read

Baraza La Nne: Maafa Ya Kawaida

Maafa Ya Kawaida

Baada ya Sala za kawaida na kumshukuru Mwenye Nguvu zote Allah, Imam (a.s.) alisema, "Ewe Mufazzal! Nimekupa maelezo kwa kinaga hoja kwa kufafanua zaidi na uchunguzi kuhusu mpango halisi na Usanii kuhusiana na wanadamu, wanyama na ufalme wa mimea. Inapasa itoshe kwa njia ya mafunzo kwa wote ambao wanatamani mwongozo.

Sasa nakupa maelezo kamili ya majanga na machafuko ambayo hutokea kwa nyakati na ambayo hawa watu wajinga husimamia kama hoja kwa ukano wao wa uumbaji na Usanii wenye dhumuni wa Muumba.

Nitaelezea vilevile kwa undani zaidi hekima iliyomo kwa kuletwa matatizo na machungu ambao walahidi na wafuasi wa dhehebu la Manichean wanakana na vile vile nitatoa maelezo kuhusu kifo na maangamizi ambayo madhehebu hizi wameyaleta kwenye mjadala, na wachunguzi wa zamani wa viumbe walivyosema.

Misiba Ya Asili

Watu hao wamesema ulimwengu huu umejitokeza na kuwepo kwa bahati tupu, hivyo basi maelezo haya yatakuwa ni yenye kutupilia mbali hoja zao. Allah (s.w.t.) awaangamize - kulioje kupotezwa kwao. Baadhi ya watu wajinga wanatafsiri matukio haya ambayo hutokea wakati kwa wakati, kwa mfano milipuko ya maradhi ya kuambukiza, kutokuwepo kwa "Chlorophyll" (Klorofil) ya miti, mvua za mawe, nzige, kama hoja ya ukano wa dhumuni la uumbaji wa Muumba.

Jibu kwa hili ni kwamba kama hakuna Msanii wa ulimwengu huu, kwa nini hakuna machafuko makali zaidi, kama kwa mfano mvurugiko kamili wa ulimwengu wote, kupasuka kwa ardhi, ukomo wa kuchomoza jua, ukaukaji wa maji katika makalio ya mito ivyo kutoacha hata tone la maji kuweza kulowesha midomo, hewa kusimama tuli na kupelekea kwenye mvurungiko wa mpangilio wa mambo, kusambaa kwa maji ya bahari kwenye ardhi na kuizamisha. Nani analinda matukio yote haya? Ni nani mpangaji wa mandhari hizi?

Wakati usemapo kwamba kama kungekuwa na Msanii na Muumba, Kundi kama hili la nzige lisingetufikia kusababisha madhara makubwa hivi, milipuko ya magonjwa haya ya kuambukiza yasingechukua kiwango kikubwa cha mamilioni ya maisha ya watu, mvua za mawe zisingekuwa kubwa na uzito hivyo hata mpaka kuharibu mashamba yetu ya nafaka. Ikiwa yote haya ni katika hakika ya mambo, kwa nini ulimwengu huu usipate kuvurugika katika taratibu za uumbaji na kupelekea kwenye uangamizi wa ulimwengu wote? Kwa nini bahari isizamishe ardhi kwa maji yabubujikayo? Kwa nini hewa isisimame na kutulia tulii na hivyo kusongeka kwa viumbe hai vyote? Kwa nini yote haya yasitokee?

Hii huonyesha kwamba Msanii yupo, ambaye huzuia tukio kama hilo ili kwamba ulimwengu usije chafuka na kuharibika wala jamii kuja kutoweka wala uharibifu kabisa wa jumla usitokee. Kinachotokea ni kwa njia ya kawaida ya matokeo kutokana na matendo ya mtu mwenyewe, ni onyo la kujizuia na maovu yafanyikayo mara kwa mara katika hali ya milipuko ya magonjwa ya kuambukiza, nzige, kuangamia kwa nafaka na mashamba, mvua za mawe n.k. Huu ni ukano wa hoja dhidi ya uumbaji wa kidhumuni. Nawauliza kwa nini hii milipuko ya magonjwa ya kuambukiza na makundi ya nzige hayaendelei moja kwa moja hivyo ili kuungamiza ulimwengu? Hufika mara chache, na baada ya muda, huondoka.
Je, huoni kwamba huu ulimwengu umehifadhiwa dhidi ya misiba hii ya kutisha na machafuko? Kama mojawapo lolote katika matukio haya lingetokea katika ulimwengu huu, ungeharibika kabisa moja kwa moja. Majanga haya hutukia mara chache, katika hali ya ukali uliopunguzwa ili tu kuwaonya watu na kuzirekebisha tabia zao kuwa nzuri.

Hayadumishwi bali huondolewa kama na wakati mtu apatapo fadhaa kuhusiana na usalama wao. Majanga haya hutukia kama onyo na kuondolewa kwa Rehema za Ki-Ungu.

Maisha Huria Bila Matatizo

Kama vile waumini wa dhehebu la Manichean wametia shaka ustahiki wa majanga haya na matatizo ambayo huwapata watu, katika njia hiyo hiyo walahidi wameshindwa kuelewa ukweli wa asili yao na kuyaelezea kama yasio na maana. Wote kwa pamoja wanasema kwamba kama ulimwengu ungeliachwa na Mwenye Huruma, Mpole na Muumba, Mwenye Rehema, Matokeo haya ya kuchukiza yasingelitokea. Ambaye kwamba amesimamisha hoja hii anajaribu kutanabali kwamba ingelikuwa bora kama maisha ya mtu katika ulimwengu huu yangekuwa huria bila ya matatizo.

Ingekuwa hivyo, kiburi cha mtu na uchoyo vingempelekea kwenye tabia ambayo isingekuwa katika ulinganifu na dini au maisha yake ya dini. Kama vile unavyoona watu wamelelewa katika anasa na wasaa (faraja) na ambao wengi wao kabisa wanasahau utu wao na hali yao ya kuwa wamelelewa na kukuzwa na mtu fulani. Wanasahau kwamba wanaweza kupata maumivu fulani au huzuni au kwamba misiba fulani inaweza kuwapata. Hata husahau iwapo kuna kuwahurumia watu wanyonge au kuwasikitikia watu wenye kuhitaji. Hawako tayari kuongozwa kuhisi kusikitika kwa matatizo ya watu wengine au kuhisi kuhurumia juu ya wanyonge au kuonyesha upendo kwa nafsi zenye matatizo.

Wakati, hata hivyo, matatizo yanapowapata, huhisi uchungu wake na hapo akili hufunguka wanazindukana kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko katika ukadiri ya ujinga wao na upumbavu. Wanaanza kutenda katika njia ambayo iliwapasa juu yao wakati wote. Kama matatizo haya yasingewapata, wangeendelea kujiona kama waungu (na) kuendesha maisha yao katika hali ya kiburi, kutokuwa na masikitiko au huruma na mtu yoyote yule. Je, tabia kama hii ingekuwa ni yenye faida kwa dini yao na ulimwengu huu? Hakika sivyo! Pamoja na dini potofu wangepata madhara ya kilimwengu. Watu wangewachukia na kuwalaani. Watu wachoyo kama hawa wangesababisha mchafuko katika ulimwengu huu katika mambo yote, kazi biashara, elimu na tabia ya wao kwa wao n.k.

Watu wanaokana mambo haya, wakiyaona kama yasiyo na maana, ni kama wale watoto wadogo ambao wanalaumu dawa vhungu na isiyo pendeza na kuchukizwa na tahadhari dhidi ya vyakula vyenye madhara. Hawataki kazi, na hupenda kucheza tu huria (bila kuzuiwa) hupenda kujiingiza katika mambo ya kipumbavu, kula na kunywa bila pingamizi au kizuizi. Hawajui kwamba ruhusa kama hii na uvivu kutadumaza ukuaji wa akili zao, uadilifu wao na miili yao, kwamba vyakula hivi vya kumezeka lakini vyenye madhara vinaweza kupelekea kwenye mateso tofauti tofauti na magonjwa. Uboreshaji wao umo katika upatikanaji wa elimu, na dawa zina faida nyingi kwao mbali na huko kutokumezeka kidogo.

Wanasema ni kwa nini watu hawakupewa tabia ya kutokufanya dhambi ili kwamba Mwenye Nguvu zote Allah hangehitajika na kuwatia adabu kwa uchungu wa matatizo. Jibu kwao litakuwa kwamba katika hali hii mtu hangekuwa na thamani ya itibari (sifa) yoyote kwa uzuri wala kupasika na malipo kwayo.

Kama wataendelea kusema zaidi kwamba kuruhusiwa kila aina ya anasa na wasaa (faraja) lingekuwepo wapi dhara lolote humo kama hangepata itibara au malipo kwa wema wa uzuri wake? Jibu litakuwa ni kulifikisha swali hili kwa mtu mwenye akili timamu na mwenye siha nzuri na kumwambia akae tu bila kufanya kazi, na kumhakikishia ukamilifu wa mahitaji yake yote bila juhudi zozote. Kisha tazama kama akili yake itakubaliana na hilo. Utamwona kuridhika zaidi na kutosheka kwa kidogo apatacho kwa juhudi yake kuliko kupata kikubwa na kingi ambacho huja kwake bila stahiki, pasipo kukifanyia juhudi. Kadhalika baraka za Akhera (ulimwengu ujao) zitakuwa zenye tabia ya namna ile ile kwao ikiwa tu kama zimepatikana kwa juhudi.

Kwa hiyo mtu anaruhusiwa boma mbili za baraka. Kwanza kabisa kupata ujira mkubwa kwa juhudi zake katika ulimwengu huu wa sasa (dunia). Pili, ameonyeshwa njia za kuitafuta kwa juhudi zake ili kwamba apate ridhio la kiwango cha juu sana kwa fanikio hilo. Ni kawaida kabisa kwa mtu kutokuruhusu kukipa thamani kitu chochote kilichopatikana bila juhudi au haki. Kinyume chake, chochote apatacho kwa matokeo ya juhudi na haki, hukiwekea bohari kubwa. Na kwa hali hiyo, baraka za Mwenye Nguvu zote Allah ambazo zitawekwa juu yake kwa wema wa kujizuia kwake ndani ya mipaka iliyoamriwa zitakuwa bora zaidi kithamani kwake kwa mlinganisho, na hali ya akili ambapo hakuwa ni mwenye kuzuia tamaa zake mbaya na kila kitu kilicho haramu kimekoma kuwa na mvuto kwa ajili yake. Katika haki hii, baraka za Akhera zilizowekwa na Mwenye Nguvu zote Allah zisingekuwa na thamani hivyo kwake. Malipo ambayo kwamba atapata kwa matokeo ya juhudi ya nguvu zake na chumo yatakuwa ya thamani kubwa sana kwake.

Kama sasa wanasema iwapo haitokei hivyo kwamba baadhi ya watu wamependezwa sana kupata baraka bila haki yoyote, kwa hiyo, hoja gani italetwa juu ya kadhiaa hizi kwa watu ambao watahisi kupendezwa kwa kupata baraka za akhera?

Jibu litakuwa kwamba hili ni somo kwamba watu watashawishika kwalo, kwamba watapata baraka za Akhera bila juhudi itapelekea kwenye namna zote za madhara yaliyoletwa makusudi, hali ya kutenda dhambi, ushukaji wa uadilifu na uovu. Nani basi angejizuia kutokana na uovu wa uadilifu au kufanya juhudi kuwa na tabia njema wakati kwamba ameshajijua mwenyewe kama mpokeaji mstahiki wa baraka za Akhera? Nani angekuwa na hakika ya hatua ya maisha, heshima na mali yake mwenyewe na ya ahali wake kuhsu madhara ambayo watu wangefanya kama kungekuwa na hofu ya adhabu na kisasi? Uharibifu kwayo ungesababishwa katika maisha haya ya sasa kwa watu kabla ya siku ya mwisho (ya ulimwengu huu).

Haki na ustadi vyote vingetupwa. Ingetiliwa shaka kama ukosekana taratibu huku na mchafuko kungeingia kwenye usanii.

Vile vile huzungumzia matatizo na usumbufu ambao wakati mwingine yana matumizi ya jumla yakiwaumiza na watu wema na kupelekea watu waovu bila kudhurika. Wanasema, itawezekana vipi kuwa Usanii wenye kufaa wa Mwenye kujua yote, hoja gani unaleta?

Jibu kwa hili itakuwa kwamba matatizo kama haya huwapata wote wema na waovu/wabaya na kuna faida kwa makundi yote zilizoamriwa na Mwenye Nguvu zote Allah. Wema huteseka kwa matatizo na usumbufu mwingi na malipo ya baraka kwao husababisha shukurani na Wokovu ndani yao.

Na kwa watu waovu matatizo yao huanza kutokea kutokana na tabia ovu. Iko faida ya uboreshaji kwa wale wote ambao wangeepushwa kutokana na kishindo cha matatizo haya.
Mbali na makundi mawili haya, kwa watu wema hali ya uzuri ni chanzo cha furaha na kishawishi zaidi na utambuzi wa uendeleaji wa tabia njema zaidi. Kwa wafanya maovu pia hifadhi dhidi ya madhara ni fadhila maalumu kutoka kwa Mwenye Nguvu zote Rehema za Allah zinaonyeshwa kwao bila ya wao kujistahiki. Hii huwavuta wawe wapole na kuwasamehe wale ambao hufanya ubaya kwao.

Mkinzani anaweza kusema kwamba matatizo kama haya huangukia mali zao, bado wakati mwingine miili yao huteseka hata kuangamia, kama vile kuunguzwa, kufa maji, kuchukuliwa na mafuriko au kuzikwa ungali hai.

Jawabu kwao litakuwa kwamba Mwenye Nguvu zote Allah ameamuru ndani yake uzuri wa makundi yote. Kwa watu wema kwa sababu ya kuutoka ulimwengu huu na matatizo yake na mauchungu yake, na kwa watu waovu ni kwamba uwezo wao wa kufanya dhambi kwayo huondolewa.

Kwa muhtasari, Mwenye Nguvu zote Allah hugeuza matokeo ya matendo yote haya kwa kujua kwake yote na Mwenye Enzi Kuu na kuelekeza wenye uboreshaji, kama vile mti unapoangushwa chini na upepo, seremala mzuri huugeuza kwa matumizi yenye faida.

Kadhalika, Mwenye Nguvu zote Msanii hugeuza matokeo ya maafa haya ambayo huzipata mali zao na miili yao kwa faida zao na uboreshwaji wao. Kama mtu atauliza kama ni kwa nini misiba hii iwapate watu, jibu litakuwa, wasije wakageukia kwenye hali ya kutenda kwa sababu ya kipindi kirefu cha Usalama, wasije watenda maovu wakajiingiza moja kwa moja katika hali ya kufanya madhambi ambapo watu wema wakawa ni wenye kuzembea katika kufanya mema.

Aina zote hizi za tabia huwazidi nguvu watu wakati wanapopewa muda mrefu wa starehe na faraja. Matukio kama haya huwafanya kuonyeka na kuwaepusha kutokana na tabia hizi - na ndani yao muna uzuri kwao.

Kama wangeondolewa matatizo moja kwa moja, wangevuka mipaka ya kufanya dhambi kama vile walivyofanya watu wa nyakati zilizopita hivyo kwamba ilibidi wateketezwa kwa dharika kuisafisha ardhi kutokana nao.

Kifo

Kuna nukta moja imefungwa kwenye akili za wakanushaji hawa wa Usanii na dhumuni, kuitaja ni, kifo na uharibifu. Wanafikiri kwamba ingekuwa sawasawa kama mtu angepewa hai wa milele bila tatizo lolote au dhara.

Ni muhimu kuchukua hoja hii na kuipeleka kwenye mwishilizio wa kihoja ili kuona kwamba inapelekea kwenye maokeo gani. Hebu tazama kwamba kama watu wote, wangeishi maisha ya umilele, ardhi hii ingekuwa finyu sana kwao; wasingepata nafasi ya kutosha kwa makazi yao, kilimo chao na mahitaji ya riziki kwa kuendeshea maisha yao. Ijapokuwa shoka la kudumu la kifo linafanya kazi wakati wote, wakati ambapo kuna migongano kuhusiana na makazi na mashamba ya nafaka, hata vita hupiganwa na damu kumwagwa juu ya suala hili. Ingekuwa vipi hali yao kama asingekufa hata mtu mmoja wakati uzazi wa watu wapya unaendelea? Sasa hivi hata ingawa vifo vinaendelea, tunayo matatizo haya.

Je, kungekuwa na hatari za namna gani kama daima asingekufa hata mtu mmoja? Watu wangezidiwa nguvu kwa choyo, tamaa mbaya na ugumu wa nyoyo. Kama wangehakikishiwa uhai wa umilele, hakuna ambaye angetosheka na anavyomiliki. Hakuna ambaye angekubali kutoa chochote kwa wenye kuhitajia (mafukara na masikini), wala kusingekuwa na faraja baada ya msiba. Wangechoshwa na maisha na mambo yote ya ulimwengu. Mtu mwenye maisha marefu huchoshwa nayo, hutamani mno kutokewa na kifo na kupata afueni.

Wanasema kwamba ingepaswa iamriwe kwamba matatizo yote na maradhi yangeondolewa kutoka miongoni mwao, hivyo kwamba wasingependelea kukiomba kifo wala kuwa ni wenye kukitamani. Jibu kwa hili ni kwamba wangetumbukia kwenye njia za uovu na utovu wa utii.

Kama wakisema kwamba kuondoa fadhaa na upungufu wa nyumba na hali (mbaya) za maisha, uzazi wao ungesimamishwa, jibu litakuwa kwamba katika hali hiyo idadi isiyoelezeka ya viumbe ingekoseshwa fursa ya kuingia katika ulimwengu huu na hivyo kukoseshwa baraka za Mwenye Nguvu zote Allah katika uhai wa ulimwengu huu na wa Akhera, ikiwa kizazi kimoja kingeruhusiwa kuingia bila uwezo wa uzazi zaidi.

Na kisha wangesema kwamba Yeye (s.w.t.) angeliumba watu wote,wale waliozaliwa na wale watakaozaliwa katika siku zijazo, katika mkupuo mmoja.

Jibu kwao litakuwa, kama lilivyokwisha elezwa tayari, kwamba matukio yatajitokeza kama vile upungufu wa nyumba na njia za Kilimo. Wapi nafasi ya kutosha ingepatikana kwa kjengea nyumba, kuendeshea kilimo, kuanzishwa kwa mawasiliano. Katika hali hiyo kutokuwepo kwa mahusiano ya kijinsia (kwa ngono), kusingekuwa na faida za kujamii (umma) niongoni mwa jamaa na ndugu, hakuna msaada wa wao kwa wao katika nyakati za shida na huzuni. Wapi ingepatikana furaha ya mzazi katika kuwalea watoto?

Hii huonyesha kwamba upande woote mawazo yasogeavyo mbali kutoka Usanii wa kidhumuni, huhakikisha kuwa siyo wa kuthibitika ni upumbavu na upuuzi.

Dhuluma

Mkinzani anaweza, pengine, kuleta pingamizi kutoka nukta nyingine ya mtazamo na kusema kuwa vipi itaweza kujulikana kwamba kuna Muumba na Msanii, wakati tunaona katika maisha mtu mwenye nguvu akijitwalia kila kitu, mwenye nguvu kumkandamiza mnyonge, wakati ambapo mnyonge anaonewa na anatukanwa. Wema ni windo la taabu na matatizo wakati mwovu mno ni mwenye afya na tajiri. Yule ambaye haheshimu kanuni na kawaida haadhibiwi kwa haraka.

Kwa hayo inamaliziwa kwa kusema kwamba kama kungekuwa na Usanii ueneao na kuujaza ulimwengu wote, shughuli zote zingeendeshwa sawasawa. Watu wema wangelishwa vizuri na wabaya na waovu wangepata hasara. Wenye nguvu wangezuiwa kuwakandamiza wanyonge. Mwenye kutenda uovu angepata adhabu haraka.

Jibu kwa hili litakuwa kwamba katika hali hii wema, ubora maalum wa mtu ungepoteza thamani yake. Vilivyobaki katika Uumbaji havina ubora wa ushawishi katika ahadi za malipo ya Mwenye Nguvu zote Allah na hivyo kutoa tamaa zao kwenye nidhamu ya tabia ya uzuri. Wao, katika hali hiyo wangekuwa kama wanyama wa miguu minne, ambao wako chini ya udhibiti kwa fito (fimbo) na uhitajio wa tumbo. Kwa wao daima ama huonyeshwa jambia, au hupewa ukoka kuwaweka katika mpango. Hakuna hata mmoja ambaye angetenda katika upasiko pamoja na ushawishi wa kupata jaha ya Kiroho au Jahannamu. Wangedhalilishwa na kushushwa daraja kutoka daraja ya ubinadamu kupewa ile ya unyama. Hakuna ambaye angejali baraka za Kiroho. Mtu angefanyia bidii shughuli za malipo ya mara moja ya wakati huo huo (papo hapo). Mtu mwema angetenda kwa kujipatia chakula tu na kwa mali za kilimwengu, wakati mtu mwovu angejizuia kutokana na ukandamizaji na uonevu kwa sababu tu ya hofu ya adhabu ya ghafla ya wakati kuo huo hivyo kwamba matendo yote ya watu yangevutwa katika hali ya papo hapo ya wakati huo. Kusingekuwepo na wazo hata la mbali sana kwa ajili ya malipo mema na adhabu zilizoamriwa na Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.) wala wasingepasika kwenye baraka za Kiroho za Akhera. Yote haya, yangepelekea kwenye hali mbaya.

Ijapokuwa, na yote haya, umasikini na ukwasi uliotajwa na mkizani haviko moja kwa moja mbali na ilivyokusudiwa. Ni ukweli kwamba kama watu wanavyofahamu watu wema pia hupata rasilimali za mali za ulimwengu huu, hivyo kwamba watu wasije wakadhania kwamba ni wasioamini tu (Makafiri) ndiyo waliopendelewa nayo, hali ya kwamba watu wema wamenyimwa starehe za maisha haya (ya dunia) wasije watu kwa ujumla wakajichukulia tabia ya ujeuri. Unaona vile vile kwamba wajeuri wanaadhibiwa katika ulimwengu huu, wakati ujeuri wao unapovuka mipaka yote na watu wakadhurika mno kutokana na jeuri zao hizo, kama vile Firauni alikufa maji, Nebukadreza aliumbuliwa na Bilbis aliuwawa.

Kama katika maelezo ya baadhi ya Dhumuni la Maana sana, nje ya uwezo wa watu, baadhi ya waovu wanapewa raha kidogo au baadhi ya watu wema malipo yao yanaahirishwa mpaka siku ya baadaye, hakugeuzi kusudio na maana ya Usanii, kwani kadhia kama hizo hufanyika pia hata katika watawala wa ulimwengu.

Hii hata hivyo, haipunguzi nguvu ya sera. Kwa ukweli Kadhia hizi, wakati zinachelewesha, zinaonekana kuwa zenye ulinganifu zaidi na sera za utawala na ni zenye kuona mbali. Na kama ushahidi mzito wa kutosha wenye nguvu na mwishilizio kwayo yote haya yakalazimisha kwenye imani ya kwamba lazima kuwepo Muumba na Msanii wa vitu vyote vya ulimwengu huu, kitu gani kinaweza kumzuia Yeye (s.w.t.) kupanga uzuri kwa viumbe vyake? Hakuna akili ya mwanadamu iwezayo kudhania kwamba Muumba atauwacha Uumbaji wake hivi hivi tu (huria), isipokuwa iwe kwamba kwa ukosefu wa nguvu na uwezo, kwa ujinga au umakusudi, yote haya ambayo ni mageni kwa Usanii wa Allah Mwenye Nguvu zote. Allah (s.w.t.) Si Asiye na uwezo kwa uboreshaji wa Uumbaji Wake, wala Si Asiye na habari na hali zao, wala Allah (s.w.t.) aepushilie mbali, Yeye kimakusudi anapotoka.

Kushindwa kufanya vizuri kwa sababu ya kukosa nguvu na uwezo, ujinga na upunguani, kunaeleweka zaidi kama ilivyo kwamba asiye na nguvu na uwezo hana uwezo wa kuumba viumbe watakatifu hawa wa ajabu, mjinga hana utambuzi wa njia za maadili na ustadi wakati mkaidi hawezi kugeuka akawa kwenye Uumbaji Mtukufu huu wa kazi hii muhimu na ya ufundi mkuu.

Na mambo kuwa kama yalivyo, hueleweka kwamba Muumba wa ulimwengu atakuwa, kama jambo la kweli na sawa, aangalia kwenye uboreshaji wa Uumbaji wake ingawaje maana ya Usanii yaweza isitambulikane kwa watu kwa ujumla. Hata mamlaka za kiulimwengu hazifahamiki, ambazo kwa kuchunguza zaweza kuonekana sahihi wakati zikiwekwa kwenye kipimo.

Ikiwa una mashaka na asili ya dawa au lishe, na baada ya majaribio mara mbili au tatu asili yake ikawa dhahiri kabisa, je, hutaiondolea mashaka yote kuhusu asili yake kwenye akili yako?

Kwa nini basi usilipasikie jambo hili na kipimo? Kwa nini usitambue kwamba lolote linaloamriwa na Mwenye Nguvu zote Allah ni katika faida zilizo bora mno kuliko zote kwa viumbe vyake? Vipi basi kuhusu hawa watu wajinga, ambao mbele za ushahidi mzito huu, ambao hauwezi kukadiriwa hawawezi kuvutika na Muumba na Msanii wa ulimwengu?

Hata kama nusu ya ulimwengu na vilivyomo vingeonekana kuwa vimeharibika na visivyo na mpango, itakuwa hoja mbovu na elimu potofu. Kuufikiria kama usio na Dhumuni na Usanii, kwa kuwa nusu nyingine iko katika hali ya ukamilifu na uzuri, ambao huondoa mara moja neno lisilothibitika. Huwezekana vipi neno kama hili lisilothibitika likubaliwe kwa kuwa kila kitu katika ulimwengu kinaonekana kwa kuchunguzwa na uangalizi, kuwa vilivyopangwa na hali ya uzuri zaidi, kiasi hivyo kwamba hakuna kinachoweza kudhaniwa ambacho hakina mfano bora zaidi miongoni mwa Uumbaji wa Ki-Mungu.

Elewa kwamba ulimwengu unaitwa kwa jina la 'Cosmos', ambalo lina maana ya mapambo katika lugha ya Kiyunani, na Mafilosofa na wajifanyao wahenga. Imeitwa hivyo kwa sababu ya ukamilifu wa mpangilio. Kwa nini wasiuite Amri ya Ki-Mungu? Jina la 'Cosmos' huonyesha kwamba mpango mzuri wa maongozi ya Mungu yako kwenye msingi wa utashi na umaridadi.

Nashangazwa na watu hawa ambao wanaachilia makosa katika elimu ya uganga, ambayo ni yenye hitilafu sana, lakini huleta hoja za kutaka kujua mpango wa ulimwengu, ambao ni kamili bila waa (kosa).

Nashangazwa na mwenendo wa wadai wa filosofia, ambao hawana elimu ya utukufu wa Uumbaj na bado wanahoji utukufu wa Mwenye Nguvu zote Allah. Namshangaa hususan mtu huyu mwenye bahati mbaya na duni, Mani, ambaye anadai kuelewa maajabu ya elimu wakati ni mjinga halisi wa hoja za ubora mno wa Uumbaji, na hivyo kujitia kwenye kuhoji Hekima Kuu ya Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.) katika Kadhia ya Uumbaji.

Kuwepo Kwa Mwenyezi Mungu

Juu ya wote hao, Walahidi ni wa kuhurumiwa, ambao wanataka kumwona kwa macho yao Yule Ambaye ni fumbo hara kwa akili, wameamua kukana kabisa kuwepo kwake. Walidai kwa nini Hawezi kuzunguukwa ndani ya akili? Hushinda akili kama vile vitu vilivyo nje ya fani ya kuona, haviwezi kutambulika kwa macho.

Kama kwa mfano, unaona kipande cha jiwe kinapita juu angani (kimerushwa), mantiki ya maana utakayo chukuwa ni kwamba mtu fulani kalitupa juu. Jicho linaweza likawa halikuliona (likitupwa) na bado akili hutambua hivyo kwa sababu ya uwezo wake wa utambuzi, ya kwamba kipande cha jiwe hakiwezi kujirusha chenyewe juu angani. Unaona kwamba jicho limesimama katika hatua fulani na haliwezi kuendelea mbele. Kadhalika akili husimama ghafla katika mpaka wake ilioruhusiwa katika kadhia ya kuwapo pote kiroho. Haiwezi kuendelea mbele zaidi.

Tunasema, hata hivyo, kwamba akili ambayo hutambua kwamba mtu humiliki dhati na nafsi (roho), ijapokuwa ni ukweli kwamba hakuna aliyeiona dhati kwa macho ya umbo, akili hiyo hiyo yapasa kuwa na uwezo wa kufahamu na kukubali kuwepo kwa Muumba, bila kuwa na uwezo wa kutambua Nafzi Yake.

Na kama sasa wakiuliza kwa nini Ameweka wajibat (ulazima) juu ya mtu mdogo kupata utambuzi Wake kwa akili zake kwa kuwa hawezi kutambua Yeye kikamilifu, jibu litakuwa kwamba dai la kumtambua Yeye ni kwenye masharti kwa kiwango ambacho akili ya mwanadamu inaweza kufanya, kwa uwezo ilionao. Ni kuamini kuwepo Kwake na Kutii amri na makatazo Yake. Hawatakiwi kuzunguuka kuwepo Kwake Pote (kila mahali) na Sifa Zake. Hakuna mtawala atakaye raia zake wajue hali ya miliki na ukamilifu wake, Yote yale atakiwayo ni uaminifu na utii kwa sheria za nchi.

Wazia kwamba mtu atausogelea moango wa Ikulu ya Kifalme na kumtaka Mtawala ajitokeze kwake ili amjue kikamilifu, tena zaidi angeweza akaacha kumtii, hujiweka Mwenyewe wazi katika hatia. Kadhalika yeye ambaye hushurutia imani yake kwa Mwenye Nguvu zote Muumba kwa elimu kamili ya kuwepo Kwake Pote humchukiza Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.).

Na kama watauliza kuwa ni kwa nini ni mpungufu, jibu litakuwa kwamba dhana haiwezi kuruka kina cha utukufu wake na bado ijaribu kupata kimo kile ambacho ni nje ye uwezo wake, kwa kweli hata utambuzi wa vitu vya hali ya chini viko nje ya mpaka wake.

Jua hutoa kielelezo Kwayo. Unaliona hutoa mwanga kwenye ulimwengu wote na bado hakuna anayejua ukweli uliopo unaolihusu. Mna idadi ya mambo yasiyothibitika (yanayokubaliwa kwa ajili ya hoja tu) kulihusu (hilo jua) kwa maelezo hayo na kwa kuwa maoni tofauti miongoni mwa wanachuoni yapo kuhusu hilo.

Baadhi wanazema ni umbo Kimbinguni lenye uwazi ndani uliojaa moto unaotoa miali kutoka tundu mahsusi. Baadhi husema kwamba ni namna ya "nebula" (jamii ya nyota nyingi kama wingu). Baadhi wanasema liko kama kioo katika kimaumbile, lenye uwezo wa kuhifadhi joto na kisha kutapanya nuru yake ulimwenguni. Baadhi wanasema kwamba ni umbo nyororo kabisa lililotangamana na maji. Wengine wanasema kwamba asili nyingi mbalimbali za moto zimeungana pamoja.

Bado wengine wanathibitisha kwa maneno ya hoja tu kwamba ni ziada ya kitu cha asili kwa vile vingine vinne vya asili (ardhi, maji, hewa na moto).
Watu hawa wamehitilafiana (wametofautiana) miongoni mwao wenyewe kwa wenyewe kuhusu umbo lake (jua). Wengine wanasema liko bapa kama ukurasa (wa kitabu), wengine hulifikiria kama mpira usunguukao. Vile vile kuna tofauti kwenye ukubwa wake. Baadhi hufikiria kuwa sawa kwa ukubwa kama ardhi. Wengine wanafikiri ni dogo kwa ukubwa kuliko ardhi. Baadhi wanasema ni kubwa kuliko kisiwa hiki kikubwa mno (dunia). Watu wa elimu ya jometri (geometry) wanasema kwamba liko mara mia moja na sabini kwa ukubwa wa ardhi.

Inaonyeshwa na maelezo yanayokinzana ya watu hawa kwamba hawajui asili yake. Akili imekuwa haina uwezo wa kuelewa asili ya jua ambalo macho yanaweza kuona na akili kutambua, yawezekana vipi basi Nafsi Yake iwe ifahamike Ambaye ni nje ya weupe wa akili na kufichika kutokana na mawazo?

Kama wao, basi wanasema kwa nini Amefichika kutokana na mawazo, jibu litakuwa kwamba hakujificha kwa kitu kilichotengenezwa kama mtu anavyoweza kuwa nyume ya milango na mapazia kutokana na kuonwa (kuonekana) na watu wengine. Wakati tunaposema kwamba Mwenye Nguvu zote Allah haonekani kwa macho tunamaanisha kwamba kuwapo Kwake Pote ku-laini mno kwa mawazo na akili za kiumbo kuweza kufahamu kuwapo Kwake Pote, kama vile nafsi (roho) ni laini mno, ingawa ipo pia ni moja miongoni mwa Uumbaji na bado ni nje ya duru ya mawazo.

Kama sasa watasema ni kwa nini Yulaini mno kuwepo juu ya kila kitu, swali hili litakuwa lisilothibitika, kwani zaidi sana sana Muumba wa kila kitu lazima awe juu ya kila kitu na dhahiri kwayo.

Utukufu Uwe Kwa Mwenye Nguvu Zote Allah!

Kama wanauliza kwamba kwa nini imejulikana kwamba Yeye ni juu ya kila kitu na dhahiri kwayo?
Jibu litakuwa kwamba kuna ilani nne za elimu katika niaba hii:-
(1) Kuona kama kuwapo kwa kitu ni thabiti.
(2) Asili halisi na nafsi kwayo.
(3) Ni sifa gani ilizonazo?
(4) Kwa nini ni kwa vipi kuwapo Kwake.

Hakuna kiumbe anayeweza kutumia ilani hizi katika kuhusiana na Muumba, ila kujua tu kwamba Yupo. Hakuna anayeweza kujua kuhusu nafsi yake. Kuuliza kwa nini na kuwepo Kwake wapi kumhusu Yeye moja kwa moja (ni swali) lisilothibitika, kwa kuona kuwa Yeye ni Muumba wa kila kitu, na hakuna chochote kiwezacho kusimama kama chanzo au sababu ya kuwapo Kwake.

Kwa vile watu wamekwisha elewa kwamba Yeye yupo, siyo lazima kwamba wajue na Nafsi Yake pia, kame vile uelewaji wa roho hakufanyi kuwa na elimu ya asili. Hali ni sawa hivyo hivyo kwa asili ya vitu vingine vya Kiroho. Kama wanasema kwamba unamzungumzia Yeye kama aliye mbali na kutambuliwa kwa vile Yeye ni Hai asiyejulikana, jibu litakuwa kwamba kwa upande mmoja kimaoni kwa kweli ni hivyo, kama akili inataka kupata elimu ya Nafsi/Asili yake. Kwa upande mwingine wa maoni, hata hivyo, Yeye yuko karibu kuliko kila kitu, kwa kuwa ufanisi wa hoja umefanya kuthibitisha kuwapo Kwake.

Kwa hiyo, kutoka mtazamo wa upande mmoja, Yeye yuko dhahiri, na hakufichika kwa ye yote, kutoka mtazamo wa upande mwingine Yeye amefichika kwa kufikiwa na akili za hisia za mwili wa mwanadamu. Ni hivyo hivyo na akili. Hujulikana kwa hoja na ushahidi lakini asili yake ni fumbo.

Wataalamu wa viumbe hai na mimea wanasema maumbile hayafanyi chochote bure wala kuacha chochote feleti (bila kufanyika) ambayo hupelekea kwenye ukamilifu wa kitu, hutoa ushuhude kwa hili. Jibu Kwao litakuwa, nani aliyefundisha maumbile ustadi huu na elimu ya mipaka ya kila kitu, isiruke mipaka ya maana halisi na kwenda nje ya uwezo wote, wakati ambapo hili ni jambo ambalo akili haijifundishi hata baada ya majaribio ya uchunguzi wa mara kwa mara?

Kama wanasema kwamba maumbile yana hali ya kujua yote na kuweza yote, kwa hiyo wanakubali kile walichokikana, kwani hizi ni sifa za Muumba, kwamba Yeye ni Mwenye Kujua yote (Hekima Kuu) na ni Mwenye Kuweza yote (Enzi zote). Wamempa Yeye jina la "maumbile", sisi tunamwita Yeye Allah, Mwenye Nguvu zote, Mwenye Kujua yote, Mwenye Kuweza yote n.k. Kama wanakana hilo, basi Uumbaji wote huu wenye Ustadi unaita kwa nguvu kwamba ulimwengu huu sharti uwe ni kazi ya Muumba ambaye ana sifa hii kubwa mno - Mwenye kujua yote.

Miongoni mwa watu wa kale walikuwepo baadhi ambao walikana Dhumuni na Usanii. Waliamini kwamba ulimwengu ulijitokeza na kuwepo wenyewe kwa bahati tu.

Hoja yao ilikuwa kwamba wakati mwingine watoto wachanga wanazaliwa tofauti na umbo la kawaida kama vile waweza kuwa wameharibika viungo kwa ongezeko la kidole au kwa ubaya wa sura usio wa kawaida. Wamehoji kwamba ulimwengu umejitokeza kuwapo bila dhumuni na mpango. Kwamba (watoto hao) wamejitokeza kuwa hai wenyewe na kwa bahati tu.

Mtaalam mmoja aitwae Aristotle alikania hoja yao. Jibu lake lilikuwa kwamba kama kitu chochote, hutokea kwa kadiri ionekanavyo kwa bahati, hicho pia kina sababu mahsusi ambazo hukipotea kutoka shughuli zake za kawaida. Bahati ile kamwe haiko kwenye daraja la shughuli za Kawaida ambazo huenda zikaendelea daima.

Unaona jamii tofauti za wanyama wafuatao mtindo wa kawaida na kupata maumbo dhahiri, kwa mfano mtoto mchanga wa kibinadamu wakati anazaliwa ana mikono miwili, miguu miwili na vidole vitano (vya mikono na miguu) kila mmoja kama inavyoonekana kikawaida miongoni mwa watu. Hata hivyo, wakati mwingine, mambo huwa tofauti - kinyume kutokana na baadhi ya sababu zinazoathiri jauhari za uzazi ambazo hufanya kukua kwa kilengwa katika mfuko wa uzazi; kama vile inavyotokea hivyo kwa sababu ya baadhi ya khitilafu katika ala (zana za kazi), ambazo anafanyizia kitu maalum ambacho kinatengenezwa, hakiji sawa na usanii wa fundi.

Kadhalika, sababu fulanihutambaa kwa mtoto wa wanyama ambazo hupelekea kuharibika viungo, kupungua au kuongezeka katika mipaka, lakini kijumla wako kikawaida mfumo sawa bila kombo.

Kama vile khitilafu itambaavyo, kwenye mambo fulani katika hali ya njia halisi bila kuwa kinyume na mpango na bila kutoa ushahidi kwamba siyo vyombo vya ufundi vya mafundi; kadhalika mambo fulani yanaathiwa na vikwazo fulani katika shughuli za kawaida za maumbile, hauwezi kufanya kuwa ni sababu katika pendeleo la kutokea hivi hivi na bahati. Kwa hiyo yeyote, ambaye juu ya msingi wa kweli kinume na maumbile, husema kwamba kila kitu kimejitokeza kuwepo kwa bahati tu, anafanya kitu kisichothibitika na maelezo yasiyo na akili.

Kama wanasema ni kwa nini vitu fulani vina maumbo kamili ambapo vingine vina kasoro moja, jibu litakuwa kwamba ni kuonyesha kwamba vitu vya ulimwengu haviko kwa sababu ya ulazimisho wa maumbile wala si lazima kwamba kama ilikuwa kwa sababu ya maumbile, vyote vingepaswa kuwa na mfumo mmoja kama wakinzani hawa wanavyosema. Yote haya hutokea chini ya kupenda na Dhumuni la Mwenye Nguvu zote, Muumba kwamba, Yeye Ameweka mfumo fulani na kiutaratibu kwa vingi ambapo ameruhusu kasoro kwenye taratibu katika baadhi ya mambo kuonyesha kwamba maumbile pia yako chini ya udhibiti wa mpango bora na ustadi, kwamba yenyewe pia, yanategemea juu ya kupenda kwa Muumba kwa shughuli zake na ukamilifu.

Utukufu uwe kwa mwenye nguvu zote allah, mhifadhi wa malimwengu !

Elimu ambayo nimeiweka juu yako yapasa isomwe kwa moyo. Yapasa uwe na shukurani kwa Mwenye Nguvu zote Allah na Mhimidi Yeye kwa baraka Zake. Yapasa uwatii Wapenzi Wake.

Nimetoa kidogo jumla yote ya elimu na ushahidi wa Mpango mkamilifu na Dhumuni kama hoja kwa uumbaji wa ulimwengu huu. Fikiri na tafakari juu ya hii na jifunze somo kwayo.”

Nilimuahidi Imam (a.s.) kupambanua siri ya maana ya yote haya.

Imam (a.s.) aliweka mkono juu ya kifua changu na akasema: "Kumbuka yote haya na hutayasahau".
Nilizirai. Wakati nilipopata fahamu zangu, Imam (a.s.) akasema: "Ewe Mufazzal! Unajisikiaje sasa?"

Nilijibu: "Kwa msaada wa Mola wangu, ninajitegemea kwa kurejea kwenye kitabu hiki ambacho nimekiandika. Kila kitu kiko kwenye kumbukumbu yangu kama vile naweza kuonyesha yote kutoka viganja vya midono yangu. Utukufu uwe kwa Mola wangu Mwenye Nguvu zote Allah, ambaye kwake zinastahiki Shukurani na Sifa njema kama zinavyopasika."

Imam (a.s.) akasema: “Ewe Mufazzal! Uwe mkamilifu kwenye utulivu katika akili yako, ubongo na hoja. Insha-Allah, nitakupa maelezo ya mbingu na ardhi na vitu vyote vilivyoumbwa na Mwenye Nguvu zote Allah kama maajabu yake ya Uumbaji na jamii mbalimbali na makundi ya malaika mpaka uu kabisa kwenye "zenith" na sifa zao pamoja na viumbe vyote kuchangnya majini na binadamu, mpaka kwenye nukta ya mwisho ya "nadir", ili uelewe kwamba uliyojifundisha kwa sasa ni sehemu ndogo tu ya yote.

Unaweza kwenda sasa. Unayo nafasi tukufu karibu yetu na heshima hii katika nyoyo za maumini kama inavyohisika hamu ya maji wakati mtu ana kiu. Usiniulize kuhusu niliyokuahidi mpaka mimi mwenyewe nisikie kupenda kuzungumza na wewe kwayo.”

Nilirudi kutoka kwa Imam (a.s.) na tunu ambayo hakuna mtu yeyote amediriki kuipokea.

Mufazzal Ibn Umar