read

Tawba

320. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika Al-Mahajjat-ul-Baydha:

“Majonzi makubwa ya watu wa Jahannam ni kuahirisha kwao Tawba”

321. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika Was’il al-Shiah, J.16, Uk.74:

“Yeyote yule anayefanya Tawba ni sawa na yule mtu ambaye hana mzigo wowote wa madhambi ya aina yoyote ile.”

322. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.Amesema katika Qurar-ul-Hikam, Uk. 240:

“Wapo waahirishaji ambao huahirisha kufanya Tawba hadi hapo mauti inapowafikia.”

323. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., katika Bihar al- Anwar, J. 77, Uk. 63:

“Ewe ‘Ali ! Amebarikiwa yule ambaye anatazwa na Allah swt wakati pale anapolia kwa ajili ya kutaka msamaha wa madhambi ambayo hakuna mwingine ajuaye illa Allah swt tu.”

(Baadhi ya Ahadith zinasisitiza kuwa haimpasi mtu kuwaambia watu wengine juu ya madhambi yake mwenyewe. Hivyo inambidi aungame madhambi yake kwa Allah swt tu na wala si kwa mtu mwingine.)

324. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar, J. 3, Uk. 314:

“Katika kila sehemu ya tatu ya usiku na usiku wa kuamkia Ijumaa kuanzia usiku uingiapo (hadi alfajiri) Allah swt huwatuma Malaika mbinguni ili kuita: ‘Je yupo mwenye kuomba ili nimtimizie ombi lake? Je yupo yeyote mwenye kufanya tawba ili nimrejee ? Je yupo aombaye msamaha ili nimsamehe ?’”

Tanbihi: Katika utamaduni wa Kiislamu, tunafundishwa kuwa kulala katika usiku wa kuamkia Ijumaa kunaitwa usingizi wa masikitiko ; kwa sababu Siku ya Qiyama watu watakuwa wakisikitika mno kwa kulala usiku hizo.

325. Amesema Al-Imam Ja’far as-Sadiq a.s.katika Bihar al-Anwar, J. 92, Uk. 216:

“Fungeni milango ya madhambi kwa kumwomba Allah swt, na mufungue milango ya utiifuu kwa kusema Bismillah-ir-Rahmaan-ir-Rahiim.”