read

Sala za Usiku wa Manane

32. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , Bihar-ul-Anwaar, J. 77, Uk. 20:

“Heshima ya Mumiin ipo katika kukesha kwake usiku na utukufu wake upo katika kujitawala mwenyewe miongoni mwa watu.”

33. Amesema Amir-ul-Muminiin Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Ghurar-ul-Hikam, Uk. 289:

“Yeyote yule alalae zaidi wakati wa usiku, lazima atapoteza kitu mujimu kabisa katika matendo yake (yaani sala ya usiku) ambayo hataweza kuipata wakati wa mchana.”

34. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s., Bihar al- Anwar , J. 13, Uk. 329:

Allah swt katika ufunuo wake kwa Mtume Musa a.s., mwana wa ‘Imran a.s. alisema: “Ewe Mwana wa ‘Imran ! Wale tu ambao wanadai kunipenda mimi, wasema uongo, kwani usiku unapoingia wao hulala huku wakiniacha mimi.”

35. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s., Bihar al- Anwar , J.83, Uk. 127:

“Kamwe usiikose Sala ya usiku wa manane ! Kwa sababu, ukweli ni kwamba, mpotezaji ni yule anayeikosa (faida zake).”

36. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s., Khisal cha Sadduq, Uk. 72:

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. alimwambia Jibrail amwambie chochote, naye alimwambia: “ Ishi utakavyo huku ukitambua kuwa utakuja kufa; penda chochote kile utakacho lakini utatengana nacho; tenda utakavyo lakini utakutana nacho ( na kulipwa malipo yake). Heshima ya Mumin ni Sala yake ya Layl (usiku wa manane), na utukufu wake upo katika kujiepusha sifa za watu.”

37. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s., Biharal-Anwar J. 75, Uk. 107:

“Vipo vitu vitatu ambavyo ndivyo sifa za Muumin na ndivyo vito vya thamani kwake humu duniani na Aakhera. Navyo ni: Sala katika sehemu ya mwisho wa usiku (Salat ul-Layl), kutotamani au kuwa na wivu kwa kile kidogo kilicho mikononi mwa watu, na mapenzi (na uongozi ) wa Imam kutokana na kizazi cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.”

38. Amesema Al-Imam Muhammad ibn ‘Ali al-Jawad ul-‘A’immah a.s. , Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 79:

“Yeyote yule aliye na imani kamili juu ya Allah swt, anaona furaha; na yeyote amwaminiye, basi anatosheleza matendo yake.”