read

Elimu na Fadhila za Kuifundisha

115. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika Ithna-Ahariyyah, Uk. 11:

“Mtu yeyote aliyekuwa na elimu kuhusu swala fulani na akaificha pale atakapoulizwa basi Allah swt atamkasirikia kwa ghadhabu za moto.”

(yaani mtu anapokuwa na habari ambazo zitamsaidia mtu aliyepatwa na shida na ikaweza kumsaidia kuimarisha hali yake, badala ya kumsaidia yeye akaificha, basi hapo kwa hakika ametenda dhambi kubwa.)

116. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar, J. 92, Uk. 19:

“Qur’an Tukufu ni chuo kikuu; hivyo jielimisheni kiasi muwezavyo kutokea chuo hiki.”

117. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika Sunnahn-i-ibn-Majah, J. 1, Uk.88:

“Kwa hakika, kile kitakachoendelea kumfikia mtu hata baada ya kufa kwake, miongoni mwa matendo yake mema ni: elimu ambayo yeye amewafundisha na kuieneza kwa wengineo, mtoto mwema aliyemwacha, kuacha Qur’an Tukufu ikapatikana.”

118. Amesema al-Imam ‘Ali ar-Ridha a.s. katika Ma’anil Akhbaar, Uk. 180 na ‘Uyun-il-Akhbaar –ir- Ridha, J. 1, Uk. 207:

“Rehema za Allah swt ziwe juu ya yule ambaye anazihuisha amri zetu.”

Na alikuwapo mtu akamwuliza Imam a.s. Ni vipi wanaweza kuhuisha amri zao, na Imam a.s. alimjibu:

“Anaweza akijifunza elimu zetu na akawafundisha watu. Kwa hakika, iwapo watu wangelikuwa wamezijua faida na mema ya semi zetu, basi kwa hakika wangalitufuata sisi.”

Elimu – Hekima – Ma’arifa

119. Elimu ni fidia kwa juhudi za akili.

120. Wema ni sababu kuu ya elimu.

121. Kumwogopa Allah swt ni matokeo ya elimu.

122. Jumla ya utukufu wote, ni elimu au ma’arifa.

123. Yeyote afundishaye herufi moja, amenifunganisha nae minyororo.

124. Elimu iliyo bora ni ile inayomfaa mwenye kuwa nayo.

125. Elimu ni hazina na maisha.

126. Unyenyekevu ni matokeo ya elimu na ma’arifa.

127. Mtu mwenye elimu yu hai hata kama amekufa.

128. Dini ni ghala na elimu ni mwongozo wa kuifikia ghala.

129. Ili kupata ufanisi itikia elimu na kupuuzia ujahiliya.

130. Wengi wanaelezea ma’arifa, lakini ni wachache waiingizayo akilini mwao.

131. Bakhshishi iliyo kamili ya Allah swt ni ile maisha iliyotegemea elimu na hekima.

132. Wapumbavu wengi mno wanawafanya wasomi kuwa wachache.

133. Aliyeelimika anamwelewa vyema mjinga kwani yeye binafsi alikuwa mjinga awali.

134. Na mtu aliye jahili hataweza kumwelewa mtu aliyeelimika kwani hajaelimika mwenyewe.

135. Wana elimu wanaishi katika kiwiliwili kilichokufa cha ujahili.

136. Ma’arifa huuwa ujahili.

137. Elimu ndiyo iipatiayo maisha Roho.

138. Ma’arifa chache (ya Allah swt) huharibu mwenendo wa mtu.

139. Hakuna chochote kile pasi na nuru ya kweli tu itakayokutakasisha.

140. Kuwaheshimu waliosoma ni kumheshimu Allah swt.

141. Ma’arifa ni chanzo cha khofu ya Allah swt

142. Kile kikomazacho ma’arifa ni matendo kwa kutumia hekima na ma’arifa hayo.

143. Kufundisha ndiko kujifunza.