read

2. Asiyelipa Zaka Ni Kafiri

Kama tulivyokwisha ona hapo awali kuhusu masuala ya zaka na kutokulipa kwake ni dhambi kuu. Iwapo mtu atamlazimu kulipa Zaka na kwa sababu za ubakhili wake, halipi basi atakuwa kafiri na najis kwani Zaka ni slawa na kufaradhishiwa kutimiza kama Sala na swala moja muhimu katika Dini na kwa kutokutimiza misingi ya dini, basi kunamtoa mtu nje ya dini. Zipo riwaya nyingi ambazo zinazumngumzia kukufurishwa kwa mtu asiyetoa Zaka kwa sababu za ubakhili wake. Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) amesema katika Wasa’il as-Shiah,mlango 4, Hadith 2, J.6, Uk 18:

“Bila shaka Allah (swt) amewawekea hisa mafukara na wenye shida katika mali za matajiriambayo imefaradhishwa. Faradhi ambayo inapotimizwa inakuwa ni yenye kuwafakharisha matajiri hao na ni kwa sababu ya kutoa huko Zaka kunakoharamisha kumwagwa damu yao na wanaolipa zaka wanaitwa Waislamu.”

Yaani wenye mali iwapo hawatatoa Zaka iliyofaradhishwa kwa kukataa, basi hao si Waislamu na hivyo kumwagwa kwa damu yao haiharamishwi.

Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) amesema, Wasa’il as-Shiah,, J.6, Uk18:
“Mtu yeyote yule ambaye hatatoa Zaka hata lau kwa kiasi cha Qirat (1.20 Dinar yaani punje nne za Shayiri) basi huyo si Mumin wala si Mwislamu na watu kama hawa ndivyo alivyoelezea Allah (swt) kuwa watakuwa wakitaka warudishwe humu duniani ili watekeleze mema.”

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) ameeleza katika Wasa’il as-Shiah,, J.6, Uk18:
“Mtu yeyote yule ambaye hatatoa Zaka hata kwa kiasi cha Qirat moja (sawa na punje nne za Shayiri) basi huyo atakuwa bila imani na kufa kwa mauti ya Myahudi au Mnasara.”

Amesema vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) katika Wasa’il as-Shiah, ZAKAT, mlango 3, Hadith 1, J.6, Uk. 19 na Kafi:
“Allah (swt) ameruhusu kumwagwa damu ya watu wa aina mbili ambapo hukumu hii itatekelezwa pale atakapodhihiri Al-Imam Muhammad Mahdi, sahibuz-zamaan, (a.s) na hivyo mmoja miongoni mwa watu hao wawili ni yule anayefanya zinaa ilhali anayo mke wake hivyo atauawa kwa kupigwa mawe hadi kufa kwake na wa pili ni yule asiyetoa Zaka, huyo atakatwa kichwa.”

Vile vile amesema, katika Wasa’il as-Shiah, mlango 5, Hadith 8, J.6, Uk20:
“Mali haipotei katika majangwa na Baharini ispokuwa ile isiyolipiwa Zaka na atakapodhihiri Al-Imam Muhammad Mahdi, sahibuz-zamaan, (a.s) basi wale wote wasiolipa Zaka watasakwa na kukamtwa na watakatwa shingo zao.”

Amesema Allah (swt) katika Quran: Surah al –Fussilat,41, Ayah 6 – 8:
“Ole wao wanaomshirikisha, ambao hawatoi Zaka na wanaikataa Aakhera.” (41:6-8)

Amesema Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) , katika Al-mustadrak:
“Kwa kiapo cha Allah (swt) ambaye anayoanayo roho ya Mtume Wake katika kudura yake, kuwa hakuna mtu anayemfanyia khiana Allah (swt) isipokuwa Mushrikina kama hawa ambao hawatoi Zaka kutoka mali zao.”

Vile vile Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) alimwambia Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s), katika Al-Khisal, Uk. 450, Mlango Kumi:
“Ya Ali ! Katika Ummah wangu wapo makafiri wa makundi kumi
1. Mfitini na mchonganishi

2. Mchawi

3. Dayyuth yaani mwanamme yule ambaye anajua kuwa mke wake anazini lakini hajali bali anapuuzia,

4. Mwanamme yule ambaye anauroho wa kiharamu wa kutafuta wanawake mbalimbal kwa kulawiti,

5. Anayewalawiti wanyama

6. Anayezini pamoja na wale walioharamishwa kwake yaani ambao ni mahram kwake,

7. Anayechochea na kuzidisha moto wa fitina na chuki miongoni mwa watu,

8. Anayewasaidia makafiri kihali na mali kupigana dhidi ya Waislamu,

9. Asiyetoa Zaka

10. Asiye Hijji ilhali ana uwezo kamili na kutimiza masharti yake na akifa katika hali hiyo.”

Kwa kuzingatia riwaya kama hizi tunaona kuwa kutokusali, kutokutoa Zaka na kutokuhiji wakati hali inaruhusu, kwa misingi ya ujauri wetu wenyewe, basi huyo ni kafiri na atakosa baraka na neema za Aakhera ambayo ni kumwokoa kutoka Jahannam na vile vile humu duniani hatakuwa toharifu kama Waislamu na hataruhusiwa kurithi, kuoana pamoja na waislamu, n.k., lakini iwapo mtu hatoi Zaka kwa ubakhili wake (Ingawaje hakatai wala kupinga Zaka) basi huyo hawezi kuwa kafiri. Ingawaje kidhahiri yeye ni Mwislamu lakini kiundani mwake anayo sifa mojawapo ya ukafiri na iwapo atakufa, basi atatumbukizwa katika adhabu kali mno, kama vile ilivyoahidiwa.