read

Sifa za Kuzitambua Hadith

Ili kuweza kuzitambua ni Hadith za aina gani zilizo za uongo, Ma’ulamaa wetu wametupatia dalili ambazo zitakazotujulisha usahihi na ukweli wa Hadith hizo na masharti ni kwamba mtu yeyote asijitumbukize katika kuzieneza na kuzisherehesha Hadith hadi hapo atakapoweza kuthibitisha kuwa zinastahili hivyo. Hapa tunawaleteeni kwa mukhtasari:

Habari zilizoelezwa katika Hadith zisiwe zikipingana na Ayah za Qur’an tukufu, yaani zisipingane na maamrisho ya Allah swt. Angalieni kuwa mara nyingi ‘Aam, khaas, mutlaq, muqayyad – kwa kutokujua mambo haya watu wanafikia uamuzi wa kusema kuwa Hadith fulani inakwenda kinyume na Ahadith, kunaleta hatari kubwa ya kupotosha maana sahihi ya Hadith.

• Hadith kamwe isiwe kinyume na akili bali iwe kwa mujibu wa akili.

• Iwapo Hadith itakuwa ni salama kwa Dini na Madhehebu, basi ipokelewe.

Kwa kuitambua Hadith mambo yafuatayo yanatosha:

    a. Ujue lugha ya Kiarabu na kanuni zake kwa ukamilifu,

    b. Zaidi ya hayo inabidi Lisan-i-Suduur yaani kujua maarifa na ubalagha wa lugha ya Ma’sumiin a.s.

    c. Inabidi kuwa mjuzi wa historia ya Kiislamu na sirah za Ma’sumiin a.s.

    d. Ni lazima ajue Madhehebu na mwanzo wao na kuzijua itikadi zao kwa vyema.

    e. Itabidi mtu huyo awe amejiepusha na ta’assub yaani chuki za aina yoyote ile kwani hapo ndipo hapo atakapoweza kushughulikia bila ya upendeleo au ushawishi wa aina yoyote ile.