read

Kuomba Dua

56. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s., Al-Kafi J. 2, Uk.493:

“Dua yoyote inayoombwa kwa Allah swt, inakuwa imezuiwa na mbingu hadi hapo iwe imeshirikishwa na Salawat i.e. kumsaliwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.pamoja na Ahlil Bayt a.s.”

57. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s. Al-Kafi J.2, Uk.491:

“Muminiin waombao Dua zao hazikukubaliwa humu duniani watatamani kuwa dua zao hata moja zisingelikubaliwa pale watakapoonyeshwa hapo Aakhera, mema kupita kiasi ya thawabu (atakayopewa yeye kwa kutokujibiwa Dua zake na kwa mateso na shida alizozipata akiwa humu duniani).”

58. Amesema Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Bihar al-Anwar, J.93,Uk. 295:

“Tendo lipendwalo sana mbele ya Allah swt humu duniani ni Dua na ibada iliyo bora kabisa mbele Yake ni unyenyekevu na ucha-Allah swt.”

59. Amesema Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Al-Khisal cha Sadduq, Uk. 302:

“Milango ya Peponi ipo wazi kwa nyakati tano: wakati mvua inyeshapo; wakati wa Vita vitukufu; wakati wito wa Sala utolewapo (wanapotoa Adhaan); wakati wa kusoma Qur’an Tukufu wakati ambapo jua linazama na linachomoza alfajiri.”

60. Amesema Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Bihar al-Anwar, J.93,Uk. 343:

“Mujiweke tayari kuomba Dua katika nyakati tano: Wakati isomwapo Qur’an; Wakati utolewapo Aadhaan; Wakati inaponyesha mvua; Wakati wa kwenda kupigana katika vita vitakatifu kwa ajili ya kuwa shahidi; Wakati madhulumu anapoomba dua, kwa sababu yeye hana kizuizi cha aina yoyote chini ya mbingu.”

61. Amesema Al Imam Hussain ibn ‘Ali bin Abi Talib a.s. , katika Dua-i-‘Arafah:

“Ewe Mola Wangu! Wewe U karibu kabisa wa kuombwa; Na mwepesi wa kujibu; na Wewe Mkarimu wa kutoa; na unamtosheleza umpaye; unamsikia vyema akuulizae; Ewe Uliye Rahmaan wa dunia na Aakhera na Mremehevu kote!”

62. Amesema Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Nahjul Balagha, Msemo 135:

“Anayejaaliwa vitu vinne hanyimwi vinne: Anayejaaliwa kuomba Dua hanyimwi kukubalika kwake; anayejaaliwa kufanya Tawba hanyimwi kukubalika kwake; anayejaaliwa kuomba msamaha hanyimwi kusamehewa kwake; anayejaaliwa kutoa shukuurani zake hanyimwi kuongezewa kwake.”

63. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s. Bihar al- Anwar J. 78, Uk. 216:

“Siku ya Qiyama, Allah swt atazihesabu Dua zote alizokuwa akiziomba mja wake na kuzibadilisha katika matendo mema na kwa hayo atawapandisha daraja katika Jannah (Peponi).”

64. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s. At- Tahdhib, J. 4, Uk. 112:

“Ponyesheni magonjwa yenu kwa kutoa Sadaka1 na mujiepushe na balaa za kila aina kwa Dua

65. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s. Wasail-ush-Shi’ah J. 7, Uk. 60:

“Mwombe Allah swt maombi yako na daima uwe ukisisitiza katika kumwomba kwani Allah swt mwenyewe anapenda mno kubakia kwa kumsisitiza miongoni mwa waja wake Muminiin.”

66. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s. Al-Kafi, J. 2, Uk. 467:

“Ninakuusieni muombe Dua’, kwa sababu hamtaweza kumkaribia Allah swt kwa vinginevyo kama hivyo.”

67. Amesema Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Ghurar-ul-Hikam, Uk. 185:

“Inawezekana kuwa wewe umemwomba Allah swt Dua ya kitu fulani ambacho yeye hakukujaalia kwa sababu yeye anataka kukupa kitu kilicho bora zaidi ya kile ulichokuwa umekiomba, hapo mbeleni(unatakiwa kufanya subira - mtarjum).”

  • 1. Nimetarjumu maandiko juu ya sadaqah na hivyo utaweza kupata mengi katika kitabu nilichokiipa jina la Dhambi Kuu la Kutokulipa Zaka, Khums na Sadaqah