read

Zawadi na Kuwafurahisha Muumin

533. Mtume Muhammad s.a.w.w. Amesema, Al-Ithna-'Asheriyyah, Uk. 223:

“Wakati sadaka inapotolewa na mtu kutoka mikononi mwake, basi hiyo sadaka inasema:

Mimi nilikuwa kitu cha kwisha, lakini wewe umenipa maisha;

Mimi nilikuwa sina thamani sasa wewe umenifanya niwe na thamani kubwa;

mimi nilikuwa ni adui nawe umenifanya mie kuwa rafiki;

Wewe ulikuwa daima ukinilinda na kunihifadhi lakini sasa mimi nitakulinda na kukuhifadhi hadi siku ya Qiyamah.”

534. Amesema Al Imam Musa al-Kadhim a.s., Bihar al-Anwaar, J. 74 Uk. 314:

“Yeyote yule atakaye mfurahisha Muumin, basi kwa hakika kwanza kabisa amemfurahisha Allah swt, na pili amemfurahisha Mtume Muhammad s.a.w.w. na tatu ametufurahisha sisi Ahlul Bayt a.s. ”

535. Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Nahjul Balagha Uk. 533, Msemo. 328:

“Allah swt ameweka mahitaji ya wale wasio na uwezo katika mali ya matajiri. Kwa hivyo atakapokuwa mtu asiye na uwezo akabakia katika hali ya njaa basi ni kwa sababu matajiri wamemnyima haki yake.”

536. Al Imam Ja’far as-Sadiq a.s. Amesema, Bihar al-Anwaar, J. 75, Uk. 314:

“Kwa kiapo cha Allah swt ! Yeyote yule anayeizuia mali yake isiwasaidie Mumin wenye shida basi siku ya Qiyamah kamwe hawataonja chakula cha Jannah wala Kinywaji kilichopigwa Lakiri.”