read

Dhuluma na Uonevu

336. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika Thawab-ul-A’amaal, Uk. 309:

“Siku ya Qiyama, mwitaji ataita: “Je wako wapi wadhalimu na wasaidizi wao na wale wote walio watengenezea wino au walio watengenezea na kuwakazia mifuko yao au walio wapatia wino kwa ajili ya kalamu zao ? Kwa hivyo, wakusanye watu wote hawa pamoja nao!’”

337. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema katika Nahjul-Balagha, Uk. 347:

“Kwa kiapo cha Allah swt, Iwapo nitapewa umiliki wa nchi zote pamoja na yale yote yaliyomo chini ya mbingu zilizo wazi ili nimuasi Allah swt kwa kiasi cha mimi kunyofoa punje moja ya shairi kutoka kwa sisimizi, basi mimi kamwe sitafanya hivyo.”

338. Amesema Al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika Al-Kafi, J. 2, Uk. 330:

“Zipo aina tatu za dhuluma: moja, ni ile ambayo Allah swt anasamehe, pili, ile ambayo Allah swt haisamehe, na tatu ni ile ambayo Allah swt haipuuzii.

Hivyo, dhuluma ambayo Allah swt haisamehe ni ukafiri dhidi ya Allah swt. Na dhambi ambayo Allah swt anaisamehe ni ile mtu anachojifanyia dhidi yake mwenyewe na Allah swt. Lakini dhambi ambayo Allah swt haipuuzii ni ile ambayo inavunja haki za watu. “

Ufafanuzi

Aina ya tatu ya dhuluma ni ile ambayo mtu hukiuka na kuvunja haki za watu. Njia saheli ya kutaka kusamehewa ni kwanza kumridhisha yule ambaye haki zake zimekiukwa na kuvunjwa. Iwapo mtu huyo atamsamehe yule aliyemvunjia haki zake, basi hapo dhuluma hiyo itageuka kuwa dhuluma dhidi yake binafsi. Na hapo ndipo ataweza kuwa mstahiki wa kuomba msamaha wa Allah swt.

339. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema katika Tasnif Ghurarul Hikam, J. 2, Uk.36:

“Dhuluma husababisha miguu kupotoka, inaondoa baraka na kuangamiza umma au taifa.”

340. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema katika Nahjul-Balagha, Barua na 53:

“Hakuna kitu kinachovutia na kuharakisha kuondolewa kwa neema za Allah swt ispokuwa kuendekea kwa dhuluma, kwa sababu Allah swt anazisikiliza dua za madhulumu na huwa yuko tahadhari pamoja na madhalimu.”