Ahadith Mchanganyiko
1416. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Yanabiul Mawaddah, uk. 584 na 485 :
“Mimi ni mbora wa Manabii na Ali a.s. ni mbora wa Mawasii. Mawasii wangu baada yangu ni kumi na wawili. Wa kwanza wao ni Ali a.s. na wa mwisho wao ni Mahdi a.s.”
1417. Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu , Sura al-Ahzab, 33 Ayah 33,
‘Allah anataka kukuondoleeni uchafu, enyi watu wa Nyumba (ya Mtume ) na kukutakaseni kabisa kabisa.’
1418. Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu , Sura al-Ahzab, 33 Ayah 56,
‘Hakika Allah na Malaika Wake wanamteremshia Rehema Mtume, basi enyi Waumini (Waislamu) msalieni Mtume na muombeeni Amani’
1419. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Yanabiul Mawaddah, uk 42, 217 :
“Mimi nawaachia nyinyi Makhalifa wawili; Kitabu cha Allah swt : ni kamba iliyonyoshwa kutoka mbinguni mpaka ardhini, na Jamaa zangu wa Nyumba yangu (Ahlul-Bait a.s.)”
1420. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Yanabiul Mawaddah, uk 30/31
“Mfano wa Ahlul Bait zangu kwenu ni kama mfano wa jahazi ya Nuh a.s., mwenye kupanda jahazi hiyo ameokoka na mwenye kuiachilia, kapotea.”
1421. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Sahih Muslim, Kitabu Al-Fadhail, mlango wa Fadhail Ali a.s. kwa kiingereza ni : J.4, uk. 1286, Hadith nambari 5920 :
“….Enyi watu ! …. Ninawaachia nyinyi vizito viwili : Cha kwanza ni Kitabu cha Allah swt chenye uongozi na mwangaza basi shikamaneni na Kitabu cha Allah swt …. Na watu wa Nyumba yangu (Ahlul Bait a.s. )”
1422. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. Musnad Bin Hanbal, j. 4; uk. 437 :
“Hakika Ali ni kiongozi wa kila Mumiin baada yangu.”
1423. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika At-Tirmidhi, j.5, uk. 66 Na.3786
“Enyi Watu ! Mimi hakika nimekuacheni vitu viwili navyo ni Kitabu cha Allah swt (Qur’an ) na watu wa ukoo wa Nyumba yangu (Ahlul-Bait a.s.). Mkivishika viwili hivyo milele hamtapotea.”
1424. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema
“Mkipata neema chache msirudishe kwa uchache wa shukurani.”
1425. Allah swt amesema katika Qur'an Tukuf, Sura Al-Imran, 3, Ayah 169 :
وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ
‘Wala usidhani wale waliouawa katika njia ya Allah swt kuwa ni wafu, bali wahai wanaruzukiwa kwa Mola wao.’
1426. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema :
“Changanyikeni na watu kiasi ambacho kama mkifa watawalilia na mkiishi watatamani kuwa nanyi.”
1427. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Al-Ghadiir :
“Siku ya Ghadiir Khum ni Idi bora mno kwa Ummah wangu.”
1428. Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu, Surah Al Imran 3 Ayay 103,
وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا
‘Shikamaneni na kamba ya Allah na wala msifarakane.’
Semi Mchanganyiko
1429. “Uwe mpole na mwenye huruma kwa wale walioko chini yako au amri yako.”
1430. “Uchukue tahadhari na wala usidanganyike na ving’aavyo.”
1431. “Umwie ndugu yako kwa uwema hata kama ametokezea kwako kukudhuru. Yeye anapo puuzia au kuukanusha udugu nawe, umwijie kindugu, utokezee awapo katika shida na ujaribu sana ili uweze kumsaidia katika hali hiyo. Awapo mchoyo au bahili kwako na akupuuzapo pale uwapo na mahitaji ya msaada wa kifedha, uwe mkarimu na umsaidie kifedha kwa kiasi uwezacho. Iwapo yeye ni mjuvi na mkatili kwako, basi wewe uwe mpole na umhali yeye. Iwapo anakudhuru, uyakubalie hoja zake. Uishi nae kama kwamba wewe ni mfaidika. Lakini uwe mwangalifu sana kuwa wewe usiwe hivyo kwa wasio stahiki na walio waovu.
1432. “Usiimarishe urafiki na maadui wa marafiki wako kwani na rafiki yako atakugeuka wewe na kujitokezea mbele yako kama adui pia.”
1433. “Umshauri na kumpatia mawaidha mema na bora sana rafiki yako hata kama yeye hatapendelea hivyo.”
1434. “Uimarishe vyema na kusawazisha hasira, kwa sababu mimi sijawahi kuona faida yoyote ile iliyo zaidi kuliko kujizuia hivyo.”
1435. “Usimkorofishe mtu ambaye akufikiriaye wewe kuwa u mzuri na mwema na wala usijaribu kumfanya ajaribu kukugeuka.
1436. “Usiwe mbaya kwa watu wa nyumbani mwako (mke, watoto na wakutegemeao) na wala usiwe kwao kwa ghadhabu na mkatili yungali hai.”
1437. “Usimkimbilie yule akupuuzaye.”
1438. “Kamwe usiwaijie kwa ubaya wale waliokufanyia hisani.”
1439. “Masikini ni yule ambaye hana marafiki. Yeyote yule akunashaye haki na kujiona kuwa maisha yake yanamzonga na zenye kumtatanisha basi ni mtatanishi.”
1440. “Uhasiano ulio bora kabisa ni ule kati ya mtu na Allah swt.”
1441. “Uahirishe matendo yako maovu kwa kipindi kirefu kwani wewe unaweza kuyatenda popote pale utakapo penda (kwa hivyo kwa nini uwe na haraka ya kutenda?)”
1442. “Uchukue mambo mema kutoka kila tawi la elime kama vile nyuki atafutavyo asali (utamutamu) kutoka kila ua zuri.
1443. “Kumbuka kuwa chochote kile kilivyo kidogo ambacho umepatiwa na Allah swt kitakuwa ni chenye manufaa zaidi na huduma zaidi kwako na ni yenye heshima kwa uwingi usio na maana. Uelewe vyema kuwa kiasi chochote kile mtu mwingine atakacho kukupatia ni sehemu mojawapo ya kiasi alichomjaalia Allah swt.”
1444. “Hasara uipatayo wewe kutokana na ukimya wako unaweza kufidiwa kwa urahisi, lakini hasara itakayotokana na kusema kupita kiasi na kusema ovyo itakuwa vigumu kuyarudia. Je hauoni kuwa njia iliyo bora ya kuyalinda maji katika bwawa ni kwa kuufunga mdomo wake?”
1445. “Kulinda na kuhifadhi kile ulichonacho na kilicho chako ni afadhali kuliko kuomba na kutamani vile walivyonavyo wengine.”
1446. “Marejeo yatokanayo na kazi za mikono au uhodari wa ufundi kwa njia ya heshima na utukufu ingawaje hata kama ikiwa ni kidogo, ni heri ya utajiri ambao wewe unaweza kuupata/kuulimbika kwa kufanya madhambi maovu.”
1447. “Hakuna mhifadhi bora wa siri zako kuliko wewe mwenyewe.”
1448. “Kwa mara nyingi mtu anajaribu kila njia kujipatia kitu ambacho ndicho chenye kumletea madhara yeye. Na mara nyingi mtu hujitakia mabaya ya madhara mwenyewe.”
1449. “Yule aliye na tabia ya kusema sana, ndiye afanyaye makosa mengi.”
1450. “Yule ambaye huwa na tabia ya kufikiri na kuyadhatiti mambo, huendeleza nguvu zake za kina na fikara na nuru ya macho.”
1451. “Riziki inayopatikana kwa njia isiyo halali ni njia ovu kabisa ya kupata riziki.”
1452. “Kwa kujijumuisha pamoja na watu wema, wewe utaendeleza uwema katika tabia yako na kwa kujiepusha na makundi ya waovu, basi uwema ilivyo bora.”
1453. “Iwapo huruma au upole wako utatokezea kutendwa kwa ukatili na uonevu basi ukomeshaji na kutilia mkazo mkali ndiyo huruma na uwema ilivyo bora.”
1454. “Kamwe usitumainie uzushi kwani ndizo rasilimali za wajinga au wapumbavu.”
1455. “Busara ndilo jina la mkondo wa kukumbuka uzoefu na kuitumia. Uzoefu uliyo bora zaidi ni ule ambao ukupatiao tahadhari iliyo bora na mawaidha yaliyo bora.”
1456. “Kila mmoja ajaribuaye siye afanikiwae.”
1457. “Yeyote yule atakaeiaga (kufa) hii dunia, basi ajue kuwa hatarudipo tena.”
1458. “Karibuni utakipata kile alicho kuidhinishia Allah swt kwa ajili yako.”
1459. Allah swt Amesema katika Qur'an Tukufu, Surah Az-Zumar, 39 , Ayah 13 - 15 :
“Mimi naogopa adhabu ya siku kama nikimuasi Mola wangu.
Sema: “Namuabudu Allah swt kwa kumuitikadi kuwa yeye tu ndiye Allah swt .”
“Basi nyinyi abuduni mnachopenda kisichokuwa yeye.” (khiari yenu, lakini Allah swt atakulipeni tu); Sema: “Hakika watakao pata hasara ni wale walizotia hasarani nafsi zao na watu wao siku ya Qiyama. Angalieni! Hiyo ndiyo hasara iliyo dhahiri.”