema katika Wasail-as-shiah, mlango 3, J.6, Uk. 11:
“Mtu yeyote ambaye hatatoa na kulipa Zaka ya mali yake basiSiku ya Qiyamah Allah (swt) atamwadhibu kwa miale ya mioto katika sura ya nyoka wakubwa ambao watakuwa wakinyofoa na kula nyama yake hadi hapo hisabu yake itakapokwisha.”

Vile vile Al Imam Muhammad al-Baqir (a.s) amesema katika Tafsir Minhaj as-Sadiqiin kuwa:
“Iwapo mtu aliye na mali na utajiri atakapoijiwa na ndugu au jamaa yake kwa ajili kuomba msaada kutokea mali na utajiri huo alionao, na yeye kwa sababu ya ubakhili wake akimnyima, basi Allah (swt) atamtoa nyoka mkubwa kabisa kutokea mioto ya Jahannam ambaye huizungusha ulimi wake mdomoni ili kwamba mtu huyo amwijie ili aweze kujiviringa shingoni mwake kama mnyororo mzito.”

Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) amesema katika Wasa’il as-Shiah, ZAKAT, mlango 3, Hadith 1, J.6, Uk. 11 Kafi:
“Mtu yeyote anayemiliki dhahabu na fedha na asipotoa Zaka yake iliyofaradhishwa (au Khums, kama vile inavyoelezwa katika Tafsir al-Qummi), basi Allah (swt) atamfunga kifungo katika mahala pa upweke na atamwekea nyoka mkubwa kabisa ambaye atakuwa amedondosha nywele zake kwa sababu ya sumu kali aliyonayo, na wakati nyoka huyoatakapotaka kumshika basi mtu huyo atakuwa akijarbu sana kukikmibia lakiniatkaposhindwa hatimaye atakapotambua kuwa hataweza kujiokoa basi atamnyooshea mikono nyake mbele ya nyoka huyo. Lakini nyoka huyo atazitafuna mikono hiyo kama vile anavyotafunwa mtoto mdogo wa ngamia na atajiviringisha shingoni mwake kama mnyororo. Na hapo Allah (swt) anatuambia kuwa ‘Yeyote yule anayemiliki mifugo, ng’ombe na ngamia na siyetoa Zaka ya mali yake, basi Allah (swt) Siku ya Qiyamah atamfunga kifungo cha upweke na kila mnyama atamwuma na kila mnyama mwenye meno makali atampasua na yeyote yule ambaye hatoi Zaka kutokea mitende, mizabibu na mazao yake ya kilimo, basi huyo siku ya Qiyamah basi atafungwa shingoni mwake kwa mnyororo wenye urefu wa takriban magorofa saba.”

Al Imam Muhammad al-Baqir (a.s) amesema katika Wasa’il as-Shiah Mlango 3, J.6, Uk.11:
“Allah (swt) amefaradhisha Zaka pamoja na Sala. Ameamrisha kutekeleza Sala na kutoa Zaka hivyo iwapo mtu atasali bila ya kutoa Zaka, basi atakuwa hakukamilisha Sala.”

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) Wasa’il as-Shiah, ZAKAT, mlango 3, Hadith 13, J.6, Uk. 11: amesema kuwa:
“Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) aliingia katika Masjid an-Nabawi, na aliwataja watu watano kwa majina yao na akasema kuwa inukeni na mtoke humu Msikitini na wala msisali kwani nyinyi hamutoi Zaka.”
(Wasiolipa Zaka wamefukuzwa kutoka Msikitini!)

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) anasema katika Wasa’il as-Shiah, ZAKAT, mlango 3, Hadith 24, J.6, Uk 14:
“Mtu yeyote asiyelipa Zaka ya mali yake basi yeye wakati wa mauti yake atataka kurudishwa humu duniani ili aweze kutoa na kulipa Zaka, kama vile Allah (swt) anatuambia: ‘Ewe Allah (swt) nirudishe tena ili nikafanye mema niliyokuwa nimeyaacha!’ Yaani wakati wa kifo chake atasema kuwa arudishwe humu duniani ili akaitumie mali aliyoilimbikiza katika njia njema, lakini atajibiwa kuwa kamwe haitawezekana hivyo kurudi kwake.”

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) ameelezea tafsir ya Ayah isemayo kuwa: ‘Allah (swt) atawaonyesha matendo yao katika hali ya kusikitisha mno kuwa wao hawatatoka nje ya Jahannam’ kama ifuatavyo katika wasl Wasa’il as-Shiah, mlango 5, Hadith 5, J.6, Uk21:
“Mtu yule ambaye anakusanya na kulimbikiza mali yake na anafanya ubakhili katika kuitumia katika mambo mema na kwa kutoa zaka n.k., basi anapokufa huku amewaachia mali hiyo wale ambao watatumia mali hiyo katika utiifu wa Allah (swt) au kwa kutenda madhambi, basiiwapo itatumiwa katika utiifu wa Allah (swt) basi atakuwa mtu wa kujivuna na iwapo itatumiwa katika maasi na madhambi basi itamdhalilisha.”

Riwaya hii imenakiliwa na ‘Ayyashi, Mufiid, Sadduq na Tabarasi katika vitabu vyao na vile vile wamewanakili Maimamu Al Imam Muhammad al-Baqir (a.s) na Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s)

Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) amesema, Wasa’il as-Shiah, mlango 5, Hadith 5, J.6, Uk2:
“Hakuna kitu kinachokimaliza Islam kama Ubakhili na njia ya Ubakhili ni sawa na njia ya sisimizi ambayo haionekanina yenyewe ipo kama Shirk ambayo inayo aina nyingi.”

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) amesema katika Safinat al-Bihar, J.1 Uk. 155:
“Watu watakapokataa kutoa Zaka, basi baraka itakuwa imeondolewa kutoka ardhini kwa kutoa mazao na matunda kutoka mashamba yao, na madini.”

Vile vile Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) amesema katika Wasa’il as-Shiah, Mlango 1, Hadith 13:
“Muwatibu wagonjwa wenu kwa kutoa Sadaqah na mutokomeze balaa, maafa kwa Du’a na muhifadhi mali zenu kwa kutoa Zaka.”

Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) amesema Wasa’il as-Shiah,mlango 5, Hadith 10, J.6, Uk23 :
“Allah (swt) anazo mahala pengi humu ardhini ambazo huitwa ‘kilipiza kisasi’ hivyo Allah (swt) anapomjaalia mtu mali na utajiri, na huyo mtu haitumii kwa kutoa malipo aliyofaradhishiwa, basi huwekewa nafasi mahala hap. Mali ambayo anakusanya kwa mbinu zake zote, inampotoka na anaiacha kwa wengine.”

Na katika riwaya zinginezo imeelezwa kuwa mtu ambaye anafanya ubakhili wa kutumia mali yake katika njia njema basi itatokea kuwa ataitumia katika njia potofu na riwaya ambazo zimeelezwa katika mlango wa Zaka, zipo nyingi, lakini hadi hapa zinatosheleza.