read

Mapenzi ya Ahlul-Bayt A.S.

74. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Al-Jami’-ul-Saghir, J. 1 Uk. 14:

“Wafunzeni watoto wenu vitu vitatu: Mapenzi ya Mtume wenu, Mapenzi ya Ahlul-Bayt, usomaji wa Qur’an.”

75. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s., Bihar al- Anwar , J. 74, uk. 354:

“Mtu yeyote ambaye hawezi kutufanyia wema wowote sisi Ahlul-Bayt basi wawafanyie mema wafuasi wetu walio wema; na yeyote yule asiyeweza kutuzuru, basi wanaweza kuwazuru wafuasi wetu walio wema ambavyo thawabu za kutuzuru sisi zitaandikiwa.”

76. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s., Al-Kafi, J.1,Uk. 187:

“Kwa kile kilicho bora kabisa kwa mja kumkaribia Allah swt ni utiifu kwake Allah swt, utiifu kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. na utiifu kwa ulil Amr.”

Aliendelea kusema:

“Mapenzi yetu (ya Ahlul-Bayt) ni Imani na chuki dhidi yetu ni kufr.”

77. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s. Bihar al- Anwar , J.27, Uk.91:

“Kwa hakika zipo daraja za ibada, lakini mapenzi yetu, Ahlul-Bayt, ni ibada iliyo bora kabisa.”