read

Elimu na Fadhila za Kujifunza

108. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar , J. 1, Uk. 184:

“Yeyote yule atafutaye elimu ni sawa na mtu anayefunga saumu mchana na akikesha macho usiku kucha akifanya ibada. Iwapo atajifunza elimu kwa sehemu fulani, basi itakuwa kwake ni afadhali kabisa hata kuliko kuwa na dhahabu ya ukubwa wa mlima Abu Qubais na ambayo itagawiwa sadaqa katika njia ya Allah swt.”

109. Al-Imam Zaynul ‘Aabediin a.s. Amesema katika Usul-i-Kafi, J. 1, Uk. 35:

“Iwapo watu wangalikuwa wakitambua kile kilichopo ndani ya kutafuta elimu, basi wao wangali itafuta hata kama itawabidi kusafiri na hata kuhatarisha maisha yao katika kuipata.”

110. . Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema, Qurar-ul-Hikam, Uk. 348:

“Kutafuta elimu haitawezakana wakati mwili unastareheshwa.” (yaani mtu hataki kutaabika)

111. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s. katika Bihar al- Anwar, J. 2, Uk.152:

“Hifadhini maandiko na vitabu vyenu kwa sababu hautapita muda mutakapovihitaji.”

112. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema katika Al-Kafi, J. 1, Uk. 30:

“Kwa hakika, kukamilika kwa Dini ni kule kuitafuta elimu na kuitekeleza ipasavyo, na muelewe waziwazi kuwa kutafuta elimu ni faradhi zaidi kwenu nyinyi kuliko kutafuta mali na utajiri.”

113. Amesema al-Imam al-Hassan ibn Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. katika Bihar al- Anwar, J. 78, Uk. 111:

“Wafundisheni watu wengine elimu muliyonayo na mujaribu kujifunza elimu waliyonayo wengineo.”

114. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar , J. 1, Uk.167:

“Fadhila za elimu zinapendwa zaidi na Allah swt hata kuliko fadhila za ibada.”