read

Hadith ya Ufunguzi

1. Amesema al-Imam as- Zayn al-‘Aabidiin a.s., katika Bihar al- Anwar, j. 90, uk 187 na Sahifah as-Sajjadiyyah, uk. 572:

“Sifa zote ni za Allah swt, na kusifiwa Kwake ni haki Yake: sifa zisizo na kifani ndizo zinazomstahiki Yeye. Na mimi najiepusha kwa msaada wake dhidi ya shari za nafsi yangu: Kwa hakika mwanadamu yupo katika kutenda madhambi isipokuwa wale waliobarikiwa na Mola wao. Naomba msaada wake Allah swt dhidi ya maovu ya Shaytani ambaye daima ananiongezea dhambi moja juu ya lingine. Naomba msaada wake Allah swt dhidi ya watawala waovu, watawala katili, na maadui wa nguvu.”

“Ewe Mola ! Naomba unifanye mimi kuwa mmoja wa Majeshi yako, kwa sababu kwa hakika Majeshi Yako tu ndiyo yenye kushinda; na unifanye miongoni mwa wanachama Wako, kwani kwa hakika, chama Chako tu ndicho kitakachofanikiwa; na unikubalie kama mmoja wa wapenzi Wako, kwani kwa hakika, wapenzi wa Allah swt hawana hofu na kamwe hawatahuzunika.”

“Ewe Mola ! Naomba uniimarishie Dini kwa ajili yangu, kwani hiyo ndiyo hifadhi ya matendo yangu yote; na unitengenezee Aakhera yangu, kwa sababu hakuna shaka kuwa hiyo ndiyo mwisho wangu wa kudumu na kuepukana na watu wenye dharau na dhihaka, na uyafanye maisha yangu yawe ya kuniongezea mema, na mauti yangu yawe ndiyo kujitoa huru kutokana na kila aina ya kasoro za magonjwa.”

“Ewe Mola ! Mbariki Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Mtume wa mwisho katika jamii ya Mitume yote, na Ahli Bayti a.s. tukufu, na vile vile Masahaba wake wema, na naomba unijaalie mahitaji matatu kwa leo: Usinibakizie dhambi yoyote ile isipokuwa umenisamehe na wala huzuni yoyote ile isipokuwa umeniondolea, wala kusikwapo na adui isipokuwa wewe umemwondosha kwa jina lako tukufu la Allah ambayo ni jina bora kabisa i.e.Bismillah, Mola wa Mbingu na Ardhi …..”

Kumjua Allah Swt, Ukuu na Baraka Zake

2. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Al-Khisal,322:

“Enyi Watu ! Kwa hakika hakutakuwapo na Mtume baada yangu, na wala hakutakuwapo na Ummah baada yenu (Waislamu). Hivyo, Muwe waangalifu katika kumwabudu Allah swt, musali sala tano za siku, mufunge saumu katika mwezi uliowekwa (Ramadhaan al-Mubarak), mufanye Hijja ya Nyumba ya Allah swt (Al-Ka’aba huko Makkah al-Mukaramah), mutoe Zaka kutoka mali zenu kwa ajili ya kuitakasisha nafis zenu kwa hayo, na mutii amri za Wale wenye mamlaka, ili muweze kuingia Pepo ya Mola wenu.”

3. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema, katika Nahjul-Balagha, Semi na.129:

“Kwa kuwa na tasawwuri (ufahamu) ya Ukuu wa Mola wako basi itakufanya wewe utambue udogo wa viumbe katika mitazamo yako.”

5. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema, katika Bihar al- Anwar, j. 77, uk. 289:

“Tawba ni kwa ajili ya yule ambaye ametakasisha kwa ajili ya Allah swt matendo, elimu, mapenzi, bughudha, kuchukua, kutoa, misemo, ukimya, matendo na asemavyo.”

7. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s., katika Bihar al- Anwar, j. 70, uk. 25:

“Moyo ni mahala pa takatifu pa Allah swt, hivyo, basi hakikisha hapaingii kitu kingine chochote isipokuwa Allah swt tu.” (Moyo mtukufu ni wa Allah swt tu. Hivyo mapenzi ya dunia isivyo sahihi, lazima iwekwe mbali.)

9. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s., katika Bihar al- Anwar,j. 93, uk. 162:

“Wafuasi wetu ni wale ambao wanapokuwa peke yao, wanamkubuka Allah swt kwa kupita kiasi.” (Kwa hivyo, wao hujiepusha kutenda madhambi wanapokuwa peke yao wakati ambapo hakuna kizuizi cha kuwazuia wao wasitende madhambi na badala yake humkumbuka Allah swt kwa kupita kiasi.).

11. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s., katika Al-Kafi, J.2, Uk. 426:

“Kwa kiapo cha Allah swt ! Yeye, aliyetukuka, huwategemea kwa mawili:wao waungame na kushukuru Kwake kwa neema ili Yeye awaongezee; na waungame kwa madhambi yao ili kwamba Yeye awasamehe madhambi yao.”

13. Amesema al-Imam Husayn ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s., katika Safinat-ul-Bihar, J. 2, Uk. 180:

“Kwa hakika, Allah swt, aliye Mkuu, hakuwaumba wanadamu isipokuwa kwa kumjua Yeye na baada ya kumjua Yeye kumwabudu kwa kumjua Yeye; na wakati wanapomwabudu basi kusikuwepo na haja tena ya kumwabudu yeyote mwingine isipokuwa Yeye peke yake.”

15. Amesema al-Imam Zayn-al-‘Aabediin a.s., katika Safinat-ul-Bihar, uk. 517:

“Hakuna maangamizo (Jahannam au Motoni) kwa ajili ya Mumiin aliye na sifa tatu: Kuungama na kukubali kuwa hakuna Allah swt mwingine isipokuwa Allah swt tu peke yake, pekee ambaye hana mshiriki; Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni mtetezi; ukubwa usio na kipimo cha Rehema za Allah swt.”