read

Utangulizi

Allah swt anatuambia katika Al-Qur’an tukufu: Sura al-Nahl, 16, Ayah 43

وَمَا أَرْسَلْنَا مِنْ قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُوحِي إِلَيْهِمْ ۚ فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِنْ كُنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

“Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi (Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.”

Sura Al-Ambiya, 21, Ayah 7

وَمَا أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ إِلَّا رِجَالًا نُوحِي إِلَيْهِمْ ۖ فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِنْ كُنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

“Na kabla yako hatukuwatuma ila watu wanaume tulio wapa Wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye elimu ikiwa nyinyi hamjui.”

Ayah hii Tukufu inawasihi Waumini kujielekeza kwa Ahl-Dhikr yaani watu wenye busara na Wanazuoni wa Ummah ili kuweza kubainisha baina ya haki na batili, wakati ambapo Waumini wanapokumbana na shida au ugumu katika masuala mbalimbali, kwa sababu Allah swt baada ya kuwafundisha elimu, aliwachagua hao kwa hayo. Hivyo, wao wamebobea katika elimu na ambao ndio watu halisi wanaoielewa, kuifundisha na kuitekeleza kwa usahihi mafunzo ya Qur’an.

Ayah hii iliteremshwa kwa ajili ya kuwatambulisha Ahlul-Bayt a.s. nao ni Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s), Fatimah (a.s.) , Al-Imam Hassan ibn Abi Talib (a.s.) na Al-Imam Husayn ibn Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib( a.s.) , ambao kwa ujumla wanaitwa Watukufu Watano au ‘Al-i-‘Aba ambapo pamoja na hao wameongezeka Ma-Imamu a.s. wengine tisa kutokea kizazi cha al-Imam Husayn ibn Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.mara nyingi katika nyakati mbalimbali aliwatambulisha hao kuwa ni Ma-Imam waongozi, nuru katika kiza, na ni wale ambao wamebobea katika elimu na bila shaka Allah swt amewajaalia Elimu ya Kitabu Kitukufu.

Ukweli huu, kama ilivyorejewa mahala pengi katika Ahadith mbalimbali kuanzia zama za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.kuanzia ufunuo hadi leo hii, na vile vile wanazuoni wengi na Wafasiri kutokea Ahl-Sunnah wamekiri waziwazi katika vitabu vyao kuwa Ayah hizi za Qur’an zilikuwa zimeteremshwa hususan kwa ajili ya kuelezea na kuwatambulisha Ahl-ul-Bayt a.s. Baadhi ya mifano ya vitabu vyenyewe ni kama ifuatavyo:

1. Imam Tha’labi katika tafsiri ya kitabu chake juu ya Ayah hiyo ya 42 kutokea Sura An-Nahl, namba 16

2. Tafsir ibn Kathir, j.2, Uk.591

3. Tafsir at-Tabari, j.14, Uk.75

4. Tafsir-i-Alusi, ijukanavyo kama: Rahul-Bayan , j. 14, Uk. 134

5. Tafsir-i-Qartabi, j.11, Uk. 272

6. Tafsir-i-Hakim, au Shawahid-ut-Tanzil, j. 1, Uk. 334

7. Tafsir-i-Shabistrary, au: Ihqaq-ul-Haq, j.3, Uk.482

8. Yanabi’-ul-Muwaddah, cha Ghanduzi Hanafi, Uk. 119

Kwa kutegemea ukweli huu, sisi lazima tujielekeze kwa Wananyumba ya Ahlul-Bayt a.s., na kutekeleza maneno yatuongozayo ili kuelekeza maisha yetu mema. Kwa sura hii, Imam-ul-Hadi a.s. anasema katika Man la Yahdhuruh-ul-Faqih, Tahdhib na ‘Uyun-i-Akh-bar-ur-Ridha:

“Maneno yenu yenye busara yanatupa nuru, maamrisho yenu ni hidaya kwa watu na usia zenu ni Taqwa na usawa.”