read

Kutenda Mema na Kuzuia Kutenda Mabaya

354. Allah swt anatuambia katika Qur’an Sura Al Imran, 3, ayah 104.

وَلْتَكُنْ مِنْكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ ۚ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.

355. Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w., Bihar al-Anwaar, J. 100, Uk. 92.

“Itakapofika wakati katika umma wangu ambapo Waislam watakuwa hawa hamasishi wengine wafuate mema na wajizuie na mabaya, basi kwa hakika watakuwa wametangaza vita dhidi ya Allah swt.”

356. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema Bihar al Anwaar, J. 100, Uk. 94.

“Yeyote yule anayeacha kukataza wengine wasifanye maovu kwa maneno na kwa matendo (ni tofauti na kuona maovu yakitendeka) basi huyo ni maiti inayotembea miongoni mwa walio hai.”

357. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Mustadrak Al-Wasa'il-ush-Shi’ah, J. 11, Uk. 278:

“Kumzuia Muislam asitende matendo maovu ni sawa na Allah swt kumlipa thawabu za Hija 70 zilizokubaliwa…”

358. Alisema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Nahjul Balagha, Uk. 392 Barua no. 31:

“Ambizeni miongoni mwenu kutenda mema; basi mtakuwa miongoni mwa watendao mema. Muwazuie wengine wasitende maovu kwa maneno yenu, na mujiepushe, na uwezo wenu wote, na yeyote yule anayetenda hivyo. Mumtumikie Allah swt kama ni wajibu wenu; na angalieni kusiwepo na mlaumiaji au lawama yoyote itakayoweza kuwazuia nyie katika kutekeleza maswala ya Allah swt. Jitupeni katika hatari kwa ajili ya kunusuru ukweli popote pale itakapo hitajika.”

359. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. Amesema, Al-Kafi, J. 5, Uk.56:

“Kwa hakika kuwaambia watu yaliyoya kweli na kuwazuia kwa yale yaliyo potofu ndiyo sirah ya Mitume a.s. na waja wema. Kwa hakika ni jambo moja kubwa (wajib) kutokana na hiyo mambo mengine mengi yaliyo faradhishwa yanaweza kubakia, Ummah zingine zinaweza kunusurika, maelewano ni halali, dhuluma imekatazwa, na hakika amani itajaa juu ya ardhi hii …”

360. Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Ghurar-ul-Hikam,Uk. 236:

“Uimara wa dini ni kule kuamrisha yaliyo mema na kukatza yale yaliyo maovu, na kubakia katika mipaka ya Allah swt.”

361. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Wasa'il ush-Shi'ah, J. 16, uk. 135

“Yeyote anayeona maovu au mabaya yanatendeka basi ayazuie kwa matendo yake, kama ana uwezo huo, bila shaka; kama hawezi kufanya hivyo, basi azuie kwa ulimi wake, na kama hawezi kufanya hivyo pia basi anaweza kulaani kimoyoni.”

362. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. At-Tahdhib, J. 6, Uk. 181:

“Yeyote yule katika ‘Umma wangu anayechukua jukumu la kuamrisha mema na kukataza maovu na anaye jihusisha katika ucha-Allah swt, wataishi kwa raha na mustarehe na watakapo acha kufanya hivyo, basi baraka na neema za Allah swt zitaondolewa kwao.”

363. Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Nahjul Balagha, Barua No. 47, Uk. 422:

Akiwaambia Al Imam Hassan ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s. na Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s. wakati Ibn Muljam (Laana za Allah swt zile juu yake) alipompiga dharuba kali katika Masjid Kufa… “Muogopeni Allah swt (Na akasema tena)Muogopeni Allah swt katika mambo ya Jihad, (Jitihada za vita vitakatifu), kwa misaada ya mali, maisha na mazungumzo yenu katika njia ya Allah swt…”

Msiache kuamrisha mema na kukataza maovu isije hawa waovu wakachukua nafasi juu yenu, na baadaye (Katika hali hiyo) mtakapo Sali basi salah zenu hazita kubaliwa…

364. Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Mustadrak Al-Wasa'il-ush-Shiah, J. 12, Uk. 185:

“Kuamrisha mambo mema ni jambo mmoja jema kabisa miongoni mwa watu.”

365. Amesema Al Imam Ja’far as-Sadiq a.s., Bihar al-Anwaar, J. 100, Uk. 89:

“Matendo mema yote kwa ujumla, ikiwemu Jitihada za vita vitakatifu vya Jihad katika njia ya Allah swt, kwa kulinganisha na kuamrisha mema na kukataza mabaya, ni sawa na kiasi kidogo cha mate ya kulinganisha na bahari yenye kina kirefu.”

366. Amesema Al Imam Muhammad al-Baqir a.s., Al-Kafi J. 5, Uk. 56:

“Allah swt alimteremshia Wahyi Mtume Shua’ib a.s

“Mimi nitawaadhibu watu wako kiasi cha laki moja na kati yao arobaini elfu ni waovu na elfu sitini ni katika watendao wema.”

Mtume Shua’ib a.s aliulizia hawa waovu wanastahili adhaabu lakini hawa watendao wema je? akasema kwa hayo Allah swt alimterenshia wahi tena, “Wao (walio wema) wamehusiana na watendao dhambi na hawakuwa wakali wala hawa kughadhabishwa na matendo maovu wala kwa sababu ya adhabu na khofu zangu.”

367. Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Wasa'il ush-Shi'ah, J. 16, Uk. 120:

“Wambieni wenzenu watende wema na wajizui na ubaya kwani hamutambui kuwa kwa kuamrisha mema kamwe haikaribishi mauti wala kukatisha riziki.

368. Amesema Al Imam Ja’far as-Sadiq a.s., Mustadrak-ul-Wasa'il, J. 12, Uk.181:

“Ole wale watu ambao hawaisaidi Dini ya Allah swt kwa kuamrisha mema na kwa kutaza maovu.