read

Kughushi Katika Biashara.

923. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Safinat-ul-Bihar, J. 2, Uk. 318:

“Yeyote yule anaye lala huku akiwa amepanga njama dhidi ya Muislam mwenzake moyoni mwake, basi amelala katika adhabu za Allah swt, na atabakia katika hali hiyo hadi pale afanye Tawba.”

924. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Wasa'il ush-Shi'ah, J. 17, Uk. 283:

“Na yeyote yule anayemlaghai ndugu yake Mwislam, basi Allah swt humwondoshea riziki kwa wingi na huharibu maisha yake na kumwachia katika hali yake mwenyewe.1

925. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., At-Tahdhib, J. 7, Uk. 13:

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ameharamisha kuchanganywa kwa maji katika maziwa wakati wa kuuza.”

926. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema,

“Yeyote yule anayewaghushi Waislam kwa ujumla basi huyo hayupo nasi.”

927. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 80:

“Mtu yeyote anaye walaghai Waislam wenzake katika kununua au kuuza kitu chochote, hayupo miongoni mwetu, na siku ya Qiyamah atainuliwa akiwa miongoni mwa Wayahudi, kwa sababu wao wamekuwa daima wakiwadanganya na kuwaghushia Waislam.”

  • 1. Yaani kuachiwa wewe mwenyewe ujitegemee maana yake baraka na rehema Allah swt hazitakuwa pamoja nawe naye hatakuwa mwenye kukunusuru na kukusaidia kwa hiyo matendo yako hayo yatakufanya wewe ujitoe katika rehema, neema na uhifadhi wa Allah swt.