read

Ulimi na Maovu Yake

369. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Bihar al-Anwaar, J. 71, Uk.286:

“Matokeo yatokanayo na ulimi ni mabaya kabisa, kuliko dharuba ya upanga mkali!”

370. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Bihar al-Anwaar J. 71 Uk.277:

“Miongoni mwa mambo yote, ulimi unastahili kuwekwa katika mahabusu kwa kipindi kirefu zaidi kuliko kitu kingine chochote. (Kwa sababu madhambi yetu mengi yana tokana nayo, kama vile kuwasuta watu, kusema uongo, kuzua mambo, kuwadhihaki wengine, na vile vile kuwa tuhumu watu wengi, n.k)

371. Amesema Al Imam Amiril Momineen a.s. Ghurar-ul-Hikam Uk. 228:

“Fikirieni na mupime kabla hamja ongea ili kwamba muweze kujizuia dhidi ya (kutenda) makosa.”

372. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Waqayi-ul-Ayyam, Uk. 297:

“Maangamizo ya mtu yako katika mambo matatu “Tumbo lake, matamaniyo yake, na ulimi wake.”

373. Amesema Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk.178:

“Hakuna mtu yeyote aliye salimika kutokana na ulimi wake hadi hapo yeye atakapo udhibiti ulimi wake.”