read

Salaam - Kusalimiana

350. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar , J. 76, Uk. 4:

“Pale munapokutana miongoni mwenu basi muwe wa kwanza kwa kutoa salaam na kukumbatiana; na munapoachana, muagane kwa kuombeana maghfirah.”

351. Al-Imam Hussein ibn Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Amesema katika Bihar al- Anwar, J. 78, Uk. 120:

“Thawabu sabini (70) ni kwa ajili ya yule ambaye anaanza kutoa salaam na thawabu moja ni kwa ajili ya yule anayeijibu hiyo salaam.”

(Wakati watu wawili wanapoonana, mtanguliaji katika kutoa salaam hupata thawabu zaidi ).

352. Al Imam Ja’far as-Sadiq a.s. Amesema katika Bihar al-Anwaar, J. 69, Uk. 393:

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliwakusanya watoto wa ‘Abdul Muttalib na kuwaambia: Enyi watoto wa Abdul Muttalib ! muwe waanzilishi wa salaamu, mujali Jama’a zenu, musali sala za usiku wakati watu wengine wanapokuwa wamelala, walisheni vyakula watu, na muongee maneno mazuri na hayo kwa hakika mutaingia Peponi kwa amani.”

353. Al Imam Ja’far as-Sadiq a.s. Amesema, Wasa'il ush-Shi'ah, J. 12, Uk. 55:

“Yeyote yule anayekuwa ni muanzilishi wa kutoa salaamu basi atakuwa ni mpenzi sana wa Allah swt pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.”