read

Baraza La Pili: Ufalme Wa Wanyama

Ufalme Wa Wanyama

Asubuhi na mapema niliwasili kwa Bwana wangu, na baada ya kupata ruhusa ya kuingia katika vyumba vyake niliketi kwa ruhusa yake.

Yeye (a.s.) alianza: Sifa zote njema zamstahiki Yeye Ambaye ni Muumba wa mabadiliko ya nyakati Ambaye huleta hatua moja baada ya nyingine na hali moja baada ya nyingine ya miongo ya muda, kuwalipa wema na kuwaadhibu waovu, kwa sababu ni Mwenye Haki. Majina yake yote yametukuzwa. Baraka zake ni adhimu. Hafanyi dhuluma hata ndogo kwa viumbe wake, walakini, mtu anajifanyia udhalimu mwenyewe!

Maneno ya Allah (s.w.t.) mwenyewe yanathibitisha ushuhuda kwa haya: "Basi atakayefanya kheri (jema) uzani wa mdudu chungu atauona. Na atakayefanya uovu uzani wa mdudu chungu (pia) atauona" (Qur'an 99:7 - 8).

Kuna Aya nyingine katika Kitabu Kitukufu katika maana hii hii zikitoa kinaganaga maelezo ya mambo yote. Uwongo hauwezi kuja mbele yake wala nyuma yake. Ni kitabu kilichofunuliwa na Mwenye Nguvu zote Mwenye Kustahiki Shukurani Allah. Ni kwa maelezo haya kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema kwa jambo hili kwamba " Matendo yenu yatarudishwa kwenu."

Imam (a.s.) aliinamisha chini kichwa chake kwa muda na akasema: "Ewe Mufazzal! Mwanadamu amefadhaika na kupotea, ni kupofu, amepumbazika katika ukaidi wake, kufuatia mashetani yao na vioja. Wana macho lakini hawaoni, wana ndimi lakini ni mabubu na hawaelewi. Wana masikio lakini hawasikii. Ni wenye furaha katika ufisadi wao duni. Wanadhania wameongozwa vema. Wamepotoshwa kutoka sifa za viumbe vyenye akili. Wanakula juu ya mboga zilizonajisiwa na uchafu wa watu wachafu. Wanadhani wenyewe wako salama kutokana na msiba wa kifo cha ghafla na adhabu ya matendo. Ole! Ajali mbaya iliyoje iwapatao watu hawa!"

Hii ilinifanya mimi nitoe machozi, na Imam (a.s.) alinifariji kwa kusema kwamba nimeokolewa, kwa sababu ya kuikubali iman na elimu ya kiroho, na nimepatiwa wokovu.

Ulimwengu Wa Wanyama

Yeye (a.s.) aliendelia: Sasa napenda kukuelezea kuhusu ulimwengu wa Wanyama, ili kwamba upate maelezo zaidi kuhusu (Ulimwengu) huo kama ulivyopata kuhusu mengine.

Hebu fikiria umbile la mwili na mfumo wa muundo uliomo katika uumbaji wao. Siyo wagumu kama mawe, kwani wangekuwa hivyo, wasingeweza kufanya shughuli, wala siyo laini kwani kwa hali hiyo wasingeweza kuzunguusha vichwa vyao au wenyewe kusimama wima bila mhimili.

Wamefanyizwa na misuli hiyo ya kupinda kama kuinama na kujikunja. Wametengenezwa kwa mifupa migumu ambayo imeshikwa kwa misuli na ambayo imefungwa pamoja kwa makano juu ya kila mfupa. Ifunikayo mifupa hii na misuli hii ni ngozi yao ambayo huenea juu ya mwili vote.

Wanasesere wa miti na matambara yaliyo zunguushwa juu yao na kufungwa na vigwe na Sandarusi ya gundi ju ya umbo lote, itafafanisha jambo hili, ifanye mbao iwe kama mifupa, matambara kama misuli, vigwe kama makano no sandarusi kama ngozi.

Kama inawezekana katika hali ya viumbe vyenye uhai na mwendo kujitokeza kuwepo kwa vyenyewe, ingekuwa busara kutegemea kutokea maumbo haya yasio na uhai. Na kama haiwezekani kwa wanasesere hawa, itakuwa ni upuuzi zaidi kwa wanyama.

Kisha angalia kwa uangalifu sana kwenye miili yao, imefanyizwa kwa misuli na mifupa kama ya wanadamu. Wamejaaliwa macho na masikio, ili kwamba kumuwezesha mtu kupata huduma kutoka kwao, wasingaliweza kutekeleza lengo lake (huyo mtu) kama wangekuwa vipofu au viziwi.

Wamenyimwa Stadi za akili na hoja, ili kwamba wabakie ni wenye kutii kwa watu na wasije wakawa wasiotii hata kama akihusishwa na kazi nzito isiyovumilika na kuelemea.

Kinzano laweza kuletwa katika hali ya watumwa wanadamu, wenye akili na hoja, hutii mabwana zao kiunyonge japokuwa ni dhiki na kazi ngumu.

Jibu kwa hili ni kwamba watu wa aina hii ni wachache kiidadi. Wengi wa watumwa ni wafanyaji kazi ngumu bila kupenda, ambapo wanyama ni watii hata katika kulemewa kuzito na wakati wa kuzunguusha kijaa n.k. hawawezi kuathirika kwa mfadhaiko kama kazi zao mahsusi zihusikavyo kwa mtu.

Kama mtu angefanya kazi ya ngamia mmoja au nyumbu, watu wengi wangehitajika, na kusababisha kizuizi katika shughuli nyingine. Majukumu haya rahisi yangechukua wafanyakazi wote, bila kuacha watu wowote kando kwa ajili ya Sanaa na Taaluma. Zaidi ya hayo watu wangepatwa na uchovu wa akili.

Hebu fikiria miundo ya aina tatu ya viumbe hai ifuatayo, na Sifa ambazo kwamba wamejaaliwa nazo.
(1) Mtu, akiwa ameamriwa kuwa na akili na hoja kufanya kazi hizo za ufundi kama useremala, uashi, uhunzi, kushona n.k. amejaaliwa kuwa na viganja vipana na vidole vinene kumwezesha kushika aina zote za ala zilizo muhimu kwa ajili ya taaluma hizi.
(2) Wanyama walao nyama, wakiwa wameamriwa kuishi kwa kula wanyama (nyama) wametunukiwa viganja laini na makucha yawezekanayo kufichika ndani. Ni wazuri kwa kuwinda lakini hawafai kwa kazi za sanaa za kitaaluma.
(3) Wanyama walao majani, wakiwa wameamriwa si kwa sanaa za kitaaluma wala kwa uwindaji, wametunukiwa, baadhi na kwato zilizopasuliwa kuwasaidia kutokana na ugumu wa ardhi wakati wa kulisha ambapo wengine wana kwato imara kuwawezesha kusimama sawa sawa juu ya ardhi kwa ulinganifu mzuri kama wanyama wa mizigo.

Wanyama walao nyama katika mfumo wao wa kuumbwa wana meno makali, kucha ngumu, na vinywa vipana kuwasaidia katika lishe yao kwa chakula cha mnyama kama ilivyoamriwa kwao, na wameumbwa ilivyo. Wamepewa silaha hizo na vyombo vya kazi kwa kuwafaa katika uwindaji.

Kwa ulinganifu wa sawa, utaona mdomo na kucha vikiwafaa kwa kazi zao mahsusi. Kama kucha hizo wangepewa wanyama walao majani, zingekuwa mbaya zaidi kuliko manufaa kwani kamwe hawawindi wala kukamata kiwiliwili. Na wanyama walao nyama wangepewa kwato badala ya kucha wangeshindwa kupata mahitaji yao katika kukosekana vifaa vya kufaa kwa mahitaji hayo.
Huoni kwamba aina zote hizi za wanyama wametunukiwa sawasawa na vitu vyenye kufaa (kwa kusudi la kila mmoja) kwa ulinganifu na haja zao, humo kwayo mna kuishi kwao.

Sasa watazame wanyama wa miguu minne na angalia jinsi wanavyowafuata Mama zao. Kamwe hawahitaji kubebwa wala kulishwa kama ilivyo kwa watoto wa kibinadamu. Hii ni kwasababu kwamba mama wa watoto hao hawana nyenzo ambazo mama wa watoto wa Kibinadamu wanazo. Wana Upendo, Huba na Elimu ya Sanaa ya Maumbile na Mikono maalum na Vidole vya kuwanyanyulia. Wamefanyizwa hivyo ili kuwasaidia katika aina zote za kazi.

Utaona namna hiyo hiyo katika ndege, kwa mfano, Vifaranga vya Kuku, Kwale na jamii ya Kuku (k.v. Kanga) huanza kuokota nafaka na kwenda huku na huko mara tu vinapoanguliwa kutoka kwenye mayai. Ndege ambao vifaranga vyao ni dhaifu, bila nguvu ya kusimama, kwa mfano wale wa porini na njiwa wa nyumbani, wana mama wenye silika zaidi za kimama, ili kwamba wawaletee lishe kwenye vinywa vya vifaranga vyao waliyoiweka kwenye maumio yao.

Malisho aina hiyo huendelea mpaka vifaranga viweze kujikimu vyenyewe. Njiwa hana makinda wengi kama kuku, kuwezesha majike kuyalea kiutoshelezaji bila kuwaua kwa njaa. Hivyo kila kimoja hupata mgao wa kutosha kutoka baraka za Mwenye Nguvu zote Mwenye Kujua yote Allah (s.w.t.)

Hebu tizama jinsi miguu ya wanyama ilivyoumbwa katika jozi kuwawezesha kutembea kwa urahisi, ambapo ingekuwa vigumu, kama ingeliumbwa katika idadi ya witir. Mnyawa atembeaye hunyanyua mguu mmoja ambapo mwingine anautuliza juu ya ardhi. Wenye miguu miwili ananyanyua mmoja na kupata msaada juu ya mwingine. Wa miguu minne hunyanyua jozi moja na kutulia juu ya pande tofauti.

Kama mnyama wa miguu minne angenyanyua jozi ya miguu katika upande mmoja, tutusa kwa jozi ya upande mwingine kungekuwa kugumu kama ambavyo ubao hauwezi kusimama juu ya miguu miwili. Mguu wa mbele wa upande wa kulia na mguu wa nyuma wa upande wa kushoto inanyanyuliwa pamoja, na kinyume chake. Kwa ajili ya mwendo thabiti.

Je, huoni kwamba punda anaendesha Kijaa kama kazi nyongeza ya ubebaji mizigo, kwa kuwa farasi anaruhusiwa pumziko na faraja kwa kulinganishwa na punda? Na ngamia anafanya kazi zaidi, ambayo haiwezi kumalizwa na idadi ya watu.

Ingekuwa hali gani kama angekataa kutii amri? Husalimu Amri hata kwa mtoto aliyepo hapo! Vipi Maksai anasalimu amri kwa Bwana wake akilima Shamba na mhimili shingoni mwake?
Farasi wenye asili bora hukimbia kuelekea makali ya panga na mikuki kama wafanyavyo mabwana zao wakati wa mapigano. Mtu mmoja anaweza akachunga kundi la kondoo. Kama kondoo wangetawanyika kila mmoja akaenda njia yake, vipi mtu angeweza kuwatafuta?

Kadhalika, Jamii nyingine za wanyama ni zenye kufaa kwa mtu, kwa nini? Hii ni kwa sababu hawana akili yoyote, wala uwezo wowote wa kuhoji mambo. Kama wangelikua na akili, wangejitoa katika kutekeleza kazi nzuri ya mahitaji ya mtu.

Ngamia angekataa kusalimu amri, na fahali angeasi dhidi ya bwana wake, kondoo wangetawanyika na kadhalika. Kama wanyama wa kuwindwa wangekuwa na akili na hoja wangeshindana kwa ajili ya vitu vya kula na watu. Nani basi angeweza kushindana na ushauri wao wa pamoja dhidi ya watu?

Je, huoni jinsi walivyozuiwa kutokana na kufanya hivyo? Wanaogopa makazi ya watu na kumkimbia mwanadamu, badala ya mwanadamu kuwaogopa wao (na kuwakimbia). Hawatoki nje wakati wa mchana kutafuta chakula, bali wakati wa usiku. Wanaogopa watu na utukufu wao wote utishao bila kupata dhara lolote au onyo kutoka kwao. Kama hii isingeamriwa hivyo, wangekuja wakirukaruka kwenye makazi ya wanadamu na kufanya maisha yao kuwa ya mashaka.

Mbwa, (akiwa) miongoni mwa hayawani, amejaaliwa tabia maalum, utii kwa bwana wake, utumishi wake kwake na ulinzi wake kwake. Huweka ulinzi wakati wa usiku wa giza, hubweka huko na huko katika nyumba akilinda usalama dhidi ya wezi. Yuko tayari kujitoa mhanga maisha yake ili kumwokoa mtu na watu wake. Huo ndio utii wake kwa bwana wake. Anaweza kujiweka na njaa na maumivu kwa ajili ya bwana wake.

Kwa nini, mbwa ameumbwa katika mfumo huu, isipokuwa tu amtumikie na kumlinda mtu, na meno yake imara, kucha madhubuti, ubwekaji wa kutisha, kwa nini? Ni kwa kuwatisha wezi na kuwazuia kukaribia mali iliyo dhaminiwa kwa ulinzi wake.

Tizama katika nyuso za wanyama wa miguu minne na angalia vipi zilivyoumbwa. Utaona kwamba macho yao yamewekwa mbele, wasije wakagonga ukuta au kutumbukia shimoni. Utaona vinywa vyao vimepasuliwa chini ya pua. Kama vingekuwa kama vile vya watu wasingeweza kuokota chochote kutoka ardhini. Huoni kwamba mtu haokoti chakula chake kwa kinywa chake? Hufanya hivyo kwa mikono yake.

Huu ni ubora wa pekee kwa mtu katika mlingano na walishi wengine. Kwa kuwa wanyama wa miguu minne hawakupata mikono kama hiyo kuwawezesha kuokota majani, sehemu ya chini ya pua imepasuliwa humwezesha kuokota majani na kuyatafuna. Anasaidiwa zaidi na midomo iliyo refushwa kufikia vitu vilivyoko mbali zaidi kama vile afikiavyo vilivyo karibu zaidi.

Fikiria mikia ya wanyama na faida zilizoamriwa kwayo. Ni aina fulani ya mfuniko kwa viungo vyake vya siri vya kutolea uchafu. Vilevile husaidia kufukuza inzi na mbu ambao hutua juu ya uchafu katika miili yao. Mkia yao imefanyiwa mfano wa mapanga boi ambayo kwa hiyo hufukuzia inzi na mbu. Vile vile hupata afueni kwa kupungia mikia yao daima.

Wanyama hawa husimama juu ya migu yote minne, hawana muda wa kuitembeza huku na huku, kwa hivyo, huhisi kufarijika kwa kupungia mikia yao.

Kuna faida nyingine hata hivyo ambazo mawazo ya mwanadamu si yenye kuweza kuzishika na ambazo zinajulikana tu inapotokea haja, miongoni mwa faida hizi, mkia ni silaha ya zaidi sana mkononi kwa kuunyongotoa kumtoa mnyama anasapo kwenye matope. Mwengo wa mkia unaweza vile vile kutumiwa na watu kwa manufao kadhaa.

Kiwiliwili cha wanyama hawa kimefanywa bapa kwa kulala juu ya miguu yote minne kurahisisha ngono kwa sababu ya hali ya sehemu zao zinazohusiana.

Tembo

Fikiria mkonga wa tembo na ustadi mkubwa uliopo katika muundo wake. Unasaidia dhumuni la kuchukua chakula na maji kupeleka ndani tumboni, kama mkono wa mtu. Bila huo tembo hawezi kunyanyua chochote kutoka ardhini, kwa kuwa shingo yake siyo ndefu vya kutosha, ambayo angeweza kuinyoosha mbele kama wanyama wa miguu minne.

Kwa kutokuwepo kwa shingo ndefu amepewa mahala pake mkonga mrefu ili kwamba aweze kuunyoosha na kukidhi haja yake. Nani aliyempa kiungo hiki kufidia kwa kutokuwepo kwa kile kilicho kosekana? Hakika, Yeye Ambaye ni Mwenye Huruma Sana juu ya Viumbe Vyake. Na hii itawezekana vipi bila kupanga Usanii kama ilivyojitokeza kwa Wataalam wapotofu na walahidi?

Kwa kinzano kwamba kwa nini hakujaaliwa kuwa na shingo sawa kama ile ya wanyama wengine, jibu ni kwamba kichwa na masikio vya tembo vikiwa ni vizito sana vingeweza kusababisha mvuto mkubwa wa nguvu, hata pia kuvunjika, hivyo kichwa chake kimeungwa moja kwa moja na mwili kukikinga dhidi ya matokeo hayo na badala yake kwa ajili hiyo mkonga umefanyizwa kushughulikia madhumuni yote hayo inayohitaji, pamoja na yale ya kulisha.

Twiga

Hebu fikiria umbo la twiga na asili mbalimbali ya viungo vyake vifananavyo na wanyama wengine mahsusi. Kichwa chake hufanana na ile cha farasi, shingo kama ile ya ngamia, kupasuka kwato kama zile za ng'ombe, na ngozi yake kama ile ya chui.

Baadhi ya watu wajinga wamedhania kwamba haya ni matokeo kutokana na muungano wa aina mbalimbali za wanyama wajao sehemu za kunyweshea, jamii moja binafsi huingia katika muungano wa ngono na jamii nyingine binafsi, na kutokea uzao wa namna hii. Na kwa hiyo unakuwa mfano wa umbo mbalimbali.

Kusema hivi ni kuudhihirisha ujinga, na ukosefu wa elimu ya kiroho ya Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.) utukufu uwe kwake. Hakuna mnyama aingiaye kwenye muungano ufanyikao kati ya farasi na ngamia jike au ngamia na ng'ombe. Muungano wa ngono unaweza kuwepo (au kutokea) tu kati ya wanyama wenye umbo linalofanana katika kuumbwa, kwa mfano farasi na punda jike hutokea (kuzaliwa) kwa nyumbu, au mbwa mwitu na mbweha hutokea (kuzaliwa) chotara.

Hata hivyo, kamwe haitokei kwamba uzao wa muungano wa namna hiyo unaweza kuchukua kiungo kimoja kutoka mmoja wa mwenzi mwingine. Twiga ana kiungo kimoja kifananacho na kile cha farasi, mwingine na kile cha ngamia ukwato wa mwingine na ule wa ng'ombe. Lakini unaona kwamba nyumbu kichwa chake, masikio yake, mgongo wake, mkia na kwato zake vi katikati baina ya vile vya punda na vya farasi, na ndivyo ulivyo mlio wake u katikati baina ya mlio wa farasi na mlio wa punda. Hoja hii yaonyesha kiutoshelezaji kwamba twiga si uzao wa muungano wa jamii inayojifanyia tu, bali ni ajabu moja ya uumbaji wa ajabu wa Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.) kuthibitisha Enzi yake Kuu.

Yapasa pia ifahamike kwamba Muumba wa jamii za Wanyama zisizo idadi Huumba viungo vyovyote vile Apendavyo ya hivyo vilivyo sawa kimoja na kingine na vile vingine ambavyo havifanani. Anaongeza katika uumbaji chochote apendacho na hukataza humo namna Apendavyo. Hii ni kwamba Enzi Yake Kuu iweze kuthibitishwa na hakuna kitu kinachoweza kumzuia katika lolote Apendalo.

Kwa nini shingo yake ni ndefu na faida gani zipatikanazo kwake kutokana nayo? Faida ipo katika kumwezesha kufikia majani na matunda ya miti mirefu kwa lishe yake ambapo anaishi, anakaa, na amezaliwa na sehemu zake za kujilishia, ni misitu minene.

Kima

Hebu fikiria uumbaji wa Kima na ufanano ambao upo kati ya viungo vyake na vile vya mtu, kichwa, mabega yote, kifua na viungo vya ndani.

Zaidi ya hayo, amepewa akili na utambuzi/uwelekevu kwa sababu ya hizo huelewa ishara na maelekezo ya bwana wake. Kwa ujumla huiga matendo ya mtu kama anavyomwona. Yuko karibu sana na mtu katika ubora wake, tabia na asili ya kuumbwa.

Inapasa iwe kama ni onyo kwa mtu kwamba azingatie akilini kwamba katika asili na umbo ni sawa na wanyama akifanana nao kwa ukaribu sana na kama asingepewa akili, ujuzi/utambuzi na uzungumzaji angekuwa sawa tu kama wanyama.

Kuna maongezeko kidogo katika muundo wa (kuumbwa) kima umtofautishao na mtu k.m. kinywa, mkia mrefu, nywele zifunikazo mwili mzima. Tofauti hizi, hata hivyo, zisingemzuia kuwa mwanadamu, kama angelipewa stadi za hoja, akili na uzungumzaji kama mtu. Tofauti yenyewe hasa ya mpaka baida yake na mtu, kwa hiyo, ni kwa ajili (ya kukosa) tu njia za hoja, akili na uzungumzaji.

Ngozi Ya Mnyama

Hebu fikiria Rehema za Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.)kwa wanyama hawa katika kuipa miili yao mfuniko wenye aina mbali mbali za nywele kuwalinda dhidi ya misukosuko/matatizo ya kipupwe. Na wamepewa kwato, zilizopasuliwa na zisizopasuliwa, au miguu fumba kwa kuwahifadhi. Si wenye mikono, wala viganja wala vidole kusokotea nyuzi na kufuma, na kwa hiyo mavazi yao yamefanywa ni pamoja na sehemu ya umbo la miili yao, kuwahifadhi maisha yote bila kutengeneza na kubadilisha.

Mtu, iwayo yote, ana mikono na ufundi wa kufuma nguo na kusokota nyuzi. Hutengeneza nguo na mara kwa mara huibadilisha kwa faida nyingi upande wake. Miongoni mwa hizo hujishughulisha na utengenezaji nguo zake na kwa hiyo akaepukana kutokana na shughuli (mbaya) zenye kudhuru na uvivu. Huiacha kazi yake ya kushona wakati apendapo kuwa nyumbani. Anaweza kutengeneza aina mbalimbali za mavazi kwa burdani apatayo katika kubadili kwa njia ya fahari na kadhalika. Hutayarisha soksi na viatu kwa njia ya utendaji mzuri kuhifadhi miguu yake. Vibarua, na wafanya biashara kwayo hupata riziki zao na riziki za jamaa zao. Hizi aina tofauti za nywele huwasaidia wanyama kama mavazi ambapo kwato zao na miguu - fumba kama viatu.

Kuzika Mfu

Hebu fikiria tabia hii ya asili ya wanyama, nayo ni, ufichaji wa miili ya wafu wakati inaokufa kama vile watu wanavozika maiti wao. Hakuna hata mwili mfu mmoja wa hayawani na wanyama unaoonekana. Hawako mbali sana kiasi cha kutokuonekana. Kwa ukweli idadi yao ni kubwa zaidi kuliko ile ya watu.

Yatazame makundi ya kulungu, nyati, punda wa porini, mbuzi mawe na paa na pia jamii mbali mbali za wanyama na hayawani kama vile simba, nyumbu, mbwa mwitu, chui n.k., na aina aina za wadudu waishio ndani ya matumbo ya ardhi na kutembea juu take, katika majangwa na milima, na kadhalika ndege warukao kama kunguru, kwale, bata, korongo, njiwa, na ndege wa mawindo. Hakuna mizoga yao tunayoiona isipokuwa michache ambayo mwindaji huipata, kama mawindo au ile inayonyafuliwa na hayawani. Likiwa ni jambo la ukweli, wakati wanyama hawa wanapopata hisia za kukaribia kifo (kufa), ujificha katika baadhi ya sehemu za siri na kufia humo.

Zitazame sanaa ambazo mtu (mwanadamu) amejifunza kutoka wanyama hawa - mfano wake wa kwanza. Aliona kunguru wawili wakipigana. Mmoja akamuua mwingine na kisha akauzika mwili wake mfu, hivyo Kabil akajifundisha kuchimba shimo na kuzika maiti ya ndugu yake Habil. Hayo yalifanyika chini ya mwongozo wa Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.). Wanyama hawa walipewa hisia hizi kumwokoa mwanadamu (mtu) kutokana na msiba wa matatizo hayo na milipuko ya magonjwa ambayo yangeweza kuja (kutokea).

Silika Za Wanyama

Fikiria silika ambazo kwazo (wanyama) kwa desturi wamepewa na Mwenye Kguvu zote Allah kwa Rehema zake zisizo na mwisho ili kwamba asiache kiumbe chochote kunyimwa Rehema zake ingawa hii haiko chini ya Stadi za kufikiria hali ya usawa.

Paa humeza nyoka lakini hanywi maji hata kama kiu yake itakavyokuwa kali namna gani, kwa kuchelea sumu inayosambaa ndani ya mwili wake ambayo kwa sababu ya maji ingemuua. Huzunguukia mapipa ya maji. Hupiga kelele kwa sababu ya ukali wa kiu lakini hagusi maji kwa kuchelea (kuogopa) kifo. Unaona kujizuia kukubwa huku ambako wanyama hawa wanako bila kujali kiu kali kwa sababu ya hofu au dhara katika hali ambayo mtu mwenye akili na busara hawesi kustahimili.

Mbweha nae, asipopata chakula kwa njia yoyote ile hujifanyia "kifo cha hadaa na kulitanua tumbo lake kuwadanganya ndege waamini kuwa kafa. Maru tuu ndege wakija kumzunguuka kwa kutaka kuunyofoa mwili uonekanao kama mzoga, huwashambulia na kufanya mlo mzito wa nyama zao.

Sasa, sema, nani aliyetoa wlekevu huu kwa mbweha asiyezungumza na asiye na akili? Hakika ni Yeye Yule Ambaye amechukua juu Yake Mwenyewe Jukumu la kumlisha. Kwa vile mbweha hawezi kufanya shughuli zile ambazo hayawani wengine wanaweza, k.m. shambulio la moja kwa moja juu ya mtesi, amepewa werevu na hadaa kama njia za kujipatia riziki (maisha).

Dolfin (Samaki kama nyangumi mdogo) huhitaji ndege kama watesi. Humkamata samaki na kumuua na kumuweka ili kwamba aelee juu ya maji ambapo yeye mwenyewe akijificha chini yake akiyavuruga maji wakati wote kuufanya mwili wake ufichike. Mara tuu ndege anapomrukia ghafla yule samaki, huruka kwa ghafla juu yake na kumshikilia yule ndege. Kwa werevu huu humpata mtesi wake (riziki).”

Chatu Na Wingu

Kisha niliomba maelezo kuhusu chatu na wingu.

Imam (a.s.) akajibu kwamba: “Wingu ni mfano wa Malaika kumkamatia (kumshikilia) chatu wake popote atakapomwona, kama vile jiwe la sumaku linavyoshikilia chuma. Hanyanyui kichwa chake kutoka ardhini kwa sababu ya kuchelea (kuogopa) wingu hilo, isipokuwa katika (majira ya) kiangazi wakati anga ni nyeupe bila dalili ya wingu na kisha litokeapo tu (hilo wingu) mara moja hutoweka.”

Niliuliza, “Kwa nini wingu limefanywa mtawala wa chatu kumshililia popote litakapomwona?”

Imam (a.s.) akajibu,"Kumwokoa mtu (mwanadamu) kutokana na madhara yake."

Siafu

Nilisema, "Maulana! umetoa maelezo ya ulimwengu wa wanyama kwa ukamilifu kufanya kama kifungua macho kwa kila mtu. Tafadhali hebu toa baadhi ya maelezo kuhusu Siafu na ndege".

Imam (a.s.) akasema,"Timaza katika taya za siafu huyu mdogo. Je, unaona kasoro yoyote ndani yao inayoathiri faida yake? Je, umetoka wapi ulinganifu huu na hadhari? Hakika ni kutokana na ustadi uleule na usanii ambao umetomika katika ujenzi wa uumbaji wote, mkubwa au mdogo.

Hebu tizama siafu jinsi wanavyokusanyika pamoja kukusanya chakula kwa ajili yao. Utaona kuwa wakati siafu wengi wakiazimia kuchukua nafaka kupeleka kwenye nymba zao wanafanana na watu wengi wanaojishughulisha na kupeleka nyumbani nafaka zao. Siafu kwa kweli huonyesha juhudi na shughuli ambazo watu hawawezi kuzifanya. Huoni jinsi wanavyosaidiana kila mmoja katika kuchukua nafaka kama watu? Wanazivunja nafaka vipande vipande zisije zikachipua na kuwa zisizo na maana kwa dhumuni lao. Kama zikipata unyevu nyevu, huzisambaza zipate kukauka.

Siafu hotoboa mashimo yao sehemu zilizonyanyuka, mbali kutokana na hatari ya mafuriko.

Shughuli zote hizi, iwayo yote, hazipo bila uamuzi wa hoja, wenye silika halisi, ambazo kwazo miundo yao imejaaliwa nazo, kwa ukarimu wa Mwenye Nguvu zote Allah.

Buibui

Hebu mtizame mdudu aitwae "Lais" (aina ya buibui) kwa kawaida huitwa simba wa inzi. Ukubwa ulioje wa werevu na ustadi na upole aliojaaliwa mao kwa utafutaji wa riziki zake. Uatona kwamba wakati ana hisia ya kufikiwa na inzi humpuuza kwa muda kujifanya kama kamba vile mwili wenyewe ni usio na uhai (umekufa). Wakati akihisi kwamba inzi hayupo katika hofu yoyote ya kukamatwa na hana habari kabisa ya kuwepo kwake (buibui) huanza kunyemelea kuielekea katika mwendo wa kunyata pole pole hatua kwa hatua mpaka amfikie karibu kiasi cha kuweza kuikamata, akiwa yu ngali ameishikilia, huikumbatia na kuizingira kwa mwili wake wote kuzuia kuponyoka kwake. Hushikilia hivyo mpaka ahisi kuwa inzi huyo ameishiwa nguvu na viungo vyake vimetulia, na hapo sasa huigeukia za kuila. Hii ndiyo njia aitumiayo kwa kuishi.

Buibui wa kawaida hutanda utando wake na kuutimia kama mtego kwa kukamatia inzi. Hukaa amejificha ndani yake. Mara tu inzi anaponaswa humrukia kumkamata na kumkata kata katika vipande. Huendelea kuishi katika njia hii. Na hali hii indivyo ilivyo kwa mbwa, simba muwinda na mtengo wa kunasia wakati wa kuwinda. Hebu angalia mdudu huyu mnyonge jinsi alivyotunukiwa na silika (akili) ya kukamatia windo lake ambalo mtu hawezi kufanya bila kutumia matengo na ala (vyombo vya kazi).

Usitoe kasoro katika kitu chochote, kwani kila kitu kina funzo (Somo) la kufundisha kama vile siafu n.k. Maana nzuri mara nyingi huelezewa kwa kitu kidogo bila kupunguza thamani yake kama vile dhahabu haipunguki thamani kama itapimwa dhidi ya (vipimo) vitu vitokanavyo na chuma.

Ndege

Hebu fikiria umbo la mwili wa ndege kama alivyoamriwa kwamba angeruka juu angani. Ametunukiwa mwili mwepesi na kiulinganifu muundo imara. Ana miguu miwili badala ya minne, vidole vinne badala ya vitano, tundu moja kwa kutolea uchafu badala ya mbili.

Ametunukiwa kifua kilichochongoka (kumuwezesha) kuruka angani kama vile mashua ilivyojengwa kupasua majini. Ana manyoya marefu magumu katika mbavu zake na mkia kumsaidia kuruka juu. Mwili wote umefunikwa na manyoya kwa kujazwa hewa ya kurukia juu angani.

Kwa kuwa imeamriwa kwake kwamba lishe yake itakuwa ya nafaka na nyama ambazo atameza bila ya kutafuna, meno yamekosekana katika umbo lake na amepewa mdomo imara kwa kutafutia chakula ambao kwa huo anaweza kuokotea chakula. Hauumizwi wakati aokotapo wala kuvunjika amegapo nyama.

Kwa vile hana meno lakini hula nafaka na nyama mbichi, joto jingi hufanyizwa ndani ya tumbo lake ambalo hufanya kazi ya kupika chakula chake bila kuhitaji kutafuna. Ni kama vile mfano wa mbegu za zabihu hutoka nje ya tumbo la mtu kama zilivyo ambapo zinapikika kabisa/kikamilifu katika tumbo la ndege.

Wameumbwa hivyo kwamba watage mayai badala ya kuzaa watoto ili kwamba wasije wakapata uzito wa aina yoyote wa kuvumilia wakati wa kuruka kwa sabubu ya kilengwa katika mfuko wa uzazi kikaacho humo ili kikuzwe kikamilifu.

Kila kitu katika muundo wake kimeumbwa hivyo ili kiwe cha kutosheleza kufaa kwa hali yake katika maisha. Iliamriwa pia kwamba ndege ambao ni wenye kuruka juu angani wakae kwa juma moja au juma mbili au juma tatu wakilalia mayai, kwa kutotoa vifaranga vyao. Kisha huvigeukia kwa hadhari yao yote.

Analo gole kubwa la kutosha kuwaletea vifaranga vyake na chakula ambacho kwama kwa hicho pia anaweza kujilisha.

Nani aliyemuwekea majukumu kwanza ajaze gole lake kwa nafaka zilizochumwa shambani, na kisha aweke mavuno hayo katika umio la vifaranga?

Kwa nini anachukua taabu yote hiyo ingawa hana stadi ya kuhoji wala hana mategemeo yoyote ambayo mtu hawazia kuhusu watoto wao - heshima, kuishi kwa jina, na urithi n.k. Hii ni shughuli ambayo huonyesha kwamba ni fadhila maalum kwa vifaranga vyake chini ya mgawo maalum wa Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.) ambao udege mwenyewe hawezi kujua, wala kuhoji juu yake. Na ni nini hicho? Ni mpango kwa ajili ya kuishi kwa taifa.

Kuku

Hebu mtizame kuku na uone jinsi alivyo na wasiwasi wa kutaga mayai na kutotoa vifaranga ingawa hana kiota chochote mahsusi wala si mayai kutoka jamii hiyo hiyo. Hupiga kidoko (mlio wa kuku mwenye vifaranga au anayetaka kutaga), hutimua manyoya yake, huacha lishe yake, isipoluwa ipewe mayai ya kulalia na kutotoa vifarange, kwa nini?

Ni hivyo ili kuhifadhi taifa. Isingeamriwa hivyo kiasili, nani ambaye angeifadhili kwa hifadhi ya taifa, ingawa haina stadi ya akili au ya kuhoji?

Hebu tizama kwenye umbo la yai na jauhari nyeupe na njano ndani yake. Sehemu moja ni kwa ajili ya kufanyizwa kifaranga ambapo inyingine ni ya kukipatia lishe mpaka wakati huo kitakapolitoka yai.

Hebu fikiria ustadi ulio ndani yake kwa vile umbo la kifaranga lilikuwa libebwe humo kiusalama ndani ya ganda (kaka) bila kuruhusu zahama yoyote ya nje, lishe yake imewekwa ndani yake ambayo ni ya kutosha mpaka kitoke nje.

Mtu ambaye amefungwa (jela) kiusalama bila ya fikio lolote kwake huwa anapatiwa chakula cha kadiri kumtosha mpaka kuachiliwa kwake.

Umio La Ndege

Hebu fikiria gole/umio la ndege na ustadi ulio ndani yake. Tumbo limekaribiwa na mrija mwembamba kuruhusu lishe kufika ndani yake kwa kiasi kidogo kidogo. Bila gole/umio nafaka ingalichukua muda kufika tumboni.

Ndege katika ujuzi wake wa kuhisia hali ngumu ya baadae, hujaza gole/umio lake kwa haraka. Gole/umio lake limeumbwa katika muundo wa shanti (aina ya mkoba) iliyoangikwa mbele yake, ili kwamba ijae kwa haraka kwa chochote kile ikipatacho, kisha pole pole hukihamishia tumboni.
Kuna faida nyingine katika gole/umio. Baadhi ya ndege hushughulika na kuhamisha chakula kuwapelekea watoto wao. Gole/umio huwasaidia kukihamisha kwa urahisi.

Manyoya Ya Ndege

Baadhi ya watu wa mafundisho haya ya maumbo ya asili hudai kwamba rangi kuwa mbalimbali na maumbo tofauti ya ndege vimetokana tu na mchanganyiko wa vitu vya asili na tabia katika linganifu mbalimbali. Havikutokea kuwa hivyo kutokana na Usanii wowote mahsusi.

Urembo huu unaouona kwenye tausi au kwale na uzuri halisi, kama kwamba msanii fulani mwenye brashi nzuri ameitimiza sanaa ya uzuri wa picha.

Utaweza vipi mchanganyiko huu usio wa akili uulete uzuri huo wenye kuonekana bila kombo yoyote?

Ikiwa vitu hivi vya sanaa vimejitokeza kuwa viumbe bila ya Msanii Mwenye Nguvu zote, ni vipi
uzuri huu na mfanano ungehifadhika?

Hebu tizama kwa makini katika manyoya ya ndege, utayaona kama nguo iliyofumwa na nyuzi nzuri. Unywele mmoja umesokotwa na mwingine kama vile kipande kimoja cha uzi kinavyosokotwa na kingine.

Tizama katika umbo lake. Kama unalifungua, hufunguka bila kuchanika kuruhusu kewa kujazwa ndani na kuruhusu ndege kuruka wakati apendao. Ndani ya unyoya utaona ufito madhubuti uliofunikwa na kitu kama unywele ili kwamba, kwa sababu ya umadhubuti wake huyashikilia (manyoya haya). Ufito u wazi ndani (kama mrija) ili kwamba usiwe mzigo kwa ndege huyo na kuzuia urukaji wake.

Ndege Wa Miguu Mirefu

Je, umewahi kuona ndege wa miguu mirefu na ukadiriki kufikiria faida aliyonayo kwa miguu mirefu hiyo?

Mara nyingi (ndege huyo) huonekana kiulinganifu katika maji ya kina kifupi. Utamwona kana kwamba yuko katika lindo mahali alipo akiwa amesimama juu ya miguu yake mirefu.
Hufanya lindo kwa vipitavyo katika maji. Akiona kitu chochote chenye kulika pole pole hukisogelea na hudaka na kumshikilia mtesi wake. Kama miguu yake ingekuwa mifupi zaidi, tumbo lake lingegusa maji katika nyendo zake za kumnyemelea mtesi wake na pengine lingevimba na kushindwa kumkamata mtesi wake. Kwa hiyo ametunukiwa na mihimili (miguu) miwili mirefu kukidhi/kutimiza haja yake bila kikwazo.

Upatiwaji Riziki

Hebu fikiria kazi nyingine za umahiri (ufundi) ambazo zimetumika katika kuumbwa kwa ndege. Unaona kila ndege mwenye kinga ya miguu mirefu amepewa shingo ndefu vilevile kumuwezesha kuokota chakula chake kutoka ardhini. Wakati mwingine hutokea kwamba mdomo mrefu unatengenezwa kufanya kazi ya shingo ndefu ikipelekea kwenye urahisi utakiwao.

Je, huoni kwamba uumbaji wowote unaofikiria utauona barabara na umejaa ustadi?
Tizama kwenye mimea ambayo ndege hawa wanaitafuta nyakati za mchana. Haitokei kamwe kwamba haipatikani lakini hawaipati ikiwa imekusanyika mahali pamoja. Wanaipata kwa kuitafuta na kwenda huku na huko. Hali kama hii hujitokeza katika viumbe wengine

Utukufu ni wake Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.). Ambaye amegawanya riziki na akapanga njia mbalimbali za namna ya kuisambaza.

Haikupangwa katika hali ya kwamba isifikiwe (isipatikane hiyo riziki) kwa viumbe ambavyo huihitaji wala haikupangwa, kwamba njia ya kuifikia iwe nyepesi na kwamba ipatikane bila juhudi zozote kufanyika kwani kuwa hivyo kungekuwa hakuna maana kama chakula kingelipatikana kwa wingi katika sehemu moja yoyote ile wanyama wangekuwa walafi, kamwe wasingeitoka sehemu hiyo, ingepelekea kutokuyeyushwa chakula tumboni na (kutokea) maangamizi.

Watu pia, kwa sababu ya uwingi (wa riziki) wangepatwa na hali ya kuwa na kiburi na majivuno na matokeo ya misiba na matendo maovu."

Ndege Wa Usiku

Imam (a.s.) aliniuliza, "Unajua kuhusi ndege kama vile bundi na popo ambao hutoka nje wakati wa usiku tu, na kuhusu vitu walavyo kama chakula chao?”

Nilijibu,"Sijui."

Yeye (a.s.) akasema, "Chakula cha hawa ni mchanganyiko wa aina mbalimbali za wadudu waliotawanyika katika anga, k.m. mbu, nondo, wadudu walio kama nzige na buibui n.k. Siku zote wako kwenye anga, hakuna sehemu ilivyo huru bila wao kuwepo. Kama ukiwasha taa usiku juu ya paa au sehemu yoyote ya eneo la nyumba, wengi wa aina mbalimbali za wadudu hao hujikusanya kuizunguuka taa (hiyo).

Wametokea wapi? Hakika wametokea sehemu za karibu tu. Kama mtu yoyote atasema kwamba wanatokea misituni na mashambani, atajibiwa kwa kuulizwa kwamba ni vipi wanafika upesi sana na vipi wanaweza kuiona taa iliyowashwa ndani ya nyumba iliyozunguukwa na nyumba nyingine nyingi, ambapo kusema kweli hawachukui muda mrefu kuja kuizunguuka hiyo taa. Ni wazi kutokana na hili kwamba wote hawa wametawanyika kila mahali katika anga na ndege wale wanaotoka usiku kuwakamata na kujilisha kwa hao.

Tizama vipi lishe ilivyoandaliwa kwa ajili ya ndege ambao wanatoka usiku kwa njia ya wadudu hawa, waliotawanyika katika anga.

Jaribu kuelewa madhumuni ya uumbaji wa viumbe hivi vyenye uhai, isije ikawa mtu fulani akafikiria kwamba vimeumbwa bure bila faida yoyote.

Popo ni kiumbe wa ajabu, yu katikati baina ya ndege na mnyama wa miguu minne, kwa kweli amejamiika zaidi kwa mnyama wa miguu minne, na masikio mawili yatokezayo, meno na nywele nzuri. Huzaa watoto wake, ambao huwalisha kwa maziwa yake. Hukojoa na kunya. Hutembea katika misimu yote minne. Tabia hizi zote ni kinyume (tofauti) na zile za ndege. Hujitokeza nje usiku tu na kujilisha kwa wadudu waliosambaa katika anga.

Baadhi (ya watu) husema hali chochote, bali huishi tu kwa hewa fufutende (vuguvugu) kama lishe.
Hii siyo sahihi kwa sababu mbili, kwani kukojoa na kunya, ni vithibitisho vya matumizi ya chakula kigumu. Kisha ana meno, kama asingekuwa anakula, meno yangekuwa hayana maana, ambapo kwamba hakuna kitu katika uumbaji kisicho na maana.

Kiumbe huyu ana sifa zijulikanazo vizuri. Kinyesi chake kimechanganyika na vitu vingine. Umbile lake la kushangaza lenyewe ni la ajabu. Huruka huku na huko kama apendavyo kwa faida yake mwenyewe - ishara ya Ujuzi Mkuu wa Mwenye Nguvu zote Allah (s.w.t.).

Ndege afumae (kiota) hujenga kiota chake wakati mwingine katika miti. Kama akiona nyoka mkubwa anaelekea kwenye Kiota chake, hupatwa na wasiwasi. Hutafuta huku na huko njia za usalama Mara tuu anapopata mbegu yenye miba huichuma na kuitupa kutokea kwa juu kwenye mdomo uliowazi wa nyoka. Nyoka huanza kugaragara kwa uchungu na humsukasuka mpaka kufikia kifo.

Kama nisingekuelezea hivi, je, ungeweza kudhania kwamba mbegu yenye miba ingeweza kuwa na faida kama hizi, au mtu yoyote angeweza kufikiri kwamba ndege mkubwa au mdogo, angeweza kufanikisha mpango kama huo?

Jifunze somo kutokana na hili. Yako mambo mengine mengi yenye faida zisizojulikana ambazo huhitaji maelezo ya matukio mapya au habari zitakiwazo kufahamika.

Nyuki

Hebu fikiria kuhusu nyuki na juhudi za pamoja za kuzalisha asali na kundi la nyuki la pande sita, na werevu mwingi wa silika uliowekwa ndani (yake). Utaona ni wa kustaajabisha mno na wa kutatanisha, wakati ukifikiria kazi zake. Utaona uzalishaji wao (wa asali) ni mkubwa kabisa na ni tumizi zuri kwa wanadamu.

Na kama utamtizama fundi huyo (nyuki) utamuona hana akili, asingeweza kujitambua mwenyewe, nini la kusema kuhusi mengine.

Hivyo kuna hoja iliyo wazi katika hili kwamba usahihi katika ufundi na ustadi si vyenye kutokana na nyuki (mwenyewe) bali ni (Ufundi na Ustadi) Wake Yeye Mwenye Kuweza yote, Ambaye amemuumba katika umbo hilo na akamtiisha kwa kuwahudumia wanadamu.

Nzige

Hebu mtizame nzige alivyo mnyonge, lakini aliye imara. Hakuna yoyote awezaye kujikinga dhidi ya kundi la nzige, kama litauvamia mji.

Je, hujui kwamba kama yeyote yule katika Wafalme wa ulimwengu mzima atoke na majeshi na jamaa zake kuwapiga nzige, asingeshinda?

Je, hii siyo hoja yenye kudhihirisha Uwezo Mkuu wa Mwenye Ngugu zote Allah (s.w.t.) kwamba (viumbe) vyenye nguvu nyingi kabisa katika uumbaji wake visingeweza kuhimili shambulio la viumbe vilivyo dhaifu kabisa katika Viumbe Vyake? Watazame jinsi wanavyoifunika ardhi yote kama mafuriko, wakizagaa juu mlimani, jangwani, uwandani na mjini, wote kwa umoja, hivyo kwamba kundi lao huzuia hata mwanga wa jua.
Sasa kadiria ni miaka mingapi ingehitajika kutengeneza kundi hilo kwa mkono (wa mtu).

Mwenye Nguvu zote Allah ametoa hapa hoja nyingine ya uwezo Wake Mkuu ambao hakuna kiwezacho kuupunguza na kwa huo hakuna kiwezacho kuuongeza.

Samaki

Hebu fikiria samaki na hili ambazo zipo chini ya mazingira iliyo amriwa kuendelea kupelekea maisha yake. Haina miguu, kwa kuwa makazi yake ni katika maji na haihitaji kutimbea (na miguu). Haina mapafu, kwa vile haiwezi kuvuta hewa. Imewekwa (iishi) chini ya uso wa maji.

Badala ya miguu, imejaaliwa na mapezi madhubuti ambayo kwayo hupazua maji katika pande zote; kama vile baharia wa mashua akatavyo maji katika pande zote kwa makasia yake. Ina mfuniko wa magamba mazito yaliyounganishwa na kile lingine kama pete za koti la deraya kujilinda dhidi ya ajali. Ina stadi kali ya kunusa, kama fidia kwa uoni dhaifu usababishwao hivyo na maji. Hunusa kitu chake kutoka kwa mbali na (hapo) hukifuatia. Ni kwa njia ipi nyingine ingeweza kutumia kufahamu asili na mahali kilipo chakula (chake)? Na, elewa vilevile, kwamba inazo tundu sehemu zote kuanzia kinywani mpaka masikioni, ambazo kwazo maji hupita na kuipa stawisho la kuburudika sawasawa kama lile linalopatikana kwa wanyama wengine kwa kuvuta kewa halisi iliyopoa ya upepo wa asubuhi.

Sasa, fikiria tabia zake za kiuzazi. Idadi ya mayai ndani ya samaki ni zaidi ya kadiri. Sababu ni kuongeza chakula kiwezekanacho kuwa kwa viumbe vingine hai kwa vile wengi zaidi katika wao wanaishi kwa kula samaki pembezoni mwa madimbwi ya maji, katikati ya mapori. Mara tu samaki apitapo, humrukia juu yake. Kwa vile samaki ni mawindo ya hayawani, ndege, watu na hata samaki wengine, mambo yamepangwa kwa namna kuiweka idadi ya samaki kuwa juu.

Hebu fikiria aina za wanyama wenye rangi mbalimbali, ma-kaka (maganda), maisha ya majini na jamii mbalimbali za samaki, kupata fununu ya ustadi mkubwa mno wa Mwenye nguvu zote Allah kwa upande mmoja na silika (maumbile) dhaifu ya elimu hii imilikiwayo na viumbe. Hawana mpaka katika idadi wala sifa zao hauziwezi hujulikana, isipokuwa kwamba asijue moja baada ya nyingine kwa fursa ziwezazo kutokea.

Kama kwa mfano "Cochineal" (vitu vyenye rangi angavu nyekundu iliyofanywa kutokana na miili iliyokauka ya aina fulani ya wadudu), rangi yake ilisomwa yote na watu, imeelezwa mbweha azururaye ufukweni mwa bahari, alimpata na kumla Halzuuni (mdudu mwenye rangi). Mdomo wake ulipatwa na rangi. Rangi hiyo iliwavutia watu ambao walianza kumtumia mdudu "Cochineal" kama rangi ya kuchovyea vitu. Viko vitu vingine vingi ambavyo tabia zao huja kujulikana kwa watu mara kwa mara.”

Ilikuwa adhuhuri. Bwana wangu aliamka kwa ajili ya Sala, akiniambia nije kwake (tena) mapema asubuhi ijayo.

Nilirejea nyumbani nikiwa nimefurahishwa maradufu kwa tunu ya maelekezo katika elimu niliyopata kutoka kwake.

Kwa shukurani nyingi kwa Mwenye Nguvu zote Allah niliupitisha usiku huo kwa kufurahia sana.