read

Dunia Inayo Hadaa, Mavutio na Sumu Yake.

939. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-Anwaar, J. 6, Uk. 161:

“Wakati jeneza maiti ya mtu inapoinuliwa na kuchukuliwa kwenda kuzikwa, basi Ruh yake inaifuata maiti na katika hali ya masikitiko makubwa inasema:
‘Enyi watoto na jama’a zangu ! Jitahadharisheni sana kuwa ulimwengu huu hauwahadai nyie kama mulivyonifanyia mimi.

Mimi nimekusanya mali yote hii bila ya kujali uhalali au uharamu wake na nimeiacha nyuma huku kwa ajili ya wengine.

Sasa mimi nimeondoka na mzigo juu yangu (kwa sababu ya kutenda kila aina ya madhambi ya uhalali na uharamu) wakati matunda yake wanafaidi watu wangineo; kwa hivyo, mujiepushe na hayo ambayo sawa na yaliyo nifika mimi.”

940. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 73, Uk. 166:

“Iwapo huyu mtu angeweza kuiona mauti yake na kasi yake inavyo mwelekea yeye basi kwa hakika angechukia na kuiacha dunia na matumaini yake yote.”

941. Al Imam Musa al-Kadhim a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 311:

“Mfano wa dunia ni kama nyoka ambaye ngozi yake ya nje ni laini na nyororo kwa kugusa wakati kuna sumu kali mno inayoua ndani mwake. Aliye na hekima anajaribu kujiepusha nayo (lakini watoto wasio na fahamu kamili) wanapendezewa na kuvutiwa nayo na wanatamani kugusa na kucheza kwa mikono yao.1

942. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi, J. 2,Uk. 315:

“Mapenzi ya dunia hii itakayo angamia ndiyo chanzo cha maovu yote.”

  • 1. Ndugu wasomaji naona jambo hili liko wazi kabisa kwa sababu dunia hii inatuvutia kwa kila aina ya raha na mazuri ambayo ndani mwake kuna maangamizo yetu wenyewe ni mfano wa nyoka unamwona mzuri ukianza kumchezea anaweza kukuuma ukapata sumu na kufa ukaangamia na vivyo hivyo ndivyo ilivyo dunia, hawa leo tunaona hata vijana pamoja na kuwa na fahamu zao kamili na akili timamu na watu wamesoma na watu wanajua mazuri na mabaya lakini wanajifanya wapumbavu kiasi kwamba wanajiingiza katika madawa ya kulevya ambazo ni raha za muda na athari zake zinateketeza maisha yao wanayaona wanayasikia lakini utaona bado wenyewe wanajitumbukiza katika maangamizo hayo. Vile vile tunaona vijana wanaume vijana kwa wazee wanavutiwa na malaya wanaojiremba wamevaa nguo nzuri T-shirt na masuruali lakini hawafikirii busara ni nini wao wanavutiwa nao na wanakwenda wanafanya uasherati nao na wanakumbwa na magonjwa maovu kabisa ambayo yanawaua na wengine wanafilisiwa pia kiasi cha kwamba wanapoteza heshima yao na kupoteza uhusiano na jamaa zao. Kwa hivyo tujaribu kuangalia kilicho kizuri tuangalie na undani wake ili tuweze kujua kile tukifanyacho kina hekima gani.