read

Kulinda Heshima ya Waumini

326. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika Bihar al- Anwar , J. 74, Uk. 301:

“Ni faradhi kwa kila Mwislamu kusitiri na kuzificha aibu sabini (70) za Mwislamu mwenzake (ili kulinda heshima yake).”

(Makosa na kasoro zake zote zishughulikiwe kibinafsi na wala zisienezwe na kutangazwa kwa watu wengine).

327. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika Bihar al- Anwar, J. 74, Uk. 165:

“Kubali msamaha akuombao Nduguyo Mwislamu na kama hakufanya hivyo, jaribu kumvumbulia hivyo.”

328. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika Mustadrak Al-Wasa’il al-Shiah’il-ush-Shiah, J. 12, Uk. 305 na 14155:

“Hali mbaya kabisa ya uhaini ni kutoboa habari zilizo siri.”

329. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika Ghurar-ul-Hikam, Uk. 322:

“Kumuonya kwako aliyetenda makosa miongoni mwao au mbele ya watu ni kumdhalilisha.” (Inakubidi uongee naye katika faragha).”

330. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s.katika Al-Kafi, J. 2, Uk. 192:

“Katika matendo yote ayapendayo Allah swt, ni kule kumletea furaha Mwislamu kwa mfano: kumshibisha, kumwondolea majonzi yake, au kumlipia madeni yake.”