read

Ahlul Bayt A.S.

68. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Bihar al- Anwar , J.27, Uk. 113:

“Mfano wa Ahlul-Bayt yangu kwa Ummah wangu ni sawa na Safina ya Mtume Nuh a.s. Wote wale watakaoipanda ndani yake basi wameokolewa na wote wale waipingao, basi wamezama na kupotea ……….”

69. Amesema Al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. Imam wa tano, Bihar al-Anwar, J. 2, Uk. 144:

“Ahadith zetu (za Alhul Bayt) zinahuisha nyoyo.”

70. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Bihar al- Anwar , J.38, Uk. 199:

“Muhuishe mikutano na mikusanyiko yenu kwa makumbusho ya ‘Ali ibn Abi Talib a.s.”

71. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Ikmal-ud- Din, J. 1, Uk.253: na yenye maana inayokaribia katika Yanabi-ul-Muwaddah, uk. 117:

Ipo riwaya kupitia Jabir-al-Ju’fi iliyopokelewa kutoka Jabir-ibn-Abdillah isemayo: Mimi nilisema: “Ewe Mtume wa Allah swt, sisi tunamwelewa Allah swt na Mtume wake s.a.w.w. Sasa jee hawa ‘Ulul-Amr ni wakina nani ambao utiifu wao umefaridhishwa sawa na wako ?

Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. alisema:

“Ewe Ja’abir ! Wao ni, baada yangu, Makhalifa wangu na Ai’mmah wa Waisilamu; wa kwanza miongoni mwao ni ‘Ali ibn Abi Talib a.s.; atafuatia (Imam) Hassan, na (Imam) Husayn; atafuatia ‘Ali ibn il Husayn; atafuatia Muhammad ibn ‘Ali; ajulikanaye katika Tawrati kama Baqir, ambaye utakutana naye, Ewe Ja’abir ! Pale utakapomtembelea, umpe salaam zangu. Baada yake Ja’far bin Muhammad; atamfuatia Musa ibn Ja’far; atafuatia ‘Ali ibn Musa, atafuatia Muhammad ibn ‘Ali; atafuatia ‘Ali ibn Muhammad, atafuatia Hassan ibn ‘Ali; na baada yake (atakuja) Al-Qaim, ambaye jina lake ni sawa na jina langu. Yeye ndiye atakaye kuwa Mamlaka Ya Allah swt juu ya ardhi hii na Aliyebakia miongoni mwa Waja wake. Yeye ndiye mwana wa (Al-Imam) Hassan ibn ‘Ali ( al-‘Askari). Huyu ndiye shakhsiyyah ambaye Allah swt atafungua Dhikiri zake Mashariki na Magharibi na huyu ndiye Shakhsiyyah ambaye atakuwa ghaibu kwa wafuasi na wapenzi wake ambavyo hakuna nyoyo zozote zile zinazoweza kukubali isipokuwa nyoyo za wale tu ambao Allah swt amekwisha kuzijaribu kwa ajili ya Imani.”

Ja’abir alisema: “Mimi nilimwuliza ‘Ewe Mtume wa Allah swt ! Je wafuasi wake watafaidika naye wakati akiwa ghaibu ? Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alijibu: ‘Naam. Kwa kiapo cha Yule aliyenichagua kuwa Mtume, wao watafaidika kwa nuru yake na watafaidika kwa ibada akiwa ghaibu kama vile kufaidika kwa watu kutokana na (nuru ya) jua hata pale linapofunikwa kwa mawingu…….’”

72. Amesema Malik ibn Anas kuhusu mema ya Imam As-Sadiq a.s. , Bihar al- Anwar J. 47. Uk. 28:

“Hakuna macho yaliyowahi kuona, hakuna masikio yaliyokwisha kusikia, na wala hakuna moyo uliyokwisha shtushwa kwamba kunaweza kuwapo na mtu yeyote aliye bora zaidi kuliko (Imam) Ja’far as- Sadiq (a.s.) katika Taqwa, elimu, ibada na Ucha-Allah swt.”

73. Amesema Al Imam Hussain ibn ‘Ali bin Abi Talib a.s., Al-Irshaad, Uk. 204:

“Kwa roho yangu, hakuna Imam isipokuwa ni Hakimu kwa Kitabu, anaimarisha uadilifu, anaamini katika Dini ya Ukweli, na anajizuia nafsi yake pamoja na njia ya Allah swt.”