read

Kutoa Mikopo

527. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w., Bihar al-Anwaar, J. 76, Uk. 369:

“Yeyote yule anayeijiwa na ndugu yake Muislam kwa ajili ya kukopa na kama yeye hampi mkopo, basi Allah swt atamharamishia kuingia Jannah siku ambayo waja mema watakuwa wakilipwa na kufidiwa.”

528. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w., Bihar al-Anwaar, J. 76, Uk. 367:

“Yeyote yule anayetakiwa na ndugu yake Muislam kwa kukopeshwa na kama yeye hamkopeshi mkopo, Allah swt atamzuia kuingia Jannah siku ambayo waja wema watakuwa wakilipwa mema yao.”