read

10. Sadaqah Na Misaada:

Wananyumba Wanaostahiki Malipo

Wanaostahiki malipo ni mke (wa ndoa ya kudumu) mtiifu na watoto wake na watoto wa watoto wake na vile inavyoendelea kuteremka chini na ambao anahitaji msaada basi ni faradhi. Vile vile baba na mama na babu mzaa baba na mama mzaa mama na vile itakavyoendelea juu na iwapo wanahitaji msaada wake na watu wngineo basi na kwa kiasi cha uwezo wake kama anao na iwapo hatawapa basi atatazamwa miongoni mwa watu kama qata’ rahmi . Na jambo hili limezungumziwa katika makala mengineyo.

Sadaqah Zilizo Sunnah

Zipo aina nyingi za malipo yaliyo Sunnah. Katika Ayah na riwaya nyingi mno kumesisitizwa mno kuwa sadaqah itolewe hususan katika siku ya Ijumaa, Siku ya ‘Arafah, katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani itolewe kwa makhususi ya majirani, majamaa n.k. Vile vile Sadaqah ni dawa ya ugonjwa, huondoa balaa, huleta riziki, huzidisha mali na huepusha vifo vya kutisha kama kuungua moto, kuzama maji na kuwazuia Majinni na kwamba huondoa balaa sabini. Kila utakavyotoa sadaqah zaidi basi matokeo yake pia yatakuwa ni mazuri zaidi. Wala haina kiwango kidogo, kiasi chochote mtu atakachokitoa kitatosha walau hata kama atatoa kokwa moja ya tende basi itatosha!

Zawadi

Ni kitu ambacho mtu mmoja anampa mtu kwa ajili ya kuongezea urafiki ama awe masikini au tajiri. Na iwapo hivyo itakuwa kwa nia ya kutaka furaha ya Allah (swt), basi itakuwa ni ‘ibada bora kabisa.

Imeripotiwa kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) katika Al-Kafi J.5, Uk. 144 kuwa:
“Iwapo mimi nitapenda kumpatia kitu rafiki yangu basi mimi nitampa zawadi kwani ninaipenda zaidi kuliko Sadaqah.”

Ugeni Na Ukarimu

Zipo riwaya nyingi mno kuhusu kuwakarimu wageni na kamba hiyo ndiyo tabia njema ya Mitume (a.s) Ipo riwaya moja kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) kwa muda wa siku saba hakupata mgeni nyumbani kwake basi alisema huku akilia:
“Nasikitika mnona ninakhofu kuwa isije Allah (swt) akaniondolea rehema na baraka zake.”

Haki Iliyo Maalumu Na Isiyo Maalum

Inatubidi sisi tuwe tumepanga viwango maalumu vya kila siku au kila wiki au kila mwezikatika mali zetu kwa ajili ya wale wenye shida na kwa ajili ya majamaa zetu ili kukidhi mahitaji yao.

Amesema Allah (swt) katika Quran: Surah al- Ma’arij, Ayah 24 – 25:

“Na ambao katika mali yao iko haki maalumu. Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba” (70:24-25)

Al Imam Musa bin Ja’afer (a.s) amepokelewa riwaya kuwa:
“Katika ukoo wa Bani Israil kulikuwa na mtu mwema ambaye alikuwa mke aliye mwema pia. Siku moja aliota ndoto ambamo aliambiwa kuwa Allah (swt) amempangia kiasi fulani cha umri wake ambapo nusu ya umri huo utapita katika raha na mustarehe wakati nusu ya umriuliobakia utapita katika shida na dhiki na umasikin.

Hivyo Allah (swt) amekupa fursa wewe kuchagua iwapo utapenda kupitisha umri wako wa nusu ya awali ya raha na mustarehe na baadaye dhiki na umasikini ? Hivyo chagua mojawapo. Kwa hayo mtu huyo alijibu kuwa : ‘Mimi ninaye mke wangu aliye mwema na hushirikiana naye katika maswala yote, hivyo nitapenda kupewa muda wa kuweza kuongea naye kabla sijatoa uamuzi wa chaguo langu.’

Mke wake alimshauri mumewe kuukubalia umri ule wenye neema uwe ndio wa kuanzia kwani: ‘Inawezekana Allah (swt) anataka kututeremshia neema na baraka zake hivyo tukaongoka.’

Hivyo usiku uliofuatia, bwana huyo aliulizwa jibu alilifikia katika uamuzi wake. Naye akajibu: ‘Mimi ninataka kuupitisha nusu ya umri wangu katika neema, raha na mustarehe.’ Kwa hayo akajibiwa kuwa hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa mujibu wa chaguo lake. Kuanzia hapo yeye alijaaliwa kila aina ya raha na akawa tajiri mkubwa mwenye mali na milki nyingi.

Katika kutajirika huku, mke wake akamwambia, ‘Ewe Bwanangu! Usiwasahau kuwasaidia na kukidhi haja za majamaa zetu na mafukara na masikinina uwe na uhusiano mwema pamoja na. na uwazawadie watu fulani fulani wakiwemo majirani na marafiki, zawadi mbalimbali.’

Mtu huyo alizingatiana kutekeleza ushauri uliokuwa umetolewa na mke wake. Na hivyo alifungua milango ya kugawa mali yake katika masuala hayo hadi ulipofika akati wa kuisha kwa nusu ya umri wake wa awali.

Kuisha huku kwa nusu ya kwanza ya umri wake, aliota ndoto tena ambamo aliambiwa kuwa: ‘Kwa kutokana na uwema wako wa kuwasaidia wenye shida na dhiki imekuwa kipaumbele kwako, basi Allah (swt) amekubadilishia sehemu hii ya pili kuwa katika raha na mustarehe kama ilivyo sasa.’”

Haki Ya Uvunaji

Wakati wa mavuno kwa kiwango kile ambacho bado Zaka haijapigiwa hisabu, inagawiwa kwa kuchota mkono moja kwa wapita njia kama vile alivyosema Allah (swt) katika Quran: Surah 69, Ayah 141:

“Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisio tambaa, na mitende,na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.” (69:141)

Katika aina za Sadaqah, aina hizi mbili za sadaqah ni Sunnah kwani Ayah ya Qur'an Tukufu pamoja na riwaya nyingi zimezungumzia na kusisitiza na ndio maana zimezungumziwa mbalimbali.

Kukopa Madeni

Yaani kuwakopa Waislamu ambao wanashida ya kukopa deni ili kukidhi masuala yao. Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) amesema, katika Al-Kafi:
“Katika mlango wa Jannat kumeandikwa ‘Yapo mema kumi kwa mtoa Sadaqah na mema kumi na nane kwa mkopeshaji madeni.’”

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) amesema, katika Al-Kafi:
“Wakati Mumin mmoja anapomkopesha Mumin mwenzake deni kwa ajili ya kutaka ridhaa ya Allah (swt) , basi Allah (swt) anihisabia deni hilo katika Sadaqah hadi kulipwa kwake.”

Kila mara mtu atakapokuwa akimpa muhula mdaiwa wake kulipa deni lake, basi Allah (swt) atakuwa akimwandikia kuwa ametoa Sadaqah kiasi hicho kwani yeye alikuwa na haki kamili ya kufanya na kulazimisha malipo lakini hakutumia nguvu kudai na badala yake amemwongezea muda mdaiwa wake, hivyo inamaanisha kuwa amemkopa mara mbili katika mali hiyo. Hivyo mtu huyo anakuwa mustahiki wa kupata thawabu za kutoa Sadaqah ka mara ya pili.

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) ameripotiwa akisema kuwa:
“Kwa kupuuzia ‘Ma’un’ (mambo ya nyumbani) ambayo Allah (swt) ameahidikatika Qur'an Tukufu adhabu, basi si Zaka inayozungumziwa, bali ni kuwasaidia kwa kuwakopa wale wenye shida na wanaodai kuwapa vitu vya nyumbani.”