read

Kubana Matumizi.

954. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 71 Uk. 346:

“Yeyote yule anaye panga matumizi yake basi kamwa hatakuwa fakiri.”1

961. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam, Uk. 182:
“Sera bora kabisa ni katika kutekeleza ukarimu.”

955. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Mustadrak-ul-Wasa'il, J. 15, Uk. 271:

“Matumizi ya kupita kiasi cha kile kinachohitajika, ni ufujaji.”

956. Al Imam Musa al-Kadhim a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 66, Uk. 334:

“Lau watu wangekuwa na tabia ya kula kwa kiasi, basi miili yao ingekuwa na nguvu.”

957. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Irshad-ul-Qulub:

“Hakuna mtu anayepita makaburini isipokuwa waliokufa wanamwambia:
‘Ewe uliye ghafilika ! Je unaelewa yale tulivyoeleweshwa sisi, itakufanya wewe damu yako ipoozwe.’”

  • 1. Kuna msemo usemao: Mali bila daftari hupotea bila habari !