read

Haki za Waislamu Wenzako

341. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar , J. 75, Uk. 150:

“Yeyote yule anayemhuzunisha Mwislamu mwenzake basi kamwe hawezi kumfidia hata kama atamlipa dunia nzima kwani haitatosha (ispokuwa iwapo atatubu na kumfurahisha Mwislamu huyo).”

342. Al-Imam Musa al-Kadhim a.s. Amesema katika Bihar al- Anwar, J. 2, Uk. 75:

“Moja ya faradhi miongoni mwenu kuelekea Mwislamu mwenzenu ni kutokumficha kitu chochote ambacho kinaweza kumfaidisha humu duniani au Aakhera.”

343. Al-Imam Al-Hassan Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.

“Watendee watu vile utakavyopenda wewe kutendewa.”

344. Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika Ghurarul-Hikam, Uk.181:

“Alla swt humrehemu mtu ambaye anahuisha yaliyo haki na kuangamiza na kuteketeza yale yaliyo batili, au hukanusha dhuluma na kuimarisha uadilifu.”

345. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s. katika Tuhfatul-Uqul, Uk. 277:

“Tabia hizi nne ni kutokea tabia za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w: haki, ukarimu, subira na kuvumilia katika shida, na kusimamia haki ya Mumiin.”

346. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika Nahjul-Balagha, Barua na 53:

“Kwa hakika ni watu wa kawaida ndio walio nguzo za Dini, nguvu ya Waislamu na hifadhi dhidi ya maadui. Hivyo mwelekeo wako daima uwe kuelekea wao na uwanyenyekee.”

347. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s.katika Al-Kafi, J. 2, Uk. 170:

“Allah swt haabudiwi zaidi ya thamani kuliko kutimiza haki ya Mumiin.”

348. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w katika Bihar al- Anwar, J. 67, Uk. 72:

“Yeyote yule anayemuudhi Mumiin, basi ameniudhi mimi.”

349. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w katika Mustadrak al-Was’il,J. 17,Uk. 89:

“Yeyote yule atakayemdhulumu Muumin mali yake pasi na hakie, basi Allah swt ataendelea kumghadhibikia na wala hatazikubali matendo yake mema atakayokuwa akiyatenda; na hakuna hata mema moja itakayoandikwa katika hisabu zake nzuri hadi hapo yeye atakapofanya tawba na kuirudisha hiyo mali kwa mwenyewe.”