read

Kumwamini Allah na Kuipata Furaha Yake

39. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s., Bihar al-Anwaar, J. 71, Uk. 208:

“Baba yangu aliniambia kuhusu baba yake kuwa mtu mmoja kutoka mji wa Kufa alimwandikia baba yake yaani Al-Husayn ibn ‘Ali a.s., akimwuliza kuhusu mema ya dunia hii na mema ya Akhera. Kwa hayo Imam a.s. alimwandikia (katika majibu):

“Kwa jina la Allah,aliye Rahmaan na Rahiim’. Baadaye akiendelea ‘Kwa hakika yeyote yule atakaye furaha ya Allah swt hata kama hata wafurahisha watu, basi Allah (swt) humtosheleza katika masuala ya watu. Lakini, yule ambaye hutaka furaha za watu wakati anamuudhi Allah swt, basi Allah swt humwachia watu (na yeye atakuwa mbali na baraka za Allah swt), Wassalaam’.”

40. Amesema Al-Imam Zayn Al-Abedin a.s. , Al-Kafi, J. 2, Uk.81:

“Yeyote yule atendaye matendo yake kwa mujibu wa vile alivyoamrisha Allah swt, ni miongoni mwa watu bora.”

42. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s., Al-Kafi, J.2, Uk. 124:

“Yeyote yule aliye na mapenzi ya Allah swt, anachukia kwa ajili yake Allah swt, na anatoa msaada kwa ajili ya Allah swt, basi huyo ni miongoni mwa wale ambao Imani yao imekamilika.”

44. Amesema Al-Imam Al-Hasaan Al-Askari, Imam wa Kumi na Moja, a.s., Bihar al-Anwaar, J.17, Uk. 218:

“Hakuna sifa zaidi ya hizi mbili: Kuwa na Imani kwa Allah swt na kuwa mwenye manufaa kwa Waislamu.”