read

Kusema Uongo

Kusema Uongo1

498. Anas Ibn Maliki Khisal-i-Sadduq, Uk. 321:

Anaelezea kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema “Chukueni mambo sita kutoka kwangu, na mimi nakubalia, na kutoa dhamana (Ya wewe kuingizwa Jannah)

1. Usiseme uongo

2. Unapo toa ahadi, usivunje

3. Unapo pewa amana na wengine, basi uwe muaminifu

4. Tazama chini (usitende dhambi ).

5. Chunga heshima yako

6. Idhibiti mikono yako na ulimi wako.

499. Amesema Imam Al Hassan al-‘Askari a.s, Bihar al-Anwaar, J. 72, Uk.263:

“Iwapo maovu yote yatawekwa katika nyunba moja, basi ufunguo (wa milango yake ) itakuwa ni uongo.”

500. Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin a.s. Tuhaful-'Uqul, Uk. 201:

“Jiepusheni na kusema uongo hata kama ni uongo mdogo au mkubwa, kama kwa uadilifu au unasema kwa kidhihaki, kwa sababu mtu anaposema uongo mdogo basi anaweza kudiriki kusema uongo mkubwa pia.

501. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Bihar al-Anwaar, J. 75, Uk. 196:

Wakati mmoja Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. aliulizwa kuhusu umbali baina ya ukweli na uongo naye akiwa akionyesha umbali huo baina ya macho yake na maskio yake kwa vidole vinne katika kutoa jibu hilo, “Kile macho yako yanayooona ni ukweli na yale yanayo sikilizwa na maskio yako kwa sehemu kubwa ni uongo.”

502. Amesema Al Imam Muhammad al-Baqir a.s., Al-Kafi, J. 2, Uk. 339:

“Kwa hakika Allah swt ameyawekea makufuli maovu fulani, na ufunguo wake Allah swt ameweka katika pombe, lakini maovu yatokanayo na kusema uongo ni zaidi hata kuliko pombe yenyewe.”

503. Amesema Al Imam ‘Ali ar-Ridha a.s., Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 347:

“Muwe wasema ukweli na mujiepushe na usemaji uongo.”

504. Amesema Al Imam Muhammad al-Baqir a.s., Al-Kafi, J. 2, Uk. 339:

“Kwa hakika Allah swt ameya wekea makufuli maovu fulani, na ufunguo wake Allah swt ameweka katika pombe, lakini maovu yatokanayo na kusema uongo ni zaidi hata kuliko pombe yenyewe.”

505. Amesema Al Imam ‘Ali ar-Ridha a.s. Bihar al-Anwaar,J. 78, Uk. 347:

“Muwe wasema ukweli na mujiepushe na usemaji uongo.”

  • 1. Ndugu msomaji maudhuhi haya yaku sema uongo nime tarjumu vitabu viwili mbalimbali ambavyo nimevipa jina Dhambi kuu katika Islam uharamisho wa uongo. Uongo ni moja katika madhambi makuu katika Islam hivyo ukitaka kusoma zaidi kuhusu uongo nakuomba utafute vitabu hivo viwili juzu ya kwanza na juzu ya pili utayaweza kuona mengi katika somo hiyo.