read

5. Aina Za Zaka Na Viwango Vyake

Zaka imegawanywa katika makundi mawili
Zaka iliyofaradhishwa

Zaka iliyo Sunnah

Na Zaka iliyofaradhishwa pia imegawanywa katika makundi mawili:
1. Zaka ya mali

2. Zaka ya Mwili ( Zakati Fitrah )

Zaka iliyofaradhishwa inayo aina tisa za mali na aina nne za nafaka (ngano, Shayiri, tende na zabibu), aina tatu za wanyama (kondoo au mbuzi, ng’ombe na ngamia) na aina mbili za madini (dhahabu na fedha).

Mahisabu ya aina nne za nafaka:
1. Ngano, Shayiri, tende na zabibu zitastahiki kutolewa Zaka iwapo zitafikia kiwango maalum ambavyo ni Saa 300 au mann 280 Tabrizi na ni pungufu kwa mithqal 45 ambayo ni sawa na takriban Kiligramu 847 .

2. Na iwapo (ngano, Shayiri, tende na zabibu ) zinalimwa kwa umwagiliaji wa maji ya mvua au mito au kwa urutubisho wa ardhi (kama zilivyo baadhi ya mazao huko Misri) basi Zaka yake itakuwa ni asilimia 10 (10 %)

3. Na iwapo inamwagiwa kwa maji ya kisima basi Zaka yake itakuwa asilimia 5. (5%)

1. Zaka ya mali

(A). Zaka Katika Wanyamaviwango Vitano Ya Kondoo Na Mbuzi

1. Idadi yao iwapo arobaini (40) basi Zaka yake ni kondoo au mbuzi mmoja (1) na iwapo hawatafika arobaini basi hakuna Zaka.

2. Idadi yao iwapo mia moja na ishirini na moja (121) basi Zaka yake itakuwa ni kondoo au mbuzi wawili (2)

3. Iwapo idadi yao ni mia mbili na moja (201) basi Zaka yao itakuwa ni kondoo au mbuzi wanne (3).

4. Iwapo idadi yao ni mia tatu na moja (01) basi Zaka yao itakuwa ni kondoo au mbuzi wanne (4).

5. Iwapo idadi yao ni mia nne (400) au zaidi basi Zaka yao itakuwa ni kondoo au mbuzi mmoja kwa kila kondoo au mbuzi mia moja (1).

Viwango Viwili Vya Ng’ombe

1. Kiwango cha kwanza ni ng’ombe 30. Iwapo mtu atakuwa na ng’ombe 30 basi itambidi alipe Zaka ambayo ni ndama dume mmoja wa ng’ombe ambaye ameingia katika umri wa mwaka wa pili. Na iwapo watapungua ng’ombe chini ya 30, basi hawatakiwi kulipa Zaka.

2. Kiango cha pili ni ng’ombe 40 na Zaka yake ni ndama jike wa ng’ombe ambaye ameshaingia katika mwaka wa tatu .

• Iwapo mtu atakuwa na ng’ombe kati ya 30 na 40 (mfano ng’ombe 39) basi anatakiwa alipe Zaka za ng’ombe 30 tu.

• Na iwapo anao ng’ombe 60 basi atalipa Zaka ya ndama 2 ambao wameingia katika mwaka wa pili.

• Na iwapo anao ng’ombe 70 basi atalipa Zaka ya ndama 1 ambaye ameingia katika mwaka wa pili na ndama jike mmoja ambaye ameingia katika mwaka wa tatu.

• Kwa kila idadi itakavyoongezeka basi itabidi kupigia hisabu kwa 30 au 40 na Zaka itatolewa hivyo.

Viwango 12 Vya Ngamia

1. Iwapo mtu atakuwa na ngamia 5 basi Zaka yake ni mbuzi au kondoo mmoja. Iwapo idadi ya ngamia 5 haitafika basi hatatakiwa kulipa Zaka.

2. Ngamia 10 na Zaka yake ni mbuzi au kondoo 2

3. Ngamia 15 na Zaka yake ni mbuzi au kondoo 3

4. Ngamia 20 na Zaka yake ni mbuzi au kondoo 4

5. Ngamia 25 na Zaka yake ni mbuzi au kondoo 5

6. Ngamia 26 na Zaka yake ni ngamia mmoja ambaye ameingia mwaka wa pili

7. Ngamia 36 na Zaka yake ni ngamia mmoja ambaye ameingia mwaka wa tatu

8. Ngamia 46 na Zaka yake ni ngamia mmoja ambaye ameingia mwaka wa nne

9. Ngamia 61 na Zaka yake ni ngamia mmoja ambaye ameingia mwaka wa tano

10. Ngamia 76 na Zaka yake ni ngamia wawili ambao wameingia mwaka wa tatu

11. Ngamia 91 na Zaka yake ni ngamia wawili ambao wameingia mwaka wa nne

12. Ngamia 121 na Zaka yake itahesabiwa ama kwa makundi ya ngami 40, na atatoa Zaka ngamia mmoja aliyeingia mwaka wa tatu na kila kikundi cha ngamia 50 atatoa ngamia mmoja aliyeingia mwaka wa nne.

(B). Viwango 2 Vya Dhahabu Na Fedha

(B). Viwango 2 Vya Dhahabu Na Fedha 1

Viwango 2 Vya Fedha

1. Kiwango cha kwanza ni Mithqaal 105, sawa na uzito wa Gramu 483.88 na kama fedha hiyo imebadilishwa katika sarafu kwa ajili ya kufanyiwa biashara na zimewekwa mahala kwa muda wa mwaka mmoja basi Zaka yake itakuwa ni asilimia 2.5 (2.5 %) Na iwapo kiwango hicho kitapungua basi hakuna Zaka itakayolipwa.

2. Kuongezeka kwa Mithqaal 21 katika Mithqaal 105 zikawa jumla ya Mithqaal 126, basi itambidi alipe Zaka ya Mithqaal 126. Na iwapo itakuwa chini ya Mithqaal 126 (kama haitafikia Mithqaal 21) basi itambidi alipie Zaka katika Mithqaal 105. Hivyo itambidi alipe sehemu 1/40 ya jumla. Lakini lazima iwe imefikia Mithqaal 21 na kama itapungua basi kiwango hicho kitabaki kilipofikia. Mfano iwapo mtu atatakiwa kulipia Mithqaal 110 basi yeye atalipia Mithqaal 105 ambayo ni sawa na 2.5% (au 2.625 Mithqaal) na mara nyingine itambidi alipie Mithqaal 5zilizozidi ambayo si faradhi.

Viwango 2 Vya Dhahabu

1. Kiwango cha kwanza ni Mithqaal 20 (Shar’ee) katika sura ya sarafu zitumiwazwo katika kufanyia biashara na zikakaa kwa muda wa mwaka mmoja mahala moja bila kutumiwa ambapo Mithqaal 1 ni sawa na uzito wa 3.456 gramu na hivyo inapofikia kiwango cha 20 Mithqaal (ispofikia hivyo, hakuna Zaka) inambidi mtu alipe Zaka kwa kiwango cha sehemu 1/40 ambayo ni sawa na uzito wa 1.728 gramu.

2. Kiwango cha pili ni kule kunapoongezeka kwa dhahabu zaidi ya Mithqaal 20 Shar’ee, iwapo kutaongezeka Mithqaal 4 Shar’ee juu ya Mithqaal 20 Shar’ee basi inambidi mtu alipe Zaka kwa kiwango chote kwa ujumla kwa kiwango cha 2.5% na iwapo kiwango cha nyongeza kitakuwa ni pungufu ya 4 Mithqaal basi Zaka italipwa kwa 20 Shar’ee Mithqaal tu na haitamlazimu kulipia Mithqaal iliyozidi ambayo ni pungufu ya 4 Mithqaal.

2. Zakat-I-Fitrah

Mtu yeyote yule ambaye katika usiku wa kuamkia Idd-ul-Fitr ( usiku wa kuamkia tarehe mosi ya Mwezi mtukufu wa Shawwaal ) baada ya kuzama kwa jua akabalehe, akawa na akili timamu na ghanii ( yaani ambaye anajitimizia mahitaji yake ya dharura ya kila mwezi, huitwa ghanii, yaani si mwenye dhiki ) basi ni faradhi juu yake na kutoa Zakat-i-Fitri yake binafsi na wale wote wanaomtegemea kimaisha na kichakula hata wale watoto wachanga wanaonyonya na vile vile kama kutatokezea mgeni basi awalipie nao pia.
Kiwango cha Fitrah ni Sa’a imoja ambayo ni sawa na kiasi cha kilogramu 3 za ngano, zabibu, tende, mchele au choc hote kile anachokitumia yeye kama chakula chakecha kila siku na itambidi awape wale wanaostahiki au anaweza kutoa thamani yake kifedha, nayo inafaa.
Tukumbuke kuwa faida ya papo hapo ya fitrani kule kubakia katika kunusurika na mauti ambazo si za kawaida kama vile ajali n.k. na imeripotiwa na Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) kuwa:
wakili wake wa matumizi kuwa aende akatoe Zakat-i-Fitrah ya wananyumba yake wote bila hata ya kumsahau mmoja wao kwa sababuiwapo hatatoa Zaka yao basi atakuwa na hofu ya kufa kwao na thawabu zake ni sawa na kukubaliwa kwa saumu za mwezi mzima.

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) amesema:
“Zakat-i-Fitrah inakamilisha saumu za mwezi Mtukufu wa Ramadhani.”

  • 1. Viwango hivi vimeletwa mbele yenu kwa kimukhtasari tu ili kuweza kuwapa mwanga juu ya masuala haya na hivyo inatubidi sisi turejee vitabu vya Fiq-hi ili tuweze kujua hukumu za Shariah kwa undani zaidi katika masuala haya na mengineyo.