read

Marafiki Wasio Wema

517. Amesema Al Imam Ja’far as-Sadiq a.s., Al-Usul-i- Kafi, J. 2, Uk. 379:

“Anayetafuta uhusiano na marafiki wa wale wanao wadhalilisha wapenzi wa Allah swt basi watambue kuwa wao wamemuasi Allah swt.”

518. Al Imam Ja’far as-Sadiq a.s. Amesema, Wasa'il ush-Shi'ah, J. 16, UK. 146:

“Mnapojulishwa kuhusu marafiki zenu wanapotenda maovu, nendeni mumwambie:

Ewe fulani bin fulani ! Ama acha kutenda madhambi au ukae mbali nasi:

Na hapo utengane naye hadi atakapo acha kutenda maovu.

519. Al Imam Ja’far as-Sadiq a.s. amenakili kutoka baba yake Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. ambaye Amesema kuwa baba yake Al Imam Hussein ibn Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema , Al-Kaf , J. 2, Uk. 641:

“Ewe mwanangu ! Jichunge na makundi matano na kamwe usifanye urafiki nao, wala usiongee nao.

Kwa hayo Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. alimuuliza baba yake

Je ni makundi gani hayo matano. Imam a.s. alimujibu:

1. Jitahadharishe na wala usifanye urafiki pamoja na yule msema uongo kwa sababu yeye ni kama mazua mazua anaye kufanyia vitu vya mbali vikawa karibu, na anakifanya kiwe mbali kile ambacho kiko karibu nawe.

2. Jihadhari na usifanye uhusiano pamoja na mtu ambaye hana tabia njema, kwa sababu atakuuza kwa thamani kwa tonge moja au hata chini ya hiyo.

3. Jihadhari na wala usifanye uhusiano na bahili kwa sababu yeye atakunyima kutoka mali yake pale wewe utakapo hitaji hasa.

4. Jihadhari na usifanye urafiki pamoja na mpumbavu, kwa sababu yeye atataka kukufaidisha wewe lakini kwa uhakika anakudhuru zaidi.

5. Jihadhari na usifanye uhusiano pamoja na yule ambaye hawajali ndugu na majama’a zake, kwa sababu mimi nimemona mtu kama huyo akilaaniwa katika kitabu cha Allah swt (yaani Qur'an Tukufu) katika sehemu tatu.

Nayo ni:

Sura Al Baqarah, 2, Ayah ya 27;

الَّذِينَ يَنْقُضُونَ عَهْدَ اللَّهِ مِنْ بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّهُ بِهِ أَنْ يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ

Wanao vunja ahadi ya Allah swt baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Allah swt kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye Khasara.

Sura Al-Raa’d, 13, ayah ya 25

وَالَّذِينَ يَنْقُضُونَ عَهْدَ اللَّهِ مِنْ بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّهُ بِهِ أَنْ يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۙ أُولَٰئِكَ لَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ

Na wale wano vunja ahadi ya Allah swt baada ya kuzifunga, na wanakataa aliyo amrisha Allah swt yaungwe, na wanafanya fisadi katika nchi: Hao ndio watakao pata laana, na watapata Nyumba mbaya.

Sura Muh'ammad, 47, ayah 22

فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِنْ تَوَلَّيْتُمْ أَنْ تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ

Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio muwe mafasidi katika nchi na mwatupe Jama’a zenu ?

520. Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Mustadrak-ul-Wasa'il, J. 12, Uk. 197:

“Ewe Kumail ! sema kile kilichopo katika hali yoyote ile. Uwe marafiki pamoja na wacha Allah swt na jiepushe na watendao maovu, jiweke mbali na wanafiki na usiwe pamoja na wadanganyifu na wahalifu na wahaini.”