Baadhi ya Dua’ za Imam Ali (a s )
1257. Ewe Allah swt, mbariki yule ambaye hazina yake kuu ni imani na silaha zake ni machozi
1258. Ewe Allah swt, wewe ni mkuu kabisa kwa kumwangamiza yule ambaye umeshakwisha kumtukuza hapo awali
1259. Sala ni silaha ya mumini
1260. Je kuna yeyote yule ambaye anaelewa vyema uwezo wa Allah swt na tena asimwogope Allah swt?
1261. Je kuna yeyote akuelewaye vile wewe ulivyo na tena asiwe na khofu yako?
1262. Ewe Allah swt, ngozi hii yangu hafifu, haitaweza kustahimili moto mkali wa Jahannam
1263. Mishale yote hailengi penye kuheshimiwa na kwa kupatwa na shida na majaribio
1264. Ewe muumba ,wewe upo pekee mwenye kuheshimiwa na mwenye kudumu daima milele na umelazimishia viumbe vyako kwa kifo na kwa kupatwa na shida na majaribio
1265. Ewe muumba, nisamehee madhambi yangu pasipo mimi kujua kwangu
1266. Ewe mola , unisamehe madhambi yangu yale ambayo yanayoweza kuniteremshia juu yangu laana na adhabu na ghadhabu zako
1267. Ewe mola wangu, nisamehee madhambi yangu yale yanayoweza kuwa sababu ya kuharibu na kuzighasi zile baraka zako zilizo juu yangu
1268. Ewe mola, nisamehe madhambi yangu ambayo ndiyo yanayozuia na kuzipoteza ibada zangu kabla ya kukufikia wewe
1269. Ewe mola wangu, nisamehee madhambi yangu yale ambayo inanikatiza mimi katika imani yangu
1270. Ewe mola, mimi nakukaribia wewe kupitia kwa kukukumbuka wewe
1271. Ewe mola, mimi nakuomba wewe uniweke furaha na niwe nimeridhika na yale wewe uliyonijaalia maishani mwangu na katika bahati yangu (kwa ajili yangu)
1272. Ewe mola wewe ni mwepesi sana wa kubariki na kurehemu, msamehe yule ambaye hana chochote ila ni ibada na sala zako tu
1273. Ewe Allah swt !, Je wewe utauachilia Moto uzikumbe nyuso ambazo zimeangukia mbele yako kwa unyenyekevu?
1274. Ewe Allah swt, zipatie nguvu mikono na miguu katika kutekeleza wajibu na huduma katika kazi zako
1275. Na uzipatie nguvu mbavu zangu ili nipate hali ya kukufikia wewe