read

Kusengenya na Kutafuta Kosa

374. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Al-Usul-i- Kafi, J. 2, Uk. 57:

“Uzushi unafanya kazi dhidi ya Imani ya Mwislamu Mumim kwa haraka zaidi kuliko ugonjwa wa Ukoma unavyo enea mwilini.”

375. Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Ghurar-ul-Hikam Uk. 307:

“Msikilizaji wa kile kinacho sengenywa ni sawa na yeye ndio msengenyaji.”

376. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Bihar al-Anwaar, J. 75, Uk. 261:

“Kuacha tabia ya kusengenya ina thamani kubwa sana mbele ya Allah swt kuliko kusali sala yenye raka’h elfu kumi zilizo sunnah.

377. Amesema ‘Abdul Mu’min-il-Ansari. Bihar al- Anwar, J. 75 , Uk. 262:

“Wakati moja yeye alikuwa mbele ya Imam Abil Hassan Musa Ibn Jaffer a.s ambapo Abdillahi Jaffer alikuwa akitokezea na Abdul Mu’min alitoa tabasamu mbele yake. Na hapo Imam a.s alimuuliza Abdul Mu’min iwapo alimpenda Abdillahi Jaffer na alipomjibu Imam kuwa yeye hakumpenda (‘Abdillah) isipokuwa yeye alikuwa ni Imam wa saba. Hapo Imam a.s alimwambia yeye ni ndugu yako, ni Mu’min na Mu’min moja ni ndugu wa Mu’min mwingine hata kama wazazi wake ni watu tofauti. Hivyo amelaaniwa yule anayemtuhumu ndugu yake wakiislamu, analaaniwa yule anayemgeuka ndugu yake Mwislamu, analaaniwa yule asiyempa muongozo mwema ndugu yake Mwislamu, na analaaniwa yule ambaye anamsengenya Mwislamu mwenzake.”

378. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema, Tara'if-ul-Hikam, Uk. 182:

“Mwovu miongoni mwa watu ni yule ambaye anatafuta kasoro za watu wengine wakati akiziacha kasoro zake.”

379. Al Imam Musa al-Kadhim a.s. Amesema, Bihar al-Anwaar, J. 74, Uk.232:

“Amelaaniwa mtu yule ambaye anawasengenya ndugu zake wengine (Waislamu wenzake).”