read

4. Zaka Na Sadaqah Huongeza Neema

Faida kuu mojawapo ya kutoa Zaka ni kuongezeka kwa neema na baraka ya mali yetu iwapo itatolewa kwa kuzingatia kanuni na ustaarabu wa kutoa hivyo, na ni kinyume na mawazo na mipango ya Ki-Shaytani, kwani mabakhili hufikiria daima kuwa kwa kutoa mali yako kwa ajili misaada na Sadaqah na Zaka, basi mali yao hupungua na hivyo wanaweza kuwa masikini na kwa hakika hayo ndiyo mawazo na upotofu wa Shaytani.

Amesema Allah (swt) katika Quran: Surah al –Baqarah, Ayah 28:

“Allah (swt) huongezea katika Sadaqah” (2:28)

Yaani huongezea baraka humu duniani na vile vile kutakuwapo na malipo mengine huko Aakhera na amesema Allah (swt) katika Quran: Surah al – Saba, 34, Ayah 39:

“Chochote kile mtakachokitoa (katika njia yake), basi Atawalipeni (humu humu duniani) malipo yake, Naye ni Mbora wa wanao ruzuku.” (34:39)

Amesema Allah (swt) katika Quran: Surah al –Rum, 30, Ayah 39 :
”Na mnachokitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Allah (swt) . Lakini mnachokitoa kwa Zaka kwa kutaka radhi ya Allah (swt), basi hao ndio watakaozidishiwa.” (30:39)

Katika Ayah hizo, tumeona kuwa kuongezeka zaidi mno na vile vile Baraka pia itakuwamo, vyote kwa pamoja. Katika kusisitiza hayo, zipo riwaya nyingi mno.

Amesema Bi. Fatimah az-Zahra bintie Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w). katika hotuba aliyoitoa kuzungumzia Fadak 1 katika Bihar al-Anwaar, J.8, Uk 109:
“Kwa ajili ya kujitakasa na dhambi la Shirk, Allah (swt) ametufadhishia kuikamilisha imani yetu ( yaani mtu yeyote anayetaka kujitakasisha na unajisi basi inambidi kuleta imani kwa moyo wake kamilifu), na Sala inamwepusha na magonjwa ya kiburi na kujifakharisha, na Zaka inamwepusha mtu kwa magonjwa ya ubahili ili mwanadamu awe mkarimu na mpenda kutoa kwa ajili ya mema ili atakasike) na hii pia ndiyo sababu kuu katika kujiongezea riziki .”

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) ameripotiwa akisema katika Al-Kafi:
“Yeyote yule anayetumia kutoka mali yake katika njia ya kheri, basi Allah (swt) anamlipa mema humu duniani na kumwongezea katika malipo yake.”

Vile vile ameripotiwa akisema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) katika Wasa’il as-Shiah : Mlango Sadaqah, Hadith 19, J.6, Uk. 259:
“Tafuteni riziki yenu kwa kutoa Sadaqah.”

Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) ameripotiwa katika Kitab ‘Uddatud-Da’I kuwa alimwuliza mtoto wake: ”Je nyumbani kuna kiasi gani kwa ajili ya matumizi ”

Naye alimjibu: “Zipo Dinar arobaini tu.”
Imam (a.s) alimwambia “Dinar zote hizo zigawe Sadaqah.”

Kwa hayo mtoto wake alimwambia Imam (a.s) “Ewe Baba! Mbali na Dinar hizi arobaini, hatutabakia na akiba yoyote.”

Imam (a.s) alimwambia: “Nakuambia kuwa zitoe Dinar zote Sadaqah kwani ni Allah (swt) tu ndiye atakayetuongezea kwa hayo. Je wewe hauelwei kuwa kila kitu kina ufunguo wake ? Na ufunguo wa riziki ni Sadaqah (kutolea mema).”

Kwa hayo, mtoto wake aliyekuwa akiitwa Muhammad, alizitoa Sadaqah Dinar hizo na hazikupita siku kumi, Imam (a.s) alitumiwa Ddinar elfu nne. Hapo Imam (a.s) alimwambia mwanae : “Ewe Mwanangu! Sisi tulitoa Dinar arobaini tu na Allah (swt) ametupa Dinar elfu nne badala yake.”

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) amesema katika Nahjul Balagha kuwa:
“Mtu anapokuwa masikini au mwenye shida basi fanyeni biashara pamoja na Allah (swt) kwa kutoa Sadaqah.”

Al Imam ‘Ali ar Ridha (a.s) alimwambia mfanyakazi wake: “Je leo umeshagawa chochote katika njia ya Allah (swt).” Mfanyakazi huyo, “La, bado sijagawa.” Kwa kuyasikia hayo Imam (a.s) alimjibu, “ Sasa kama haukufanya hivyo, basi Allah (swt) atatulipa nini badala ya tendo letu ? Hivyo hatutapata baraka wala neema yoyote kutoka kwa Allah (swt) . Tukitoa chochote ndipo Allah (swt) atatulipa kwa wingi badala yake.”

Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) ameelezea Hadith katika Al-kafi, Kitab ad-Du’a, J. 2, Uk.595 moja kwa kutokea Ayah Fahuwa Yukhlifuhu (yaani chochote kile kinachotolewa katika njia ya Allah (swt) , basi hulipa malipo yake kwa haraka sana ). Na Hadith yenyewe ni :
“Je utadhaniaje kuwa Allah (swt) anakiuka ahadi aliyoitoa?”

Basi mwandishi akajibu: “La! Sivyo hivyo.”

Ndipo Imam (a.s) alimwuliza: “Sasa je kwanini wewe haupati malipo yako kwa yale unayoyatoa na kugawa?”

Naye akajibu, “Kwa hakika mimi sijui sababu zake.”

Imam (a.s) alimjibu, “Iwapo miongoni mwenu yeyote atakayekuwa akiipata riziki yake kwa njia zilizo halali, na kama ataitumia hata Dirham moja katika njia zilizo halali, basi lazima mtapata malipo yake na kwa wingi zaidi. Na iwapo mkiona kuwa hamkupata chochote katika malipo yenu basi mutambue kuwa mali hiyo ilichumwa kwa njia zilizo haramu au ilitolewa na kutumiwa katika njia iliyoharamishwa.”

Kuhusiana na swala hili zipo Ayah na riwaya nyingi mno, lakini tunatua hapa. Marehemu Nouri katika kitabu chake Kalimah at-Tayyibah amezungumzia mengi na kwa mapana na undani zaidi kuhusu kutoa Sadaqah katika njia ya Allah (swt) na amedondoa hekaya takriban arobaini ambamo ‘Alim rabbani akhwand Mullah Fath ‘Ali amenakili kisa cha jamaa yake ategemewae ambaye amesema,
“Mwaka mmoja ambapo hali ya ughali ilikuwa imekithiri, nilikuwa na kipande kimoja cha ardhi ambapo nilikuwa nimepanda Shayiri na ikatokea kuwa shamba langu hilo likawa na mavuno mengi mno kuliko mashamba menginey. Kwa kuwa hali ilikuwa ni mbaya kwa watu wengineo, hivyo tamaa ya kujitafutia faida zaidi katika mazingara hayo niliyatoa kutoka nafsi yangu. Hivyo mimi nilkwenda moja kwa moja Msikitini na kutangaza kuwa mazao yote yaliyo shambani mwangu nimeyaacha kwa masharti kwamba yeyote mwenye shida tu ndiye aende kuchukua na masikini na mafukara waendekuchukua kwa ajili ya chakula cha familia zao. Wote wachukue kiasi wanachokihitaji. Hivyo masikini na mafukara na wenye shida walikuwa wakichukua mavuno kutoka shambani mwangu huku wakisubiri mavuno yao kukomaa. Kwa hakika nafsi yangu ilikuwa imetulia vyema kabisa kwani sikuwa na wasiwasi kwani nilikuwa nimeshajitenga navyo.

Wakulima wadogowadogo wote walipovuna mazao yao, nami nikavuna kutoka mashamba yangu mengineo na nikawaambia wafanyakazi wangu waende katika shamba ambalo nilikuwa nimeligawa kuwasaidia wenye shida wakati huo, wakaangalie kama kumebakia chochote ili waweze kuvuna.

Kwa hakika hao walipokwenda shambani humo walikuta shamba zima limejaa Shayiri kupita kiasi na baada ya kuvuna na kusafisha nilikuta kuwa nimepata mavuno mara dufu kuliko mashamba yangu mengineyo. Ingawaje humo watu wote walikuwa wakivuna kwa ajili ya chakula chao na familia zao, ilitakiwa kuwa tupu kumbe Allah (swt) amerudishia mavuno tena mara dufu.

Vile vile sisi tulikuwa ukipanda mwaka mmoja na kuipumzisha ardhi mwaka mmoja, lakini shamba hilo halikuhitaji kupumzishwa wala kuwekewa mbolea na badala yake nimekuwa nikilima na kupanda nafaka kila mwaka na nilikuwa nikipata mavuno mara dufu kila msimu.

Mimi kwa hakika nilistaajabishwa mno kuona hayo na nikajiuliza isije hiki kipande cha ardhi kikawa ni kitu kingine na mavuno yanapokuwa tayari, hupata mavuno mengi kabisa kuliko mashamba mengine yangu na ya watu wengineo.”

Mbali na hayo, Merehemu amenakiliwa kuwa:
‘Yeye alikuwa na shamba moja la mizabibu kandoni mwa barabara na kwa mara ya kwanza kulipozaa zabibu katika matawi yake, alimwammuru mtunza shamba wake kuwa zabibu zote zilizopo kando ya barabara aziache kwa ajili wapitao njia. Hivyo kila mpita njia alichuma na kula zabibu zilizokuwa hapo na wengine hata walichukua pamoja nao. Msimu ulipokwa ukiisha aliwaamuru wafanyakazi wake waende kuangalia kama kulibakia zabibu zilizokuwa zimefichika nyuma ya majani au pembeni. Lakini jambo la kustaajabisha ni kwamba, wafanyakazi waliporudi, walikuwa wamevuna zabibu mara dufu ya mashamba yake mengineyo pamoja na kwamba kila mpita njia alikuwa akichuma zabibu hapo.’

Vile vile imenakiliwa kuwa:
‘Kila msimu alipokuwa akivuna ngano na kuzisafisha, alikuwa akizileta nyumbani kwake na hapo ndipo alipokuwa akitoa Zaka yake. Lakini safari moja alipovuna na kusafisha, akiwa akielekea nyumbani kwake aliwaza kuwa inambidi alipe Zaka haraka iwezekanavyo, kwani si vyema kuchelewesha ulipaji wa Zaka. Ni ukweli kwamba ngano ipo tayari na mafukaraa na masikini pia wapo. Hivyo aliwajulisha mara moja mafukaraa na masikini waje kuchukua ngano, na hivyo akapiga mahisabu yake na kuwagawia sehemu yao na hivyo sehemu iliyobakia aliileta nyumbani kwake na kujaza madebe makubwa makubwa na alikuwa akijua ujazo wao. Lakini alikuja kuangalia hapo baadaye akakuta kuwa idadi ya ngano imeongezeka mara dufu pamoja na kwamba likuwa amepunguza kwa ajili ya kuwagawia mafukaraa na masikini.Na hivyo alikuta idadi ya ngano ipo pale pale kabla ya kutoa Zaka.’

Katika kitabu kilichotajwa, Alhaj Mahdi Sultan Abadi amenakili kuwa :
‘Mwaka mmoja mimi nilipovuna mavuno, nilipima uzito wa ngano na nikatoa na kuigawa Zaka yake. Na nafaka hizo zilibakia mahala hapo hapo kwa muda wa mwezi mmoa ambapo anyama pamoja na mapanya walikuwa wakila humo. Na nilipokuja kurudia kupima uzito wake nikakuta kuwa uzito wa ngano ulikuwa vile vile kama siku ya kwanza yaani kiasi nilichokitoa Zaka na kilicholiwa na wanyama na mapanya hakikupungua hata chembe kidogo.’

 • 1. Fadak
  Fadak kilikuwa ni kijiji kimoja chenye rutuba karibu na Madina huko Arabia na vile vile ilikuwa na ngome iliyokuwa ikiitwa ash-Shumrukh. (Mu'jamal buldan,j.4,uk.238;Mu'jam masta'jam,al-Bakri,j.3,uk.1015;ar-Rawdhal-mi'tar,al-himyari,uk.437;Wafaa'al-wafaa,j. 4,uk.1280). Fadak ilikuwa ni milki ya Mayahudi katika mwaka wa 7 baada ya Hijri na umilikaji wake ulitoka kwao ukawa chini ya Mtume (s.a.w.w). kwa mujibu wa mkataba wa amani.Sababu ya mkataba huu ni kwamba baada ya kuanguka kwa Khaybar,Mayahudi waliitambua nguvu na uwezo halisi wa Waislamu,na ushawishi wao kijeshi ulipungua na walishuhudia kuwa Mtume (s.a.w.w). aliwasamehe baadhi ya Mayahudi walipoomba hifadhi,vilevile wao walituma ujumbe wa amani kwa Mtume (s.a.w.w). na walionyesha nia yao kuwa Fadak ingeliweza kuchukuliwa kutoka kwao na kwamba eneo lao lisingeligeuzwa kuwa uwanja wa vita.Kwa hivyo, Mtume (s.a.w.w). alilikubali ombi lao na kuwapatia amani,na ardhi hiyo ikawa ndiyo milki yake binafsi ambamo hakuna aliyekuwa na hamu na wala kusingaliwezekana kuwa na hamu;kwa sababu Waislamu wanayo haki ya kugawana katika milki zile ambazo wanazoweza kuzipata baada ya kupigana Jihad, ambapo milki inayopatikana bila jihad inaitwa fay' ambayo ndiyo milki ya Mtume (s.a.w.w).peke yake na kwamba hakuna mtu mwingine yeyote aliyekuwa na haki humo.

  Kwa mujibu wa kesi ya 'dai la Fadak' ni kwamba Bi.Fatimah az-Zahra (a.s) alidai kuwa baba yake Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w). alikuwa amempatia Fadak kama Zawadi (hibah)na alikuwa ni mrithi wa sehemu iliyopatikana ya baba yake ya khums ya khaybar na mali yake huko Madina.Tukio hili limeandikwa kama ifuatavyo katika Sahih Bukhari:

  Imeripotiwa na Abdul Aziz bin Abdullah,Ibrahim bin Sa'd , Saleh na Ibn Shihab kuwa wamepewa habari na Urwah bin Zubayr kuwa imeripotiwa kutoka Aisha kuwa baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w). Bi.Fatimah (a.s) alimwambia Abubakr ampatie ile haki ya urithi wa Mtume (s.a.w.w). ambao umepewa na Mwenyezi Mungu.Hapo Abubakr aliielezea hadith isemayo kuwa 'sisi Mitume hatuachi urithi,na sehemu yetu ni sadaqah' na hapo binti yake Mtume (s.a.w.w). alighadhabika mno na tangia hapo aliacha kuzungumza na Abubakr mpaka kufariki kwake,kwani baada ya kifo cha babake,aliishi muda wa miezi sita tu. Aisha anaelezea kuwa Bi.Fatimah (a.s) alidai urithi wa Khaybar na kiunga huko Madina,lakini Abubakr alikataa katakata kumpatia. Anaendelea Aisha kusema kuwa Abubakr alisema kuwa yeye hakuwa tayari kamwe kuachia kile alichokuwa Mtume (s.a.w.w). akikifanyia kazi,bali nami pia nitaendelea kukifanyia kazi. Mimi ninaogopa katika kutahkiki iwapo nitaliachia katika amri za Mtume (s.a.w.w). basi nitatoka katika haki na kuingia katika batili.Lakini ni dhahiri kuwa baada yake Abubakr,urithi wa Madina ulipewa Imam Ali a.s na Abbas. Lakini alibakia na Khaybar na Fadak huku akidai kuwa hivyo vilikuwa ni Sadaqah ya Mtume (s.a.w.w). Mambo hayo yalikuwanayo hao wawili kwa mujibu wa matakwa yao."

  Katika Sahih Bukhari kisa hiki kimeripotiwa mahala pengi (1) Kitabul Khums,mlango faradh khums, (2)Kitabul Fadhail As-habin Nabii katika mazungumzo ya Abbas bin Abdul Muttalib (3) Kitabul Maghazi,mlango wa Ghazwah Khaybar, (4) Kitabul Maghazi,mlango Hadith Bani Nadhiir, (5) Kitabul Faraidh,mlango Qaul Nabii (s.a.w.w).: hakirithiwi tunachokiacha Sadaqah. (6) Kitab al-I'tisaam bil kitaan wa Sunnatah.

  Katika Bukhari,sehemu moja baada ya kuelezea kisa hiki cha dai la Fadak,imeelezwa hivi:
  "Bi.Fatimah az-Zahra (a.s) alikasirishwa mno na alimghadhabikia mno Abu Bakr kwa kumkatalia urithi wake,na kamwe hakuongea naye mpaka alipofariki,baada ya miezi sita tangu baba yake kufariki.Baada ya kifo chake,bwana wake Imam Ali (a.s) alimzika wakati wa usiku na Abubakr hakuruhusiwa kushiriki katika mazishi na alimsalia mwenyewe.Watu walikuwa wakimstahi Imam Ali a.s katika uhai wa Bi Fatimah (a.s) lakini baada ya kifo chake,watu walimgeuka Imam Ali (a.s) na kwa sababu hiyo Imam Ali a.s alifanya Bay'a ya Abubakr baada ya miezi sita" (Sahih Bukhari:Kitabul Maghazi,mlango gazwa Khaybar)

  Vivi hivi,kisa hiki kimeelezwa katika Sahih Muslim.Angalia Kitabul Jihad wal Siira,mlango kauli Nabii (s.a.w.w).:La nurith maa tarakna fahuwa sadaqah yaani haturithiwi kile tulichokiacha,illa ni Sadaqah.

  Kwa kuwa kisa hiki kinapatikana katika 'sahihain" (vitabu viwili sahihi:Muslim na Bukhari) basi wanahadith wanaafikiana na kukubalia.Sasa nitapenda mutafakari juu ya kisa hicho hicho katika kitabu mojawapo maarufu 'tabaqaatil Kubra' kama vilivyo maarufu Sahih Muslim na Bukhari.

  "Abubakr hakumpatia chochote Bi.Fatemah (a.s) kutoka kile alichokuwa ameacha Mtume (s.a.w.w). na kwa sababu hiyo Bi.Fatimah (a.s) alimghadhabikia mno Abubakr na kamwe hakuzungumza naye hadi kufariki kwake.Bi Fatimah (a.s) aliishi kwa muda wa miezi sita baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w). Jaafer anaripoti kuwa Bi.Fatimah (a.s) alimwijia Abubakr na kudai haki za urithi kutokana alivyoviacha Mtume (s.a.w.w). na vile vile alikuja Abbas kuja kudai urithi wake. Imam Ali (a.s) alikuwa nao.Hapo Abubakr aliwajibu kuwa Mtume (s.a.w.w). alisema kuwa 'sisi mitume haturithiwi kwa kile tunachokiacha,huwa Sadaqah' na mimi ninafanya kile alichokifanya Mtume (s.a.w.w).. Hapo Imam Ali (a.s) alimjibu kuwa katika Quran Tukufu imeandikwa kuwa urithi wa Mtume Daud (a.s) ulichukuliwa na Mtume Suleyman (a.s) na Mtume Zakariyyahh (a.s) aliomba dua ajaaliwe mtoto wa kiume ili aweze kuwa mrithi wake na wa Ale Yaaqub. Abubakr alimjibu kuwa ndivyo vivyo hivyo unavyotamka wewe lakini wewe unajua kile nikijuacho mimi. Imam Ali (a.s) alimwambia kuwa hiki ni Kitabu cha Allah kinachosema katika haqi yetu.Lakini Abubakr alikataa katakata na hapo wote watatu waliondoka kwa ukimya." (Tabaqaat Ibn Sa'ad,j.2,uk.86)

  Vile vile Imam Tabari ameelezea kwa mapana zaidi katika historia yake.Rejea Tarikh al-Umam wal Muluuk,j.3,uk.202. Allamah Baladhuri ameongezea mwangaza zaidi katika swala hili:
  "Abdullah ibn Maimun al-Maktub,Fasiil bin 'Iyaar na malik bin Jawza wamenakiliwa wakiripoti kutoka kwa baba yao kuwa Bi.Fatimah az-Zahra (a.s) alimwambia Abubakr kuwa Mtume (s.a.w.w). alimpatia zawadi na hivyo amrejeshee.Na katika kuthibitisha hivyo,Imam Ali (a.s) alitoa uthibitisho wake na hapo ndipo Abubakr alitaka kuletwa mashahidi wengineo.Ummi Aiman alitoa shahada katika dai la Bi.Fatimah (a.s) Hapo Abubakr alimwambia Bi.Fatimah (a.s) kuwa "unaelewa vyema kuwa ushahidi haukubaliki hadi kuwepo na ushahidi wa wanamme wawili au mwanamme mmoja na wanawake wawili." Hapo Bi.Fatimah (a.s) alirudi na kunijulisha hayo. Ruh al-Karabisi amenakili kwa mlolongo wa walioripoti kutoka kwa Jaafer ibn Muhammad kuwa amesema kuwa Bib.Fatimah az-Zahra (a.s) alimwambia Abubakr amrejeshee Fadak kwani Mtume (s.a.w.w). alishamzawadia (hiba)Hapo Abubakr alidai aletewe mashahidi.Hapo Bi.Fatima (a.s) aliwaleta Ummi Ayman na Rubah,mtumwa wa Mtume (s.a.w.w). kutoa ushahidi nao walitoa ushahidi wa kuthibitisha dai la Bi.Fatimah (a.s) Hapo Abubakr alisema kuwa ushahidi huo utakubaliwa pale atakapo patikana mwanamme mmoja na wanawake wawili."

  "Ameelezea Ibn Aisha Maitami kutoka Himad bin Salmah,kutoka Muhammad bin Saib Kalbi ambaye kutoka kwa Abu Salha ambaye ameelezea kutoka kwa Ummi Haani ambaye ameripoti kuwa Bi.Fatimah az-Zahra (a.s) bintiye Mtume sa.w.w. alikwenda katika baraza la Abubakr na kumwambia 'utakapokufa wewe urithi wako ataupata nani?' Abubakr alijibu kuwa 'watoto na ahali yangu' Sasa je umekuwaje kuwa umechukua urithi wa Mtume (s.a.w.w). na unakatalia kunipatia mimi mustahiki wake? Hapo Abubakr alimjibu kuwa 'mimi sijachukua dhahabu au fedha katika urithi wa baba yako na wala sikuchukua hiki au wala kile.' Bi.Fatimah az-Zahra (a.s) alimwambia'kuna hisa katika Khaybar na Fadak ni zawadi na milki yangu' Hapo Abubakr alimwambia:" Ewe Binti wa Mtume (s.a.w.w).! Mimi nilimsikia Mtume (s.a.w.w). akisema kuwa Fadak ni kitu ambacho kinazalisha na kulisha ambapo Allah (swt) hunipatia humo riziki katika uhai wangu na pale nitakapofariki,itagawiwa Waislamu wote."
  (Futuh al-Bayaan. Allamah Abul Hasan Bilazuri,chapa ya Misri,uk.44-45)