read

Afadhali Mahari Ndogo.

838. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Kanz-ul-'Ummal, J. 16, Uk. 299:

“Ndoa ile imebarikiwa ambayo ina gharama ndogo.”

839. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 236 1:

“Wanawake bora kabisa katika umma wangu ni wale ambao nyuso zao ni zenye urembo na mahari yao huwa ni ndogo.”

840. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Kanz-ul-'Ummal, J. 16, Uk. 3212:

“Oeni hata kama mtakuwa na pete ya chuma (kama mahari).

841. “Yeyote yule anayetoa hata kiasi cha tonge moja ya nafaka au tende kama mahari (kwa kukubaliwa na mwenzake), basi kwa hakika ndoa yake ni halali na sahihi kabisa.”

842. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Wasa'il ush-Shi'ah, J. 21, Uk. 251:

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alitoa mahari ya Zirah moja yenye thamani ya Dirham thelathini katika ndoa ya binti yake Fatimah az- Zahra a.s. akiwaolewa na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.”

  • 1. Hii ni kasumba katika desturi zetu watu kuwa mwanamke anapokuwa mrembo sana ndio utaona wengine wana mahari makubwa kwa sababu ni mrembo sana kwa hiyo ndio Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kila mwanamke akiwa mrembo na mahari yake yakiwa madogo basi huyo mwanamke ni bora kabisa katika umma wake.
  • 2. Sisi imekuwa ni kasumba kuwa kabla ya kuoa lazima tutengeneze vitu vya thahabu Pete, hereni, Kidani, n.k. na hii ni kasumba ya kishetani na mara nyingi utawaona watu wanaotaka kuoa hawana uwezo lakini watakopa hata watauza vitu vyao vingine ili waweze kutimiza haya mambo ambayo hawana uwezo nao lakini ili kuonyesha ati kuonyesha desturi na mila ambazo ni potofu. Hapa tumeona Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. anasema hata kama ana pete ya chuma basi uoe sio mpaka iwe dhahabu.