Dua ni ulingano ambapo mja hudhirisha ufukara, unyonge na udhaifu wake kwa Mola Mkwasi, Mwenya kumiliki kila kitu. Mja huinyosha mikono yake mitupu kwa unyenyekevu na unyonge, na kutaka msaada kutoka kwa unyenyekevu na unyonge, na kutaka msaada kutoka kwa Mkamilifu Muumba Mwenye uweza juu ya kila kitu, Mwingi wa huuma na ukarimu, Mwenye kusikia maombi ya kila anaemuomba. Dua ni lugha ya mapenzi na ni chimbuko la mahaba ya mja kwa Mola wake na ndiyo taa ya waliyo kizani na ni tulizo la wanaohangaika.