read

Kuwahudumia Watu

521. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. , Shahab-ul-Akhbar, Uk. 194:

“Yeyote yule atakaye mpunguzia ndugu yake Muislam mwenzake matatizo na shida za dunia hizi, basi Allah swt atampunguzia shida na matatizo yake huko Akhera.”

522. Amesema Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Bihar al-Anwaar, J. 7, Uk. 318:

“Kwa hakika, maombi ya shida za watu zinazokujia wewe ni miongoni mwa neema na baraka za Allah swt juu yako. Hivyo usisikitike kwa sababu ya neema na baraka hizi.”

523. Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Bihar al-Anwaar, J. 74, Uk.166:

“Popote pale utakapoona ndugu yako Muislam ana shida, jaribu kuangalia kama utaweza kumusaidia. (Usimpuuze mpaka akutamkie shida zake.)”

524. Amesema Al Imam Ja’far as-Sadiq a.s. kuwa amenakili kutoka mababu zake a.s. ambao wamemnakili Mtume Muhammad s.a.w.w. akisema, Bihar al-Anwaar, J. 74, Uk. 382:

“Yeyote yule anayemlisha muumin aliye na njaa akashiba basi Allah swt atamlisha mpaka ashibe kutoka matunda ya Jannah;

Na yeyote yule atakaye mvisha nguo yule aliye na shida za nguo, Allah swt atamvisha nguo zilizofumwa na za hariri, na yeyote yule atakaye mumalizia kiu muumin basi Allah swt atamjaalia kinywaji kilichopigwa lakiri;

Na yeyote atakaye msaidia muumin kupunguza shida yake, basi Allah swt atamweka chini ya Arshi yake siku ya Qiyama siku ambayo hakutakuwa na kivuli chochote isipokuwa kivuli cha Arshi yake.”

525. Mtume Muhammad s.a.w.w. Amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 164:

“Watu wanamtegemea Allah swt kwa ajili ya riziki, kwa hiyo mpenzi miongoni mwa watu kwake Allah swt ni yule ambaye anawasaidia wale watu wanaomtegemea Allah swt na kuwafanya watu wa familia ya nyumbani wakawa na furaha.”

526. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w., Al-Kafi, J. 2,

Uk. 199:

“Yeyote yule atakaye wasaidia Waislam ndugu zake wakati wa shida, Allah swt atamwondolea shida na matatizo sabini na tatu, moja ambayo iko humu duniani na sabini na mbili zingine zitakazo kuwa wakati wa shida kubwa, ambapo watu watakuwa mashughuli katika mambo yao ya binafsi (katika Akhera).”