read

Matendo Mema

331. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar , J. 76, Uk. 43:

“Kwa kufanya usuluhisho na amani miongoni mwa watu wawili (kwa kulinganisha) ni bora kuliko ibada za sala na saumu zake mwenyewe.”

332. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema katika Nahjul-Balagha,Uk. 511, Semi No. 248;

“Iwapo mtu atakufikia wewe kwa mema, basi inakubidi uhakikishe kuwa fikira zake zinabakia kweli.”

333. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar , J. 96, Uk. 119:

“Yeyote yule awaongozaye watu kwa taqwa (atalipwa) sawa na yale ayatendayo (aliyeongozwa) hayo matendo mema.”

334. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s.katika Al-Khisal cha Saduq, Uk. 323:

“Yapo matendo sita ambayo Mwislamu Mu’min anaweza kufaidika nayo hata baada ya kufariki kwake:

1. Kumwacha nyuma mtoto atakaye mwombea maghfira,

2. Kuacha Mus’hafu sharifu ambao watu watakuwa wakisoma,

3. Kuchimba kisima cha maji kitakachokuwa kikiwafaidisha watu,

4. Mti alioupanda yeye,

5. Sadaka aliiyoitoa katika kusababisha maji yakatirika vyema,

6. Ahadith na Sunnah nzuri atakazokuwa ameacha nyuma yake na zikifuatwa na watu.

335. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.katika Bihar al- Anwar, J. 76, Uk. 126:

“Iwapo isingalikuwa vigumu kwa Ummah wangu basi ningalikuwa nimewaamrisha kupiga miswaki kwa kila Sala.”