read

Kuwasaidia Wenye Shida

529. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w., Tuhaful-'Uqul, Uk.34:

“Waulizeni maswali walio elimika, muongee pamoja na wale wenye hekima, na mujihusishe pamoja na masikini.”

530. Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Ghurar-ul-Hikam J. 4, Uk. 190:

“Sababu mojawapo ya kuteketea na kupotea kwa mali na utajiri wa mtu ni kule kutowajali na kutowasaidia wale wenye shida.”

531. Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Al-Hayat, Volume 2, Uk. 51:

“Mtume Muhammad s.a.w.w. amemnakili Allah swt kwa kuambiwa usiku wa Mi’raj: Ewe Ahmad! Mapenzi yangu ni kule kuwapenda masikini. Wafanye masikini wawe karibu nawe na uwaweke karibu nawe ili mimi niweze kukufikia wewe………..”

532. Amesema Al Imam Ja’far as-Sadiq a.s.:

“Yeyote yule anayemmalizia muumin njaa yake kiasi kwamba akaridhika kikamilifu, basi hakuna binadamu yeyote miongoni mwetu au miongoni mwa Malaika wanaojua kiasi cha thawabu yake siku ya Qiyamah isipokuwa Allah swt Mmiliki wa Malimwengu yote. Na aliongezea: Kumlisha Muislam aliye na njaa ni njia moja kubwa sana ya kuomba Tawba (usamehevu).”

Baada ya hapo alisoma ayah ya Qur'an Tukufu Sura Al-Balad, 90, ayah 14 – 16.

أَوْ إِطْعَامٌ فِي يَوْمٍ ذِي مَسْغَبَةٍ

يَتِيمًا ذَا مَقْرَبَةٍ

أَوْ مِسْكِينًا ذَا مَتْرَبَةٍ

Au kumlisha siku ya njaa

Yatima aliye Jama’a,

Au masikini aliye vumbini.