read

Asili Ya Hadith

Muhammad Bin Sanah anasimulia kwamba Mufazzal Bin Umar alimsimulia hivi :

"Siku moja baada ya Sala ya Alasiri nilikaa baina ya Mimbari na Kuba la Mtukufu Mtume (s.a.w.) nikitafakari juu ya ukubwa wa vyeo vitukufu, ambavyo kwamba Allah (s.w.t.) amenijalia Maulana Bwana wetu Muhammad Mustafa (s.a.w.) ambavyo kwa ujumla Ummah ulikuwa hauna habari wala kwa ule ukubwa wa fadhila wala kwa sifa zake zilizo kamili wala kwa utukufu wake wa pekee.

Nikiwa nimezama katika kuwaza huko, mara alitokea Bin Abi Al Auja, kafiri mshirikina na akakaa umbali wa kuweza kumsikia. Sahiba wake alimfuata na akakaa kwa utulivu ili kusikiliza.

Bin Ali Auja alianza mazungumzo kwa kusema, "Mwenye Kuba hili amepata fadhila kubwa za pekee kwa ukamilifu wa heshima kuu katika yote aliyoyafanya." Sahaba wake aliongeza kwa kuthibitisha akasema: "Alikuwa filossofa na alifanya dai kubwa likiungwa mkono na miujiza ambayo kwamba ilishangaza akili za kawaida. Waliojifanya ni wenye hekima walizama kwa undani wa vina vya akili zao kupenya kwenye maajabu hayo (ili kuyajua) lakini bila mafanikio.

Ujumbe wake ulipokubaliwa na watu wastaarabu, wenye maarifa na wasomi watu kwa ujumla waliingia katika imani yake makundi kwa makundi. Sehemu za ibada na Misikiti ya sehemu zote ambako popote ulipofika wito wa utume wake ulianza kusikika kwa nguvu na kueleweka pamoja; na jina lake (kutajwa) sambamba na lile la Allah (s.w.t.) bila ya tofauti yoyote ya bahari na bara, mlima na tambarare, bonde, siyo mara moja lakini mara tano kwa siku wakati wa Adhana na Iqamah. Lilipata jina lake (limepata) kuambatanishwa na lile la Allah (s.w.t.) na maelezo yenye lengo la kuendeleza kumbukumbu yake na kuuweka ujumbe wake uwe ni wenye elimu ya kuendelea."

Bin Ali Auja akasema: "Weka kando habari za kumtaja Muhammad (s.a.w.) ambaye kuhusu yeye, akili yangu ina shangazwa vikubwa na mawazo yangu yamefadhaishwa.

Hebu tuongelee ukweli katika msingi wa watu kukubali imani ya Muhammad (s.a.w.) - Mwenye Rehema kwa ulimwengu. Je, kuna kiumbe wa namna hiyo au hapana?"

Kisha alirejea katika asili na uumbaji wa mpangilio mkubwa wa ulimwengu. Alifanya dai lisilosadikika kwamba hakuna aliyeviumba na hakuna Muumba, wala Msamii wala Mtengenezaji - Ulimwengu umejitokeza wenyewe. Katika kuwepo na ataendelea kuwepo na kwa hiyo hauna mwisho."

Nilijisikia vibaya umno kusikia hivi na nikamwambia : "Ewe usiye amini! Huwamini katika imani ya Allah (s.w.t.) kwa kukanusha moja kwa moja kuwepo kwake ambaye amekuumba wewe katika umbo zuri, akakugeuza kutoka hali moja kwenda hali nyingine, mpaka ukafikia katika umbo ulionalo sasa? Lau ungejifikiria wewe mwenyewe na lau akili zako nzuri zingekusaidia kiukweli, ungeweza kutambua katika nafsi yako mwenyewe hoja hizi za wazi za kuwepo kwa Allah Mtukufu Ishara ya vitu vyake vyote anavyoviruzuku na ushahidi wa Usanii wake usio na mipaka.

Alisema, "Tutajadili suala hili kama utapanga kwa utaratibu misingi ya kusadikisha hoja ambazo tutazikubali, vinginevyo huna haki ya kutia maneno yasiyo kuwemo bila ujuzi wa majadiliano. Kama wewe ni mfuasi wa Ja'far Bin Muhammad (a.s.) haikupasi wewe kuzungumza katika tabia ambayo unaifanya kwani yeye si mwenye mtindo wa kuzungumza hivi wala habishani na sisi katika hali ya utovu wa adabu namna hii. Amesikia zaidi maneno yetu kuliko ulivyofanya wewe, lakini kamwe hajatumia maneno yoyote yasiyo adabu, wala kamwe kujibu kwa ukali kuanzisha ugomvi. Ni mwenye kuvumilia sana, mwenye heshima, mwenye akili (za kuhoji) na mwanachuoni aliyepevuka.

Yeye kamwe si mkali wala si mwenye hasira. Anayasikiliza maneno yetu kwa usikivu sana. Huvuta hoja zetu kiasi kwamba wakati tunapomaliza kabisa silaha zetu (hoja) na kufikiri kwamba tumemnyamazisha yeye kwa maneno machache huibuka tena, kuyavunja maoni yetu yote na kutufanya kuwa mabubu hivyo kwamba tukaachwa bila kuwa na uwezo wa kujibu hoja za Mtukufu Mstahiki. Kama wewe ni mfuasi wake, basi zungumza nasi katika tabia hiyo hiyo.

Kwa hili, nilitoka nje nikiwa na huzuni mno na mawazo tele kwasababu ya kutokuamini kwao katika Allah (s.w.t.) na matokeo ya huzuni na majonzi ya Uislamu na Wachaji wake, kwasababu ya kutokuamini kwao na usahifi usio na maana wa ulimwengu huu.

Nilikwenda mwenyewe kwa Bwana wangu, Imam Ja'afar Al Sadiq (a.s.). Aliponiona nimehuzunika, aliniuliza sababu ya kuwa hivyo. Nilimsimulia mazungumzo ya wale mushirikina na jinsi nilivyo jaribu kuoenyesha uongo wa hoja zao.

Aliniambia nije siku inayofuatiya (yaani kesho yake) wakati atakapo weka wazi kwangu ustadi mkubwa mno wa mwenye nguvu zote msanifu aliyedhihirika katika ulimwengu wote ulio na wanyama, na ndege, wadudu, vitu vyote vilivyo hai ama viwe ni wanyama au jamii ya mimea, miti izaayo matunda au dufu na ile isiyo na matunda, mboga zinazolika na zisizolika - maelezo ya kiustadi yatakayokuwa kama kifungua macho kwa wale ambao watakubali maelekezo; faraja kwa waumini na fadhaa kwa wazushi.

Niliposikia haya, nilirudi kutoka sehemu yake tukufu nikiwa katika hali ya furaha. Ujio wa usiku ule ulionekana kuwa mrefu kwasababu ya shauku yangu kubwa ya kujifunza kutoka kwa Mwanachuo mstahiki huyo, mambo aliyoahidi kuyaeleza kesho yake.